Ni wakati nipo msibani macho yangu, yalitua
kwa mtoto mmoja aliyekuwa akilia sana, cha ajabu kilichonishangaza mimi, hakuna hata mtu mmoja aliyemjali, …nilijiuliza
ni kwanini, kiukweli hali yake hasa kimavazi haikuonekana njema, nguo zilikuwa
chafu, na kuukuu. Hata hali yake ya kiafya yaonekana ni dhoofu…lakini naye ni
muombolezaji, naye ana uchungu,….na…
Nahisi huo msiba
umemgusa,…na sijui….
Nikageuka
huku na kule, nikiwaangalia watu wengine,
watu hapo kwa ujumla walikuwa
kwenye majonzi makubwa, wengi walikuwa
wakilia, wengine wakionyesha nyuso za huzuni,…ilimradi kila mmoja alikuwa
kaguzwa na huo, masiba.
Kuna
wengine walilia hadi kupoteza fahamu…na watu kama hao, walikuwa na jamaa zao wa
akaribu wa kuwaliwaza,..lakini huyu …mtoto, niliyemuona awali, hana…hana hata
wa kumkaribia, kila aliyemuona alimtupia jicho moja, na kujifanya hajamuona…,
swali akilini mwangu likawa linajiuliza, ni sawa, wengi wameguswa na msiba huo,
hata kama sio ndugu wa karibu wa marehemu kivile…na wengi wanalia,…je huyu naye
analia kwasababu gani…ni ndugu wa karibu,….au ….
Hamasa ya
kufahamu zaidi ikanivuta….
Nikaamua
kufanya jambo, …hata hivyo, awali haikuwa rahisi,..maana kulikuwa na watu wengi
mbele yangu na kwa wingi wa watu,
nisingeliweza kuwapita kwa urahisi,
nafasi ilikuwa ndogo, ukiondoka sehemu mwingine anakuja kukaa…aah, hata hivyo,
hamasa ilizidi…
Niligeuka
kumuangalia tena,….bado alikuwa akilia, …tena kwa kwa huzuni kubwa,…hata mimi,
pale nilipo, nikavutwa na hisia za kulia,….
Msiba
unauma jamani….
Kiukweli
msiba unauma…na unauma zaidi kutegemeana na mtu huyo alikuwaje mbele ya jamii, na
zaidi kutegemeana na waombolezaji , na je kaacha nini nyuma yake,…watoto, mke
au jamaa waliokuwa wakimtegemea, na zaidi ….hata waombolezaji wenyewe, au wana
habari, wanaweza kumfanya kila mtu aliyehudhuria msiba huo aweze kulia….
Kwa jinsi ilivyo, huyu marehemu, alikuwa mtu aliyegusa watu, kimatendo,
kitabia,…ndio maana wengi walifika
kumsindikiza kwenye safari yake
ya mwisho, ambayo ndio safari ya kila mwanadamu, …kwakwe tumetoka, na kwake
ndio marejea yetu…
Nilisia
mshehereshaji akiongea mambo mazuri ya marehemu…
Kwa vyovyote
iwavyo, mtu akifariki, yatubidi tumuongelee kwa mambo mazuri, maana hayo mambo
yake mema, ndiyo taa ya mja huyo huo
endapo,…tukiyaongea, taa hii huzi kuwaka,, kamwe tusipende kuongelea mambo
yasiyo mema, hata kama aliyafanya, ili tusififishe mwanga wa taa yake..hayo ni
maneno mazuri niliyoyakumbuka kutoka kwa
watu wa imani.
Akili yangu
ikarejea kwa yule mtoto…ni…kijana, ni kijana wa takiribani, miaka kumi na mbili
hivi…….nikaamua kumsogelea, hadi pale alipochuchumaa, pembeni yake kulikuwa na
mfuko wa Rambo, na ndani yake kulionekana nguo nguo hivi….kwa muda ule yule
kijana, alikuwa kachuchumaa, naona sasa miguu imemuisha nguvu…hawezi kusimama
tena, na bado hakuna mtu aliyemjali..
Hakuna hata
aliyepoteza muda kumuangalia tena…, wengi walitekwa na matendo yanayoendelea
mbele ya jukwaa…watu wanavyoomiongelea marehemu…na mengineyo.
Mimi
nikamsogelea yule mtoto….
‘Pole
kijana…pole sana..yote ni kwa mapenzi ya mungu, …’nikasema nikimsogelea na
kumshika begani.
Yule mtoto,
..ni kijana akainua uso na kuniangalia, uso ulikuwa umefunikwa na
machozi….akatikisa kichwa…kama kusikitika. Akavuta pumzi, haalfu akasema;
‘Ni kweli
yote ni kwa mapenzi ya mungu, lakini kwangu, …..kwa-kwa…ngu, ime-ime….kuwa ni….mengine
yanauma kaka yangu,sijui nikuite kaka yangu, au baba, hata sikujui…..sijui
niseme nini…inaniuma kwa-kwa –kwa -kwe….’akasema. akishindwa kumalizia maneno.
‘Kwa muda
huu, hakuna cha kusema iliyobaki ni kumshukuru mungu, kwani yeye ndiye mwenye
mamlaka ya haya yote…, kwake tumetoka na kwake ndio marejeo yetu, ndio kauli
sahihi,..’nikasema
‘Ni
sawa…lakini mwenyewe si umeona..mimi kama mimi nitakuwa mgeni wa nani,…nimetoka
mbali nikijua nimeshafika kwa…..lakini sasa,..ooh,.. ‘akaanza kulia.
‘Umetokea
wapi…?’ nikamuuliza.
‘Yaani,..nilijua,…nikifika
nitamkuta…nitaongea naye, nita…..sasa nakutana na haya….niende wapi mie…’akasema.
‘Oh, ina
maana…’nikatakla kuongea kuhusu hisia zangu, lakini yeye akaendelea kuongea.
‘Hebu
niangalie…mimi kama mimi nitamuendea nani sasa , hebu niambie kaka yangu…ni
nani atakayeniamini, mtoto wa majalalani…niangalia nilivyo, ni nani, ata……kwa
hivi sasa sina mama, na sasa sina….ooh…’akaanza kulia,…kiukweli hata mimi
nikalia.
Baadae
nikamwambia…
‘Oh..usijali
yote ni mapenzi ya mungu, yey e ndiye atajua uta…’hapo sikuweza kuendelea yule mtoto,
au yule kijana akalala chini, na
kunyooka,…alionekana kupoteza fahamu.
Hapo sasa
baadhi ya watu wakafika na kuanza kumsaidia.
‘Huyu ni
nani…?’ akauliza mmoja wa jamaa aliyefika pale.
‘Mhh..hata
simjui…’akasema mwingine
‘Sio jamaa
au mtoto wa marehemu…’nikasema
‘Hapana,….mtoto
wa marehemu awe hivi..wewe vipi bwana….’akasema jamaa aliyeonekana kuwa ni mtu
au jamaa wa marehemu.
‘Lakini…..’nikataka
kuyarudia yale maneno ya yule mtoto, lakini huyo aliyesema…hapana, akiwa na
uhaklika kuwa huyo mtoto sio jamaa ya marehemu akaondoka, .
Kwa muda
ule huduma za kwanza za huyo mtoto zilikuwa zikiendelea, baadae akazindukana,
na alichosema kwa haraka,,,
‘Najua
hawataniamini, ..najua…kwa vile mimi sasa ni yatima, lakini, nasema hivi…haya
ni kizalia,, leo kwangu kesho itakuwa kwa mwingine…’aliposema maneno hayo, akapoteza
fahamu tena.
WAZO LA LEO: Diary yangu, inatoa pole kwa msiba wa mpendwa
wa wengi, …RIP Ruge, ..hatuna cha kuongeza, zaidi ya kukuombea makazi mema
peponi, na kuwaombea wazazi na ndugu subira njema, …kwani yote hayo ni kwa mapenzi
ya mola.
Ni mimi:
emu-three
No comments :
Post a Comment