Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Showing posts with label Ndani ya diari yangu-mateso ya usafiri. Show all posts
Showing posts with label Ndani ya diari yangu-mateso ya usafiri. Show all posts

Wednesday, April 5, 2017

MPENZI WA FACEBOOK-1



HIKI NI KISA CHA JAMAA YANGU,...anahadithia mambo aliyokutana nayo.., ni mambo haya haya ya Mapenzi ya mitandao,-Kutafuta MPENZI ndani ya FACEBOOK! 

Siku hiyo nilikutana na huyo rafiki yangu, ..nilimuona kabadilika kweli kakonda,..hana raha,…usoni kama hayupo sawa…anatembea na miguuni kavyaa ndala, zimechakaa, sio yule rafiki yangu tena aliyekuwa na gari lake, ..mnadhifu ....(sharobaro au msafi kama wanavyoitaga).

Nikaanza kumsalimia na kumuuliza kulikoni….

‘Mimi sitaki kabisa kujiunga na Facebook,…’akaanza kusema hivyo, na kunifanya nishangae, kwanini kakimbilio huko kwenye mitandao.

‘Kwanini…?’ nikamuuliza

‘Huwezi amini, …nilishachanganyikiwa kabisa, isingelikuwa juhudu za ndugu zangu, sasa hivi labda ningekuwa marehemu…maana nilishaanza kupagawa, …nikawa navua nguo, sasa sijambo, ila naogoap hata kuwa kama zamani, …yaani we acha tu..’akasema.

‘Kwanini…?’ nikamuuliza nikiwa na shauku kubwa.

Unajua mimi nilishakuwa addicted, na face book, ilikuwa simu na mimi, laptop na mimi, na kwenye simu au laptop ni mimi na facebook..na kwenye facebook, …mimi na mpenzi wangu. …’akaanza kusema.

‘Kwahiyo akawaje na huyo mpenzi wako, nakumbuka uliwahi kuniambia una mpenzi na upo mbioni kufunga ndia, sasa imekuwaje, hukunitumia kadi, wewe mbaya wewe...?' nikamwambia .

‘Unajua sikuwahi kumuona ,au kukutana na huyo mpenzi wangu kabla , lakini nilikuwa na uhakika naye, ndio maana siku tuliyokutana nawe nikakuambia nipo mbioni kufunga ndoa naye....'akasema

'Kwani sasa imekuwaje...?' nikamuuliza

'Ni kisa cha aina yake, hakuna anayeweza kuamini hayo yalinikuta..na nawaomba jamani muweni makini sana..hili ni jambo limenikuta mwenyewe na ...ndio maana nasema sitaki tena kuingi ahuko kwenye facebook.....sitaki..sitaki....'akasema

Ina maana alikudanganya..?' nikaamuuliza

'Hapana...alikuwa mkweli tu...na alinipenda sana...lakini we acha tu....'akasema

 'Sasa ilikuwaje mbona unaniacha njia panda, au...alikudanganya, au....?’ nikamuuliza

‘Aheri angelikuwa marehemu, au nimeachana naye ingelikuwa afadhali kwangu…’akasema

‘Sasa tatizo ni nini…?’ nikamuuliza

‘Ni hivi …..’ ndio akaanza kuelezea

*************

‘Mimi nilibahatika kumpata huyo  mpenzi kwenye mtandao wa Facebook,, nikaelewana naye sana, tukawa tunatumiana picha,..yaani haipiti siku bila kuchat naye,..ikawa sio siku tena, haipiti masaa,….mpaka sekunde , hutaamini, sikutamani binti mwingine yoyote zaidi ya huyo,….tuliivana sana, tena sana…

‘Unajua ilifikia muda nalala na simu kitandani, kwani huwa mara nyingi sana tunachat usiku kuliko mchana, kwasababu ya mishughuliko ya kimaisha,, na usiku huwa tunaweka live..ile ya kuchat na video, mnaonana kupitia kwenye video,..na hapo ninachati mpaka nashikiwa na usingizi na ndani ya usingizi naota tupo naye…..

Yaani ilikuwa ni ajabu, kipindi hicho kwangu niliona ni kawaida tu..ni ndoto tu, lakini baadae ndio nilikuja kuona ni kwanini ilikuwa hivyo..

Ikafika muda nikaona ni lazima nimuoe,..tuonane naye uso kwa uso..yeye alisema siwezi kumuoa uso kwa uso mpaka tujuane vyema, kwa kipindi hicho nikaona tumeshajuana kimtandao, sasa tujuane kiukweli,…ikawa ni namna ya kutembeleana, mimi nipajue kwao na yeye ikiwezekana aje kwangu..mimi naishi mwenyewe,

Basi kila nikichat naye nikawa namsihi kuwa nataka nifike nyumbani kwao, nikajitambulishe..

‘Hakuna shida honey…utafika tu, usiwe na haraka..mambo manzuri hayataki haraka…’akasema maana tulishapeana kila jina nzuri la mapenzi, ilibakia tu hiyo ya kuitwa mke wangu au mume wangu…

‘Basi tufanye wikiendi mimi nije kwenu, nitakuja mapema ili tupate muda mnzuri wa kuongea mimi na wazazi wako, baadae tutoke kidogo tuende sehemu mimi na wewe tu…’nikasema

I cant wait….’akasema nikajua amekubali.

‘Nakupenda sana mpenzi wangu…’nikasema

‘Yaani mimi sijui nisemeje, nakupenda sana, my sweetie….’akasema.

Nikiwa nimetarajia kuwa wikiend ndio naenda kwao, usiku wake sasa akaja na kipingamizi kuwa wazazi wake bado hawapo tayari nib ado mapema sana mimi nikaamwambia;

‘Mimi siwezi kulala, siwezi kusubiria tena,  bila ya kuja kuonana na wewe..’nikamwambia

Are you sure unataka kuniona….?’ Akaniuliza swali hilo, nikashtuka kidogo, nikamwambia ;

More than sure, unajuaga jinsi gani ninavyokupendaga…’nikamwambia.

‘But, nakuona haupo tayari yet, unahitajika sana …sipendi wewe ujiingize mapema hivi, nakuona bado bado wewe kama ilivyo mimi bado ni wadogo …’niliposikia hivyo nikamkatiza kwa kusema;

‘Sikuelewi ukisema hivyo ina maana hutaki tuonane, ..nilijua unanipenda sana…na umri wako mbona sawa na kwangu tumepishana kidogo tu …na leo mbona unasema hivyo, tulishakubaliana ati..na, unaongea kama vile wewe ni mkubwa sana…’nikamwambia

‘Hahaha sio hivyo mpenzi…unajua nakuonea huruma, maana ujue ukijiingiza huko mimi nitakuwa nakutegemea wewe, je umeshajiweka sawa, …unajua mimi nakupenda sana, ndio maana sitaki kukuharakishia kihivyo , nataka uwe tayari kwa maisha hayo mengine, si unajua ndoa sio lele mama, na hasa ndoa yangu mimi na wewe …’akasema

‘Hapana mimi nipo tayari, siwezi kukurupuka tu, nimeshajiandaa kwa kila kitu, nina nyumba, nina…wewe utakuja kujionea mwenyewe…’nikamwambia.

‘Najua …una maisha mazuri..lakini maisha mazuru tu hayatoshi, …ndoa, na maisha hayo ya ndoa ni kitu kingine kabisa. Unatakiwa ujiandae, usahau maisha mengine…mimi nakuomba usiharakishe kihivyo…unanielewa…’akasema, sikutaka kubishana na yeye maana nilimpenda na sikutaka kumuuzi.

Basi siku zikaenda baadae tena nikaamua sasa iwe na iwe, ni lazima nikajitambulishe kwa msichana nilitaka anielekeze kwao tu, mimi nitaenda vyovyote iwavyo, basi siku hiyo naye hakutaka kuniudhi akasema;

‘Ok, kama umeamua,na upo tayari sina budi nikuelekeze nyumbani kwangu…’akasema.

‘Sawa..nyumbani kwenu na wazazi wako au sio…kwani ni ndani ndani sana….ulisema kwenu kila mtu anapafahamu a sio…?’ nikamuuliza

‘Ndio lakini ni ndani ndani sana…’akasema

‘Gari haliwezi kuiingia..?’ nikamuuliza

‘Haliwezi…’akasema.

‘Basi mimi  nitachukua pikipiki ili nifike kwa haraka..’nikamwambia

‘Mhh…hapana  wewe chukua dala dala,…sitaki ujiharakishie, kihivyo…wewe chukua usafiri usio wa haraka, ukifika maeneo fulani nitakayokuelekeza vizuri zaidi…, na hapo utafuta maelekezo yangu..hadi utafika nyumbani kwangu…’akasema.

‘Kwako na wazazi wako au sio…?’ nikamuuliza.

‘Usijali utafika tu…nyumbani kwangu…’akasema hivyo, na hiyo ‘kwangu..’ akawa anaitaja sana kuliko awali, awali aliniambia yeye anaishi na wazazi wake, sasa hiyo kwangu ikawa, anyway ..kwa muda huo sikuona ni kitu kisicho cha kawaida.

Basi siku hiyo nikajiandaa kwelikweli…si unajua ukiwa na mpenzi, inavyokuwa na iwe ndio siku ya kwanza ya kutaka kukutana naye, halafu ndio unakwenda kutambulishwa kwa wazazi…unajikagua mara kumi kidogo, …sikuwa na shaka na utanashati wangu, hilo kwangu ni tabia….

Basi  muda ukafika,..nikafanya kama alivyotaka, daladala, japokuwa ni gari langu, hadi nikafika maeneo aliyonielekeza na hapo nikatembea hadi huo mtaa alioniekeza, hapo nikasubiria maelekezo yake na mara, ikaja ujumbe wa maandishi naelekezwa nipitia wapi na wapi..

Mimi ni mkali wa ramani ukinielekeza mara moja siwezi kupotea tena,..basi sikuwa na shaka ..nikaanza kufuatili ile ramani..nikatemba mtaa wa kwanza nikaingia uchochoro, nikatembea bara baraba, kwenye duka kubwa…halafu mti mkubwa wa mbuyu….huyooo, tembea tembea, halafu..unatokea nyumbani kwake.

Naangalia mbele sioni nyumba, …nikageuka kushoto na kulia sioni nyumba kama hiyo, nikaitizama ramani …sijakosea, naangalia hapo nilipoambiwa nitakuta nyumba, sioni zaidi ya  MAKAUBURI….

‘Ohh, huyu honey, kakosea nini..nikajaribu kumpigia simu kwa namba ile ile, lakini sasa simu haipatikani, sio kawaida yake, haijawahi kutokea,…nikarejea ramani, naona sijakosea, na siwezi kukosea mimi, najua vyema ramani…nikasubiria, nikapiga simu , haipatikani…baadaye nimejichokea nikaamua nirudi nyumbani tu…

Nilichoka, maana sio karibu kwa kutembea, niligundua hilo wakati narudi maana wakati nakwenda sikuliona hilo, nilipaona ni karibu tu. 

Nilipofika nyumbani kwangu nikajirusha kitandani, huku nikihangaika kuitafuta ile namba yake,...namba siioni, sio kawaida...nikawa nahangaika wewe...na mara  usingizi mnzito ukanijia,…

**********
2

‘Mpenzi mbona hukufika nyumbani…?’ anaulizwa
‘Nilifuata ramani kama ulivyonielekeza lakini sikuiona nyumba yenu…’nikasema
‘Siwezi kuamini, mbona nyumba yetu ipo wazi kabisa….…’akasema
‘Sikuiona hiyo nyumba honey..nilichoona mbele yangu ni makaburi….’nikasema
‘Hahaha…’akacheka sana, halafu akasema;
‘Sasa ..kwanini hukusogea mbele hadi sehemu niliyokuelekezea..?’ akaliza
‘Ilikuwa makaburini, ningepitaje..huko mbele, unaelewa ninachokuambia, mbele yangu hakukuwa na nyumba kulikuwa na makaburini…..’ nikamwambia
‘Ina maana hunipendi au..?’ akauliza

NB…Niendelee???Ni kisa kifupi tu, subiria sehemu ya pili uone vituko vya dunia, ..kuweni makini jamani ....


WAZO LA LEO: Tuweni makini sana tunapotaka urafiki, na hasa ikiwa rafiki huyo hujawahi kukutana naye kuna zamani iliitwa urafiki wa kalamu, sasa hivi urafiki wa mitandao..ni sawa kwa wenzetu, wao wapo mbali na aina hii ya urafiki, maana kwao kila kitu kipo wazi, kumbukumbu za watu picha zao, anuani, nyumba , mitaa..sisi je..hayo yapo, je ukweli wa taarifa upo…bado tupo nyuma kwa hilo..kwahiyo ni nyema, tukawa makini sana tunapotaka kuchagu rafiki kwa njia hii.
Ni mimi: emu-three

Friday, February 24, 2017

HAKI YA MJA HAIPOTEI BURE-2


‘Mama mimi nimechelewa kikaoni…’nikasema sasa nikianza kufunga funga vitu vyangu ili niweze kuondoka. Lakini yule mama ni kama hakunisikia,..na pale ofisi kulishajaa harufu ya jasho lake,…nikasogea kwenye kipozoe na kukiwasha, sikuwa na nia mbaya ya kumzarau..lakini ofisi ni ofisi, huyo mama alipoona hivyo akasema;

‘Najua unakerwa na jasho langu, jasho hilo lina thamani kubwa mbele ya mungu na ni ushahidi kwako, ili ujue ninavyoteseka, uone kuwa nimetembea maili nyingi hadi kufika hapa sina nauli nitafanyaje..….'akasikitika kwa kutikisa kichwa

'Lakini hayo hayana maana kwako, maana utafikiria nimekuja kukuomba, hapana ninachotaka ni haki yangu, haki ya mtoto wangu, na najua imeshachelewa kama ulivyosema, lakini hata kama imechelewa, nataka wewe usikie hii kauli yangu kwako…..

Muda huo mimi nimeshakasirika,....sikutaka hata kumsikiliza nilitaka atoke, ili nione nitafanya nini, maana nilishachelewa hata hicho kikao,...nitafute namna ya kumdanganya bosi wangu kama atanielewa....namfahamu sana huyo bosi mkuu, kwake muda ni kitu muhimu sana,hapotezi hata sekunde moja, ukichelewa dakika moja tu, keshafunga kikao, kitakachofuata hapo ni barua…

‘Nisikilize kwa makini, najua sana kuwa sisi watu wa chini hatuna maana kwenu, tunanuka mijasho na tutasema nini, ndio maana hatutakiwi kuja kwenye ofisi zenu, sawa nashukuru..., lakini hata hivyo tuna sehemu ya kimbilio letu, ..huyu hawezi kamwe kututupa, na kauli yangu na ujumbe wangu ni kituma kwake yeye, asiyeangalia mwili au mijasho yetu,... mola ..kwa mola wangu..….’ Akanikazia macho na huku anainua mikono juu.

Wakati huo nilishasimama mlango kumuashiria atoke, nifunge mlango, yeye akawa kasimama pale pale, na kuendelea kuongea;-

`Kauli yangu ni hii….

‘Kama kweli barua hiyo haikuwahi kufika kwako…, wewe ni mzazi kama mimi wewe ni mama kama mimi, unazaa kama mimi, mungu anaona,…hakuna anayefahamu uchungu wa mtoto zaidi ya mzazi, hasa mama….’akaweka mikono hivi kama atafanyaje.

‘Nasema hivi , kama kweli haijafika kwako, basi nisamehe,..lakini kama kweli ilifika kwako ukafanya uzembe, ukadharau, maana unaona huyo ni kilema tu, anafaa nini,..mungu anakuona…mimi sasa naondoka,..samahani sana kwa kukupotezea muda wako…’

Hayo ndio maneno aliyatamka huyo mama kabla hajaondoka, halafu alipomaliza taratibu akaanza kuondoka, kwanza, nilibaki nimeduwaa, nikakumbuka kikao, nikakurupuka lakini kabla sijafungua mlango mara katibu muhutasi wangu ananijia kwa kasi akisema;

‘Samahani bosi mimi sikumuona huyo mama akiingia….alipitia wapi, ooh, nilikuwa nimekwenda maliwatoni, samahani bosi…’akasema na mimi sikumjibu kitu..ila aliposema…..

‘Na…bosi mkuu amepiga simu anasema anakuja…’aliposema hivyo, mwili mzima ukanywea, maana hicho kikao kilikuwa kinakwenda kufanyikia ofisi kwake, sasa nimechelewa,…lishapita nusu saa sijafika huko, ..niliangalia simu yangu, nikakuta missing call tano, simu nilikuwa nimezima kutoa sauti...nikajua sasa kimenuka, ajira haipo tena!

Nikataka nitoke tu, nimuwahi huyo bosi kabla hajafika,....na kabla sijafunga mlango, mara mlango wan je ukafunguliwa, na aliyeingia alikuwa bosi mkuu… kakunja uso utafikiri sio yeye..alikuja moja kwa moja kwangu pale nilipokuwa nimesimama..

‘Kwanini hujafika kwenye kikao…?’ akaniuliza, na kabla sijamjibu vyema, akasukuma mlango wangu, ukafunguka, akawahi kuingia ofisini kwangu, na hakukaa, akanibwagia barua mezani, nilijua ni barua ya nini….nikashika kichwa,…

Huyo bosi hakusema zaidi, akatoka, na hakuaga, akatoka nje, kuondoka zake,…sikuisoma ile barua kwanza,…akili yangu ilinituma kuhakikisha jambo fulani kwanza, kwahiyo nikaliendea trei langu la barua zinazotoka, na kuingia nikawa nakagua sehemu ninapoweka barua za kuja kwangu,…haikuwa mbali,  nikaiona ile barua.

‘Oh..’nikaguna, hapo ndio nikaikumbuka tatizo la huyo mama na barua iliyotumwa kwangu, kumbe ndio huyo mama…

‘Kiukweli…, ile barua niliwahi kuisoma, kukawa na ucheleweshaji fulani, katika kufuatilia kumbukumbu zake, hazikuwa zimekamilika na ilifika ikiwa imechelewa mezani kwangu,…na mimi nilitingwa na kazi nyingine…, mpaka muda ukapita, nilipoiona tena, muda ulishapita,..hatungeliweza kufanya lolote,… kwahiyo tukaacha kama ilivyo,….leo hii huyu mama amekuja na maneno kama hayo..Ilinipa wakati mgumu sana, lakini sikuwa na la kufanya!

Nikageukia mezani, barua aliyoleta bosi ipo mezani, huenda ndio ya kufukuzwa kazi,..sasa nikaanza kukumbuka mbali…

‘Unajua kwanza niliwazia watoto wangu,..ile kauli ya huyo mama ililenga haswaa…mimi kama mama ilinigusa pale pale,..mama ukitaka kumpata gusia watoto wake,..laana ya huyo mama imeshaanza kufanya kazi, kwanza nimeshafukuzwa kazi, ya pili sijui itakuwaje…mimi nina imani sana ya dini,..lakini hapo nilitikisika kiimani… nilijikuta nikalia,..nilifikiria, sina nitawakleaje hao watoto,..

Nikasogea mezani na kuchukua ile barua, taratibu nikaitoa kwenye bahasha, na maandishi ya kwanza niliyoona, ni….’ninasikitika…’ kichwa kikaanza kuuma, nikawa sioni maandishi..mara giza…nilichokumbuka ni kauli …

‘NISAMEHE MAMA, sikufanya makusudi…’, nikazama kwenye giza! Nilipoteza fahamu,………..

NB: Kwa wale wanaotaka kujua ni nini duwa ya mja inafanya kazi soma kisa hiki, tuonane sehemu nyingine mungu akipenda.


WAZO LA LEO: Usimdharau mja wa mola..hata kama kakosea, hata kama wewe ni mubwa namna gani, kipato chako cheo chako, hakina thamani mbele ya muumba, ambaye anajua ni kwanini kamuumba mja wake hivyo..
Ni mimi: emu-three

Wednesday, January 18, 2017

Sikuomba iwe hivyo



 Ni siku ya naikumbuka sana, ni siku ambayo niliteguka nyonga, si unajua tena hii shida yetu ya usafiri, na ilitokea usiku wakati narudi kazini. Usiku sikulala, nilitamani kupambazuke haraka niwahi hospitali. Lakini tatizo la ofisi yetu ili utibiwe ni mpaka upate sick sheet, na ni lazima ufike kwanza ofisini uandike kuwa umefika, usipofanya hivyo siku hiyo inakatwa, na unakatwa kwenye mshahara.

Basi kulipopambuka tu, saa kumi nikadamka, hata kutembea shida, nanyata kama kinyonga, taratibu nikawahi kituo cha reli, maana nilijua nikipanda dala dala nitaumia zaidi, japokuwa mbeleni nitahitajika kupanda hiyo daladala, uwezo wa taxi au bajaji upo wapi!

Uzuri wa treni hainaga foleni nikafika Buguruni saa kumi na mbili, kuna mwendo wa kutembea kutoka Tazara hadi buguruni sokoni , nilijikongoja hivyo hivyo, hadi nikafika kituoni,..Nilipofika hapo kituoni, niligwaya kwani umati wa watu waliokuwepo hapo…, utafikiri magari yamegoma. Nami natakiwa kwenda ofisi moja ipo kwenye jengo moja lipo njia panda ya kwenda Kawe.

Magari ya Kawe buguruni au Kawe masaki ni kama enzi zile za magari ya kwenda mbagala, ni magari ya kugombea, watu wanarukia kwenye madirisha, ukizubaa huwezi kupanda. Na mimi siwezi hata kusimama kwa muda mrefu.

‘Jamaa yangu nakuomba unisaidie naumwa,…ugombee upate siti ili unipatie nikae…?’ nikamwambia jamaa mmoja aliyekuwa akielekea njia hiyo.

‘Mimi mwenyewe sijui kama nitapata gari, hapa nilipo najisikia vibaya…’jamaa akaniambia hivyo.
Kukuru kakara ikaja gari, ikasimama pale pale nilipokuwa nimekaa, haraka nikajitahidi nikadondokea mlangoni, watu hawakujali, wakaniparamia na kuanza kunikanyaga, hakuna aliyejali, hata nilipoweza kusimama, nilikuwa nimechafuliwa nguo. Sikujali, nikasimama na kuingia ndani ya gari.

Uzuri kondakita alikuwa kakaa kwenye kiti karibu na mlangoni, akanipisha nami nikaweza kukaka kwenye kiti! Hapo nilikuwa na maumivu makali sana, ..nijiuma meno….gari likaanza kuondoka, kwa mbele ulikuwa ni mnyororo, foleni, gari halitembei. Mpaka tunafika Karume njia panda, dakika arubaini na tano zimepita,..hapo natamani hata kulia,ni maumivu makali sana!

Nikamuomba mungu, angalau nipate usingizi, na duwa zangu zikakubaliwa, nilipitiwa na kausingizi na nilipoamuka nikakuta tupo njia panda ya magomeni, kumbe tulitumia saa moja kwenye hiyo foleni, ..hadi tunafika Moroco, ni masaa mawili na nusu yamepita. Sasa kutoka hapo Moroco kuelekea huko Kawe, hapo ilikuwa kazi, mpaka abiria wanadondoka na kuzimia, trafiki hana habari na upande wetu.

Tukaondoka hapo saa jingine limepita,..tukafika sehemu wanaita kwa Warioba, hapo kuna historia, bila nusu saa au saa nzima hamuwezi kuruhusiwa kupita,..hapo abiria wengine waliamua kushuka na kutembea kwa miguu, na wale wenye uwezo wakachukua pikipiki. Sijui kuna nini sehemu hiyo!

Nilifika ofisini saa tatu na nusu, na daftari la mahudhuria limeshachukuliwa, sikujali, mimi umuhimu ni sick sheet tu..Bosi aliposikia ninaumwa, akanijia na kuanza kunibwatukia;

‘Wewe kila siku inaumwa,..veye hutaki kazi,..sasa nenda tibiwa na baki huko huko mpaka ponaeeh, ..’akasema bosi huyo.

‘Sawa bosi lakini sikuomba iwe hivi…’nikalamika.

‘Itajua mwenyewe….’akasema kwa dharau. Na kauli yake ni moja,..ningefanya nini,..nikaondoka hapo ofisini nikiwa na mawazo mengi, nitaishije. Basi nikajikongoja hadi kwenye kituo cha dala dala..nilichokikumbuka ni kuwa nilikuwa nasimama, kwani nilikaa kwenye gogo lilikuwa limewekwa hapo kituoni.

Wakati nasimama, nikahisi maumivu makali sana,…lakini nikajitahidi hivyo hivyo….nikainua mguu , hautaki, nikajitahidi, nikaweza, nikavuta hadi mlango mwa gari, unajua tena magari ya dala dala hayana kuremba,..sijainua mguu likaanza kuondoka, nilihisi nikirushwa na kudondoka chini, na kichwa kilikoswa koswa na gurudumu, na giza likatanda usoni.


Nilizindukana na kujikuta nipo hospitalini na bandeji kichwani…

Ni mimi: emu-three

Tuesday, December 6, 2016

TOBA YA KWELI-20(hitimisho-1)




 Kitendo cha docta kusita kunipa majibu yenye uhakika kilinifanya nihisi kuwa huenda kagundua kuwa mimi mimi bado nina matatizo, lakini imani niliyokuwa nayo ilinifanya niamini kuwa mimi nimepona…niliamini toba yangu, niliamini maneno ya yule kiongozi wa imani

‘Ehee sasa ikawaje…?’ nikamuuliza

‘Sasa ikawaje..subiria uone majibu yake sasa…’akatulia akiwa anaangalia mbele…

 ‘Unajua kabla sijahitimisha kisa hiki, nikuambie ukweli, mimi nimekuwa ni shuhuda kwa vitendo,..unajua mimi nilishajulikana kuwa siwezi kuzaa …tasa,…tasa,  na hata kamaa ningeweza kuzaa kwa vipi, maana nilishaandamwa  na maradhi mabaya yanayovunja nguvu za kiume, nilipatwa na gonjwa la kisukari, ugonjwa wa moyo…vidonda vya tumbo…ooh,


Sasa mtu kama miye ambaye nilishajulikana hata hospitali kuwa siwezi kazi, ..unajua kisukari kinavyotesa..hutakiwi ule vyakula vizuri vizuri..haya presha,..haya hata nguvu za kiumwa huisha kabisa…hebu katika hali kama hiyo ni nani atakubali umuoe binti yake,…hebu fikiria hapo hata ingelikuwa ni wewe, na hata huyo binti anakupenda vipi kweli atakubali umuoe tu, kwa lipi nililokuwa nalo tena…ili aje tu kuniangalia, sina mali, sina…nilishakwisha….’akatulia

‘Kwahiyo…?’ nikauliza

‘Ndio nakuuliza wewe….ili uone nguvu ya toba ilivyo…..’akasema

‘Sasa nikurejeshe nyuma kidogo,….’akaangalia saa yake halafu akaendelea kusimulia;

‘Ukumbuke docta alishachukua vipimo vyangu,…ipo siku tulikwenda na docta akachukua vipimo vyangu, lakini hakuweza kunipa majibu siku hiyo, ilihitajia muda wa kuvifanyia kazi…na ikawa kila nikimpigia simu anasema nisubirie..nikajua hakuna jipya.

 Na ndio yakaanza kutokea haya ya huyu binti, kuumwa, na hata kwenda kwao..nielewe hapo kidogo, kuwa haili ilivyo, hata docta asingeliweza kunitetea…’akatulia.

*************
Sasa huyu binti alipofika kwao ilikuwaje…!
Huyo binti alipofika kwao, akapokelewa kwa vigelegele..hata mwenyewe alishangaa, kumbe alishaandaliwa kama mtarajiwa wa kuolewa,

Kumbe wazee, akina….baba mama, mashangazi walishapitisha kuwa huyu binti anaolewa na nani,….kumbe watu walishaleta hadi mahari, uone ilivyo kuwa ngumu..ngombe nyingi tu, zilishapokelewa, na muoaji keshapitishwa ni nani..

Sasa ndio binti anafika nyumbani akiwa kebeba taarifa yangu, na taarifa yenyewe ya mikono mitupu,.. eti mie namtaka kumuoa binti yao, unajua hata binti mwenyewe awali, aliogoapa kabisa kuliongelea hilo…Ataanzaje..

Alipoanza kuelezewa kuhusu hizo posa na sifa za muaoji,…akataka kujitetea,  akasema yeye kwa hivi sasa hataki kuolewa..na hilo swala limekuwa kwake la kushitukiziwa, anahitajia muda wa kuliwazia, hata huyo bwana mwenyewe hajawahi kuongea naye….

‘Kwanini, ina maana hutuamini sisi wazazi wako….?’akauliza na hakusema moja kwa moja, kunihusu mimi,  

‘Au labda umeshapata mwanaume mwingine, maana nyie mabinti wa siku hizi, mnajiamulia tu,…na badala ya hata mwanaume kuja kujitambulisha nyie ndio mnajitambulisha wenyewe kuwa mna wachumba…’akasema mjomba.

‘Hawezi kutuangisha binti yetu, mimi ni imani hawezi kutukataliwa chaguo letu,….’akasema shangazi.

‘Haya mnataka apewe muda gani, eti binti tukupe muda gani kuamua…?’ akaulizwa.

‘Naombeni hata mwezi….’akasema.

‘Haiwezekani, tunataka kauli yako hii leo,..labda unaona aibu kutuambia hapa,haya nenda ukaonge na shangazi yako faraghani na mama yako …’akaambiwa

Kweli ikabidi watoke na shaangazi, na mama kwenda kuongea faragha, na huko binti akaanza kuonywa, na kwa maneno makali ,..kuwa asije kuikataa hiyo ndoa, maana ina umhyimu mkubwa.

Binti akaona autumie mwanya huo kujieleza.

‘Eti nini unasema nini,  wewe binti mbona una hatari, unataka kutuletea mtihani gani huo,..huyo mtu hatakiwi, na unakumbuka, alikuwa haelewani hata na mkewe, mpaka anafariki, sasa unakuja na hoja, hiyo,..sisi hilo hatuwezi kabisa kuliongelea….’wakasema lakini binti aliposisitiza, ikabidi akina mama hao kuja kutoa taarifa kwenye kikao.

Wazee waliposikia hilo, walipandisha zile mori za kiasili,….baadaye mjomba akatuliza kikao na kusema;

‘Tulijua tu…wewe umekaa na huyo muhuni huko mjini, kakughilibu akili yako...na nyie watu hivi kwanini mlimruhusu huyu binti  mwenye maadili yetu aende kuishi na huyo muhini huko mjini, mnaona madhara yake haya…’akasema mjomba

‘Au ni kwa vile nilisikia kuwa huyo mwanaume anaumwa, hawezi kazi…au…?’akauliza mjomba kwa hasira na baba akawa kainamisha kichwa chini tu kwa aibu…huku akitamani kumrarua binti yake mbele ya kikao.

‘Hivi nyie watu kwanini mkamruhusu….’wakaulizwa tena wazazi.

‘Lakini kaka, hebu kwanza tumsikilize mwanetu, unajua yeye ndiye anatarajia kuishi na mumewe..hatujui ni kwanini akafikia uamuzi huo…lazima ana sababu za msingi , mnamfahamu vyema huyu  binti yetu, hawezi kutuabisha…’akasema mama

‘Haya atuambie tumsikie..au labda keshapachika mimba ..tuambie sasa…’akasema baba sasa.

‘Atapachikwaje mimba, wakati tunasikia huyo mwanaume, jogoo haliwiki, au ilikuwa uwongo,e…hapo tena labda mumsingizie….’akasema shangazi kwa mdhaha.

‘Sasa huyu binti ana sababu gani, atuambie la sivyo, asubirie maamuzi yetu, msimbembeleze huyu, hawa mabinti mkiwaachia mwisho wa siku aibu ni zetu..haya tuambie…’akasema mjomba

Binti alikaa kimia, hakujua hata aanzie wapi, na baba akasema;

‘Mimi naona tuchukua uamuzi wetu,  maana huyu binti anataka kutuabisha, hapa kijijini wamekuwa wakituongelea vibaya, wanatudharau,yote haya ni sababu ya mama yake, eti anamuheshimu marehemu, marehemu hayupo, …’sasa akajitetea baba.

‘Usimlaumu mkeo, kama ni makosa haya ni yenu wote….’akasema mjomba.

‘Sasa sikiliza wewe binti…, sisi kwa pamoja, tumeamua utaolewa na huyo mtu wetu tuliyemuona anakufaa, nay eye anatoka kwenye familia tunayoifahamu sisi…’akasema baba, hapo binti akaamua kufungua mdomo, na kusema;

‘Baba,..na wazazi wangu kwa ujumla… naombeni sana, mnisikilize na mimi… wazazi wangu mimi sitaki kuwakatalia mawazo yenu na maamuzi yenu, nawajali sana wazazi wangu, lakini hebu rejeeni nyuma, mkumbuke mema mangapi aliyowahi kuwafanyia marehemu..mumeshasahau hayo jamani….ni nani aliwasaidia hata kufikia kuwajengea hiki kibanda, mumeshamsahau kwa vile hayupo duniani…’akasema binti

‘Hayo yana maana gani kwetu, yanahusiana nini na maamuzi yetu…?’ akauliza shangazi.

‘Ndio…yana maana kubwa sana…, ili mfahamu ni kwanini nikakubali huyo mwanaume anioe….’akasema binti.

‘Hakuna kitu kama hicho,..usituletee uhuni hapa,….haya elezea, inahusianaje na hili….?’ Akauliza mjomba.

‘Marehemu hatuna ubaya naye, sisi ubaya wetu ni kwa huyo mume wake, mume ambaye alimtenda sana mke wake, kila mtu anazifahamu sifa zake, japokuwa mkewe hakutaka kumtangaza ubaya wake....’akasema shangazi.

‘Na hata yeye mwenyewe unamafahamu sana,  umeshasahau alichotaka kukufanyia kipindi kile,..ukaapa kuwa hutarudi tena kwake..unakumbuka,..huyo kawafanyia mangapi mabinti wa wenzake..ni mume gani huyo, unataka kutuletea mbegu mbaya kwenye kizazi chetu…wewe hujui tu..tabia nyingine mbaya hurithiwa…’akasema baba.

‘Baba huyo mnaye mzungumzia nyie alikuwa mwingine, huyu wa sasa ni tofauti baba, huyu wa sasa ni mcha mungu wa kweli, kabadilika kabisa…, alichokifanya sio rahisi mtu wa kawaida kukifanya, …niulizeni mimi niliyeishi naye hapo nyumbani..wazazi wangu nilichotaka kuwaambia ni kuwa, marehemu ndiye yeye mwenyewe aliacha usia kuwa mimi nije kuolewe na huyu mtu…’hatimaye binti akapasua ukweli.

‘Eti nini…marehemu aliwahi kukuambia hivyo….hapana kama ni watu wamekuambia hivyo, wao wamekudanganya, yule mtoto haweze kumchuuza mwenzake, mfupa ulimshinda yeye kwanini amtupie mwenzake, hana tabia hiyo, usimsingizie …’akasema mama.

‘ Ni kweli mama, ..hakuwahi kuniambia mimi moja kwa moja..lakini aliacha usia huo kwa watu , na hao watu ni watu kuaminika, na wao ndio walionishawishi mimi, sasa je mnataka nimkane marehemu…., nikiuke usia wake, mtu tuliyemuona kama ndugu yetu, nilimpenda sana, na niliahsi kumfanyia chochote….’akasema binti kwa sauti ya kusikitika.

‘Oh…unaona ulivyoghilibiwa, yeye mwenyewe mfupa ulimshinda, au sio… sasa anataka na wewe ukautafune , wewe una meno gani, kwanza hebu tuulize sisi wazazi wako kwanini hatutaki wewe uolewe naye,…tuulize, tunasababu za msingi…’akasema mjomba akiwaangalia baba na mama.

‘Je una hakika gani kuwa marehemu alitoa kauli hiyo, kuwa yeye akifariki uje kuolewa na mumewe,,..?’ akauliza baba akionyesha kushitushwa sana na kauli hiyo, na ilionekana imemgusa.

‘Ndio baba…ushahidi na mashahidi wapo…mimi sikukubali tu …..’akasema binti

‘Lakini sasa utaolewaje na mtu mgonjwa, si unafahamu matatizo yeka, au unataka kwenda kuwa mfanyakazi wake tu..hutaki kizazi…au ndio mumeshapimana huko maana nyie vijana wa siku hizi ni hatari, mnajiingiza kwenye mambo makubwa kabla ya umri wenu…?’ akaulizwa shangazi.

‘Ngojeni kwanza…, unasema una ushahidi na mashahidi…eeh, hebu tumuache atupe huo ushahidi na mashahidi,… lakini hayo,  hayawezi kubadili msimamo wetu maana tulishakubali, unatuelewa, haya elezea huo upuuzi wako….’akasema baba.

NB: Naona hitimisho litakuwa na sehemu mbili, tuwe na subira, tuone sehemu ya pili itakuwaje, je binti atakubaliwa , …ukumbuke wazazi wameshapokea mahari….


WAZO LA LEO:  Wakati mwingine ni muhimu kuwasikiliza watoto wetu, hasa inapofikia sehemu ya kuchagua ni nani anayefaa kuwa mwenza wa maisha. Yawezekana, ikawa ni  heri kwa wawili hao, yawezekana mwenza aliyemuona yeye akawa ni mwenza mwema, lakini ni muhimu, wazee kufanya uchunguzi wa kina, tusikimbilie kuangalia mali, mahari, na utajiri tu wa mwenza wa watoto wetu, tuangalie yake  mambo ya msingi, maana, ndoa ndio chimbuko la kizazi chema, ndoa ni sababu ya jamii njema , tukiharibu hapo, tumeiharibu jamii.
Ni mimi: emu-three

Tuesday, May 26, 2015

NANI KAMA MAMA-82



‘Mwanangu safari yangu ya kwenda kutibiwa India ilinijia kwenye ndoto,  siku ile nilipokuwa nimezirai sijitambui, na kila hatua ilijionyesha wazi ndani ya ndoto, na kama ningekuwa najua kuwa ni kweli ningeliwaambia kuwa msiwe na wasiwasi, lakini sikuwa na uhakika nini tafsiri ya ile ndoto, kwani nilikuwa nusu mfu.

‘Mama hata siamini...nisamehe mama nilikusahau kabisa....’nikasema huku tukiwa tumekaa ndani na muda huo yule docta aliaga akasema anaondoka kuwajibika ila atarudi tena kuona kama kila kitu kipo shwari…

‘Najua mna hamu sana ya kuongea mengi , kwa ratiba yangu mimi hapa tumemalizana mimi nahitajika kazini, kwahiyo sijui mama unasemaje…najua dereva wako atajua jinsi gani ya kukurudisha nyumbani kwako... au bado unanihitajia, maana uliniogopesha...?’ akauliza docta

‘Mhh, ilimradi nimemuona mwanangu , sina shaka tena...dereva wangu atajua jinsi gani ya kunirudisha nyumbani kiliniki kwangu..’akasema mama

‘Kilini kwako, ina maana mama bado unatibiwa...?’ nikauliza kwa mshangao

‘Mama yako kaniambia ana kliniki yake ya kuwahudumia wagonjwa wanaosumbuliwa na maumivi ya kichwa, kuumwa na kichwa kusikosikia dawa, unakunywa dawa kinatulia, bado kinarudia tena..au kuna watu wanasema wana changanyikiwa kama mashetani, mama yako kwa mkono wake anaombea kinapona...kiufupi mama yako ana utaalmu fulani anaufahamu yeye mwenyewe..'akasema docta

Nikaguka kumuangalia mama na jinsi alivyovaa, nikajaribu kukumbuka vile alivyokuwa akijifunika, ..japokuwa kiukweli alifunika kichwa, ila sasa hivi hajajifunika usoni, na docta akazidi kuongea;

'Na nimefurahi sana, maana mama yako kaniambia ana nyumba yake ambapo ndipo anapoishi kwa sasa....ila nimemwambia sikuchukua maana upo kwa mtu ambaye alichukua dhamana na wewe inabidi umsubirie huyo mtu kwanza ili muongee naye. Ili kujua kama kuna madai yoyote, huo ndio ubinadamu na ndivyo tulivyokubaliana...au sio mama....’akasema

‘Kuna madeni!?, …mmm sasa nitatoa wapi pesa za kumlipia maana wao walinichukua sijijui, nilikuwa sikumbuki kitu mama, lakini hakuwahi kuniambia kuwa nadaiwa, au ananitibu kwa mkopo….’nikasema

‘Usijali mwanangu kama kuna madeni yatalipwa..mimi mama yako nipo kwa uwezo wa muumba kila kitu kitakwenda vyema…’akasema mama, huku nikimuangalia mama bila kummaliza, hivi ni yule mama aliyekuwa omba omba….siamini

‘Sasa mlijuaje kuwa mimi nipo hapa...?’ nikauliza kwa mshangao na docta akasimama na kusema

‘Yote atakusimulia mama yakom maana kanitoa kazini kwangu kama vile nadaiwa,... ngoja mimi niwaache..’akasema docta na kuondoka.

‘Nashukuru sana docta nisamehe, lakini sikuwa na jinsi nyingine..'akasema mama, na docta akaaga na kuondoka, tukabakia na mama, na mama aksema

'Mwanagu tulihangaika sana kukutafuta unajau nilirudi sasa ni nina miezi mitatu, tumehangaika mpaka nimeenda kijijini, nikarudi, tukatfuta kila sehemu, hata wenzangu wakafikia kusema umeshakufa, nikawaambia mwanangu hajafa yupo hai, ila sijui wapi ulipo na hilo limfanyika kwa matakwa ya mungu...'akasema mama

'Poleni sana, ni kwasababu mimi nimekuwa mtu wa ndani,..nilikuwa siwezi kutembea, ila leo uliponiombea naweza...sijui kama nitashindwa, si umeona pale nimeweza kusimama kidogo...na mwili uliokuwa hauna nguvu sasa una nguvu, ...miguu sasa naweza kunyosha si unaona...

'Pole sana mwanangu, kukupata wewe ni baada ya kufika hapo muhimbili, na kukutana na huyo dakitari ….’akasema

‘Mlikuwa  na nani….?’ Nikauliza

‘Na wafanyakazi wangu , na docta mwingine ambaye alinisaidia kipindi kile cha mwanzo, lakini badaye akakkata tamaa, na ila alipokuja jana akasema tujaribu kuulizia Muhimbili, hatukuwa na wazo hilo kabla, limekuja tu na kumbe ndio ikawa sababu ya kukupata wewe, tuliwahi kufika kipindi cha mwanzo hapo muhimbili tukauliza , huyo tuliyemuuliza alisema hakuna taarifa yoyote ya mtu kama wewe, nahisi hakutaka kutusaidia, lakini safari hii docta akakutana na madocta wenzake, akawaelezea, na ndipo akatokea huyo docta akasema anakumbuka kumuhudmia mtu kama huyo... ..’akasema mama

‘Mwanangu nilishaota ndoto kuwa nisipokupata leo nitakukuta maiti….kwahiyo nilikuwa kama nimechanganyikiwa, na hata nilipofika hapo Muhimbili nikamkuta huyu docta akiwa na kazi zake, aliponiambia tu kuwa kuna mtu kama huyo aliwahi kulazwa hapo, akamuhudumia yeye , nikamwambia;

‘Naomba unipeleke nikamuonea haraka…’nikasema

‘Lakini mama mimi nipo kazini ziwezi kutoka hapa labda nikupe mawasialiano ya mtu ambaye ninamfahamu ambaye alimchukua na akasema atakuwa naye ..huyo mtu ana kiliniki yake ya ‘physiotherapy’, …ni rahisi kufika kwake’akasema mama

‘Nataka wewe unipeleke mguu kwa mguu na usipofanya hivyo kama mtoto wangu akifa na wewe utakufa…’nilimwambia hivyo na akaogopa, akasema;

‘Haya mama ngoja niage wenzangu,...' na kweli akawaaga wenzake na akawasiliana na huyo mtu aliyekufadhili, yeye yupo safarini lakini alisema kuna mdada anakusaidia hapo tunaweza kumkuta lakini kama huyo mdada hayupo, maana huyo mdada ana kazi zake nyingine, anafika hapo kusaidia tu, wafanyakazi wengine wapo watatuelekeza wapi ulipo, …’akasema mama

‘Ina maana kumbe nipo kwenye kiliniki,…mmh nilijua nipo nyumbani kwangu….na huyu mdada hapa ni mfanyakazi wa humu ...leo kachelewa sana kufika sijui kuna nini...’nikasema

‘Mdada….?’ Akauliza mama.

‘Yupo mdada huwa ndiye ananihudumia kwa kuninyosha viungo na chakula…..’nikasema

‘Mimi sijamuona, labda upande wa pili, maana wewe upo huku nyuma, hujawekwa sehemu ya wagonjwa...na ngoja tuagize chakula maana mimi nina njaa’akasema mama akatoka na mimi nilibakiwa nikiwaza mengi, haikuchukua muda mama akarudi akiwa na chakula.

'Mama utafikiri wewe ni mwenyeji, mimi bado najiona mdhaifu..'nikasema

'Umeshapona, kinachohitajika ni mazoezi machache na kuondoa ile hofu, ...'akasema mama

‘Oh, akili ilikuwa haipo mama, …sikuweza kukumbuka kitu, nilikuwa kama mfungwa wa akili….sasa mama ikawaje..?’ nikamuuliza

‘Mwanangu kabla nilishamuomba mungu kuwa niwe nawe hadi mwisho wa maisha yangu, na nilishakuota kwenye ndoto ambayo ilinielekeza mengi kuhusu wewe lakini ilifungwa kujua wapi ulipo , pamoja na karama alizonijali mungu, lakini hazikuweza kujua wapi ulipo....’akasema na kunyosha mikono juu

‘Karama gani mungu kakujalia mama....?’ nikamuuliza

‘Mungu ni mkubwa mwanangu, wanadamu tunazarauliana sana na kunyanyasana, lakini huwezi kujua huyo unayemnyanyasa mungu kamjalia nini..unakumbuka niliwahi kukuhadithia kuwa niliwahi kuitwa mama mwenye mkono wa baraka…?’ akaniuliza…’akasema

‘Mhh mama, sijakuelewa…uliwahi kunihadithia ….oh, yah, nimekumbuka na kweli kuna mambo nahitajia kujau kutoka kwako, ….nimekumbuka kuleee ulipokuwa kijijini, ukaunguzwa na moto…’nikasema

‘Ni kweli mimi nina karama hiyo ila nilikuwa sijijui, …namshukuru sana mungu, niligundua hilo zaidi nikiwa huko India, wakati nasubiria kurekebishwa sura yangu,...unajua huko nilikwenda kwa ajili ya upasuaji wa uvimbe kichwani sio swala la kurekebisha sura yangu iliyokuwa imeharibika…unaikumbuka sura yangu ilivyokuwa awali…?’ akaniuliza

‘Mama hapana….nakumbuka utundu wa utoto tulijaribu kukufunua, lakini mimi sikupenda, nilijali sana ulivyonifundisha, …kuwa na adabu kwa wazazi…sikumbuki mama…’nikasema

‘Sasa una uhakika gani kuwa mimi ni mama yako..?’ akaniuliza

‘Hahaha, mama…siwezi kukusahau ,…macho yako na yangu naona yanafanana…nakumbuka kuna picha nilikuwa nayo nikiwa mdogo, …macho yangu yapo hivyo hivyo, ila sasa yameanza kubadilika sio kama nnilivyokuwa mdogo…mimi  nina uhakika wewe ni mama yangu , japo hujanionyesha ushahidi…kwanza hebu nambie ilikuwaje huko India ulifikaje…? Nikauliza

‘Tutaongea hayo tukiwa na muda , yapo mengi ya kuongea, ..’akasema mama

‘Ehe…..’nikasema

‘Kwahiyo baada ya upasuaji kwa ajili ya uvimbe kwenye ubongo kufanikiwa nikawa nasuburiwa kurudi nyumbani, hakukuwa na pesa hiyo ya kurekebisha sura yangu, kwani mfadhili aliyefika huko aliulizwa kama kuna pesa kwa ajili tatizo hilo akasema yeye hakupewa hilo fungu, kwahiyo nirudi nyumbani kama itapatikana hiyo pesa basi nitarudishwa tena huko India.

‘Basi siku hiyo wakati nasubiria vipimo vingine kuhakikisha kuwa nimeshapona, akaja dakitari huyo bingwa wa upasuaji wa kurekebisha sura, alifika kujua kama anaweza kufanya hiyo kazi, yeye anfanyia hapo hapo hospitalini, lakini alikuwa katuzoea sana, alikuwa kila mara anakuja kunisalimia, na siku hiyo alipofika akawa analalamika kuwa anaumwa kichwa

‘Kichwa changu kinauma sana,....’akawa analalamika alikuwa akiongea kiingereza huku akiwa ameshika kichwa, ilionyesha anaumwa kweli mpaka machozi yanamtoka, na unajua mganga hajigangi, pamoja na utaalamu wake lakini alitumia dawa zote anazozifahamu yeye lakini hakuweza kupona kabisa huwa kinarudia mara kwa mara. Basi hata sijui kwanini ...mimi nikamwambia mfadhili wangu amwambie huyo docta nimuombee huenda kitapona

‘Wewe mama mwenyewe ulishindwa kujiombea, mpaka ukaletwa huku, ....achana na hao watu wewe tusubiri hivyo vipimo tuondoke zetu....’akaniambia huyo mfadhili wangu

‘Mganga hajigangi, wewe mwambie hivyo hisia zinanituma kuwa nikimombea huyo dakitari kichwa chake atapona kabisa....’nikamwambia na yeye hakukutaa akaenda kumwambia hivyo huyo dakitari wakati huo kakaa chini kainama kichwa kinamuuma kweli, ya mungu mengi ...akakubali. akasema niende pale alipokaa maana alikuwa hawezi hata kusimama na ubingwa wake wote  wa udakitari

Nikaenda hadi pale alipokaa nikanyosha mkono wangu na kuuweka kichwani kwake, nikamuombea,.....akapona......’akasema mama


‘Mama ulimuombejae....?’ nikamuuliza mama kwa bashasha

‘Nani kama mama mwanagu, ....mungu muweza uliyejalia uzima, na kumjalia mama kupata mtoto kwa njia ya mateso, akiwa na imani thabiti akamtegemea mungu dua yake haina kipangamizi mwanagu,… maneno ya kumuombea huja hapo hapo, siwezi kukumbuka ni maneno gani kwa hivi sasa... kwani maneno yangu ya karama hutokea kutegeemeana na tatizo la mtu, na hunijia tu nikianza kuomba .....’akasema

‘Mhh mama, kwahiyo hata mimi kupona kwangu uliniombea au ilikuwaje maana mama ulipokuja hapa sikuwa nakumbuka chochote, na nilipokuona tu kichwa kikaanza kuuma, nikawa kama nachanganyikiwa, akili ilikuwa kama sio yangu, nikaanza kuona vitu vya ajabu kichwani, kichwa kikawa kinauma karibu kupasuka, lakini ulivyoweka mkono wako kichwani, mama ikawa ni ajabu kabisa ....’nikasema

‘Mama ikawa kama vile umenimwagia maji ya baridi yakipooza hayo maumivi ndani kwa ndani, na cha ajabu maji hayo yana hisia, ikapooza maumivu na hapo hapo ikawa inasisimua ubongo na mwili uliopooza, .....ajabu kabisa mama....ulifanyaje mama?’ nikauliza, na mama akawa kimia nikasema;

‘Mama hebu fikiria mwili ambao ulikuwa hauwezi kufanya kitu, nilikuwa natembelea hicho kigari hapo, mwili ulikuwa umepooza, siwezi kusimama, nifanya kujikokota  kwa shida, kuna muda najaribu kusimama lakini miguu inakuwa haina nguvu, na hicho kigari cha kusukuma, ndio miguu yangu…lakini sasa mama naweza kusimama.

‘Mama nimepona, si unaoana...nikasimama nikayumba kidogo, lakini nikajitahidi na kuanza kutembea huku na kule, nikaruka kwa raha,...

‘Mama nimepona,.....nakushukuru sana mama yangu....’nikasema na kumsogelea, kumkumbatia mama akasema;

‘Mshukuru mungu....unasikia nyosha mikono juu umshukuru mungu wako, na kawaida mtu akipona yeye ndiye anataja kiwango gani cha kunilipa mimi, kwahiyo taja unataka unilipe nini....’ mama akasema


‘Mwanagu karama za mungu ni nyingi, na ukiwa nazo hata wewe mwenyewe huwezi kuzisema tu, kwani unafanya hivyo sio kama wewe, ni mungu mwenyewe anashusha nguvu zake na kuzijaza mdomoni mwako, sio wewe ....kwahiyo siwezi nikasema mimi ndiye natenda hizo karama, hapana, sio mimi mponyaji au mtoa baraka ni mungu mwenyewe kwa kupitia mkono alionijalia na pumzi alionijali na mdomo, ulimi wa kusema alionijalia, sio mimi mwanagu mimi ni njia tu..’akasema mama

‘Mama.....mmh, na umasikini wangu huu, mama nitakununulia eeh, gari zuri saan la kutembelea....’nikajikuta nimesema hivyo wakati mimi sina kitu , hohe hahe

‘Sawa mwanangu, wewe ni mtoto wangu, japokuwa sihitaji hilo gari maana mimi ninalo gari langu, lakini ndio masharti ya karama hii ukipona ni wewe mwenyewe unataja gharama kutokana na uwezo wako, na mara nyingi kauli hiyo huja kwa uwezo wa muumba,....’akasema

‘lakini mama ukifanya hivyo watu si watakudhulumu, wengine hawatataja kutokana na uwezo wao, wenye mioyo ya dhuluma,,,,,’ nikamwambia mama , na mama akatabasamu na kucheka, akasema

‘Nikiwa India alikuja tajiri mmoja, tajiri huyo licha ya utajiri wake, lakini alikuwa akisumbuliwa sana na maumivu ya kichwa, kichwa ambacho alikihangaikia sana akatafuta madakitari wa kila namna lakini hakupona, na tajiri huyo alkuwa na tatizo kubwa la ubahili, roho mbaya.....dhuluma, na hakujua kuwa kichwa hicho kinamuuma kwasababu ya dhuluma, na tabia yake hiyo...’akasema mama

‘Ikawaje…’ nikatulia kusikiliza

‘Basi alipokuja nikamuombea, akapona kichwa chake, kama kawaida akaniuliza ushuru, nikamwambia yeye ataje atanilipa nini…akasema dola elifu moja, watu waliokuwepo hapo wakashangaa maana ni tajiri kweli pesa hiyo aliyotaja kwake ni pesa ndogo sana

‘Sawa ..’mimi nikamwambia na akatoa akaondoka, na kwa muda huo huo akafika mtu mmoja yeye ni masikini , wanamjua sana watu wa huko, alikuwa na tatizo hilo hilo, nilipomuomba nikasema ataje kiwango, akasema dola laki moja…watu wakacheka, mimi nikamwambia ‘sawa’

‘Nenda kazilete….’nikamwambia maana nilijua hana, lakini kauli hiyo sio yake, ni kauli imetoka kwa mungu,…akaondoka, haikupita siku hiyo akaja na hiyo pesa…’akasema mama

‘Aliipata wapi,…?’ nikauliza

‘Kutoka kwa yule tajiri wa mwanzo,..’akasema mama

‘Kwa vipi..?’ nikauliza kwa hamasa

‘Yule masikini alipotoka hapo, alikwenda masikani kwake, ….unajua maswala ya haja, haja ndogo tu, yanaweza kumpata mtu popote pale ukashindwa kuvumilia, kule kuna sehemu kuna sheria hutakiw kukojoa ovyo..

Huyu masikini ana simu yake ya kuchukua picha aliiokota tu, sasa alipofika masikani kwake, yule tajiri alikuwa akipita na gari lake, alishikwa na haja, hakujua eneo hilo kuna mtu anaishi, akazarau akijua ni uchochoroni tu, yule tajiri akawa anajisaidia, ni uchochoro, lakini ni eneo lenye sheria hizo, alishikwa na haja hakuweza kuvumilia, yule masikini akatoa kamera yake haraka akamchukua picha ya video jamaa hajui..kamaliza haja yake, anataka kuondoka masikini yule akamkabili

‘Umevunja sheria…’akasema na walinzi wakamsogelea wakita kuhakikisha bosi wao hazuriki, akawaambia walinzi wamuache tu, maana yeye anamfahamu huyo masikini akamuuliza nimevunja sheria gani

‘Umekojoa eneo lisiloruhusiwa..’akasema na huyo tajiri akashituka hakujua kabisa kuwa kaonekana, akamuuliza
‘Una ushahidi gani..?’ akauliza

‘Utaujualia mahakamani..’akasema masikini, na yule tajiri kwanza alitaka kutumia nguvu lakini akashituka akaujua ni lazima huyo masikini atakuwa na kitu cha kuweza kumsaidia, akasema

‘Unataka nikupe nini, ili usinishitaki….?’ Akauliza

‘Dola laki moja na nusu…’akasema

‘Nini…wewe unaota nini…’akasema

‘Na huo ushahidi nimeshauhifadhi kwenye mtandao  huwezi kuuondoa, mpaka mwenyewe nikubali..’akasema, na yule tajiri akasema;

‘Haya twende nyumba ni nikakupe..akijua akifika huko atamfanyia vituko, lakini masikini yule alikuwa mjanja, alikuwa na akili japokuwa nakama zilimuandama, akasema

‘Mpaka awepo mwanasheria wangu..’akasema na walinzi wakacheka, na hakujali kicheko chake akampigia wakili mmoja anayejulikana sana, wakili ambaye sifa yake kubwa ni kuwasaidia wasiojiweza , anajitolea ..hakuipita muda akafika huyo wakili, yule tajiri akaona sasa anaumbuka.

‘Kwani wewe una ushahidi gani…?’ aakmuuliza

‘Yule masikini akatoa simu yake akampa yule wakili na yule wakili akaliona hilo tendo, na wakili sasa akawa anaongea na huyo tajiri, yule masikini akakaa pembeni.

‘mteja wangu aantaka dola laki mbili pamoja na gharama zangu,,….’akasema wakili
‘Eti nini…?’ akasema huyo tajiri

‘Kama hutoi tutakuita mahakamani, na ujue vyombo vya habari viatakuwepo…’akasema, na kwanini huyo tajiri asitoe hizo pesa, na yule masikini kwa haraka akaja kunipa hizo pesa na nyingine akampa yule wakili ushuru wake, na akabakiwa na haki yake…’akasema mama

‘Mama ni hadithi au ni kweli…’nikamuuliza mama

‘Mwanagu kutokana na matatizo haya, kutokana na karama hii nimekutana na mambo mengi ya ajabu, na ukitaka nikusimulie yaliyonikuta tutakesha, ila wewe elewa kuwa mungu ndiye mtoa riziki, na hata uwe tajiri vipi kama mungu kapanga kuwa riziki uliyo nayo itakwenda kwa mtu mwingine kamwe hutaweza kuzuia,..’akasema mama

‘Sawa mama turudi kwa huyo dakitari bingwa ikawaje kwake..?’ nikamuuliza

‘Kutokana na lile tendo, maana wakati namuombea walifika madakitari wengine wa hapo wakawa wanataka kushuhudia, mama muafrika anawezaje kumtibu huyo dakitari bingwa, ilienea kwa hara ka sana.

Mimi nilipomaliza kufanya yale maombi nilishangaa nimezungukwa, madakitari manesi wa hapo wamakuja kushuhudia,….’akasema mama

‘Nilipomaliza nikageuka kwa mfadhili wangu nikamwambia;

‘Nimemaliza, atapona tu hicho kichwa chake, kwa uwezo wa mungu…’hata huyo mfadhili wangu hakuamini, maana yule dakitari alisimama akaniangalai sana akasema

‘Nitakufanyia huo upasuaji kwa gharama zangu mwenyewe…, nahis kichwa kimepona, …its like a magic….’akasema

‘Kweli mama, ikawa hivyo…?’ nikauliza

‘Ndio hivyo nikafanyiwa huo upasuaji na sura yangu ikarekebishwa, japokuwa niliandamwa na ugonjwa wa ngozi nahis ni aleji, nikawa natokwa na vipele,..lakini vilikuja kuisha ndio maana unaniona hivi…. na baada ya hapo wakataka kuniajiri niwe mfanyakazi wao…nikakataa, nikasema ninaweza kukaa hapo kuwasaidia watu, kwa muda, lakini sio kwa kuajiriwa…

‘Basi wakanikubalia, lakini kwa sharti kuwa ni lazima kuwe na malipo, ili niweze kuwalipia kodi na hapo hospitalini, wao wakataka kupanga kiwango nikawaambia mimi karama yangu haina kiwango, kiwango kinatokana na uwezo wa mtu kama wanataka sawa, kama hawataki narudi kwetu..wakakubali…’akasema mama
‘Basi kwa kupitia huyo dakitari nikajulikana, …unajua kuna watu wengi wana matatizo ya kichwa, kichwa kinauma sana, na wengine hufikia hadi kuchanganyikiwa, na kutokana na karama hii nimeweza kuwasaidia watu wengi,…watoto wanaolia lia, matatizo ya kupoooza viungo kutokana na maumivi ya kichwa..’akasema mama

‘Kwahiyo mama ukawa tajiri…?’ nikamuuliza mama

‘Kwa uwezo wa mungu na karama zake sasa hivi mwanagu hatuna shida tena, walitaka nikae huko India lakini sikukubali, baada ya miezi kadhaa nikawaambia narudi nyumbani, nakwenda kumtafuta mwanangu najua mwaanngu yupo matatizoni.

‘Waliniomba sana, nikawaambia nitarudi, hapo nitakapohakikisha nimemuokoa mwanangu..na ndio nikarudi nikakuta nyumba imeshajengwa, na ipo kliniki imeshajengwa, kutokana na ahadi za wale nilioaombea na gari hilo hapo nje....kwahiyo mwanangu tuna nyumba yetu nzuri tu, kiliniki , na gari..na p[esa nyingi tu…’akasema mama

‘Nyumba yetu....?’ nikauliza

‘Ndio ni yetu mimi na wewe...sina mtoto mwingine zaidi yako,.....na kama nisingelikupata basi sijui.....ingekuwa haina maana kwangu....’akasema mama

‘Oh mama...ina maana…,’nikasema

‘Mwanangu ukiwa na shida ukiwa na matatizo usikate tamaa, shida hiyo ni mithani ya mungu kukuelekeza kwenye jambo la heri...shida hiyo ni mitihani ili msimamo wako kwa muumbako ujulikane...ukitulia , ukatuliza mawazo ukaelekeza uso wako kwa mungu...utafanikiwa tu mwanangu...’akasema mama

‘Mwanagu kuna ile ndoto niliyoota, unakumbuka nilikuahadithia kuhusu ile ndoto...Niligundua ukweli wa ile ndoto nilipokuwa nasubiri urekebishwaji wa sura yangu.

Nawashukuru sana wafadhili waliojitolea kuhakikisha naondolewa huo uvimbe na sura yangu kurejea hapa ilipo…hata mimi sikuamini pale nilipoambiwa nijitizame kwenye kiyoo, ilikuwa kama najiona wakati nipo msichana…’ aliongea mama huku namtizama usoni

Nilijaribu kumuwazia alivyouwa awali, bila kufanikiwa, kwa maelezo yake sura yake iliharibia sana, hata haitizamiki, ilifikia hata yeye mwenyewe alijichukia, na kutokana na jinsi alivyouwa  wengi waliamua hata kumuita mwanga kwa ajili ya michirizi na kuchanikachanika usoni, na sura kuwa ya kutisha, na ukichanganya na macho yake yaliyouwa na utofauti fulani, basi ilikuwa kama kisingizo.... leo hii ni mwanamama mwenye sura ya kipekee…

Ni ajabu iliyoje yale macho ukiwa na sura kama ile ya utisha alionekana wa ajabu, na kuonekana ni mwanga, mchawi…lakini sasa akiwa na sura nzuri, macho hayo yalimfanya mama aonekane mrembo,…nilijikuta nikitabasamu na kusema moyoni, ama kweli mama alijaliwa uzuri

‘Mungu ni mkubwa mama, siamini hadi sasa naona kama namtizama ndugu  yako, kwani sikumbuki kuiona sura yako ukiwa katika hali nzuri kama hii..’nikasema

‘Nitakuonyesha picha zote nilizopiga nikiwa huko kabla na baada ya huo upasuaji, ili ujue kuwa dunia hii kuna wataalamu, tuwashukuru sana madakitari ambao fani yao  kwakweli ni ya kujali uhai wa mwanadamu…’ akasema mama

Mama akaongezea kusema, `Kumbuka nilikimbiwa, niliitwa mchawi, nikadharauliwa sababu ya  sura ile, ambayo sikupenda kabisa iwe vile, ila ni kwasababu ya watu wenye roho mbaya…’akasema mama .

‘Mwanangu ndani ya ndoto yangu niliota kuwa upo katika hali mbaya, na  yale yaliyomtokea mama yako akimbiwe kuwa ni mchawi, yamekuandama kwa namna nyingine, watu wanakukimbia na kunynyapaa kwa hali uliyo nayo, kukonda kwako kumekuwa ni sababu ya kuonekana si mwanadamu….yote hayo  niliyaona kwenye ndoto kwa namna ya fumbo, lakini usijali mwanangu kwani yote hayo ni mitihani ya kimaisha, ikija unatakiwa uwe na subira, na usimamie katika haki…’ mama akanishika kichwa.

‘Kwahiyo mama unataka kuondoka..?’ nikamuuliza

‘Nakwenda kuwawahi wateja , wataje ni wafalme, nitapitia hapo kuangalia gharama zako, nijue nikiasi gani halafu nitakuja kulipia, tutaondoka sote….’akasema mama

Sawa mama, lakini kabla hujaondoka … unakumbuka uliwahi kunihadithia maisha yako ulipopitia na  nakumbuka ulikatisha siku ile ulipozidiwa ukashindwa kunimalizia kuwa ilikuwaje , je yule mama kule hospitalini alikuwa wewe  au nani na siku ile alipoondoka kule nyumbani kwa dada yake nesi alikwenda wapi na je alimpataje mtoto wake, na huyo mtoto ndio mimi au alikuwa mwingine…?’ nikamuuliza maswali mengi kwa pamoja.

Mama alimwangalia mwanae kwa muda, halafu akatabasamu na kusema, ‘hivi mwanangu bado una hamu na vidonda vinavyoonza kupona, huoni ukiyawaza hayo , ukayahadithia , yanatia simanzi , na mwishowe unakaribisha hasira za visasi, mimi naona  tusahau hayo tugange yajayo…’Mama akasema akiinuka kuondoka.

NB: Je mnahitaji kujua hayo, yaliyokuwa yamebakia huko kijijini, je unahitajia kujua jinsi mama alivyokwenda India, …kama mnapenda, tuelezane, vnginevyo, kisa kinaweza kuishia hapa, iliyobakia ni hitimisho tu…


WAZO LA LEO: Dunia tulivyo, mnaweza mkahangaika pamoja, kutafuta pamoja, lakini pale mnapopata tabia hubadilika, uchu, uchoyo ubinafsi huteka nyoyo zetu, tunaweza kusahau kabisa jinsi gani tulivyohangaika pamoja, na huenda hata katika kuhangaika mmoja au wachache ndio waliokuwa wakitumika zaidi, lakini wale wategaji, wajanja-wajanja, waongeaji sana bila vitendo,  ndio wanaweza kudai masilahi zaidi ya wengine…huo sio uungwa, huo sio upendo, huo sio uadilifu, ili kweli tuwe wachamungu wa kweli, wepenzi wa kweli, ni pale kila mmoja atakapokuwa tayari kutoa , au hata kuacha ili mwenzake apate, kuoneana huruma, hata kama ni kidogo uwe radhi mwenzako apate wewe ukose, je kuna upendo kama huo,. Je watu kama hao wapo kwenye hii dunia?

Ni mimi: emu-three

Friday, May 22, 2015

NANI KAMA MAMA-81


 ‘Hivi kweli mimi nina mke, mke wangu yupoje, anafananaje, je ananipenda…naona atafurahi sana akiniona nimepona, au…oh nahis huenda tulikuwa na furaha sana,’ yalikuwa maswali mengi kichwani, na sijui kwanini nilikuwa nikiwaza hili la mke sana,  kuliko mambo mengine.

Nilifikia kuwaza jinsi tulivyokutana tukapendana,….tukafikia kuoana..nikajenga taswira nyingi za huyo mwanamke kuwa ni mrembo sana….nikajaribu kufikiria sura nzuri zaidi,…na mimi mwenyewe kujiona kijana mtanashati…yaani mawazo mawazo….

‘Sijui sasa mke wangu atakuwaje…kakonda, hapana, ni ….mmmh….’nikajikuta naongea peke yangu.

 Nikawa nasubiri kuwaona hao jamaa zangu ambao niliambiwa wanakuja kila siku, nakumbuka kuna watu huwa wanakuja, tunasalimiana na wanandoka, lakini sijui ni akina nani, labda ndio hao jamaa zangu sikuwa na uhakika kwa kweli.

Siku hiyo niliwaza sana, nikiwa na matumaini ya kuwaona hao ndugu zangu, nikiwa na matumaini ya kwenda kupaona hapo nyumbani kwangu, sikuwa najua ni wapi, na kama nina nyumba au nimepanga,…

Wakati nawaza haya nikashikwa na usingizi, na ndani ya usingizi nikamuona mwanamke mmoja akiwa, kavaa nguo zinazomeremeta, alikuwa kakaa kwenye kiti, halafu anakunywa kinywaji kweny gilasi, alikuwa mwanamke mrembo wa kuvutia, na alionekana hataki kuguswa na takataka, kwani kila mara alikuwa akijiangalia na kila akiona kitu tofauti anakifuta,…alikuwa anameta meta

Baadaye nikaona hali inabdilika, ile sura yake ikawa inabadilika taratibu, na ilna akawa anaingiwa na madoa ya uchafu , na kila kiona hivyo anahangaika kuyaondoa hayo madoa lakini yakwa yanamjia kwa aksi, akawa anabadilika hata sura, na baadaye ile rangi ikawa sura ya kutisha ajabu, mdomoni akawa anatoa uchafu, ….ulikuwa unatoa harufu mbaya ajabu. Na alipofunua meno yake yakawa ya kutisha kama ya shetani…

Nikawa sitaki kumtizama yule mwanamke, naye anakazania nimtizame kile anachotoa mdomoni, na mara akatokea mwanamke mwingine akiwa kajifunika usoni, alikuwa akimtizama yule mwanamke kwa macho ya huruma, halafu akanitizama mimi, na akawa kama ananionya kuwa huyo mwanamke atanilisha uchafu wake nisogee pembeni, nikawa najaribu kusogea lakini sikuweza kuinua hata mkono.

Yule mwanamke anayetoa uchafu mdomoni, akacheka kicheko cha dharau, huyo mwanamke mwingine ambaye kajifunika, akatikisa kichwa na kunyosha mkono wake kuniweka kichwani, lakini kila akijaribu kunisogelea yule mwanamke anayetoa uchafu anamzuia, ikawa kama wanashindana, na mimi siwezi kuinuka, wala kufanya lolote….

Na katika juhudi hizo ,yule mwanamke aliyejifunika uso, akaweza kunifikia na mkono wake akanifikia kichwani,  ilikuwa kama ubaridi fulani, au kitu ambacho huamusha hisia mwilini, …kwani nilihisi mwili ambao ulikuwa joto unapoa, mwili ambao ulikuwa hauna hisia unahisi kitu fulani.

Mara yule mwanamke anayetoa uchafu akaanza kubadilika sura, na kama vile anaoza, na kuanza kumomonyoka, na baadaye akawa anapotoea kidogokidogo huku anapiga ukulele. Huyu mwanamke aliyenishika kichwani akawa ananitizama usoni, lakini nilikuwa simuoni vyema sura yake kwani alikuwa amejifunika usoni kwa nguo.

Baadaye yule mwanamke aliyebadilika akapotoea kabisa nikabakia na huyo mwanamke aliyejifunika usoni, akaniuliza,. ..

‘Unajisikiaje kwa sasa,….?’ Akaniuliza nikajaribu kupanua mdomo niongee sikuweza, basi nikawa namjibu kwa hisia

‘Naona nimepona…’nikasema kwa hisia, halafu akaniuliza;

‘Unajua mimi ni nani?’ akauliza yeye alikuwa anatoa sauti, mimi nikamjibu kwa hisia tu.

‘Nitajuaje we ni nani wakati umejifunika uso wako….’ Na nikijibu kwa hisia anaelewa, nikaongezea kumuuliza kwa hisia;

‘Naomba ujifunue uso wako maana naona wewe ni mtu mwema sana ….kwani wewe unanifahamu kuwa mimi ni nani….?’ Akanitizama, alitoa sauti kama ya kicheko, halafu akasema;

‘Mimi nakufahamu sana, hata kama wewe ungejifunika kama mimi ningekufahamu pia,…’akasema

‘Kwa vipi, kwani wewe ni nani mpaka unifahamu kihivyo,..?’ nikauliza kwa hisia nikionyesha mshangao

‘Mimi nakujua ,a kukufahamu hata kabla wewe hujajiua wewe ni nani…’akasema

‘Mhh, basi wewe sio binadamu wa kawaida…naomba nikufahamu wewe ni nani…kwani kuna ubaya….naomba pia nikuone sura yako….’nikasema kwa hisia

‘Ipo siku utaniona vyema kwani kwasasa siwezi kutizimika,….nilivyo watu, hata wewe hutatamani kunitizama, ….’akasema

‘Kwanini huwezi kutizamika, kwani sura yako ipoje, inatisha, au imefanyaje au wewe sio binadamu wa kawaida? …mimi kwa vyovyote uwavyo nitafurahi kukuona sura yako…’nikasema kwa hisia, na yeye akasema.

‘Yote ni mapenzi ya mungu, na yote yametokea ili mapenzi ya kweli ya mama na mtoto wake yaonekane…’akasema

‘Mama na mtoto wake…?’ nikauliza

‘Nikuulize wewe je unamfahamu mama yako ni nani, mama yako wa kweli, aliyekuzaa, akakulea, …?’

Nikijaribu kufunua mdomo ili nitamke neno mama, lakini haukuweza, nikasema kwa hisa ile ile,

‘Mama, mama yangu, yupo wapi…mimi simjui mama yangu….’nikasema

‘Unaona..wewe humjui mama, je kweli mtoto anaweza kuzaliwa bila mama yake..?’ akaniuliza

‘Hapana….najua kuwa nina mama, lakini sijawahi kumuona..’nikasema kwa hisia

‘Lakini mama yako anakujua na anajua ana mtoto kama wewe hata kama kumbukumbu zake hazipo, …unajua ni kwanini?’ akauliza
‘Mhh…sijui…’nikasema hivyo hivyo kwa hisia, nikashngaa kwanini kaniuliz vile, na kabla sijasema neno kwa hisia akasema ,

`Nikuonyesha kuwa hakuna kama mama, kwani mama anakujua wewe kabla hujajiua, alikuhisi ukiwa tumboni mwake, ukacheza huko ndani ukampiga mateke, akakuzaa kwa shida, wewe hujui na wala hujijui, je atawezaje kukusahau baada ya kukuzaa…’akasema.

‘Lakini ….wewe ni nani, basi niambie mama yangu ni nani na yupo wapi…’ nikauliza swali na akasema

‘Usiwe na haraka, utamfahamu kwa wakati muafaka…kwani ukimfahamu sasa hivi huenda, kwa hali ya kibinadamu ukaweza kuingiwa na huzuni, na hata kuchukia, na mwisho wake utakosa radhi,,,vuta subira kwani kila jambop la heri huja kwa amani na kwa wakati muafaka...’huyo mama akasema na akawa kama anapotoea

‘Mama…mama yangu yupo wapi…’sasa kilichotamka ni mdomo, na nilipoweza kutamka hivyo, mara nikazindukana kutoka kwenye ile ndoto.

 Nilipogundua kuwa ilikuwa ndoto nikapapasa macho na kutizam huku na kule, nilijikuta nimezungukwa na baadhi ya watu akiwemo dakitari na wanaume wawili na mwanamke mmoja…akili ilianza kufanya kazi kuwa hawa watu sio mara ya kwanza kuwaona, nikajaribu kukumbuka wapi niliwaona lakini ikawa vigumu.

‘Hawa ndio jamaa zako niliokuambia, …inaonekana ulikuwa kwenye ndoto kali , na hatukutaka kukuamusha maana ilionekana ni ndoto njema, mwanzoni uliweweseka na kupiga ukelele, lakini baadaye ukaonyesha furaha, unaweza kutuambia ulikuwa unaota nini..?’ docta akauliza.

‘Mhh, hata sikumbuki…mmh, ngoja nikumbuke, nilikuwa naongea na mtu, na wanawake wawili, na wote wamepotoea, .’ nikasema

‘Hukuweza kuwakumbuka sura zao, na je unawafahamu ni akina nani..?’ akauliza dakitari.

‘Kwa kweli siwajui, ila mmoja anatisha, sitaki hata kukumbuka alikuwa anatoa harufu mbaya mdomoni na kila neno analoongea linanuka…aah, sijui ni kwanini…’nikasema

‘Na huyo mwingine…?’ akauliza docta

‘Mhh huyu wa mwisho alikuwa mwema sana, alinishika kichwani, nikajiona nimepona, aliniambia maneno matamu ambayo nilitamani kuyasikiliza wakati wote, ila aliniuliza swali moja kabla sijamjibu akawa mumeniamusha, ….huyu mwanamke amejifunika uso mzima, …sijui kwanini…’ nikawaangalia kama vile walikuwepo kwenye ndoto , na wao wakabakia kushangaa.

‘Hebu tuambie sasa unajisikiaje sasa, maana umesharuhusiwa, na hawa ndio jamaa zako….’akasema docta na wale watu wakanisogelea

‘Haya inuka tuondoke…maana umesharuhusiwa , docta kasema huhitajiki kuendelea kukaa hapa kwani hali yako inaendelea vyema, ni swala la kurudisha kumbukumbu tu ndilo limebakia…na tumekuja na kigari utakuwa unakitumia hadi hapo utakapoweza kutembea vyema’ akasema mwanaume mmojawapo na yule mwanamke alikuwa akikusanya vitu nilivyokuwa nikitumia, nikajiuliza ndio mke wangu nini, mbona ni mkarimu sana kwangu.

Nilikiangalia kile kigari nikawa najissikia vibaya, kwani kutokuweza kutembea vyema ndio tatizo jingine lililokuwa likinikera docta alisema hayo yanatokana na tatizo kwenye ubongo, kumbukumbu zikikaa vyema na hata kutembea kutarudi,…

‘Inaoenekana unawaza sana, hujakumbuka lolote..?’ aliyeuliza hivyo alikuwa ni yule dakitari wangu wa kila siku.

‘Kukumbuka, …hapana, nakumbuka ulisema mke wangu yupo, ndio yupi, nilitarajia angekuja kuniona leo, au…’ nikamgeukia yule mwanamke aliyekuwa akikusanya vitu , yeye hakuwa akituskiliza kwani alikuwa akihangaika kukusanya vitu, na alipogeuka akakuta ninamtizama, akashangaa na kutuangalia.

‘Vipi mbona wote mnanitizama mimi..’ akauliza huyo mwanamke

‘Mgonjwa anahisi wewe ni mkewe…’ akasema mwanaume mmoja

‘Hahaha kweli….unafikiria hivyo, …basi usiwe na wasiwasi mimi ni mke mwema sana, nikipata bahati ya kuwa na wewe hutapata shida, utapona kabisa..’ akasema huku anaweka vifaa kwenye kapu.

Na mimi nikawa nashangaa, kuwa mbona kanijibu kama vila utani, mimi nilizania kuwa yeye ndiye mke wangu halafu anajibu kinyume na matarajio yangu.

Tuliondoka hapo hospitalini hadi kwenye nyumba moja nzuri, hapo nikaambiwa kuwa patakuwa nyumbani kwangu,…nikashangaa kwa akuli hiyo

 `Patakuwa nyumbani kwangu, kwani kwangu ni wapi..nikajiuliza lakini sikutaka kuuliza sana, nikawa mara nyingi namwangalia yule mwanamke kwa kujiiba, na alikuwa mkarimu kwangu kupita kiasi, wakati mwingine ananikanda akisema kufanya vile kunasaidia kurudisha hisia za mwilini na kunipa mazoezi hasa ya miguu ili iweze kuwa na nguvu ya kutembea.

Hali yangu ilikuwa ikirudi kidogokidogo sana, mwili ukaanza kuingiwa na nguvu, na kuongezeka kidogo kidogo, maana nilikonda sana,…na nilionekana kama mzee, lakini sasa sura ikaanza kutakaka, lakini tatizo likawa ni  kumbukumbu na kuweza kutembea vyema, nikawa natumia kigari cha kukaa…..ilinikera sana hiyo hali.

Miezi ikapita mingi tu na mwaka sasa unaingia….sijaweza kukumbuka au kuweza kutembea bila kutumia kigari, san asana nikisimama natumia fimbo, na napaat shida na husihia kudondoka chini.

 Siku moja tulibakia mimi na huyo mwanamke, akawa nanifanyia `masaji’ na alipomaliza nilihisi  msisimuko mwilini, msisimuko ambao sikuwahi kuuhisi kabla, kwani mara nyingi mwili wangu ulikuwa kama una ganzi fulani, lakini kila mara alipokuwa akinishika huyu mwanamke, nilikuwa nahisi kuwa kweli ananishika tofauti na awali.

‘Nahisi msisimuko, leo umenipaka nini mwilini..?’ nikauliza, na yule mwanamke akacheka na kutabasamu, akasema ni mafuta yale, yale ya kawaida. Nilimtizama machoni mpaka akaona aibu, akaniuliza kuwa nawaza nini, nikamwambia nahisi kuwa yeye ni mke wangu,

Nilipoatamka hivyo akacheka sana ,hakusema kitu akamaliza kazi zake na baaadaye akaja akakaa karibu name, akaniuliza

‘Kwanini unahisi kuwa mimi ni mke wako..?’ akaniuliza

‘Maana docta aliniambia yupo mke wangu, na tangu nifike hapa sijamuona nakuona wewe, sasa kwanini nisikubali kuwa wewe ni mke wangu.

‘Unamfahamu vyema huyo mke wangu..?’ nikamuuliza.

‘Mhh,..si unajua tatizo langu, sina kumbukumbu za nyuma, sikumbuki kitu, simkumbuki hata nikimuona..hata sura siikumbuki…’nikasema

‘Mhh, sasa kwanini unifikirie kuwa mimi ni mkeo ….?’ Akaniuliza

‘Ni kama nilivyokuambia, wewe ndiye upo karibu nami, na kama kweli nina mke kwanini hajafika kuniona..zaidi yako wewe….au wewe unamfahamu mke wangu…?’nikasema na kumuuliza

‘Nitamjua wapi wako, wakati tangu tuanze kukuuguza , ukatoka hospitalini, tumekuleta hapa tumekaa wote, tumeulizia jamaa zako, lakini hakuna aliyejitokeza, kwa kweli hatujawahi kumuona ndugu yako yoyote aliyewahi kuja kukuona….! ..’akasema na hapo nikahisi mwili ukinyong’onyea, ina maana kumbe hawa sio ndugu zangu ni wasamaria wema tu.

‘Mhh, ina maana nyie sio ndugu zangu…?’ nikauliza
‘Kiukweli sisi sio ndugu zako, tunasubiri upone labda utatuambia ndugu zako ni nani, maana hatuna njia nyingine ya kuwajua, tumejitahdi tuwezavyo, tumefikia hatua tumekata tamaa..’ akasema yule mwanamke.

‘Wewe umeolewa…?’ nikamuuliza, na yule mwanamke akacheka sana.

‘Hahaha…swali gani hilo mpendwa, kama sijaolewa unataka kunioa wewe…utaniweza lakini?’ akaniuliza

‘Kwanini nisikuweze, niambia ukweli kama hujaolewa….’nikasema

‘Mimi ndio nimeolewa….sasa nikuambia ukweli’akasema na hapo mwili ukazidi kuisha nguvu sijui ni wivu sijui ni-nini

‘Umeolewa na nani…nilijua tu ni huyo mwanamue unayekuja naye mara kwa mara…na siku hizi simuoni tena, yupo wapi, ndiye mume wako…, lakini mbona sijasikia mkiitana mke wangu, mume wangu…sioni dalili kama hiyo..?’ nikauliza na yeye akanitizama usoni, akasema,

‘Ndio…si umateka nikuambie ukweli,  mimi- nimeolewa- na –wewe, umefurahi sasa… hebu kumbuka vyema , yaani wewe unamsahau hata mke wako, mmh wewe ni mume gani , ….’ akasema na kunitizama usoni, alinitizama hivyo kwa muda mpaka nikawa anjiuliza kwanini alikuwa akinitizama hivyo, nami nilihisi kitu fulani moyoni, nilimuona kama mwanamke mwema, mrembo , na nilitamani awe kweli ni mke wangu.

‘Mhh, sasa hapo unanichanganya,…mwanzoni ulisema wewe sio mke wangu,…sasa tena unasema wewe ni mke wangu, hebu niambie ukweli ili nisichanganyikiwe zaidi..’nikasema

‘Kwani wewe ulitakaje..hebu nambie ukweli wako, wewe ulitaka iwe vipi?’ akaniuliza

‘Mimi eeh, ..nataka hivi kama hujaolewa…eeh, unajua nikuambie ukweli wewe ni mwanamke mwema sana, wanaume wanatafuta mke kama wewe, wewe unaonekana ni mke mwema sana…na kama kweli sina mke …au mke wangu hanitaki,…maana naanza kuamini kuwa wewe kweli sio mke wangu, ..’nikatulia kidogo na yeye alipoona nimetulia akaniangalia akasema

‘Kwanini sasa uaamini hivyo, kuwa mimi sio mke wako…?’ akaniuliza

‘Mhh, kama wewe kweli ni mke wangu, mbona hujawahi kuja kulala na mimi..’nikasema na yeye akasimama, maana muda wote alikuwa kaka karibu yangu , alianza kukusanya vitu, akawa kimia kwa muda.

‘Kama kweli nina mke kwanini huyo mke wangu haji kuniona, unajua siamini,…siamini kama kweli nina mke…., sizani, mimi nahisi sina mke, eti hata wewe huwezi kuliona hilo….! Kusema ukweli natamani wewe uwe mke wangu…’ nikasema nay eye akageuka kuniangalia huku akitabasamu akasema.

‘Usijali, najua ukipona utabadili mawazo, …hiyo ni kawaida kwasababu nipo karibu nawe muda wote, kwahiyo unahisi kuwa mimi ni wa pekee sana, akili ikichanganya na kuwaona wanawake wengine, au akija mke wako, utagundua kuwa mimi si chochote mbele yao….’ Akasema huku ananimiminia gilasi ya juice ya matunda.

Nilipomaliza kunywa huyo mwanamke akaondoka, nikabakia peke yangu, nami niliendelea kutawaliwa na hisia ambazo sio za kawaida, hisia hizi zilinitawala akilini, na akili ikawa kama inawanga vile…na ingawaje yule mwanamke alishaondoka, lakini nilikuwa bado namuwaza yeye, nikawa natamani kumuita arudi lakini alishaondoka na akiondoka kurudi kwake hapo ni muda wa chakula cha mchana.

Siku zikaenda na hali ilikuwa ni ile ile…na siku moja nikiwa nimepumzika, nikitafakari dunia ilivyo, nilishajiona mwenye mapungufu mwili, maana kama siwezi kutembea vyema mpaka kutumia kigari, na kama siwezi kukumbuka vyema basi mimi ni nani..

Niliwaza sana na kitu kikanijia kichwani, kikiniambia mimi ni bora nife tu, nitafute sumu nijiue,…sijui kwanini wazo hilo lilinijia muda kaam huo, kujiua, kwanini nijiue, kwasababu sina faida, kwasababu mimi ni mtu wa kuhudumiwa tu, sina ndugu, sina thamani yoyote duniani

Wazo lilianza kama mzaha, nikajikuta natafuta njia za kujiua, kwa sumu au kwa kujinyonga…nikawa nawazia kila njia, akili sasa ikaganda kwenye hilo wazo, nikaenda mlangoni nikaufunga kwa ndani, sikutaka watu waje kunikatiza nilitaka nife kimia kimia…

Na wakati napanga njia rahisi ya kutenda tendo hilo, mara nikasikia hodi mlangoni…

Kwa muda huo nilikuwa nimekaa kwenye hicho kigari cha kukokotwa na kusukumwa kwa mikono, nilikuwa najaribu kuangalia njia ya kutenda hilo wazo lililonijia akilini, hodi ndio iliyolipoteza hilo wazo..nikageuka kuangalia mlangoni, sikutarajia hodi kwa muda huo..nikawa najiuliza ni nani huyo..

Sikupoteza muda nikasukuma magudumu ya kile kigari change cha kusukuma hadi mlangoni.. nilikuwa nimefunga mlango kwa ndani,…ili nikifanya nikaufungua

Aliyekuwa kasimama mlangoni alikuwa alikuwa ni mwanamke mmoja akiwa kashika begi dogo, na nyuma yake yupo docta. Nilipomuangalai yule mwanamke nikajikuta kama nashikwa na kitu kama kizunguzungu na mara sura nyingi zikawa zinakua kichwani, na sauti nyingi sana, ilikuwa kama mtu kawekwa kwenye chumba cha giza ambacho kinakuja mwanga wa sura za watu, halafu makelele mengi…

Hi ile ikanitesa sana na kichwa kikawa kinauma kweli, nikashika kichwa na kuhangaika  nikawa kama nachanganyikiwa, nikashika kichwa na kuanza kulalamika kichwa changu , kichwa changu, huku nahangaika sana , na docta akaja karibu yangu na kuniambia nimeze dawa ya maumivu ya kichwa, lakini sikumuuelewa. Na sikutaka kumsikiliza..kwani sauti yake ilikuwa kama kero fulani inapaa kama mwangi, nikawa nimeshikilia kichwa nalia…

Yule mwanamke aliyeshika begi mkononi akawa anashangaa na kunionea huruma, akanisogelea, na kumuomba docta asogee pembeni, akanitizama usoni, na nikaona machozi yakimtoka …akatikisa kichwa na mara akainua mkono wake, na kunishika kichwani.

Ajabu ilioje, nilihisi ubaridi ukiniingia mwilini, nilihisi kitu fulani kikisafaisha yale mahangaiko na makelele kwenye ubongo wangu , maumivu yote yakapotea…na mwili ukawa kama unaingiwa na ubaridi na hisia kutoka kichwani taratbu ukashuka hadi miguuni..

Ilikuwa ni maajabu, nikainua kichwa kumtizama yule mwanamke na mkono wake ukiwa bado kichwani mwangu…na mara kumbukumbu zikaanza kunijia kwa  mbali, nikawa nakumbuka kitu,…nikawa nayaona maisha yaliyopita kama vile mtu anajitizama kitu kwenye runinga….

NB: Mhh, kidole kinauma tusihie hapa kwa leo

WAZO LA LEO: Ugumu wa maisha ,mawazo,  matatizo, shida fedheha, vinaweza kumtuma mtu kufanya jambo ambalo hata hakulikusudia,…wengine hukimbilia kulewa, lakini je itasaidia,…. muhimu ukijiona upo kwenye hali hii mkumbuke mola wako, kumbuka kuwa kuna watu walipata matatizo zaidi yako kumbuke wale waliopo chini yako,…kuna watu wasio na uwezo kabisa,..lakini bado wanaishi, wana furaha, na wanafanya hayo kwa sababu gani,kwasababu wamemuweka mungu mbele wakijua kuwa mungu ndiye mjuzi wa hayo yote,kwake yeye yote yanawezekana.


Ni mimi: emu-three