Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary', na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..pia tunakaribisha mijadala na yale yote unayopenda yawemo humu. Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu. SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthreeFriday, March 11, 2011

Sema, useme, usiseme, itakuwa...!


‘Nauli zimepanda hamjui , kawaulizeni Sumatra..’ ilikuwa kauli ya dharau na ya kebehi kutoka kwa kondacta, huku akiwa kamkazia macho mama mmoja ambaye alikuwa kambeba mtoto wake. Yule mama ilivyoonekana alikuwa akimpeleka mtoto wake hospitali ya Msasani ya CCBRT. Alipapasa kwenye mkoba wake akitafuta hela ya ziada anayodaiwa, lakini ilionekana hata angetafuta siku nzima asingeipata.


‘Mwanangu sina hela nyingine ya kukuongezea, na hata wakati wa kurudi sijui nitarudije, nampeleka mtoto hospitalini, na huko siajua gharama yakeitakuwaje, sasa mnaniambia kuwa nauli zimepanda.., kwasababu, nilikuwa sijui kama nauli zimepanda…’ akajitetea yule mama.

‘We mama usilete dharau kwenye kazi za watu, matangazo kila siku kwenye taarifa za habari, magazetini , vipeperushi, watu wanaongea mabarabarani, hata maandamano wamefanya kupinga, …eti wanapinga nauli sizipande, ..mbona hampingi bei za vyakula zikipanda..nipe hela yangu mama unaniwekea kiwingu, kama huna nauli shuka…’ akasema kondacta huku akimkazia yule mama macho.

‘Hivi wewe kondacta huna Huruma, hapo imepungua shilingi ngapi tu, hiyo hamsini au mia inakutoa ubinadamu, je hiyo hela uliyompa huyo mpiga debe hapo nje , kafanya nini cha zaidi, kapiga debe huku gari limejaa amefanya nini,… kumbe mnapata hela nyingi mpaka mnawapa hawo wavuta unga mabarabarani bila kazi yoyote,…kafanya nini hapo zaidi ya kusisimama hapo mlangoni akisema `Gongolamboto Msasani, hata sauti haisikiki,..’ akasema jamaa mmoja.

‘Kweli ukiangalia hela wanayodaiwa na tajiri wao kwa siku wanaipata na ziada, kama wasingeipata wasingekodisha `dei waka’, wasingewapa hawo wapiga debe, ambao wanapiga debe hata kama gari limejaa, na wanawalipa hela…’ akasema mama mmoja.

Mimi nilikajikuta nawaza mbali kuhusina jinsi gani maisha yatakavyokuwa kwani bidhaa madukani bei ni juu kwa juu, kila kukicha vitu vinapanda bei na hakuna wakuweza kuzuia, na vingina hata kutangazwa havitangazwi na wala havina tume ya kudhibitio bei kama ilivyo Sumatra. Tumetoka kupandishiwa umeme, umeme ambao kuupata ni kwa mgawo, hebu fikiria mtu umelipia LUKU! Umelipia kabla ya huduma, lakini umeme hupati, hela yako inatumika wakati huduma hujaipata, na unaipata hiyo huduma kwa msharti ya mgawo, hii kweli ni halali…

‘Wewe konda unamlaumu huyu mama kuwa hajasikia matangazo, wewe unafikiri kila mtu ana redio, au anaweza kununua gazeti…wengine hata kusafiri kwenda mjini ni mpaka itokee shida kubwa sana, kama huyo mama huoni anampeleka mtoto hospitali, hana jinsi inabidi asafiri…hela keshaipangia kuwa hii nauli , hii gharama ya matibabu, sasa anakutana na kupanda kwa nauli, ataipata wapi hela ya ziada…keshapangiwa na mumewe, akirudi atamuelezaje mumewe, kuwa nauli imepanda…’ akasema mama mwingine aliyekaa kiti cha nyuma.

‘Acheni kuniyeyusha nyie, hivi…niwaulize nani kapandisha nauli ,ni mimi au ni serikali yenu…mumeshindwaje kujitetea ilihali mlipewa miezi miwili ya kutoa maoni yenu, …nani aliyekwenda kuweka pingamizi, mnasubiri hatua imechukuliwa mnaleta longolongo…’ akasema dereva.

‘Wewe serikali ikishaamua imeamua hata kama tungeandamana, hata kama tungekutana na kujadili, bei walishapanga iwe hivyo, sidhani kama ingetokea mabadiliko. Mfano bei ya umeme, watu walikutana na kutoa maelezo mengi, lakini ilipofika siku ile waliyopanga bei itapanda , ikapanda…kwahiyo useme, usiseme, waliloamua wao litakuwa…sisi ni hatuna usemi, kauli yetu ni butu…kauli yetu ilikuwa siku ile ya uchaguzi, lakini hatukuitumia sasa cha moto tunakiona…’ akasema jamaa mmoja.

Na kweli cha moto tutakiona, kwani nani anayejua dhahama ya giza, kama ulikuwa umeweka umeme, huyo unayetaka akutetee, nyumbani kwake kuna generator…huyu unayetaka akutetee kuhus kupand kwa nauli ana gari lake, na huenda gharama ya petrol analipiwa, huyo anayetakiwa akutetee kuhusu bei za vitu haijui hata hiyo bei, kwani kila ikifika mwishoo wa mwezi ana posho…inayoitwa `meal allowance…huyo unayetaka akutete kwa hili, yeye keshapewa fungu maalumu kwa maina tofauti, mpaka fungu la starehe…eti wanaita `entertainment allowance’…mwisho wa wiki anapanga honeymoon akaifanyie wapi, kama sio Zanzibar ni mikumi

‘Sawa bwana, watunyanyase, tu, lakini …wote tutakutana huko Loliondo,...’ Jamaa mmoja akaamua kuchekesha watu. Na mazungumzo yakahama kutoka kwenye nauli kwenda kwenye habari iliyopewa kipaumbele ya Loliondo.

Kwa ujumla hali ya maisha ya Mtanzania hasa wa kima cha chini, hasa mtu wa kawaida ambaye kazi yake ni kubangaiza hapa na pale, hasa mkulima ambaye nguvu zake zote zinategemea jembe la mkononi, hasa akina mama ambao kila kukicha wanahangaika na ndoo mkononi kutafuta maji, kutafuta kuni, kutafuta chochote ili watoto wasilie njaa, ili watoto waende choo…je nani atajua haya kama watetezi wetu, na mabosi wetu maofisini hawajui wala kusikia njaa ipoje, giza lipoje, foleni ya magari na adha zake zipoje… sio rahisi kujua kwasababu maisha yao yamesharahisishwa, na siju mishahara ya wakubwa hawa siku hizi ni shilingi ngapi.

Labda tubakie kusema, kuwa vyovyote iwavyo, sote ni wanadamu tunatakiwa tuishi na tupate huduma zote za msingi, ikiwemo chakula, maji , malazi afya nk , sasa kama hivi vitu bei inakuwa juu zaidi ya kipato cha mtu huyu ataishije…sijui..najiuliza nakosa jibu!

Hili ndilo wazo la Ijumaa ya leo.

Ni mimi: emu-three

5 comments :

Anonymous said...

Mkuu Mzee Mzima(emu-three), sijui nimepatia maana nilikuwa najiuliza maana ya emu-three nikakosa ndio nikabuni nikuute hivi.
Kama unavyoona mapaka sasa hakuna aliyesema kitu, sio kwasababu haiwagusi, la-khasa, inawagusa na ujumbe wako ni sahii, lakini....wengi ndio hao...sasa watasema nini!
Labda niseme kuwa tumejitakiwa wenyewe, kura ilikuwa silaha, imeshindikana, sasa mwataka iweje...sipendi kutokee fujo, kwani watakaoumia ni wale wasio na makosa.
Nyakati zitasema, na watu wasikate tamaa, tupige kazi, mkokoteni sukuma mkokoteni wako, mkulima, lima mpaka uzimie, mfanyakazi ...hivyo hivyo, tutafika na tutafanikiwa...lakini kukitokea fuo na nchi kama hii, hali itazidi kuwa mbaya saaaana...naandika huku nasuuuza kidogo kinywaji...naondoa mawazo mkuu, au ukinywa huwezi kuandika, mbona mimi naandika!
kwaheri

SIMON KITURURU said...

Kila kitu lakini kina mwisho wake watu wakichoka vyakutosha!

Na angalau siku hizi watu wameanza kusema kwa kuwa kuna wakati watu walikuwa wanajikalia kimya tu!:-(

Ijumaa njema Mkuu!

emu-three said...

Na kweli muda utasema, sidhani kama nchi hii ina shida kiasi hicho.
Leo nimekutana na mzee mmoja, akaniambia kuwa unakumbuka kile kipindi wakati tunapiga foleni ya mkate wa siha, foleni ya sukari, ...ukiwa na sabuni ya kunikia unaitwa mlanguzi...sasa vitu vipo madukani bwerere, lakini pesa hakuna.
Kweli kila kitu na wakati wake.
Ijumaa njema na wewe mkuu!

John Maembe said...

Leo nimechelewa kidogo lakini nimewahi kwa7b mada ya Jumamosi bado kurushwa hewani.
Hili swala bwana ni la kwetu sote mambo ya mmoja kufaidi zaidi ya mwenzie umefikia mwisho, kwa jinsi ninavyofahamu mimi kama m2 unalalia godoro liwe la rafiki yako au nyumbani kwenu(sio lako) ilimradi hupati adha yoyote na wala hubugudhiwi na m2 kamwe hauwezi kuijua adha yake na hata ukielezwa adha yake huwezi kujali zaidi ya kujifanya unajali na licha ya hivyo huwezi kulinunu lako mwenyewe 7b husumbuliwi na m2.
Sasa mimi nasemaje wa2 washachoka kuonewa kila siku na mwisho umekaribia waendelee tu kula vinono lakini siku so nyingi kitanuka cha kunuka na hapo vigogo lazima wataiona Libya imehamia Tz, Mkuu M-3 hatuombi itokee lakini Punda ukimchapa sana ili akufikishie mzigo wako sijui kama utaenda nae sawa, kinachonisikitisha zaidi ni jinsi walivyozuia ghafla huduma ya Loliondo ikiwa wao wamekwisha kujitibia na huko so kusitisha ila ni mbinu tu ili mradi waanza kupewa viongozi & wa2 maarufu kwanza kisha ndo sisi tunafuata mi inaniuma sana; Wahenga walisema "SIKIO LA KUFA HALISIKII DAWA" So, hata km vp hawawezi kubadilika mpaka tuwaonyeshe kwamba sisi tushachoka na sera zao za kila ki2 kifanyiwe uchunguzi kwanza. Kwaheri Emu-3 jana sikuwa on air thus way.

emu-three said...

Ni kweli Mkuu Maembe, `sikio la kufa halisikii dawa..' watu wanalalamika wee, lakini wahusika wanajifanya kama hawasikii, kwasababu gani...sikio la kufa haliskii dawa...`muda utafika...' tu!
Shukurani J.Maembe, karinu sana