Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha
Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..
Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.
MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.
TUPO PAMOJA DAIMA
Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;
https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:
https://www.facebook.com/diaryyangu/
`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;
Friday, June 4, 2010
Changamoto kwa viongozi
Pembeni yangu alisimama baba mmoja akiwa kamshikilia mwanae mkono, naye alikuwa katika harakati za kutafuta usafiri. Lile basi la wanafunzi lilipopita yule mtoto aliliangalia sana, na mwishowe akamwangalia baba yake. Baba yake kwa muda alikuwa akimvuta mkono ili wasogee kwenye upenyo watakaoweza kuvuka barabara. Alishangaa akimvuta mtoto wake alikuwa hasogei, alimpomwangalia akamuona analiangalia lile basi, naye akavutika kuliangalia vizuri. Akainamisha kichwa kumwangalia mwanae, na macho yao yakakutana.
Je unafikiri walikuwa wakiwaza nini?
Mimi nikakumbuka tukio moja lililotokea siku za nyuma, baba kama huyu aliwashikilia watoto wake wawili, mmoja alikuwa mdogo wa shule ya msingi au chekechea na wa pili alikuwa wa kidato cha kwanza. Walikuwa katika harakatii za kuvuka barabara, na baba alihakikisha amewashikilia watoto wote wawili mkono, tatizo kwa muda ule madaladala yalikuwa yakisimama ovyo, kwahiyo kwa upande mwingine wa barabara itokayo Gongolamboto ulikuwa huoni gari linalokuja vyema, kwa kukwa kulikwa na basi lililokuwa linapakia abiria.
Baba mtu, akasogea kidogo mbele, na yule mtoto mkubwa akaangalia huku na kule akaona kuna upenyo wa yeye kuvuka, kumbe kuna gari linalotoka Gongolamboto kwa kasi, likatanua barabara na kuingia upande ule waliposimama watu wakisubiri magari, na kwa muda huo yule kijana wa yule baba alikuwa keshasogea hatua moja mbele ya baba yake ambaye alishamuachia mkono akijua hakuna hatari. IIlikuwa ni ajali ya kusikitisha sana, kwani lile gari lililokuwa likija kasi lilimgonga yula kija na kumkosakosa yule baba na mtoto wake mdogo. Yue kijana alifariki hapohapo.
Kila mmoja aliyekuwepo hapo alisikitika na wengine kutoa machozi. Jaribu kulifikiria hili tukio mwenyewe akilini! Huyu yupo na mzazi wake, je wale wanaokwenda wenyewe shuleni wakiwa hawana hata mzazi wa kuwasindikiza inakuwaje?
Ninachotaka kusema hapa ni zile ahadi za magari ya wanafunzi, je ilikuwa lugha ya kampeni au yanakuja lini? Je hii adha ya usafiri hasa kwa watoto wetu itaisha lini? Na kwanini vituo haviwekwi kiusalama zaidi mabasi yawe yanaingia kituoni na kutoka kuliko ile hali ya mabasi kusimama juu kwa juu, katikati ya barabara huku watu wakikoswakoswa na mabasi mengine? Tunaona ajali kila siku, ni mmoja mmoja lakini kwa mwaka wanakuwa wangapi?
Sijui lakini mimi nahisi kuna haja ya kutungwa kwa sheria kuwa viongozi wakitoa ahadi kwenye kampeni na isipotimizwa waweze kushitakiwa! Hili litakuwa changamoto kwa viongozi wetu au nyie mnasemaje?
.
Hilo ndio wazo langu la leo
From miram3
1 comment :
Duu hiyo barabara ya wapi vile, eehe, kutoka Mombasa kwenda kwa Diwani, au Moshi bar, hutaithamini kuwa ni barabara iliyopo Dar, hivi Mbunge wenu ni nani. Na kule hakuna nauli ya serikali, inaanzia mia tatu siku, mia tano, au bodaboda elifu moja na nusu...mtakoma ubishi nani kawaambia muishi huko. Basi hata umeme ni mgawo kila ikifika saa moja au saa mbili usiku taaa! Giza totorooo
Post a Comment