Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Tuesday, October 30, 2012

Uchungu wa mwana aujuaye ni mzazi-16



Binti Kis kama walivyokuwa wakimuita, akiwa keshafika ndani ya jengo takatifu, ghafla woga ukaanza kuiteka nafsi yake, akihis sura nyingi za watu zikimtizama, na moja wapo ilikuwa ya yule mzee anayetisha, na huku akikumbuka maelezo mengi yanayosimulia kuhusu mahali hapo,  mwanzoni alikuwa haogopi, lakini pale mguu wake ulipokanyaga eneo jeupe la aradhi ya sehemu hiyo akili mwili ulilegea.

Akawa kaam sio yeye, akawa anatembea kwa uwoga, na ile hali ilimfanya awe kama mgonjwa anayejikokota kufika kituo cha matibabu, na huku akili yake ikianza kukumbuka yale aliyowahi kusimuliwa na bibi yake kuhusu eneo hilo, na sauti ya bibi yake iliposikika kwenye ubongo wake,akahisi ageuka na kuanza kukimbia kutoka eneo hilo.

Lakini cha ajabu hakuweza, miguu yake ikiwa imeisha nguvu, akwa anajikongoka kuelekea sehemu kulipojengwa jengo, na humo ndani kuna mahadaki mengi, ambayo humilikiwa na koo mbali mbali kama ofisi zao, na sauti ya bibi yake ikaanza kumjia akilini ikimuelezea kwanini eneo hilo likaitwa mahali patakatifu;

‘Mjukuu wangu enzi zetu tulipohamia hapa nilikuwa bado mbichi, mwali ambaye alikuja kula fungate na mume wangu mpenzi, nilikuwa nampenda sana, kama alivyonipenda mimi,, huyo ndiye babu yako ambaye aliponioa tu, ikaja taarifa hiyo kuwa baadhi tunahamia makao mapya, yalibashiriwa, na mimi niliipokea taarifa hiyo kwa furaha.

‘Ina maana ulifurahia kuwaacha wazazi wako na kwenda kuishi sehemu ngeni?’ akauliza mjukuu.

‘Unapoolewa ujue utamuacha mama na baba yako, hata kama unawapenda vipi, na hili tulishaambiwa na mashangazi, na walimuw ajadi, kuwa mume wako sasa ndiye atakayekuwa mzazi wako wa pili, yeye na wewe mnakuwa kitu kimoja.

‘Ndio kuna ilehali ya kuhisia hivyo, kwa vile wazazi ni wazazi, hawawezi kuwa mtu mwingine,na uchungu wa mwana aujuaye ni mzazi,lakini lazima ndoa iwepo, lazima mume na mke wawepo, ili kujenga kizazi kipya, na vyema yake ni kukipaat hicho kizazi mkiwa wawili, mke na mume...

Mimi kwa usichana wangu na kazi nyingi zanyumbani, nilikuwa najiona nachoka sana,nikajua kuwa anenda kuolewa na nitapata muda wa kuwa na mume wangu ambaye kila mara nilikuwa nikfokwa pindi ninapotaka kwenda kuongea na yeye, sasa nitakuwa huru,kwanu  keshanioa, na tunakwenda kuanz maisha ya raha, maana kuolewa wengi tunajua hivyo, kuwa umeshampata mwenzako unayempenda, basi mtaishi kwa raha…’

‘Siku babu yako aliponiambia kuwa tunekwenda eneo jipya, ili tuweze kuwa huru zaidi, nilimwambia, kokote unapotaka kwenda mimi nipo na wewe na nipo tayari kwenda, kwani mimi ni mkeo wako nipo tayari kwa ajili yako, na nitatii kila utakachonielekeza nikifanye, najua yote uliyopanga ni kwa ajili yetu sote’,

‘Lakini huko tunapokwenda koo nyingi zimepanga kwenda huko, huenda tukaanza kugombana wenyewe kwa wenyewe, kwahiyo ujiandae kwenda kuishi maisha ya vita’akaniambia, na mimi nikakubali sikujua lolote kuhusu vita, maana nilichukuliwa kwenye mikono ya wazazi wangu nikiwa nalelewa kama mtoto, licha ya kuwa vita vilikuwepo vya hapa na pale,lakini sisi watoto tulichungwa sana, tulilindwa kuhakikisha kuwa akili zetu hazitekwi na mambo ya kivita.

‘Mimi na babu yako tukaanza maisha, lakini siku zote yeye alikuwa msituni, wakipigana, na wakati mwingine anarudi akiwa kaumia , ana majeraha kila sehemu ya mwili,  mimi ndiye nahangaika kumtibia, na ingawaje ujuzi wa matibabu niliupata toka huko kwetu, lakini uzoefu zaidi wa kutibia watu walijeruhiwa kwenye vita niliupatia kwenye eneo hilo takatifu.

Kila mume wangu aliporudi na kumtibia akapona haraka ndivyo taarifa za ujuzi wangu zilivyozidi kuzagaa, na hata kutolewa kwenda mstari wa mbele wa vita kuwatibia majeruhi. Nikawa sasa naishi vitani, natabia watu walioumia, na wakati mwingine naitwa majumbani kama kuna wakina mama wanaotaka kujifungua, au watoto wagonjwa nikawa tibabu wa eneo lote hili.

‘Eneo hilo takatifu  ndipo babu yako alipofarikia, akiwa akimtetea mfalme, kiongozi wa kwanza ambaye tulihama naye, alijitoa nafsi yake kuhakikisha kuwa kiongozi huyo haumizwi, na alikufa kifo cha kishujaa..’akasema bibi.

‘Kifo gani hicho, cha kishujaa,mbona sisi hatupo kwenye eneo takatifu na kutambulikana kama wafamilia ya watu mashuhuru, hata kuolewa nimekataliwa eti sisi sio familia mashuhuri?’ akaulizwa bibi.

‘Eneo hio kila mmoja likuwa akiligombea, kwani ndilo walilotabiriwa kuwa ni eneo takatifu, na kila ukoo ulitaka ulimilki , kwahiyo kila kiongozi wa ukoo, alifika hapo na jeshil lake, kukawa na mapigano ya huku na kule, kila mmoja akipigana na mwenzake.. wakati mwingine ni vita vya kuviziana, huyu akimuone mwenzake ni ukoo wa mwingine anajitahidi amuue, ....

Babu yako yeye alikuwa mlinzi wa kiongozi wa ukoo wetu, na katika vita hivyo, ikatokea tukazidiwa na kiongozi wetu akazingirwa, babu yako akawa anapigana nao, na kuna muda wenzao maadui walitupa mishale, babu yako akajiweka mbele ya kiongozi wake, na mishale ile ikazama mwilini mwake, ….’akasema bibi kwa uchungu.

‘Na huyo kiongozi ikawaje?’ akauliza.

Yule kiongozi alipiga magozi akawa anamlilia babu yako, huku akiwa haamini, na hutaamini wengi wa viongozi wakafanya hivyo wakapiga magoti, kila mmoja akimlilia mlinzi wake, maana maaskari wengi walishafariki, waliobakia ni majeruhi tu.

Na kumbe huku tulipotoka walishafikia uamuzi watume jeshi kubwa kuja kudhibiti hiyo hali, jeshi lilipofika ndio likakuta hiyo hali imeshakuw ambaya, waliobakia ni viongozi wa ukoo, na mjeruhu wengi,wakavamia na kuwaweka wote chini ya ulinzi, na amri ikatolewa kuwa hakuna kupigana tena, kwani mizumu na mababu waliozikwa eneo hilo wamekasirika.



‘Mtamwaga damu zenu mpaka lini, hamjui nyie ni ndugu, mkirudi kinyumenyume kimaisha babu zetu walikuwa ndugu baba na mama mmoja, wakazaliwa hadi mkafikia kizazi chenu nyie, leo hii mnawakata matumbo wazee wenu,maana kuuana ni sawa ni kuwakata wazee wenu matumbo yao…

‘Sasa basi,amri moja, sitisheni vita na toka leo eneo hili litakuwa takatifu, sheri mtapewa kutoka huko mlipokuwa awali, kuwa eneo hili halitakiwi madhambi tena, kila mmoja ni lazima afuate sheria hizo na yule atakayekiuka adhabu kali itamuandama, na ikithibitishwa kuwa yeye ndiye mkosaji, atatoswa kwenye mto,huo mto umejaa mamba waliokuwa wakifungwa na wazee waliokuwa wakiishi hapa awali,..mamba hao ni wakurithi, wana baraka zake,kazi yao ni kula miili iliyotenda dahambiili hizo dhambi zipotee kabisa, ….

‘Sasa toka leo yule mkosaji atatupwa kwenye huo mto,..’ ikatolewa amri na kiongozi mpya akachaguliwa, na viongozi wengine wa kila koo, sisi hatukupa nafasi hiyo, maana watoto wangu walikuwa bado wadogo, walikuwa kwenye jeshi jipya. Na tangu siki hiyo ikawa sheria msimeno kile mkosaji hakuonewa huruma, akawa anatoswa ziwani, mpaka watu wakaanza kuogopa. Ilifikia muda mtu akifanya dhambi kwa siri, anajikuta kafichuliwa bila hata kujua ni nani aliyefichua hiyo siri, watu wakaanza kuogopa, na sheri ikaanza kufuatwa…

‘Kwahiyo mjuu wangu ukifika kwenye eneo hilo takatifi usije ukajidanganya kuwa hauonekani, wapo watu waliokufa hapo kwenye vita wanakuona, roho zao kila mara zinapita kupalinda hapo mahali,na mwenyewe ukifika mhali hapo, kama ni mkosaji utajihisi kweli wewe ni mkosaji, uatahisi watu wanakuangalia, wanakupigia makelele, na unaweza ukadondoka na kupoteza fahamu….’maneno ya bibi yake, yalimfanya ahisi kuwa yeye ni mkosaji,na alipohisi mwili ukisha nguvu, akajua muda wowote anaweza akadondoka na kupoteza fahamu, na alichowaza ni kugeuka nyuma na kurudi huko alipotoka.


‘Usiwe na wasiwasi, wewe ndiye mke halali wa yule mwanaume unayempenda,pigania kwa nguvu zote, huoni kila anateyka kukuoa anashidwa, usiogoe, sisi tupo nyuma yako…’akakumbuka yale maneno aliyoambiwa na mume wangu…na mara akasikia mtu akiwa nyuma yake, aliogopa kugeuka, akijua sasa anambuliwa, kumbe alikuwa mmoja wa walinzi ambaye alimwambia aendelee mbele,..

‘Hapa sasa hakuna kurudi nyuma..’akasema kimoyo moyo, na kusonga mbele, licha ya kuwa  mwili mzima ulikuwa ukisisimukwa kuashiri awoga na kuhisi kuwa hizo roho zinamuona kwa hicho anachotaka kukifanya,lakini baadaye akasema kimoyomoyo;

‘Mimi sifanyi haya kwa nia mbaya,nafanya haya kwa ajili ya mtu ninayempenda, na nina nia safi ya kuwa mke mwema kumtumikia yeye vyovyote iwavyo, tatizo ni kuwa wengi hawanijui kuwa mimi ni mke mwema….’ akasema kimoyomoyo huku akijitahidi kutembea akiigiza vile vile anavyotembea bibi yake, na wale maaskari vijana walionekana kutokumtilia mashaka, waliinama kwa adabu na yeye akapita kwa mwendo ule ule wa kibibi-kibibi.

Alishukuru sana mzaha wake aliokuwa akimfanyia bibi yake, kwani mara kwa mara alizoea kumuigiza bibi yake anavyotembea na akifanya hivyo bibi yake humkimbiza kwa fimbo. Siku moja alivaa nguo za bibi yake, na kujifunika kama anavyovaa bibi yake. Bibi yake huwa anavaa na kujifunika mwili mzima na kuacha sehemu ya macho,kwani sehemu hiyo takatifu hawafiki wanawake bila kazi maalumu na kuna sehemu ambayo anakaa malikia, ndipo hapo wanawake wanaweza kufika,

Siku hiyo alivaa kama anavyovaa bibi yake akawa anatembea kama anavyotembea bibi yake, na kupita mbele ya baba yake,. Baba yake alijua kabisa ni mama yake anayepita, akainuka na kuinama kwa adabu, baadaye akaanza kucheka.

‘Wewe binti, yaani umefikia kumchezea mama yangu, nitakupiga kipigo ambacho hutakisahau, wewe hujui thamani ya bibi yako, bibi yako ni mama mtakatifu, tibabu wa eneo hili, anaheshimik,a akipita kila mmoja huiana chini. Yeye alistahili kuwa malikia wa eneo hili, ila watu wabaya walimfanyai fitina’akasema baba yake.

‘Usimpige mjukuu wangu, huoni kuwa ananirithi, hata nikifa najua nina mtu anayelandana na mimi, na hata hivyo sikuhitaji kuwa malikia, kwani ningeliolewa tena, na mimi sikutaka kuolewa,tena, baba yako alikuwa ndiye mume wangu pekee, alipofariki, na mimi nilitaka nimfuete, ….nilitaka kujiua, na hilo tendo likaniondolea sifa ya kuwa malikia wa eneo letu’akasema.

Leo hii hakuwa anagiza, alitakiwa afanye kweli, kama alivyokuwa akifanya bibii yake, kuvaa kutembea, na kila kitu, vinginevyo akijulikana atakuwa chakula cha mamba na atamkosa yule aliyempenda,na kuwaaingiza wengine kwenye matatizo makubwa akaona kumbe kabeba dhamana kubwa, na ni lazima aitekeleze.

Akawa anawaza jinsi gani alivyofamyia bibi yake, na ilibidi afanye hivyo,kwani bibi yake asingelikubaliana na hayo anayotaka kuyafanya, akawa ana wasiwasi, akiogopa kuwa huenda dawa aliyompulizia bibi yake inaweza ikwa nyingi, tofauti na walivyoagizwa na kama ni nyingi inaweza kumuua kabisa bibi yake, kitu ambacho asingeliweza kukivumilia, kwani kama bibi yake atakufa na yeye itabidi ajiue.

‘Umpulizie kidogo tu bibi yako kwa mbali asiokuone, na akilala, chukua nguo zake, na mengine ni kama nilivyokuagiza’akakumbuka alivyoelekezwa, na hayo hakutaka kuelekezwa zaidi kwani yeye ni mtaalamu wa kuigiza, kama angelipewa nafasi hiyo angelikuwa muigizaji wa kimtaifa.

Akaingia ndani ya lile jengo na yule jemedari akainama na kumruhusu apite, hakuamini kwani sifa za huyo jemedari ni kuwa anaweza kunusa kuwa huyu ni adui, …lakini aliona ajabu ya huyo jemedari kuinama na kumuheshimu akijua kuwa huyu ni mama tibabu, bibi yake. Yeye akapita na kuingia ndani ya jengo hilo. Alipoingia huyo jemedari alikuwa nyuma yake, akachungulia mara moja kuhakikisha kila kitu kipo tayari, halafu akasema;

‘Kama unahitaji msaada wowote niite nipo hapo nje’akasema huyo jemedari , na yeye akatikisa kichwa huku akijifanya yupo kazini, kwa kuushika shika ule mwili, hadi alipohakikisha kuwa yule jemedari katoka nje. Akashisha pumzi kwa nguvu huku akimshukuru mungu wake!

Aliushika ule mwili na kuanza kuuvua nguo zote, akaupaka dawa ya kulainisha ngozi kama alivyoagizwa, halafu akazivua nguo zake na kuuvalisha ule mwili, na yeye wakati huo ameshavaa nguo za ule mwili, na alipohakikisha kuwa kila kitu kipo tayari, akauchukua ule mwili na kuulaza chini, huku akiwa kaufunika uso, na kuhakikisha kuwa hakuna atakaye gundua haraka ni nani huyo binti. Kawaida mwanamke anajifunika mwili mzima, na nguo zao maalumu za ngozi za wanyama laini.

Alipohakikisha kila kitu kipo tayari, akapanda kitandani, na kuchukua dawa kiasi kwenye kidole chake ile nyingine akawa kaificha ndani ya nguo zake akalala na kujifunika uso kama ulivyokuwa ule mwili, akaivuta ile dawa puani, na huku akapiga ukelele….akazama kwenye giza.

*******

Huku nje mume wangu alikuwa keshafika na vijana wenzake wakiwa wamejificha sehemu maalumu na kuvaa mavazi wanayotumia maadui zao, kwani kila ukoo ulikuwa na uvaaji wake,wakawa wanasubiri sihara, ishara ambayo ni kilio,..

Babu alikuwa na kikao maalumu na wazee wenzake kweye shemu maalumu, sehemu ambayo haingiliki ovyo, na hata watu wakipiga kelele huko nje huwa hawasikii, na kuna vijana wakuleta taarifa kama kuna lolote limetokea, wao walikuwa kwenye mazungumzo maalumu na wazee wenzake;

‘Jamani mimi niewaita, maana siku moja niliwauliza kwanini mwenzetu anatayarisha jeshi msituni, nyie mkasema ni jeshi la ukoo, sasa wakati umefika wa kumuuliza kuwa je hilo jeshi kama ni la koo zote mbona hawachukui vijana wa ukoo nyingine’akasema.

‘Kwani tuna wasiwasi gani, kama anataka kuleta fujo sisi tuna vijana wetu, na swala la kuwaita na kuwaandaa, na hilo haliwezi kutokea maana tuna kiapo kikuu, akikiuka wenzetu watakuja atashikwa na vijana wake watatupiwa mamba’akasema mzee mmoja.

‘Muwe na akili yakufikiri, hivi akishavamia na vijana wake, akahakikisha amechukua madaraka, na kutumaliza sisi wazee wote, akapata kura za wazee wenzake, ni nani atapata muda wa kwenda kutoa taarifa, na hata hawo wakifika huko hamuoni kuwa atakuwa keshajipanga na uwongo mwingine’akasema babu.

‘Tukuulize wewe mzee mwenzetu una lengo gani kusema hivyo, una wasiwasi gani au umekuja na hoja gani?’ akaulizwa.

‘Mimi hoja yangu ni kuwa na kikosi chetu kama hicho, na tukiulizwa majibu yetu yatakuwa kama wao, na vijana wetu wapo tayari muda wowote, ni kiasi cha kuwapa maelekezo’

‘Hilo ni wazo jema sana, na hata mimi nilikuwa nikiwaza hivyo hivyo..’akasema mzee mwingine.

‘Jingine ni kuhusu huo mwili waliouchukua kama ushahidi, ….nahitaji msaada wenu, hapo muda ukifika,kuna jambo nalifuatilia kwanza, hilo sitawaambia kwa sasa.Nafanya hivyo kwasababu tunahisi wenzetu wana lengo kubwa, na lengo lao ni kuhakikihs kuwa ukoo wetu hauna nafasi ya madakara, kwahiyo tunachohitaji ni kuhakiksiha kuwa huo mwili unarudi mikononi mwetu’akasema babu.

‘Kwa vipi naye kaushikilia na kuulinda kwa nguvu zote…na kwanini tuhangaika na maiti,?’akaulizwa.
Hilo nitakuja kuwaambia baadaye ni kwa maslahi yetu sote, vijana wetu wapo, wataifanya hiyo kazi, ila lolote litakalotokea naomba tuwe pamoja’akasema babu.

‘Tupo pamoja mkuu wetu’wakaitikia na mara akaingia kijana mmoja akihema

‘Vipi kuna nini huko?’ akaulizwa.

‘Kuna ukelele umetokea upande ule wa maadui, na huenda kuna tatizo, ..’akasema huyo kijana mtoa taarifa.
Wale wazee wakainuka na kutoka mle ndani na kuelekea huko ulipotokea huo ukelele.

WAZO LA LEO:Sio vyema ukitenda kosa kumsingizia mwenzako, kama umeona umetenda kosa ni vyema ukakiri kuwa umekosea ili kusahihiswa, unapolisukumia hilo kosa kwa mtu mwingine unakuwa umetenda kosa mara mbili, kosa la awali ulilolitenda na kosa la kumsingizia mwenzako, huo ubaya ni roho mbaya, kumbuka kutenda kosa sio kosa, bali kurudia kosa ndio kosa.


Ni mimi: emu-three

Monday, October 29, 2012

Uchungu wa mwana aujuaye ni mzazi-15




Mume wangu alipopata taarifa hiyo toka kwa babu kuwa huyo msichana aliye mchukua bado yupo hai, wakati yeye alijua kabisa kuwa kabeba maiti, na huenda kumbe huenda huyo msichana ndiye yule aliyewahi kutabiriwa kuwa atakuwa maliki wa koo zao, na kwahiyo atakayemuoa , anayakiwa kumwa kiondozi wa koo zote.

Kawaida kablahili lenye koo ndogo ndogo nyingi,huwa zinamchagua mama , au malikia ambaye anapewa heshima kama mama wa kabila, mama ambaye anaheshimiwa kama mkuu wa kabila, ni sawa na kuitwa mfalme.  Mume wake ndiye mtawala wa kabila na ndiye amiri jeshi , kiongozi wa mapambano, ..pamoja na sifa nyingine anatakiwa awe keshawahi kupambana na simba peke yakem na kumuua,

Mume wangu alishapitia mitihani hiyo, alishawahi kumuua simba peke yake, lakini pamoja na hayo asingeliweza kuingia kwenye eneo takatifu mpaka mambo mengine ya kiutawala yapitishwe, kama vile kukubaliwa na nusu ya wajumbe wote, na asiwe na sifa zozote mbaya, ikiwemo kuchafua eneo takatafu kwa matendo yasiyokubalika.

Kutokana na utabiri wa mtabiri mkuu, ambaye alipokuja kuwatembelea wakati wanazindua eneo hilo jipya,aliwaambia ukoo huo ili uwe na nguvu, utahitajika kumpata malikia, lakini malikia huyo hatatokana na wao,..licha ya kuwa damu ya asili ni wao, lakini atakuwa kazaliwa sehemu nyingine, huyo atakuja hapo kwa njia ya kipekee kabisa….’huyo mtabiri akasema na walipomuuliza njia gani hiyo ya kipekee, alisema;

‘Hayo mambo ya ndani sana, hata mimi siwezi kuyajua, ila ujio wake, sio wa kawaida, na juhudi zenu ndizo zitamfanya aweze kuolewa na miongoni wa vijana wenu, na huyo kijana muda wake ukifikia, kuwa mtawala, atamiliki eneo hili, ila itachukua muda mpaka kukubalika…’akasema.

Waliambiwa akifika hapo kutatokea mambo mengi, ambayo yatakuja kijileta yenyewe hadi ifikie hatua ya kutawaza kuwa malikia, lakini yote hayo yanategemeana na juhudi za kila ukoo ili mmoja wa kijana wao aweze kuwa mume wa huyo binti. Mume wake atakabiliwa na mitihani mingi, lakini mwisho wa siku ndiye atakayekuwa mtawala wa eneo hilo, hapo umri ukifikia.

‘Babu isije ikawa mimi ndiye niliyetabiriwa na huyo binti ndiye malikia mtarajiwa?’ akasema mume wangu.

‘Usiitoe hiyo kauli tena, kama ni wewe hayo yatajileta yenyewe, maana wenzako wakisikia hilo, watafanya kila mbinu kuhakikisha kuwa huyo binti, wanampata wao, au ikishindikana wakiona hawatampata wao wanaweza hata kumuua,.. hilo hakuna mwenye uhakika nalo kuwa ni nani aliyetabiriwa ni siri kubwa sana, hata huyo mtabiri hajui ni nani mstahili…’akasema babu.

‘Cha muhimu kwa sasa ni kuhakikisha tunamuokoa, na hapa la muhimu zaidi ni muda, ..kwani ikifika saa kumbi mbili, hatutaweza kumpata tena, na huenda ikawa ndio mwisho wake wa kuishi, sasa tutaingiaje mle ndani,..?’ akajiuliza babu.

‘Babu kama ni hivyo,basi tutumie nguvu,mimi nitawatayarisha vijana wenzagu tutavamia na kumteka huyo binti’akasema mjukuu.

‘Hilo likitokea hiyo sifa ya huyo mtu wa kumuoa huyo malikia itakuwa imefutika, na ukumbuke kuwa mwenzetu alishajiandaa kwa lolote lile, kama unakumbuka vyema,siku za nyuma hapa mwenzetu huyu amakuwa akiandaa jeshi , mapaka tukawa tunajiuliza lengo lake hasa ni nini, wakati tumeshasuluhishwa, na wote kwa hivi sasa bado wapo maporini wakijifunza mbinu za kivita, wameandaliwa tayari kwa lolote,akitoa amri wataibuka toka huko mafichoni,…’akasema babu.

‘Sasa tufanyeje?’ akauliza.

‘Wewe ndiye unatakwia kufikiria, ujue mtawala bora ni yule anayefikiria zaidi ya wengine, na mawazo yake yanakuwa na tija, ..hasa kipindi kama hiki, amacho kila mmoja anakuwa na mawazo yake, ubinafsi mwingi, na kila ukoo unavutia kwake, lakini mtawala bora mwenye hekima ataweza kuwaunganisha na kuwa kitu kimoja, bila kujali tofauti zao…’akasema babu.

‘Sawa nimekuelewa babu, naomba nikayafanyie kazi mawazo yako, ngoja niwahi, maana naona muda unakwisha, na tusipofanikiwa hili, moyo wangu utauma sana,kwani mimi ndiye niliyemchukua binti wa watu nikijua kuwa ni maiti, kwahiyo lolote baya likitokea nitakuja kujilaumu kwenye nafsi yangu, licha ya hayo mengine, ..’akasema na babu yake akamshika kichwa, ishara yao ambayo inajulikana kama ishara ya baraka.

Alipoondoka,  babu akabakia akiwaza jinsi gani ya kuingia mle ndani, lakini akilini mwake akajua kuwa mjukuu wake atafanikiwa, cha muhimu yeye ni kuhakikisha kuwa anaweza kuwashawishi wazee wengine ili wamuunge mkono.Akainuka na kuelekea eneo lao walijualo kama eneo takatifu.

*********

Katika upande wa pili, nyumbani kwa mpinzani, kulikuwa na punda wa kimila, punda huyo alikaribia kujifungua, na anatakiwa akijifungua,maziwa ya kwanza yanyewe na mzee wa kimila na ya pili yanyewe na kijana ambaye wanamtambua kama mtarajiwa wa kuingia kwenye uongozi , na muda wa kumtafuta kijana kama huyo ulishakaribia.

Wao kama wazee kazi yao ni kutoa maelekezo, na vijana ndio watenda kazi, na ili hilo lifanikiwe ni lazima awepo jemedari, jemedari huyo ni yule atakayemuoa malikia, malikia ndiye mama mtawala, anayeheshimika, mlezi wa koo zote.

Babu ambaye ni mpinzani wa mume wangu alikuwa haondoki kule makao makuu kwa ajili ya kulinda mwili ambao alishauona ni ushahidi wa kummaiza adui yake kisiasa. Yeye kutokana na taarifa na ushahidi alio nao, alishaliona kuwa mpinzani wake ana makosa, na akiweza kuuwakilisha mbele ya wazee wenzake, mwenzake huko atafukuzwa, na kijana wake anayemtegemea anaweza kuhukumiwa kuwa chakula cha mamba.

Lakini kuna mambo ya kimila ambayo katika ukoo wake, inabidi ashiriki, kwao waoo punda ni mnyama muhimu sana, akijifungua, wanaona ni sehemu ya baraka, na maziwa yake, yanachukuliwa kama dawa, pia kama maziwa ya baraka. Na yeye kama mkuu wa ukoo, anatakuwa awe wa kwanza kuyanywa , na kuhakikisha kuwa mjukuu wake ambaye ndiye waliyemuandaa kwenye kugombea ujemedari wan a uongozi wa kabila anakuwa wa pili kuyanywa hayo..

Alishawaambia nyumbani kwake, kuwa huyo punda akikaribia kujifungua aitwe haraka, lakini akajikuta ana akzi hiyo muhimu ambayo aliihitaji yeye mwenyewe aisimamie, kwani wengine wanaweza kushawsihika wakaachia nafasi muhimu kama hiyo. Akawa anawaza je ikitokea huyo punda akajifungua siku hiyo atafanyeje, kwani yote hayo yanamuhitaji yeye, alipowaza hilo akamuita mmoja wa makamanda wake, akamwambia;

‘Huenda nikaitwa nyumbani, nikiondoka hapa nataka wewe ubakie hapa mlangoni, hakikisha haingii mtu yoyote humo ndani, hasa hawa wapinzani wetu, mtu utakayemruhusu kuingia hapa ni yule mama tibabu ambaye anatakiwa kuhakikihsa humo mwili hauozi kabla ya wakati wake…..’akatoa amri.

‘Sawa mzee,mimi nipo kwa ajili yako’akasema huyo jemedari ni kutoka nje akisubir amri nyingine.

********
Wakati huo huo, mume wangu alifika eneo ambalo ni la ukoo wa maadui zao, kipindi cha nyuma walikuwa wakitembeleana, lakini ni kwa nadra sana na kwa kificho, na akiingia mtu wa upande wa pili anaangaliwa kwa makini ili watu wajue nini anachofuata. Mume wangu alitumia mbinu za kificho asionekane, akijua kuwa akionekana anaweza hata kuuwawa.

‘Bibi Kis, najua unampenda mtoto wa mzee, adui wa ukoo wetu, lakini yeye hakupendi kwa vile unatoka katika familia ya kimasikini, leo nimekuja na jambo litakalokuwezesha kuolewa na huyo unayempenda, ikifuata masharti yangu’akasema mume wangu baada ya kuweza kupenda hadi kwenye familia hiyo kwa uficho, na akatafuta mbinu za kumuita huyo binti, kwenuye kichaka, ambapo walianza kuongea kwa sauti ya chini kwa chini.

Binti huyo alikuwa miongoni wa warembo wa hapo kijijini,na alikuwa miongoni wa ukoo wa babu adui wa ukoo wa mume wangu.Binti huyo, aliwahi kukutana naye kipindi cha nyuma na mume wangu alitokea kumpenda sana, lakini kutokna na hisitoa ya uadui wao, hakukubaliwa kumuoa, kutoka kwao, na kutoka kwa koo hiyo ambayo ni adu mkubwa wa ukoo wao. Kutokana na uadui wao, hakuna aliyejenga nyumba, ambazo ni ni mahandaki mlango, ukaelekea upande wa maadui zao.

Huyu binti hakuwa akimpenda sana mume wangu, kwasababu hizo zakihistoria, alijua hawezi kuolewa naye tena, akawa akimpenda sana mtoto wa babu huyo adui wa ukoo wa mume wangu. Na mapenzi yao yalifikia hadi kutaka kuoana, lakini walipolifikisha hilo mbele ya wazee wa ukoo, wakalipinga, wakidai kuwa huyo binti hastahili kuolewa na huyo kijana, kwani hana sifa zinazotakiwa,kwani malkia mtarajiwa anasubiriwa.

‘Na ukumbuke familia zote hapa, koo zote hapa, zinamsubiri malikia mtarajiwa ambaye tumeambiwa atakuja kwa njia ya ajabu, wewe sio huyo malikia, maana wewe ni mzaliwa wa hapapapa,na huyo malikia atakuja kutoka nje,ndiye atakayeolewa na kijana wetu,…’akaambiwa,

Wazee hawo wakisema neno, linakubalika mara moja, hakuna anayepinga, kwani ukipinga lazima utakutwa na mambo mabaya, ambayo yanaweza hata kuimaliza familia nzima kwa vifo vya ajabu ajabu au magonjwa yasiyotibika. Huyu binti alijua hilo, kwahiyo akatulia na kusubiri mume mwingine, lakini alipokuja huyo mume mwingine ambaye ndiye mume wangu, akakataliwa nay eye, hapo akakata tamaa.

Aliwauliza wazazi wake, je ina maana yeye hataolewa tena, maana watu wawili aliowapenda wanakataliwa. Wazazi wake wakampa matumaini kuwa ipo siku atakuja ambaye anamfaa, anachotakiuwa ni kuvuta subira.

*******

‘Wewe umefuata nini tena hapa, hukumbuki tulivyoambiwa kuwa nyie ni maadui wa ukoo wetu, hustahli kunioa, kama isingelikuwa hivyo, ningekubali unioe kuliko kubakia hapa nyumbani, wenzangu wote wa umri wangu wameshaolewa, mimi kila mume anayekuja kunitaka kunioa nakataliwa…’akasema huyo binti.

‘Usijali binti, kila jambo lina muda wake, na natumai sasa utaolewa, lakini yote inategemea ujasiri wako,…’akaambiwa. Yule binti, akashikwa na mshangao, akatizama huku na kule akiogopa asije akaonekana, kwani alishabigwa marufuku kukutana na huyu mwanaume aliyesimama mbele yake,akauliza kwa mshangao

‘Ujasiri  gani huo!?’ akauliza.

 Walikaa kwa muda huku mume wangu akimuelekeza nini cha kufanya , na yule binti alipoelewa, akakubali, na kusema yupo tayari kujitolea kwa hilo ilimradi, ahakikishe kuwa mwisho a yote hatapata madhara.

‘Kiutaratibu, wewe hutadhurika,kwasababu kwaza huyo atakaye kuoa anakupenda, na mambo yakikamiliak na kufanyika ndani ya jengo takatifu, hayastahili kutenguliwa tena,…na hilo lutachukuliwa kama majaliwa ya wazee, na mzimu ya hapo, …cha muhimu ni kuhakikisha mbinu hizi unazifuatilia hatu kwa hatua, bila kutetereka.

‘Sawa, ngoja nikajiandae, na najua bibi yangu anazo hizo dawa, ….’akasema akijua kuwa bibi yake ndiye tibabu wa ukoo kwa wanawake, na ndiye peke yake aliyeruhusiwa kuingia kuuona huo mwili, na bibi yake ni mtiifi mkubwa wa wazee, na anatambulikana na kuheshimika. Alijua atamdanganya hatamwambia ukweli nini anachotaka kufanya.

‘Dawa sio shida dawa hizi hapa ninazo..’akasema huku akimkabidhi vifurushi vidogo viwili vya dawa huku akisema;

‘Hii dawa ya jani hili lililokaula ni ya kumzindua huyo binti ni ya unga unga, imo humo ndani, na akishazindukana, wewe utapiga ukelele, …’akasema kwa haraka haraka, na yule binti akatabasamu, na kusema;

‘Nimekuelewa, …najua kwanini nipige ukelele, ili waingie, wakiingia, mimi nitakuwa nimechukua nafasi ya hiyo wanayoiita maiti, lakini je wakinichunguza, si wanaweza kunigundua kuwa ni mimi , ndoa itafungwaje na pia, huyo ….hiyo maiti itakayofufuka, isipofuata hayo ,mnayotaka nyie, yafanyike itakuwaje?’ akauliza.

‘Hayo hayatakuhusu tena, kuna watu watakuwa wanafutailia kila hatua, …wewe usiwe na shaka’akaambiwa.

‘Basi kama ni hivyo tu, mbona rahisi sana …, mimi nipo tayari kufanya lolote ilimradi nihakikishe nimeolewa na yule mume, lakini kikwazo ni babu yake, …namuogopa yule mzee,mpaka wakati mwingine namuota kama shetani, ananijia huku akinitisha, ..lakini licha ya hayo yote, nina uhakika nikishaolewa pale watanifurahia baadaye kuwa kweli wamepata mke…’akasema huku akitabasamu kwa furaha.

‘Lakini kumbuka maelekezo yangu,kwenye hiyo dawa ya pili, hiyo ina nguvu sana, ukishainusa tu puani kwako, unakuwa kama umekufa….kwahiyo hakikisha kuwa kabla hujainusa,uwe umeshajiandaa, uwe umeshavaa nguo za huyo binti, na uwe umeshalala sehemu yake, kwani ukiivuta tu, utashikwa na usingizi mnzito sawa na mtu aliyekufa…’akaambiwa.

Yule binti kwanza akasita akiwazia hilo neno kuwa atakuwa kama mtu aliyekufa,akajiuliza je wasiponiwahi ndio maana nimeshakuwa marehemu. Lakini wasiwasi huo ukaondolewa kwani aliambiwa;

‘Usiwe na wasiwasi, utawahiwa kama sio wao, mimi mwenyewe nitakuja kukunusisha hiyo dawa ili uzindukane, kwani  kuinuka kwako ni  mpaka kukunusisha dawa nyingine, na hilo litafanyika tu usiwe na shaka’ Binti aliposikia hivyo akaichukua zile dawa, huku akiwa na mawazo mengi kichwani.

Baadaye wakaagana na huyo jamaa,ambaye ndiye mume wangu, na akarudi nyumbani haraka, alipofika nyumbani kwao,kabla hajapumzika tu ili ajiandae kwa kazi hiyo aliyopewa, akasikia hodi, na alipofungua mlango akakutana uso kwa uso na babu , babu ambaye amekuwa kikwazo katika mapenzi yake na mjuuku wa huyo babu, akahisi mwili ukiisha nguvu, akatoa macho kwa woga na kabla hajasema neno,yule babu akasema;

‘Nimekuja kukupa onyo…nimesikia kuwa wewe ni msaliti,wewe unatoa taarifa zetu kwa maadui zangu , kwa yule kijana, wao, ….kwanza nimeshakuambia, kuwa hatutaki kabisa ukoo wetu kuolewa huko, …pili wewe hustahiki kuolewa na mjuu wangu, kwasababu ambazo huhitajiki kuzijua..‘akasema huku akiwa katoa macho , macho ambayo binti huyu alikuwa akiyaogopa kama nini.

‘Sasa siku nikikufuma na huyo kijana, siku nikipata ushahidi, nitahakikisha unakuwa nyama ya mamba, nitakubeba mwenyewe na kuhakikisha umetafunwa hadi mfupa wa mwisho…’akasema huku akimnyoshea fimbo yake iliyovikwa ngozi ya nyoka.

‘Kama nikuolewa utaolewa na kijana yoyote wa ukoo wetu, ..lakini sio mjukuu wangu, hilo ulisikie na uliweke akilini, unasikia?’ yule babu akasema huku akitoa macho yake ya  kutisha,na hakusubiri yule binti atamke kitu, akageuka na kuondoka, na kumuacha yule binti akiwa anatetemeka mwili mnzima.

NB: Umeme umekuwa kikwazo, lakini hiki kipnde kwa leo kinatosha.

WAZO LA LEO: Mitihani ni sehemu ya maisha, tunahitajika kukabiliana nayo, tukijua kuwa mungu yupo pamoja nasi wakati wote, tuzidi kumuomba kila mara, ipo siku tutafanikiwa, tusikate tamaa.
Ni mimi: emu-three

Thursday, October 25, 2012

Uchungu wa mwana aujuaye ni mzani-14



Sasa turejee kule porini, kama mnakumbuka, yule mwanadada aliyemuokoa Maua, ndio alikuwa akihadithia kisa cha maisha yake, jinsi gani alivyoweza kuingia mikononi mwa hawo watu wa msituni. Na ukumbuke kipindi kirefu kimepita na sasa Maua keshafikia muda wa kujifungua, na anatakiwa kupelekwa karibu na lile bwawa la Mamba, ambapo anatakiwa akijifungua tu, hata damu yake haitakiwi iguse ardhi ya kijiji hicho.

Wao wana imani kuwa damu ya watu waliopotea na wakawa wametenda kosa ni najisi kubwa sana,inaleta mikosi, lakini ikifika mdomoni mwa mamba,mkosi ule hugeuka na kuwa ni baraka. Ndio maana Maua alitakiwa akijifungua tu,yeye atupwe ndani ya huo mto, akaliwe na mamba, ili kuleta baraka badala ya mikosi.

Hili lilikuwa likifuatiliwa kwa karibu sana na wazee wengine ambao ni wapinzani wa babu  wa mume wangu. Hayo yalifanyikwa kwa vile, kuna kugombea madaraka na visasi vya kihsitoria, vilivyokuwepo ndani ya eneo linalojulikana  kuwa eneo takatifu, Eneo hilo liliundwa na wapinzani wa kivita wa siku nyingi. Ilibidi ifanyike hivyo, ili kuweza kukutanisha koo zote na kuwa kitu kimoja, lakini hisia zilizopita zilikuwa bado mioyoni wa miongoni wa wakuu wa koo. …’akasema yule mwanadada wakati anamsimulia Maua.

‘Maua alitulia akivumilia uchungu uliokuwa ukiongezeka kila dakika, aliona ni heri avumilie hata kama ni kujifungulia hapo hapo, na yule mwanadada alikuwa akindelea kuelezea maisha yake.Moyoni mwa Maua aliona kama ingeliwezekana angejifungulia pale pale, lakini haikuwa rahisi hivyo,kwanii huyo mwenyewe anayemuhadithia alishapewa onyo kali,kuwa damu ikimwangika humo ndani, basi na yeye anatakiwa kuwa chakula cha mamba.

Yule mwanadada akatulia kidogo alipomuona Maua akikunja uso kwa maumivu, akamsogelea na kumchunguza, akatikisa kichwa kuashiria kuwa sasa muda unakaribia, na akawa kama anakumbuka jambo,akamwangalia Maua kwa macho ya huruma, lakini hakujua afanyeje, akasema;

‘Itabidi utusamehe tu,kwani kwa hali ilivyo, sijui kama mume wangu anaweza kufanya jambo lolote, kwani hadi sasa hajarudi,ina maana wamemkatalia, au kazuiliwa huko huko, hadi wahakikishe hilo wanalotaka kufanya limekamilika…’akasema.

‘Wewe usijali endelea kunisimulia, nikikusikiliza nasahau machungu, ingawaje hayasahauliki, ….endelea pale ulipoishia ulipoteza fahamu ukiwa umeshajitundika juu ya mti, ilikuwaje baada ya hapo?’akasema Maua akijafanya hasikii maumivu, lakini ….

‘Mimi nilipozindukana tu, nilijikuta nipo sehemu ngeni kabisa, maana ni kama upo kwenye kaburi, na na ndivyo nilivyoanza kuwaza kuwa nimeshazikwa sasa nipo kaburini, na kama kuna watu karibu, hwo ni malaika,  akili ilikuwa siyo yangu, na nilizindukana baaada ya kupiga chafya mara nyingi, na kila nikipiga chafya ndio akili inakuwa kama inazindukana.

Na kabla sijaelewa nini kinachoendelea mara nikahisi mtu yupo karibu yangu, kwanza mwili ulisismuka, nikajaribu kuiweka akili yangu sawa, je nipo hai au ni maiti, nikahisi huyo mtu akinisogelea, alikuwa ni mwanaume,lakini nilikuwa sijaweza kumuona sura yake vizuri akasema;.

‘Mimi ndiye niliyekuokoa ukiwa pale juu ya mti ,na kiiutaratibu natakiwa mimi niwe mume wako..’akasema na kunishika usoni,

‘Kwanini mnifanyie hivi, na utanioaje bila ya rizaa yangu, na hapa nipo wapi?’ akauliza huyo mwanadada.

‘Kuna mawili ya kuchagua ukatupwe kwenye mamba uliwe kama kafara au uolewe na mjukuu wangu, na hili linatakiwa lifanyike haraka sana,kabla ya saa kumi na mbili’ nikasikia sauti nyingine ikitokea humo humo ndani sikuweza kumuona muongeaji.

Na huyo alikuwa akiongea kwa lugha ya kwao iliyochanganyika na lugha ya kwetu. Hawa watu wanaweza kuongea lugha yao na lugha yetu kidogo, na nilikuja kugudua baadaye kuwa huyo alikuwa ni babu yake. Na wakati huo akili yangu ilikuwa haijakaa sawa, pale nilijua kuwa mimi na maiti tu, na kwahiyo mimi sina cha kuamua ni kuacha hawo watu sijui ni malaika au ni wachawi, wafanye wanalolitaka.

‘Ina maana mimi hapa ni maiti?’ nikajiuliza na kabla sijapata jibu, nikahisi mkono ukinigusa usoni. Ulikuwa mkono ulikakamaa,na ulikuwa na manyoya, nikashituka na kuinuka kwa haraka nikiwa naogopa, nikihisi huenda ni mnyama. Na hapo nikakumbuka ya nyuma, kuwa mimi nilikuwa nimejinyonga, na mimi ni maiti na huenda hawa watu ni wachawi, wanaokwenda kwenye makaburi na kufufua watu. Nikiwaza hivyo sijui kwanini.

‘Usiogope …’sauti ikasema na maneno mengine ambayo sikuweza kuyaelewa maana yake . Nikatulia na kusema kimoyo moyo, toka lini maiti ikaogopa, nikageuza kichwa na kumwangalia huyo mtu au mnyama, nilikuta ni sura ya mtu, mwanaume.

‘Nilikuona ukiwa umening’inia juu ya mti na kamba ikiwa imekukaba, ikiwa na maana kuwa ulikuwa umejinyonga au kunyongwa, sasa….’sauti ikasema na kufuatiwa na maneno mengine nisiyoyafahamu vyema, ilikuwa lugha ya hawa watu ambayo nilikuja kujifunza baadaye, kumbe alikuwa akiniambia kuwa yeye wakati anapita kutoka mawindoni, aliniona nikiwa nimening’inia kama mfu,  akapanda haraka juu ya mti na kukata ile kamba.

Aliniambia kuwa, alishajua kuwa nimeshakufa,kwahiyo nia na lengo lao ni kunichukua mimi nikawe chakula cha mamba. Wao wana imani yao kuwa wakiona mtu wa aina zetu na kumpeleka kwa hawo mamba akamtoa kuwa chakula cha mamba inakuwa kafara na akiomba shida yake, anafanikiwa. Na yeye kwa muda hup alikuwa na shida sana, alikuwa hana mbele wala nyuma.

Akaniambai kwamba, alinichukua akanibeba,na kuanza kukimba naye hadi huko msituni, na waakti anafanya hivyo, alikuwa akiogopa wenzake wasimuona, kwani wakmuona itatokea vita tena ya kumgombea, kwani kila mmoja alikuwa katika mpango wa kuwinda watu wa namna hiyo, ili wafanikiwe, ndio imani zao.

Anasema lakini hata hivyo, ili afanikiwe ni lazima akutane na mmoja wa wazee wao, anayeheshimika yeye atafanya mambo yao, na matambiko yao, ili hata mwili wangu ukikabidhiwa kwa hawo mamba maombi yafanye kazi vizuri, na ili afike huko lazima atakutana na walinzi watiifu wa hawo wazee.

Kwahiyo alichofanya kwanza ni kuufikisha mwili wangu kwenye pango lake, humo, akanivikwa nguo za ngozi,ili kunificha, halafu ndio akanibeba, kwahiyo njiani walijua kwua kambeba mgonjwa au mtu wake, na kweli kila aliyekutana naye, alimwambia kuwa huyo ni mgonjwa anampeleka kwa tibabu wao, na walipotaka kumsaidia alikataa.

Basi akafika huko kwenye eneo ambalo wao wanaliita eneo takatifu, ni eneo wanapoishi wazee na wakuu wa jadi. Na kwa vile yeye mwenyewe ni ukoo wa wakuu wa jadi, haikuwa vigumu kwake, aliweza kuingia hadi sehemu inayostahili, akauweka mwili wangu, na kumtafuta mtu wake ambaye nib au yake, mmoja wa watu mashuhuri humo.

‘Babu nimekuja, nimekuja kwa jambo muhimu sana, kama unajua hali zetu kwa sasa ni ngumu, na inavyojulikana tunatakiwa tutafute damu ya kuwapa mizimu yetu na damu nzuri ni ile ya hawa watu wa waliopotea,’akasema.

‘Kwahiyo umeshampata ?’ babu akamuuliza.

‘Ndio nimempata..’akasema.

‘yupo wapi, ni mwanamke au ni mwanaume?’ akaulizwa

‘Ni mwanamke’akasema na babu yake akahema,kwa muda, akazungumza maneno yao ya maombi, halafu wakaongozana hadi pale alipokuwa kaniacha, lakini alipofika pale hakunikuta. Ikabidi ashituke na kuanz akutafuta huku na kule.

‘Niliuacha mwili wake hapa, kuna mtu kauchukua’akasema na msakao ukaanza , na sikuweza kuonekaan kwa haraka, ndipo babu akaitisha kikao cha haraka cha wazee humo ndani, na babu alikuwa mmoja wa wakuu, anayeheshimika, wakuu mle wakakutana na kuanza kusikiliza hilo tatizo.

‘Jamani mnajua hapa ni sehemu takatifu, na tendo lililofanyka hapa ni tendoo ambalo halistahili sehemu kama hii, kwanza kabla ya yote naomba yule ambaye aliuchukua mwili wa kafara ulioletwa na mjukuu wangu ajitokeze kabla hatua nyingine hazijachukuliwa.’ Babu akasema na watu pale walikuwa wakimuogopa sana.
Mara akatokea mmoja wa wazee wa pale, ni mkuu na yeye, akakohoa na kusema kwa sauti ya kutisha,;

‘Una uhakika na hilo unalotaka kulisema; kuwa mwili wa kafara uliletwa hapa, huoni kuwa unakwenda kinyume na maadili yetu, kuwa ili mwili utambullikane kama ni mwili wa kafara kwanza huyo mtu anatakiwa kweli alistahili kuadhibiwa, na pili kama keshakufa, uchunguzi ufanyike ijulikane kafa kwa kitu gani,na kabla ya kufa alikuwa na makosa, yanayostahili kuadhibiwa...na hili linatakiwa lipitie kwenye utaratubu wa mila na desturi zetu?’ akasema huyo mzee.

‘Kwanini nisiwe nauhakika wakati mjuu wangu ndiye aliyeuokota huko nyikani, na aliukuta ukiwa umejitundika, ina maana kuwa huyo mtu aliuliwa kwa makosa,au aliamua kujiua mwenyewe na hilo ni kosa,kwahiyo anastahili kuliwa na mamba wetu’akasema babu.

‘Naona mzee mwenzangu unaanza kukiuka mamb muhimu ya hapa , hii ni sehemu takatifu, na tunatakiwa tuihehimu, na ili mtu wa namna hiyo, akubalike kuwa anafaa kwa kafara ilihitajika tukutane,na tupitishe hukumu kwa pamoja je hilo lilifanyika?’ akauliza huyo mzee.

‘Hili lingelifanyika, nilitarajia baada ya kuuona huo mwili, niwaite tukutane, na nilipofika sehemu aulipowekwa huo mwili tukakuta haupo, je huoo mwili upo kwako?’ akauliza huyo mzee.

‘Kwanza tumalize moja, ukubali kuwa umekosea,’akasema huyo mzee ambaya mara nyingi amekuwa mpinzani wa babu wa mume wake,na wamekuwa wakishindania madaraka, na hata ilifikia hatua waliingia kwenye mapigano, kati ya familia hizo mbili.

‘Siweze kukubali makosa ambayo sijayafanya’akasema babu, kwani kama angekubali, ingebidi ashushwe daraja, kutoka kwa wazee wa juu hadi chini, ambapo asingeliruhusiwa kuingia kwenye uongozi au kushiriki kwenye maamuzi ya kimahakama.

‘Basi mimi naomba tuitishe baraza la wazee tuhukumu hili, maana tukiliachia likiendelea kuwepo heshima ya mahali hapa itaharibika’akasema huyo mzee mwenzake na hata kabla hajajibiwa akatoka ikiwa na maana anakwenda kuwaita wazee wa mahakama.

Shauri likapitishwa kuwa kikao hicho kifanyike,a usiku, sasa ukumbuke mimi natambulikana kuwa ni maiti, je maiti ingeliweza kukaa siku tatu, maana hiyo ilikuwa siku ya tatu , tangu nichukuliwe kule nilipokuwa nimejitundika. Wao wana dawa za kuufanya mwili usioze, lakini mwili ukikaa zaidi ya siku tatuu haifai tena kwa tambiko.

‘Babu akajaribu kuwaona wazee wenzake kulielezea hilo, lakini ilishindikana kwana kauli ya huyo mzee wao inahehimika , kwa vile ana wafuasi ambao wapo nyuma yake na ambao ni nusu ya wajumbe, kwani kwa muda ule alishatafuta wazee wa namna hiyo waliomunga mkono, na wakizidi nusu basi ombi lake linakuwa na nguvu.

‘Mjukuu wangu naona hilo limeshindikana, na iliyobakia hapa ni jinsi gani ya kujilinda ili nisije nikashushwa daraja, na pia kuhakikisha hawa watu watoi adhabu kubwa ambayo huenda ikaleta majonzi kwenye familia yetu.’akasema Babu.

‘Babu nisamehe,sikujua kuwa ninaweza kukuingiza kwenye matatizo kama haya ..’akasema mume wangu

‘Ndio maisha mjukuu wangu, katika maisha mambo kama haya hutokea, cha muhimu ni kujipa moyo na kutafuta njia ya kukabiliana nayo’akasema Babu.

‘Sasa tutafanyaje?’ akauliza mjuu wake.

‘Hapa  kwanza niachie muda nifikiri, na nitalifanyia kazi hili jambo,  kwani ni lazima nifanye uchunguzi nijue ni nini kilitokea, na kama kuna jambo tulijue tutafanyaje,maana mwenzangu asingelifanya haya yote kama hana ushahidi na anajua kuwa hata nikifanay nini sitaweza kumshinda, kwanza inabidi nitoke, kidogo’. Ikabidi Babu atoke humo asafiri sehemu ya mbali kwa haraka.

‘Huko alipokwenda ni kijiji ambacho sheria nyingi za mila zao ndipo zilipoasisiwa, wao walihamia hapo baadaye ili kutafuta maisha lakini sheria zao nyingi zinatoka huko walipozaliwa mababu wa mababu zao. Huko alitakiwa kukutana na wazee wa jadi , na pia kuna wataalamu ambao huangalia matukio kwa mbali zaidi. Babu aliwaendea hawo akijua ndio kimbilio lake, ….

Babu alipofika huko kwa hawo wataalamu ndio wakamuelezea ilivyokuwa, kuwa huyo binti hana hatia, ni binti aliyenusurika na uzalilishaji , na hata kuzaliwa kwake ni mizimu yao iliyobariki, na ilijulikana kuwa ipo siku atarudi hapo, halafu aolewe... Na wenzake walishajua kuwa huyu anaweza kuwa mmoja wa warithi wa mama wa ukoo, na ndio maana na hastahili kutupwa kwa mamba, na wenzake wanalijua hilo...’

‘Kwa vipi aolewe maana sisi tujuavyo ni  maiti’akauliza babu.

‘Huyo binti hajafa, kapoteza fahamu tu, lakini kama ikifika saa kumi na mbili anaweza asizindukane kabisa, kitakachomuokoa ni dawa nitakazokupa wewe, hata wao hawajajua kuwa huyo binti anaweza kuzindukana kutokana na dawa maalumu, wangelijua wangeshafikia mbali kufanya mamboo yao….’akasema huyo mtaalamu.

‘Sasa cha muhumi hapa ni muda, kwanza chukua hizi dawa nenda kamnusishe puani, na akizindukana mfungisheni ndoa haraka, …’akaambiwa na babu akaingiwa na hamasa, kwani aliwahi kuota ndoto inayomuelekeza kuwa amtafutie huyo mjukuu wake mke, mke ambaye anaweza kusaidia familia yao kuwa watawala wa hilo kabila lao.

‘Lakini hilo linatakiwa lifanyike kabla ya saa kumi na mbili jioni , kwani  ikifikia hapo huyo binti hataweza kuzindukana tena, atakuwa keshakata roho, ..nyie cha kufanya ni kuhakikisha ndoa inafanyika,na baada ya ndoa inatakiwa kweli tendo la mke na mume liwe limeshafanyika, ili kuhalalisha na kuondoa kosa hilo ambalo mpinzani wako anataka kukushika nalo’ akapewa hayo masharti.

‘Lakini kwanini ,ina maana hawajui kuwa yupo hai, na kama wanajua hilo kwanini wanafanya hivyo makusidi ili huyo binti asizinduakne tena?’ akasema babu.

‘Hilo sio muhimu kwa sasa,….huenda bado hawajalifahamu hilo, kwasababu huu utaalamu tunazidiana, nyie fanyeni kwa upande wenu, ili mjiokoe, haraka, na mumuokoe huyo binti’, wa kusema lolote,..’akasema huyo mtaalamu.

‘Wenzenu hilo wamejpanga vyema,na mkifanya kosa, hamtakuwepo humo tena na mbaya zaidi yatawaandama, fanyeni muwezavyo, na swala la muhimu hapo ni muda.....’akasema huyo mtaalamu.
Babu aliondoka hapo akiwa na mawazo mengi, hakujua kuwa mwenzake kumbe muda wote huo, alikuwa abdo anamtafuta, yeye alijua kuwa wameshapatanishwa na uadui haupo tena, lakini kumbe wenzake wanahamu ya kuwaondoa humo kwenye uongozi na ikibidi waangamizwe yeye na ukoo wake.

 ‘Kwa jinsi ilivyo, na kwa vile ukoo wa huyu jamaa ni mkubwa na una wajumbe wengi, najua watampigia kura yeye ili aonekane ni mkweli’. Babu akachanganyikiwa maana huyo ni mjuu wake toka kwa binti yake kipenzi. Muda ulikuwa umekwenda kweli,na ilibidi arudi huko mapema, ili kumuokoa huyo binti, kabla hajafanyiwa lolote…

Babu alipofika tu, akamchukua mjukuu wake na kumsomesha, nini kinatakiwa kifanyike, kwa haraka, akawatafuta vijana wengine wawili wanaomtii  wa ukoo wao, na wakaanza kuutafuta mwili wangu ulipo, maana hadi muda huo nilikuwa kama maiti tu.

Walikuja kugundua kuwa nipo sehemu anayokaa huyo mshindani wake, ambapo ili uingie hapo nilipo  inabidi ukutane na huyo mshindani wake. Na yeye alijitahidi muda wote kuwepo hapo, na kama hayupo wanakuwepo walinzi wake watiifu.

NB    BLOG YENU INAWATAKIA IDD-EL HAJ NJEMA, 













Ni mimi: emu-three

Tuesday, October 23, 2012

Uchungu wa mwana aujuaye ni mzazi-13



Wazazi wangu walikaa muda mrefu baada ya kuoana bila kupata mtoto, wao wenyewe walijionea ni kawaida tu, wakijua kwa vile hawana tatizo lolote la kiafya ni swala la muda tu, kwani walishachunguzwa na kuonekana kuwa hawana tatizo. Wao walijipa matumaini kuwa ipo siku watapata mtoto, hawakujali sana, lakini ndugu na majirani, walikuwa ni tatizo, hawakuisha kuwasumbua, na ndio waliochangia hata wazazi wangu waanze kuhangaika.

Kuhangaika kwao ndio kunanitia uchungu,maana hata nikifika jijini,sipendi watu wanione,…wakiniona naangaliwa kwa jicho baya, nanyoshewa vidole,nanyanyapaliwa kwa kitu ambacho hata sikijui, na sina uhakika kama ni kweli au …mungu mwenyewe ndiye anajua.

Wazazi wangu walikuwa kila wakikaa, hodi ikipigwa, wanaogopa hata kufungua mlango,maana mtu akija mazungumzo ni hayo hayo,..

‘Nyie mbona hamzai,ina mana hamtaki watoto?’ wakawa wanaulizwa.

‘Bado hatujajaliwa, ipo siku tutapata watoto kwani yote ni majaliwa ya mungu’akasema mama na baba.

‘Nyie kaeni kusema hivyo hivyo…ni majaliwa ni majaliwa siku zinakwenda, mnatakiwa muhangaike, mengine yanahitajika kuhangaika, sio yote yaliyopo yapo kama yalivyo, kuna nguvu za giza, hangaikeni…’ siku alikuja mmoja wa ndugu zao, akawa anawashauri.

‘Lakini ndugu yangu, tumeshakwenda hospitalini wakatuchunguza afya zetu na kumchunguza mke wangu njia za uzazi, wakaona hakuna tatizo, na mimi mwenyewe walinichunguza wakaonahakuna tatizo, kwahiyo mimi nionavyo ni mipango ya mungu,’akasema baba.

‘Hili siwakatalii,huko ni kwa wataalamu wa kisasa, lakini zamani hatukuwa nao, tulikuwa na njia zetu za asili na zilikuwa zikitusaidia, wapo watu wa namna hiyo hadi sasa, wana dawa, wana njia za asili za kuzindua kizazi kilicholala, ‘akasema huyo mzee,

Hata alipoondoka wapendwa hawa wawili walikaa na kujadiliana, wakaona hayo yote ni majaribu, wakijikita kwenye mambo hayo huenda wakaingia kwenye mitego ambayo hawakuipenda. Wakakubalina wazidi kuvuta subira.

Wazazi wangu walikuwa ni watu wenye msimamo wao, na kwa vile walikuwa wameishi mjini Arusha na kuishi na wazungu, na wasomi mawazo yao yalikuwa hayafanani sana na pale kijijini, licha ya kuwa walikuwa mara nyingi wanarudi na kuishi hapo kijijini.

Baba yangu alikuwa mafanyabiashara, alianzia mbali sana, na kuna muda alikuwa tajiri ,kuna muda alifirisikia , kwahiyo alikuwa akijua amisha yote, na hakuwahi kukata tamaa. Na kipindi hichoanasakamwa, alikuwa yupo kijijini, alikuwa kafungua duka kubwa hapo kijijini.

Mama naye hakukosa watu wakumshauri,na siku hiyo alikuwa akisemwa na mama mkwe, ambaye aliona kuwa hunda mama ana tatizo, ndio maana hawataki kwenda kwenye sehemu nyingine, wakiwa na maana kwa wataalamu, waganga wa miti shamba. Mama mkwe baada ya maongezi,alisema;

‘Au labda kama mnajijua kuwa hamzai, maana tusije tukawa tunahagaika kuwauliza kumbe wenyewe mnajijua kuwa ni tasa’yalikwua maneno ya mama huyo,ambayo yalimuuma sana mama, akijua kuwa hana tatizoo kama livyo mume wake, lakini alitulia tu,akimuheshimu mkwe wake.

Ndugu walipoona wanandoa hawa wawili hawajali,wakaanza kumnyoshea mama kidole moja kwa moja, kuwa yeye ni tasa hawezi kuzaa,na huenda kamfanyao kitu mume wake ndio maana hasikii ushauri wa wanandugu

‘Kama ni tasa inawahusu nini,mimi na yeye tumekubaliana iwe hivyo,’akasema baba kwa hasira.

‘Hapana ndugu yetu , usiseme hivyo, manpooana mnatarajia nini, kama sio kupata kizazi, ili kizazi hicho kiendeleze kizazi, kwahiyo kama mke wako ni tasa, tunakushauri ndugu yetu ukaoe mke mwingine’wakasema.

‘Mimi nimeshasikia ushauri wenu, kwahiyo tuachieni wenyewe tufikirie, maana huwezi moja kwa moja ukamnyoshea mke wangu mkono kuwa ni tasa, Je kama mimi ndiye mwenye tatizo, mtasemaje?’ akasema baba kwa hasira.

‘Sisi kwenye familia yetu hatuna hilo tatizo, ,tunajua ni mke wako,kwa vile keshakuweka sawa ndio maana hutaki hata kuhangaika, kama huwezi kuifanya hiyo kazi tutahangaika sisi wenyewe maana damu ni nzito kuliko maji, na tutahakikihsa kuwa huyo mke wako anakimbia hapo nyumbani’wakasema wanandugu  lakini baba kwa jinsi alivyokuwa akimpenda mke wake, hakujali akisema kimoyo moyo yeye hatishwi nyau.

Baba kipindi hicho ndio alikuwa kajiingiza kwenye biashara za madini, na katika heka heka za huko, akaumia, na kurudi kijijini, na pesa walizokuwa nazo, wakatumia kwamatiubabau hadi zikaisha, na hali ya babau haikuwa nzuri, na kipindi hicho hicho, ndio baba alishauriana na mke wake kuwa wahangaike kumtafuta huyo mtaalamu, kwani kumbe pia alikuwa mjuzi wa kutibu matatizo mengine.

‘Mke wangu tatizo hili linanipa wasiwasi sana, maana hata vyomvii vya uchunguzi kama x-ray, vinaonyesha sina tatizo, lakini mguu na kiuono, havitaki kuniachia, mbona naingiwa na wasiwasi’akasema baba.

Kwa hilo ikabidi waende kumuona huyo mtaalamu, na katiak kuelezea hilo, wakaambiwana huyo mtalaamu, kuwa tatizo lao, linahusiana na mgando wa damu, na asipoangalia huenda asizae tena, kwahiyo ni nyema ajitahidi angalau apate mtoto mapema.

‘Kwa vipi sasa mtaalamu, maana sisi tunachohitaji ni dawa hayo mengine hatuna umuhimu nayo, sisi hatujali kuwa tuna maadui, kama ni uadui wao waachie wenyewe’wakamwambia.

‘Sawa nendeni mii nitawatafutia dawa, kwanza chukua dawa hii ya kuyeyusha hiyo damu, halfu mkirudi nitawapa dawa ya kizazi, …’wakaambiwa.

Mambo hayo yakafanyika na yaliyofanyika zaidi ni siri yao baba na mama, mimi ninachojua ni kuwa mama akashika uja uzito na nikazaliwa mimi. Na ilikuwa furaha sana kwa familia hiyo, na ulezi wangu ulikuwa wa kinamna, maana ilikuwa kama mgumba kupata mtoto.

Nikalelewa kama yai, nilidekezwa sana, na kila nilichokitaka nilipewa, ilikuwa hata nikigombana na mwenzangu, hata kama mimi ndiye mkosaji, mwenzagu ndiye alionekana ni mbaya, na hali hii ilisababisha wengi kunichukia.

Na kwasababu hiyo, na mimi nikajenga tabia ya kiburi, nikawa hata walimu siwaheshimu sana, kwani nikichapwa naenda kusema nyumbani , na wazazi wangu wanakuja kugombana na walimu. Nikajiona mtoto wa kipekee sana.

Kipindi hicho baba hali ikawa nzuri, kipato chake kikaongezeka, kwani aliamua kufuatilia bisahara ya madini, akawa mmoja wa mawakala wa madini huko Mererani na huko akajenga kukawa kama nyumbani. 
Tukahamia huko na mimi nikawa nasoma shule za huko Mererani,….

Ndio maana hata nilipokuwa mkubwa huko nilikuona kama nyumbani, nilikupenda sana maana ndipo maisha ya raha yalipokuwa, kabla mambo hayabadilika, na hata yalipobadilika mimi niliamua kuwa huko ndipo kutakuwa nyumbani kwangu.

Mambo yalibadilika pale nilipokuwa na umri mkubwa, ghalfa nikaona watu wakiniangalia na kuanza kunong’ona, mpaka nikaingiwa na mashaka, na kujiuliza hawa watu kwanini wananiangalia na kuanza kuteta pembeni, nikajua kabisa walikuwa wakiniteta mimi, nikaamua kufanya udadisi , na ndipo mmoja wa marafiki zangu akaniambai ukweli.

‘Unajua watu wanasema sura yako inafanana sana na yule mganga, mtaalamu wa mambo ya uzazi, kwahiyo wanahisi kuwa huenda ndiye baba yako, maana hamna udugu wowote kwanini mfanane na yeye’akasema huyo rafiki yangu.

‘Mtaalamu gani huyo wa uzazi, mbona mimi simfahamu’nikauliza.

‘Wewe hujui, nimesikia toka kwa wazazi wangu wakisema kuwa baba na mama yako walipoona hawazai walikwenda kwa huyo mtaalamu, na huko huenda huyo mtaalamu aliwachezea ujanja na ndipo ikapatikana mimba yako’akasema huyo rafiki yangu,na kauli hiyo iliniuma sana,ikabidi niende kumuuliza mama.

Mama aliposikia hivyo, kwanza alishituka , na kuniangalia sana kwa makini, na baadaye akasema kwa hamaki;

‘Ninani kakuambia uchafu huo, sitaki hata kusikia kauli hiyo,unasikia, wewe ni mtoto halali wa baba yako, na huko kufanana wanakosema mbona mimi sikuoni, na hata kama mnafanana, binadamu hutokea wakafanana, achana nao’akasema .

Haya hayakuishia hapo kwani wandugu wale wale waliokuwa wakiwasakama baba na mama kuwa hawana watoto, na wanahitajika kwenda kwa mtaalamu, waligeuka  na kuanza kumsakama baba kuwa huenda mke wake katembea na huyo mtaalamu, kwahiyo ambane mama aseme ukweli . Baba mwanzoni hakujali hayo maneno, lakini yalipozidi sana, ikabidi amuulize mke wake.

‘Hivi kweli haya maneno unayaonaje, maana kiukweli, ukimwangalia binti yetu anafanana na huyo mtaalmu, imakuwaje, ina maana  kweli dawa zake zinaweza kusababisha hayo,au kuna mengine yalifanyika mimi siyajui’akasema baba. Na mama kauli hiyo ilimuuma sana , na toka siku hiyo wakawa hawalewani, mama alimwambia mume wake kuwa;

‘Mume wangu hivi na wewe umekubaliana na hayo maneno ya watu, kwani watu hawafanani, mimi sijawahi kufanya uchafu huo, na ningeliufanya saa ngapi na wakati wote tulikuwa tukienda kwake pamoja’akasema mama.

Baba akawa mtu wa mawazo, kwani ndugu, majirani wakawa wakimzonga, na hili likamfanya sasa afikiria kuoa mke mwingine, wazo ambao hakuwa anlo kabla, na  kwa msaada wa andugu zake ndipo akaoa mke mwingine, na mama akawa anasakamwa kuwa ni malaya, eti,kisiri alikuwa akitembea na huyo mtaalamu.

‘Mume wangu nakupenda sana, na tumetoka mbali, najua kwa hali ilivyo, hata kama nitaamua kuvumilia, bado utasakamwa, mimi siogopi kuishi na mke mwanzangu, lakini nashindwa kuishi na ndugu zako, na najua hayo hayataishai hapo, huyo mke mwanzangu nimjuavyo mimi,anaweza kutekwa na maneno ya ndugu zako, na mwisho wa siku tukawa maadui’akasema mama.

‘Mke wangu, mimi nimeamua kuoa mke mwingine ili nione ukweli, ili tuwahakikishie hawa watu kuwa na sisi tunaweza kupata watoto, na hayo wanayozungumza sio kweli, lakini bado ankupenda na nataak tuwe pamoja kwa hili’akasema baba.

‘Wewe unaamua kuoa mke mwingine kwasababu ya kupata watoto, je mimi, sitaki watoto?’ akauliza mama.

‘Kwahiyo ndio maana ukatembea na huyo mtaalamu, ili unionyeshe kuwa unaweza kupata mtoto?’ akasema baba, na kauli hiyo ilimuuma sana mama, akiumbuka kuwa hadi kwenda huko kwa huyo mtaalamu hakupenda, ni shinikizo lao, na hajui kabisa kwanini binti yake, yaani mim nafanana na huyo mtaalamu. 

Alihuzunika sana, na akawa hara raha, akakonda sana, kwani kila siku akawa anasakamwa na wandugu, wakawa wanamuita malaya, na mimi nikawa naitwa majina mbaya,hatukuwa na raha, …mwishowe mama akaamua moja kuondoka.

Baba alikuwa ananipenda kiukweli, …hakutaka kabisa kuniachia , walikubaliana na mama kuwa niwe huru, yaani siku chache nakaa  na baba na siku nyingine kwa mama, lakini kwa baba kulikuwa hakuna amani, nilionekana kama doa ndani ya familia.

Mimi nilipomaliza darasa la saba tu, nikawa mara nyingi naishi na mama, ambaye alikuwa huko Arusha alipoolewa tena na baba mwingine,na huko nikakutana na rafiki yangu mmoja, huyo ndiye alinifundisha mambo mengi. Kipindi hicho baba hali ya kiuchumi ilikuwa mbaya, alikuwa kauza kila kitu huko Arusha na kuhamia kijijini, na hata wakati wanaachana na mama alikuwa yupo kijijini.

Rafiki yangu huyo, alikuwa kama mimi, alikuwa mpenzi sana wa maisha ya Mererani, tukawa tunajadiliana jinsi gai ya kuishi hapo maeneo ya machimbo, na yeye akawa ananifundisha mambo mengi ya kikubwa, na ndipo nikajikuta name nimlowea, nikajua jinsi gani ya kupata pesa….

Kiujumla mimi rafiki yangu, maisha yangu, na ndugu yangu ni pesa, kama huna pesa, wewe na mimi ni paka na panya…..’akasema huku akikunja uso.

‘Mimi sina pesa,mimi ni masikini ,ndio nakwenda kutafuta maisha, ….’Adam akajikuta akisema hivyo.
Yule binti akageuka na kumwangalia Adam usoni kwa muda, akashika kidevu na kujikuna, halafu akasema;

‘Wewe siumeniambia mjomba wako, ni yule tajiri wa madini..au sio?’ akauliza na kutulia na kabla Adam hajajibu huyo binti akasema; ‘Kama ni yule mimi namfahamu sana’akasema huyo binti huku akitikisa kichwa kwa madaha.’ Akatuliwa kwa muda na baadaye akasema kwa ndogo;

‘Huwa anajifanya sana,haingiliki…..sasa, naona ataingilika tu….’akasema huku akiendelea kutikisa kichwa.

‘Kwahiyo unataka kusema nini?’ akauliza Adam.

‘Tatizo lako hutaki kunielewa,lakini utanielewa tu, nikuambie ukweli mimi sijawahi kupenda, na wala sijui kama kuna kupenda, wewe uliwahi kupenda katika maisha yko?' akamuuliza Adam.

'Kiukweli ndio,yupeniliyempenda sana, lakini sijui ypo wapi kwa hivi sasa, na najua huenda yeye kama nilivyoskia,ndiye kanisaidia safari hii iwepo haraka zaidi, kwahiyo huko alipo namshukuru sana, na kama tukikutana....'akatulia na kuinamisha kichwa.

'Hayo mimi sielewi,sijui kwanini mtu upende, hadi kiasi cha kuumia,ili iweje,..hebu niembie kama huna pesa unaweza ukaishi kwa raha, hata kama mnapendana?' akauliza.

'Ndio mbona wazazi watu..'akasema na huyo binti akamkatisha na kusema;

'Labda kuna mapenzi kama hayo, ya kudanganyana, kama hayo ya wazazi wetu,unaishi na mtu huku unaumia kila siku,....labda, huenda wewe ukawa wa kwanza kupendana na mimi,lakini tatizo ni hilo, mimi mpenzi wangu ni pesa, na najua wewe ….labda, kutokana na wewe nitapata pesa..nina uhakika na hilo’akasema yule binti na kuangalia juu huku akionyesha uso wenye tabasamu.

Adam,hakuelewa, akatulia akiwaza, na kutafakari, …..na hapo wakwa wameshanibgia Mererani.


NB: Hiki ni moja ya visa vilivyokusanywa kama Riwaya, ndio maana vinakuwa na wahusika wengi, lengo ni kufikisha ujumbe uliotokana na watu wengi,....na mara nyingi naandika kwa hali ngumu kidogo, muda unakuwa hautishi, sipati muda wa kupitia tena, ndio maana huenda sehemu nyingine nakatiza, lakini mwisho wa siku tutaona ni nini hasa tunatakiwa tukijue kwenye kisa hiki.

 Lengo langu ni kuwa hapa nipatumie kama sehemu ya kukusanya `kazi mbambali' ili baadaye tuweze kutengeneza vitabu, kwenye vitabu ndipo tutaweza kuviweka hivi visa katika hali iliyo bora zaidi.LAKINI ni kazi ngumu, ambo magumu sio mchezo .....tuombeane heri

WAZO LA LEO: Kumpenda mwenzako, rafiki yako,ni pale unapokuwa tayari kumpa,kumasaidia na kutoa kile unachokipenda sana, na upo tayari kukosa kwa ajili yake, hayo ndiyo mapenzi ya kweli, je katika dunia hii yapo?


Ni mimi: emu-three

Monday, October 22, 2012

Uchungu wa mwana aujuaye ni mzazi-12




Adamu alimwangalia yule binti akiongea, na kuingiwa na hamasa naye, hasa pale alipokuwa akiongea kwa haraka haraka, kama redio iliyofunguliwa kwa mwendo kasi, Adam akawa anamwangalia huku akimsikiliza kwa makini, na kwa vile kulishapambazuka,aliweza kumuona vyema usoni. Kwa muda alikuwa keshaondoa ile khanga aliyokuwa kajifunika.Na nywele zake zilikuwa ndefu.zikiwa kama zimepakwa rangi,...

Adam akamwangalia usoni, anavyotabasamu anavyobenua mdomo kwa dharau, kwakweli kila kitu chake kilimvutia sana Adam.

'Huyuu binti mnzuri sana,mbona sijawahi kumuona kabla?' akajiuliza kimoyomoyo,na hapo hapo akamkumbuka binti rafiki yake wa shuleni, na kumlinganisha na huyu binti, akashindwa kutofautisha nani zadi, baadaye akamuliza yule binti;

‘Hebu niambie wewe ulifikaje Mererani, maana naona wewe unaonekana ni mwenyeji huko, na unaonekana kufahamu mengi ya huko kama vile na wewe ni mmoja wa wachimbaji wa madini,  uliwahi kuingia machimboni nini?’ akauliza Adam.

Yule binti akacheka kidogo, uso ukameremeta, halafu ghafla ukawa unafifia, uso ukawa unabadilika kutoka kwenye tabasamu na kwenda kwenye huzuni. Adam aliangalia yote yale, alimuona huyu binti kama wale waigizaji aliowahi kuwaona kwenye sinema.

Yule binti alitulia kidogo kama anatafakari kitu, halafu akamuangalia Adam kwa makini,na yale macho yake, gololi za ndani zikawa zinazunguka, kama vile anamchora Adam. Macho yake yalikuwa makubwa  yanayovutia, na yalionekana kuwa na usiri mkubwa, au jambo ambalo limejificha ndani ya nafsi za huyu dada, na huenda alitaka kuliongea lakini bado alikuwa na wasiwasi, Adam alihisi hivyo, na pia Adam, aliingiwa na mawazo mengine kuwa huyu binti sio kuwa ana mvuto, bali inaonekana kuwa ana kitu cha zaidi.

Adam, huwa ana kipaji cha kumsoma mtu, lakini yeye mwenyewe hajijui kuwa yupo hivyo, hili alikuwa nalo tangu akiwa shuleni, alijikuta yupo hivyo tu, kuwa anaweza akamwangalia mtu akamjua kuwa huyu ana kusudio gani, au ana nia gani, huenda ikawa mbaya au nzuri, na kweli akimwangaia mlengwa ,huyo mlengwa anasema kweli alikusidio hivyo. Hata siku moja alipomuuliza baba yake kwanini ana hulka hiyo, baba yake akamwambia;

‘Binadamu tulivyo, kila mmoja kazaliwa na kipaji chake, na hili utaweza kulifahamu  kwa mtoto wako akiwa bado mdogo, sisi wazazi wako tulikugundua hivyo, kuwa una kipaji fulani, tangia ukiwa mtoto, na tulijua kuwa huenda kipaji hicho kikakusaidia kuwa msomi mzuri, lakini tulishangaa, ulivyobadilika ghafla.

Kweli mwanzoni darasani Adam alikuwa akifanya vizuri sana, lakini alipoingia darasa la tano akaanza kupoteza muelekeo, akawa akifika darasani anaonekana kuwa na mawazo sana, na kidogo kidogo akaanza kushuka kielimu, na ikifika mahali hata darasani haingii, kabisa, au anaweza akaonekana mara moja moja.

Walimu walijaribu kumhoji, na hata kuwaita wazazi wake, lakini haikusaidia kitu, ikabakia kusubiria amalize hilo darasa la saba akabidhiwe kwa wazazi wake. Hii hali ilianza pale alipokuwa akirudi nyumbani na kukuta wazazi wake wakigombana, au wakati mwingine anakuta ndugu kwa ndugu wanagombana, baba yake na baba wengine, au wakati mwingine anakuta baba na mama yake hawaelewani kwasababu hali ya uchumi ni ngumu, basi Adam akajiona hana raha.

Haya aliyaongea siku baba yake alipotumia mbinu nyingi za kumbana mwanae, baada ya kugundua kuwa kutumia nguvu, kwa kumchapa viboko haikusaidia lolote, akaamua kutumia hekima, na kuwa karibu naye, na siku mmoja kijana wake akamwambia baba yake kwanini hali ilifikia kiasi hicho, akasema;

‘Baba mimi nimebadilika kutokana na hali halisi iliyopo hapa nyumbani, mimi sioni raha nikiwaona wazazi wangu mnataabika, kula kwa shida, matatizo mengi yakugombea ardhi, wakati mwingine mimi nagombana na ndugu zangu, nyie mnaingilia, unakuwa ugomvi mkubwa. Mimi naona ajabu sana wewe na ndugu yako juzi mumegomabana kwasababu ya ardhi, sehemu ndogo tu, sasa nikaona labda ni kwasababu ya umasikini wetu’akasema Adam.

‘Sio hivyo mwanangu, hayo yote ni kwasababu wote tulikaa tukitegemea mali ya baba, urithi wa baba, baba yetu alikuwa tajiri sana enzi zake, na kutokana na utajiri wake, sisi watoto tukalemaa, kila mmoja akiwa anauchungulia huo utajiri, kuwa na mimi nimo, hatukutaka kusoma, na mama zetu wakawa wanatukumatia kila mmoja na watoto wake,…hilo ndilo kosa tulilofanya.

‘Baba yangu alipofariki tu, tukaanza kugombea mali yake, kila mmoja akidai haki yake na kuona anahitaji zaidi ya mwingine, haki ambayo hatukuitolea jasho, na wala hatujui jinsi gani baba na wazazi wetu kwa ujumla walivyohangaika na wake zao hadi kufikia hapo na kuitwa matajiri wa enzi hizo…

‘Maana baba yangu alikuwa na wake wengi enzi zake. Alikuwa ni mmoja wa viongozi wa kabila letu, kwahiyo,pamoja na mali nyingi, pia alitakiwa kuwa na wake wengi….alikuwa na mifugo mingi, mashamba , ambayo wake zake walikuwa wakiyahudumia kwa bidii kubwa. Enzi zao wake walichaguliwa kutokana na bidii zao katika kazi..

‘Hayo ni maisha ya baba yangu na enzi zake, lakini sio maisha yetu, sio maisha yenu, maisha yetu, na sasa yenu yamegeuka, enzi zeni bila shule utakuwa mtumwa wa wenzako,…usituige sisi kwasababu tulilemaa, kwa vile hatukutaka kujiendeleza, hatukutaka kutafuta kwa jasho letu,ili tuweze kukiendeleza kile alichokiacha baba yetu, ili kiwe kikubwa zaidi.

‘Mwanangu, hakuna kitu kinachorudisha maendeleo kama kugombana, kama kuwekeana chuki, kwani ndani yake kuna adui shetani, ambaye kawekeza kwenye ubinafsi, kila matu anaona kila kitu ni chake,na anahitaji zaidi sio kwa kuhangaika,bali kwa kumdoea mwenzake,na kumuonea kijicho. Maana sisi tulibakia kukigombea kile kidogo alichokiacha baba, kilionekana kidogoo kwasababu ya wingi wetu, na hatukutosheka na mgawo, tukawa tunaingiwa na husuda.

‘Mimi na ndugu zangu tukawekeana kijicho, kila mmoja sasa anataka kuchukua haki ya mwingine, tukajenga uadui, ndugu kwa ndugu wa damu moja. Kwasababu baba alikuwa na wake wengi, kwahiyo hata watoto walikuwa wengi pia, na itikadi tofauti, na hilo lilichangia sana kukuza mgogoro. Mgogoro ukikita kwenye itikadi ya mtu, unafanya mambo yanadumaa, hata akili ya kutafakari, kutumia hekima, au kutumia ile elimu yenyewe ya itikadi ile inasimama,kinachobakia mbele ni ubinafsi …ni hii ni hatari kubwa

‘Vita vya wenyewe kwa wenyewe vikazuka, …mwanangu usione hivi kumepoa, hapa kulikuwa hakukaliki, kila mara kulikuwa na vita vya kupigana mapanga mimi na ndugu zangu, kwa kosa dogo tu, ilimradi kila mmoja anatafuta chanzo, ili aweze kumuondoa mwenzake, tumesahahu kuwa enzi za baba tulikuwa tunakaa meza moja tunakula pamoja.

‘Enzi za baba ilikuwa kama sherehe, baba anatukutanisha pamoja, tunakula pamoja, tunahadithiana hadithi , tunacheza, yaani kulikuwa na raha ya aina yake, lakini mdudu mtu amekuja pale tu wazazi wetu hawo, walipoondka duniani, kila mmoja na mama yake, kila mmoja na mambo yake,tukawa tunaanza kunyosheana vidole na hata kuitana wachawi…tulisuluhishwa sana, na baadaye sijui upepo gani umepita, wengi wameamua kutawanyika, kutafuta maisha sehemu nyingine maana ile mali tuliyokuwa tukigombea imekwisha.

‘Ina maana baba, kumbe babu yangu alikuwa tajiri, na pia mgogoro w augomvi wenu umatulia baada ya watu kutawanyika kwenda sehemu nyingine kutafuta maisha?’ akauliza Adam.

‘Sio tajiri tu, baba yagu alikuwa mmoja wa viongozi wa kabila letu, sisi ukoo wetu ni mashuhuri sana, lakini ulikuja kuharibika kipindi chetu. Baba yetu alituacha tukiwa bado vijana, na mawazo yakuona  mbali yalikuwa hayapo, kwasababu tulilelewa kitajiri, kila tunachotaka tunapata, hatutaka kujituma zaidi.

‘Ndio maana mwanangu nataka usome ili uweze kuirudisha heshima ya ukoo wetu, tunajua ukisoma ukawa na elimu, kizazi chako kitaiga, na ukoo huu utasonga mbele, kuliko kuwa na tamaa ya mali ambayo kuipata kwake ni kwa kubahatisha na hata ukiipata hutaweza kujua jinsi gani ya kuiendeleza, na ili ujue hayo ni kwa kupata elimu safi.

‘Baba mimi akili yangu ni kuondokana na huu umasikini, na sioni sababu ya kusoma, wangapi wamesoma lakini hali zao hazina tofauti na mimi, na baba ukumbuke kuwa elimu yenyewe inahitaji pesa, siku hizi elimi bila pesa hakuna, sasa hizo pesa mnatarajia tutazipata wapi, nasikia enzi za nyuma wenzangu mlikuwa mkisoma bure, siku hizi hiyo haipo tena!’

‘Tutatafuta mwanangu,…tutachangishana, wanafamilia tupo, kidogo kidogo utasoma’akasema baba.

`Sasa ina maana tuanze kuchangishana,wanandugu, wanandugu wenyewe kula yao ni shida, wanandugu wenyewe hamuelewani, na hebu nikuulize, mkishachangishana nikaamua kusoma, na bahati nifanaikiwa na kupata kazi, ni nan nitamsaidia maana kila mmoja atakuwa na matarajio kutoka kwangu kutokana na mchango wake alioufanya kwangu?’ Adam akamuuliza baba yake.

‘Ukisha pata elimu, ukapata kazi, utakuwa na mwanya wa kuwasaidia wenzako kwa njia nyingi tu, kwa mfano unaweza ukawa kiongozi, kama vile  mbunge wa eneo letu, utakuwa na nafasi ya kuwasaidia wenzako  kwa mapana zaidi, sio tu familia yenu tu, bali wilaya nzima, huoni ni faida kubwa sana,..’akasema baba yake Adam, lakini Adam hakumuelewa.

‘Niwe mbunge,niwe meneja,lini…baba tuwe wakweli, angalia majirani zetu, watoto wao wamesoma,nini walichofanya…wengine wamekuwa walevi, wengine, ndio hawo, kila siku wapo wa mabarabarani, wamegeuka wanasiasa wasio na jukwa, kila mahali kwao…baba mimi nipeni mwanya, mtaona wenyewe’akasema huku akionyesha ngumi mbele.

Baba alimwangalia mtoto wake kwa muda, akiwa haamini kuwa huyu ndiye yule mtoto wake aliyemuelewa, au ni mwingine, akatikisa kichwa,  na kwa muda huo Adam,alikuwa akiendelea kutikisa ngumi hewani

Adamu alikuwa mbali akiwazia mali, akiwazia kuchuma kwa haraka ili aondokane na huo umasikini ulikithiri ndani ya familia yao, na aliona sehemu muhimu ya kupatia hiyo mali ni huko machimboni. Na hili lilijijenga pale alipomuona mjomba wake akiwa katajirika, ana miradi na ana maisha mzuri, akaaona huko ndiko kwa kupatia maisha bora,

******

Adam alishituka toka kwenye mawazo ya familia yake, pale yule mwanadada alipomshika bega, alihisi ulani wa mkono wa yule mwanadada, na mwili ukamsisimuka, na akilini akawa anajiuliza, vipi mkono laini kama huo ukaweza kufanya kazi, ina maana huyu mwanadada huko machimbo atakuwa anafanya nini…

Yule mwanadada hakusema kitu kwa muda ule, alitulia kimiya huku mkono ukiwa bado umeshikilia bega la Adam,  na Adam akatulia akisubiri, kuwa huyo mwanadada atasema lolote, lakin hakuna neno, alilosema huyo mwanadada, alikuwa kimiya, alishangaa sana kuona ukimiya huo wa ghafla wa yule mwanadada, kinyume na jinsi alivyomzoea kwa muda huo mfupi waliokuwa naye, akahisi huenda hilo swali alilomuuliza mwanzoni limemkera.

Huyu binti alikuwa akianza kuongea anakuwa kama redio iliyofungulia kwa sauti ya kasi, huwa anaongea kwa haraka haraka bila kutulia, utafikiri anaogopa muda utaisha kabla hajamaliza kile alichokusudia kukisema. Akageuza uso na kwamwangalia moja kwa moja Adam machoni mwake, na akatabasamu, na kusema;

‘Adam hivi mimi unanionaje?’ Adam, akashangaa kwa lile swali.

‘Nakuonaje kwa vipi…?’ akamwangalia kwa muda halafu alipomuona yupo kimiya na huku kamkazia macho Adam akasema;

‘Mimi nakuona ni binti mrembo, na sioni kwanini usiolewe na kutulia na mume wako kuliko kwenda huko Machimbo, ambapo nahisi kwa binti kama wewe hakukufai’akasema Adam.

Yule binti akawa akawa anajiangalia kama vile anajikagua, halafu akatulia huku kainamisha kichwa chini, alitulia vile kwa muda, hadi Adam akahisi kuna kitu kizito ambacho huenda kakisema na kumkwaza huyo binti.

Adam,  akajaribu kurejea mazungumzo yake kichwani, jinsi walivyokuwa wakiongea, ili kuona kama kuna kitu kakisema ambacho anaweza kukihisi kuwa ndicho kimesababisha hayo yote, na ndipo akakumbuka hali hiyo ilijitokeza pale alipomuuliza huyo binti kama aliwahi kuingia machimboni, na alikumbuka alipomuuliza hivyo, ndipo hapo huyo binti alipotulia ghafla na kuwa kama anawaza jambo

Adam, akaona aliulize tena lile swali ili kuona kama ndilo linalomfanya huyo binti awe hana raha, kwanza akamuangalia yule binti kwa makini, na wakati huo huyo binti alikuwa kainama chini, na mkono mmoja kautumia kama kushika kichwani karibu na macho, kama vila anataka kulala, lakini yale macho yalionekena hayajafumbwa, ina maana alikuwa akiwaza jambo.

Baadaye yule binti akahisi anaangaliwa, akainua uso kumwangalia Adam, halafu akatabasamu, na huku bado anamwangalia Adam usoni, na wakawa wanaangaliana kwa muda bila kusema kitu.

Adam, hapo alihisi kitu kwenye mwili, wake, alihisi kitu kwenye fikara zake, na kutamani kumwangalia huyo binti, na ile hali ikamfanya yule binti ashikwe na aibu, na kuinama chini, halafu akainua uso tena na kumwangalia Adam, na kusema;

‘Hivi mimi naonekana Malaya?’ akauliza swali ambalo Adam hakulitegemea kabisa, na Adam, akaangalia pembeni kuwaangalia abiria wengine waliopo humo ndani kama wamsikiea hiyo kauli, lakini wengi wao walikwua wametulia, kila mmoja akiwa na mawazo yake, Adam, akageuka kumwangalia yule binti, aakmkuta kama anaangalia hewani,au juu,akionyesha kuwa mwingi wa mawazo, na Adam akasema;

‘Kwanini unaniuliza swali kama hilo, mimi sikujui  vyema, na siwezi nikamwambia msichana mrembo kama wewe neno kama hilo, kiujumla huonekani hivyo, ..kwanini umeniuliza hivyo?’ akauliza Adam.

Yule binti akatulia na mara macho yakajawa na ukungu, na ghfala machozi yakaanza kumtoka yule binti, na baadaye kwa haraka akayafuta na kuangalai pembeni, hakusema kitu kwa muda, alikuwa kimiya kiasi kwamba Adam alijiona mpweke, na ndipo akaona ni bora amuulize tena huyo binti, na kaba hajauliza yule binti akasema;

‘Mimi naweza kuwalaumu wazazi wangu kwa haya yote, ingawaje sio vizuri, kwani wao kwa muda huo walikuwa wakiona kuwa wanachonifanyia ni  sawa, na wanafanya hivyo kwa vile wananipenda,lakini kumbe walikuwa wakinitumbukiza shimoni, shomo la tala, shimo la moto….’ akasema huyu binti huku machozi yakiwa yametanda usoni, na ndipo akaanza kusimulia maisha yake.


Ni mimi: emu-three

Thursday, October 18, 2012

Ndugu wakigombana chukua jembe ukalime....



Nilishangaa nilipokutana na `school mate’(yaani jamaa tuliyesoma naye) mitaa ya Kariakoo, akiwa kabeba vifaa vyake vya biashara, akaniambia anakwenda kwenye duka lake. Nikajiuliza kichwanii huenda katoroka kazini , na kwenda kuangalia duka lake mara moja, lakini alivyo , yaani nguo na muonekano wake ulikuwa sio wa kiofisini, kama nilivyokuwa namjua awali.

‘Kwani kazini vipi?’ nikamuuliza.

‘Kazini wapi vipi bwana, mimii siku hizi nimejiajiri,nimeacha kazi za kuajiriwa muda mrefu mbona, baada ya wao kutangaza kuwa anayetaka kupunguzwa ajiorozeshe,mimi nikaona ndio nafasi yangu, ili angalau nipate msingi, msingi ambao kwa kwelii umenisaidia, ingawaje ulikuwa mdogo, lakini niliweza kufungua duka langu,na nashukuru mungu, watoto wanakwenda choo’akasema huku akitabasamu.

Nilimuangalia jamaa yangu huyu, na kukumbuka maisha yetu ya shuleni, kwani darasani alikuwa ni wale wenye kipaji maalumu, alikuwa akifanya vizuri sana hata mtihani wa mwisho, alikuwa mmoja wa waliofanya vyema kitaifa, na kuchaguliwa kwenda chuo kikuu.

Yeye alipomaliza chuo kikuu, ndio akaajiriwa kwenye kampuni hiyo kubwa hapa nchini, na nikajua kuwa hatachukua muda, kwa jinsi alivyo na akili, atateuliwa kuwa bosi ,au kupelekwa nje kusoma zaidi,maana akili aliyo nayo sio ya mchezo. Leo hii nakutana naye mitaa ya Kariakoo, kavaa kimitaani, sikuamini.

‘Ndugu yangu nilichoka na maisha ya ofisini, niliona napoteza muda wangu, na akili yangu bure na mwisho wa siku naishia kuchanganyikiwa, maana juhudi, akili na kujituma kwangu kote mwisho wa siku unapata eti kinachoitwa mshahara, mshahara wa siku thelathini, mimi huo naweza kuupata kwa siku mbili, katika biashara zangu….hebu angalia ningelijua hilo mapema ningelikuwa wapi,lakini bado sijachelewa..’akasema akiangalia saa yake.

‘Ina maana biashara yako ni kubwa sana?’ nikamuuliza.

‘Sio kubwa ya kutisha, ni ya kawaida tu, mimi sio mwizi,mimi sio fisadi ndio maana nimeamua kutafuta chumo halali, na kiukweli mimi sifanyi biashara ya kilanguzi, nafuata sheria, kwahiyo faida yanguu ni ya kawaida tu, ninachotumia ni akili yangu na elimu yangu tu’akasema.
‘Sasa niembie kwanini uliacha kazi,maana mimi naona unapoteza hazina, elimu uliyo nayo ni hazina kwa taifa, ulitakiwa uitumie vyema ofisini, kama ulivyosomea?’ nikamuuliza.

‘Sizani kama serikali inanihitaji mtu kama mimi, mimi ni mtoto wa mkulima, masikini, ambaye hana usemi mbele ya watoto wa wakubwa, sikupenda kuacha kazi, wakati nimesoma, nimetumia muda mwingi shuleni hadi chuo kikuu, lakini niliona kama nitaendelea kuwa kazini, nitaishia kubaya, ningeliweza kufa kwa kihoro, au kupatwa na ugonjwa wa moyo, au kiharusi.

‘Kazini,sisi watoto wa wakulima,mshahara wetu unajulikana, sio sawa na watoto wa wenzetu, waliosoma nje, …hili liliniuma sana.Hayo ni madogo tu, lakini kuna mambo yalikuwa yakitendeka humo ndani, mimi sikuyapenda,…uhujumu wa mali, ubinfasi wa wakubwa, na utendaji mbovu, ulinifanya nifikirie mara mbili. Usione mashirika yetu hayo, yaliyokuwa yakiitwa ya Uma yamekufa, yaliuliwa na sisi wenyewe,kwa mpango maalumu, …inaniuma sana.

‘Mimi akili yangu sio ya kutapeli, sio ya kufanya ujanja ujanja ili nipate kipato kisicho halali, akili yangu ni kufanya kile nilichokisomea, ili mwisho wa siku nione manufaa yake, kifamilia, kiofisi na kitaifa, lakini sivyo ilivyokuwa. Na sikuweza kupewa nafasi hiyo, na nilionekana kama `kipingamizi’ fulani…

‘Wenzangu wakifika ofisini wapo na juhusi ya kutafuta `dili’ wanatafuta masoko, ambayo yatawapatia `teni parcent’ yatawaingizia kitu,angalau kwa siku wasikose chochote,na kuna safari ambazo kila mtu alikuwa akizipigania, watu wasafiri, ili wapate marupurupu, humo kuna madudu yanafanyika, maana mtu anapewa fungu,lakini halifanyi kazi iliyotakiwa, ili akirudi awe na akiba…, kuna spea bandia zinanunuliwa, zinaandikiwa kuwa ni spea mpya….aaah, mimi nilishindwa, kwani sikukosomea hayo..

‘Rafiki yangu, aliye nacho anacho, sisi huenda tulitakiwa tuwe wasindikizaji tu, huenda tulipata nafasi ya kusoma ili ijulikane kuwa kila mtu kapewa nafasi hiyo, lakini kiukweli, wapo wanaotakiwa kufaidi, wapo walioandaliwa, na ndio hawo wanaoshika madaraka,kila kukicha,…mimi niliiona hiyo hali nikasema,ngoja nisije nikaja kuujutia umri wangu bure, nikajitoa mapemaaa.

‘Nilichofanya ni kubuni aina ya biashara, nikitumia elimu yangu, nikagundua kuwa nguvu zangu hazitapotea bure, kwa kuanzia ilikuwa sio kazi rahisi, maana ili upate leseni, inabidi uende maofisini tena, kuna makodi yasiohesabika,…lakini ilibidi iwe hivyo, na sasa sijutii uamuzi wangu huo, na hata siku moja hutaniona nikikatisha maofisini eti ninatafuta kazi, nitaenda kwamambo mengine...

'Mimi nimesoma na vyeti vyangu vipo, vizuri tu, lakini elimu yangu sio vyeti, elimu yangu ipo hapa kichwani,...'akashika kichwa chake kwa kidole. Lakini vyeti, au kutahiniwa, sijui `interview' kwangu hiyo elimu, ni kutafutana ni nani mwenzetu. Nasema hivi,hivyo vyeti vyangu watakuja kuvisoma watoto wangu, ili wasije kusema baba hakusoma. Wao nawasomesha nataka wafike mbali zaidi, najuaa huko mbele huenda mambo yakabadilika, sijui lini.....

Mara daladala likaja akaingia na kuondoka zake na kuniacha mimi nikiwa nimeduwaa, sikuamini, lakini ndivyo ilivyo. Nilibakia pale nikjiuliza hivi kweli ndivyo ilivyo, kuwa kuna watu ambao hatuna nafasi, tupo kama wasindikizaji tu, hata tufanye nini, tutaishia kumeza mate huku wenzetuu wameshika uma na kijiko,mezani kuku, pembeni kuna gari sijui linaitwaje….

Haya ndiyo maisha yetu, na ndio hali halisi ya maisha yetu, inabidi tukubali kuwa, kila mtu ana maisha yake, na ana mtizamo wake, lakini tukumbuke (angalizo) kuwa, kila linalotokea usilichukulie juu juu  tu, lina sababu. Na wenzetu wanalijua hilo, na wanajua kuwa wengi wetu tutayachukua kama yalivyotokea, na kuishia kubishana, kunyosheana vidole, hata kupigana…na ndio lengo lao, wakati nyie mnabishana, wao wanasonga mbele.

Nikakumbuka huo msemo kuwa `ndugu wakigombana chukua jembe ukalime, na siku wakipatana,(kamakweli watapatana) maana dunia hii sijui kama kuna kupatana tena, wewe chukua kapu ukavune!

Tupo pamoja daima.


Ni mimi: emu-three