Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Showing posts with label Mapenzi na ndoa. Show all posts
Showing posts with label Mapenzi na ndoa. Show all posts

Friday, July 12, 2019

IMANI HUTOKA MOYONI


IMANI YA KWELI HUTOKA MOYONI , NA SIRI HIYO AIJUE NI MOLA PEKEE.

Hiki sio kisa ni ukweli,

Katika maisha yangu… niliwahi kuajiriwa kwenye kampuni moja, nilipofika hapo nikazoeana na msichana mmoja,…nilimzoea kwa vile yeye ndiye alinikaribisha, na kunionyesha mazingira ya hapo kazini, ufanyeje, uende wapi kiutawala na sehemu ya kula, ofsini ipi ni ipo, vitu kama hivyo.

Basi kila nikihitajia kitu namuuliza yeye, na kiukweli hakuwa na hiyana, aliweza kunielekeza vyema tu, na kuna muda watu wakaanza kutuangalia kwa macho ya kujiuliza, huenda tumekuwa marafiki, lakini moyoni mwangu sikuwa na mawazo hayo kabisa.

Siku zikapita, na ule ukaribu wetu na huyo mdada ukapungua, maana sikuwa na cha kumuuliza tena, mimi nipo idara nyingine na yeye yupo idara nyingine, …sasa katika mazungumzo, nikaja kujua kuwa huyo msichana ni wale wenye msimamo mkali…mtakuwa marafiki lakini sio kwenye tendo la ndoa.

‘Huyu dada ni bikira bwana,…’watu wakawa wanamtania.

‘Labda bikira wa sehemu nyingine, mimi sidanganyiki  ‘mmoja akasema.

‘Kwanini, na wewe unamfahamu, tokea tuajiriwe hapa ulishawahi kumuona na mvulana, ..maana hapa hakuna siri, na hata huko nyumbani kwake si unakufahamu, uliwahi kumuona akiwa na mvulana..?’ akaulizwa.

‘Siri ya mtu anaijua yeye mwenyewe..ila mimi siamini kwa umri ule, atakuwa bado bikira, ni lazima atakuwa na mtu wa siri..’akasema huyo jamaa, na wengi hawakumshabikia, waliona ni wale wasiopenda maendeleo yaw engine.

Ikawa ni utani tu, wengi wakawa wanamtania huyo mdada kwa kumuita ‘sister bikira..’ akawa anaitwa hivyo.

Kiukweli mimi sikuweza kumuuliza huyo mdada kama hayo maneno na utani yana ukweli ndani yake,..niliamini kuwa yawezekana,…mtu ukiamua unaweza ukaishii hivyo,, na kwa vile ule ukaribiu wetu wa kumuuliza hiki na kile ulishakwisha, nikawa sikupata muda wa kuwa naye karibu tena, kila mtu kwenye idara yake na maisha yakaendelea.\

 Ila mimi niliamini waliyosema watu kuwa huyo mdada ni mgumu, sivyo kama walivyokuwa wanadada wengine, huyo mdada hakuwahi kuwa na rafiki wa kiume, niliyewahi kumuona au kuambiwa …kama ilitokea kukutana naye hasa kwenye chakula maana tulikuwa na mgawahawa wafanyakazi wote hukutana humo, huyo mdada..alionekana kivyake vyake tu..na ole mvulana ajaribu kumgusa, hata kiutani, ataambulia matusi,…

Hapo kazini karibu kila mmoja alijulikana ni nani na mwenzake wa jinsia tofauti ni nani, na wengine wakatokea hata kuoana kabisa,…lakini kwa miaka kadhaa niliyofanya hapo, sikuweza kumgundua rafiki wa huyo msichana…moyoni nikasema,..basi huyo ni ‘sister bikira kweli’.

Miaka kama miwili ikapita…nikaja kufikiria kama mimi nina tabia yangu kuwa  msichana wangu wa kwanza kukutana naye nikutane naye ndani ya ndoa, sasa kwanini nisifanye urafiki na huyo mdada, ambaye naye anaonekana ana msimamo huo..lilikuwa wazo katika kuhangaika kumpata mwenza wa maisha, ilikuwa wazo, na nikawa na mikakati hiyo, lakini siweza kulifanikisha, maana kiukweli moyoni sikuweza kuvutika na mdada huyo kimapenzi. Nafsi hupenda kile kinachomvutia mtu.

Bahati mbaya, nikahama hiyo kampuni…

Baada ya miaka kadhaa, nikasikia, kuwa yule msichana kafariki,

‘Kafariki!!!... ilikuwaje jamani…?’ nikauliza kwa mshangao na masikitiko.

‘Alianza kuumwa, umwa..akawa anapungua, baadae akazidiwa, anatibiwa, anapona hali inarejea, anaanza kuumwa tena,..baadae..akapelekwa kwao…yaani binadamu hubadilika haraka sana, unamfahamu jinsi alivyokuwa mrembo,...watu waliomuoana kipindi kazidiwa, wanasema ule urembo ulikwisha akawa kama mzee, alikuja kubadilika akawa…mweusi….’akasema jamaa,

‘Mhh...kwasababu ya huko kuumwa au, , kwani alikuwa anaumwa nini…?’ nikauliza moyo sasa ukinienda mbio. 

Unajua kipindi cha nyuma, watu wakiumwa sana, na kukonda, na kubadilika mwili, moja kwa moja unajau ni ugonjwa gani,..kipindi hiho kulikuwa hakuna dawa za kusaidia kuongeza nguvu, kwahiyo watu wengi waliougua ugonjwa huo, waliteseka sana kabla ya umri wao kuisha. Kwa vyovyote iwavayo kila mtu ana umri wake.

‘Unauliza jibu bwana, mdada alipatwa na maambukizi, na ..huwezi amini, ..hata ndugu zake hawakuamini wakasema kalogwa, lakini hakuna siri, aliyemuambukiza aligundulikana, kwani naye kwa kipindi hicho alikuwa akiugua ugonjwa huo huo..na alipoulizwa, yeye alidai huyo mdada ndiye kamuambukiza, lakini uchunguzi zaidi ulionyesha kuwa huyo mvulana alikuwa hajatulia, yeye ndiye alimuambukiza huyo msichana.

‘Mhh..lakini si mlisema huyo mdada ni bikira.

‘Hahaha, tulijua hivyo, kiukweli hata mimi niliamini hivyo…hadi msichana huyo anafikia kuumwa, sote tuliamini hivyo….’akasema.

‘Haiwezekani…japokuwa kila kifo lazima kiwe na sababu..nahis aiumwa maradhi mengine tu..hata hivyo....’nikasema na jamaa akanikatisha kwa kusema.

‘Iliwezekana sasa, na alitembea na cha pombe fulani, wakati yeye alikuwa akituzarau pale kazini kuwa hatuna maana, walevi, eeh..si unakumbuka, alivyokuwa,akitudharau, ...wewe uliondoka, sasa ilifikia mahali hamgusi mtu....anasema yeye ana bwana wake yupo Ulaya...sasa kumbe alikuwa na mvulana cha pombe tu..hakuwa na hadhi kwa yule mdada,…sijui ilikuwaje..masikini mungu amsamahe tu...’akasema huyo jamaa.

‘Kwani hamkujua ilikuwaje..?’ nikauliza.

‘Aaah. ilikuwa kujulikana dunia hii ina siri,na kwa vile alikuwa akiringa, jamaa zake walikuja kuvujisha siri..tukajua kila kitu, ikawa kufuatilia kuhakiki tu....unajua msijifanmye mna imani sana ya dini, aheri muwe kama sisi...unajua imani. ya.kweli ya mtu aijue ni mungu pekee, ujidanganya ipo sisku imani hiyo inataisha kidogo kidogo kama mshumaa unavyokwisha halafu utakuja kuumbuka, ila niliumia sana, yule mdada nilimpenda, nilitamani nimuoe, akanikataa,…’akasema huyo jamaa akionyesha kusikitika.

'Mhh..lakini kweli wewe ukizi  kulewa, nani angekubali umuoe....'nikasema kwa utani.

'A wapi mimi nilikuwa nakunywa kistaarabu, sema, ndio hivyo kila kitu kwa wakati wake, ni kweli kuna muda nilizidisha, nikaumwa karibu ya kufa...kifua ikawa TB,...aisee, nilijua nakufa...nilipopona nikabadilika, ...hapo nikaona umuhimu wa kuoa...sasa huyo mdada alitolea nje kabisa, ..'akasema

'Labda alikuwa na mtu wake kweli...'nikasema

'Ndio yupo jamaa mmoja yupo Ulaya kweli, lakini jamaa huyo akaja kumuoa mzungu, na ndio maana huyo mdada akachanganyikiwa akaanza kulewa...japo hakujionyesha,...nasikia ndio hapo akaja kukumbana na cha pombe..lakini kwa siri kubwa...hayo ni mambo ya ndani, ...'akasema

'Oh, siku zake zilishafika...'nikasema

 Ni kweli kwa taarifa za kifamilia, japo ilikuwa siri, msichana huyo alifariki kwa HIV, kutokana na dalili, na hata vipimo,  kiukweli mimi sikuamini, wengi hawakuamini..japo kwa hivi sasa HIV, unaweza kuipata kwa njia nyingine ila kwa huyo mdada ilikuja kuthibistishwa..aliipata kwa namna gani

Watu katika kuchunguza sana, kumbe, huyo mdada alikuwa akitembea na mvulana kwa siri sana kwa vile alikuwa ni jirani yake..ilikuwa ni kwa siri sana…wanasema alifanya hivyo kwa siri, na hakufanya kwa vile anampenda huyo mvulana, maana kiukweli hawakuwa wanaendana..ila kulikuwa na sababu za kuchanganyikiwa....

Ilivyoonekana, alifanya hivyo, pale anapozidiwa, mawazo na mengine yaliyokuja kusemwa baadae msichana huyo akatokea kuwa mpweke, alikuwa hana rafiki tena, akawa anawachukia wanaume, kila mwanume kwake ni sawa na huyo aliyemuacha solemba, swali likawa ilikuwaje huyo cha pombe amuone sio sawa na wanaume wengine.

Tatizo huyo msichana hakupenbda kuwa muwazi, na .maumbile ya kibinadamu hufikia sehemu utashindwa kuvumilia hasa ukiwa unatumia kilevi..kiukweli yasemakana, siku katika masiku ubinadamu ulimzidi, akakwaana na huyo mvulana, ilikuwa kwa bahati mbaya tu kama alivyokuja kusema..

'Hiyo bahati mbaya, ikaja kuwa mazoea hasa akizidiwa, 'alijitetea.

'Ilikuwa nawaza sana, ..mpaka nataka kujiua,...sasa huyo mvulana akawa ndiye mtu wangu wa karibu wa kuniliwaza,,,akawa anakuja kwangu, usiku wa manane maana nilikuwa naishi naye nyumba moja sema ni chumba tofauti, wote ni wapangaji'

Kiukweli huyo msichana  hakutaka kabisa watu wajue, na kiukweli hakumpenda kabisa huyo mvulana,..na yeye alitaka watu wajue kuwa yupo hivyo, ..bikira. Ila kilichoharibu ni kwa sababu ya huyo mchumba wake kumtelekeza.

Na zaidi ya hapo huyo mdada ndoto zake, zilikuwa  yeye aje kuolewa na watu wenye uwezo kwasababu wapo wengi walimtaka tena kindoa akawakataa.

‘Mimi siwezi kuolewa na mtu kama huyo…hana nyumba wala gari….mmh, mimi siwezi kuolewa na mtu kama huyo hajasoma,..ikawa zake ndio hivyo, siku zikaenda, hadi mauti yanamkuta,
Sasa ilikuwaje aje kutembea na huyo mvulana, ambaye hata kazi ya maana hana,..msikuma mkokoteni, na akipata peza zke ni kulewa tu,..siri ikaja kuvuja,!

**********

Inatokea, kiubinadamu,..tunahitajia umaarufu Fulani, lakini umaarufu huo, uwe wa kweli  , utoke moyoni. Usiwe wa kuwaonyesha wanadamu tu....na hasa umaarufu wa imani. 

Umaarufu wa imani haudanganyiki, utawadanganya wanadamu wenzao, lakini sio muumba wetu,…mola wetu anatufahamu zaidi tunavyojifahamu wenyewe, yeye anajua imani ya mja wake ni ipi ya kweli. Kiukweli  wapo wanajitahidi lakini nafsini mwao, kuna mambo mengi ya tamaa, husuda chuki, nk...na, wapo wanafanya mengi mabaya kwa hisia..nafsi zao zina siri kubwa sana.

Cha muhimu ni kumuomba mole wetu atusaidie tuweze kufikia malengo yetu..yale tunayotamani yawe, yale ya haki, yaweze kuwa hivyo,..na atusaidie kuziondoa tamaa mbaya nafsini mwetu, atujalie tuweze kuwapata wenza wema katika maisha yetu.


Ni mimi: emu-three

Wednesday, October 3, 2018

YOTE NI KWA MAPENZII YA MUNGU-53



‘Huyo muhasibu yupo hai…’sauti ikasema

‘Wewe ni nani hebu pita huku mbele…’akasema hakimu

Watu sasa wakawa wanampisha huyo mtu…safari hii ni  tofauti na ilivyokuwa awali, huyo mtu alipishwa kwa nidhamu, hadi akafika sehemu ya kuonekana, maana licha ya kuzuiwa watu kujaa, bado wengi waliweza kuingia,

Jamaa sasa akawa keshafika mbele, kwa upeo wa kuonekana na kila mtu,..akawa anatembea taratibu kama vile anataka kila mtu amuone, ..hadi akafika sehemu karibu na shahidi aliyekuwa akihojiwa.

‘Wewe ni kwanini na kwanini hufuati taratibu za mahakama…?’ kaulizwa

‘Muheshimiwa hakimu, kama ningeamua kusubiria utaratibu huenda nisingelipata nafasi ya kufika hapa hii leo…kuna mengi hamjayafahamu bado..’akasema , na hakimu akawa anamuangalia kwa makini, na jamaa alipoona hakimu anamuangalia sana akasema

‘Najua labda …sina uhakika lakini, hakimu unaweza kunikumbuka…mimi nakukumbuka sana, wengi wa leo, wakiniona hapa, wasio kuwa na moyo wa uvumilivu wanaweza kukimbia, au kuzimia…’akasema

Hakimu akawa anateta na wenzake, halafu baadae akasema

‘Kwa upendeleo wa dharura, shahidi uliyekuwa ukiongea, usubiria kwanza, ili tuweze kumsikia huyu mtu, nataka kufahamu zaidi kuhusu yeye, na kwanini anatoa kauli kama hiyo ambayo, inasigishana na kauli yako, …’akasema hakimu.

Hakimu akamuangalia wakili, kama vile anataka kumuarisha afanye jambo, na wakili akawa kimia tu.

Mimi pale nilipo nikamtupia jicho Dalali, Dalali alikuwa vile vile kama kagandishwa akimuangalia huyo mtu aliyeingia, mpaka nikaingiwa na wasiwasi, na kwa haraka nikageuka kumtafuta mama mjane kwa macho, sikumuona ile sehemu yake aliyokuwa amekaa awali, sijui kama alitoka kidogo, au kaenda wapi, sikuwa na muda wa kumfuatilia, mawazo yangu yakaelekea kwa huyo mtu aliyeingia sasa hivi, nikijiuliza je ni nani huyu mtu, na kwanini uwepo wake umeweza kumdatisha Dalali.

Mimi nikamsogelea wakili , na kumnong’oneza jambo, na kwa haraka akamtupia jicho Dalali, halafu akatikisa kichwa kama kusikitika

‘Unahisi yupo sawa…?’ nikamuuliza

‘Atakuwa sawa, sema labda hakutarajia kumuona huyo mtu,…’akasema

‘Kwanini…?’ nikamuuliza wakili

‘Wewe subiria tu,….’akasema wakili na kunifanya na mimi niwe gizani, sikuipenda hiyo hali, …

 Dalali sasa akawa kama kalegea hivyo, kaegemea upande mmoja, kama anataka kudondoka,…na docta aliyekuwa mbali akanyosha mkono, huku akiashria kwa hakimu amuangalia Dalali, na hakimu akamuona..akatambua docta ana maana gani.

‘Vipi wewe Dalali una nini…?’ akauliza hakimu sasa akimshangaa Dalali ambaye alikuwa kalegea kabisa,…na Hakim kuona hivyo, akasema

‘Docta hebu muangalia huyo mgonjwa wako, kama ana tatizo lolote…’akasema hakimu na docta akasogea pale alipokuwa Dalali na kuanza kumpima pima, baada Dalali, akawa kama kazindukana, na kwa haraka akawa kama anataka kusimama, lakini akawa anashindwa..baadae sauti ikatoka kwa Dalali ikisema;.

‘Haiwezekani, huu ni mzuka….’akasema Dalali akiendelea kumtolea macho huyo jamaa aliyeingia.

Yule jamaa sasa akawa kamkaribia Dalali….Dalali…akajaribu kuinua miguu, lakini hakuweza, huyo akaporomoka chini…watu wakawa wanasukumana ili kuona kinachoendelea huko mbele..

‘Watu wa usalama …’akasema hakimi na watu wa usalama wengine wakawa wanawatuliza watu wengine wakimsaidia Dalali kuweza kukaa kwenye kiti chake tena.

‘Vipi wewe unaogopa nini…?’ akauliza

‘Huyu siamini kama …ni binadamu…’akasema

‘Kwanini…?’ akalizwa

‘Nijuavyo mimi alikufa na kuzikwa hata mkienda makaburini mtaliona kaburi lake…’akasema

Huyo mtu hakujali hicho anachoongea Dalali, yeye akajisogeza hadi mbele, na kusimama, …..

‘Haya hebu tuambie wewe ni nani, na kwanini unaingilia Mahakam , si unajua tarataibu za mahakama, kwanini unapayuka huko nyuma…?’ akaulizwa

‘Imebidi nifanye hivyo, kwa maana kama ningelikwenda moja kwa moja kwa watu wangu nikajitambulisha, nina imani wengine wangelikimbia…kama unavyoona huyu hapa…ananifahamu vyema, na anafahamu kuwa mimi ni marehemu…’akasema

‘Ina maana wewe ndio huyo….’kabla hajamaliza kuulizwa, yeye mwenyewe akasema;

‘Mimi nilikuwa muhasibu wa benki kabla sijafukuzwa, na kutambuliwa kuwa nimeshafariki,…ndivyo inavyojulikana hadi hii leo…huko benkia nilifukuzwa kwasababu ya njama za bosi wangu,..’akasema


‘Bosi wako ndio yupi..?’ akulizwa


‘Majaliwa…’akasema


‘Tuambie ilikuwaje…?’ akaulizwa


‘Ukweli wa hili jambo naufahamu sana mimi kuliko yoyote hapa..,..na ndio maana ilisaidikiwa kuwa mimi nimekufa..lakini sikuwa nimekufa, nililipwa pesa nyingi, nitoweke, na ni baada ya kuonekana hivyo, kuwa mimi nimeshafariki,..lakini kuna kitu kilinifanya nirudi tena…’akasema


‘Kitu gani…?’ akaulizwa


‘Marehemu mtaalamu ni baba yangu wa kufikia, …yeye alizaa na mama yangu, na kupatikana kwa mimba hiyo ni kutokana na michezo yake mibaya, nilikuja kuambiwa na bibi, mama yake mama yangu..


Bibi aliniambia, kuwa …baada ya kuzaliwa mimi, mama alinitambulisha kwa huyo baba, …kiukweli huyo baba hakunikataa kama unavyoona tunafanana naye sana,..alipokubali hilo, akafanya mambo yake na mama yangu akawa anaumwa sana, ulimi ukawa unavimba, akawa hawezi tena kuongea, hadi anafariki…’akasema.


‘Kwanini mama yako aliumwa hivyo, ni ugonjwa wa namna gani.?’ Akaulizwa


‘Marehemu ..alikuwa na tabia hiyo, kuwachezea wanawake, baadae akiwachoka anawateketeza kwa mbinu hizo, lengo lake ni kutaka wasije kusema lolote kumuhusu yeye..na niliposikia hii kesi nikaona wakati umefika wa kuyabainisha haya…


Yaliyotokea kwa mama yake Majaliwa ni hayohayo yaliyotokea kwa mama yangu, na Dalali, alihadaiwa afanye hayo,… kama kinga, hakulijua hilo…mimi nimehangaika sana kumtafuta…Majaliwa, ili niongee naye sikufanikiwa, nikaona nije hapa, lolote liwalo na liwe…Huyu Dalali, yawezekana siku ile yeye alitumiwa hivyo, ambake huyo binti, kuuficha ukweli wa marehemu…na huenda hiyo mimba ni ..ya marehemu…’akasema


‘Niliposikia habari ikiongelewa, kuhusu yaliyotokea kwa mama wa…Majaliwa,.. imeniuma sana… nikakumbuka kilichotokea kwa mama yangu na wengine wengi walioafanyiwa hivyo, nimeshindwa kuvumilia, nipo tayari kuhatarisha maisha yangu, kwa ajili ya hili….’akasema


‘Ehe, haya…tuambie sasa hayo ya bank…?’ akaulizwa


‘Bila shaka….mimi …, nitawaambia kila kitu…ninatambua baadhi ya njama za hayo madeni maana nilikuwepo yakifanyika, …na baadhi ya mbinu za kulifanikisha hilo ilitokana na marehemu,..’akatulia

‘Kuna watu hawajui, kuwa mtaalamu,…aliwahi kufanya kazi benki…akaacha, na kujiingiza kwenye mambo ya kiganga, anasema aliacha kwa kutii wito wa mizimu, kwahiyo mambo ya benk anayafahamu…yeye ndiye alifanya mipango nikajaariwa benki…na kila mara alikuwa akinitembelea kazini, hasa akiwa na shida ya pesa, na… siku moja aliniambia, amegundua jambo, nikamuuliza jambo gani, akasema;


‘Unajua kuna sahihi za watu wawili zinafanana, na hao watu ni maadui zangu, ila hawajui kuwa wao ni maadui zangu, nataka kuwamaliza, na kuna mtu naye …tutamtumia lakini hatakiwi kulifahamu hilo, hata yeye ni adui za hao watu…’akasema hivyo.


‘Wawili hao ni akina nani…na mimi nahusikanaje na hilo…?’ nikamuuliza


‘Wawili hao ni Dalali na kaka yake, je wewe si mahasimu wa hao watu?’ akaniuliza

‘Ni kweli lakini mimi sina haja ya kuwafanya lolote, nilishawasamehe tu…’nikamwambia


‘Sikiliza bwana mdogo, mimi…nimegundua jambo, hata kama umewasamehe..lakini kwa kupitia wao, tunaweza kufaidi,..wewe wataka kuishi masikini mpaka ufe…’akasema. Kiukweli hiyo familia ni watu wasio na uhusiani mnzuri na familia yetu…kuna migogoro ya maeneo unajua tena..’akasema


Basi nikamuuliza mtaalamu,kwahiyo…unataka iweje?’ nikamuuliza


‘Usiwe mjinga bwana…mimi najuana na huyo meneja wa benki, alikuja kwangu, akitaka nimfanyie mambo fulani, fulani…unajua mambo mengine hujileta tu,..Dalali, aliwahi kuniambia sahihi yake inafanana na ya kaka yake…sikumoja alipokuja huyo meneja, anakuja kwa kunizoea, pamoja na mambo yake mengine,nikaongea naye kuhusu kufanana kwa sahihi, …huyo meneja ni mjanja sana, …akanielewa, ila hakuwa anawafahamu watu vizuri, ni nani wa kushirikiana naye..’akasema


‘Una maana huyo meneja bosi wangu, aje kwako kwa mambo kam hayo, kwa umasikini gani alio nao,…haiwezekani…?’ nikamuuliza


‘Hayo mengine huhitajiki kuyafahamu, wewe si unataka kuwa tajiri, sasa wakati umefika, nimeshaongea na huyo mkuu kasema hayo nimuachie,…ila yeye anahitajia mambo fulani kutoka kwa mtu wa nje…ndio maana alipofika kwangu, kwa shida zake akaniamini..’akasema.



‘Mhh,…mimi sikuelewi, sasa wewe unataka mimi nifanye nini…?’ nikamuuliza.


‘Nimekuambia…mengine hayakuhusu..kuna mambo nitakuwa nakuambia uyafanye, usiulize kwanini niyafanye…ila wewe utalipwa vizuri sana, unasikia,..umasikini bye bye..kama utafanya nitakavyokuagizia, utakuja kunishukuru, mimi niliacha kazi benki lakini bado nina ndoto za kupata utajiri kwa wazo langu hilo, na wazo hilo kumbe kuna mwenzangu naye alikuwa nalo…’akaniambia.


‘Kiukweli nililipinga sana hilo…lakini kukatokea hali ya mchafuko hapo banki,..mageuzi, mbali mbali, nikajikuta na mimi ni miongoni mwa watu wanaotakiwa kupunguzwa hapo kazini..lakini kwa haraka nikahisi ni mbaya wangu, bosi Majaliwa…’akasema.


‘Kabla ya kufikia hatua hiyo ya kupunguzwa kazi,  ndio mtaalamu akanijia , na kuniambia, sasa umeonaeeh…usijali kwa haya yaliyotokea, kuwa wewe unapunguzwa kazi, hiyo ni sehem ya mikakati ya kukufanya wewe uwe tajiri, lakini kabla ya kuondoka,  kuna mambo yanatakiwa wewe uyayafanye kwa haraka…’akasema


‘Umefahamuje kuwa kuna zoezi kama hilo…haya ni mambo ya ndani ya benki…?’ nikamuuliza


‘Usiulize sana…wewe utapunguzwa kazi, ni katika kufanikisha mambo ya utajiri, unielewe hapo, na usipofanya hayo, unajua ni nini kitatokea kwako, kwanza utakosa nini, eeh, wewe waenda kijijini utaishije, au unafikiri utapata kazi haraka, kazi hapa nilikufanyia mpango mimi…’akasema.


‘Kiukweli nilishajua kuwa kazi sitakuwa nayo tena, ..nikakubaliana nao, nilichotakiwa kukifanya ni kusimamia mikopo, kuwasainisha watu, wanaohusika…sasa mojawapo  ya vocha hizo ni ya huyo marehemu, na kwa vile sahihi yake marehemu inafanana na y a Dalali, mimi sikuwa na tatizo, nikampigia simu Dalali, akaja…


‘Nilimuelezea kuwa hapo benki kuna mabadiliko, na ni ya haraka, yeye anatakiwa kwanza akalete Dole gumba la kaka yake, na sahihi yake…lakini muhimu ni dole gumba la kaka yake, sahihi hata yeye anaweza kuiweka…’akasema


‘Dalali, alikubali,…hakutaka hata kuuliza zaidi..kesho yake nikapata nilichokitaka na yeye akaweka sahihi…kwa kila nilichomuambia aweke sahihi…, hakufahamu kuwa anapitisha deni la kaka yake…kiukweli sikupenda hilo, lakini ningelifanya nini…watu hawamfahamu mtaalamu, ni mchawi wa kutupwa….’akasema.


‘Kwa vipi, na tutaaminije hayo unayotuambia, unaongea kuhusu marehemu nay eye hayupo hapa kujitetea..?’ nikamuuliza.


‘Kuamini haya mtafuteni huyo meneja wa hiyo benki ya zamani, mtajua kila kitu…na chunguzeni kufukuzwa kwangu kama sio kwa njama…ulizeni kufariki kwangu kulikuwaje, je watu wanaonifahamu wanajuaje kuhusu mimi, …’akasema


‘Mimi baada ya kupokea barua ya kuachishwa kazi , ilitakiwa nionekane nimejiua, kutokana na kuonea, halafu maisha magumu, iliandaliwa hivyo, walioshuhudia kifo changu waliona huo ujumbe niliouwacha....na kuna dawa nilipewa na mtaalamu, nilipomaliza kuzinywa, nilipoteza fahamu, hata mtu akinipima anaona nimekufa kabisa,…’akasema.




‘Una uhakina na unachokiongea, na kwanini hukukataaa aukutoa taarifa polisi, na kama ulikufa hukuzikwa, au hapo ilikuwaje..?’ akaulizwa.

‘Sikuzikwa mimi, ulizikwa mgomba, mimi baadae nilisafirishwa usiku hadi mikoani, huko nikapewa dawa ya kunirejesha fahamu…na pesa nyingi za kutumia, na onyo, kuwa mimi kuanzia muda huo sipo duniani,..na ikitokea nikarejea  Dar, basi ndio itakuwa mwisho wangu wa kiukweli…wataniua…kwahiyo, eeh…ikatambulikana hivyo kuwa mimi nimeshakufa, na hata familia yangu ilijua hivyo, huko nilikaa na kuoa mke mwingine..’akasema.

‘Ulioa..!!  na mke wako na watoto wako walikwenda wapi…?’ akaulizwa


‘Hiyo pia ni moja ya mipango yao ya kunifanya niisahau familia yangu,..awali nilijua ndio hivyo …hata hivyo…kabla mambo hayajawekwa hivyo, mimi kufa na kutoweka, nilipewa nichague moja, niachane na familia yangu, iwe hai, huru na tajiri, au nisaliti huo mpango, familia yangu iteketee, tena kwa moto…’akatulia

‘Unajua watu hawa wanapenda sana kutumia moto kuangamiza jambo….wakitaka jambo lipotee kabisa, wanatumia moto…sasa kwa vile nilishawahi kuona matendo hayo kwa watu wengine waliofanyiwa hivyo, sikupenda kabisa hilo lije kutokea kwenye familia yangu, nikaamua kufuata watakavyo wao…nikimuomba mungu kuwa ipo siku haki itatenda…mungu yupo…

‘Kwahiyo mimi nilifanya hayo baada ya kutishiwa maisha yangu, mimi na familia yangu, kuna mambo makubwa yalitokea kwenye familia yangu, kabla ya ..kufikia huko, familia yangu iliteseka sana…nisingelipenda kuyaelezea hayo, wenyewe mkiwauliza watawaambia, huo ni ushahidi kwenu, sitaki kuuingilia…’akatulia

‘Ndugu zanguni…haya sio utani, utaamini hayo ninayoyasema siku yakija kukukuta, watu hao waliamini kwenye mali, na adui wao ni yule anayeingilia mipango yao..na ukiwa adui yao, …tiketi yako ni kifo…tiketi yako, ni kukatwa ulimi…kama watataka uendelee kuishi kidogo, lakini lazima watakumaliza…na wanaweza kukupatia sumu, ikakutesa, na ikaonekana ni kansa…utakufa tu…’akatulia

‘Sasa swali mtaniuliza kama hayo yapo na yanafanyika, ..je kwanini sasa nimeamua kurudi, siogopi tena,  kiukweli kilichonipa nguvu yakurudi huku ni kwa vile nimesikia Mtaalamu hayupo tena duniani, huyu kwa hapa nchini ndiye walimtegemea kwa kuangamiza, kimiya kimia au kwa nguvu za giza, ..pia ni kwa vile…mfadhili wao, kakimbia hapa nchini, hayupo tena, hawana pesa tena…’akasema.

Hapo hakimu akawa anaongea na watu wake, baadae akamgeukia huyo mzungumzaji mpya, na huyo mzungumzaji akasema;


‘Na ndugu zanguni …hili jambo lilikuwa sio mpango wa  mtu mdogo kama Majaliwa,  kama…eeh…hata huyo marehemu, sawa yeye alipewa hiyo kazi tu kwa vile ni mjuvi wa mambo ya giza na kwa vile ni wao walimfundisha hizo nguvu za giza, walimuona ana kipaji hicho cha kurisi…lakini wanaofadika na wengine analipwa nini , kidogo tu.


‘Haya ...huyo Majaliwa, sizani, kama alikuwa akifahamu mpango huo kiundani, labda…mimi sijui zaidi, maana sikuambiwa, haya ninayowambia nimeambiwa….jinsi mipango ilivyopangwa, huyo Majaliwa, …yeye kaingizwa kama kiini macho tu, kwa vile ana visasi vyake, basi ikaelekezwa huko, ionekane hivyo…labda mimi sijui zaidi…lakini nina imani yeye hajui zaidi ya hivyo nijuavyo mimi...’akatulia kidogo.

‘Hata mimi….kuyafahamu hayo…ni baada ya kuwasiliana na mtaalamu, wakati anakaribia kukata roho, nilifika kwa siri kumuona aliponiona alinisikitikia sana, kwanini nimerudi, na nilipofanya ukazidi wa kurudi huko nilipotoka ndio akaniambia…


‘Kijana mimi nakufa, sitaishi tena, sasa kama huamini haya shauri lako, kwa vile sitaishi sana, nitakusimulia, ila nataka uwe na ushahdi unaoweza kuja kukusaidia, chukua video, ili iwe ushahidi, nahisi hili litanipunguzia dhambi zangu..na kwako wewe hata sijui nikusaidieje,…ila nataka uje kuwasaidia baadhi ya watu wanaotumika bila kujijua, wajue kuwa wapo hatarini…mzee mtupe anaweza kukusaidia,…haya ni mikakati ya kundi haramu…wao wakikuchoka, wanakumaliza…’akasema

‘Kundi gani hilo mtaalamu…?’ nikamuuliza

‘Hapo ndio…yeye  akanisimulia kila kitu..na ushahidi ninao hapa, kanda ya video, niliyorekodi, yeye akiongea, akiwa taabani, akikaribia kukata roho..kama mnataka kusikiliza ushahidi huo, huu hapa…’akasema akitoa kanda ya videoa

‘Sasa …, mimi sijui zaidi ya hicho nilichokisikia kutoka kwa huyo mtaalamu mwenyewe, na wengi wa wahanga …wametumiwa tu, kupitia kwenye visasi vyao,…’akasema.


‘Kuna jingine..hili sikutaka kulisema, lakini..kwa hivi sasa inabidi,…kumbe hata mke niliyemuoa, alikuwa ni mtu wao,..yaani ilifanyika hivyo, nimuoe, ili ahakikishe mimi sifungui mdomo, na ninakuja kufariki kimia kimia…’akatulia

‘Hamuelewi haya..yapo ndugu zanguni, msipende kujiunga kwenye makundi ambayo yanajifanya yana utajiri, au yanaweza kukufanya wewe uwe tajiri….., kumbe huyo mke ni muathirika wa HIV…, anajijua na anatumiwa kuambukiza wahanga wanaotakiwa waambukizwe, na mbaya zaidi, ukishaupata huo ugonjwa, kuna dawa utapewa, za kukumaliz haraka,…na ukipimwa itaonekana umefariki kwa kupitoa ugonjwa huo, wao sasa hivi wanatumia ugonjwa huo, na ugonjwa wa kansa, kuwamaliza maadui zao…ukifa ukipimwa inaonekana ulikufa kwa ugonjwa, unaojulikana unaua…’akatulia kidogo.

‘Haya nisingeliyefahamu bila kupitia kwa mtaalamu, na niliporejea nyumbani sikumkuta tena huyo mke, alishaondoka, na alicha ujumbe kuwa nisimtafute, kwani sitampata, tutaona kuzimu..…kazi aliyopewa ilitakiwa iwe imekamilika, lakini sijui ni kwa kudra ya mungu, au ni kwa …huruma ya huyo mke, lakini mimi najua yote ni kwa mapenzii ya mungu, ndiye aliyefanya hilo liwezekane….siku zote nilizoishi na huyo mke,..huyo mke, alinisihi nitumie kinga…na nashukuru kwa hilo, kwani nimeshapima, sina maambukizi..

Alitulia kidogo, na alipoona haulizwi maswali, akaendelea kuongea…


‘Hilo deni na mengine ni mpango kabambe ya huyo meneja, mtafuteni, kama bado yupo hai, ataambia kila kitu, na hata hiyo benki hamjui tu, ni moja ya miradi ya hilo kundi…’akageuka kumuangalia wakili

‘Mimi  ….sijui zaidi ya maelezo ya mtaalamu, mtasikia wenyewe akielezea japo kwa sauti ya shida,…ilitakiwa baada ya kumaliza kazi yao waliyopanga, hiyo benki iwabambikie marehemu madeni mengi sana, halafi ipambana na kukusanya pesa kupitoa huko, kupiga minada mali za marehemu, ndio hivyo wanavyowekeza

‘Sasa ni..nini watapata…hebu fikiria wameshapiga minada nyumba ngapi, majumba ya watu yenye thamani kubwa tu…ujanja ujanja wa kupitia kwa watu, waliowasoma wakaona kwa kupitia kwao inawezekana…’akasema


Hakim alionekana kufuatili hayo maelezo, kwa uso wa kushanga , ni kama haamini hayo kuwa kweli yapo..na sasa aliyeuliza swali alikuwa ni wakili ….


‘Ina maana gani hapo, kiukweli hayo maelezo yako yapo kama mikakati pia ya kuuficha ukweli halisi, ni kama njama za kuwatetea hao watu Majaliwa, Dalali na kundi lake,,… kwa vile yaonekana labda una damu damu nao…sasa utuambie ukweli, ni nani kakuambia uje kuyasema haya, maana hapa ni mahakamani..uwongo wako utakufanya uozee jela.?’ Akaulizwa.

‘Ushahidi nimesema ninao hapa, na…nilishawaambia watu wenu, wafuatilie hayo…, wachunguze, mbona ukweli upo bayana….kiukweli mimi siogopi kufa tena, nimeshajitolea muhanga, najua kama hilo kundi halitakamatwa, basi, maisha yangu yapo hatarini, lakini bora nife kihivyo kuliko kufa kidhambi, najua wengi hamtaam,ini haya, lakini, kama watu wenu watafanya kazi vyema, nina imani…….’


Kabla hajamaliza, mara akaingia mpelelezi , akiwa na bahasha kubwa mkononi, akamsogelea wakili na akawa anamnong’oneza kitu, wakawa wanateta kwa sauti ndogo…’

Nilimuangalia yule shahidi aliyekuwa akiongea, ..yaonekana alikuwa na mashaka sana, nikageuka kumuangalia Dalali…alikuwa kama hayupo, docta alikuwa karibu yake akihakikisha mambo yanakwenda sawa, ila kiukweli hali ya Dalali, ilionekana ipo mashakani.

‘Samahani muheshimiwa hakimu ule ushahidi tuliokuwa tukiusubira , umeshafika,..huu ni zaidi ya …tulivyofikiria, …naomba nitete na mpelelezi wetu…’ akasema, akionyesha ishara ya heshima…na hakimu akageuka kuongea na wasaidizi wake.

Mimi nikawa nawasikiliza wawili hawa wakiongea, pale nilipo niliweza kuwasikia vyema, na walipomaliza kuongea, wakili akanigeukia na kusema;

‘Tumemaliza kazi …’akasema akiniangalia mimi, na mimi nikabakia kimia, wakati ule nilikuwa najiuliza mama mjane kaenda wapi, maana hayupo kabisa mle ndani,.nimejaribu kutizima pande zote hayupo.

Hakimu akawa anasubiria tu, naona sasa aliona akae kimia, aone ni nini kaleta huyo mpelelezi, maana hii kesi sasa sio kesi ya madeni tu, imekwenda zaidi ya hapo.


‘Safi kabisa …, ‘wakili akawa anakubali, akionyesha ushahidi na maelezo ya huyo mpelelezi,…

‘Sasa kazi imekwisha….’akasema na sasa akasogea mbele na kumuangalia muheshimiwa hakimu, akasema;

‘Muheshimiwa hakimu,  tulikugusia kuwa kuna ushahidi mkubwa unakuja kwa ajili ya kulimaliza hilo kundi haramu,..’akasema

‘Ni kundi haramu lililojifanya ni wajanja wa kugeuza geuza mambo,….sasa mpelelezi wetu ameshafika, je ni kweli Majaliwa, Dalali na kundi lao hawahusiki ..au ni njama zao, je ni nini ukweli wa hayo madeni, tunao ushahidi wote, na …tunataka tuliweke hili wazi, haki iweze kutendeka kwa kupitia kwako muheshimiwa hakimu.

Hakimu akaangalia saa…halafu akageuka kuongea na wasaidizi wake


NB: KESI IMEKWISHAJE..


WAZO LA LEO: Usiwe mwepesi wa kuamini kila jambo unaloambiwa, au kusambaza kila ujumbe unaotumiwa. Au kuwa mwepezi kusambaza taarifa usizokuwa na uhakika nazo….Kuna watu kazi yao ni kusoma mazingira na watu, kutafuta fursa kwa kupitia kwenye tabia na hulka za watu, na wanatumia mitandao kufanikisha malengo yao…Nia kubwa ni kupata washabiki wengi, na wingi wa washabiki, ndio wingi wa kuingiza kipato kwao. Tuweni makini kwa hilo, tunageuzwa chambo cha biashara kwa wengine.

Ni mimi: emu-three

Thursday, September 27, 2018

YOTE NI KWA MAPENZI YA MUNGU-52


'Ndugu muheshimiwa hakimu, nawakilisha ushahidi huo…unao-onyesha sahihi za ndugu yetu Dalali, sahihi ambazo zinafanana...ile ya kwenye malipo inafanana na sahihi ya kitambulisho cha Dalali,..na sahihi hiyo ipo kwenye malipo yaliyofanyika benki kwa ajili ya mkopo, ulitolewa kwa jina la marehemu…’akasema wakili akipeleka ushahid ule mbele ya hakimi.
'Na pia inafanana na sahihi iliyopo kwenye mkataba...'akaongezea wakili huyo
Hakimu akawa anakagua…na kuwaonyesha wenzake, na wote wakawa wanatikisa kichwa kukubaliana na hilo, kuwa kweli sahihi hizo zinafanana..hakimu akauliza.
‘Dalali…hiyo sahihi kwenye malipo sio yako…?’ akaulizwa Dalali.
‘Si-sio ya kwangu muheshimiwa ha-ha-kimu…..’akasema na hakimu akarejea kuchunguza ile sahihi, na aliporidhika akasema.
‘Tutawaomba wataalamu wa maandishi waje kututhibitishia hilo, na kama ni ya kwako, ujue umeidanganya mahakama…’akaambiwa Dalali..
‘Lakini muheshimiwa kabla ya kulifanya hilo, ninaomba..muda, sijui ilivyotokea, nasema ukweli muheshimiwa, sio mimi…sijui ilikuwaje, sina uhakika muheshimiwa…..’akasema akihangaika kwenye kiti.
Mimi nikamsogelea Dalali, na kusema…
‘Dalali tuambie ukweli..kwanini sahihi yako inafanana na hii hapa ya kwenye malipo ya huo mkopo,…?’ akaulizwa Dalali sasa akiwa katulia.
Dalali akabakia kimia.
Mimi nikachukua zile nakala za ushahidi nikamuonyesha Dalali,..
‘Unaona hapa Dalali, chunguza mwenyewe kwa makini…hapa kwenye mkataba pia,..sahihi hii hapa ni ya kwako,..au tusema, inafanana naya kwako…wewe si umesema sio wewe uliyeweka sahihi yako, ..labda kwa niaba ya marehemu…iweje sasa sahihi hii hapa, ifanane ya kwako… eeh…?’ Dalali akaulizwa sasa yeye akawa anaangalia tu ile sehemu ya sahihi, hajibu kitu.
Hakimu akawa anawaangalia watu hao kwa uso wa kujiuliza, hakutaka kuingilia kati, aliacha mazungumzo hayo ya maswali na majibu yaendelee tu..
‘Dalali bora tu ukiri kosa, tuone haki ikitendeka, kukiri kosa ni uwajibikaji wa muungwana,…hakuna kilichobakia sasa, ukweli sasa upo bayana, ni muda muafaka wa kukiri kosa, utuambie tu ilikuwaje,…au unaoenewa .. je hii hapa sio sahihi yako…?’ nikamuuliza akabakia kimia;
‘Au labda eeh… utuambie kitu, labda, useme… sahihi zenu wewe na marehemu zinafanana ndio hivyo au…?’ nikamuuliza, na hapo Dalali naye akachungulia tena zile sahihi, halafu kwa sauti ya mashaka akasema;
‘Ni kweli sahihi zetu zinafanana,…’akasema na watu wakacheka.
‘Sahihi zenu zinafanana, sasa hivi unasema hivyo, ok…haya tuambie kwa vipi…?’ akaulizwa. Na watu wakacheka na kukatokea mngurumo wa mnong’ono, watu wengi wakinong’ona inakuwa ni mngurumo…Hakimu akagonga rungu lake , kukawa kimia
Dalali akasema akiwaangalia watu…
‘Ni kweli msicheke,…unajua nilishikwa na butwaa baada ya kuona hivyo…na sijui kwanini sikuweza kulisema hili mapema,..ni kweli kuwa sahihi zetu zinafanana, hata mwandiko, mimi nilikuwa napenda kumfuatisha sana kaka yangu huyo kila anachofanya tokea utotoni, nikawa naiga hata mwandiko wake,…na ikaja hata kwenye kuweka sahihi…sasa kwenye sahihi, tofauti yangu na bro,..bro yeye...’watu wakaguna.
‘Ni kweli jamani…bro yeye huwa anaweka nukta hapa mbele…’akasema, akionyeshea sehemu nukta inapowekwa…
‘Inua juu watu waone unachoongea…nahisi ungelikuwa na kalamu ungeiweka hiyo nukata,…au sio…lakini umeshachelewa Dalali…kubali tu yaishe…’akaambiwa na wakili, Dalali akainua ile nakala ya mlipo akionyesha wapi nukata inapowekwa.
Wakati anafanya hivyo mimi nikachukua karatasi nyingine ya malipo, ambayo ilionyesha malipo yaliyofanywa na kusainiwa na kaka yake…nikasema;
‘Kama hii hapa, au sio…hii ndio sahihi kamili ya kaka yako au sio…?’ nikamuonyesha na yeye akaangalia, halafu akasema.
‘Ndio kama hiyo hapo muheshimiwa, hiyo ni sahihi ya kaka …haina shaka…’akasema kwa sauti yenye kuparuza…koo limekauka ghafla;
‘Sasa kama ni hivyo, kwenye hii stakabadhi ya malipo, au kwenye huu mkataba,… wewe usema tu,…ulisahau kuweka hiyo nukta ili ionekane kuwa kaka yako ndiye kachukua hizo pesa, umeliona hilo kosa ulilolifanya eeh…, au ni yeye alisahau kuweka hiyo nukta,..?’ nikamuuliza na Dalali akabakia kimia.
‘Dalali, Dalali… tuambie ukweli Dalali, muda unakwenda, au tumuachie hakimu yeye mwenyewe atajua jinsi gani ya kufanya, ila muhimu hadi hapa, hili deni sio la marehemu, hili deni ni la kwako, ..japokuwa huku juu limewekwa jina la mlipwaji ni l;a kaka yako, lakini huku kwenye sahihi sio ya kwake..kwanini, ..sasa utuambie wewe....’nikasema
Dalali, sasa akawa anahema tu…, kiti akakiona hakimtoshi,..jasho linamtoka, akawa anazichungulia zile stakabadahi za malipo, nikamsogelea na kumshika mkono..
‘Naona nikusaidie usimame, ..utoke kwenye hicho, kiti maana kinakubana, au sio..?’ nikasema na watu wakacheka.
Dalali hakujali hilo, sasa akasema;
‘Lakini mimi sijui lolote kuhusu hilo, kwangu imekuwa mshtuko, na hapa nilipo kweli naanza kukubali kuwa huenda kweli hilo deni sio la marehemu….naanza kuliona hilo….’akasema
‘Ehee..tuambie ukweli ni la nani, …?’ akaulizwa
‘Hapa inabidi tuwaulize vyema watu wa benki…’akasema
‘Kwanini wakati sahihi ni yako, ukumbuke wewe unawaamini sana watu wa benki, wao wana utaratibu wao mnzuri tu..si umelisema hilo tena na tena, au…kwanini sasa unaanza kuwatilia mashaka…?’ nikamuuliza
‘Kiukweli muheshimiwa,..ndugu yangu…hili….linanifanya niwe kwenye mshtuko, je ina maana mizimu,…ina maana benki, ..haiwezekani…siamini hiki, kuwa ni mimi niliweka hiyo sahihi…hapana lazima kuna mtu….’watu wakacheka.
‘Mizimu ndio iliweka sahihi, hiyo au una maana gani hapo…?’ nikauliza na watu wakazidi kucheka.
‘Msicheke jamani, hapa…mnacheza na maisha ya watu, ..huu ni uonevu, mimi sijawahi kuweka hiyo sahihim mkicheka mnanifanya mimi ni mjinga, mimi sio mjinga hapa naongea ukweli, na huo ukweli utakuja kuwasuta mwisho wa siku, ukweli ukija kubainika, kuwa mimi sihusiki na lolote hilo…nasema hivi, mimi sikumbuki kufanya hivyo, hata sijui,…mimi nasema ukweli kabisa, muheshimiwa hakimu…’akasema
Watu sasa wakabakia kimia,..na hakimu akawa anatuangalia tu…
‘Labda kwa kumbukumbu zako,…Je wewe uliwahi kuweka sahihi kwenye kitu kama hiki, au kwenye mkataba wowote huko benki kwasababu fulani nyingine,…?’ nikamuuliza
Dalali akawa kama anawaza halafu akasema;
‘Haa-ha-hapana..sio mimi niliyeweka bwana…’akasema hivyo, na watu wakacheka na hakimu akagonga rungu lake watu watulie.
‘Naona upo mbali sana…nauliza hivi, Ina maana wewe hujawahi kuweka sahihi…kwenye mkataba,… labda ulipewa tu huko benki na labda kwa bahati mbaya,… hukuwahi kuusoma kuwa ni mkataba,…labda…, kwa haraka zako wewe ukaweka sahihi yako tu, labda…eeh. Hebu kumbuka..?’ akaulizwa
‘Hata sikumbuki…..’akasema na watu wakacheka.
‘Dalali…kumbuka vyema ndugu yangu, hili sasa ni lako…sio la kaka yako tena, huu mkopo sasa ni wa kwako…’akasema wakili
‘Kwanini uwe ni mkopo wangu, mimi sijachukua huo mkopo,…siwezi kukubaliana na hilo kamwe….’akasema
‘Sasa Dalali, sisi tutakusaidiaje….hebu tusema hivi…, labda katika mabadiliko ya kibenki, ..eeh huko benki, si kulitokea mabadiliko …hilo si unalijua, au sio, maana wewe ulikuwa unafuatilia sana hilo….labda kipindi hicho, wewe…ulipewa nasema kwa mfano, maana haa hivyo haiji…au sio…’nikasema
‘Sijakuelewa muheshimiwa…?’ akaniuliza
‘Nasema hivi, jaribu kuvuta kumbukumbu zako, ukumbuke vyeka, kuwa labda ulitakiwa wewe uweke sahihi yako kwa niaba ya kaka yako…maana hapa kweli. hakuna nukta, kuashiria kuwa hayo malipo hakuweka sahihi marehemu , au siowewe ndiye uliweka hiyo sahihi,…?’ akaulizwa na akaendelea kuzitizama zile karatasi.
‘Dalali, hiyo sio sahihi yako……?’ akaulizwa
‘Inaonekana kama ya kwangu….’akasema
‘Lakini sio sahihi yako…?’ akaulizwa
‘Mimi siwezi kuwa na uhakika….’akasema
‘Kwanini…?’ akaulizwa
‘Ni kweli, kuna …kipindi nimeshawahi kuweka sahihi kwenye stakabadhi za benki kwa niaba ya kaka….na..na ..hata kwenye malipo…lakini aliniambia yeye mwenyewe kutokana na ya kwua alikuwa mbali, na alihitajia pesa kwa haraka….’akasema
‘Dalaliii….ujanja wako upo wapi, unakumbuka awali ulisemaje, kuwa kama ni malipo ya benki, wewe hujawahi kuweka sahihi, kaka yako ndiye alikuwa akifanya hivyo, wewe hukuwahi kuweka sahihi yako kwenye malipo,…hukusema hivyo awali…?’ akauliza na hapo akabakia kimia
‘Dalali,Dalali ....tuamini lipo sasa ndugu yangu, kauli ya kwanza au hii ya pili…?’ nikamuuliza
‘Awali nilisema nikimaanisha malipo, ndio…bro mara nyingi kwenye malipo alikuwa akiandika yeye na kuweka sahihi yeye, na ananipa mimi nikalipe au kuchukua pesa, ..lakini ilitokea dharura kama hiyo, ..ni mara moja au mbili hivi tu…’akasema na watu wakacheka,.
‘Ni mara moja au mara mbili hivi ti…, na huenda ya tatu na ya nne, au zaidi ya hapo, ndio ikawa hii ya kusaini malipo ya mkopo na mkataba, au sio…?’ nikamwambia kama kumuuliza, na yeye akakunja uso kama kukerwa, halafu akasema
‘Sio kweli muheshimiwa, mimi sijaweka sahihi kwenye huo mkopo, siwezi ku-ku-jua hilo lilitokeaje,..naombeni muda wa kufikiria tafadhali…’akasema
‘Unahitajia muda gani hivi wa kufikiri, maana tupo mahakamani, na muda ni muhimu sana, eeh, tuambie unahitajia muda gani wa kufikiri…?’ akauliza na hapo akabakia kimia…na alipoona anasubiria yeye kujibu akasema;
‘Nasema hivi,…kwenye malipo ilitokea hiyo dharura, nikafanya hivyo, lakini sio kwa huo mkopo, huo mkopo mimi sijui..na kiukweli kuna mambo mengine ambayo sio ya malipo, bro, alikuwa akisema niweke sahihi kwa niaba yake…’akasema
‘Kwahiyo ile kauli yako ya mwanzo unaikana…?’ akaulizwa, na kukaa kimia
‘Sijaikana,…mnielewe jamani…kuna utaratibu na dharura…kikawaida utaratibu wa bro ilikuwa hivyo,..lakini ikatokea dharura…’akajitetea hivyo.
‘Na je kwenye mkataba wa benki ilikuwaje maana ni sahihi yako pia…unaiona ilivyo,…, haina nukta mbele, hebu ikague vizuri, usije kusema imefutwa na nukta ya kaka yako, inakolea sana, nimepitia malipo yote aliyoweka sahihi…ni hivyo hivyo, angalia, hii nah ii na hii hapa, nukta imekolea sio y akugusa…naona alihakikisha hiyo nukta inaonekana vyema…’akaambiwa
‘Ni kweli, yeye alihakikisha kwenye sahihi zake zote hiyo nukta inaonekana vyema, aliwahi kuniambia kwenye sahihi, kila kitu kwake ni muhimu, na …hiyo nukta ikawa …ni kama nembo yake, kwenye sahihi yake kutofautisha na sahihi yangu…’akasema Dalali.
‘Hapo umetusaidia sana..sasa tuambie…eeh au, bado unahitajia muda wa kufikiria zaidi…?’ akauliza na akabakia kimia
‘Au bwana Dalali…, labda tukusaidie hivi..…labda uliambiwa uweke sahihi hiyo na benki bila yaw ewe kujua,…mhh, au danganya danganya hivi, kujitetea..labda kuna mtu alikuhadaa, …kijana wako labda,…?’ akauliza na bado akabakia kimia
‘Au…labda, ….yeye huyu huyo, alikuambia kuna mambo ya kibenki,…akakuhadaa hivyo, na wewe ukaweka sahihi …ukijua ni ni mambo ya kibenki, ukiweka kwa niaba ya kaka yako hukujua kama ni mkopo, au…?’ akaulizwa.
‘Mhhh….lakini sio mkataba…ilikuwa kitu kingine, mimi mkataba nakuwa nao makini sana, kiukweli,..nimechanganyikiwa…’akasema
‘Haya hicho kitu kingine ni kipi labda…?’ akaulizwa
‘Kiukweli mimi sikumbuki jamani… mimi kiukweli, nikiambiwa kitu ‘m-ka-ta-ba’ ninakuwa makini sana na kilichoandikwa, ..na hii inatokana na kazi yangu ilivyo,…sasa hili hata sielewi, ilikuwaje, kiukweli mimi nisikumbuki, na kiukweli sijui lolote kuhusu hilo deni, kuwa ni mimi niliweka hiyo sahihi…sikumbuki, …ngoja nifikirie..’akasema sasa akishika kichwa
‘Haya chukua muda wa kufikiria, tunakusubiria …’akaambiwa, na hakimu akasema;
‘Kwa vile tumeongea sana, natoa dakika chache za mapumziko, huku shahid naye akipata muda wa kukumbuka,….’akasema hakimu, na mimi pake nikamuangalia Dalali, halafu nikageuka kwenda sehemu yangu ya kukaa..
Kabla sijatulia vyema nikaguswa bega na mtu, nikageuka kuangalia ni ndani, nikapewa karatasi, imeandikwa.
‘Naomba niongee na wewe…’ mama mjane.
Nikgeuka upande ule alipokaa mama mjane, sikumuona, nikageuka upande wa pembeni, nikamuona kasimama, huku akiangalia upande huo tulipokaa, nikajua ananisubiria mimi, akilini nikawa najiuliza huyu mama kagundua nini
Nikamuelezea wakili kuwa natoka kidogo.
‘Unataka kwenda wapi, huyo mtu ni wa kwako…’akasema akimaanisha Dalali.
‘Nipo,..siende mbali…’nikasema na kuanza kutoka ile sehemu kuelekea upande wa kuelelea mlango wa chooni, ndio nikamkuta mama mjane ananisubiria.
‘Vipi dada, kuna nini….maana unajua mimi ndio natakiwa kumuhoji shemeji yako…?’ nikamuuliza
‘Ndio maana nikakuhitajia, ni kuhusu hilo hilo, kumuhusu Dalali…’akasema
‘Ehee..ongea kwa haraka kidogo, …ana nini…?’ nikamuuliza
‘Dalali anasema kweli, kuwa hilo deni halitambui…’akasema na kunifanya nimuangalia mara mbili tatu, nikajikuta nimesema hivi
‘Shemu…ooh, dada wewe na Dalali, mna nini…unajua nimegundua kitu, wewe unapenda kumtetea sana..je huoni kuwa tayari keshaingia kwenye hali ya kukubali, kuwa hilo deni sio la kaka yake, bado kidogo tu ataongea kila kitu…’nikasema
‘Kaka, pamoja na hayo, sema ukweli wako, je unaamini kuwa kweli Dalali anaweza kulifanya hilo kwa kaka yake…?’ akaniuliza
‘Ndio maana nimetaka nimuhoji mimi…nitakuja kumweka mahali atasema ukweli wote…..inawezekana katumiwa, lakini anaogopa kumsema huyo mtu aliyemtumia,…’nikasema
‘Dalali…hajui lolote,….sio kwamba nasema haya kwa kumtetea, au kama unavyofikiria wewe..hapana, mimi namfahamu sana shemeji yangu, akisema jambo la uwongo, ukimuuliza mara mbili tatu, …atakubali tu, na kuna dalili usoni, y akumtambua kuwa anasema ukweli au uwongo, hajui, kudanganya kwa muda mrefu…’akasema mama mjane
‘Kwahiyo unatakaje…maana kama sio yeye, basi ni mume wako…’nikasema
‘Mume wako hahusiki na hilo deni, na pia Dalali, atakuwa hajui…nakuomba usimshinikize kwenye jambo ambali hajalifanya…’akasema mama mjane
‘Mhh…sawa …je wewe unahisi ni nani basi…maana unaongea kama vile unamfahamu mtu mwingine…au wewe kuna kitu unakifahamu kutokana na hilo deni…?’ nikamuuliza
‘Kiukweli hapa nilipo …kwanza nina furaha kuwa hilo deni sasa linatambulikana kuwa sio la marehemu..lakini bado sijawa na amani, ni nani alilifanya hilo, kiukweli sina mtu ninayemuwazia…na..ni nani alifanya mpaka akapata ajali…’akasema kwa sauti ya huzuni.
‘Sawa nimekuelewa shemeji, ngoja tukaendelee maana hakimu huyo kaingia…’nikasema na kuachana na huyo mama mjane…wakati naondoka nikageuka kumuangalia, nilimuona akiuta machozi.
Hakimu akasema kesi iendelee…na mimi nikamsogelea Dalali, na kumuuliza.
‘Bwana Dalali, natumai umepata muda wa kutosha, kufikiria, je sasa umekumbuka,…?’ nikamuuliza na Dalali, kwanza akatulia kidogo, baadae akasema;
‘Oooh…nimekumbuka, ….sasa nimekumbuka,…’akasema akijaribu kama kusimama, halafu akajiweka vyema
‘Unataka kusimama…?’ nikamuuliza na yeye akatikisa kichwa kukataa..
‘Basi ongea…tukusikie…’nikasema
‘Yah…nimekumbuka….sijui kwanini nililisahau hilo…kunaah. Eeh…. kipindi kulikuwa na mabadiliko pale benk, kwenye hiyo benki kulitokea kitu kama mageuzi, kiongozi yule wa zamani wa hiyo benki, aliachishwa, akaletwa mwingine, kabla ya …hayo mageuzi, nakumbuka kulitokea mabadiliko, tukaambiwa wenye akaunti, wanatakiwa kupeleka kumbukumbu zao upya……ndio ndio..…sasa nimekumbuka…’akaniangalia na mimi nikawa kimia tu.
‘Inaonekana wewe unalifahamu hili, ndio maana unanisaidia nikumbuke na kunisihi sana nikumbuke....’akasema akiniangalia mimi.
‘Mimi sijui kitu, nataka wewe ukumbuke tu, maana wewe ndio ulikuwepo…’nikasema
‘Ndio…nashukuru sana kwa hilo,…umesaidia kukumbuka…, lakini eeh…sina uhakika saana…, kuna muhasibu mmoja alinisainisha, kitu kama hicho…’akasema na kukaa kimia kidogo.
‘Ile siku ilikuwa na shughuli nyingi pale benki…na mimi mwenyewe nilitngwa na shughuli nyingi sana…na hata bro, alikuwa na kazi zake za kibiashara alitakiwa kusafiri, kwahiyo …nilipomuambia hilo, kuwa kuna kumbukumbu zinahitajika, yeye alisema kila kitu chake kipo benki,..hawezi kupoteza muda kwa hilo…akaniagiza pesa kidogo…’akatulia
‘Nilipofika, nikaambiwa mpaka niwasilishe hizo kumbukumbu..nikampigia bro simu…akaniambia basi, kama haiwezekani kwa leo, basi, niache tu…sasa wakati nataka kuondoka,…maana kulikuwa na pilika pilika nyingi sana,.., akaunti nyingi zilikuwa zinarekebishwa, watu wanataka pesa…na ndio muhasibu akaniita…’akatulia
‘Kwa ile hali…na..nakumbuka nilikuwa na mnada wa kufanya, wenzangu walishanipigia simu kuwa nachelewa,…sasa kwa hiyo hali,..nahitajika huko, huku benki muhasibu ananiambia kaniita, ..na anajua hawezi kuniita kwa jambo lisilo la muhimu…nikamuendea
‘Aliniambia akaunti ya kaka yangu haina shida ila mwenye akaunti anahitajika kuweka sahihi zake na inatakiwa siku hiyo hiyo…, ndio maana tulitangaziwa…na kama isipofanyika hivyo, itabidi afuate taratibu zote kama kufungua akaunti upya…
Unajua kitu kikipangwa kimepangwa,…nikamwambia huyo muhasibu..
‘Kwani nikimuwekea sahihi kwa niaba yake…haina shida,….unaona sahihi yangu na yake zinafanana kabisa,na hata kama nitakosea yeye mwenyewe....baadae bro, atakuja kuliweka sawa, hatuna muda wa kufungua tena akaunti, inasumbua…’nikasema
‘Haiwezekani, anatakiwa yeye mwenyewe aweke sahihi…’akaniambia na mimi pale nikampigia simu Bro, akawa hapatikani…nilichofanya nikuchukua zile eeh, kwa pale mimi niliona kuwa ni..kumbukumbu za kibenki za kuweka sawa akaunti za watu..juu ilionyesha hivyo, …sasa mimi sijui kwa ndani, sikusoma…kwa haraka nikatafuta sehemu ya sahihi nikaweka,….’akasema
‘Mhh…umefikria sana, kubuni hadithi hiyo…’nikasema
‘Ni kweli muheshimiwa,..na kwa vile nilimuamini sana yule muhasibu,…nikafanya haraka kuweka sahihi nikamrejeshea, akaniuliza je keshaweka sahihi, nikamwambia ndio..’
‘Na dole gumba, ..’akasema na mimi nikamwambia
‘Jamani ataweka dole guma mara ngapi…juzi tu ulinipatia zile…karatasi nimpelekee akaweka dole gumba, na sahihi yake sasa ya nini tena…?’ nikamuuliza
‘Ok…ok, nimekumbuka,..kumbe ..basi hilo halina shida…’akasema hivyo..
‘Sasa kiukweli mimi sikupata nafasi ya kusoma maelezo yote, nilisoma tu pale juu…huo ndio uzembe wangu…’akasema.
‘Kwahiyo huo ni mkataba, je kwenye kuweka sahihi ya mkopo wenyewe, maana huu hapa unaonekana, kiasi, jina la mkopaji, ..inajieleza hapa haijifichi kitu, uliwekaje hii sahihi hapa…?’ nikamuuliza
‘Siku ile ile nakumbuka …eeh, ndio yule muhasibu, alisainisha kitu…alisema kwa vile kuna kuhamishwa,…pesa kutoka akaunti ya zamani,..anahitajika kuweka sahihi kwenye karatasi ya malipo…mimi niliangalia nikaona jina la bro..ni jina lake…nikafanya vile nikatoka nje, na baadae nikarejesha,…ilikuwa kitendo cha haraka…’akasema.
‘Hukusoma kabisa kilichoandikwa…?’ nikamuuliza.
‘Kiukweli kwa siku ile ni mara yangu ya kwanza kufanya uzembe huo, sikuweza kusoma….’akasema
‘Huyo muhasibu ndio nani…?’ akaulizwa
‘Alikuwa muhasibu wa benki kipindi hicho…’akasema
‘Yupo wapi huyo mtu kwa hivi sasa…, bado yupo benki au alishaacha kazi…?’ akaulizwa
‘Ni marehemu…’Dalali akasema na hapo watu wakacheka…kicheko kile kilimfanya Dalali, awageukie watu, na kusema;
‘Mnacheka nini sasa..ni kweli ninayoongea, ..msione kuwa ni mzaha huu…hili lilifanyika, waulizeni watu wa benki kama tendo hilo halikutokea,…aliniita huyo muhasibu, tatizo huyo muhasibu hayupo tena duniani…’akasema
‘Alifariki lini…?’ akaulizwa
‘Nahisi ni kipindi kile kile…baada ya hilo tukio, niliwahi kufika pale banki nikamuulizia, nikaambiwa huyo muhasibu hayupo tena duniani…kiukweli iliniuma sana, maana alikuwa mhasibu aliyependa kusaidia watu…’akasema
‘Unauhakika …?’ akaulizwa
‘Uhakika gani sasa, huyo muhasibu ni marehemu, kaulizeni huko benki…au huyo wakili hapo, anaweza kunisaidia kwa hilo…’akasema akimuangalia wakili wa benki ambaye alikuwa kama hana habari na maelezo yake.
‘Wakili wa benki anamfahamu sio,..kuwa huyo muhasibu ni marehemu, naona wakili hata hana habari na maelezo yako anaona unadanganya…?’ akaulizwa
‘Huyo wakili anaweza kunisaidia kulifuatilia hilo, kama mnataka , huyo muhasibu ni marehemu, alikuwa anaitwa nani…mmh, jina lake..…’akasema akawa kama anatafakari
‘Sasa kama huyo mtu ni marehemu, atakusaidiaje kwenye maelezoo yako, na hata jina lake hulikumbuki, na wewe kiuzoefu huwa husau mambo, iweje leo…?’ akaulizwa, na hapo akabakia kimia
‘Huyo ndio shahidi wako wa kukutetea,..lakini atakuteteaje kama alifanya hivyo kwa nia ya kukubebesha huo mkopo, na kwanini afanye hivyo…?’ akaulizwa.
‘Ndio hapo….hata mimi sijui…ila nazungumzia hivyo, kama ulivyosema nikumbuke, ni kweli nilisainishwa kitu kama hicho,…na sio kusainishwa, niliweka sahihi mimi mwenyewe, nilijua sahihi ya ngu na bro, hazitofautiani, …ama wa hiyo nukta mara nyingi nasahau….na kwa kipindi kile mimi nilijua ni kwa ajili ya utaratibu wa kibenki..na..sikuwa na ..sikuwa makini, kuwa huo ni mkataba wa kibenki…’akasema
‘Dalali anasema …sasa anasema hivyo, kuwa yeye alisainishwa au aliamua kuweka sahihi kwenye kitu asichokijua,,…awali alisema yeye yupo makini sana kwenye vitu kama mkataba kutokana na uzoefu wa kazi yake…
Sasa anadai kuwa aliyemfanyia hivyo hadi akaweka sahihi, ila hana uhakika ilikuwa ni kitu gani,..aliyefanikisha hilo …ni marehemu…jamani,…mnamuelewa huyu mtu…’nikauliza nikiangalia watu.
Watu wakacheka kidogo.
Na mara sauti kubwa ikasikika kwa nyuma ikisema;
‘Huyo muhasibu sio marehemu, yupo hai….’…
Watu wote wakageuka kuangalia wapi sauti ilipotokea, …na hakimu naye akawa anaaangalia usawa wa watu, kuitafuta hiyo sauti ilipotokea,…na ile sauti ikarudia tena..
‘Huyo muhasibu yupo hai…samahani kwa kuingilia ila mimi ninao ushahidi kuwa huyo muhasibu hajafa, na kama Dalali kasema hivyo kwa nia ya kufiria kuwa huyo muhasibu hayupo duniani, kiukweli…huyo muhasibu bado yupo hai …’sauti ikasema
Sasa ile sauti ikajulikana inatokea wapi…
‘Wewe ni nani hebu pita huku mbele…’kasema hakimu…, na watu wakawa wanampisha huyo mtu…safari hii ni tofauti na ilivyokuwa awali, mtu akitaka kupita mbele ni mpaka itokee kusukumana…
Huyo mtu akasogea hadi mbele, …..
NB: Raha si raha…nakatiza kwa muda….

WAZO LA LEO: Kila mtu anapenda kupata,..kila mtu anapenda yeye aonekane zaidi, au ajulikane zaidi, (umaarufu), na watu kama hao, wanapenda mambo yao yapewe kipaumbele na yasipofanyiwa hivyo, inakuwa ni taabu kwao…. Watu kama hao, hata kama wanacho, bado watakuwa wanataka zaidi,(hawatosheki) .Huo ndio ubinafsi wa kibinadamu, ukiendelea hivyo, ndio dhuluma inakuja kuchukua nafasi, hakuna kujaliana tena hapo.

emu-three