‘Huyo muhasibu yupo
hai…’sauti ikasema
‘Wewe ni nani hebu
pita huku mbele…’akasema hakimu
Watu sasa wakawa
wanampisha huyo mtu…safari hii ni
tofauti na ilivyokuwa awali, huyo mtu alipishwa kwa nidhamu, hadi
akafika sehemu ya kuonekana, maana licha ya kuzuiwa watu kujaa, bado wengi
waliweza kuingia,
Jamaa sasa akawa
keshafika mbele, kwa upeo wa kuonekana na kila mtu,..akawa anatembea taratibu
kama vile anataka kila mtu amuone, ..hadi akafika sehemu karibu na shahidi
aliyekuwa akihojiwa.
‘Wewe ni kwanini na
kwanini hufuati taratibu za mahakama…?’ kaulizwa
‘Muheshimiwa hakimu,
kama ningeamua kusubiria utaratibu huenda nisingelipata nafasi ya kufika hapa
hii leo…kuna mengi hamjayafahamu bado..’akasema , na hakimu akawa anamuangalia
kwa makini, na jamaa alipoona hakimu anamuangalia sana akasema
‘Najua labda …sina
uhakika lakini, hakimu unaweza kunikumbuka…mimi nakukumbuka sana, wengi wa leo,
wakiniona hapa, wasio kuwa na moyo wa uvumilivu wanaweza kukimbia, au
kuzimia…’akasema
Hakimu akawa anateta
na wenzake, halafu baadae akasema
‘Kwa upendeleo wa
dharura, shahidi uliyekuwa ukiongea, usubiria kwanza, ili tuweze kumsikia huyu
mtu, nataka kufahamu zaidi kuhusu yeye, na kwanini anatoa kauli kama hiyo
ambayo, inasigishana na kauli yako, …’akasema hakimu.
Hakimu akamuangalia
wakili, kama vile anataka kumuarisha afanye jambo, na wakili akawa kimia tu.
Mimi pale nilipo
nikamtupia jicho Dalali, Dalali alikuwa vile vile kama kagandishwa akimuangalia
huyo mtu aliyeingia, mpaka nikaingiwa na wasiwasi, na kwa haraka nikageuka
kumtafuta mama mjane kwa macho, sikumuona ile sehemu yake aliyokuwa amekaa
awali, sijui kama alitoka kidogo, au kaenda wapi, sikuwa na muda wa kumfuatilia,
mawazo yangu yakaelekea kwa huyo mtu aliyeingia sasa hivi, nikijiuliza je ni
nani huyu mtu, na kwanini uwepo wake umeweza kumdatisha Dalali.
Mimi nikamsogelea
wakili , na kumnong’oneza jambo, na kwa haraka akamtupia jicho Dalali, halafu
akatikisa kichwa kama kusikitika
‘Unahisi yupo sawa…?’
nikamuuliza
‘Atakuwa sawa, sema
labda hakutarajia kumuona huyo mtu,…’akasema
‘Kwanini…?’
nikamuuliza wakili
‘Wewe subiria
tu,….’akasema wakili na kunifanya na mimi niwe gizani, sikuipenda hiyo hali, …
Dalali sasa akawa kama kalegea hivyo, kaegemea
upande mmoja, kama anataka kudondoka,…na docta aliyekuwa mbali akanyosha mkono,
huku akiashria kwa hakimu amuangalia Dalali, na hakimu akamuona..akatambua
docta ana maana gani.
‘Vipi wewe Dalali una
nini…?’ akauliza hakimu sasa akimshangaa Dalali ambaye alikuwa kalegea
kabisa,…na Hakim kuona hivyo, akasema
‘Docta hebu muangalia
huyo mgonjwa wako, kama ana tatizo lolote…’akasema hakimu na docta akasogea
pale alipokuwa Dalali na kuanza kumpima pima, baada Dalali, akawa kama
kazindukana, na kwa haraka akawa kama anataka kusimama, lakini akawa
anashindwa..baadae sauti ikatoka kwa Dalali ikisema;.
‘Haiwezekani, huu ni
mzuka….’akasema Dalali akiendelea kumtolea macho huyo jamaa aliyeingia.
Yule jamaa sasa akawa
kamkaribia Dalali….Dalali…akajaribu kuinua miguu, lakini hakuweza, huyo
akaporomoka chini…watu wakawa wanasukumana ili kuona kinachoendelea huko
mbele..
‘Watu wa usalama
…’akasema hakimi na watu wa usalama wengine wakawa wanawatuliza watu wengine
wakimsaidia Dalali kuweza kukaa kwenye kiti chake tena.
‘Vipi wewe unaogopa
nini…?’ akauliza
‘Huyu siamini kama …ni
binadamu…’akasema
‘Kwanini…?’ akalizwa
‘Nijuavyo mimi alikufa
na kuzikwa hata mkienda makaburini mtaliona kaburi lake…’akasema
Huyo mtu hakujali hicho
anachoongea Dalali, yeye akajisogeza hadi mbele, na kusimama, …..
‘Haya hebu tuambie
wewe ni nani, na kwanini unaingilia Mahakam , si unajua tarataibu za mahakama,
kwanini unapayuka huko nyuma…?’ akaulizwa
‘Imebidi nifanye
hivyo, kwa maana kama ningelikwenda moja kwa moja kwa watu wangu
nikajitambulisha, nina imani wengine wangelikimbia…kama unavyoona huyu
hapa…ananifahamu vyema, na anafahamu kuwa mimi ni marehemu…’akasema
‘Ina maana wewe ndio
huyo….’kabla hajamaliza kuulizwa, yeye mwenyewe akasema;
‘Mimi nilikuwa muhasibu
wa benki kabla sijafukuzwa, na kutambuliwa kuwa nimeshafariki,…ndivyo
inavyojulikana hadi hii leo…huko benkia nilifukuzwa kwasababu ya njama za bosi
wangu,..’akasema
‘Bosi wako ndio
yupi..?’ akulizwa
‘Majaliwa…’akasema
‘Tuambie ilikuwaje…?’
akaulizwa
‘Ukweli wa hili jambo
naufahamu sana mimi kuliko yoyote hapa..,..na ndio maana ilisaidikiwa kuwa mimi
nimekufa..lakini sikuwa nimekufa, nililipwa pesa nyingi, nitoweke, na ni baada
ya kuonekana hivyo, kuwa mimi nimeshafariki,..lakini kuna kitu kilinifanya
nirudi tena…’akasema
‘Kitu gani…?’
akaulizwa
‘Marehemu mtaalamu ni
baba yangu wa kufikia, …yeye alizaa na mama yangu, na kupatikana kwa mimba hiyo
ni kutokana na michezo yake mibaya, nilikuja kuambiwa na bibi, mama yake mama
yangu..
Bibi aliniambia, kuwa …baada
ya kuzaliwa mimi, mama alinitambulisha kwa huyo baba, …kiukweli huyo baba
hakunikataa kama unavyoona tunafanana naye sana,..alipokubali hilo, akafanya
mambo yake na mama yangu akawa anaumwa sana, ulimi ukawa unavimba, akawa hawezi
tena kuongea, hadi anafariki…’akasema.
‘Kwanini mama yako
aliumwa hivyo, ni ugonjwa wa namna gani.?’ Akaulizwa
‘Marehemu ..alikuwa na
tabia hiyo, kuwachezea wanawake, baadae akiwachoka anawateketeza kwa mbinu
hizo, lengo lake ni kutaka wasije kusema lolote kumuhusu yeye..na niliposikia
hii kesi nikaona wakati umefika wa kuyabainisha haya…
Yaliyotokea kwa mama
yake Majaliwa ni hayohayo yaliyotokea kwa mama yangu, na Dalali, alihadaiwa
afanye hayo,… kama kinga, hakulijua hilo…mimi nimehangaika sana
kumtafuta…Majaliwa, ili niongee naye sikufanikiwa, nikaona nije hapa, lolote
liwalo na liwe…Huyu Dalali, yawezekana siku ile yeye alitumiwa hivyo, ambake
huyo binti, kuuficha ukweli wa marehemu…na huenda hiyo mimba ni ..ya
marehemu…’akasema
‘Niliposikia habari
ikiongelewa, kuhusu yaliyotokea kwa mama wa…Majaliwa,.. imeniuma sana…
nikakumbuka kilichotokea kwa mama yangu na wengine wengi walioafanyiwa hivyo, nimeshindwa
kuvumilia, nipo tayari kuhatarisha maisha yangu, kwa ajili ya hili….’akasema
‘Ehe, haya…tuambie
sasa hayo ya bank…?’ akaulizwa
‘Bila shaka….mimi …,
nitawaambia kila kitu…ninatambua baadhi ya njama za hayo madeni maana
nilikuwepo yakifanyika, …na baadhi ya mbinu za kulifanikisha hilo ilitokana na
marehemu,..’akatulia
‘Kuna watu hawajui,
kuwa mtaalamu,…aliwahi kufanya kazi benki…akaacha, na kujiingiza kwenye mambo
ya kiganga, anasema aliacha kwa kutii wito wa mizimu, kwahiyo mambo ya benk
anayafahamu…yeye ndiye alifanya mipango nikajaariwa benki…na kila mara alikuwa
akinitembelea kazini, hasa akiwa na shida ya pesa, na… siku moja aliniambia,
amegundua jambo, nikamuuliza jambo gani, akasema;
‘Unajua kuna sahihi za
watu wawili zinafanana, na hao watu ni maadui zangu, ila hawajui kuwa wao ni
maadui zangu, nataka kuwamaliza, na kuna mtu naye …tutamtumia lakini hatakiwi
kulifahamu hilo, hata yeye ni adui za hao watu…’akasema hivyo.
‘Wawili hao ni akina
nani…na mimi nahusikanaje na hilo…?’ nikamuuliza
‘Wawili hao ni Dalali
na kaka yake, je wewe si mahasimu wa hao watu?’ akaniuliza
‘Ni kweli lakini mimi
sina haja ya kuwafanya lolote, nilishawasamehe tu…’nikamwambia
‘Sikiliza bwana mdogo,
mimi…nimegundua jambo, hata kama umewasamehe..lakini kwa kupitia wao, tunaweza
kufaidi,..wewe wataka kuishi masikini mpaka ufe…’akasema. Kiukweli hiyo familia
ni watu wasio na uhusiani mnzuri na familia yetu…kuna migogoro ya maeneo unajua
tena..’akasema
Basi nikamuuliza
mtaalamu,kwahiyo…unataka iweje?’ nikamuuliza
‘Usiwe mjinga
bwana…mimi najuana na huyo meneja wa benki, alikuja kwangu, akitaka nimfanyie
mambo fulani, fulani…unajua mambo mengine hujileta tu,..Dalali, aliwahi
kuniambia sahihi yake inafanana na ya kaka yake…sikumoja alipokuja huyo meneja,
anakuja kwa kunizoea, pamoja na mambo yake mengine,nikaongea naye kuhusu
kufanana kwa sahihi, …huyo meneja ni mjanja sana, …akanielewa, ila hakuwa
anawafahamu watu vizuri, ni nani wa kushirikiana naye..’akasema
‘Una maana huyo meneja
bosi wangu, aje kwako kwa mambo kam hayo, kwa umasikini gani alio nao,…haiwezekani…?’
nikamuuliza
‘Hayo mengine
huhitajiki kuyafahamu, wewe si unataka kuwa tajiri, sasa wakati umefika,
nimeshaongea na huyo mkuu kasema hayo nimuachie,…ila yeye anahitajia mambo
fulani kutoka kwa mtu wa nje…ndio maana alipofika kwangu, kwa shida zake
akaniamini..’akasema.
‘Mhh,…mimi sikuelewi, sasa
wewe unataka mimi nifanye nini…?’ nikamuuliza.
‘Nimekuambia…mengine
hayakuhusu..kuna mambo nitakuwa nakuambia uyafanye, usiulize kwanini niyafanye…ila
wewe utalipwa vizuri sana, unasikia,..umasikini bye bye..kama utafanya
nitakavyokuagizia, utakuja kunishukuru, mimi niliacha kazi benki lakini bado
nina ndoto za kupata utajiri kwa wazo langu hilo, na wazo hilo kumbe kuna
mwenzangu naye alikuwa nalo…’akaniambia.
‘Kiukweli nililipinga
sana hilo…lakini kukatokea hali ya mchafuko hapo banki,..mageuzi, mbali mbali,
nikajikuta na mimi ni miongoni mwa watu wanaotakiwa kupunguzwa hapo
kazini..lakini kwa haraka nikahisi ni mbaya wangu, bosi Majaliwa…’akasema.
‘Kabla ya kufikia
hatua hiyo ya kupunguzwa kazi, ndio
mtaalamu akanijia , na kuniambia, sasa umeonaeeh…usijali kwa haya yaliyotokea,
kuwa wewe unapunguzwa kazi, hiyo ni sehem ya mikakati ya kukufanya wewe uwe
tajiri, lakini kabla ya kuondoka, kuna
mambo yanatakiwa wewe uyayafanye kwa haraka…’akasema
‘Umefahamuje kuwa kuna
zoezi kama hilo…haya ni mambo ya ndani ya benki…?’ nikamuuliza
‘Usiulize sana…wewe
utapunguzwa kazi, ni katika kufanikisha mambo ya utajiri, unielewe hapo, na
usipofanya hayo, unajua ni nini kitatokea kwako, kwanza utakosa nini, eeh, wewe
waenda kijijini utaishije, au unafikiri utapata kazi haraka, kazi hapa
nilikufanyia mpango mimi…’akasema.
‘Kiukweli nilishajua
kuwa kazi sitakuwa nayo tena, ..nikakubaliana nao, nilichotakiwa kukifanya ni
kusimamia mikopo, kuwasainisha watu, wanaohusika…sasa mojawapo ya vocha hizo ni ya huyo marehemu, na kwa
vile sahihi yake marehemu inafanana na y a Dalali, mimi sikuwa na tatizo,
nikampigia simu Dalali, akaja…
‘Nilimuelezea kuwa
hapo benki kuna mabadiliko, na ni ya haraka, yeye anatakiwa kwanza akalete Dole
gumba la kaka yake, na sahihi yake…lakini muhimu ni dole gumba la kaka yake,
sahihi hata yeye anaweza kuiweka…’akasema
‘Dalali,
alikubali,…hakutaka hata kuuliza zaidi..kesho yake nikapata nilichokitaka na
yeye akaweka sahihi…kwa kila nilichomuambia aweke sahihi…, hakufahamu kuwa
anapitisha deni la kaka yake…kiukweli sikupenda hilo, lakini ningelifanya
nini…watu hawamfahamu mtaalamu, ni mchawi wa kutupwa….’akasema.
‘Kwa vipi, na
tutaaminije hayo unayotuambia, unaongea kuhusu marehemu nay eye hayupo hapa
kujitetea..?’ nikamuuliza.
‘Kuamini haya
mtafuteni huyo meneja wa hiyo benki ya zamani, mtajua kila kitu…na chunguzeni
kufukuzwa kwangu kama sio kwa njama…ulizeni kufariki kwangu kulikuwaje, je watu
wanaonifahamu wanajuaje kuhusu mimi, …’akasema
‘Mimi baada ya kupokea
barua ya kuachishwa kazi , ilitakiwa nionekane nimejiua, kutokana na kuonea,
halafu maisha magumu, iliandaliwa hivyo, walioshuhudia kifo changu waliona huo
ujumbe niliouwacha....na kuna dawa nilipewa na mtaalamu, nilipomaliza kuzinywa,
nilipoteza fahamu, hata mtu akinipima anaona nimekufa kabisa,…’akasema.
‘Una uhakina na
unachokiongea, na kwanini hukukataaa aukutoa taarifa polisi, na kama ulikufa
hukuzikwa, au hapo ilikuwaje..?’ akaulizwa.
‘Sikuzikwa mimi,
ulizikwa mgomba, mimi baadae nilisafirishwa usiku hadi mikoani, huko nikapewa
dawa ya kunirejesha fahamu…na pesa nyingi za kutumia, na onyo, kuwa mimi
kuanzia muda huo sipo duniani,..na ikitokea nikarejea Dar, basi ndio itakuwa mwisho wangu wa
kiukweli…wataniua…kwahiyo, eeh…ikatambulikana hivyo kuwa mimi nimeshakufa, na
hata familia yangu ilijua hivyo, huko nilikaa na kuoa mke mwingine..’akasema.
‘Ulioa..!! na mke wako na watoto wako walikwenda wapi…?’
akaulizwa
‘Hiyo pia ni moja ya
mipango yao ya kunifanya niisahau familia yangu,..awali nilijua ndio hivyo …hata
hivyo…kabla mambo hayajawekwa hivyo, mimi kufa na kutoweka, nilipewa nichague
moja, niachane na familia yangu, iwe hai, huru na tajiri, au nisaliti huo
mpango, familia yangu iteketee, tena kwa moto…’akatulia
‘Unajua watu hawa
wanapenda sana kutumia moto kuangamiza jambo….wakitaka jambo lipotee kabisa,
wanatumia moto…sasa kwa vile nilishawahi kuona matendo hayo kwa watu wengine
waliofanyiwa hivyo, sikupenda kabisa hilo lije kutokea kwenye familia yangu,
nikaamua kufuata watakavyo wao…nikimuomba mungu kuwa ipo siku haki itatenda…mungu
yupo…
‘Kwahiyo mimi
nilifanya hayo baada ya kutishiwa maisha yangu, mimi na familia yangu, kuna
mambo makubwa yalitokea kwenye familia yangu, kabla ya ..kufikia huko, familia
yangu iliteseka sana…nisingelipenda kuyaelezea hayo, wenyewe mkiwauliza
watawaambia, huo ni ushahidi kwenu, sitaki kuuingilia…’akatulia
‘Ndugu zanguni…haya
sio utani, utaamini hayo ninayoyasema siku yakija kukukuta, watu hao waliamini
kwenye mali, na adui wao ni yule anayeingilia mipango yao..na ukiwa adui yao, …tiketi
yako ni kifo…tiketi yako, ni kukatwa ulimi…kama watataka uendelee kuishi
kidogo, lakini lazima watakumaliza…na wanaweza kukupatia sumu, ikakutesa, na
ikaonekana ni kansa…utakufa tu…’akatulia
‘Sasa swali mtaniuliza
kama hayo yapo na yanafanyika, ..je kwanini sasa nimeamua kurudi, siogopi tena,
kiukweli kilichonipa nguvu yakurudi huku
ni kwa vile nimesikia Mtaalamu hayupo tena duniani, huyu kwa hapa nchini ndiye
walimtegemea kwa kuangamiza, kimiya kimia au kwa nguvu za giza, ..pia ni kwa
vile…mfadhili wao, kakimbia hapa nchini, hayupo tena, hawana pesa tena…’akasema.
Hapo hakimu akawa
anaongea na watu wake, baadae akamgeukia huyo mzungumzaji mpya, na huyo
mzungumzaji akasema;
‘Na ndugu zanguni …hili
jambo lilikuwa sio mpango wa mtu mdogo
kama Majaliwa, kama…eeh…hata huyo
marehemu, sawa yeye alipewa hiyo kazi tu kwa vile ni mjuvi wa mambo ya giza na kwa
vile ni wao walimfundisha hizo nguvu za giza, walimuona ana kipaji hicho cha
kurisi…lakini wanaofadika na wengine analipwa nini , kidogo tu.
‘Haya ...huyo
Majaliwa, sizani, kama alikuwa akifahamu mpango huo kiundani, labda…mimi sijui
zaidi, maana sikuambiwa, haya ninayowambia nimeambiwa….jinsi mipango ilivyopangwa,
huyo Majaliwa, …yeye kaingizwa kama kiini macho tu, kwa vile ana visasi vyake,
basi ikaelekezwa huko, ionekane hivyo…labda mimi sijui zaidi…lakini nina imani
yeye hajui zaidi ya hivyo nijuavyo mimi...’akatulia kidogo.
‘Hata mimi….kuyafahamu
hayo…ni baada ya kuwasiliana na mtaalamu, wakati anakaribia kukata roho,
nilifika kwa siri kumuona aliponiona alinisikitikia sana, kwanini nimerudi, na
nilipofanya ukazidi wa kurudi huko nilipotoka ndio akaniambia…
‘Kijana mimi nakufa,
sitaishi tena, sasa kama huamini haya shauri lako, kwa vile sitaishi sana,
nitakusimulia, ila nataka uwe na ushahdi unaoweza kuja kukusaidia, chukua
video, ili iwe ushahidi, nahisi hili litanipunguzia dhambi zangu..na kwako wewe
hata sijui nikusaidieje,…ila nataka uje kuwasaidia baadhi ya watu wanaotumika
bila kujijua, wajue kuwa wapo hatarini…mzee mtupe anaweza kukusaidia,…haya ni
mikakati ya kundi haramu…wao wakikuchoka, wanakumaliza…’akasema
‘Kundi gani hilo
mtaalamu…?’ nikamuuliza
‘Hapo ndio…yeye akanisimulia kila kitu..na ushahidi ninao hapa,
kanda ya video, niliyorekodi, yeye akiongea, akiwa taabani, akikaribia kukata
roho..kama mnataka kusikiliza ushahidi huo, huu hapa…’akasema akitoa kanda ya
videoa
‘Sasa …, mimi sijui
zaidi ya hicho nilichokisikia kutoka kwa huyo mtaalamu mwenyewe, na wengi wa
wahanga …wametumiwa tu, kupitia kwenye visasi vyao,…’akasema.
‘Kuna jingine..hili
sikutaka kulisema, lakini..kwa hivi sasa inabidi,…kumbe hata mke niliyemuoa,
alikuwa ni mtu wao,..yaani ilifanyika hivyo, nimuoe, ili ahakikishe mimi sifungui
mdomo, na ninakuja kufariki kimia kimia…’akatulia
‘Hamuelewi haya..yapo
ndugu zanguni, msipende kujiunga kwenye makundi ambayo yanajifanya yana
utajiri, au yanaweza kukufanya wewe uwe tajiri….., kumbe huyo mke ni muathirika
wa HIV…, anajijua na anatumiwa kuambukiza wahanga wanaotakiwa waambukizwe, na
mbaya zaidi, ukishaupata huo ugonjwa, kuna dawa utapewa, za kukumaliz haraka,…na
ukipimwa itaonekana umefariki kwa kupitoa ugonjwa huo, wao sasa hivi wanatumia
ugonjwa huo, na ugonjwa wa kansa, kuwamaliza maadui zao…ukifa ukipimwa
inaonekana ulikufa kwa ugonjwa, unaojulikana unaua…’akatulia kidogo.
‘Haya
nisingeliyefahamu bila kupitia kwa mtaalamu, na niliporejea nyumbani sikumkuta
tena huyo mke, alishaondoka, na alicha ujumbe kuwa nisimtafute, kwani
sitampata, tutaona kuzimu..…kazi aliyopewa ilitakiwa iwe imekamilika, lakini
sijui ni kwa kudra ya mungu, au ni kwa …huruma ya huyo mke, lakini mimi najua
yote ni kwa mapenzii ya mungu, ndiye aliyefanya hilo liwezekane….siku zote nilizoishi
na huyo mke,..huyo mke, alinisihi nitumie kinga…na nashukuru kwa hilo, kwani
nimeshapima, sina maambukizi..
Alitulia kidogo, na
alipoona haulizwi maswali, akaendelea kuongea…
‘Hilo deni na mengine
ni mpango kabambe ya huyo meneja, mtafuteni, kama bado yupo hai, ataambia kila
kitu, na hata hiyo benki hamjui tu, ni moja ya miradi ya hilo kundi…’akageuka
kumuangalia wakili
‘Mimi ….sijui zaidi ya maelezo ya mtaalamu, mtasikia
wenyewe akielezea japo kwa sauti ya shida,…ilitakiwa baada ya kumaliza kazi yao
waliyopanga, hiyo benki iwabambikie marehemu madeni mengi sana, halafi ipambana
na kukusanya pesa kupitoa huko, kupiga minada mali za marehemu, ndio hivyo
wanavyowekeza
‘Sasa ni..nini
watapata…hebu fikiria wameshapiga minada nyumba ngapi, majumba ya watu yenye
thamani kubwa tu…ujanja ujanja wa kupitia kwa watu, waliowasoma wakaona kwa
kupitia kwao inawezekana…’akasema
Hakim alionekana kufuatili
hayo maelezo, kwa uso wa kushanga , ni kama haamini hayo kuwa kweli yapo..na
sasa aliyeuliza swali alikuwa ni wakili ….
‘Ina maana gani hapo,
kiukweli hayo maelezo yako yapo kama mikakati pia ya kuuficha ukweli halisi, ni
kama njama za kuwatetea hao watu Majaliwa, Dalali na kundi lake,,… kwa vile
yaonekana labda una damu damu nao…sasa utuambie ukweli, ni nani kakuambia uje
kuyasema haya, maana hapa ni mahakamani..uwongo wako utakufanya uozee jela.?’ Akaulizwa.
‘Ushahidi nimesema
ninao hapa, na…nilishawaambia watu wenu, wafuatilie hayo…, wachunguze, mbona
ukweli upo bayana….kiukweli mimi siogopi kufa tena, nimeshajitolea muhanga,
najua kama hilo kundi halitakamatwa, basi, maisha yangu yapo hatarini, lakini
bora nife kihivyo kuliko kufa kidhambi, najua wengi hamtaam,ini haya, lakini,
kama watu wenu watafanya kazi vyema, nina imani…….’
Kabla hajamaliza, mara
akaingia mpelelezi , akiwa na bahasha kubwa mkononi, akamsogelea wakili na
akawa anamnong’oneza kitu, wakawa wanateta kwa sauti ndogo…’
Nilimuangalia yule
shahidi aliyekuwa akiongea, ..yaonekana alikuwa na mashaka sana, nikageuka
kumuangalia Dalali…alikuwa kama hayupo, docta alikuwa karibu yake akihakikisha
mambo yanakwenda sawa, ila kiukweli hali ya Dalali, ilionekana ipo mashakani.
‘Samahani muheshimiwa hakimu
ule ushahidi tuliokuwa tukiusubira , umeshafika,..huu ni zaidi ya …tulivyofikiria,
…naomba nitete na mpelelezi wetu…’ akasema, akionyesha ishara ya heshima…na
hakimu akageuka kuongea na wasaidizi wake.
Mimi nikawa
nawasikiliza wawili hawa wakiongea, pale nilipo niliweza kuwasikia vyema, na
walipomaliza kuongea, wakili akanigeukia na kusema;
‘Tumemaliza kazi …’akasema
akiniangalia mimi, na mimi nikabakia kimia, wakati ule nilikuwa najiuliza mama
mjane kaenda wapi, maana hayupo kabisa mle ndani,.nimejaribu kutizima pande
zote hayupo.
Hakimu akawa anasubiria
tu, naona sasa aliona akae kimia, aone ni nini kaleta huyo mpelelezi, maana hii
kesi sasa sio kesi ya madeni tu, imekwenda zaidi ya hapo.
‘Safi kabisa …, ‘wakili
akawa anakubali, akionyesha ushahidi na maelezo ya huyo mpelelezi,…
‘Sasa kazi imekwisha….’akasema
na sasa akasogea mbele na kumuangalia muheshimiwa hakimu, akasema;
‘Muheshimiwa hakimu, tulikugusia kuwa kuna ushahidi mkubwa unakuja
kwa ajili ya kulimaliza hilo kundi haramu,..’akasema
‘Ni kundi haramu lililojifanya
ni wajanja wa kugeuza geuza mambo,….sasa mpelelezi wetu ameshafika, je ni kweli
Majaliwa, Dalali na kundi lao hawahusiki ..au ni njama zao, je ni nini ukweli
wa hayo madeni, tunao ushahidi wote, na …tunataka tuliweke hili wazi, haki
iweze kutendeka kwa kupitia kwako muheshimiwa hakimu.
Hakimu akaangalia saa…halafu
akageuka kuongea na wasaidizi wake
NB: KESI IMEKWISHAJE..
WAZO LA LEO: Usiwe mwepesi wa kuamini kila jambo unaloambiwa, au kusambaza
kila ujumbe unaotumiwa. Au kuwa mwepezi kusambaza taarifa usizokuwa na uhakika
nazo….Kuna watu kazi yao ni kusoma mazingira na watu, kutafuta fursa kwa
kupitia kwenye tabia na hulka za watu, na wanatumia mitandao kufanikisha
malengo yao…Nia kubwa ni kupata washabiki wengi, na wingi wa washabiki, ndio
wingi wa kuingiza kipato kwao. Tuweni makini kwa hilo, tunageuzwa chambo cha
biashara kwa wengine.
Ni mimi:
emu-three
No comments :
Post a Comment