‘Nahisi rafiki yangu
atakuwa mikononi mwa huyo wakili, kwani aliniambia mtoto wake, alitekwa nyara
na watu wasiojulikana, na baadaye akapigiwa simu, kuwa ili ampate mtoto wake
inabidi kusaini mkataba walioandaa hawo watu...
‘Kwasababu ya mtoto wangu
sikuwa na hiari, nilikubali kusaini huo mkataba..’ hata mimi kama mzazi
ningefanya hivyo, nikajisemea kimoyo moyo.
Ina maana huyo rafiki
yangu, akasaini huo mkataba, na huyo rafiki yangu alikuja kugundua kuwa mkataba
huo hakuwa na madhara sana kwake, zaidi ni dhuluma kwa watu wengine, ...lakini
hakuwa hiari, akakubali, akasaini, na alitarajia kumpata mtoto wake...hakusema
kuwa alimpata au la,na nafikiri hawo watu wamemzunguka, au...’ndivyo
nilivyomwambia rafiki wa mume wangu, na huku nikiwaza mengine,
Kama kwaida ya rafiki
wa mume, wangu, kupinga kila kitu, akawa ananiuliza maswali mengi,ambayo sikuwa
na majibu nayo....kwani wakiti huo akili yangu ilishakuwa na mawazo mengine.
Wakati huo akili yangu
ilishaona kuwa rafiki yangu huko alipo yupo matatani,hasa baada ya huyu rafiki
wa mume wangu kuniambia kuwa Makabrsha ana ofisi huko uwanja wa ndege, na pia
rafiki yangu aliniambia kuwa yupo huko uwanja wa ndege, na wakati anataka
kunielezea zaidi simu yake ilikatika, mkatiko ambao uliashiria kuwa huko hakuna
mema.
Kwangu mimi moyoni,
nilihisi hawo watu waliomteka mtoto wake, wamemgeuka, na lolote linaweza
kutokea, na mimi kama rafiki yake, ilibidi niende nikamsaidie, hata kama kuna
hizo tetesi ambazo zinanichanganya, na mpaka sasa akili yangu ilikuwa hajaamini...
‘Ni lazima nifanye
lolote, japokuwa nilikuwa nimechelewa....
Endelea na kisa chetu.....
********
WAO LA LEO:Kila
kazi ina ujuzi wake na taratibu zake, ndio maana watu wanakwenda kuzisomea hizo
kazi, tusijifanye kuwa tunafahamu kila kitu, eti kwa vile ulipitia pitia
shuleni, kuna vitabu umesomasoma , hiyo peke yake haitoshi ...ndio maana kuna
taaluma tofautitofauti, na kila taaluma, ina mabingwa, ina wataalamu wake, ina
watu wanapewa madaraja na nyazifa mbalimbali, kuonyesha kuwa hizo ni fani zinazojitegemea,
tusipende kujiingiza kwenye kazi za watu ambazo huenda ni za kitaalamu zaidi,
na kujifanya tunaufahamu nazo, ilihali hatujazisomea, tujue kuwa kuongea na kutenda ni vitu viwili tofauti,..tuweni makini na fani za watu.
Ni mimi:
emu-three
2 comments :
Shukrani m3..
Pam shukurani na ww pia kwa kuwa pamoja nami na wengine wote. TUPO PAMOJA
Post a Comment