Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Showing posts with label visa vyenye mafundisho. Show all posts
Showing posts with label visa vyenye mafundisho. Show all posts

Wednesday, October 30, 2019

CHUMA ULETE-6


 Hata sijui ni kwanini...

Mimi  sikuweza kumuamini huyu mtu wa jamii, kuwa ataweza kunisaidia kwenye hili janga, kwangu mimi, sana sana  niliona yeye anataka kutumia hili tukio, ili aweza kukamilisha utafiti wake tu..na hii kesi inahitajia pesa, inahitajia wakili mwenye ujuzi mkubwa,...mimi sina pesa, rafiki yangu halidhalika, na cha ajabu rafiki yangu kaenda kuniletea mtu ambaye, hana pesa., ...sio wakili kisheria,

‘Huyu mtu atanisaidia nini mimi..’ nilijikuta nawaza na kusema hivyo kwa sauti ndogo.


 Tulibakia wawili , mimi na mtu wa jamii, yeye akaniuliza maswali machache, muda wa kuongea na wageni ulishakwisha, yeye  akaondoka akisema anataka kuonana na mkuu wa hicho kituo, sijui waliongea nini....

Siku hiyo ikapita sikuchukuliwa kwenda Ukonga, niliona ajabu sana...,na hakuna aliyekuja kuniambia ni kwanini..lakini nilijua ni swala la muda, nitachukuliwa tu..

Kisa kinaendelea.....

**************


Kesho yake akaja shemeji, macho yamemuiva, na nilibahatika kuyaona hayo macho yake baada ya yeye kuvua miwani, aliyokuwa amevaa, nahisi aliivaa hiyo miwani kwa makusudi ya kuficha hayo macho yake, ni dhahiri kuwa anavuta bangi, japokuwa yeye, halikubali hilo.


'Shem, kwanini unaniuza..'akaanza kuniambia hivyo, hata bila ya salamu.


'Kwa vipi shem...?'nikamuuliza, nilishamzoea, maana kila tukikutana, mimi na yeye, tunaishia kwenye ugomvi tu, jamaa huyu ananichukia sana, ila kama dada yake yupo, jamaa huyu  anajifanya kuwa ni muungwana kwangu.

'Mimi nimejitolea muhanga kukusaidia wewe, ...unajua ni nini nilichokifanya, imeniuma sana, kukusaidia wewe na haki ya dada yangu ipotee....’akatikisa kichwa.

‘Unaja nikuambie ukweli, tukio hili  ilikuwa ndio wakati mnzuri wa kukumaliza kabisa...ulichokifanya, hakistahiki kusamehewa,..unahitajika kunyongwa,..lakini kwa upumbavu wangu, nikaogopa....niliogopa, nitaambiwa nimechukua sheria mikononi mwangu, na mimi sitaki kuingia kwenye mikono ya polisi...ndio hivyo tu...sasa wewe umeharibu..’akasema

‘Mimi nimeharibu kwa vipi shemu...?’ nikamuuliza

‘Wewe unawatangazia watu kuwa  mimi ndiye niliyekupiga kichwa....kweli si kweli...?’ akaniuliza sasa akinikazia macho, awali nilikuwa nikimuogopa sana huyu jamaa, lakini ikafikia mahali nikaanza kumzoea,..kwahiyo hapo sikujali, nikamkabili, japokuwa siwezi kupambana naye kimabavu.

'Nimemtangaza nani kuhusu hilo, wewe usiwe unasikiliza majungu watu,..ilivyo, hata taarifa ya polisi inasema dada yako ndiye aliniumiza...’nikasema, na jamaa akabenua mdomo kwa dharau.

'Sikiliza, najua wewe na mimi hatuivani kabisa..., na ukiona mimi nimefanya jambo la kukusaidia, ujue kuna gharama, na gharama yake ni kubwa sana...,’akasema na nilikuwa nalisubiria hilo.

'Natakiwa nikulipe shilingi ngapi..hata hivyo ukumbuke mimi ni shemeji yako....’nikasema

'Mjinga mkubwa wewe, wewe moyoni mwangu sio shemeji yangu, kabisa kabisa..., natamka hilo unielewe, na najua unanielewa hivyo...mengine ninafanya kwa heshima ya dada yangu...’akatulia akikunja uso , niliona kama ana sikitika.

‘Mimi  niliapa sitakutambua wewe kama shemeji yangu, kamwe,..nitafanya hivyo tu, pale dada akiwepo, kumridhisha yeye...sasa wewe unataka gharama si ndio hivyo,...haya, je nikikuambia nataka nyumba yako utasemaje..’akasema akitizama miwani yake aliyokuwa kashikilia mkononi.

'Shemeji, huko unapokwendsanaa ni mbali...’nikasema nikihis mwili ukinicheza cheza..nilijua tu, huyu jamaa kalenga jambo.

'Mimi eeh, nimekwenda mbali sio.., najua utakuwa mgumu kwa hilo......sasa kipi bora, nyumba yako ipigwe mnada kwa ajili ya milion chache ulizokopa au...nichukue mimi hiyo nyumba, halafu nipambane na huyo anayekudai,...na dada angelikuwepo, ningewachia muishi,humo, lakini kwa vile...’hapo akatulia.

'Siwezi kufanya ujinga huo, unajua thamani ya ile nyumba,...hahaha, eti ipigwe mnada, kwa deni gani hilo,....hata hivyo, mimi nitamlipa huyo jamaa pesa yake...’nikasema

'Hahaha, wewe mpuuzi, kweli kweli, sitamani hata kukuita shemeji, hebu niambie kwa hali yako, wewe utapatia wapi hizo  pesa, kapuku kama wewe , dada yangu mjinga kweli kweli, sijui alipumbazika na nini kukubali wewe uwe mke wake,..’akakohoa
 Mfululizo, nahisi mate yalimkoholeza.

‘Dada kuolewa na masikini kama wewe ni kosa kubwa sana... wewe hujui tu, ...wakati nyie mumeishiwa kabisa, mimi ndiye nilikuwa nawalisha, sikutaka dada yangu akuambie hilo ila leo nimekuambia ili uelewe kosa ulilolifanya...kiukweli mimi nampenda sana dada yangu, na sikutaka apate shida...’akatulia kidogo

‘Lakini sio kweli, angeliniambia ...’nikajitetea

‘Hivi wewe hukuwa unaona ajabu, ukirudi nyumbani unakuta  chakula kipo, wakati hujaacha hata senti moja, ulifikiri mke angelikula wapi, wakati hukutaka hata aende sokoni, eeh...usitake niseme mengi..’akasema hivyo

Kiukweli, kipindi nimekwamba kabisa, kuna wakati nikrudi nyumbani nikiwa sijaacha chochote, bado nakuta chakula, ...na kila nikitaka kufunua mdomo kumuuliza mke wangu najikuta nashikwa na kigugumizi,ungesema nini tena, huna kitu, nilijua ni jitahada za mke za hapa na pale, ...sikufikia kumdahani mke wangu vibaya...ila  nilishafikia wakati, nilitaka nimuulize...bahati mbaya ndio yakatokea haya ya kutokea.


‘Sasa shemu, nilitumai wewe umewahi kuja hapa jela, kwa nia ya  kunisaidia mimi nitoke hapa, hapa sio sehemu nzuri, na natakiwa kufuatilia maswala ya...ooh, hata sijui kinachoendelea,..sasa wewe kumbe  umekuja kuniongezea maumivu tu, huo ndio ubinadamu gani shemu,?’ nikauliza.

‘Hahaha, mimi nije kukusaidia wewe,...kama ningelipewa nafasi, ya kukufanya chochote,mimi ningekukata kata vipande niwe nameza nyama yako..na kuitema, mimi nakuchukia, unajua kuchukia, we acha tu, lakini siku zinahesabika ..utakuja kuona ..’akasema kwa sauti ya kibabe.

‘Lakini kosa langu ni....’ kabla sijamaliza, akaendelea kusema;

‘Na nikuambie ukweli... kama ingelifaa, mimi ninataka wewe wakufunge ufie huko huko jela,..hapo ndio moyo wangu utatulia, lakini kwanza, kabla hujaenda kuzimu..nataka unilipe..na malipo yangu, kama nilivyokuambia, ...’akatulia.

‘Kuwa ....’nikataka kuongea anakiniashiria kwa mkono ninyamaze kwanza

Nimeshakuambia...nataka nyumba , hilo sikutanii...mimi nitakuja na hati ya makubaliano, ..la sivyo, jamaa mwenye deni atakuja kwako...unamjua alivyo...na ukumbuke yeye anajua mengi kukuhusu wewe...si niliwahi kukugusia,...anakujua fika, kuwa wewe ni muuaji, ..lakini nilikudhamini mimi...’akasema.

‘Sasa kwanini wewe ulinidhamini...?’nikauliza sasa kwa mashaka, maana niliona kweli huyu mtu alinitega.

‘Hahaha, bwege mkubwa wewe..nilishakuambia, mimi siwezi kukufanya jambo kwako lenye manufaaa na wewe..., maana wewe ni nani kwangu, muuaji mkubwa wewe, usitake ni badilike hapa, ..’akanisogelea, nilijua kichwa kinakuja nikakwepa hewa.

‘Hahaha, unakwepa nini sasa, mimi sio mjinga,... hapa siwezi kukufanya hivyo, ila ujue jambo moja, wewe na mimi, ni kama mafuta na maji, eeh, na ,...utajuta kuzaliwa kwa ulichomfanyia dada eeh...sijaanza malipizo yake bado...’akasonya.

‘Lakini ..eeh ili twende sawa, niume na kupiliza...fanya nilivyokuambia,...na unaweza kuona utanivunga, au utasita kukubaliana na mimi...kwanza ukumbuke, mimi ndiye nilitoa kauli ya kukusaidia,..lakini ile ni kauli tata,....bado haina mshiko, kuwa, nilisema hivyo, kuwa dada yangu alikupiga,..hiyo haina mshiko saana, ...’akawa ananichoma choma ni kidole kifuani.

‘Mimi naweza kuitengua hiyo kauli wakati wowote..kumbuka jela kulivyo...eeh, uliponea tundu la sindani, unakumbuka, eeh...sasa kule ni cha mtoto, huko..Ukonga, kule wapo jamaa zangu wengi tu, tunajuana...usijali kwa vipi..., nilishawatipu, ukikanyaga tu pale Ukonga, wewe ni chakula chao, utashindwa hata kutembea..hahaha...’akasimama na kuanza kuondoka.

Nilibakia nimeduwaa...maana nimjuavyo huyu jamaa hana utani, akisema jambo, hatanii....nitafanya nini sasa, dada yake wa kunitetea ndio hivyo hayupo,..jamaa aliponiona nimeduwaa, akarudi na kuanza kunipiga piga begani kwa ngumi kama kunipa moyo, lakini upigaji wake  unahsi  maumivu...nikawa najaribu kuukwepa huo mkono.

‘Sikiliza hii ni dili, hati inakuja,..tena sio kesho leo...na jiulize ni kwanini hadi sasa hujapelekwa Ukonga, eeh...jibu unalo, si ndio hivyo, mimi natoka hapa, nakwenda kwa mwanasheria wangu, keshaikamilisha hiyo hati,..nikirudi tutaelewana, ..’akahema kidogo.

‘Shemu,....’nikataka kusema neon, jamaa akanitolea macho,...halafu akasema;

‘Hata hivyo, wewe una thamani gani..ulitakiwe ufe...nyumba ile ni yangu kwa hivi sasa,..na mimi nitamlipa huyo anayekudai, unasikia, mengine niachie mimi...natumaii umenielewa, mimi sitaki longo longo...unanijua nilivyo..’akaanza kuondoka.

 Kabla hajafika mlangoni, mlangoo ukagongwa, jamaa akavaa miwani yake kwa haraka, mlango ukafunguliwa, mtu wa jamii akaingia, nyuma yake yupo mtu wa dini. Nilifahamu huyo ni mtu wa dini kutokana na mavazi yake, ..moyoni nikasema, huyu mtu wa jamii hana la kunisaidia, yeye kaenda kunileta huyo mtu wa dini  ili aniombee..kuombewa kwa hivi sasa kutasaidia nini kwa hali kama hii.

‘Hapa ninakabiliwa na kesi ya mauaji...na huyu shemu sasa hivi tu, kaniletea janga jingine, anataka nyumba iwe yake kitapeli,..nitafanyaje sasa...nyumba ndio mali yangu pekee ya kujivunia, kiukweli ni nyumba nzuri, na niliijenga kwa gharama kubwa sana...’nikawa nawaza hivyo.

Shemu akasita kuondoka akawa kasimama, na mtu wa jamii, akamsalimia ..lakini shemu hakuitikia hiyo salamu, jamaa akawa kama kashikilia mlango, lakini akawa kasimama tu.

‘Nimekuja, ..kuanza kazi, ..na..huyu ni mtu wa dini, kuna mambo nataka atusaidie,..nikuulize jambo moja,.’akasema mtu wa jamii, kwanza akageuka kumuangalia shemu, shemu akajifanya kama anataka kufungua mlango, lakini hakufanya hivyo kwa haraka.

‘Umeshapata taarifa yoyote, ya kuhusu mkeo, ..je kuna taratibu zozote, maana nijuavyo mimi , nilivyosikia,..mwili wake umehifadhiwa, sehemu ambayo haitakiwi kuonekana...’akasema mtu wa jamii.

‘Mwili wake una maana gani kusema hivyo...?’ nikauliza sasa kwa mashaka, ujue kukweli kuna hisia mbili akilini mwangu, kuna hisia ambayo, bado inatamani kuwa mke wangu bado yupo hai, nyingine inahisi kuwa mimi nimemuua mke wangu.

‘Ina maana huna taarifa hizo, au...?’ akasema mtu wa jamii, sasa na yeye akionyesha wasiwasi Fulani hivi.

Sasa sauti ikatokea mlangoni...

‘Una unakika na unachokisema wewe, ni nani wewe kwanza, wa kumuongelea dada yangu, eeh..mwili, mwili, .....?’ ilkuwa sauti nzito ya shemu, na sasa alikuwa anakuja kukabiliana na mtu wa jamii, sote tukabakia kushangaa,  tukawa tunamuangalia tu..nilitaka kumuambia mtu wa jamii awe makini, maana huyo jamaa kichwa kinamtoka kama mshale..


WAZO LA LEO: Tuweni makini na mikataba tunayoandikishana, hasa ya madeni,na ikiwa ni lazima kuandikishana hivyo, tuhakikishe tumepata ushauri wa mawakili, kabla hatujaweka sahihi zetu,..kwani sio kile anayekuchekea, ana furaha na wewe.
Ni mimi: emu-three

Wednesday, October 23, 2019

CHUMA ULETE 2


‘Chuma ulete...!..’nikang’aka. Na msimuliaji wa hiki kisa akatabasamu japo uso ulionekana na huzuni, na alikaa kimia kwa muda.

‘Una maana gani au ndio hizo imani za watu kuwa,...’ nikamuuliza pale nilipoaana yupo kimia.

'Ndio,...chuma ulete... ndivyo alivyoniambia hivyo mke wangu, mke ambaye awali hakupenda kabisa imani hizo za kishirikina,...uchawi tuseme...kiukweli nilishangaa kidogo, kwani awali hakuwa akiamini mambo hayo..'akasema, na kutulia kidogo

'Nikajaribu kumuasa mke wangu kihekima na kiimani, unajua tena...eeh...kuwa uchawi upo sikatai, lakini ukimuamini mungu, ukamuomba yeye, bila kuweka nafsi ya shiriki, huwezi kushindwa jambo..’akasema.

‘Na nikaendelea  kumuasa...’

''Mke wangu, tusiamini sana hayo mambo maana ukiyaamini sana hayo mambo, mwisho wake utaingia kwenye shirki, na imani yetu haitaki hivyo, ...nikamwambia mke wangu’’.

Awali alijifanya kunielewa, lakini mambo hayakuendelea hivyo....’msimuliaji akaendelea kuongea, na alipofika hapo alitulia kidogo.

'Kwa vipi...kwani kulitokea nini tena zaidi...'nikauliza sasa nikiwa na shauku zaidi.

'Sikuacha kumnasihi, mke wangu, nikijua kuwa mimi ndio  mume wake, na mimi ndiye kichwa cha familia,  unasikia sana...’akasema.

‘Sawa kabisa...’

‘Lakini..eeh, ndugu yangu wee, kumlea mtu mnzima ni kazi sana..ni mpaka yeye mwenyewe akubaliane na wewe...moyoni nikadhamiria kutumia nguvu japo kidogo.., mimi najua wengi watanilaumu sana kwa hilo, unajua ni kwanini nilitaka kufanya hivyo, kwa akili yangu, niliona bila hivyo, hataweza kuachana na ushetani huo...sumu ya ushetani, ilishapenyezwa kwenye ubongo wake,..’akatulia.

‘Sijakuelewa...’nikasema.

‘Yule mke niliyemuamini...ambaye nilikuwa namuasa jambo, ananisikia kwa unyenyekevu. Yule mke mpole, mwelekevu, hakuwa yeye tena, najuta kwanini nilimpatia nafasi hiyo ya kujichanganya...nahisi tamaa za nafsi na ushawishi wa mashoga, vilishamteka nafsi yake...’hapo akahema kwa nguvu.

‘Ndugu yangu makosa yaliendelea kujirudia, kidogo kidogo,akawa sasa haambiliki,hata kauli zake zikawa za kijeuri jeuri hivi, japo sio kwa moja kwa moja...kila hatua akawa ananipandisha presha...'akaendelea.

Niliumia sana..ilifika mahali naanza kukata tamaa, nilimpenda sana mke wangu, sikupenda abadilike, sikupenda, nije nianze kutumia nguvu, maana naogopa...naogopa sana kupiga,...naogopa sana, najijua nilivyo, nikianza..sirudi nyuma, nina hasira za mbali lakini zikipanda, ooh, ndugu yangu...sitaki kuua tena...’akasema na kushtuka, nahisi hakupenda kutamka hivyo.

‘Kuua tena, ina maana uliwahi kuua...?’ nikauliza kwa mshangao.

‘We acha tu, hayo yalishapita....samahani kwa hilo, limetoka tu..sija-jawahi..ku-kua bwana...’akasema sasa kwa kusita sita.

***********

Kisa kikaendelea....

Haikupita muda, hali ikaanza kubadilika, maisha yakaanza kuwa magumu, biashara haziendi , pesa haikamatiki...sikufichi,...kuna wakati imani ikaanza kushuka, maana unaambiwa mengi,..wanakushauri wengi..fikiria kutoka maduka hadi...genge la nyanya mbili tatu, na...ikawa mbaya zaidi ya hapo, hata ingelikuwa ni wewe....ila,  hata hivyo, sikufikia hatua ya ...kuamini maneno ya mke wangu...’akatulia kama anawaza jambo.

‘Maneno gani...?’ nikauliza kama sijui.

'Umasikini ni mtihani ndugu yangu, ...tatizo sasa ikawa kwa  mwenzangu yeye anaendelea kudai matumizi tu, hata pale ninapomwambia sina kitu na wakati mwingine anafikia hata kunikasirikia,..na kuanza kutoa maneno ya kashfa...sikupenda hilo....maana alivuka mpaka...’akaendelea bila kujali swali langu.

'Mke wangu hali unaiona, na mitihani hii ni kawaida kwenye familia, awali ulikuwa unavumilia nakueleza kitu unanielewa,... hivi nimekosea nini mke wangu, kosa langu mimi ni kukupatia uhuru, au...?’ nikamuuliza.

‘Hapana mume wangu, nahisi kosa ni la kwangu mimi....kukuambia ukweli...’akasema

‘Ukweli upi...?’ nikamuuliza.

‘Aaah..sitaki tena kuongea...maana wewe ndio mume...nitasema nini tena mbele yako, nina nini tena mtoto yatima,...wewe ndio baba, wewe ndio mama yangu...’akasema.

‘Nahitajia ushauri wenye tija, sio imani haba na mambo ya kuambiwa..’nikasema.

‘Nikushauri nini tena mume wangu, ushauri wangu nilishakuambia,..kwanza nilikuambia tujiunga na michezo ya kupeana, hukukubali, ..na..na hali hii ambayo nimeshaiona, wewe hutaki kuniamini..mume wangu tatizo lipo humu ndani...’akaniambia na kabla sijamkatisha akaniambia

‘Najua unanidharau, kwa vile ni mwanamke,..sio vibaya,...lakini ..mmh,...mimi  kuna mambo nayaona, ila wewe hutaki kuniamini....utakuja kunikumbuka kwa hili...’akasema kwa sauti ya unyonge.

‘Una maana gani...?’ nikauliza sasa nikimuangalia kwa mashaka mashaka.

‘Mume wangu, u-meingiliwa na chuma ulete...fanya haraka kabla hali haijawa mbaya...’akasema sasa akishika kichwa na kuangalia huku na huku kama ana wasiwasi ...na ile hali ya kukuna kuna kichwa, kama kinamuwasha ikanipa mashaka.

‘Nini.....’nikang’aka hivyo, nikimuangalia kwa kumkagua akijikuna kuna kichwani.
Kiukweli hadi hapo mimi  nilishaamini, mke wangu sio mwaminifu tena...nilimuona kama anajifanyiza tu, kunivunga mimi.

  Unakumbuka nilivyokuambia awali, huko nilipomtoa mke wangu, sifa yake kubwa ni uaminifu...hadi hapo niliona ni uwongo, labda ...walinidanganya...... awali ilikuwa hivyo sio sasa..na hebu niambie, hata kama ingelikuwa ni wewe..ungefanya nini hapo, maana sio mara moja, au mbili...imekuwa ni kawaida,..’akasema akiniangalia mimi usoni.

Hapo sikuwa na jibu la kumuambia, nikasubiria aendelee...

**********
Unajua tena, katika kuishi na watu unaweza ukawa na marafiki, na kati ya hao, ikatokea mmoja au hata wawili ukawaamini, japo mimi nina hulka yangu, sio rahisi kumuamini mtu,...hasa kwenye maswala ya imani, msimamo wangu ni thabiti.....kuna rafiki yangu mmoja, muungwana, ana busara sana, siku moja nikaongea naye nikitaka ushauri kwake.

‘Ndugu yangu kabla hujaanza kuingia huko, kwenye hasira, mkaja kukosana wewe na mke wako, hebu fanya uchunguzi wako wa kina..yawezekana tatizo lipo humo humo ndani, au...majirani,..siwezi kukupinga, au kupinga mawazo ya mkeo, maana hayo mambo yapo....’akanishauri.

‘Yawezekana tatizo lipo humo humo ndani kwa vipi...?’ nikauliza hivyo.

‘Yaani...yawezekana...ila...uchunguzi kwanza, usiwe na papara...’akasema.

‘Unajua ndugu yangu, mimi nimefanya kila uchunguzi, sijawahi kuona dalili ya kumshuku mtu baki, na nikuambie ukweli nyumbani kwangu watu hawaingii mara kwa mara, wananiogopa...’nikasema.

‘Sawa....lakini ...’nikamkatisha.

‘Ninasema hivyo kwasababu..mke wangu nilishamkanya,..sitaki majirani waingie ndani, mimi naafahamu sana majirani wangu...kwahiyo, kama ni kukutana na hao watu watakuwa wanakutana huko huko nje hasa  hao mashoga , waliomuharibu akili yake...mimi sina mfanyakazi wa ndani au ndugu ninayeishi naye, ni mimi na mke wangu tu...’nikasema.

‘Kwahiyo shaka yako kubwa ..ni kwa mke wako..si ndio hivyo..?’ akaniuliza.

‘Siwezi mshuku mtu wa nje..sijui unanielewa hapo...shuku itakwendaje nje kwanza, eeh... pesa ipotee humo humo ndani...na nipo mimi na mke wangu, nitamshukuje mtu wa nje kwa vipi, mlango haujavunjwa,...sijui unanielewa hapo....’nikasema kumuamboa huyo rafiki yangu.

‘Basi...vuta subira..ngoja nilifanyie hilo kazi rafiki yangu..’akaniambia huyo rafiki yangu. Kwa pale, sikuelewa, atalifanyiaje kazi, hata hivyo sikutaka kumdadisi, nikaachana naye...maana akili ilikuwa na mikakati mingine ya kibiashara.

***********

Siku moja  nikarudi nyumbani mapema....nilikuwa na pesa nimekopa mahali..., kwa ajili yakuanzisha biashara tena.., niliona nianze mtindo huo wa kukopa na kurejesha, labda nitafanikiwa, japo nianze kidogo kidogo.

Nilishapanga bajeti yangu vyema, iliyobaki ni kununua vifaa na kuingia sokoni,..kiukweli nilishapanga nitoke, kihivyo, ...na ndoto nyingi za Alinicha ziliuteka ubongo wangu, si unajua tena, ukikwama, na ukaja kuzishika pesa, ...mmh, akili inakuwa na mengi sana.

Pamoja  na shauku ya biashara,...bado  mwili ulikuwa hauna nguvu, sijui kwanini siku ile ilikuwa hivyo, na hali ile..ilinianza pale nilipozishika hizo pesa, nahisi hivyo.....maana hata kula sasa kulikuwa kwa shida, mawazo mengi kupitiliza.

Nikafika nyumbani...sikumkuta mke wangu, nikajua katoka kidogo, nikavua koti langu, nikatundika kwenye kabati la nguo...sikuwa na shaka, kwenye lile koti ndio niliweka pesa, nikajilaza kitandani...sijui usingizi ulitoka wapi, ...mwili ukalegea,...sijui nielezeje, nikashikwa na usinginzi mnzito ajabu,...nashtuka nasikia mke wangu anaongea nje...anaagana na mtu.

‘Kwaheri ...’

‘Kwaheri...’

Mimi kwa haraka  nikashtuka nikikumbuka natakiwa kwenda kununua bidhaa muda umeshapita, hata sijui kama nitakuta maduka ya jumla yapo wazi..sikukata tamaa, na sikupenda nilale na hizo pesa ndani, nikiogopa hayo yanayoendelea, hapo ilishafika jioni kama saa kumi na moja hivi.

Nikachukua koti langu,..nikavaa, wakati navaa,  mke wangu akaingia, aliponiona akashtuka, na kusema;

‘Oh, la azizi wangu umerudi mapema leo....,vipi kuna tatizo, sikujua kaam upo humu ndani.. kumbuka kauli hiyo,...’

‘Ndio mke wangu,...ume-rudi saa ngapi...?’ nikauliza, na kbla hajanijibu nikasikia mtu anagonga mlango.

‘Ni nani tena, kwanza sikiliza ,maana nimechelewa, nataka kutoka, nikirudi tutaongea vizuri..’nikasema,

Mke wangu akatulia akinisikiliza huku mtu anayegonga mlango anaendelea.

‘Sasa sikiliza....chukua pesa hii ufanye fanye mambo, japo ni pesa ya kukopa, lakini aheri, ntoe kidogo, tule chakula kizuri leo japo kidogo...au sio mke wangu’nikasema sasa naingiza mkono mfukoni kutoa pesa,..mkono ukazunguka kwenye mfuko wa koti...moyo ukaanza kunienda mbio, siamini.....


WAZO LA LEO: Tusiwe na tabia ya kuzania dhana mbaya, kabla hatujafanya uchunguzi wa kutosha,..dhana mbaya, hupunguza imani moyoni.
Ni mimi: emu-three

Monday, September 23, 2019

KILA MCHUMA JANGA...2



KILA MCHUMA JANGA.....

'Mwiziii, mwizi...'ni kelele za asubuh, asubuh....haikupita muda, tukaona moto. Ulikuwa moto mkali na mlio wa kitu kama kinapasuka ukasikika...
Awali tulijua ni ajali...kwa haraka mimi nikajongea japo sio karibu na kwenye tukioa...nikaona watu wakimbeba mama mmoja...

‘Vipi ni ajali ya moto...?’ nikauliza

‘Hapana, ni mwizi...’akasema jamaa mmoja akikimbia mbali na eneo la tukio, sikupenda hili tukio linipite, mwizi..halafu moto, akilini nikahisi vinginevyo, lakini mwizi ..adhabu yake iwe hiyo, akili haikunipa amani, nikazidi kusogea, na watu wakawa wanakimbia ..nikajua huenda ni polisi, nikasimama, na bahati nzuri wakatokea watu wengine walikuwa hawana hawakimbii

‘Vipi moto wa nini ule...?’ nikauliza..


'Ni adhabu ya moto, hao watu dawa yao ni kuwachoma moto tu..'akasema shuhuda mmoja.


'Mumemchoma moto kibaka!' Mzee mmoja akang'aka huyu alikuwa miongoni mwa hao watu, lakini alionekana na huzuni kubwa usono


'Ndio....nyie wazee ndio mnatufugia wezi,...’akasema shuhuda

‘Lakini sio kwa adhabu hiyo, mnaona Yule mama yake alivyopoteza fahamu, mimi namfahamu sana Yule mama, mimi namfahamu sana huyu kijana ..mareh-hemu...’huyu mzee akasema sasa kwa uchungu.

‘Mzee, na bado..hata Yule kijana wako..siku zake zinahesabiwa,....hawa watu wanatusumbua sana , tunafanya kazi, tunaumia huku na kule, hawa, vibaka, watoto wa hawa wazee...wanatuibia, leo zaa arubaini zake zimefika,.hiyo ndio adhabu yao...' akasema mtu mwingine.

‘Sawa...nyie hamjui tu..sisi wazee, tumejichokea, twawategemea nyie...sasa kama mnaiba sisi hatujui tufanyeje...eeh, sikizliza niwaambie..yule mama, ni mama mjane, na Yule mtoto alikuwa mtoto wake pekee...yule mama ana maradhi mabaya sana, dawa zake ni aghali kupundikia,..na mtoto wake alimuahidi mama yake, atamuhudumia ,,mpaka mwisho..’akasema mzee

‘Ndio atuibie...’akasema Yule shuhuda.

‘Sikiliza sasa nikuambie, ulisikia Yule mama kabla ya kupoteza fahamu , baada ya kushuhudia mtoto wake akiteketea na moto alisemaje...’ni kosa langu, ni kosa la maradhi yangu..sasa nitaishije, na mimi nichomeni moto...ndio akapoteza fahamu..mnafahamu fumbo hilo..nawaambia ukweli...kwa hili hamtaishia kwema, ...’akasema huyo mzee

‘Mtatuloga eeh, ndio mnafikiria hivyo, mzee, nakuambia hili na usikie....hamtuwezi mzee, sisi tunalindwa na damu.....’sikusikia alichoendelea kuongea, mimi akili ilishazama kuwazia, kauli ya huyo mzee...

‘...yule mama, ni mama mjane, na Yule mtoto alikuwa mtoto wake pekee...yule mama ana maradhi mabaya sana, dawa zake ni aghali kupundikia,..na mtoto wake alimuahidi mama yake, atamuhudumia ,,mpaka mwisho..’

Nikapanga nije kuongea na huyo mzee, nikisikie kisa kamili cha huyo mama mjane...


Leo asubuhi hii...., eneo la relini, huko Kipunguni... wakati tunapita tukashuhudia moto ukiwaka, kuulizia, tukaambiwa ni mwizi wa bajaji anachomwa moto....!


‘Mhh..mwezi tena, na adhabu yake ni kuchomwa moto ....hivi kweli  mwizi adhabu yake ni kuchomwa moto, nikauliza wenzangu, na mjadala ukazuka.....sitapenda kuuandika  huo mjadala hapa, jadilini na wenzeko uko mlipo,...

 
Ni kweli huyo mwizi anayechomwa moto  akawa ni jambazi kweli na kiukweli..., jambazi ni muuaji, anaiba hata kuua, huyu, kwa vile anaua, ilitakiwa naye auwawe...hata hivyo, jambazi akifikishwa jela...kuna sheria za haki za binadamu, zinawatetea, kuwa muuaji asiuwawe...hapa sasa naona ajabu, kibaka anachomwa moto!


'Jambazi alianiza huko kwenye ukibaka..tunatakiwa tumuwahi mapema, kwa kumchoma moto...’nikakumbuka kauli ya Yule shuhuda.
.
‘ Hii sasa ndio adhabu ya wezi,...’alisema mwingine, swali nikamuuliza, je wewe hujawahi kuiba, ofisini kwako kila siku unamuibia muajiri wako,...nawewe dereva wa bajaji, kila siku mnawadhulumu abiria, ...

‘Lakini sisi tunaiba kiujanga...’wakajitetea

Huko tupaache....


 Tujiulize swali moja, ni kwanini raia wanachukua sheria mikononi mwao..na hili kosa la wezi, wavunja sheria, ni kosa la nani, ni nani alaumiwe...

Raia wanajitetea kuwa wameamua kufanya hivyo kujichukulia sheria mikononi mwao, eti..wezi hao wakikamatwa, wakipelekwa vituoni, kesho yake wapo mitaani,..hata jambazi katetewa na haki za binadamu, karudi mitaani tena ..sasa ni ni jamabazi sugu , mwaliwa wa majambazi... je hili ni Kosa ni la nani...!


Kuna wakati tuliandika habari za majirani kugombana, kisa ni mtoto... !


Mtoto kadokoa kitu cha jirani, mzazi jirani akamuadhibu huyo mtoto mdokozi, mama wa mtoto mdokozi akaja juu, kwanini mwanae kachapwa, ikawa kesi, maana kesi ya mtoto, iliwafanya wazazi wa pande mbili kuingilia kati na kuanza kugombana...hili ni janga..tumelianza wenyewe..sijui mnanielewa hapa...


Tatizo huanzia hapa, tunalichuma janga sis wenyewe na kuliingiza majumbani kwetu...janga hili limeanzia kwenye malezi ya watoto, hakuna elimu ya dini, ilitakiwa shule za watoto wadogo ziwe za kidini, iwe ni sheria, watoto chini ya miaka saba, kwanza wapiti shule za kidini..tutengeze kizazi cha waumini wa kweli..dini mnazipiga vita mnategemea nini...majanga tunayapanga sisi wenyewe.
.
Jukumu la ulezi wa watoto huanzia kwa mzazi, sawa..jirani ni mzazi, sawa, je jirani yupo tayari mtoto wake aadhibiwe na mzazi mwimngine..hilo hatupendi..serikali, nayo vipi,...kwanini mnataka shule za watoto za kufundidhs lugha za kigeni,lakini swala la dini, la kuwajenga watoto kiimani hamlipi kipaumbele..eti mnaogopa imani kali..haya tuone,...kama mtu hamuogopi mungu wake ataogopa kuiba,na kuiba, sio lazima bajaji,..hao walanguzi,wezi wa mali ya umma, wao sio wezi kwanini hawachomwi moto, tusipolitambua hili, tutakuwa tunajenga janga...!


Nawausia enyi wenzangu, yapo mengi tunayapuuzia, vizazi sasa vinaharibika, tuanze sasa kuchukua tahadhari...elimu ya dini inahitajika sana..tena sana, ...elimu sio lugha tu, lakini kuna elimu muhimu ya IMANI..ya kumuogopa Yule muumbaji wetu, ili mtu aaogope kuiba hata akiwa peke yake, tusipolitambua hili, basi tutarajie kuzalisha wezi, mabaradhulu, mashoga..wavuta unga...nk...na amani itakuwa ni msamiati adimu. Wahenga walisemaje, Kila mchuma janga..., itakuwaje vile...



Ni mimi: emu-three

Friday, July 12, 2019

IMANI HUTOKA MOYONI


IMANI YA KWELI HUTOKA MOYONI , NA SIRI HIYO AIJUE NI MOLA PEKEE.

Hiki sio kisa ni ukweli,

Katika maisha yangu… niliwahi kuajiriwa kwenye kampuni moja, nilipofika hapo nikazoeana na msichana mmoja,…nilimzoea kwa vile yeye ndiye alinikaribisha, na kunionyesha mazingira ya hapo kazini, ufanyeje, uende wapi kiutawala na sehemu ya kula, ofsini ipi ni ipo, vitu kama hivyo.

Basi kila nikihitajia kitu namuuliza yeye, na kiukweli hakuwa na hiyana, aliweza kunielekeza vyema tu, na kuna muda watu wakaanza kutuangalia kwa macho ya kujiuliza, huenda tumekuwa marafiki, lakini moyoni mwangu sikuwa na mawazo hayo kabisa.

Siku zikapita, na ule ukaribu wetu na huyo mdada ukapungua, maana sikuwa na cha kumuuliza tena, mimi nipo idara nyingine na yeye yupo idara nyingine, …sasa katika mazungumzo, nikaja kujua kuwa huyo msichana ni wale wenye msimamo mkali…mtakuwa marafiki lakini sio kwenye tendo la ndoa.

‘Huyu dada ni bikira bwana,…’watu wakawa wanamtania.

‘Labda bikira wa sehemu nyingine, mimi sidanganyiki  ‘mmoja akasema.

‘Kwanini, na wewe unamfahamu, tokea tuajiriwe hapa ulishawahi kumuona na mvulana, ..maana hapa hakuna siri, na hata huko nyumbani kwake si unakufahamu, uliwahi kumuona akiwa na mvulana..?’ akaulizwa.

‘Siri ya mtu anaijua yeye mwenyewe..ila mimi siamini kwa umri ule, atakuwa bado bikira, ni lazima atakuwa na mtu wa siri..’akasema huyo jamaa, na wengi hawakumshabikia, waliona ni wale wasiopenda maendeleo yaw engine.

Ikawa ni utani tu, wengi wakawa wanamtania huyo mdada kwa kumuita ‘sister bikira..’ akawa anaitwa hivyo.

Kiukweli mimi sikuweza kumuuliza huyo mdada kama hayo maneno na utani yana ukweli ndani yake,..niliamini kuwa yawezekana,…mtu ukiamua unaweza ukaishii hivyo,, na kwa vile ule ukaribiu wetu wa kumuuliza hiki na kile ulishakwisha, nikawa sikupata muda wa kuwa naye karibu tena, kila mtu kwenye idara yake na maisha yakaendelea.\

 Ila mimi niliamini waliyosema watu kuwa huyo mdada ni mgumu, sivyo kama walivyokuwa wanadada wengine, huyo mdada hakuwahi kuwa na rafiki wa kiume, niliyewahi kumuona au kuambiwa …kama ilitokea kukutana naye hasa kwenye chakula maana tulikuwa na mgawahawa wafanyakazi wote hukutana humo, huyo mdada..alionekana kivyake vyake tu..na ole mvulana ajaribu kumgusa, hata kiutani, ataambulia matusi,…

Hapo kazini karibu kila mmoja alijulikana ni nani na mwenzake wa jinsia tofauti ni nani, na wengine wakatokea hata kuoana kabisa,…lakini kwa miaka kadhaa niliyofanya hapo, sikuweza kumgundua rafiki wa huyo msichana…moyoni nikasema,..basi huyo ni ‘sister bikira kweli’.

Miaka kama miwili ikapita…nikaja kufikiria kama mimi nina tabia yangu kuwa  msichana wangu wa kwanza kukutana naye nikutane naye ndani ya ndoa, sasa kwanini nisifanye urafiki na huyo mdada, ambaye naye anaonekana ana msimamo huo..lilikuwa wazo katika kuhangaika kumpata mwenza wa maisha, ilikuwa wazo, na nikawa na mikakati hiyo, lakini siweza kulifanikisha, maana kiukweli moyoni sikuweza kuvutika na mdada huyo kimapenzi. Nafsi hupenda kile kinachomvutia mtu.

Bahati mbaya, nikahama hiyo kampuni…

Baada ya miaka kadhaa, nikasikia, kuwa yule msichana kafariki,

‘Kafariki!!!... ilikuwaje jamani…?’ nikauliza kwa mshangao na masikitiko.

‘Alianza kuumwa, umwa..akawa anapungua, baadae akazidiwa, anatibiwa, anapona hali inarejea, anaanza kuumwa tena,..baadae..akapelekwa kwao…yaani binadamu hubadilika haraka sana, unamfahamu jinsi alivyokuwa mrembo,...watu waliomuoana kipindi kazidiwa, wanasema ule urembo ulikwisha akawa kama mzee, alikuja kubadilika akawa…mweusi….’akasema jamaa,

‘Mhh...kwasababu ya huko kuumwa au, , kwani alikuwa anaumwa nini…?’ nikauliza moyo sasa ukinienda mbio. 

Unajua kipindi cha nyuma, watu wakiumwa sana, na kukonda, na kubadilika mwili, moja kwa moja unajau ni ugonjwa gani,..kipindi hiho kulikuwa hakuna dawa za kusaidia kuongeza nguvu, kwahiyo watu wengi waliougua ugonjwa huo, waliteseka sana kabla ya umri wao kuisha. Kwa vyovyote iwavayo kila mtu ana umri wake.

‘Unauliza jibu bwana, mdada alipatwa na maambukizi, na ..huwezi amini, ..hata ndugu zake hawakuamini wakasema kalogwa, lakini hakuna siri, aliyemuambukiza aligundulikana, kwani naye kwa kipindi hicho alikuwa akiugua ugonjwa huo huo..na alipoulizwa, yeye alidai huyo mdada ndiye kamuambukiza, lakini uchunguzi zaidi ulionyesha kuwa huyo mvulana alikuwa hajatulia, yeye ndiye alimuambukiza huyo msichana.

‘Mhh..lakini si mlisema huyo mdada ni bikira.

‘Hahaha, tulijua hivyo, kiukweli hata mimi niliamini hivyo…hadi msichana huyo anafikia kuumwa, sote tuliamini hivyo….’akasema.

‘Haiwezekani…japokuwa kila kifo lazima kiwe na sababu..nahis aiumwa maradhi mengine tu..hata hivyo....’nikasema na jamaa akanikatisha kwa kusema.

‘Iliwezekana sasa, na alitembea na cha pombe fulani, wakati yeye alikuwa akituzarau pale kazini kuwa hatuna maana, walevi, eeh..si unakumbuka, alivyokuwa,akitudharau, ...wewe uliondoka, sasa ilifikia mahali hamgusi mtu....anasema yeye ana bwana wake yupo Ulaya...sasa kumbe alikuwa na mvulana cha pombe tu..hakuwa na hadhi kwa yule mdada,…sijui ilikuwaje..masikini mungu amsamahe tu...’akasema huyo jamaa.

‘Kwani hamkujua ilikuwaje..?’ nikauliza.

‘Aaah. ilikuwa kujulikana dunia hii ina siri,na kwa vile alikuwa akiringa, jamaa zake walikuja kuvujisha siri..tukajua kila kitu, ikawa kufuatilia kuhakiki tu....unajua msijifanmye mna imani sana ya dini, aheri muwe kama sisi...unajua imani. ya.kweli ya mtu aijue ni mungu pekee, ujidanganya ipo sisku imani hiyo inataisha kidogo kidogo kama mshumaa unavyokwisha halafu utakuja kuumbuka, ila niliumia sana, yule mdada nilimpenda, nilitamani nimuoe, akanikataa,…’akasema huyo jamaa akionyesha kusikitika.

'Mhh..lakini kweli wewe ukizi  kulewa, nani angekubali umuoe....'nikasema kwa utani.

'A wapi mimi nilikuwa nakunywa kistaarabu, sema, ndio hivyo kila kitu kwa wakati wake, ni kweli kuna muda nilizidisha, nikaumwa karibu ya kufa...kifua ikawa TB,...aisee, nilijua nakufa...nilipopona nikabadilika, ...hapo nikaona umuhimu wa kuoa...sasa huyo mdada alitolea nje kabisa, ..'akasema

'Labda alikuwa na mtu wake kweli...'nikasema

'Ndio yupo jamaa mmoja yupo Ulaya kweli, lakini jamaa huyo akaja kumuoa mzungu, na ndio maana huyo mdada akachanganyikiwa akaanza kulewa...japo hakujionyesha,...nasikia ndio hapo akaja kukumbana na cha pombe..lakini kwa siri kubwa...hayo ni mambo ya ndani, ...'akasema

'Oh, siku zake zilishafika...'nikasema

 Ni kweli kwa taarifa za kifamilia, japo ilikuwa siri, msichana huyo alifariki kwa HIV, kutokana na dalili, na hata vipimo,  kiukweli mimi sikuamini, wengi hawakuamini..japo kwa hivi sasa HIV, unaweza kuipata kwa njia nyingine ila kwa huyo mdada ilikuja kuthibistishwa..aliipata kwa namna gani

Watu katika kuchunguza sana, kumbe, huyo mdada alikuwa akitembea na mvulana kwa siri sana kwa vile alikuwa ni jirani yake..ilikuwa ni kwa siri sana…wanasema alifanya hivyo kwa siri, na hakufanya kwa vile anampenda huyo mvulana, maana kiukweli hawakuwa wanaendana..ila kulikuwa na sababu za kuchanganyikiwa....

Ilivyoonekana, alifanya hivyo, pale anapozidiwa, mawazo na mengine yaliyokuja kusemwa baadae msichana huyo akatokea kuwa mpweke, alikuwa hana rafiki tena, akawa anawachukia wanaume, kila mwanume kwake ni sawa na huyo aliyemuacha solemba, swali likawa ilikuwaje huyo cha pombe amuone sio sawa na wanaume wengine.

Tatizo huyo msichana hakupenbda kuwa muwazi, na .maumbile ya kibinadamu hufikia sehemu utashindwa kuvumilia hasa ukiwa unatumia kilevi..kiukweli yasemakana, siku katika masiku ubinadamu ulimzidi, akakwaana na huyo mvulana, ilikuwa kwa bahati mbaya tu kama alivyokuja kusema..

'Hiyo bahati mbaya, ikaja kuwa mazoea hasa akizidiwa, 'alijitetea.

'Ilikuwa nawaza sana, ..mpaka nataka kujiua,...sasa huyo mvulana akawa ndiye mtu wangu wa karibu wa kuniliwaza,,,akawa anakuja kwangu, usiku wa manane maana nilikuwa naishi naye nyumba moja sema ni chumba tofauti, wote ni wapangaji'

Kiukweli huyo msichana  hakutaka kabisa watu wajue, na kiukweli hakumpenda kabisa huyo mvulana,..na yeye alitaka watu wajue kuwa yupo hivyo, ..bikira. Ila kilichoharibu ni kwa sababu ya huyo mchumba wake kumtelekeza.

Na zaidi ya hapo huyo mdada ndoto zake, zilikuwa  yeye aje kuolewa na watu wenye uwezo kwasababu wapo wengi walimtaka tena kindoa akawakataa.

‘Mimi siwezi kuolewa na mtu kama huyo…hana nyumba wala gari….mmh, mimi siwezi kuolewa na mtu kama huyo hajasoma,..ikawa zake ndio hivyo, siku zikaenda, hadi mauti yanamkuta,
Sasa ilikuwaje aje kutembea na huyo mvulana, ambaye hata kazi ya maana hana,..msikuma mkokoteni, na akipata peza zke ni kulewa tu,..siri ikaja kuvuja,!

**********

Inatokea, kiubinadamu,..tunahitajia umaarufu Fulani, lakini umaarufu huo, uwe wa kweli  , utoke moyoni. Usiwe wa kuwaonyesha wanadamu tu....na hasa umaarufu wa imani. 

Umaarufu wa imani haudanganyiki, utawadanganya wanadamu wenzao, lakini sio muumba wetu,…mola wetu anatufahamu zaidi tunavyojifahamu wenyewe, yeye anajua imani ya mja wake ni ipi ya kweli. Kiukweli  wapo wanajitahidi lakini nafsini mwao, kuna mambo mengi ya tamaa, husuda chuki, nk...na, wapo wanafanya mengi mabaya kwa hisia..nafsi zao zina siri kubwa sana.

Cha muhimu ni kumuomba mole wetu atusaidie tuweze kufikia malengo yetu..yale tunayotamani yawe, yale ya haki, yaweze kuwa hivyo,..na atusaidie kuziondoa tamaa mbaya nafsini mwetu, atujalie tuweze kuwapata wenza wema katika maisha yetu.


Ni mimi: emu-three

Saturday, July 6, 2019

HUJAFA HUJAUMBIKA...



'Hivi kwanini mimi,...., nimemkosea nini mwenyezimungu...'nilisikia suti hiyo ya huzuni na kunifanya nisimame ghafla, na kunifanya nisite kuendekea na safari yangu, nilihisi mwili ukinisisimuka...'nimemkosea ni mwenyezimungu...' kauli hiyo ilinifanya nigeuze kichwa kuangalia kule nilipohisi sauti hiyo imetokea.

'Oh Mungu, nimekosa nini mimi jamani mpaka nipitie majaribu yote haya, ..mungu wangu naomba unionyeshe tu njia...'maneno ya huzuni yaliendelea wakati huo nimeshageuza kichwa kuangalia sauti hiyo inatokea kwa nani.

Kwa sauti tu,nilihisi ni sauti ya mwanadada, lakini macho yangu yalipotua kwa huyo ninayehisi kuwa ndiye aliyekuwa wakiongea, niligwaya.

Alikuwa binti mdogo sana, tofauti na nilivyodhania.

Kwanza kwa tahadhari nilitembeza macho huku na kule..maana dunia hii imegauka sivyo ndivyo, ya walimwengu ni mengi... kuna mitego mingi ya wahalifu inafanyika hivyo, unajitoa kwa wema unaangukia kwenye mitego ya hao watu, wanakudhuru au kukunyanganya kila na kukuacha uchi. Ila kilichonitia matumaini ni kuwa eneo hilo lina nyumba za watu, na nyumba nyingi ni kubwa zenye ukuta, na wengi wameweka nyaya za ulinzi, kuashiria kuwa wanaoishii humo ni watu wenye uwezo wao.

Niliangalia eneo lile alipokuwa huyo binti..nyumba hiyo kama nyingine ilikuwa na ukuta mkubwa tu na, ..juu yake ilionyesha kuna ulinzi wa kitaalam, ..nikajiuliza huyo binti anafanya nini kwenye eneo hilo, ..hajui kuwa nyumba hiyo ina ulinzi, na wenye nyumba hiyo hawatakubali watu kukaa eneo hilo kiusalama...na kwanini kakaa hapo, na anamlilia nani..

Nilipoona nazidi kutingwa na maswali, ....nikaamua jambo, nikavuta hatua moja, mbili....kabla sijafika pale alipo huyo binti,...na ukumbuke kwa muda huo, bado alikuwa akiongea kwa kulalamika kuhusu masahibu anayokumbana nayo...

Mwili uliendelea kunisisimuka, na hii ni kuashiria kuwa kuna hatari,...mimi nina hisia hizo, mwili ukinisisimuka, ujue kuna jambo la hatari ...lakini nafsi haikunipa uwoga, nafsi ilinipa ujasiri, kuwa nahitajia kujua, nikijua nitajua la kufanya...nikawa sasa navuta hatua, ...

'Ewe mola wangu, nionyeshe kosa langu, hadi nitaabike hivi...nimekuwa mtumwa wa walimwengu, wananichezea kama mpira wa karatasi, naadhirika, na hata wale niliowategemea kuwa watakuwa msaada kwangu wanageuka kunidha....dha...lilisha...'hapo kwikwi ya kilio.

Hapo na mimi nikasita mguu ukawa mnzito kuendelea ...nikatulia kwanza, akilini nikichanganua, je haya ni yangu, ..yasije yakawa maji mazito kwangu, ..aah, nikajipa moyo, ..ngoja nikasikia kwa kulikono,...nikaendelea kutembea...na sikuvuta hatua mbili, mara nikasikia...

'Mimi  ...siwezi tena..bora nife ..bora nijiue.'

Mungu wangu, bora nijiue...

Hapo sikuweza kusubiria, nikahisi nina dhamana, hii ni dhamana maana ni kwanini mola akanifanya niweze kuyasikia hayo, na ni kwanini, niache kiumbe kama huyu ..binti mdogo tu, aje kufanya, hilo alolodhamiria,na ni mashahibu gani yamemkuta hadi kufikia kudhamiria hivyo. Nafsi ikaingiwa na mshawashwa,..ikatamani kujua,...

Nikamsogelea,,,,.

Hata pale niliposegea hadi kumkaribia, bado alikuwa hajafahamu kuwa kuna mtu alikuwa bado hajafahamu kuwa mimi nipo hapo karibu yake, na hata kabla sijaweza kutoa sauti ya kumsalimia huyo binti , nikasikia sauti kali ikitokea ndani mwa hiyo nyumba, ambapo huyo binti kajiegemeza ukutani mwake.

'Huyu mshenzi kaenda wapi....we Taabu, ...we Taabu,...' sauti hiyo ilimfanya yule binti akaurupuke, na kusimama, hapo akaniona, akashika mkono kuziba mdomoni, lakini ...

'Usigope mimi sio mtu mbaya
'Ina maana umesikia nilichokuwa nikiongea
'Hapana...sijui uliongea nini...'nikasema
'Mungu wangu ..'akasema hivyo tu na haraka akakimbilia ndani

Kesho yake nilipita eneo hilo tena, nia ni kukutana na huyo binti, nijue ni nini kinachoendelea kwenye hiyo nyumba, nilipofika hapo nilikuwa watu wamejikusanya
'Kuna nini jamani...?' nikauliza
'Kuna binti kataka kujiua,...'akasema
'Kwanini
'Hata sisi tumebakia kujiuliza tu, na wenye nyumba hawataki kuelezea ukweli, wanasema hata wao hawajui
 Mara nikaona gari la wagonjwa likitoka, ..nikajua watakuwa wamemuwahi, ...
'Akipona ashukuru mungu...'ilikuwa kauli ya askari mmoja aliyetoka kwenye hiyo nyumba
'Kwanini unasema hivyo?'
'Sumu aliyokunywa ni kali sana...na walichelewa kutoa taarifa...'akasema askari

Kiukweli niliumia sana, ni kwanini sikufanya jitihada za ziada kukutana na huyo binti, nikasema na hata hivyo sikukata tamaa, nikafanya utafiti kujua huyo binti kapelekwa hospitalini gani, na wakati nauliza uliza ndio nikakutana na mama mmoja aliyesema anamfahamu huyo binti tokea akiwa mdogo.

'Sasa kwanini kakimbilia kutaka kujiua...?' nikauliza

'Mhh...we acha tu, hujafa hujaumbika, usilolijua ni sawa na kiza cha totoro...yule binti kapitia masahibu mengi, na huwezi amini huyo anayeishi naye ni mama wa kambo, mama yake alishafariki....

NB: Bado tupo kwenye maajribio, ili tuweze kurudi tena.

Ni mimi: emu-three

Tuesday, March 5, 2019

LA KUVUNDA HALINA UBANI...


 Ni wakati nipo msibani macho yangu, yalitua kwa mtoto mmoja aliyekuwa akilia sana, cha ajabu kilichonishangaza mimi,  hakuna hata mtu mmoja aliyemjali, …nilijiuliza ni kwanini, kiukweli hali yake hasa kimavazi haikuonekana njema, nguo zilikuwa chafu, na kuukuu. Hata hali yake ya kiafya yaonekana ni dhoofu…lakini naye ni muombolezaji, naye ana uchungu,….na…
Nahisi huo msiba umemgusa,…na sijui….

Nikageuka huku na kule, nikiwaangalia watu wengine,  watu hapo kwa ujumla  walikuwa kwenye majonzi makubwa,  wengi walikuwa wakilia, wengine wakionyesha nyuso za huzuni,…ilimradi kila mmoja alikuwa kaguzwa na huo, masiba.

Kuna wengine walilia hadi kupoteza fahamu…na watu kama hao, walikuwa na jamaa zao wa akaribu wa kuwaliwaza,..lakini huyu …mtoto, niliyemuona awali, hana…hana hata wa kumkaribia, kila aliyemuona alimtupia jicho moja, na kujifanya hajamuona…, swali akilini mwangu likawa linajiuliza, ni sawa, wengi wameguswa na msiba huo, hata kama sio ndugu wa karibu wa marehemu kivile…na wengi wanalia,…je huyu naye analia kwasababu gani…ni ndugu wa karibu,….au ….

Hamasa ya kufahamu zaidi ikanivuta….

Nikaamua kufanya jambo, …hata hivyo, awali haikuwa rahisi,..maana kulikuwa na watu wengi  mbele yangu na kwa wingi wa watu, nisingeliweza kuwapita  kwa urahisi, nafasi ilikuwa ndogo, ukiondoka sehemu mwingine anakuja kukaa…aah, hata hivyo, hamasa ilizidi…
Niligeuka kumuangalia tena,….bado alikuwa akilia, …tena kwa kwa huzuni kubwa,…hata mimi, pale nilipo, nikavutwa na hisia za kulia,….

Msiba unauma jamani….

Kiukweli msiba unauma…na unauma zaidi kutegemeana na mtu huyo alikuwaje mbele ya jamii, na zaidi kutegemeana na waombolezaji , na je kaacha nini nyuma yake,…watoto, mke au jamaa waliokuwa wakimtegemea, na zaidi ….hata waombolezaji wenyewe, au wana habari, wanaweza kumfanya kila mtu aliyehudhuria msiba huo aweze kulia….

Kwa  jinsi ilivyo, huyu marehemu,  alikuwa mtu aliyegusa watu, kimatendo, kitabia,…ndio maana wengi walifika  kumsindikiza kwenye safari  yake ya mwisho, ambayo ndio safari ya kila mwanadamu, …kwakwe tumetoka, na kwake ndio marejea yetu…

Nilisia mshehereshaji akiongea mambo mazuri ya marehemu…

Kwa vyovyote iwavyo, mtu akifariki, yatubidi tumuongelee kwa mambo mazuri, maana hayo mambo yake mema,  ndiyo taa ya mja huyo huo endapo,…tukiyaongea, taa hii huzi kuwaka,, kamwe tusipende kuongelea mambo yasiyo mema, hata kama aliyafanya, ili tusififishe mwanga wa taa yake..hayo ni maneno mazuri  niliyoyakumbuka kutoka kwa watu wa imani.

Akili yangu ikarejea kwa yule mtoto…ni…kijana, ni kijana wa takiribani, miaka kumi na mbili hivi…….nikaamua kumsogelea, hadi pale alipochuchumaa, pembeni yake kulikuwa na mfuko wa Rambo, na ndani yake kulionekana nguo nguo hivi….kwa muda ule yule kijana, alikuwa kachuchumaa, naona sasa miguu imemuisha nguvu…hawezi kusimama tena, na bado hakuna mtu aliyemjali..

Hakuna hata aliyepoteza muda kumuangalia tena…, wengi walitekwa na matendo yanayoendelea mbele ya jukwaa…watu wanavyoomiongelea  marehemu…na mengineyo.
Mimi nikamsogelea yule mtoto….

‘Pole kijana…pole sana..yote ni kwa mapenzi ya mungu, …’nikasema nikimsogelea na kumshika begani.

Yule mtoto, ..ni kijana akainua uso na kuniangalia, uso ulikuwa umefunikwa na machozi….akatikisa kichwa…kama kusikitika. Akavuta pumzi, haalfu akasema;

‘Ni kweli yote ni kwa mapenzi ya mungu, lakini kwangu, …..kwa-kwa…ngu, ime-ime….kuwa ni….mengine yanauma kaka yangu,sijui nikuite kaka yangu, au baba, hata sikujui…..sijui niseme nini…inaniuma kwa-kwa –kwa -kwe….’akasema. akishindwa kumalizia maneno.

‘Kwa muda huu, hakuna cha kusema iliyobaki ni kumshukuru mungu, kwani yeye ndiye mwenye mamlaka ya haya yote…, kwake tumetoka na kwake ndio marejeo yetu, ndio kauli sahihi,..’nikasema

‘Ni sawa…lakini mwenyewe si umeona..mimi kama mimi nitakuwa mgeni wa nani,…nimetoka mbali nikijua nimeshafika kwa…..lakini sasa,..ooh,.. ‘akaanza kulia.

‘Umetokea wapi…?’ nikamuuliza.

‘Yaani,..nilijua,…nikifika nitamkuta…nitaongea naye, nita…..sasa nakutana na haya….niende wapi mie…’akasema.

‘Oh, ina maana…’nikatakla kuongea kuhusu hisia zangu, lakini yeye akaendelea kuongea.

‘Hebu niangalie…mimi kama mimi nitamuendea nani sasa , hebu niambie kaka yangu…ni nani atakayeniamini, mtoto wa majalalani…niangalia nilivyo, ni nani, ata……kwa hivi sasa sina mama, na sasa sina….ooh…’akaanza kulia,…kiukweli hata mimi nikalia.
Baadae nikamwambia…

‘Oh..usijali yote ni mapenzi ya mungu, yey e ndiye atajua uta…’hapo sikuweza kuendelea yule mtoto, au yule kijana  akalala chini, na kunyooka,…alionekana kupoteza fahamu.
Hapo sasa baadhi ya watu wakafika na kuanza kumsaidia.

‘Huyu ni nani…?’ akauliza mmoja wa jamaa aliyefika pale.

‘Mhh..hata simjui…’akasema mwingine

‘Sio jamaa au mtoto wa marehemu…’nikasema

‘Hapana,….mtoto wa marehemu awe hivi..wewe vipi bwana….’akasema jamaa aliyeonekana kuwa ni mtu au jamaa wa  marehemu.

‘Lakini…..’nikataka kuyarudia yale maneno ya yule mtoto, lakini huyo aliyesema…hapana, akiwa na uhaklika kuwa huyo mtoto sio jamaa ya marehemu akaondoka, .
Kwa muda ule huduma za kwanza za huyo mtoto zilikuwa zikiendelea, baadae akazindukana, na alichosema kwa haraka,,,

‘Najua hawataniamini, ..najua…kwa vile mimi sasa ni yatima, lakini, nasema hivi…haya ni kizalia,, leo kwangu kesho itakuwa kwa mwingine…’aliposema maneno hayo, akapoteza fahamu tena.


WAZO LA LEO: Diary yangu, inatoa pole kwa msiba wa mpendwa wa wengi, …RIP Ruge, ..hatuna cha kuongeza, zaidi ya kukuombea makazi mema peponi, na kuwaombea wazazi na ndugu subira njema, …kwani yote hayo ni kwa mapenzi ya mola.

Ni mimi: emu-three