KILA MCHUMA JANGA.....
'Mwiziii, mwizi...'ni kelele za
asubuh, asubuh....haikupita muda, tukaona moto. Ulikuwa moto mkali na mlio wa
kitu kama kinapasuka ukasikika...
Awali tulijua ni ajali...kwa haraka
mimi nikajongea japo sio karibu na kwenye tukioa...nikaona watu wakimbeba mama
mmoja...
‘Vipi ni ajali ya moto...?’ nikauliza
‘Hapana, ni mwizi...’akasema jamaa
mmoja akikimbia mbali na eneo la tukio, sikupenda hili tukio linipite,
mwizi..halafu moto, akilini nikahisi vinginevyo, lakini mwizi ..adhabu yake iwe
hiyo, akili haikunipa amani, nikazidi kusogea, na watu wakawa wanakimbia
..nikajua huenda ni polisi, nikasimama, na bahati nzuri wakatokea watu wengine
walikuwa hawana hawakimbii
‘Vipi moto wa nini ule...?’ nikauliza..
'Ni adhabu ya moto, hao watu dawa yao
ni kuwachoma moto tu..'akasema shuhuda mmoja.
'Mumemchoma moto kibaka!' Mzee mmoja
akang'aka huyu alikuwa miongoni mwa hao watu, lakini alionekana na huzuni kubwa
usono
'Ndio....nyie wazee ndio mnatufugia
wezi,...’akasema shuhuda
‘Lakini sio kwa adhabu hiyo, mnaona Yule
mama yake alivyopoteza fahamu, mimi namfahamu sana Yule mama, mimi namfahamu
sana huyu kijana ..mareh-hemu...’huyu mzee akasema sasa kwa uchungu.
‘Mzee, na bado..hata Yule kijana
wako..siku zake zinahesabiwa,....hawa watu wanatusumbua sana , tunafanya kazi,
tunaumia huku na kule, hawa, vibaka, watoto wa hawa wazee...wanatuibia, leo zaa
arubaini zake zimefika,.hiyo ndio adhabu yao...' akasema mtu mwingine.
‘Sawa...nyie hamjui tu..sisi wazee,
tumejichokea, twawategemea nyie...sasa kama mnaiba sisi hatujui
tufanyeje...eeh, sikizliza niwaambie..yule mama, ni mama mjane, na Yule mtoto alikuwa
mtoto wake pekee...yule mama ana maradhi mabaya sana, dawa zake ni aghali
kupundikia,..na mtoto wake alimuahidi mama yake, atamuhudumia ,,mpaka mwisho..’akasema
mzee
‘Ndio atuibie...’akasema Yule shuhuda.
‘Sikiliza sasa nikuambie, ulisikia Yule
mama kabla ya kupoteza fahamu , baada ya kushuhudia mtoto wake akiteketea na
moto alisemaje...’ni kosa langu, ni kosa la maradhi yangu..sasa nitaishije, na
mimi nichomeni moto...ndio akapoteza fahamu..mnafahamu fumbo hilo..nawaambia
ukweli...kwa hili hamtaishia kwema, ...’akasema huyo mzee
‘Mtatuloga eeh, ndio mnafikiria
hivyo, mzee, nakuambia hili na usikie....hamtuwezi mzee, sisi tunalindwa na
damu.....’sikusikia alichoendelea kuongea, mimi akili ilishazama kuwazia, kauli
ya huyo mzee...
‘...yule mama, ni mama
mjane, na Yule mtoto alikuwa mtoto wake pekee...yule mama ana maradhi mabaya
sana, dawa zake ni aghali kupundikia,..na mtoto wake alimuahidi mama yake,
atamuhudumia ,,mpaka mwisho..’
Nikapanga nije kuongea na huyo mzee, nikisikie kisa kamili cha huyo mama
mjane...
Leo asubuhi hii...., eneo la relini,
huko Kipunguni... wakati tunapita tukashuhudia moto ukiwaka, kuulizia,
tukaambiwa ni mwizi wa bajaji anachomwa moto....!
‘Mhh..mwezi tena, na adhabu yake ni
kuchomwa moto ....hivi kweli mwizi
adhabu yake ni kuchomwa moto, nikauliza wenzangu, na mjadala ukazuka.....sitapenda
kuuandika huo mjadala hapa, jadilini na
wenzeko uko mlipo,...
Ni kweli huyo mwizi anayechomwa moto akawa ni jambazi kweli na kiukweli..., jambazi
ni muuaji, anaiba hata kuua, huyu, kwa vile anaua, ilitakiwa naye auwawe...hata
hivyo, jambazi akifikishwa jela...kuna sheria za haki za binadamu, zinawatetea,
kuwa muuaji asiuwawe...hapa sasa naona ajabu, kibaka anachomwa moto!
'Jambazi alianiza huko kwenye
ukibaka..tunatakiwa tumuwahi mapema, kwa kumchoma moto...’nikakumbuka kauli ya Yule
shuhuda.
.
‘ Hii sasa ndio adhabu ya wezi,...’alisema
mwingine, swali nikamuuliza, je wewe hujawahi kuiba, ofisini kwako kila siku
unamuibia muajiri wako,...nawewe dereva wa bajaji, kila siku mnawadhulumu
abiria, ...
‘Lakini sisi tunaiba kiujanga...’wakajitetea
Huko tupaache....
Tujiulize swali moja, ni kwanini raia wanachukua
sheria mikononi mwao..na hili kosa la wezi, wavunja sheria, ni kosa la nani, ni
nani alaumiwe...
Raia wanajitetea kuwa wameamua kufanya
hivyo kujichukulia sheria mikononi mwao, eti..wezi hao wakikamatwa, wakipelekwa
vituoni, kesho yake wapo mitaani,..hata jambazi katetewa na haki za binadamu,
karudi mitaani tena ..sasa ni ni jamabazi sugu , mwaliwa wa majambazi... je
hili ni Kosa ni la nani...!
Kuna wakati tuliandika habari za
majirani kugombana, kisa ni mtoto... !
Mtoto kadokoa kitu cha jirani, mzazi
jirani akamuadhibu huyo mtoto mdokozi, mama wa mtoto mdokozi akaja juu, kwanini
mwanae kachapwa, ikawa kesi, maana kesi ya mtoto, iliwafanya wazazi wa pande
mbili kuingilia kati na kuanza kugombana...hili ni janga..tumelianza
wenyewe..sijui mnanielewa hapa...
Tatizo huanzia hapa, tunalichuma
janga sis wenyewe na kuliingiza majumbani kwetu...janga hili limeanzia kwenye
malezi ya watoto, hakuna elimu ya dini, ilitakiwa shule za watoto wadogo ziwe
za kidini, iwe ni sheria, watoto chini ya miaka saba, kwanza wapiti shule za
kidini..tutengeze kizazi cha waumini wa kweli..dini mnazipiga vita mnategemea
nini...majanga tunayapanga sisi wenyewe.
.
Jukumu la ulezi wa watoto huanzia kwa
mzazi, sawa..jirani ni mzazi, sawa, je jirani yupo tayari mtoto wake aadhibiwe
na mzazi mwimngine..hilo hatupendi..serikali, nayo vipi,...kwanini mnataka
shule za watoto za kufundidhs lugha za kigeni,lakini swala la dini, la
kuwajenga watoto kiimani hamlipi kipaumbele..eti mnaogopa imani kali..haya
tuone,...kama mtu hamuogopi mungu wake ataogopa kuiba,na kuiba, sio lazima
bajaji,..hao walanguzi,wezi wa mali ya umma, wao sio wezi kwanini hawachomwi
moto, tusipolitambua hili, tutakuwa tunajenga janga...!
Nawausia enyi wenzangu, yapo mengi
tunayapuuzia, vizazi sasa vinaharibika, tuanze sasa kuchukua tahadhari...elimu
ya dini inahitajika sana..tena sana, ...elimu sio lugha tu, lakini kuna elimu
muhimu ya IMANI..ya kumuogopa Yule muumbaji wetu, ili mtu aaogope kuiba hata
akiwa peke yake, tusipolitambua hili, basi tutarajie kuzalisha wezi, mabaradhulu,
mashoga..wavuta unga...nk...na amani itakuwa ni msamiati adimu. Wahenga
walisemaje, Kila mchuma janga..., itakuwaje vile...
Ni mimi:
emu-three
No comments :
Post a Comment