Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Friday, December 8, 2017

MKUKI KWA NGURUWE-37



'Kuna mambo muhimu sana, nataka kuongea na wewe....'

‘Kuhusu huyo wakili wa mume wako.....’

‘Huyu mtu ni hatari sana, kama tusipofanya haraka, utakuja kujijutia..’

‘Ndio kuna jingine mimi…, nimegundua mambo mengi sana juu yake, na sipendi niyaongelee hapa kwenye simu, tuonane sehemu tuongee tuone tutafanya nini, ni muhimu sana, kabla hujachelewa...’

Kisa kinaendelea....


************

Ilikuwa siku ya aina yake, maana foleni likuwa kila mahali, sikuweza kufika uwanja wa ndege, na sasa nimeamua kurudi ili nionane na huyo rafiki wa mume wangu, na foleni ikanifanya nichelewe hadi usiku ukaingia.

Lakini kwasababu ya kusikia ni kitu gani alichokigundua huyo docta, ikabidi nipitie kazini kwake, kwani bado alikuwa ofisini..nikafika kwenye hospitali yake, nikasimamisha gari langu kwenye eneo la maegesho ya mgari.

Hiyo ilikuwa hospitali yake ambayo anaifanyia kazi baada ya muda wa kazi, kuanzia saa kumi na mbili mpaka saa sita usiku…kwahiyo muda wote huo utakuwata wagonjwa wapo.

Niliingia ndani hadi mapokezi, niliangalia mlango wa kuingia kwenye ofisi ya huyo docta, nikawaona wapo wagonjwa wawili tu  wanasubiria kuonana naye. Nikaona nisubiria waishe hao wagonjwa, lakini walipoisha hao wakaongezeka wengine…

Nilitaka nimpigie simu kumuelezea kuwa nimeshafika, lakini nikaona nimpe muda, maana nitawadhulumu hao watu wenye shida ya kutibiwa, wao ni waginjwa wamefika kutibiwa, na mimi siumwi, japokuwa nina mambo muhimu na huyo docta, ....

Na niwakati natafakari hayo, mara mlango wa ile ofisi yake ukafunguliwa, na yeye akatoka, na kuangalia sehemu mapokezi, ambapo, nilikuwa bado nimesimama, inaonyesha alikuwa keshajua kuwa nimeshafika. Akanionyeshea ishara ya tano, nikafahamu kuwa ananiambia nimpe dakika tano, na mimi nikatikisa kichwa kumkubalia,...

Nikasogea sehemu ya kupumzikia wageni, kuna masofa, nikachagua sehemu ya kukaa, ili niwe naone kule kwenye ofisi ya huyo mwenyeji wangu,nikawa naangalia runinga. Na baada ya dakika tano, nilimuona akitoka tena, na safari hii, alionekana akimuita mtu, nahisi alikuwa akimuita msaidizi wake, na huyo aliyeitwa alipofika,wakaongea naye kidogo.

Walipomaliza kuongea, nikamuona akija sehemu hiyo niliyokuwa nimekaa, na aliponikaribia, akanionyeshea ishara kwa mkono kuwa twende sehemu ambayo alihitajia tukaongee, ni kwenye chumba kingine.

‘Kwanini usingemalizana na mgonjwa wako kwanza...naona kuna watu wawili tu pale wamebakia, ila kila wakiisha wawili wanakuja wengine, pole na majukumu, hivi unapumzika saa ngapi..?’ nikamuuliza.

‘Wale sio wagonjwa, wale ni vijana wangu wamekuja kunipa taarifa mbalimbali, hawana haraka, wanaweza kunisubiria tu..’akasema,

‘Vijana wako, wewe unafanya kazi ngapi…?’ nikamuuliza

‘Hahaha, ushaanza kunichimba, ..unakumbuka nilikuambia wakati nasoma nilipendelea sana kuwa mpelelezi, lakini udakitari ukazidi nguvu ile ndoto yangu y utotoni, kwahiyo chini kwa chini nimekuwa nikijifunza mwenyewe mambo ya upelelezi kupitia mitandao kwa kujifurahisha tu…’akasema akitabasamu

‘Ili uwachunguze watu, na ndoa zao au…’nikasema

‘Ikibidi kwa watu ninaowajali kama nyie..kama wewe…’akasema akinipiga piga mgongoni, nikawa nauzuia mkono wake.

Tukafika kwenye hicho chumba, na tulipoingia, akasimama kidogo, kama vile ananipisha, lakini, nikamuona akinisogelea, kama anataka kunikumbatia, na mimi nikamsukuma;

‘Jiheshimu, kumbuka nafasi yako na yangu pia....’nikasema.

‘Samahani, unajua tena, kuna mda nashindwa kujizuia,…hahaha, nisamehe tu mwenzako, nisije kuongeza madhara, maana siku hizi tuwe makini sana…hata hivyo nilitaka kukusalimia, ....kwani kusalimia kwa kukumbatiana kuna nia mbaya,....usiwe mshamba bwana....’akasema.

‘Sawa acha niwe mshamba, lakini nafahami ni kitu gani ninachokifanya, naheshimu ndoa yangu na wewe fanya hivyo hivyo...’nikasema.
‘Ni kweli samahani….’akasema huku sasa akiwa mbali na mimi.

 Tukaingia ndani, akanisogeza kiti, ili mimi nikae, na nilipokaa, yeye akatembea hadi  kwenye kiti kikubwa, ilikuwa ofisi yake, maalumu, kulikuwa na kila kitu muhimu cha ofisi, alipokaa akaniangalia moja kwa moja usoni, hapo tulitengenishwa na meza. Mimi sikujali huku kuniangalia kwake, nikatulia kama vile mgonjwa anavyosubiria kuhudumiwa na dakitari.

Nilisubiri kidogo, kumuachia nafasi hiyo ya kuniangalia, maana sijui alikuwa na maana gani, au ndio hulka hizo za wanaume…kwani alivyokuwa akifanya ni kama mtu anayemwangalia mpenzi wake, na hali kama hiyo sikuipenda, lakini kwa vile nilishamfahamu tabia yake, sikujali, ...nikatulia kimiya, na aliponiona nipo kimiya sicheki nimeangalia mbele, akasema;

‘Nimekuita hapa sio kama mgonjwa, na sio kama nimekuitia hapa kwa maswala ya masihara, ya uchumba wetu wa zilipendwa, ila siwezi kuficha nakupenda sana, japokuwa siwezi kufanya lolote kwa sasa….hahaha, usijali,…hayo tuyaache mimi nimekuita hapa kwa jambo muhimu sana zaidi ya hilo..’akasema.

‘Mhh,...niambie, najua usingelipoteza muda wako kuniita..’ nikasema;

‘Kutokana na vyanzo vyangu vya habari, unafahamu ukiwa katika hali kama hii yetu ya kujiajiri, hasa ukawa na miradi yenye wateja wengi , na maadui wengi kibiashara, ni lazima pia uwe na vyanzo vyako vya kukupatia taarifa muhimu, naomba unielewe hivyo tu, mimi siwezi kukuficha kuwa nasubiria tu wateja, wakati mwingine inabidi uhangaike kama hivyo, kujua wenzako wanavyofanya..’akasema

‘Sawa nakuelewa, kila mtu anafanya hivyo, kwa masilahi ya biashara yake…’nikasema

‘Sawa kabisa, tuachane na mimi,..nataka kuongelea kuhusu wewe…’akasema

‘Nimefanya nini tena…’nikasema

‘Ni hivi, usione kama ni kwanini, kiukweli, sio siri nimekuwa nikifuatilia ndoa yenu hatua kwa hatua, sio kwa nia mbaya, bali kwa ajili ya kukulinda wewe, hujui tu..hili nimeshakuambia mara nyingi, …’akasema

‘Pole sana…’nikasema

‘Sasa… siku ile nilipoona mume wako yupo na huyo wakili, nikaingiwa na mashaka, sio kwa vile sikuamini wewe…lakini huyu mtu,…nimeshasikia tetesi zake na sikutarajia kuwa atakuja kuingia kwenye anga zangu….’akasema

‘Ndio hajaingilia biashara zangu au maisha yangu, lakini yule anayekugusa wewe kanigusa mimi..sisemi kinafiki, ila kutoka moyoni, na wazazi wako wanalifahamu hilo, kuwa  mimi ndiye mlinzi wako,..tuliache hilo hivyo.

Mimi huyo mtu, nimesikia sifa zake nyingi,..mbaya na nzuri, mimi awali sikulichukulia hilo maanani, kwasababu sikuwa na sababu yoyote na mtu huyo...kabisa kabisa….’akasema.

‘Sawa ..naogopa kukatali, lakini naomba yasiwe ya kujirudia rudia endelea...’nikasema.

‘Nafahamu una kazi nyingi sana, nafahamu angelikuwepo yule rafiki yako yupo hili  ungelimtumia yeye, na mimi nisngelikuwa na nafasi hii tena, kwa vile hayupo basi mimi  nikaona nikusaidie kwa hili, na kwa vile rafiki sasa kakugeuka, hilo utakuja kuligundua mwenyewe baadae , sio sasa, sasa hivi nataka kukuweka wazi ni kwanini nimekuwa nikikufuatilia hivyo…’akasema na mimi hapo sikusema kitu.

‘Pole sana na foleni, ya kutoka uwanja wa ndege, natumai ulikwenda kuonana na rafiki yako, na nashukuru hukuweza kuonana naye , vinginevyo mtego uliotayarishwa, ungekunasa, na sijui ni nini kingelitokea baada ya hapo..’akasema.

‘Umefahamu vipi kuwa nilikwenda huko kumfuatilia huyo rafiki yangu, mbona unapenda kunifuatilia sana nyendo zangu, unanitafutia nini wewe ?’ nikamuuliza.

‘Nimeshakuamba kuwa mimi nina vyanzo vyangu vya kunipatia taarifa kama nina umuhimu na jambo fulani, na kufuatilia nyendo zako ni kwa ajili ya kuhakikishia usalama wako, na nitahakikisha nafanya hivyo,utake usitake, kwani niliahidi mbele ya wazazi wako, na kwako pia, kuwa nitafanya hivyo, ...’akasema

‘Yatakushinda,  wewe niambie ulichoniitia masaa yamekwenda sana , unajua nimechelewa kufika nyumbani, kama mume wangu angelikuwepo nyumbani, ningekuwa na kesi ya kujibu…lakini hata kama hayupo nyumbani isiwe ndio ababu ya kuvunja miiko ya ndoa, sitakiwi nifanye mambo ya kunivunjia heshima yangu, unanielewa hapo…’nikasema huku nikiangalia saa yangu.

‘Ni kweli kabisa kwa hilo mimi nakuvulia kofia, …sina shaka na wewe.., hata mimi sijafanya hivi kwa nia mbaya, hili ni muhimu sana..’akasema na kukaa vyema, halafu akaniangalia tena machoni, na kusema;

‘Haya nitakayokuambia sasa hivi, ni muhimu kuliko hayo unayoyafuatulia wewe…nakuomba unielewe hivyo’akasema

‘Sawa , mima nakupa robo saa, nakusikiliza, baada y ahapo naondoka zangu…’nikasema

‘Kuna mambo bado hayajathibitishwa, ila ya kikamilika, nitakuambia ila kwasasa nataka kukuelezea jambo kubwa tuliloligundua....kwa kukutahadharisha, na kukuomba usifanye hayo uliyoyakusudia kuyafanya hadi hapo utakapoambiwa, kwa manufaa yako na ya watu wengine wanaokujali...’akasema, na mimi nikatulia kusikiliza.

Akaangalia saa yake halafu akasema

‘Robo saa sio, inatosha kabisa baada ya hapo utakuwa huru kuondoka, naahidi hivyo…’akasema akiandika kwenye karatasi yake.

‘Mhh..haya, yaseme…’nikasema nikiona kama ananipotezea muda, kiukweli pale nilipo bado nilikuwa namuwazia huyo rafiki yangu je kumeendelea nini huko, isije ikawa yupo matatani..sikufikiria ubaya wake zaidi..niliwazia ubinadamu, hasa mtoto wake.

‘Mpendwa, sio kwamba nakulaumu, na mimi kama walivyo wazazi wako, tulishakuambia kuhusu mume wako, kwani tabia za watu za asili, kizalia, huwa hazibadiliki sana, labda mtu mwenyewe aamue kiukweli kufanya hivyo, ila akipata mwanya, kurudia asili yake haichelewi, mtu habadili kwa hivyo kama mwenyewe hatataka kujibadili...’akasema.

Mimi nikakaa kimia, najua huyu ni mtu wa wazazi wangu, nilishamzoea,…

‘Na nafahamu hali uliyo nayo kwa sasa, kwani mume unampenda sana hata pamoja na hayo yaliyotokea...lakini huko kunapoelekea, itabidi ufikirie hilo mara mbili, sio kwamba nakushauri uachane naye, hapana,..hautakiwi kufanya hivyo, …hata wazazi wako hwataki ufanye hivyo…’akatulia kidogo

‘Ni kweli wazazi wako wamelifikiria sana hilo ya kuwa, mna watoto, nakadhalika… sio vyema mkaachana, lakini sasa mtaishije kwa hali kama hiyo, hilo ni lenu wawili,..muhimu uishi naye ukiwa na tahadhari tofauti na awali, sasa kwa hayo waliyopanga, itakuwaje, ni kazi ambayo inafanyiwa kazi,..

‘Kwangu mimi kwa hivi sasa nataka kukuelezea yale tuliyoyagundua ambayo, yatakushtua,..maana hata mimi sikuamini, lakini ukweli ni ukweli tu, na ukweli huo hatutaweza kuupata zaidi , ikiwa wewe utachukulia jazba, nafahamu itafikia sehemu utasema basi liwalo na liwe, hapana, kwa vita hivi, bado tunahitajia uvumiliv wako....’akasema.

‘Kwanini unazunguka, unanipotezea muda, na kuniweka roho juu, niambie ulichoniitia, nina mambo mengi ya kufanya…’ nikasema kwa hasira.

‘Huo ni utangulizi mpendwa, nilazima nikuambie hayo kama ilivyotakiwa nikuambie.....’akasema

‘Ulivyoambiwa na nani, na wazazi wangu au…?’ nikauliza

‘Kwanza ni kuhusu huyo wakili wa mume wako, anayejiita wakili wa kujitegemea, ni kweli kitaaluma ni wakili..na sio kwamba hana fani hiyo, anayo na kaisomea kweli, vyeti anavyo na kazi pia anaifahamu, akisimama mahakamani sio mchezo,  ila yeye n ndumilakuwili,…na tabia isiyopendezahula na tabia yake ndivyo vinamkosoa...’akasema

 Nilitaka kumuambia hayo nayafahamu lakini nikaa kimia ili nimsikilize zaidi, huenda kuna kitu cha zaidi sikifahamu

‘Sasa huyo anataka kuwatumia marafiki zako,…bila ya wao kujua, kuhakikisha anakamilisha lengo lake , akiwemo huyo mume wako…huyu jamaa ni mjanja kweli kweli ..na hutaamini keshafanikiwa…’akasema

‘Marafiki zangu..!!’nikasema kwa mshangao.

‘Ndio…marafiki zako wameshatekwa kimawazo, na kwa jinsi ilivyofanyika, hawana ujanja, na kiukweli huenda hata wao hawafahamu ni kwanini, wameingizwa huko, ni ujanja wa hali ya juu,….na usione mengine yanatokea ukaona ni bahati mbaya, ni mpango wenye masihali fulani ya kisiasa…’akasema

‘Mhh..sasa ni siasa, awali ilikuwa ni maswal ya kindoa, mimi simjali mume wangu, ikaja …mume huenda kasalitio ndoa, sasa imekuwa ni mambo ya kisiasa, kweli mnahangaika sana, nikuambie kitu, hili hebu niechieni mwenyewe, nafahamu sana, kuwa wazazi wangu wananijali, lakini nimeshakuwa mtu mnzima, najua kujitetea, kwanini niendelee kuwatesa wazazi wangu, waacheni wapumzike, nitapambana kivyangu…’nikasema

‘Mtoto hakuwi mbele ya wazazi wake, ilimradi wapo hai, hata kama ni vikongwe, unasikia, msidharau wazazi wenu hata siku moja…pamoja na yote unayofanya, usifikirie kuwa utakuja kuwazidi wazazi wako, ….kumbuka wao wamepitia mengi, na utu uzima wao ni dawa..wao wana hekima ambayo hujaipata…mungu huwapa watu wazima maono ambayo wewe huwezi kuyafahamu…’akasema

‘Sikatai, hilo siwezi kupinga lakini pia wanahitajika kumpumzika, niwasaidie na mimi, nitawasaidia lini, eeh…’nikasema.

‘Haya ninayokuambia sio kwamba naongea tu,… ni kitu kilichofanyiwa uchunguzi na nina ushahidi wa kikao hicho kilichofanywa na maadui zenu…, ukitaka nitakupatia…ni hujuma zimepangwa kisayansi ya kisiasa…, na ni kweli zilianzia ndani ya familia yako, na sasa zimekwenda zaidi ya hapo, siasa imeshaingizwa..’akasema

‘Mimi sio mwanasiasa na sitarajii kuingia huko, sipendi siasa kabisa…’nikasema

‘Lakini baba yako ni mwanasiasa, kajiingiza huko pamoja na shughuli zake,  je humjali…?’akasema kuniuliza

‘Hayo ni maisha yake, mimi sipo huko ndio maana nikajitenga naye, na nimekuwa mbali naye, na nilishamuambia, sitaki tuingiliane, ili nisije kumuharibia mambo yake…’nikamwambia docta

‘Sikiliza, kwenye uwanja wa siasa, kila kitu ni silaha kwa adui yako, …na wengi wanakimbilia kuangalia familia zinavyoishi hilo kwa upande mmoja japokuwa huku kwetu Afrika sio sana, lakini zaidi ni vitega uchumi, mali nak, je havina mkono wa pesa chafu, je hakuna ukikuwaji wa maadili, kwenye zabuni nk, rushwa na vitu kama hivyo…’akasema

‘Najitahidi sana kukwepa hayo…nikasema

‘Baba yako alijitahidi sana kuwasaidia, na alijitahidi sana kuona kuwa nyie mnaendesha biashara kimaadili, sasa huo msaada unafuatiliwa, ulitokaje, na je huko unapokwenda, umefanyia nini,…unaona mtego uliopo hapo, msaada unageuka kuwa mtihani…’akasema

‘Ni kweli , mimi sijavunja miiko ya biashara, nafuata sheria, kwahiyo baba hastahiki kuogopa kwa hilo, sijafanyia vibaya mtaji alionipa kwenye biashara zangu, kama kuna ubaya, niambieni…’nikasema

‘Je mume wako anafanya hivyo..anafuta sheria, analipa kodi, anafanya biashara halali kwenye zabuni na serikali, je, matumizi yake, je..hajafanya mambo yasiyo mema kwenye jamii, kimaadili..nyie wote mnamulikwa kihivyo..?’ akaniuliza

‘Mimi sijui…’nikasema

‘Wewe hujui lakini maadui wa siasa wanilijua hilo, hebu nikuulize kwa hivi sasa mume wako ikatokea tatizo kwake, wewe utaziba masikio yako kuwa hayakuhusu, angalia huo ugonjwa wake, umefanya nini, ulilala kitandani…chukulia kafanya madhambi, unafikiri jamii itasemaje, hasa maadui wa kimaisha, hasa katika Nyanja za kisiasa maana mabo yako ni ya kisiasa, kuongea, kutoa propaganda potofu, watasemaje hapo, je wanataja jina la baba yako au jina la baba wa mume wako…kisiasa…?’akauliza

‘Ndio maana nilimuambia baba, mimi anichie maisha yangu, sikutaka kabisa yeye ajiingize kwangu, mtaji wake uwe ni mkopo kwangu nikiurejesha ajitoa kabisa na mimi, wala asitambulikane, ..lakini hajataka kunisikia..’nikasema

‘Je uliwahi kurejesha huo mkopo, ..?’ akaniuliza

‘Nitaurejesha, mambo hayajakaa sawa..’nikasema

‘Mpaka muda huo, unafikiri mangapi yamefanyika …nakuambia haya kwa mawazo mapana,…, huyo jamaa , wakili wa mume wako, ndio jembe la mpinzani wa baba yako, unielewe hapo, yeye alipikwa akasomeshwa na mpinzani mkubwa wa baba yako kisiasa,..sasa natakiwa kulipa fadhila, ndio hayo anayafanya je anayafanya bure bure tu, kuwa anataka masilahi ya pesa tu, jiulize kwa makini, ..’akatulia

‘Mimi sijui…’nikasema

‘Kitu kikubwa watu walikuwa wakijiuliza bila kupata jibu ni kwanini huyu jamaa anajiamini hivyo, ni kwanini hakamatwi, na akifunguliwa mashitaka hapatikani na hatia, ni kwanini…n hebu sikia alivyokuwa akikujibu pale hospitalini ni kwanini alijiamini hivyo, jiulize hapo…’akasema

‘Na wewe ni jembe la baba yangu, au…?’ nikauliza

‘Usifanye utani, hili ni jambo nyeti sana, sivyo kama unavyofikiria wewe, achana na hulika yako kuwa labda nafanya haya kwa vile, …hapana hili ni jambo nyeti na ukicheza, utajiharibu wewe na familia yako yote, kuanzia kwa wazazi wako, na  utakuja kujuta wakati umeshachelewa…’akasema

‘Kwa mume wangu ulisema hivyo hivyo, na huyo ni rafiki yako, sasa umemgeuka, sasa ni kwa wazazi wangu, ni nini, siasa au sio, lakini mimi zipo huko, na baba akipatwa na matatizo, wasinisingizie mimi, ..niakuambie kitu…’nikasema

‘Tunamuongelea huyo jamaa, tusipoteze muda, najua umenipa dakika ngapi, au umeziongeza ….sikiliza sasa…’akasema

‘Natumai huyu jamaa unamfahamu kwa juu juu tu, nitakuelezea sifa za huyu mtu, ambaye kitaaluma ni wakili wa kujitegemea, na polisi wamekuwa wakitafuta kila njia kumnasa, kutokana malalamiko ya watu wengi, waliowahi kufanyiwa utapeli na huyu mtu, akitumia mgongo wa taaluma yake hiyo, lakini kutokana na ujanja wake hajawahi kukamatwa.....’akasema.

‘Unaposema huyo jamaa una maana wakili Makabrasha...?’ nikauliza.

‘Nisingelipendelea kumtaja jina lake kihivyo, lakini ndio huyo,...mtu huyu ni rafiki wa mume wako toka utotoni, na tabia zao  zinafanana, japokuwa mume wako alikuja kubadilika baada ya wewe kuolewa na yeye, huo ndio ukweli,....’akatulia kidogo.

‘Mume wako, alikuwa akishirikiana na huyu jamaa kabla, jamaa akitoka ulaya, rafiki yake mkubwa alikuwa mume wako…wakawa wanashikirikiana  kwenye mambo mbalimbali, ya kutafuta maisha… kipindi hicho mume wako alikuwa akihangaika tu kazi yoyote anafanya, maisha yalikuwa magumu sana kwake, kwa hiyo tunaweza tusimlaumu moja kwa moja, japo sio sababu ya kufanya mabaya kwenye jamii..’akasema....

‘Mkaja kupendana,…na hatimaye kuvuruga uchumba wetu,…sio nakulaumu, ila nakuelezea hali ilivyoweza kubadilika, ni kweli ulimsaidia sana, na kweli kipindi hicho aliamua kubadilika kiukweli, lakini kunguru hafugiki.

‘Watu wanasema huenda, rafiki yake huyo wakili, ndiye aliyemshauri rafiki yake afanye kila awezavyo mpaka akuoe, ili baadae iwe ni chambo, au mlango wa kuingilia, lakini sio kweli…huyu jamaa alikupenda kiukweli, ila tamaa ndio iliyomuharibu,sio tamaa tu, bali hulka ya kuzaliwa, ilikuw na nguvu zaidi…’akasema

‘Una ushahidi gani..?’ nikamuuliza

‘Kila kitu kipo, mpaka nimeamua kukuita hapa nimeshahakikisha kila kitu kipo kiushahidi, maana mimi nakufahamu wewe ulivyo, lakini kwa leo nitakuelezea tu, ili kwanza nitimize wajibu wangu kama mimi na pili, niwakilishe ujumbe kutoka kwa wazazi wako, japokuwa hawajanituma nikuambie hivyo…’akasema

‘Endelea…’nikasema

‘Ulipoolewa na huyo jamaa, rafiki yake akawa anakusoma, anawasoma kufahamu madhaifi yenu,…kwanza alitaka kumweka sawa mume wako ili apitie kwake, kwa kujifanya anamjenga ili lolote likitokea asija kuadhirika..akajaribu akashindwa, …kwasababu ulishamweka sawa mume wako…;lakini jamaa alishajua kuwa kuna muda muafaka utafika, kunguru hafugiki, unanielewa hapo …’akatulia

Jamaa akaja kwa mgongo wa taaluma yake, akitaka awe wakili wenu, mume wako alimkubalia, lakini wewe ukaja kuvuruga, lakini hakukata tamaa, akawa anatafuta njia ya kuwaingilia,….. lakini kwanini afanye hivyo, jiulize ni kwanini, ni mali tu..,..au kuna nini cha kumfanya ahangaike hivyo…’akatulia

‘Mali ni nyenzo mojawapo, lakini sio sababu kubwa sana, hili hata polisi walikuwa hawajaligundua wao macho na masikio yao ni kwenye mali,..rejea niliyokuambia kuwa wakili huyu alipikwa na mwanasiasa adui, mpinzani wa baba yako…ukirejea huko ndio utanielewa vyema…’akasema

‘Je atawezaje kuingilia ngome iliyojengwa imara, kimaadili, kisomi, na mnajitahidi kila namna kuhakikisha kuwa hamna kashfa, …sasa nikuambie kitu baada ya kuona bado ni shida kuingilia ngoma ya baba yako zikapikwa kashfa…

‘Zikapikwa kashfa kwa vipi…?’ akauliza

‘Haya mambo ya dunia hii, yaone tu, usione nchi zinapigana ukafikiri ni wao tu propoganda potofu, kashfa, hujuma, jamii kuchonganishwa, bila wao kujua, wanakuja kukosana,…kashfa nyingine hutengezwa, na kwa ushahidi…, kashfa imeshaingia kwenye familia yenu, sasa ni ya kutengenezwa au ni kweli ilifanyika kiuzembe, ndio nilichokuitia hapa, ili ulifahamu hilo, kuwa sio jambo dogo kihivyo, limeshakwenda zaidi ya kifamilia, sasa chagua kuwasaidia wazazi wako, au ..…’akatulia hivyo hakumalizia, akaangalia saa 

‘Kashfa gani unayozungumzia hapa, ni huyo mtoto wa rafiki yangu, si ndio hiyo, lakini nimegundua kitu...na nilikuwa nakifuatilia, huko uwanja wa ndege, ndio ukaniwahi, nina uhakika ningelilimaliza hilo, na utata wote ungeliisha…?’ nikauliza na kusema

'Hahaha, hujua kuwa unajipeleka kwenye mdomo wa ..kenge,..huo ni mtego ulitayarishwa, inajualikana ulitakiwa uende huko, ukajinase...najua nia yako ni kupata damu ya huyo mtoto ukapime DNA,lakini usingeliweza kumpata...kuna mchezo ulitakiwa ufanyike, lakini sasa...'akaangalia saa yake

‘Ahadi ni deni, dakika ulizonipa zimekwisha, unasemaje, tuendelee…’


WAZO LA LEO: Ukisikia taarifa yoyote ifanyie kazi kwanza, hata kama unaona kuwa ni taarifa yenye masilahi kwako, usiwe na papara nayo, inaweza ikawa nzuri kumbe ndani yake kuna ubaya, kuna mitego, walimwengu sio wema…, inaweza ikawa kama asali yenye sumu ndani yake, kumbuka kuwa sio kila taarifa ina lengo jema kwako... Ipokee taarifa, ichunguze ukweli wake, na angalia athari zake, je inaweza kupokeleka, vinginevyo, ipuuze, weka subira, mola yupo pamoja nawe, na muda utasema
Ni mimi: emu-three

No comments :