TUYAKUMBUKE MAUTI…
'Inalillah wainaillah Rajiuna,..., kwake tumetoka na kwake ndio
marejeo yetu..' ndizo lugha tunazisikia kila siku, pale tunaposikia kuwa
mwenzatu katangulia mbele ya haki...
Siku za karibuni tu hapa,
nimesikia ustaadhi mmoja kagongwa na gari, kafariki, mcha mungu, kiongozi wa
dini, na alifariki akiwa anatimiza wajibu wake wa kiimani,..na kila siku
taarifa kama hizi hazikosi kusikika masikioni,..siku zilizopita ajali ya
kivuko, wengi wameondoka watoto kwa wakubwa…
Mimi najiuliza tu, je tunapozisikia taarifa hizi au kututokea
kwa jamaa zetu, akilini mwetu tunajiuliza nini, je kuna maswali gani twatakiwa
kujiuliza..au basi siku yake imefika basi,...sijui ni mimi tu, lakini najaribu
kuwaza mbali, licha ya masikitiko kuwa mwenzetu safari yake imeshafika, lakini
pia kuna maswali muhimu kwangu mimi na wewe yabidi tujiulize
‘Sisi ni nani, ni wajanja
sana , au ndio tunapendwa sana na mungu,…ndio maana bado tupo hai….?’
-Kama wanaondoka wanazuoni waliojaa imani ya dini, kama
wanaondoka viongozi wa dini, tuliokuwa tukiwaendea tukiwa na mataizo
watuombee,sisi maamuma, sisi wafuasi tuna nini cha kusema hapo…,
-Kama wanaondoka watoto wadogo, wasio na hata dhambi, je sisi wakubwa
ambao tuna madhambi yenye kunuka, tunasema nini hapo….
-Kama wanaondoka vijana, wenye nguvu zao, damu zinachemka
kabisa, ambao wangeliweza kupigana na huyo mtoa roho,,…je sisi ambao, umrii
umeshakwenda tutasemaje..
-Kama wanaondoka matajiri wenye pesa zao, wenye walinzi wa kila
hali, wenye silaha za hali ya juu, na viona mbali, sembuse mimi na wewe ambaye,
ulinzi wetu ni wa majaliwa ya mungu, tuna nini cha kusema.Hebu fikiria kwanza hapa…,
hawa matajiri si wana walinzi, kwanini hawawatumii hao walinzi wao kupambana na mtoa roho, lakini wapi….siku
ikifika hakuna cha tajiri wala masikini…hakuna mtoto wala mkubwa..sote
tutaondoka kila mmoja kwa wakati wake
Sasa ndio najiuliza, …kwanini hatupendani, kwanini hatumtii yule
aliyetuumba, kwanini tunatakabari, na kujaa kiburi, kwenye hii nyumba ya
kupanga, maana dunia ni nyumba ya kupanga siku yoyote tutaondoka, swali hapa,
je siku yangu ikifika nina nini…nitakwenda na nini huko akhera, au kufa ni kufa
tu
TUYAKUMBUKE MAUTI…
Tujiulize….siku yangu ikifika nimewekeza nini,nina nini kama akiba
yangu ya huko mbeleni, na nini akina ya
huko mbeleni…
Tunaambiwa akiba ya huko mbeleni… ni matendo yetu mema, je hayo
matendo mema sisi tunayo,, wakati kila siku kila mtu kwa nafasi yake anafikiria
jinsi gani ya KUDHULUMU, sasa hivi ni kamari, kukusanya vijisentI vya watu,
walalahoi, viende kwa mtu mmoja tu…, imekuwa ni dili sasa, mpaka hata yule aliyekuwa
hana wazo hilo anatamani kufanya,…sababu ya matangazo yake…
Ukienda huko kwa wafanyabiashara, biashara siku hizi ni
kudanganyana tu, kuwa hiki ni kizuri, kumbe kimeoza..maofisini mabosi kuwadhulumu
watu, nguvu kazi zao, wanapata faida kwa migongo ya wavuja jasho lakini ni nini
wanawalipa hawa watu, je kinaendana na jasho lao, hatujali, si kaja mwenyewe....yaani…kila
mtu kwa nafsi yake anatafuta njia ya ‘kudhulumu tu..’ hata ndio matendo
mema..??
TUYAKUMBUKE MAUTI….
Haya ….najiusia mimi
mwenyewe na kuwausia wenzangu nyie…, tuyakumbuke mauti, tuikumbuke hiyo siku,
siku ambayo, haina jina siku isiyojulikana, ..siku hiyo ikifika, utamuacha
umpendaye, utakiacha ukipendacho, utayaacha maisha yako ya utajiri, uongozi nk…
yaliyokujaza kiburi…cha kusema ‘unanijua mimi nani…’
Ewe mola wetu tunakuomba uwasamehe madhambi yao ndugu,zetu,
na jamaa zetu na marafiki zetu, majirani
zetu, waliotangulia mbele ya haki…
Ewe mola wetu, tunakuomba utupe mwisho mwema.
Aamin….
Ni mimi:
emu-three
No comments :
Post a Comment