Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Wednesday, August 19, 2026

KILA KITU 'AI...' hakuna kufikiria...

KILA KITU SASA MPAKA TUMUULIZE NANI VILE.... ‘.AI’

Nikiwa nakatisha mitaa ya Dar, niliona jinsi jiji linavyobadilika kwa haraka, nahisi mtu aliyesafiri miaka mitano nyuma akifika kwenye jiji hili atashangaa sana.

Kuna sehemu zenye majina ya asili, nimekuwa nikijitahid sana kupita pita maeneo hayo nione jinsi gani kulivyo kwa hivi sasa, nikajiwa na mawazo..

1: Mnazi mmoja ni jina maarufu, bila hata kuuliza hapo awali kulikuwa na mnazi mmoja mrefu sana...sijui kama ulikuwa peke yake...kwangu mimi ningelipendekeza, kwa historia ya vizazi vijavyo, basi kuwe na mnazi...ama wa kupanda, au utengenezwa mnazi mmoja, ...japo naona kuna alama ya mwenge wa uhuru....au jina libadilike liitwe, mwenye wa uhuru....

Ni mawazo tu...

Huku mjini kuna sehemu kama clock tower, kuna mnara wa simu, kwanini usiboreshwe, ukawa mrefu na simu kubwa yenye kuonekana kwa mbali.

Kama sikosei, maana niliwahi kufika Ujerumani kipindi fulani, nikaona jinsi gani wanavyoboresha mandhari yao ya zamani, iwe kama kipindi hicho...

Kipindi nafika walikuwa wakiboresha majengo ya zamani, yaonekane kama ilivyokuwa, sijajua lile kanisa lilibomolewa kwa mabomu kama wameshaliboresha,....

Na zaidi ya hayo kwenye treni zao, kuna watangazaji wanaelezea maeneo na historia zake,

Nilivutika sana na wenzetu..

Mbona hata sisi tunaweza

Mwendo kasi huoo...ni ubunifu mnzuri.., unafanya kazi zake,...tunahitaji na treni pia za kutoka mjini hadi nje ya jiji...na humoo....eeh, kuwe na watangazaji wa kelezea maeneo,

‘Hapa ni...eneo fulani, kwa maarufu kunaitwa kadhaa....asili ya jina hilo limetokana na kadhaa..eeh....watu wanavutika, hasa watalii....’

Jamani sio kila kitu tukione kwa wenzetu ndio tujifunze, watu wa kumbukumbu mpo wapi, wanahistoria, wajenzi, wakufunzi mpo wapi jamani...au ndio tunasubiria tuwe tunamuuliza AI....

Kwangu mimi, elimu kichwani mwa watu inashuka,...usomaji wa vitabu unashuka...hii ina maana gani...

Tutafakari tusije tukaingia kwenye mtego wa kutawaliwa ‘KIFIKIRA’...tukawa watu wa ...kufikirishwa,

Kila jambo, Tugoogle, tumtafute AI...ni maendeleo ndio , lakini akili za wengi zitalala....watu hawatahangaika kusoma, ....sijui mnanielewa!

Ni hayo tu kwa leo kwenye diary yangu....

Ni mimi: emu-three

No comments :