Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Saturday, November 23, 2024

Dunia hii .....



Wiki sasa nimekuwa nikimkuta kijana wa miaka 20 au 22 hivi, akiwa amelala pambeni mwa majengo ya maduka eneo la posta, ni kijana ana nguvu, japo leo nilipomuuliza aanasema ana tatizo la bawasiri, linampa shida sana

'Vipi ndugu yangu waendeleaje
'Sijambo hivyo hivyot tu....ndio nasubiri nipate nauli nizrudi kwetu

'Kufika kwenu nauli ni bei gani

'Elif 55

'Sasa hivi una shilingi ngapi

'Nina elif 25, kuna mdada mmoja alinisaidia hizo pesa

'Sasa hivi unafanya shughuli gani yaani ukitoka hapo ulipolala

'Naokota chupa kama unavyoona...'

Alinionyesha mfuko uliopo pembeni mwake, ni mchafu, hata yeye mwenyewe nguo zako zilikuwa chafu, sijui kama anafua au hata kuoga.....

Niliwaza sana mbali, ..

Huyu ni kijana mdogo, taifa la kesho, yupo hapo anateseka, yupo kwenye maeneo ya ofisi na maduka, wapo wafanya biashara wenye pesa, wapo wenye bajaji na madaladala, hakuna hata mmoja aliyefikia kuwaza huyu mwenzetu tumsaidiaje, je ana tatizo gani

Sio rahisi kwa dunia ya leo,mtu kumfikiria mwingine wakati yeye mwenyewe ana matatizo yake mengi kichwani, anawaza vipi ataishi, vipi ataendesha maisha yake, nk

Nimeona hii niiweke kwenye shajara yetu ya leo...tukiendelea kumfuatilia

Ni mimi: emu-three

No comments :