Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha
Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..
Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.
MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.
TUPO PAMOJA DAIMA
Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;
https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:
https://www.facebook.com/diaryyangu/
`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;
Monday, June 7, 2010
Kaamuka vipi!
'Nimefurahi kupata kazi, lakini jinsi nilivyotegemea inakuwa kinyume, sio sababu ya mshahara, hapana, ni yale mazingira ya kazi. Mimi ni mgeni, na sina uzoefu wa kazi , ina maana ninachokijua sana ni kile nilichofundishwa chuoni, kwahiyo nilihitaji msaada wa wazoefu, ili niweze kuunganisha na elimu yangu na kufanya kitu bora. Lakini imekuwa ngumu, kiasi kwamba najiona kama sijasoma vile. Fikiria ukihitaji taarifa ndogo tu kwa muhudumu au mtu yoyote anayehusika, huwezi kupewa kirahisi, utazungushwa, mara utaambiwa subiri nina kazi, mara nenda kamuulize mtu fulani, kwahiyo wewe unakuwa mtu wa kuzungushwazungushwa kama `pia' mwisho wa siku hujui hata umefanaya nini...' akawa analalamika kijana wetu.
'Kila jambo jipya lina ugumu wake, na ugumu huo unaweza ukawa msaada kwako baadaye, kuliko ungekuta kila kitu kipo wazi, ungejifunzaje..' nikamwambia kumpa matumaini.
'Kama ni hivyo hatutaendela, manake kila ukifika mahali unakuwa kama unaanzisha wewe. Ninasema hivyo sio kwasababu sioni umuhimu wa kujifunza kila kitu, lakini ule masaada wa kukipata unakuwa shida na huupati kwa muda muafaka. Huyo aliyekuwa akizifanya hizo kazi nilizokabidhiwa hakuacha maelezo kuwa hiki kipo wapi na kwanini hiki kilifanyika vile. Utakuta hata kwenye mtandao kaandika maelezo kiufupi, kiasi kwamba kuelewa wewe mgeni mpaka upate maelezo ya mtu mwingine aliyehusika kwasababu mtendaji hayupo, na huyo utakayemuuliza inategemea kaamuka vipi. Mwingine amekuja na visirani vyake toka nyumbani, ukimuuliza anakupandishia, utasikia, wewe sasa umesoma nin, nyie vijana wa siku hizi bure kabisa. Kiasi kwamba unaona kazi ni ngumu kuliko maelzo, kitu ambacho sio kweli...' akazidi kunielezea.
Ni kweli hayo aliyoelezea bwana mdogo tumeyakuta sehemu nyingi. Watu wengine hawana tabia ya kuweka kumbukumbu zao vyema, kiasi kwamba akiondoka inakuwa vigumu kwa mwingine kugundua nini mwenzake alifanya. Huenda wengine wanafanya hivyo kiuchoyo, au kwa-kutokujua na wengine wanasema kabisa, siwezi kuumia ili mwenzangu akija apate ubwete. Hiyo sio sawa, na hii ni kutojua jukumu lako la kazi. Mtaalamu mwema ni yule anayefanya kitu kibakie historia njema kwa wengine, kiasi kwamba akija mwingine anabakia kumsifia aliyepita, kwasababu hapati ugumu wa kuendeleza pale mwenzake alipoishia.
Kama tutafanya kazi kwa jinsi ulivyomuka, jinsi ulivyotoka nyumbani kwako basi hiyoo itakuwa kazi isiyo na ufanisi. Ni vyema ya nyumbani yakabakia huko huko, na ukifika ofisini ujue kazi ni moja ya kufanikisha kile ulichokabidhiwa kama dhamana.
Wakati mwingine ni vigumu sana, najua hayo kiuzoefu lakini watu wa hekima wanasema kazi njema huanzia nyumbani, ni sawa, ina maana ukitoka nyumbani vyema, na kazini utafanya vyema, lakini kwa hali ya kimaisha yetu, huwezi ukaangunisha haya mawili, ukitaka kuyaunganisha haya mawili utakuwa kila siku unafanya vibaya. Vipato ni vidogo, havilingani na hali halisi ya kimaisha, na wengi wanatoka majumbani wakiwa na mihangaiko ya akili ya jinsi gani ya kuziba viraka vya tofauti ya ugumu wa misha na kipato kisichokuwepo. Sasa haya ukiyaleta kazini, ndio huko vijana wetu wanasema `inategemea umuulizaye kaamuka vipi.'
Vyovyote utakavyoamuka, ujue kazi ni dhamana, na dhamana ni deni, timiza wajibu ipo siku utaona tija yake!
From miram3
1 comment :
Lakini hiyo ni kweli, inamtokea kila mtu. Ipo siku unaamuka hutaki hata kuongea na mtu, na ukichangia na hali mbaya ya uchumi, we-acha tu
Post a Comment