Mdada alifungua mlango , akionyesha kabisa yupo
tayari kwa shari, mimi nikawa nasubiria nione ni kitu gani cha kufanya, sikuwa
na amani pale nilipokuwa nimekaa, hata hivyo wa muda ule sikuweza kuingilia,
nikasubiria kwanza. Mlango ukafunguka nusu, nikashangaa kumuona mdada kasimama huku
kaduwaa, na huku kashikilia mlango, mara nikasikia akisema;
‘Oh ni wewe....’akasema
huu akifungua mlango zaidi na kuchungulia kwa nje, halafu akasema;
‘Lakini sio
wewe uliyegonga mlango mwanzoni, yupo wapi aliyegonga mlango mwanzoni?’
akauliza, na sauti niliyokuja kuitambua kuwa ni mfanyakazi wa humo hotelini
ikasema;
‘Mimi nimeambiwa
nije kufungua chumba hiki, na kuangalia kama ninaweza kufanya usafi, kwani kuna
wakubwa wanakuja kufanyia mkutano wao humu, sina habari ya mtu huyo
unayemuulizia,….’akasema huyo mfanyakazi wa hiyo hoteli na mdada akasema;
‘Haiwezekani,..hata
hivyo, kwani nyie mnakuja kufanya usafi hata kama mwenyewe hayupo, hii ni ofisi
ya watu au sio, kuna mtu anatumia chumba hiki kama ofisi,ulimfahamisha hilo?’
akauliza mdada
‘Mimi sijui
hayo, maswali kama hayo kamuulize bosi wangu, ninachofanya mimi ni kufuata amri,
hata hivyo nimesikia kuwa huyo mtu anayetumia hii ofisi hayupo, hapatikani,…
hata kwenye simu akipigiwa hapatikani, kazima simu yake...nasikia alikuwa huko
mahakamani, wametumwa watu huko hawakumkuta, ndio hivyo ikawa haina jinsi maana
wakubwa wanahitaji hii ofisi…’akasema.
Ni kweli
mdada,alininiambia awali kuwa nizime simu yangu kwahiyo huenda kweli
walimtafuta kwenye simu wakanikosa;
‘Lakini hao
ni wakubwa gani, au ni wale walinionifanyia usahili, ...’nikawa najiuliza mdada,
na wakati huo mdada alikuwa kanigeukia, na kusema;
‘Una mgeni
wako, anataka kufanya usafi humu ndani...’akasema na bila kusubiri kauli yangu
akamgeukia huyo mfanyakazi na kusema;
‘Haya
unaweza kufanya usafi , lakini sioni kama kunahitajika huo usafi, kupo poa, au
vipi, hebu ingia mwenyewe maana nisikuingilie kazi yako...’akasema na akamshika
yule mfanyakazi mkono, na kusema;
‘Utasema
kila kitu kipo sawa, nitahakikisha hilo au unasemaje....’akamuongelesha kwa
sauti ndogo na yule mfanyakazi akasema;
‘Na wewe
dada bwana, huachi vituko vyako, haikuwa na haja kufanya hivyo, sawa mimi sina
shida, nimemaliza...’akasema na kuondoka
‘Mhasibu,
huyu mtu aliyegonga, kayeyuka, nahisi yupo mahali, anakusubiria, sasa mimi
sitacheza mbali, mpaka nionane naye leo hiii, nina hamu ya kuonana naye, sitamuacha
hivi hivi , nataka anikome,...’akasema
‘Una uhakika
kuwa ndio yeye aliyegonga...?’ nikamuuliza
‘Nina
uhakika, nina macho ya nyuma na mbele, mimi sio kama unavyonifikiria, unasikia
hata kama nisipoonana naye leo, ukionana naye, mwambie anikome, ....’akasema
mdada
‘Sawa mjumbe
hauwawi, ...lakini jamaa huyo hana matatizo kabisa, ni wewe tu unayemfikiria
vibaya...’nikasema
‘Sasa
sikiliza kwa kauli ya huyu mhudumu, ni kuwa unatafutwa na wakubwa zako, kinachotakiwa
sasa washa simu yako, wakikuuliza sema iliisha chaji au vyovyote vile,na usije
kusema ulikuwa na mimi…’akasema mdada huku akitembea kuelekea kwenye lile
kabati lililokuwa na nyaraka,akalichunguza halafu akageuka kuniangalia na kuuliza;
‘Una uhakika
kuziona hizo nyaraka karibuni na lini kwa mara ya mwisho ulifungua hili
kabati...?’ akauliza
‘Jana, hata
asubuhi wakati nimefika hapa ofisini abla sijaelekea huko mahakamani,
nilifungua kabati na kila kitu kilikuwepo, basi kama ni mtu kaja kuchuua
kafanya hivyo, kipindi tukiwa mahakamani,....’nikasema
‘Atakuwa
nani,...na kwanini afanye hivyo?’ akauliza mdada huku akiwa akiniangalia kwa
macho ya kujiuliza
‘Siwezi
kujua kabisa, kwani walishaniambia kuwa hakutakiwi kitu chochote kiyolewe humu
ndani, na vyote vipo kwenye mikono yangu, ndio maana wakanipa ufunguo za hizo
kabati, kama kuna mtu atahitaji kitu inabidi awasiliane na mimi, na kwa hili
lilitokea, inabidi nitoe taarifa...’nikasema
‘Usifanye
hivyo, kaa kimiya kama hujui kitu...’akasema mdada na kunifanya nimuangalia kwa
mshangao.
‘Kwanini
sasa, kama nisipofanya hivyo huoni mimi naweza kushukiwa vibaya, watu wameniona
mimi na wewe tukiingia humu,....’nikasema
‘Ndio maana
nasema usiseme kitu, kwani utaonekana kama unajihami, cha msingi kama utaulizwa
chochote kuhusiana na hizo nyaraka, wewe sema kwa mara ya mwisho
uliziona,...hujafaungua tena hili kabati, inatosha, mengine waachie wao
wenyewe, usiumize kichwa kuwafikiria wao, kitu gani watasema, ...’akasema mdada
‘Tatizo lako
mdada, kila mara unataka kunitia matatani, hujui hiyo ni dhamana ya watu nilikabidhiwa
mimi, ..’nikasema
‘Hebu kidogo
nifikirie....’akasema na kushika kichwa, halafu akageuka na kusema;
‘Hao jamaa
wanaokuja kufanya kikao, nawashuku,kuna kitu wanataka kuhakikisha, na huenda
hawataulizia hilo, na nia yao ni kubadili kumbukumbu, wanaweza kuja na
makabrasha mengine yakiwa na orodha ya vitu vingine, lakini , …’akasita kidogo
‘Lakini
nini?’ nikauliza
‘Hizo
nyaraka za awali hazitatambulika tena, ndio zimeshapotea hivyo, sijui kwanini
sikulifanyia hili kazi mapema,...hata hivyo, bado nina ushahidi mwingine mkubwa
tu...’akasema
‘Ushahidi
gani?’ nikauliza
‘Unakumbuka,....
marehemu alipokuwa kwangu, alikuwa akitaka nini wangu,..moja ya vitu alivyouwa
akivitafuta kutoka kwangu ni pamoja na nyaraka muhimu nilizokuwa nazo
mimi,,....wakati tupo mle ndani, kuna watu walivunja kabati langu la kumbukumbu
zangu, wakijaribu kuzitafuta hizo nyaraka, lakini hawakuzipata, bado nina nondo
za kutosha...’akasema
‘Sikuelewi..wewe
hizo nyaraka ulizipata vipi.? ’nikamuuliza
‘Sio tatizo,
usiumie kichwa kwa kuliwazia hilo, ...’akasema mdada,na kabla hajamaliza simu
yangu ikaanza kuita,nikaangalia jina la mpigaji, na mdada akaniuliza ni nani, na kwa muda huo
alikuwa na simu yake mononi akiangalai kitu, na mimi niasema;
‘Hii namba
ni ngeni kwangu, sijui ni nani….’nikasema na mdada akaniashiria nisubiri
kidogo, wakati huo simu inaendelea kuita, mdada akawa anaangalia kitu kwenye simu
yake, akawa anafanya jambo na kwa haraka akasema;
‘Pokea hiyo
simu…’na huu akiendelea kuangalia simu yake
‘Upo wapi,mbona
hupokei simu, ulikuwa umelala nini, sisi tunakutafuta sehemu zote hupatikani na
simu ulikuwa umezima, sasa sikiliza, tunahitajia kufanya kikao hapo kwenye
ofisi yako, lakini hatujui upo wapi,…’sauti ikasema
‘Mbona nipo
hotelini kwangu…’nikasema
‘Sawa..hamna
shida, ila ni kukuarifu tu kuwa, kuna mfanyakazi wa hapa hotelini tulimtuma
kuja kufanya usafi, usije kushangaa, maana hukuwa hewani, pili sisi tupo njiani
tutafika tuonane hapo ofisini kwako..’sauti ikasema
‘Sawa
nitafika hamna shida..’nikasema
‘Nusu saa
inatosha, au sio, tukukute ofisini kwao, hatutachukua muda wako mrefu, …’sauti
ikasema na mzungumzaji akakata simu, na mdada akasema;
‘Hawa watu
wamo humu humu ndani kwenye hoteli, wapo chini,wamesema nini...?’akauliza mdada
‘Mbona
wamesema wapo njiani, ?’ nikamuuliza na yeye akatabasamu na kusema
‘Wapo humu
ndani, hii ni kuonyesha kuwa kuna jambo, sio watu wa kawaida, ni wakubwa lakini
wanajua ni nini wanachokifanya kuwa makini...’akasema huku akiangalia saa yake,
na kusema;
‘Umepewa
nusu saa, au sio...’akawa kama ananiuliza huku akikikagua hicho chumba kwa
macho, na baadaye ukaingia ujumbe kwenye simu yake, akausoma na kusema;
‘Hao ni
wakubwa wa idara ya ushuru, ni kweli,wana kikao leo hapa ofisini kwako, sio
kikao rasimu, kwahiyo kuna ajenda ya siri, unatakiwa kujiandaa kujibu maswali
yao,na sijui utasema nini wakiuliza kuhusu hizo nyaraka, na sizani kama
watauliza hilo, na huenda wakaja ya nyaraka nyingine, kuwa makini na hilo…’akasema
na akachukua ufungua wa lile kabati.
Wakati huo ufunguo, ulikuwa mezani, akauchukua ule ufunguo lakini mononi alikuwa leso, inaonekana hakutaka kuligusa lile kabati kwa mikono yake mitupu, akalifungua lile kabati,
akachukua simu yake na kupiga picha mle ndani, na akawa anachukua picha za video kwa sekunde chache, alipomaliza akatoa kitambaa kikasha, na kutoa kitambaa cheupe, akawa anapitisha kwenye mshikio wa
hilo kabati, alikuwa akifanya hivyo kwa tahadhari, hakutaka kugusa kitu, nahisi
alikuwa akichukua alama za vidole.
‘Najaribu
kufanya hivi, japokuwa haisaidii sana, ...’akasema na kukiweka kile kitambaa
kwenye kikasha fulani, ...okey, nimemaliza, akafunga, halafu akaichukua ile
fungua akiwa na leso, akaifuta vyema, na kunikabidhi mimi...
‘Lakini huo
sio ufunguo wangu...’nikasema.
‘Okey, sawa,
nimesahau...’akasema na uzichukua funguo zake, akaziweka kwenye mkoba wake,
halafu akasema;
‘Nahisi hawa
watu ndio wamezichukua hizo nyaraka, ngoja vijana wangu wafanye hiyo kazi...’akasema
na kuandika ujumbe kwenye simu yake
‘Kama
walizichukua wao,ina maana wana ufunguo wa hapo,kwanini sasa wakawa wanakutafuta
wewe ili waweze kuingia humu,huoni kama kuna kitu ..anyway,let the time tell, …watakuwa wameomba wa wahusika wa hapa
hotelini, bila shaka’akasema mdada akiangalia saa yake na kusema
‘Nenda
hotelini kwako,kachukue hizo ufunguo,na uje hapa haraka, zimebakia dakika kumi
na tano…’akasema
‘Na wewe,?’
nikauliza na yeye hakuniangalia akawa anaendelea kukagua hicho chumba kwa
macho, na mimi nikamuuliza tena;
‘Na wewe
unafanya nini humu ndani,..maana sizani kama itakuwa vyema uendelee kubakia
wewe mwenyewe humu ndani…?’ nikiamuuliza
‘Wewe nenda
kajiandae kukutana nao,…hayo mengine niachie mimi mwenyewe, bado natafakari
kuhusu huyu mtu wako, nina imani ndiye aliyefika mwanzoni akagonga mlango,pili
kuna mambo nayaweka sawa, ….’akasema
akitoa vifaa kwenye mkoba wake, nikaona nisipoteze muda, nikasema;
‘Kama ndio
yeye huyu unayesema ni jamaa yangu kuwa ndiye aliyeginga mlango, kwanini mhudumu
hakumuona….?’nikauliza
‘Janja yake
nitagundua tu….inaonekana sio mtu wa kawaida, lakini ajue mimi ni zaidi yake’akasema
mdada na kuanza kuwasiliana na watu wake, na wakati huo mimi nikaondoka na
kuelekea chumbani kwangu,nikafika na kufungua mlango,nikiwa na haraka maana
muda ulikuwa unakwenda kwa kasi, nikaona niwashe taa...
‘Wewe huwa
unawasha taa hata mchana….’Nikasikia sauti ikitoka nyuma yangu na kunifanya
nishituke karibu ya kudondoka chini, ilikuwa ni sauti ya mpelelezi aliyekuwa
kasimama pembeni ya mlango
‘Oh
umeingiaje humu ndani namna gani?’ nikamuuliza nilipohakikisha kuwa nay eye na
yeye akatabasamu na kusema;
‘Ukiwa kwenye
kazi kama yangu hilo swali sio muhimu sana …naweza kuingia mahali popote, cha
muhimu ni kuhakikisha kuwa usalama upo…’akasema
‘Sina muda
wakubwa wanatakakuonana na mimi na sijui ni kitu gani wanatakakuongea na
mimi…’nikasema
‘Je
ulifanikiwa kumzuia mdada asizichukue hizo nyaraka?’ akaniuliza
‘Umejuaje
kuwa anazihitajia hizo nyaraka,…?’ nikauliza
‘Jibu swali
langu,ni muhimu sana’akasema
‘Hizo
nyaraka hazipokwenye hilo kabati, na walasijui ni nani kazichukua…’nikasema
‘Haiwezekani,…sasa
hilo ni tatizo,una uhakika hajazichukua huyo mdada…?’ akaniuliza
‘Yeye ndio
alikuwa akizihitajia, na akanishauro nifungue kabati, na tulipofungua
hatukukuta kitu, hata yeye alishikwa na mshangao, hajui ni nani
kazichukua..’nikasema
Mpelelezi,akachukua
simu yake na kuongea na mtu, nilimisikia akisema;
‘Ule
ushahidi umetoweka…’akasema na kusikiliza kwa muda
‘Sawa,..kwahiyo
tufanyaje, sijajua ni nani kazichukua …yah,nitamtafuta , na ni lazima atagundua
kuwa ni nakala,….’akasema na kusikiliza
kwa muda, halafu akasema;
‘Ndio,anakwenda
kuonana nao….hamna shida,..’akakata simu na kunigeukia, akasema;
‘Sasa
sikiliza,hao unakwenda kuonana nao,ni wakuu wa hizo idara unazotarajia kufanya
kazi,tunahisi wanakwenda kukukabidhi majukumu, lakini kablaya yote usikubali
kupewa majukumu bila kuandikishana kwa kila kitu kilichomo humo,na usikubali
kabisa kusaini mkataba mpaka uhakikishe vyote vilivyoorozeshwa kwenye huo
mkataba vipo na umeviona…’akasema mpelelezi
‘Kwani hizo
nyaraka zimekwenda wapi?’ akauliza
‘Ndilo swali
hata mimi najiuliza,maana hizo nyaraka ni muhimu sana, na zilitarajiwa kutumiwa
kama ushahidi, na huyo aliyezichukua atakuwa ni mhusika mkuu wa hili kundi
ambaye anafahamu umuhimu wa hizo nyaraka na alifahamukuwa zipo humo…’akasema
‘Atakuwa ni
nani?’ nikauliza
‘Wewe
unakwenda kuongea na hao watu,wasikilize vyema uone kama watazungumzia hizo
nyaraka,na kama kwenye hiyo mikataba ya makabidhiano ukiona hizo nyaraka
zimeorodheshwa,hakikisha unauliza wapi zilipo,lakini nina uhakika wanaweza
wasiziweke ndio maana zimetoweka….’akasema
‘Mimi naona
muda umekwena ngoja niende kuonana nao…’nikasema na mpelelezi,akanionyeshea
ishara kuwa niondoke, yeye akawa kasimama humo humo ndani, nikatoka, na
nilipofungua mlango nikakutana na mdada akiwa kasimama mlangoni
‘Nimesikia
kama unaongea na mtu,ni nani?’ akaniuliza
‘Nlikuwa
naongea na simu, vipi wameshafika hao wakubwa?’ nikauliza
‘Hawajafika
lakini wapo chini, nahisi wanapata kinywaji,wewe nenda kawasubiri,mimi
nitakusubiri cumbani kwako….’akasema
‘Kwanini
unisubiri chumbani kwangu wakati mwenyewe sipo…’nikasema nikiwa na wasiwasi
kuwa mdada akiingia humo ndani atakutana na mpelelezi na lolote linaweza
kutokea
‘Usiwe na
wasiwasi na mimi siwezi kupekua pekua vitu vyako,na hata nikitaka
nisingelikuambia,ningelikuja kwa wakati wangu na kufanya ninachokitaka,wewe
harakisha kwenda mimi utanikuta humo ndani….’akasema na kushikilia kitasa cha
mlango,mimi nikawa sina la kufanya, kwani muda ulishakwenda na simu yangu
ikaita
Nilipokea haraka
haraka bila kuangalia mpigaji, sauti ikasema;
‘Sisi
tunakuja, natumai umeshafika ofisini kwako,….’sauti ikasema
‘Ndio
ndio...’nikasema nikionyesha wasiwasi
Nilimuona
mdada akiwa kasimama mlangoni, akisikiliza naongea nini na nilipomaliza
kuongea, na ile simu, akanipungia mkono, n kusukuma mlango wa chumba changu
kuingia, na mimi sikuwa na kufanya kwa muda huo, kwa haraka nikaanza kutembea
kuelekea ofisini kuonana na hao wakuu
NB: Kwa leo
tuishie hapa, mvua, mtandao, ilifanya jana tusiwe pamoja
WAZO LA LEO:Sio kila kitu kinafaa kuiga, hata
kama anayekitenda hicho kitu ni mtu maarufu sana,yeye akifanya hivyo kwa hali
yake inawezekana ikaonekana ni sahihi, kwa vile ni maarufu, ni tajiri nk, na
huenda kwao ina maana fulani, je wewe unayeiga hayo anayoyafanya huyo mtu
maarufu kama unavyomuona wewe, unafahamu maana ya hicho kitu anachokifanya,
kuvaa au kutenda?
Tusiwe
wepesi wa kuiga tu bila uchunguzi,kwani mengine tunayoiga ni kinyume cha
maadili, na huenda yana athari kubwa kwetu kiafya, kitamaduni na hata
kimaendeleo.
Kwa uoni
wangu, kabla ya kuiga jambo hebu tuangalie umuhimu wa hilo jambo, kijamii ,
kiitikadi na kimaendeleo, tusiige tu kutaka sifa, kwani badala ya sifa tunaweza
kuzalilika, japo wewe unatafuta umaarufu.
Ni vyema, tukaiga mambo yenye tija, yenye
kuleta maendeleo,na faida kwa vizazi vyetu . Tujue kuwa kuiga sana ni utumwa na
kutokujiamini.
Ni mimi:
emu-three
No comments :
Post a Comment