Wazazi wangu walikaa muda mrefu baada ya kuoana bila kupata
mtoto, wao wenyewe walijionea ni kawaida tu, wakijua kwa vile hawana tatizo
lolote la kiafya ni swala la muda tu, kwani walishachunguzwa na kuonekana kuwa
hawana tatizo. Wao walijipa matumaini kuwa ipo siku watapata mtoto, hawakujali
sana, lakini ndugu na majirani, walikuwa ni tatizo, hawakuisha kuwasumbua, na ndio
waliochangia hata wazazi wangu waanze kuhangaika.
Kuhangaika kwao ndio kunanitia uchungu,maana hata nikifika
jijini,sipendi watu wanione,…wakiniona naangaliwa kwa jicho baya, nanyoshewa
vidole,nanyanyapaliwa kwa kitu ambacho hata sikijui, na sina uhakika kama ni
kweli au …mungu mwenyewe ndiye anajua.
Wazazi wangu walikuwa kila wakikaa, hodi ikipigwa, wanaogopa
hata kufungua mlango,maana mtu akija mazungumzo ni hayo hayo,..
‘Nyie mbona hamzai,ina mana hamtaki watoto?’ wakawa
wanaulizwa.
‘Bado hatujajaliwa, ipo siku tutapata watoto kwani yote ni
majaliwa ya mungu’akasema mama na baba.
‘Nyie kaeni kusema hivyo hivyo…ni majaliwa ni majaliwa siku
zinakwenda, mnatakiwa muhangaike, mengine yanahitajika kuhangaika, sio yote
yaliyopo yapo kama yalivyo, kuna nguvu za giza, hangaikeni…’ siku alikuja mmoja
wa ndugu zao, akawa anawashauri.
‘Lakini ndugu yangu, tumeshakwenda hospitalini
wakatuchunguza afya zetu na kumchunguza mke wangu njia za uzazi, wakaona hakuna
tatizo, na mimi mwenyewe walinichunguza wakaonahakuna tatizo, kwahiyo mimi
nionavyo ni mipango ya mungu,’akasema baba.
‘Hili siwakatalii,huko ni kwa wataalamu wa kisasa, lakini
zamani hatukuwa nao, tulikuwa na njia zetu za asili na zilikuwa zikitusaidia,
wapo watu wa namna hiyo hadi sasa, wana dawa, wana njia za asili za kuzindua
kizazi kilicholala, ‘akasema huyo mzee,
Hata alipoondoka wapendwa hawa wawili walikaa na
kujadiliana, wakaona hayo yote ni majaribu, wakijikita kwenye mambo hayo huenda
wakaingia kwenye mitego ambayo hawakuipenda. Wakakubalina wazidi kuvuta subira.
Wazazi wangu walikuwa ni watu wenye msimamo wao, na kwa vile
walikuwa wameishi mjini Arusha na kuishi na wazungu, na wasomi mawazo yao
yalikuwa hayafanani sana na pale kijijini, licha ya kuwa walikuwa mara nyingi
wanarudi na kuishi hapo kijijini.
Baba yangu alikuwa mafanyabiashara, alianzia mbali sana, na
kuna muda alikuwa tajiri ,kuna muda alifirisikia , kwahiyo alikuwa akijua
amisha yote, na hakuwahi kukata tamaa. Na kipindi hichoanasakamwa, alikuwa yupo
kijijini, alikuwa kafungua duka kubwa hapo kijijini.
Mama naye hakukosa watu wakumshauri,na siku hiyo alikuwa
akisemwa na mama mkwe, ambaye aliona kuwa hunda mama ana tatizo, ndio maana
hawataki kwenda kwenye sehemu nyingine, wakiwa na maana kwa wataalamu, waganga
wa miti shamba. Mama mkwe baada ya maongezi,alisema;
‘Au labda kama mnajijua kuwa hamzai, maana tusije tukawa
tunahagaika kuwauliza kumbe wenyewe mnajijua kuwa ni tasa’yalikwua maneno ya mama
huyo,ambayo yalimuuma sana mama, akijua kuwa hana tatizoo kama livyo mume wake,
lakini alitulia tu,akimuheshimu mkwe wake.
Ndugu walipoona wanandoa hawa wawili hawajali,wakaanza
kumnyoshea mama kidole moja kwa moja, kuwa yeye ni tasa hawezi kuzaa,na huenda
kamfanyao kitu mume wake ndio maana hasikii ushauri wa wanandugu
‘Kama ni tasa inawahusu nini,mimi na yeye tumekubaliana iwe
hivyo,’akasema baba kwa hasira.
‘Hapana ndugu yetu , usiseme hivyo, manpooana mnatarajia
nini, kama sio kupata kizazi, ili kizazi hicho kiendeleze kizazi, kwahiyo kama
mke wako ni tasa, tunakushauri ndugu yetu ukaoe mke mwingine’wakasema.
‘Mimi nimeshasikia ushauri wenu, kwahiyo tuachieni wenyewe
tufikirie, maana huwezi moja kwa moja ukamnyoshea mke wangu mkono kuwa ni tasa,
Je kama mimi ndiye mwenye tatizo, mtasemaje?’ akasema baba kwa hasira.
‘Sisi kwenye familia yetu hatuna hilo tatizo, ,tunajua ni
mke wako,kwa vile keshakuweka sawa ndio maana hutaki hata kuhangaika, kama
huwezi kuifanya hiyo kazi tutahangaika sisi wenyewe maana damu ni nzito kuliko
maji, na tutahakikihsa kuwa huyo mke wako anakimbia hapo nyumbani’wakasema wanandugu
lakini baba kwa jinsi alivyokuwa akimpenda
mke wake, hakujali akisema kimoyo moyo yeye hatishwi nyau.
Baba kipindi hicho ndio alikuwa kajiingiza kwenye biashara
za madini, na katika heka heka za huko, akaumia, na kurudi kijijini, na pesa
walizokuwa nazo, wakatumia kwamatiubabau hadi zikaisha, na hali ya babau
haikuwa nzuri, na kipindi hicho hicho, ndio baba alishauriana na mke wake kuwa
wahangaike kumtafuta huyo mtaalamu, kwani kumbe pia alikuwa mjuzi wa kutibu
matatizo mengine.
‘Mke wangu tatizo hili linanipa wasiwasi sana, maana hata
vyomvii vya uchunguzi kama x-ray, vinaonyesha sina tatizo, lakini mguu na
kiuono, havitaki kuniachia, mbona naingiwa na wasiwasi’akasema baba.
Kwa hilo ikabidi waende kumuona huyo mtaalamu, na katiak
kuelezea hilo, wakaambiwana huyo mtalaamu, kuwa tatizo lao, linahusiana na
mgando wa damu, na asipoangalia huenda asizae tena, kwahiyo ni nyema ajitahidi
angalau apate mtoto mapema.
‘Kwa vipi sasa mtaalamu, maana sisi tunachohitaji ni dawa
hayo mengine hatuna umuhimu nayo, sisi hatujali kuwa tuna maadui, kama ni uadui
wao waachie wenyewe’wakamwambia.
‘Sawa nendeni mii nitawatafutia dawa, kwanza chukua dawa hii
ya kuyeyusha hiyo damu, halfu mkirudi nitawapa dawa ya kizazi, …’wakaambiwa.
Mambo hayo yakafanyika na yaliyofanyika zaidi ni siri yao
baba na mama, mimi ninachojua ni kuwa mama akashika uja uzito na nikazaliwa
mimi. Na ilikuwa furaha sana kwa familia hiyo, na ulezi wangu ulikuwa wa
kinamna, maana ilikuwa kama mgumba kupata mtoto.
Nikalelewa kama yai, nilidekezwa sana, na kila nilichokitaka
nilipewa, ilikuwa hata nikigombana na mwenzangu, hata kama mimi ndiye mkosaji,
mwenzagu ndiye alionekana ni mbaya, na hali hii ilisababisha wengi kunichukia.
Na kwasababu hiyo, na mimi nikajenga tabia ya kiburi, nikawa
hata walimu siwaheshimu sana, kwani nikichapwa naenda kusema nyumbani , na
wazazi wangu wanakuja kugombana na walimu. Nikajiona mtoto wa kipekee sana.
Kipindi hicho baba hali ikawa nzuri, kipato chake
kikaongezeka, kwani aliamua kufuatilia bisahara ya madini, akawa mmoja wa
mawakala wa madini huko Mererani na huko akajenga kukawa kama nyumbani.
Tukahamia
huko na mimi nikawa nasoma shule za huko Mererani,….
Ndio maana hata nilipokuwa mkubwa huko nilikuona kama
nyumbani, nilikupenda sana maana ndipo maisha ya raha yalipokuwa, kabla mambo
hayabadilika, na hata yalipobadilika mimi niliamua kuwa huko ndipo kutakuwa
nyumbani kwangu.
Mambo yalibadilika pale nilipokuwa na umri mkubwa, ghalfa nikaona
watu wakiniangalia na kuanza kunong’ona, mpaka nikaingiwa na mashaka, na
kujiuliza hawa watu kwanini wananiangalia na kuanza kuteta pembeni, nikajua
kabisa walikuwa wakiniteta mimi, nikaamua kufanya udadisi , na ndipo mmoja wa
marafiki zangu akaniambai ukweli.
‘Unajua watu wanasema sura yako inafanana sana na yule
mganga, mtaalamu wa mambo ya uzazi, kwahiyo wanahisi kuwa huenda ndiye baba
yako, maana hamna udugu wowote kwanini mfanane na yeye’akasema huyo rafiki
yangu.
‘Mtaalamu gani huyo wa uzazi, mbona mimi
simfahamu’nikauliza.
‘Wewe hujui, nimesikia toka kwa wazazi wangu wakisema kuwa
baba na mama yako walipoona hawazai walikwenda kwa huyo mtaalamu, na huko
huenda huyo mtaalamu aliwachezea ujanja na ndipo ikapatikana mimba yako’akasema
huyo rafiki yangu,na kauli hiyo iliniuma sana,ikabidi niende kumuuliza mama.
Mama aliposikia hivyo, kwanza alishituka , na kuniangalia
sana kwa makini, na baadaye akasema kwa hamaki;
‘Ninani kakuambia uchafu huo, sitaki hata kusikia kauli
hiyo,unasikia, wewe ni mtoto halali wa baba yako, na huko kufanana wanakosema
mbona mimi sikuoni, na hata kama mnafanana, binadamu hutokea wakafanana, achana
nao’akasema .
Haya hayakuishia hapo kwani wandugu wale wale waliokuwa
wakiwasakama baba na mama kuwa hawana watoto, na wanahitajika kwenda kwa
mtaalamu, waligeuka na kuanza kumsakama
baba kuwa huenda mke wake katembea na huyo mtaalamu, kwahiyo ambane mama aseme
ukweli . Baba mwanzoni hakujali hayo maneno, lakini yalipozidi sana, ikabidi
amuulize mke wake.
‘Hivi kweli haya maneno unayaonaje, maana kiukweli,
ukimwangalia binti yetu anafanana na huyo mtaalmu, imakuwaje, ina maana kweli dawa zake zinaweza kusababisha hayo,au
kuna mengine yalifanyika mimi siyajui’akasema baba. Na mama kauli hiyo ilimuuma
sana , na toka siku hiyo wakawa hawalewani, mama alimwambia mume wake kuwa;
‘Mume wangu hivi na wewe umekubaliana na hayo maneno ya
watu, kwani watu hawafanani, mimi sijawahi kufanya uchafu huo, na ningeliufanya
saa ngapi na wakati wote tulikuwa tukienda kwake pamoja’akasema mama.
Baba akawa mtu wa mawazo, kwani ndugu, majirani wakawa
wakimzonga, na hili likamfanya sasa afikiria kuoa mke mwingine, wazo ambao
hakuwa anlo kabla, na kwa msaada wa
andugu zake ndipo akaoa mke mwingine, na mama akawa anasakamwa kuwa ni malaya,
eti,kisiri alikuwa akitembea na huyo mtaalamu.
‘Mume wangu nakupenda sana, na tumetoka mbali, najua kwa
hali ilivyo, hata kama nitaamua kuvumilia, bado utasakamwa, mimi siogopi kuishi
na mke mwanzangu, lakini nashindwa kuishi na ndugu zako, na najua hayo
hayataishai hapo, huyo mke mwanzangu nimjuavyo mimi,anaweza kutekwa na maneno
ya ndugu zako, na mwisho wa siku tukawa maadui’akasema mama.
‘Mke wangu, mimi nimeamua kuoa mke mwingine ili nione ukweli,
ili tuwahakikishie hawa watu kuwa na sisi tunaweza kupata watoto, na hayo
wanayozungumza sio kweli, lakini bado ankupenda na nataak tuwe pamoja kwa hili’akasema
baba.
‘Wewe unaamua kuoa mke mwingine kwasababu ya kupata watoto,
je mimi, sitaki watoto?’ akauliza mama.
‘Kwahiyo ndio maana ukatembea na huyo mtaalamu, ili
unionyeshe kuwa unaweza kupata mtoto?’ akasema baba, na kauli hiyo ilimuuma
sana mama, akiumbuka kuwa hadi kwenda huko kwa huyo mtaalamu hakupenda, ni
shinikizo lao, na hajui kabisa kwanini binti yake, yaani mim nafanana na huyo
mtaalamu.
Alihuzunika sana, na akawa hara raha, akakonda sana, kwani kila siku
akawa anasakamwa na wandugu, wakawa wanamuita malaya, na mimi nikawa naitwa
majina mbaya,hatukuwa na raha, …mwishowe mama akaamua moja kuondoka.
Baba alikuwa ananipenda kiukweli, …hakutaka kabisa kuniachia
, walikubaliana na mama kuwa niwe huru, yaani siku chache nakaa na baba na siku nyingine kwa mama, lakini kwa
baba kulikuwa hakuna amani, nilionekana kama doa ndani ya familia.
Mimi nilipomaliza darasa la saba tu, nikawa mara nyingi
naishi na mama, ambaye alikuwa huko Arusha alipoolewa tena na baba mwingine,na
huko nikakutana na rafiki yangu mmoja, huyo ndiye alinifundisha mambo mengi.
Kipindi hicho baba hali ya kiuchumi ilikuwa mbaya, alikuwa kauza kila kitu huko
Arusha na kuhamia kijijini, na hata wakati wanaachana na mama alikuwa yupo
kijijini.
Rafiki yangu huyo, alikuwa kama mimi, alikuwa mpenzi sana wa
maisha ya Mererani, tukawa tunajadiliana jinsi gai ya kuishi hapo maeneo ya
machimbo, na yeye akawa ananifundisha mambo mengi ya kikubwa, na ndipo
nikajikuta name nimlowea, nikajua jinsi gani ya kupata pesa….
Kiujumla mimi rafiki yangu, maisha yangu, na ndugu yangu ni
pesa, kama huna pesa, wewe na mimi ni paka na panya…..’akasema huku akikunja
uso.
‘Mimi sina pesa,mimi ni masikini ,ndio nakwenda kutafuta
maisha, ….’Adam akajikuta akisema hivyo.
Yule binti akageuka na kumwangalia Adam usoni kwa muda,
akashika kidevu na kujikuna, halafu akasema;
‘Wewe siumeniambia mjomba wako, ni yule tajiri wa madini..au
sio?’ akauliza na kutulia na kabla Adam hajajibu huyo binti akasema; ‘Kama ni
yule mimi namfahamu sana’akasema huyo binti huku akitikisa kichwa kwa madaha.’ Akatuliwa
kwa muda na baadaye akasema kwa ndogo;
‘Huwa anajifanya sana,haingiliki…..sasa, naona ataingilika
tu….’akasema huku akiendelea kutikisa kichwa.
‘Kwahiyo unataka kusema nini?’ akauliza Adam.
‘Tatizo lako hutaki kunielewa,lakini utanielewa tu, nikuambie
ukweli mimi sijawahi kupenda, na wala sijui kama kuna kupenda, wewe uliwahi kupenda katika maisha yko?' akamuuliza Adam.
'Kiukweli ndio,yupeniliyempenda sana, lakini sijui ypo wapi kwa hivi sasa, na najua huenda yeye kama nilivyoskia,ndiye kanisaidia safari hii iwepo haraka zaidi, kwahiyo huko alipo namshukuru sana, na kama tukikutana....'akatulia na kuinamisha kichwa.
'Hayo mimi sielewi,sijui kwanini mtu upende, hadi kiasi cha kuumia,ili iweje,..hebu niembie kama huna pesa unaweza ukaishi kwa raha, hata kama mnapendana?' akauliza.
'Ndio mbona wazazi watu..'akasema na huyo binti akamkatisha na kusema;
'Labda kuna mapenzi kama hayo, ya kudanganyana, kama hayo ya wazazi wetu,unaishi na mtu huku unaumia kila siku,....labda, huenda wewe
ukawa wa kwanza kupendana na mimi,lakini tatizo ni hilo, mimi mpenzi wangu ni pesa,
na najua wewe ….labda, kutokana na wewe nitapata pesa..nina uhakika na hilo’akasema
yule binti na kuangalia juu huku akionyesha uso wenye tabasamu.
Adam,hakuelewa, akatulia akiwaza, na kutafakari, …..na hapo
wakwa wameshanibgia Mererani.
NB: Hiki ni moja ya visa vilivyokusanywa kama Riwaya, ndio maana vinakuwa na wahusika wengi, lengo ni kufikisha ujumbe uliotokana na watu wengi,....na mara nyingi naandika kwa hali ngumu kidogo, muda unakuwa hautishi, sipati muda wa kupitia tena, ndio maana huenda sehemu nyingine nakatiza, lakini mwisho wa siku tutaona ni nini hasa tunatakiwa tukijue kwenye kisa hiki.
Lengo langu ni kuwa hapa nipatumie kama sehemu ya kukusanya `kazi mbambali' ili baadaye tuweze kutengeneza vitabu, kwenye vitabu ndipo tutaweza kuviweka hivi visa katika hali iliyo bora zaidi.LAKINI ni kazi ngumu, ambo magumu sio mchezo .....tuombeane heri
WAZO LA LEO: Kumpenda mwenzako, rafiki yako,ni pale unapokuwa tayari kumpa,kumasaidia na kutoa kile unachokipenda sana, na upo tayari kukosa kwa ajili yake, hayo ndiyo mapenzi ya kweli, je katika dunia hii yapo?
Ni mimi:
emu-three
5 comments :
m3 pole na changamoto za maisha lakini usikate tamaa songa mbele tupo pamoja
Mungu atakujalia baraka kutokana na juhudi yako hii
I was сurious if you eveг considered chаnging the
ѕtructure of your ωebsіtе?
Ιts very well written; I love whаt уouve got tο say.
But maybe you could a little mοre in the waу οf content so people could connect with it bеtter.
Youve got an aωful lot of teхt for only having one or 2 images.
Maybe you could spаcе it out better?
Here is my web site : Tenant Screening Service
Jirani umesalimika? nimepita tu kuacha zangu salamu.
Jirani yangu Edna, nimashukuru mungu, hatujambo, kwa ule usemi usemao, KUFA HATUFI LAKINI CHA MOTO TUNAKIONA. Nashukuru kwa kujali ujirani, Ubarikiwe sana.
Post a Comment