Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Showing posts with label Uchumi na maendeleo-Barabara. Show all posts
Showing posts with label Uchumi na maendeleo-Barabara. Show all posts

Monday, February 20, 2012

Akufaaye kwa dhiki ndiye rafiki wa kweli-83 hitimisho-27



Mama wawili aliinama chini kwa muda, hakuamini hayo aliyokuwa akiambiwa, akatulia bila kusema kitu, na kumfanya mpelelezi naye atulie akisubiri kilio,....akahesabu moja mbili, tatu ….kimiya, akainua uso kumwangalia mjane, ….mjane alikuwa katoa jicho tu, hasemi, hatingishiki, ….ghafla mama wawili akainuka pale alipokuwa kakaa, taratibu akahesabu hatua, moja mbili tatu, akaingia chumbani kwake na wakasikia mlango ukifungwa na fungua kwa ndani….

Shangazi alipoona vile , mbio mbio akakimbilia kwenye ule mlango na kugonga afunguliwe, lakini haikuwa rahisi hivyo, akabembeleza kila lugha aliyoijua, lakini haikusaidia kitu, na mwishowe akakata tamaa na kumgeukiwa mpelelezi, asikie naye atasema nini;

‘Naona umpe muda, najua hali ilivyo, hakutarajia…, na ndivyo ilivyo katika kufiwa, wengi inapotokea hali kama hiyo tunakuwa hatuamini, lakini yote ni mapenzi ya mungu….naomba tumpe muda, na tuombe Mungu ampe subira, maana hatujui dhamira yake ya kujifungia ndani, je kafanya hivyo kwa minajili gani, hatujui nini kilichopo mioyoni mwa kila mmoja wetu, mjuaji wa yote ni yeye aliyetuumba, na anayemiliki nafsi za kila mja wake, ….’akasema mpelelezi na kumfuata shangazi pale aliposimama na kumshika mkono kumrudisha akae kwenye kiti.

‘Hakikisha unazilinda hizo familia kwa nguvu zako zote, maana hawo sio wenyeji wa huko, …..’Mpelelezi alikumbuka maneno ya Inspekta na kujiona katika wakati mgumu, maana kwa muda ule alitakiwa kuwa kwenye uwanja mwingine wa mapambano, lakini inashindikana mpaka ahakikishe hali ya hapo ipo shwari.

Baadaye wakasikia mlango ukifunguliwa kwa ufunguo kwa ndani, wakajua mama atatoka, lakini haikuwa hivyo, na walipoona kuko kimiya tena, shangazi akamuangalia mpelelezi, na mpelelezi akatingisha kichwa kukubali alichotaka kukifanya shangazi, na bila ajizi shangazi akainuka pale alipokuwa kakaa, huku akiwa kaweka mikono mbele, na baadaye kuifikisha usoni, na akafuta jasho lisilokuwepo, halafu kwa taratibu akaufungua mlangoo na kuingia ndani ya kile chumba, akamkuta wifi yake kakaa pembeni mwa kitanda…

‘Wifi ili usiumie ni vyema ukalia kidogo, ukiumia kindani ndani itakutesa sana….yote hiyo ni mipango ya mungu, sisi tulimpenda ndugu yetu, mume wako kipenzi, lakini yeye kampenda zaidi na yeye ndiye mwenye mamlaka na uhai wetu, hatuna jinsi, tunachotakiwa ni kumuombea heri, ….’akasema wifi mtu na kabla hajamaliza mama alizindukana na kuanza kuongea…..

‘Kwanini wasiniambie pale pale , wanatuleta hadi huku nyumbani,….kwanini nisipate muda wa kumuona mume wangu kwa mara ya mwisho, ….unajua wifi wazee hawo wangeshaniangamiza muda mrefu tu, lakini kwa vile tunapendana na mume wangu, wamehindwa, sasa wameona wamuondoe duniani, najua itakuwa wao na mambo yao ya kimila….’akasema na kutikisa kichwa kama anakubali, na wifi yake alikuwa kaka kimiya tu.

‘Kama sio wao kwanini wasiniruhusu na mimi nikafika hape eneo la msibani, kwani kiutaratibu wao huwa familia zote hukutana huko wanakokuita sehemu ya ukoo, eti mimi siruhusiwi kwenda huko kwenye eneo la msiba na hata mazishi yake nisi hudhurie, kwasababu gani, mimi sio mke wake, …hata kama mtoto hawamtambui, lakini ipo ndoa, …hapana hilo sikubali, nitafanya kila njia niende huko huko kama nikuniua waniulie uko huko…vinginevyo, waseme, kuwa kuna jambo…,’ akainuka pale kitandani na kuanza kutingishika mwili mzima.

‘Nahisi kuna jambo, oooh, mume wangu ina maana sitakuona tena, hata,mazishI yako nisihudhurie, nimekukosea nini jamani, oooh, nilijua tu pale uliponiaga ulisema buriani ya kuonana, sikuelewa hayo maneno ya maana gani….ooooh, mume wangu..oooh..’akaanza kulia , na kulia, ni kila dakika akawa anoneza sauti, na mwili ukawa unatetemeka, mpaka akapandwa na shinikizo la damu, akadondoka chini na kuzimia…

‘Jamani muiteni dakitari, hali ya wifi sio nzuri….’alitoka shangazi mbio mbio, kumwambia Mpelelezi, na mpelelezi bila kusita akapiga simu kumuita dakitari. Na wakati anasubiri akawa anaongea na shangazi.

‘Hali ya binti yenu ni nzuri, hana shaka, ila ilibidi akapumzishwe hospitalini, na madakitari wamemshughulikia na sasa yupo njiani anakuja, hana shida, …’akasema mpelelezi.
‘Na huyo mwingine yupo wapi..?’ akauliza shangazi.

‘Sikutaka kusema zaidi mbele ya mama yake, lakini Rose hatujamuona bado, tunazania huenda huyo jamaa tunayemtafuta kamteka nyara, kwasababu jengo lote hayupo, …’akasema mpelelezi.
‘Sasa atakuwa katokea wapi, na mlango wa kutokea ni mmoja tu, na sisi muda mwingi tulikuwepo hapo mlangoni….’akauliza shangazi.

‘Hata mimi hapo naingiwa na mashaka huenda miongoni mwetu kuna mtu kahusika kumtorosha kinamna, huyo jamaa ni mjanja sana, ana mbinu nyingi sana , kiasi kwamba watu wanamuita kinyonga, lakini za mwizi ni arubaini, tutampata tu…’akasema mpelelezi.

‘Sisi tunachotaka ni binti yetu, huyo mnayemuita kinyonga hatuhusu, kama yeye ni kinyonga anaweza hata kumbadili binti yetu naye apite pale na sisi tusimtambue, …vyovyote iwavyo, tunachoomba ukamfuatilie binti yetu, maana naona hii nchi yenu haikaliki…’akasema shangazi,

‘Wapo vijana wangu wanamtafuta kila kona, mimi nilitaka niwafikishe hapa na kuhakikisha kwua mpo salama, na nje tutaweka walizni wa kutosha, na kama likitokea tatizo nitawaelekeza jinsi ya kuwasiliana na mimi haraka, …na naomba umshauri sana wifi yako asije akakaidi na kwenda kwenye huo msiba, maana wale wazee walinisistiza sana kuwa haruhusiwi kabisa kufika huko, na hawataki kumuona, akionekana lolote litakalo tokea hawatalaumiwa, kwasababu kukitokea msiba kama huo kwa jadi zao mke anaweza akatolewa kafara….’akasema mpelelezi.

‘Eti nini , kutolewa kafara ndio kufanywa nini huko, hapana siamini hayo ninayoyasikia hata katika karne hii….!, kwanini wafanye hivyo wakati huyo ni mke wake halali..?’ akauliza shangazi.

‘Shangazi, nchi hii ipo kwenye mpito, na hali kama hii ipo kwenye nchi zetu hizi za Afrika, mila na tamaduni za namna hiyo zimejikita sana , na baya zaidi zinaendekeza kuwabagua wanawake, …lakini hayo ni ya mpito tu….’akasema mpelelezi huku akiinuka alipomuona dakitari akitoka na shangazi naye akasimama na kutaka kuingia ndani akamuone wifi yake.

‘Subiri kwanza usiingie ndani, kwani amepitiwa na usingizi , anatakiwa atulie kwa muda kwani hali hiyo imetokana na mshituko alioupata, hayupo katika hali mbaya sana, ni kawaida tu, cha muhimu ni kuhakikisha kuwa anatulia hakuna jingine kubwa, …’akasema docta huku akifunga funga mfuko wake wa madawa na vyombo, akatoa karatasi ya gharama za matibabu.

‘Naomba uniandikie sahihi yako hapa….’akasema yule dakitari na kumwangalia mpelelezi, mpelelezi akaichukua ile katatasi ni kuisoma, halafu akaandika saini yake na alipomaliza akamkabidhi yule dakitaru ambaye aliiweka ile katasi kwenye begi lake kuaga kuwa anaondoka na akasema;

‘Kama kutatokea lolote nipigieni simu maana kwa hivi sasa nawahi nimeitwa mahala pengine….’akasema na kuondoka zake.
Alipoondoka huyo dakitari mpelelezi akaangalai saa yake, na kuangalai nje kwa muda kwa kupitia dirishani, halafu akasogea mlengoni mwa chumba, akafungua kidogo na kuchungulia ndani, halafu akarudi na kumuelekea shangazi akasema;

‘Kwa hivi sasa nawaomba mtulie kabisa hapa nyumbani, msijaribu kutoka toka kufuatilia lolote mambo mengine tutayamaliza na kila kitu kitakuwa shwari, …’akasema mpelelezi.

‘Ndio tutafanya hivyo, lakini ukumbuke sisi tumekuja hapa kwa kibali cha muda, hatuna muda mrefu wa kukaa hapa, na ni heri mambo yakaenda haraka, ukichukulia kuwa wifi yangu zio mzaliwa wa hapa kaolewa tu, sasa kuna mambo ya mirathi, hatujui taratibu za huku, na mimi hapa ndiye ndugu pekee nahitajika kuwa naye, ili nijue kipi kitaendaje…?’ akasema shangazi huku akiontesha uso wa huzuni.

‘Hayo yana taratibu zake, hata kama kuna mambo ya kimila, lakini hayataingilia mambo ya kisheria, huyo anakubalika hapa kama raia wa hapa, kaolewa na raia wa hapa na kuzaa hapa hapa, na ndoa yake inakubalika kisheria, …..ila kama yeye mwenyewe ataamua kuukana huo uraia wake, hilo litafuata baadaye, chamuhimu ni kuangalia kuwa hayo yao ya kimilia hatuuaingilii kwanza, kwani hawo wazee hawana utani inapofiki huko kwenye mila zao….’akasema mpelelezi.

‘Mila mila, mila mpaka karine hii, na mila hizo heri zingekuwa na heri kwa wanadamu, lakini mambo yake, mmmh, mimi nayaogopa, ….watu wanakimbili kutoa kafara, eti kafara la damu ya mtu, hawo ni watu au nimuumiani…!’akasema shangazi kwa hasira.

‘Ni watu kabisa na watu wenye heshima zo tu, na hizo ni imani zao, zimejijenga kwenye mioyo yao, na wanafanya hivyo wakiwa na maslahi nazo, sio hivyo hivyo tu, na hizo ni zama zao,zitakuja kupita tu, sizani watoto au wajukuu zao watazifuata tena, ..zmimi nina imani kuwa zitaisha tu….’akasema mpelelezi.

‘Wewe wasema tu,….hujasikia hivi sasa kuna kundi kubwa limezuka duniani, ambalo lina mambo kama hayo, na lengo lao ni utajiri, na utajiri huo umegubikwa na wimbi la damu za watu, …na nasikia ni wasomi, na ni watu matajiri, …sizani kama mambo kama hayo yataisha, kwani wengi wetu tulijua kuwa ni mambo ya watu wa hali ya chini, ….hawo wanaofanya hivyo ni matajiri, watu wakubwa …kuisha labda ndio mwisho wa dunia, ..’akasema shangazi.

‘Hayo ni Makundi tu, na mwisho wake yataisha, hilo liskutie shaka, kila jambo lina mwanzo na mwisho wake, na sizani kaam ubaya unadumu milele, na kiuzoefu na ilivyo kawaida, ubaya hauna mwisho mwema, …yataisha tu..’akasema mpelelezi.

‘Haya yetu macho, ….na kweli mwisho wa uabaya ni fedheha tu….lakini huku nako kumezidi, vita ani visivyoisha, hadi…oh, nani tena huyo….’akasema na kabla hajamaliza mara mlango ukagongwa, na mara akaingia askari mmoja na kumuita mpelelezi pembeni. Wakateta kwa muda, na baadaye wakatoka nje wote wawili, haikuchukua muda mara wakaingia na jamaa mmoja, akiwa kavaa kofia kubwa , na midevu mingi, mdomoni kaweka kiko, akipuliza mosho utafikiri gari mosho, na mkononi kashikilia bakora, …

‘Mimi ni mmoja wa familia ya marehemu, nimekuja hapa kumchukua shemeji, nikiwa na maana mke wa marehemu na mtoto wake, kuna mambo mengine ya kimila wanatakiwa kuhudhuria…’akasema huyo mtu.

‘Wewe ni ndugu wa familia kivipi…maana mimi sikujui, ile familia naijua vyema,….hebu niambie wewe ni nani, na umezaliwa na mzee yupi pale….?’ akauliza mpelelezi huku akitilia shaka, maana yeye alionana ana kwa ana na wazee, wazazi wa marehemu, wakamwambia kuwa mke wa marehemu haruhusiwi kabisa kukanyaga kwenye maeneo yao,

‘Mimi ni ndugu yake marehemu nilikuwa sipo kwa muda, na taarifa hiyo ya msiba nimeipata nikiwa njiani kuja kuwaona na mambo mengine ya kifamilia, na nilipofika nikawa na mambo mengine, nilipogundua kuwa mke wa andugu yangu hajafika eneo ambalo sote tunatakiwa tuwepo, nikaondoka kuja hapa kumchukua, sikuongea sana na wazee hao maana walikuwa katika mambo yao ya kimila, ila ilivyo ni kuwa mke wa marehemu anatakiwa awepo pale kukamilisha taratibu nyingine, hilo linajulikana wazi…’akasema huyo mtu.

‘Hapana…, nafikiri hukuonana na wazee wahusika,…. mimi nimeongea nao, na wakaniagiza nini nije nimuambie mjane, mke wa marahemu, na nafuata walichoniagiza, wewe kakutuma mzee yupi..?’ akauliza mpelelezi.

‘Mimi ni ndugu wa marehemu najua taratibu zote, na mke wa marehemu ni shemeji yangu, na huenda kiuataribu nikamrithi mimi, sasa sihitaji kuagizwa na mtu, natakiwa kuwajibika, tusipoteze muda,. Waambie shemeji na binti yake wavae au wajitayarishe tuondoke, kwanza wapo wapi, mbona siwaoni hapa….?’ Akauliza akiangali huku na kule na hakutaka kabisa kumwangalia shangazi.

‘Nafikiri hatujaelewana, umenisikia swali langu, kakutuma mzee gani, …maana hivyo hatutaelewana , na kiutaratibu wetu hataondoka mtu hapa, nenda huko kama wanahitajika mimi mwenyewe nitakuja nao , na kwa hivi hawapo hapa, kama huna jingine, naomba uondoke, maana hatutaki mabishano mengi yaendelee hapa, kutokana na hali ilivyo….’akasema mpelelezi.

‘Unajua wewe unaingilia mambo yasiyokuhsu, haya ni mambo ya kimila, na wewe ni mtu wa serikali, hutakiwi kuyaingilia, na unasema hawapo humu ndani , ….mbona nimeambiwa kuwa wapo humu ndani, au mnataka kunificha hata mimi…’akasema huyo jamaa.

‘Nani kakuambia wapo humu ndani…?’ akauliza Mpelelezi na kumwangali kwa mashaka,
‘Haya habari ndio hizo, najua wapo humu ndani, na binti naye hajafika huku, maana nasikia alikuwa haonekani,…?’akaulia akiangali huku na kule.

‘Nikuulize swali, nini hasa kilichokuleta humu, …naona unachunguza chunguza na hata yasiyo kuhusu, au una jambo jingine hujatuambia….?’ Akauliza mpelelezi.

‘Umesahau kuwa nyumba hii ni ya ndugu yangu, nahitajika kujua kila kitu, wakiwemo wanafamilia na wageni, hujui kwamba nilitakiwa niwe hapa sehemu aliyokuwa akiishi ndugu yangu, hujui kuwa mimi ndiye natakiwa kurithi kila kitu, huna habari kuwa mali ya ndugu yangu inajumuisha na mali yangu….hata hivyo huna haja ya kujua, utajua baadaye….’akasema huku akiangali huku na huko.

‘Mimi kiutaratibu natakiwa niwasindikize mke na mtoto wake, na kwa taarifa yako mimi natakiwa kuwa mrithi wa mke wake, na ….na mali yake, kwahiyo kila kitu kinachomuhusu ndugu yangu, nahitajika kukijua, …serikali haiingilii hapa, wakiingilia tutapambana nayo, …ujumbe huo nakupa, kama wewe ni mwakilishi wao , waambia wahusika, wasijaribu kuingili mambo ya kimila, watajuta…kwanza nimeshangaa, maana nilisikia wamakumaliza hawa wahuni…..lakini sawa hayo hayanihusu sana…
’akasema huyo mtu kwa dharau na kuondoka kwa mwendo wa pole pole na alipofika mlangoni akageuka na kuwatiazama na sasa macho yake yalimwangalia shangazi kwa muda, akataka kama kurudi lakini akasita na kuuliza;

‘Wewe mna uhusisiano gani na marehemu au mke wa marehemu?’ akauliza huku anamwangalia shangazi, na kabla shangazi hajasema kitu mpelelezi akadakia;

‘Hayo hayakuhusu, nafikiri nimeshakueleze hali halisi , kama itakuja muda wa kutambulishana ni baadaye sio sasa …’akasema mpelelezi.

‘Hivi nikuulize wewe una……aah, ngoja nisiongee mengi, …’akageuka na kuondoka.
Mpelelezi akatoa simu yake na kuanza kuongea nayo, akawa anatoa amri kwa vijana wake;
‘Mfuatilie huyo mtu aliyetoka hapa, hakikisha unamfuatilia kila hatua na uwe makini asijue…’akasema na kugeuka kumwangalia shangazi.

‘Haya ndio maisha ya hapa, wazee huku wanautawala wao , wana nguvu ya ajabu, kwani sehemu kubwa bado inatawaliwa na wakuu wa jadi, lakini hayo yataisha pole pole, maana mambo ya kisiasa na demokrasia yanaingia kwa kasi..’akasema mpelelezi.

‘Yaani huyo mtu alivyo anatisha, namuhisi vibaya…., anavyoonekana sio kama alivyo, nahisi ni mtu mwingine, aliyejificha kwenye hiyo miguo-guo yake ananukia hatari tupu….’akasema shangazi.

‘Tutajua ukweli karibuni, hawawezi kucheza na nuvu ya dola, …’akasema mpelelezi na mara simu yake ikaita;

‘Ehe, nipe taarifa, eti nini….’akasikiliza kwa muda halafu akageuka kumwangalia shangazi

‘Itabidi niwaache maana siamini, huyo jamaa aliyetoka hapa eti kawapotea kiajabu, huyo jamaa anaonekana sio kama alivyokuwa akionekana, ngoja nikaonane nao huko huko….’akasema mpelelezi.

‘Nilijua tu, jinsi alivyokuwa akionakena, ni kama chui ndani ya ngozi ya kondoo , lakini hawo maaskari wako kweli wanajua kazi yao, kwani ilikuwaje…?’akauliza shanagzi kwa shauku.

‘Eti alifika akaingia kwenye jengo moja la vipodozi na nguo , hilo ni duka ambalo wengi wanaoingia hapo ni wanawake au kama ni mwanamume anakuwa kamsindikiza mkewe tu, na huyu jamaa alipokuja hapa alikuja na mwanamke mmoja alimuacha ndani ya gari, waliingia naye humo, na maaskari wakawa nje wanamsubiri, wanasema hawakuwahi kumuona akitoka, na aliyetoka ni yule mwanamke ambaye aliingia kwenye gari peke yake akaondoka, baadaye hawo vijana ndio , wakaamua kuingia kukagua wakakuta hayupo..’akasema mpelelezi.

‘Na walipowauliza wahusika, au hawo wanawake waliokuwa hapo ndani walisemaje, …wote ni washirika wake nini….?’ Akauliza shangazi.

‘Wao walidai walimuona akiingia na huyo mwanamke, na akawa kabakia sehemu ya wageni, ambapo hakuna mtu anakujali sana, , na kwa vile alikuwa mwanaume, walijua kamsindikiza mke wake, na kuna muda walimuona akiingia chooni, na toka hapo hawakumuona tena, na mwanamke wake aliaga muda sio mfupi, akaondoka, wao hawakuwa na shauku yoyote na wao, kwahiyo hawajui wapi, ni nani hawo,…’akasema mpelelezi.

‘Hapo mimi siamini,…lazima kuna jambo hapo, nafikiri anajuana na hao wanawake wa humo ndani….’akasema shangazi.

‘Inawezekana, au iswe hivyo, ila ninauhakika kuwa, atakuwa alitoka hapo hapo, akiwa kajibadilisha kwa kuvaa nguo za kike…huyo jamaa ana mbinu za kila aina….’akasema na wakati anataka kuondoka mara simu yake ikaita, akaiskiliza kwa muda, halafu akasema, ;

‘Hakikisha hakuna mtu mwingine anayeingia humo au kutoka, na hakikisha kuwa kuna ulinzi wa kutosha,na huyo dakitari akitoka muhakikishe kuna usalama, na yupi dakitari mliye Muita hapo…..?’

‘Oooh, huyo safi ni mtu wetu, ….ila muhakikishe kuwa mumemuwekea mtu wa kuhakikisha anafika kwake salama, na kumpa tahadhari zote, ….sawa kama mumefanya hivyo, inatosha, ….mimi nipo njiani ila napitia sehemu, kuna jambo nafuatilia nitafika huko muda sio mrefu…..ila narudia tena, hakikisha hakuna anyetoka au kuingia huo ndani,nafikiri unanielewa,….’alipomaliza kuongea akamgeukia shangazi na kusema;

‘Rose kapatikana lakini hali yake sio salama, ila yupo dakitari anamshughulikia, hilo tuachieni kwa sasa, nitawajulisha zaidi baadaye …’akasema na hakusubiri shangazi kumuuliza swali akaondoka.

‘Shangazi alibakia akiwa kaduwaa, na akaona ni vyema akamfahamishe wifi yake kwani alisikia kitu kama sauti ndani, alipoingia ndani akakuta hakuna mtu, akaingia sehemu ya choo cha ndani, akakuta hakuna mtu, akaanza kuhaha kwa wasiwasi, …..

Nb Leo ndio sehemu yet hiyo inaishia hapo, kulikoni, Jumatatu njema. Nawashukuru noye kwa kuwa pamoja nami na wale wanachangia Muungu awabariki sana.

WAZO LA LEO:Msibaa uusikie kwa mwenzako tu, kufiwa ni mtihani mkubwa sana. Na mara nyingi Utajua umuhimu wa mtu pale anapotoweka,....!

Nachukua nafasi hii kuwapa pole wale waliofiwa na waume zao au na wake zao, na hasa wale ambao baada ya kufiwa wamejikuta pia wakizalilishwa kwa kunyang'anywa mali walizochuma na waume zao, wakati wanahangaika wanandoa hawa hawa wanandugu hawakuwpo, hawajui jinsi walivyoumia, jinsi walivyojinyima, sasa mmoja kati ya wanandoa hawo kaondoka, wanandugu wanakuja, wanajitokeza....na hata kama wapo mayatima, hakuna anayewajali tena, jamani tunajichumia laana, mali hiyo ni sawa na kumeza bomu tumboni...
Ni mimi: emu-three

Friday, May 20, 2011

Dunia ya leo sio ile ya jana



Wakati napita kwenye shamba moja lenye miti , niliona kitu cha ajabu sana, nikakumbuka ile hadithi na juha, lakini hii sio hadithi, hii ni kweli, nikapikicha macho yangu kuhakikisha kuwa hili nionalo ni kweli au naota, au nakumbuka kichwani ile hadithi ya juha.
‘Halooh hapo juu ya mti, mbona unafanya kitu cha hatari..wewe huoni kuwa hiyo ni hatari..’ nikamwambia yule jamaa
‘Hatari gani wewe, hebu pita la lako maana nyie watu mna midomo mibaya mnaweza kumfanya mtu  kweli akadhurika kiukweli’ akasema yule jamaa huku akiendelea kukata lile tawi.
 ‘Nakushauri hivi, kaa upande huo wa shina, wakati unakat hilo tawi maana ulivyokaa hivyo, tawi likianza kukatika utaanguka nalo…’ nikamwambia.
‘Hahahahah…wewe wafikiri kazi hii nimeianza leo, huu ni mwaka wa kumi tano, na utaalamu wangu ni huu, huu wa kukata miti, naitwa kukata matawi yaliyohatarini, kama haya, hapa kinachohijika ni `timing’ tu…likifikia mahala fulani mbio naelekea upande wa shinani….sina wasiwasi na kazi yangu..’ akasema huku anaendelea kukata tawi.
 Hutaamini niliyoona, jamaa alikuwa akikata tawi la mti halafu amekalia kule ambapo likianguka anaanguka nalo, hana wasiwasi anasema anajua kazi yake. Nikacheka na kusema kumbe majuha wapo wengi, kwanini uweke rehani maisha yako kwa kitu kama kile, kuwa umzoefu na tawi likiaanza kukatika utakimbilia upende wa shinani, je likikuwahi utamlaumu nani…wakati nasema haya nikasikia mlioo wa tatatata….hilo tawi likiaanza kuvunjika, nikageuka haraka nione uzoefu wa yule jama…wapi, ikawa purukushani, …
Loooh, toba walahi, nilimuiona jamaa akielea hewani na lile tawi huku akihangaika kushika tawi ambalo lilikuwa likielea hewani nay eye….duuuuh! Bahati nzuri jamaa akadondokea kwenye jalala lilo na majani mengi hakuumia sana. Nikamsogelea kumpa pole kama anahitaji msaada nimsaidie.
‘Wewe nuksi kweli…haijawahi kutokea tangu nianze kazi hii ya kukata miti…wewe umesema nitazurika, nitaanguka na tawi na kweli imetokea hivyo…ina maana wewe unaweza ukasema nitakufa na kweli nikafa..ondoka katika upeo wa macho yangu kabla sijakumaliza na hili panga…nuksi mkubwa wewe’ akainuka na kunionyeshea panga, ikabidi kweli nikimbie maana jamaa alishapandisha hasira.
 Wakati nawaza tukio hili huku natembea nikiwa na wasiwasi jamaa asije akawa anakuja kwa nyuma mara nikawaona vijana watano wamejificha kichakani, na nilivyowaona wakajifanya hawanijali, walikuwa wakivuta bangi, na mmoja kashikilia sindani ya kujidunga…oooh, nikashituka nikataka kuwasemesha , lakini wakajifanya hawanisikii, wao waliendelea na kazi yao kama vile hawanioni,  nikajisemea mwenyewe  moyoni kumbe majuha wapo wengi, yule alikuwa akikata tawi huku kalikalia huyu anakata nguvu za mwili wake na kuumaliza uhai wa maisha yake huku anajiona…kumbe wapo wengi hawa, nikajisema mwenyewe.
 Ama kweli, kila mji una juha wake na mchimba kisima huingia mwenyewe, maana  maisha yetu yalivyo, kila mmoja ana njia yake ya kuumaliza uhai wake  mwenyewe, na mbaya zaidi kwa mikono yake mwanyewe. Huyu anavuta sigara kama gari moshi, yule anavuta bangi, yule anakula madawa ya kulevya, yule mzinzi na musherati…ilimradi kila mmoja ana bididii ya kumaliza uhai wa maisha yake mwenyewe, ole wako umkanye…! Umesikia wale wanasiasa wanalalamika pale wanapoonywa kuhusu udhaifu na utendaji wao, au wale wanaofisidi dhamana waliyopewa, …nini kitakachofuata kama sio kuja juu, na hata kutoa vitisho, hebu angalia sasa hivi shida ya usafiri ilivyo, tatizo sugu au tuseme donda ndugu la mgawo wa umeme…jamani ina maana tunashindwa kujua kuwa  tufanyacho ni sawa na kulikata tawi huku umelikalia…angalieni sana dunia inavyobadilika, dunia ya leo sio ile ya zamani…
Huu ndio ujumbe wangu wa Ijumaa ya leo. 

Ni mimi: emu-three

Friday, March 11, 2011

Sema, useme, usiseme, itakuwa...!


‘Nauli zimepanda hamjui , kawaulizeni Sumatra..’ ilikuwa kauli ya dharau na ya kebehi kutoka kwa kondacta, huku akiwa kamkazia macho mama mmoja ambaye alikuwa kambeba mtoto wake. Yule mama ilivyoonekana alikuwa akimpeleka mtoto wake hospitali ya Msasani ya CCBRT. Alipapasa kwenye mkoba wake akitafuta hela ya ziada anayodaiwa, lakini ilionekana hata angetafuta siku nzima asingeipata.


‘Mwanangu sina hela nyingine ya kukuongezea, na hata wakati wa kurudi sijui nitarudije, nampeleka mtoto hospitalini, na huko siajua gharama yakeitakuwaje, sasa mnaniambia kuwa nauli zimepanda.., kwasababu, nilikuwa sijui kama nauli zimepanda…’ akajitetea yule mama.

‘We mama usilete dharau kwenye kazi za watu, matangazo kila siku kwenye taarifa za habari, magazetini , vipeperushi, watu wanaongea mabarabarani, hata maandamano wamefanya kupinga, …eti wanapinga nauli sizipande, ..mbona hampingi bei za vyakula zikipanda..nipe hela yangu mama unaniwekea kiwingu, kama huna nauli shuka…’ akasema kondacta huku akimkazia yule mama macho.

‘Hivi wewe kondacta huna Huruma, hapo imepungua shilingi ngapi tu, hiyo hamsini au mia inakutoa ubinadamu, je hiyo hela uliyompa huyo mpiga debe hapo nje , kafanya nini cha zaidi, kapiga debe huku gari limejaa amefanya nini,… kumbe mnapata hela nyingi mpaka mnawapa hawo wavuta unga mabarabarani bila kazi yoyote,…kafanya nini hapo zaidi ya kusisimama hapo mlangoni akisema `Gongolamboto Msasani, hata sauti haisikiki,..’ akasema jamaa mmoja.

‘Kweli ukiangalia hela wanayodaiwa na tajiri wao kwa siku wanaipata na ziada, kama wasingeipata wasingekodisha `dei waka’, wasingewapa hawo wapiga debe, ambao wanapiga debe hata kama gari limejaa, na wanawalipa hela…’ akasema mama mmoja.

Mimi nilikajikuta nawaza mbali kuhusina jinsi gani maisha yatakavyokuwa kwani bidhaa madukani bei ni juu kwa juu, kila kukicha vitu vinapanda bei na hakuna wakuweza kuzuia, na vingina hata kutangazwa havitangazwi na wala havina tume ya kudhibitio bei kama ilivyo Sumatra. Tumetoka kupandishiwa umeme, umeme ambao kuupata ni kwa mgawo, hebu fikiria mtu umelipia LUKU! Umelipia kabla ya huduma, lakini umeme hupati, hela yako inatumika wakati huduma hujaipata, na unaipata hiyo huduma kwa msharti ya mgawo, hii kweli ni halali…

‘Wewe konda unamlaumu huyu mama kuwa hajasikia matangazo, wewe unafikiri kila mtu ana redio, au anaweza kununua gazeti…wengine hata kusafiri kwenda mjini ni mpaka itokee shida kubwa sana, kama huyo mama huoni anampeleka mtoto hospitali, hana jinsi inabidi asafiri…hela keshaipangia kuwa hii nauli , hii gharama ya matibabu, sasa anakutana na kupanda kwa nauli, ataipata wapi hela ya ziada…keshapangiwa na mumewe, akirudi atamuelezaje mumewe, kuwa nauli imepanda…’ akasema mama mwingine aliyekaa kiti cha nyuma.

‘Acheni kuniyeyusha nyie, hivi…niwaulize nani kapandisha nauli ,ni mimi au ni serikali yenu…mumeshindwaje kujitetea ilihali mlipewa miezi miwili ya kutoa maoni yenu, …nani aliyekwenda kuweka pingamizi, mnasubiri hatua imechukuliwa mnaleta longolongo…’ akasema dereva.

‘Wewe serikali ikishaamua imeamua hata kama tungeandamana, hata kama tungekutana na kujadili, bei walishapanga iwe hivyo, sidhani kama ingetokea mabadiliko. Mfano bei ya umeme, watu walikutana na kutoa maelezo mengi, lakini ilipofika siku ile waliyopanga bei itapanda , ikapanda…kwahiyo useme, usiseme, waliloamua wao litakuwa…sisi ni hatuna usemi, kauli yetu ni butu…kauli yetu ilikuwa siku ile ya uchaguzi, lakini hatukuitumia sasa cha moto tunakiona…’ akasema jamaa mmoja.

Na kweli cha moto tutakiona, kwani nani anayejua dhahama ya giza, kama ulikuwa umeweka umeme, huyo unayetaka akutetee, nyumbani kwake kuna generator…huyu unayetaka akutetee kuhus kupand kwa nauli ana gari lake, na huenda gharama ya petrol analipiwa, huyo anayetakiwa akutetee kuhusu bei za vitu haijui hata hiyo bei, kwani kila ikifika mwishoo wa mwezi ana posho…inayoitwa `meal allowance…huyo unayetaka akutete kwa hili, yeye keshapewa fungu maalumu kwa maina tofauti, mpaka fungu la starehe…eti wanaita `entertainment allowance’…mwisho wa wiki anapanga honeymoon akaifanyie wapi, kama sio Zanzibar ni mikumi

‘Sawa bwana, watunyanyase, tu, lakini …wote tutakutana huko Loliondo,...’ Jamaa mmoja akaamua kuchekesha watu. Na mazungumzo yakahama kutoka kwenye nauli kwenda kwenye habari iliyopewa kipaumbele ya Loliondo.

Kwa ujumla hali ya maisha ya Mtanzania hasa wa kima cha chini, hasa mtu wa kawaida ambaye kazi yake ni kubangaiza hapa na pale, hasa mkulima ambaye nguvu zake zote zinategemea jembe la mkononi, hasa akina mama ambao kila kukicha wanahangaika na ndoo mkononi kutafuta maji, kutafuta kuni, kutafuta chochote ili watoto wasilie njaa, ili watoto waende choo…je nani atajua haya kama watetezi wetu, na mabosi wetu maofisini hawajui wala kusikia njaa ipoje, giza lipoje, foleni ya magari na adha zake zipoje… sio rahisi kujua kwasababu maisha yao yamesharahisishwa, na siju mishahara ya wakubwa hawa siku hizi ni shilingi ngapi.

Labda tubakie kusema, kuwa vyovyote iwavyo, sote ni wanadamu tunatakiwa tuishi na tupate huduma zote za msingi, ikiwemo chakula, maji , malazi afya nk , sasa kama hivi vitu bei inakuwa juu zaidi ya kipato cha mtu huyu ataishije…sijui..najiuliza nakosa jibu!

Hili ndilo wazo la Ijumaa ya leo.

Ni mimi: emu-three

Tuesday, August 17, 2010

Foleni dar sasa ni kero

Leo nimefika kazini saa nne kasorobo, lakini nyumbani nimetoka saa kumi na moja na nusu za alifajiri. Kuupata usafiri ilikuwa kazi kubwa sana, huwa tumezoea kupanda gari kwa mtindo unaoitwa `kugeuza nalo’ yaani unalipa nauli na kwenda na hilo gari hadi linpaogeuzia ili pate nafasi ya kuingia ndani ya gari, na hapo unalipa nauli mara mbili. Leo hata nafasi ya kuingia ili ugeuze nalo ilikuwa shida. Foleni imeanza mapema kwenda huko kwa kugeuza nalo ni foleni ukirudi nalo ni foleni.


Nimegundua kuwa matrafiki wanapokuwa wao ndio wanao-ongoza magari badala ya taa foleni huwa ndefu sana, kwani wao wanaita upande mmoja muda mrefu sana, wakati mwingine wanaita hata kama hakuna magari, jamani mnaita hewa. Yaani leo kila mmoja alikasirika lakini utafanyeje.

Kitu ambacho kinanisikitisha ni kuwa muda mwingi tunaupotezea ndani ya magari, na kumbuka humo ndani tumajazwa kama magunia, unasimama kwa mguu mmoja ukiteremsha wa pili utasikia kilio `umenikanyaga, wewe huoni, huna adabu….na matusi kwa kwenda mbele..’ sasa jamani utasimama na mguu mmoja kama jini, si utachoka, na wakati mwingine unakosa balansi na kumdondokea abiria mwingine hapo utaipata pata. Yule aliyekaa anajiona kama mfalme, hajui kuwa kesho naye anaweza kuwa kasimama na huko kusimama wanaita `kupaka rangi’

Sasa jaribu kufikiria mwenyewe mumeazana haswa na mabasi mengine madirisha hayafunguki vizuri, hewa ya shida, mijasho kuhemeana nk, unafikiri mwisho wa siku itakuwaje kama sio kuambikizana magonjwa. Achilia mbali watoto kuna wagonjwa ambao kusimama muda mrefu ni kuwatesa, lakini matafiki hawalioni hili wanaita upande mmoja weee, sijui ni kwanini?

Nakumbuka katika makala zilizopita nilitoa mapendeezo ambayo watu wengi wameshayaongelea kuwa zipo barabara zisizo rasmi kwanini zisiruhusiwe kupitisha haya mabasi makubwa, zirekebishwe kwa muda zitumike kuliko hili balaa la foleni. Na pia kama inawezekana watu watumia mabasi zaidi kuliko kutumia magari yao binafsi, hii imgepunguza wingi wa magari barabarani. Hizi ziwe njia zamuda mfupi huku nmikakati ya muda mrefu kama barabara za juu kwa juu zikiandaliwa au usafiri wa treni ukiandaliwa.

Hutaamini unaweza ukafika morogoro kabla ya abiria anayetoka Gongolamboto hadi Msasani hajafika mwisho wa kituo. Sasa haya maendeleo tutayapata kweli kama muda unaishia ndani ya daladala?

Ni mimi: emu-three

Tuesday, August 3, 2010

Yote mapenzi ya Mungu


Mapikipiki yalikuwa yameongozana kuelekea makaburini, na kuleta mshangao kwa wapita njia, na wale wasiopitwa na kitu wakaanza kuyafuatilia nyuma. Na sisi ambao tulikuwa tukijua ninii kinachoendelea tuakaona ni heri tufike eneo la makaburini ili kuhudhuria mazishi ya jirani yetu. Na wakati tunatembea kuelekea huko makaburini, ndipo udadisi ukaanza.
'Hivi hizi ajali za pikipiki mbona zinaongezeka' mmoja akasema
'Lakini hii huiwezi kuiita ajali, huu ni ujambazi, kwasababu huyu hakufa kwasababu ya ajali, bali aliuliwa na majambazi' akasema mmojawapo.
 Kwa taarifa tulizozipata, marehemu alikuwa kijiweni kwake akisubiri abiria, na ilipofika saa tatu na nusu usiku mwenzake akaja kumwambia kuwa waondoke, kwani muda huo sio mnzuri tena kumsafirisha abiria hasa wa maeneo ya mbali.
'Ngoja kidogo tunaweza kumpata mtu anayeelekea njia ya nyumbani' akasema marehemu. Lakini muda ukapita bila kupata abiria na wakaona waondoke. Na kabla hawajaingia barabarani, mara watu wanne wakaja, wakitaka kupelekwa huko wanapokwenda. Jamaa kwa vile walitaja njia ambayo inaelekea wanapokaa huyu marehemu wakasema sawa. Basi wawili wakapanda kwa merehemu na wawili wakapanda kwa rafiki yake, na safari ikaanza.
 Walipofika kwenye bonde ambalo lipo mbali na makazi ya watu, marehemu aliyekuwa mbele akasimamisha pikipiki ghafla, na kumfanya mwenzake aliyekuwa akimfuatilia nyuma afunge `break' za haraka. Na kabla huyu rafiki yake hajajua nini kimetokea akasikia kitu kizito kikigonga kichwani mwake na nguvu zikamwishia na kujikuta anodondoka chini, na kabla hajajitetea na kilichotokea akasikia tofali likipasiuka kichwani mwake na kupoteza fahamu.
 Kwa taarifa zaidi ya watu ambao wanasema walifika mahala hapo muda mfupi baadaye wanasema waliona kikundi cha watu kikikimbilia maeneo ya vichakani na pikipiki na huenda ndio hawo majambazi na inavyoonyesha ni mpango uliosukwa na kikundii cha watu, kwani waliowaona hawo watu wakikimbilia vichakani wanasema ni zaidi ya watu kumi.
 'Nasikia pia biashara ya injini za pikipiki imakuwa kubwa kwani wateja wakubwa ni wavuvi wa samaki wanaohitaji kwa ajili ya kutengenezea injini za maboti' akasema jamaa mwingine.
 Vyovyote iwavyo juhudi kubwa kwa polisi wa usalama barabarani kwa upande mmoja na usalama wa raia kwa upande mwingine zinahitajika ili kukomesha wimbi hili la ajali na ujambazi unahusishwa na pikipiki. Vijana wengi wamepoteza viungo kwa jali za pikipiki na wengine wapo taabani mahospitalini. Na hutaamini kila kjana ana mpango wa kutafuta pikipiki kwasababu wanasema biashara hiyo inalipa.
 Majmabazi nao hawapo nyuma, wamgundua kuwa biashara ya pikipiki ni nzuri na zaid  ni kuwa injini za pikipiki zinatafutwa sana kwa ajili ya maboti ya wavuvi baharini na maziwani. Wao kuua sio jrahisi sio jambo dogo, ilimradi wamepata wanachokitaka, na hapo ndipo wanausalama mnapotakiwa kuwajibika ili kutimiza ile dhamira ya kulinda raia na mali zao.
'Yote ni mapenzi ya mungu tunakubali kwa hilo' lakini tahadhari ni muhimu kwani wimbi hili la ujambazi ni kubwa kuliko watu wanavyodharau, na inavyokwendaa itafikia kuporwa kitu umeshika mkononi na mwendesha pikipikii akapotea mitaa mingine, utamkimbizaje wakati yupo juu ya pikipiki na mwendo wa pikipiki unaujua. Hii ni kwasababu pikipiki zitakuwa nyingi kuliko wateja na vijana wenye tamaa hawatakubali kukaa bila kupta pesa na hapo watahamankia na wizi huo kama wanavyoona kwenye sinema.
 Tahadhari kubwa ni kwa waendesha pikipiki wenyewe kukubali kusitisha biashara hiyo inapofikia muda wa ioni kama mtu hujapata basi riziki haipo subiri kesho ili madhara hayo ya ujambzi yapungue na hata wakigundua njia nyingine bado mtakuwa mumejipanga vizuri.Na jingine ambalo mnalijua ni sheria za uendeshaji wa hiyo pikipiki je umeshaijua vyema kabla hujaingia barabrani?
Ni mimi: emu-three

Friday, June 4, 2010

Changamoto kwa viongozi

 Tukiwa kituoni lilipita basi la wanafunzi la St. nini vile...!Ok, nimesahau kidogo, lakini lilikuwa kubwa kama yale mabsi ya kwenda Kenya. Wengi kimawazo tulijisemea kuwa ingefaa wanafunzi wote wapate usafiri kama huo, kwani kiusalama na hata kiafya ni vyema kwa watoto wetu. Nilisogea mbele kulipisha lipite kwani kwa msongamano wa magari kila gari linatafuta upenyo wa kupita, wanaitaa `kutanua'

 Pembeni yangu alisimama baba mmoja akiwa kamshikilia mwanae mkono, naye alikuwa katika harakati za kutafuta usafiri. Lile basi la wanafunzi lilipopita yule mtoto aliliangalia sana, na mwishowe akamwangalia baba yake. Baba yake kwa muda alikuwa akimvuta mkono ili wasogee kwenye upenyo watakaoweza kuvuka barabara. Alishangaa akimvuta mtoto wake alikuwa hasogei, alimpomwangalia akamuona analiangalia lile basi, naye akavutika kuliangalia vizuri. Akainamisha kichwa kumwangalia mwanae, na macho yao yakakutana.

 Je unafikiri walikuwa wakiwaza nini?

 Mimi nikakumbuka tukio moja lililotokea siku za nyuma, baba kama huyu aliwashikilia watoto wake wawili, mmoja alikuwa mdogo wa shule ya msingi au chekechea na wa pili alikuwa wa kidato cha kwanza. Walikuwa katika harakatii za kuvuka barabara, na baba alihakikisha amewashikilia watoto wote wawili mkono, tatizo kwa muda ule madaladala yalikuwa yakisimama ovyo, kwahiyo kwa upande mwingine wa barabara itokayo Gongolamboto ulikuwa huoni gari linalokuja vyema, kwa kukwa kulikwa na basi lililokuwa linapakia abiria.
 Baba mtu, akasogea kidogo mbele, na yule mtoto mkubwa akaangalia huku na kule akaona kuna upenyo wa yeye kuvuka, kumbe kuna gari linalotoka Gongolamboto kwa kasi, likatanua barabara na kuingia upande ule waliposimama watu wakisubiri magari, na kwa muda huo yule kijana wa yule baba alikuwa keshasogea hatua moja mbele ya baba yake ambaye alishamuachia mkono akijua hakuna hatari. IIlikuwa ni ajali ya kusikitisha sana, kwani lile gari lililokuwa likija kasi lilimgonga yula kija na kumkosakosa yule baba na mtoto wake mdogo. Yue kijana alifariki hapohapo.

 Kila mmoja aliyekuwepo hapo alisikitika na wengine kutoa machozi. Jaribu kulifikiria hili tukio mwenyewe akilini! Huyu yupo na mzazi wake, je wale wanaokwenda wenyewe shuleni wakiwa hawana hata mzazi wa kuwasindikiza inakuwaje?

 Ninachotaka kusema hapa ni zile ahadi za magari ya wanafunzi, je ilikuwa lugha ya kampeni au yanakuja lini? Je hii adha ya usafiri hasa kwa watoto wetu itaisha lini? Na kwanini vituo haviwekwi kiusalama zaidi mabasi yawe yanaingia kituoni na kutoka kuliko ile hali ya mabasi kusimama juu kwa juu, katikati ya barabara huku watu wakikoswakoswa na mabasi mengine? Tunaona ajali kila siku, ni mmoja mmoja lakini kwa mwaka wanakuwa wangapi?

 Sijui lakini mimi nahisi kuna haja ya kutungwa kwa sheria kuwa viongozi wakitoa ahadi kwenye kampeni na isipotimizwa waweze kushitakiwa! Hili litakuwa changamoto kwa viongozi wetu au nyie mnasemaje?
.
 Hilo ndio wazo langu la leo

From miram3

Friday, May 7, 2010

barabara za uchaguzi

`Jamani hizi barabara za uchaguzi zitaumbua wengi’ akasema jamaa tukiwa ndani ya daladala ambalo lilikuwa likiyumba huku na huko kutafuta maeneo ya kupita, hutaamini kuwa vichochoro tulivyopita vilikuwa havipiti gari, lakini leo imekuwa ndio ahueni yetu, vinginevyo tungechelewa makazini, na sidhani kuwa mabosi wangetuelewa, na wataelewaje na wao wana vimotomoto!


‘Kweli hizi barabara za kampeni, zilitakiwa ziwe changamoto kwetu wapiga kura, hawa jamaa ikifika mwezi wa nane, na tisa watajifanya kuja kujaza kifusi huku wakinadi kuwa wakichaguliwa watamalizia kuweka lami, nasi kwa ujima wetu tunasema sawa bwana mkubwa, kura hiyo’ akasema mmoja wa abiria.

‘Hebu jamani tuamuke tutadanganywa mpaka lini, mimi simjui hata mbunge wetu kwa sura, namsikia tu kuwa kawa, sijui naibu mu-waziri, lakini jimboni kwake kunatia aibu. Tuamukeni jamani, huyu mtu akija kwenye kampeni tumuulize ni nini kakifanya katika miaka yake mitano’ akasema mama mmoja

‘Na nyie akina mama ndio wakwanza kudanganywa na vikanga’ akasema mzee mmoja

‘Na nyie je, mashati mnayopewa hamuayaoni, swala ni kupokea lakini akili kichwani mwako’ akasema Yule mama wa awali

‘Hata mseme nini, hawo msiowataka watakuwepo hadi waseme hatutaki, kwani nyie wenyewe hamtaki wasiwepo, niwaulize ni wangapi wanaopiga kura’ akasema jamaa mwingine.

Ni kweli zipo barabara za uchaguzi, hizi hufukiwa na vifusi siku za uchaguzi zikikaribia, na vifusi venyewe ni danganya toto, mvua ikinyesha hubadilika na kuwa matope yasiyokanyagika hebu tembelea barabara ya mji wa Kenya hadi Moshi Bar, na nyingine kama hizo utajionea mwenyewe, utafikiri sio Dar.

Tunaomba jamani mwaka huu hizi barabara ziendane na mji, na sio kwa maneno na ahadi, Umeme shida, barabara shida, maji ndio usiombe, ni mwendo wa visima ndoo...oh, subirini mkinipa ubunge nitawafanyie yote..hii ndiokauli yetu!

From miram3

Thursday, April 22, 2010

Tunajikaanga kwa mafuta yetu wenyewe

 Mvua zinanyesha na ni neema, lakini barabara zetu hasa tuishio maeneo yaliyosahauliwa inakuwa kero. Magari yanakuwa shida na yakipatikana yanajipandishia nauli wapendavyo, `kama hutaki chukua bodaboda'. Hii imenipata leo asubuhi, na nilishangaa abiria wenzangu walivyoamua kukiuka sheria baada ya mwenye daladala kuamua kuongeza nauli.
 Baadhi ya abiria wakakataa kutoa nauli aliyojipangia kondakta, lakini baadhi ya waliowengi wakasema haina haja watalipa. Wachache tuliokataa kulipa ikabidi tushuke na hapo tilishafika mbali kidoo na kituo tulichoanzia. Nilijaribu kuwaelimisha wenzangu kuwa tukiwa na umoja hawa watu wanaokiuka sheria tutawashinda, kinachotakiwa ni kulipa nauli halali na vinginevyo twende polisi
'Bwana sisi tuna haraka, hiyo shilingi hamsini aliyoongeza itamsaidia nini, kama hutaki shuka' mwanamama mmoja akasema kwa hasira.
 Hivi ndivyo tunavyoamua kujikaanga kwa mafuta yetu wenyewe, tunaona tunachofanya ni kitu kidogo kwa muda ule lakini madhara yake ni mengi. Huyo mwenye daladala anachotaka ni faida na akijaribu mara mbili ataona ni kawida na matokeo yake ni kuumia kwa abiria walio wengi. Wewe ambaye unayeona hiyo hamsini ni ndogo ungejaribu kuchukua taxi ukawaachia walalahoi wakapanda kwa nauli iliyohalali.
 Hili ni moja ya tukio ambalo sisi wananchi tunachangia kuharibu utawala bora wa sheria, na matokeo yake tutakuja kuwalaumu viongozi. Tunachotakiwa ni sisi walengwa , ambao ni wananchi kuwa mstari wa mbele kuzilinda sheria, na tukiona mtu anazivunja tuwasilishe mahala panahusika. Kama tutaona tuna haraka, au ni pesa ndogo iliyoongezwa tujue uharaka na udogo huo ni madhara ambayo hatimaye ni kuchipuka kwa mafisadi uchwara.
From miram3

Tuesday, April 6, 2010

Mtu akiumwa na nyoka...!

‘Jamani ajali muisikie tu, imenifanya hata kupanda gari nijiulize mara mbili tatu. Kilichotokea siku ile ilikuwa kama ndoto’ Huyu alikuwa dada yangu akielezea ajali iliyomkuta.


Siku ile tulikuwa tumeenda kwenye kikao nje ya ofisi, na tuliporudi usafiri ukawa shida kweli. Siunajua tena mabosi waliondoka na magari yao, sisi ikabidi tuanze kuhangaika na madaladala, nina imani kabisa kama mabosi wangeamua kutuchukua kwenye magari yao, kila mmoja akabeba wawili-wawili tungeondoka wote, lakini kila mmoja alidai kuna mahali anapitia, siunajua tena walitaka kwenda kuzimua!

Mvua ikawa imesababisha mengi, usafiri ukawa wa shida, gari likija ni wale wenye nguvu ndio wanaopata nafassi ya kuingia, wengine wakawa wanarukia madirishani, yaani ni mchafukoge. Sisi akina mama na nguo zetu ikawa mtihani, inabidi ujibarague, lakini ilifikia mahali kila mmoja akajisahau kuwa kavaaje, gari likija ni kusukumana tu. Lakini asilimia kubwa tukawa bado hatujapata gari. Na wakati tumekata tama likatokea basi moja, likasimama. Hapo nami nikabahatika kuingia na bahati nzuri nikapata kiti.

Gari lenyewe likawa lakusukuma, likaondoka huku nikiwa na mashaka, kwani hata huyo dereva wake inaonekana ni hao wanaowaita dereva wa siku au `day-worker’. Alikuwa akilikimbiza gari hata pasipo na sababu, wakati mwingine ilibidi akatishe njia na kuingia kusipo na barabara, kukatisha njia, vichochoroni …jamani!

Tulifika sehemu kuna foleni ndefu, hapo tulisimama karibu saa nzima, magari yakawa yanaondoka kidogokidogo, kwasababu foleni ni ndefu. Dereve wetu kama kawaida yake akaanza utundu, anatoka kwenye foleni na kuingia njia ya magari yanayokuja, upande wa pili anaendesha hadi akifika sehemu ambapo anaona gari linakuja mbele anaomba magari yaliyopo kwenye foleni anaingia kwenye foleni, tunasogea mblele. Alifanya hivi karibu mara tatu, ya nne ikawa mbaya. Alitoka kwenye njia yake akaendesha kwa kasi, akafika kwenye barabara inayokatisha kuingia, kumbe kulikuwa na gari linakatisha. Na lenyewe lilikuwa likija kwa kasi. Hamadi,…nilichosikia hapo ni mlio wa ajabu, na mara tukasikia tunapaishwa na …..

Nilijiona nipo kwenye ndoto, nilijaribu kufumbua macho kuchungulia lakini macho yakawa hayafumbuki, lakini nilihisi nipo kwene gari, na nilichungulia kwa juu nikaona madirisha ya viyoo yapo mbali ajabu, na mvua ya mawe, na mawe yenyewe kama kokoto yakawa yanatudondokea. Niliinua mkono ili nijifunike na begi nililokuwa nalo, lakini mkono haukusogea. Kitu cha ajabu nilichohisi ni watu kunitumia mimi kama ngazi wananikanyaga na kurukia juu kule ninapoona kwa mbali, nilihisi ni dirishhani, lakini dirisha hilo nililiona kwa mbali ajabu.

Mara akili ikaniruudia na nilishangaa kujiona nipo peke yangu. Moshi ulikuwa umetanda sehemu zote za gari, kiaso kwamba nilikuwa sioni nini kilichopo mbele yangu. Wazo la kwanza nilijaribu kujiinua ili kuona kuwa kweli nipo mzima, kwani kumbukumbu za kuwa tumepata ajali zilshanijia. Nilipoona hakuna sehemu iliyovunjika nikajitutumua kuinuka. Nikahisi kama nipo kwenye kidaraja Fulani, manake miguu ilikuwa imekanyaga sehemu ndogo tu, na nikikosea naweza kuzama chini, na huko chini sikujua kuna umbali gani, lakini nilihisi kuna maji. Je tupo kwenye mto, niliwaza bila jibu, Akili ikanijia kuwa nipige kelele. Na kweli kelele ikanisaidia, kwani mara niliona watu wakinyosha mikono kupitia dirishani wakaniambia nikamate ile mikono ili wanivute kwa nje.

Kwanza wazo la wezi likanijia kichwani, je hawo niwasamaria wema au ni wezi. Nafikiri walinielewa wakasema kuwa nisiwe na wasiwasi wao ni waokozi wema. Nikanyosha mikono na mara nikawa naelewa hewani huku nikivutwa kwa juu. Kumbe gari lilikuwa limelala upande kwenye mtaro wa maji machafu, na ile mvua ya mawe ilikuwa sio mvua ni viyoo vilivvyovunjika ndivyo vilikuwa vikiniangukia vilikuwa vimesagikasagika. Nilipotolewa nje wazo langu kubwa lilikuwa kukimbia, lakini watu walinishika barabara. Nikabakia kupiga kelele, sijui ni kwanini.

Jamani mpaka nafikishwa hospitali sikujua kuwa nimeumia, nilijiona mzima kabisa. Ila kila muda uliokuwa ukipita ndipo maumivu ya mwili yalivyoanza kunijia, Na mara mwili ukaanza kuhumuka, nilkuwa kama kinyago Fulani hivi. Nafikiri ni kwasababu ya kukannyagwa na wenzangu, lakini nashukuru mungu waliponipima hawakuona sehemu iliyoumia kwa ndani..’ Huyu ni dada yangu akihadithia ajali yake ilivyokuwa na wengi wetu tumeshakumbana na ajali kama hizi. Wapo ambao hawajiwezi, wapo waliopoteza viuongo vyao, na wapo waliopoteza maisha, lakini hatimaye tunasahau.

Hii ni hulka ya kibinadamu kusahau, hata kama ajali iliyokupata ni kubwa kiasi gani, tunaishia kusahau! Na kama tusingeweza kusahau huenda hata akina mama wasingelipenda kubeba mimba mara ya pili. Kwani kuna wengine wanaponea tundu la sindano. Lakini kila mtu hufa kwa wakati wake, au sio. Zipo ajali za kujitakia na hizo zikipita tunasahau, na huenda wakati zinatokea mtu huahidi kuwa mimi sitarudia tena, lakini siku kadhaaa mtu huyohuyo yupo palepale, na sie tulioshuhudia tunamuunga mkono, na kumpa sifa. Jamani si mtu akiumwa na nyoka huogopa hata unyasi! Ndio huogopa hata unyasi kwa siku kadhaa baadaye husau!



From miram3

Wednesday, March 10, 2010

Umri unakwisha na mengi

  Ilikuwa saa saba na nusu, nikiwa ndani ya ofisi moja , mbele yangu alikuwa kakaa bosi wa hiyo kampuni. Mara mfanyakazi wa huduma akaingia akiwa amebeba vyakula toka hoteli za kisasa. Nasema za kisasa manake vyakula vilikuwa vimefungwa vizuri. Hapo mate yakaanza kunitoka, siunajua tena ukiwa umefunga mkanda wa hali ngumu. Bosi Yule akaanza kula na kushushia na vinyaji huku akiperuzi laptop yake. Hakuna cha karibu hapo, tumbo linanguruma kwa njaa!


‘Vipi huendi lunch?’ bosi akaniuliza

‘Mhh, nilitoka kidogo, mmh…’ nikajiumauma nikiogopa kusema ukweli kuwa nimefulia, tangu asubuhi sijapata chochote zaiidi ya chai ya asubuhi.

Nikakumbuka swali liloulizwa kwanini umri wa Mtanzania kwa wastani unakuwa chini ukilinganisha na wenzetu wa mataifa yenye nacho! Majibu yapo mengi, sio ya kubahatisha.

Angalia hali za ofisini, wenye makampuni wanajua wanachokupa hakitoshi, wao wanachokulipa ndio matumizi yake ya siku mbili. Hali hii inawafanya wafanyakazi wafanye kazi kwa shida, njaa na kukata tamaa, na wengine huzidiwa na hatimaye kufanya kinyume na taaluma zao. Na mwisho wa siku umri unapungua.

Ilipofika jioni, nilishukuru mungu na kuharakisha kukimbilia kituoni. Nilipofika nilikata tamaa, kwani umati uliokuwepo utafikiri Dar nzima imehamia hapo. Nilijipapasa mfukoni kuangalia kuwa nauli ipo, angalau nitembee hadi vituo vya mbele ili nipata gari la kugeuza nalo. Hapo ina maana nilipa nauli mara mbili, nikaona nauli haitoshi. Nakakaa chini ili nisubiri bahati ya kugombea. Nilikaa karibu masaa mawili nikisubiri gari na bahati hilo likaja limeshajaa, lakini bado konda anaita watu kwa kusema kuna siti za kumwaga, ikawa kukuru kakara hadi nikapenya ndani. Oh, nilivyosimama hakuna cha kugeuka au kusogeza mguu, haya twende.

Fikiria hali kama hii, tumejazwa kama magunia, ukipumua unapumua kama sio mgongoni kwa mwenzako ni usoni kwake, na ukikohoa,…ohoo, inabidi uzibe mdomo. Waliokaa walikuwa wakilalamika kwani sie tuliosimama tulikuwa tukiwasonga hata kuwaangukia, utafanyaje nawe upo bongo. Kwa hali kama hii lazima umri utakuwa unapungua. Utapungua kiafya, kwa kuambukizwa magonjwa au hali ya hewa inavyokuwa nzito.

Wakati nawaza haya tukasikia mtoto akilia, alilia kiasi kwamba kila aliyekuwepo alimuonea huruma, ilibidi waliokaa dirishani wampishe Yule mama, ili Yule mtoto apate hewa. Na si huyo tu kukawa na mama mmoja mwenye presha alizidiwa hadi akaanguka ikabidi walikaa wampishe akae karibu na dirisha, safari ikawa inaendelea.

Nilikumbuka asubuhi nilivypata shida ya usafiri, nikiwa na watoto ambao niliongozana nao ili wawahi shuleni. Nilikataliwa kila gari lililopita eti kwasababu nina wanafunzi. Ilibidi niwalipie nauli ya wakubwa ndio tukapata kuondoka. Haya ni matatizo tunayopambana nayo asubuhi kabla hujafika kazini, achilia mbali ada, nauli na mengineyo, haya yanachangia kwa kiasi kikubwa kupunguza umri wetu! Hapa jikumbushe na tukio hili la adha ya usafiri dar

Labda tujiulize kama ndio hivyo tufanyeje. Nakumbuka niliwahi kufanya kazi kwenye kampuni iliyokuwa ikitoa chakula kwa wafanyakazi., na ilikuwa na mpango wa kununua gari la wafanyakazi, kwanini hii isifanyike kwa kila kampuni? Utakuta meneja ananunuliwa gari la hela nyingi tu, mshahara wake mkubwa watoto wake wanasomeshwa, sasa wao ni nani na wewe ni nani. Kwa kufupi wao ndio wao na wewe ndio wewe. Umri unakwisha ukizidi kuwaza hayo!

From miram3

Thursday, August 27, 2009

SHIDA YA USAFIRI NA FOLENI DAR

Leo tarehe 27-08-2009, niliona niitoe kero yangu katika tovuti ya http://www.wananchi.go.tz/
Tunawashukuru sana kwa kutoa Tovuti hii, na nivyema wananchi tukaitumia vyema kwa kutoa kero zetu, kutoa maoni au pongezi. Nami kwa kuanzia ningependa kutoa dukuduku langu kuhusiana na tatizo la usafiri hasa kwa wakazi wale tunaishi nje ya mji kama vile Majohe,Kipunguni nk, ambapo hakuna magari ya moja kwa moja kuelekea sehemu kama vile Msasani, Kawe, au Kunduchi nk ,na fikiria unatakiwa ufike ofisini saa mbili, bila hivyo kazi huna.

Maoni yangu ni kuwa kuna haja ya wahusika wa usafiri kuruhusu magari ya kutoka maeneo kama hayo ya moja kwa moja kwa kutoa nauli yenye unafuu, kuliko hili la kupanda magari mawili au matatu na mojawapo unalipa nauli ya masafwa marefu(sh 450/-). Na hii ina mana kuwa kwa siku unatakiwa kulipia nauli si chini ya sh 1400/- kama umebahatisha kupanda magari mawili, lakini mara nyingi haiwi hivyo kwasababu inakubidi ulipie nauli ya kugeuza nalo,ili angalau upate kiti au uweze kuingia ndani ya gari bila kudandia (Huwa asubuhi au jioni kama hujui kudandia huwezi kuingia ndani, magari haya hayasimami kituoni kwa kukwepa wanafunzi.) kwahiyo kutumia nauli zaidi ya sh 1900/-kwasiku.
Kero hii inatukwaza sana sisi watu wa maeneo haya kwasababu, sio tu kwa swala la nauli, lakini pia inatubidi tuamuke saa kumi za alifajiri kila siku ya kazi , ili kukwepa foleni ambayo huanzia saa kumi na mbili, na hutaamini kama utakutana nahii foleni unaweza ukatumia zaidi ya masaa matatu kutoka Msasani hadi Gongolamboto bado hujatafuta usafiri wa kwenda Majohe au Kipinguni unapoishi. Kwa minajili hii familia yako unaiacha ikiwa imelalana huenda ukarudi ukaikuta imeshalala pia.
Kwa maoni yangu kuhusiana na tatizo la foleni ndefu, kama inawezekana ni kuanzisha barabara za moja kwa moja, yaani magari yakienda yasirudie njia ileile, nafikiri inawezekana kwasababu zipo njia za mkato kutoka Gongolamboto hadi Ubungo, au Gongolamboto hadi Mbagala, na ndani kwa ndani zipo barabara za mikato ambazo tumeyaona magari ya daladala yakipitia kukwepa foleni, hizi zote zikiwekwa vizuri itapunguza foleni kwa kiasi kikubwa. Na kama inawezekana usafiri wa treni kwa maeneo haya ungefaa pia!
Na pia wakati mataa hayafanyi kazi,matrafiki hutumia muda mrefu kuita sehemu moja tu, sijui hufanya hivi kwasababu gani,kwanini wasitumie `stop-watch’ ili kutowaumiza abiria ambao hujazwa ndani ya daladala kama magunia. Nimeshuhudia abiria wakizimia ndani ya magari haya kwasababu ya kusimama muda mrefu na kukosa hewa!
Natumai wahusika wanalifanyia kazi tatizo hili,lakini ni sie waathirika inabidi tutoe sauti zetu ili mjue kweli tunaumia, kwani tusiposema mtajuaje shida zetu

Ahsanteni na poleni sana kwa majukumu haya mazito.
NB. mfadhaiko nilioushuhudia ndani ya daladala nitautoa kesho Mungu akipenda.

From miram3.com