Sasa turejee kule porini, kama mnakumbuka, yule mwanadada
aliyemuokoa Maua, ndio alikuwa akihadithia kisa cha maisha yake, jinsi gani
alivyoweza kuingia mikononi mwa hawo watu wa msituni. Na ukumbuke kipindi kirefu kimepita na sasa Maua keshafikia muda wa kujifungua, na anatakiwa kupelekwa karibu na lile bwawa
la Mamba, ambapo anatakiwa akijifungua tu, hata damu yake haitakiwi iguse ardhi
ya kijiji hicho.
Wao wana imani kuwa damu ya watu waliopotea na wakawa
wametenda kosa ni najisi kubwa sana,inaleta mikosi, lakini ikifika mdomoni mwa
mamba,mkosi ule hugeuka na kuwa ni baraka. Ndio maana Maua alitakiwa
akijifungua tu,yeye atupwe ndani ya huo mto, akaliwe na mamba, ili kuleta
baraka badala ya mikosi.
Hili lilikuwa likifuatiliwa kwa karibu sana na wazee wengine
ambao ni wapinzani wa babu wa mume wangu.
Hayo yalifanyikwa kwa vile, kuna kugombea madaraka na visasi vya kihsitoria,
vilivyokuwepo ndani ya eneo linalojulikana kuwa eneo takatifu, Eneo hilo liliundwa na
wapinzani wa kivita wa siku nyingi. Ilibidi ifanyike hivyo, ili kuweza
kukutanisha koo zote na kuwa kitu kimoja, lakini hisia zilizopita zilikuwa bado
mioyoni wa miongoni wa wakuu wa koo. …’akasema yule mwanadada wakati anamsimulia
Maua.
‘Maua alitulia akivumilia uchungu uliokuwa ukiongezeka kila
dakika, aliona ni heri avumilie hata kama ni kujifungulia hapo hapo, na yule
mwanadada alikuwa akindelea kuelezea maisha yake.Moyoni mwa Maua aliona kama
ingeliwezekana angejifungulia pale pale, lakini haikuwa rahisi hivyo,kwanii
huyo mwenyewe anayemuhadithia alishapewa onyo kali,kuwa damu ikimwangika humo
ndani, basi na yeye anatakiwa kuwa chakula cha mamba.
Yule mwanadada akatulia kidogo alipomuona Maua akikunja uso
kwa maumivu, akamsogelea na kumchunguza, akatikisa kichwa kuashiria kuwa sasa
muda unakaribia, na akawa kama anakumbuka jambo,akamwangalia Maua kwa macho ya
huruma, lakini hakujua afanyeje, akasema;
‘Itabidi utusamehe tu,kwani kwa hali ilivyo, sijui kama mume
wangu anaweza kufanya jambo lolote, kwani hadi sasa hajarudi,ina maana
wamemkatalia, au kazuiliwa huko huko, hadi wahakikishe hilo wanalotaka kufanya
limekamilika…’akasema.
‘Wewe usijali endelea kunisimulia, nikikusikiliza nasahau
machungu, ingawaje hayasahauliki, ….endelea pale ulipoishia ulipoteza fahamu
ukiwa umeshajitundika juu ya mti, ilikuwaje baada ya hapo?’akasema Maua
akijafanya hasikii maumivu, lakini ….
‘Mimi nilipozindukana tu, nilijikuta nipo sehemu ngeni kabisa,
maana ni kama upo kwenye kaburi, na na ndivyo nilivyoanza kuwaza kuwa
nimeshazikwa sasa nipo kaburini, na kama kuna watu karibu, hwo ni malaika, akili ilikuwa siyo yangu, na nilizindukana
baaada ya kupiga chafya mara nyingi, na kila nikipiga chafya ndio akili inakuwa
kama inazindukana.
Na kabla sijaelewa nini kinachoendelea mara nikahisi mtu
yupo karibu yangu, kwanza mwili ulisismuka, nikajaribu kuiweka akili yangu
sawa, je nipo hai au ni maiti, nikahisi huyo mtu akinisogelea, alikuwa ni
mwanaume,lakini nilikuwa sijaweza kumuona sura yake vizuri akasema;.
‘Mimi ndiye niliyekuokoa ukiwa pale juu ya mti ,na
kiiutaratibu natakiwa mimi niwe mume wako..’akasema na kunishika usoni,
‘Kwanini mnifanyie hivi, na utanioaje bila ya rizaa yangu,
na hapa nipo wapi?’ akauliza huyo mwanadada.
‘Kuna mawili ya kuchagua ukatupwe kwenye mamba uliwe kama
kafara au uolewe na mjukuu wangu, na hili linatakiwa lifanyike haraka
sana,kabla ya saa kumi na mbili’ nikasikia sauti nyingine ikitokea humo humo
ndani sikuweza kumuona muongeaji.
Na huyo alikuwa akiongea kwa lugha ya kwao iliyochanganyika
na lugha ya kwetu. Hawa watu wanaweza kuongea lugha yao na lugha yetu kidogo,
na nilikuja kugudua baadaye kuwa huyo alikuwa ni babu yake. Na wakati huo akili
yangu ilikuwa haijakaa sawa, pale nilijua kuwa mimi na maiti tu, na kwahiyo
mimi sina cha kuamua ni kuacha hawo watu sijui ni malaika au ni wachawi,
wafanye wanalolitaka.
‘Ina maana mimi hapa ni maiti?’ nikajiuliza na kabla
sijapata jibu, nikahisi mkono ukinigusa usoni. Ulikuwa mkono ulikakamaa,na
ulikuwa na manyoya, nikashituka na kuinuka kwa haraka nikiwa naogopa, nikihisi
huenda ni mnyama. Na hapo nikakumbuka ya nyuma, kuwa mimi nilikuwa
nimejinyonga, na mimi ni maiti na huenda hawa watu ni wachawi, wanaokwenda
kwenye makaburi na kufufua watu. Nikiwaza hivyo sijui kwanini.
‘Usiogope …’sauti ikasema na maneno mengine ambayo sikuweza
kuyaelewa maana yake . Nikatulia na kusema kimoyo moyo, toka lini maiti
ikaogopa, nikageuza kichwa na kumwangalia huyo mtu au mnyama, nilikuta ni sura
ya mtu, mwanaume.
‘Nilikuona ukiwa umening’inia juu ya mti na kamba ikiwa
imekukaba, ikiwa na maana kuwa ulikuwa umejinyonga au kunyongwa, sasa….’sauti
ikasema na kufuatiwa na maneno mengine nisiyoyafahamu vyema, ilikuwa lugha ya
hawa watu ambayo nilikuja kujifunza baadaye, kumbe alikuwa akiniambia kuwa yeye
wakati anapita kutoka mawindoni, aliniona nikiwa nimening’inia kama mfu, akapanda haraka juu ya mti na kukata ile
kamba.
Aliniambia kuwa, alishajua kuwa nimeshakufa,kwahiyo nia na
lengo lao ni kunichukua mimi nikawe chakula cha mamba. Wao wana imani yao kuwa
wakiona mtu wa aina zetu na kumpeleka kwa hawo mamba akamtoa kuwa chakula cha
mamba inakuwa kafara na akiomba shida yake, anafanikiwa. Na yeye kwa muda hup
alikuwa na shida sana, alikuwa hana mbele wala nyuma.
Akaniambai kwamba, alinichukua akanibeba,na kuanza kukimba
naye hadi huko msituni, na waakti anafanya hivyo, alikuwa akiogopa wenzake
wasimuona, kwani wakmuona itatokea vita tena ya kumgombea, kwani kila mmoja
alikuwa katika mpango wa kuwinda watu wa namna hiyo, ili wafanikiwe, ndio imani
zao.
Anasema lakini hata hivyo, ili afanikiwe ni lazima akutane
na mmoja wa wazee wao, anayeheshimika yeye atafanya mambo yao, na matambiko
yao, ili hata mwili wangu ukikabidhiwa kwa hawo mamba maombi yafanye kazi
vizuri, na ili afike huko lazima atakutana na walinzi watiifu wa hawo wazee.
Kwahiyo alichofanya kwanza ni kuufikisha mwili wangu kwenye
pango lake, humo, akanivikwa nguo za ngozi,ili kunificha, halafu ndio
akanibeba, kwahiyo njiani walijua kwua kambeba mgonjwa au mtu wake, na kweli
kila aliyekutana naye, alimwambia kuwa huyo ni mgonjwa anampeleka kwa tibabu
wao, na walipotaka kumsaidia alikataa.
Basi akafika huko kwenye eneo ambalo wao wanaliita eneo
takatifu, ni eneo wanapoishi wazee na wakuu wa jadi. Na kwa vile yeye mwenyewe
ni ukoo wa wakuu wa jadi, haikuwa vigumu kwake, aliweza kuingia hadi sehemu
inayostahili, akauweka mwili wangu, na kumtafuta mtu wake ambaye nib au yake,
mmoja wa watu mashuhuri humo.
‘Babu nimekuja, nimekuja kwa jambo muhimu sana, kama unajua
hali zetu kwa sasa ni ngumu, na inavyojulikana tunatakiwa tutafute damu ya
kuwapa mizimu yetu na damu nzuri ni ile ya hawa watu wa waliopotea,’akasema.
‘Kwahiyo umeshampata ?’ babu akamuuliza.
‘Ndio nimempata..’akasema.
‘yupo wapi, ni mwanamke au ni mwanaume?’ akaulizwa
‘Ni mwanamke’akasema na babu yake akahema,kwa muda,
akazungumza maneno yao ya maombi, halafu wakaongozana hadi pale alipokuwa
kaniacha, lakini alipofika pale hakunikuta. Ikabidi ashituke na kuanz akutafuta
huku na kule.
‘Niliuacha mwili wake hapa, kuna mtu kauchukua’akasema na
msakao ukaanza , na sikuweza kuonekaan kwa haraka, ndipo babu akaitisha kikao
cha haraka cha wazee humo ndani, na babu alikuwa mmoja wa wakuu,
anayeheshimika, wakuu mle wakakutana na kuanza kusikiliza hilo tatizo.
‘Jamani mnajua hapa ni sehemu takatifu, na tendo
lililofanyka hapa ni tendoo ambalo halistahili sehemu kama hii, kwanza kabla ya
yote naomba yule ambaye aliuchukua mwili wa kafara ulioletwa na mjukuu wangu
ajitokeze kabla hatua nyingine hazijachukuliwa.’ Babu akasema na watu pale
walikuwa wakimuogopa sana.
Mara akatokea mmoja wa wazee wa pale, ni mkuu na yeye,
akakohoa na kusema kwa sauti ya kutisha,;
‘Una uhakika na hilo unalotaka kulisema; kuwa mwili wa
kafara uliletwa hapa, huoni kuwa unakwenda kinyume na maadili yetu, kuwa ili mwili utambullikane kama ni mwili wa kafara kwanza huyo mtu anatakiwa kweli alistahili kuadhibiwa, na pili kama keshakufa, uchunguzi ufanyike ijulikane kafa kwa kitu gani,na kabla ya kufa alikuwa na makosa, yanayostahili kuadhibiwa...na hili linatakiwa lipitie kwenye utaratubu wa mila na desturi zetu?’ akasema huyo mzee.
‘Kwanini nisiwe nauhakika wakati mjuu wangu ndiye
aliyeuokota huko nyikani, na aliukuta ukiwa umejitundika, ina maana kuwa huyo
mtu aliuliwa kwa makosa,au aliamua kujiua mwenyewe na hilo ni kosa,kwahiyo
anastahili kuliwa na mamba wetu’akasema babu.
‘Naona mzee mwenzangu unaanza kukiuka mamb muhimu ya hapa ,
hii ni sehemu takatifu, na tunatakiwa tuihehimu, na ili mtu wa namna hiyo,
akubalike kuwa anafaa kwa kafara ilihitajika tukutane,na tupitishe hukumu kwa
pamoja je hilo lilifanyika?’ akauliza huyo mzee.
‘Hili lingelifanyika, nilitarajia baada ya kuuona huo mwili,
niwaite tukutane, na nilipofika sehemu aulipowekwa huo mwili tukakuta haupo, je
huoo mwili upo kwako?’ akauliza huyo mzee.
‘Kwanza tumalize moja, ukubali kuwa umekosea,’akasema huyo
mzee ambaya mara nyingi amekuwa mpinzani wa babu wa mume wake,na wamekuwa
wakishindania madaraka, na hata ilifikia hatua waliingia kwenye mapigano, kati
ya familia hizo mbili.
‘Siweze kukubali makosa ambayo sijayafanya’akasema babu,
kwani kama angekubali, ingebidi ashushwe daraja, kutoka kwa wazee wa juu hadi
chini, ambapo asingeliruhusiwa kuingia kwenye uongozi au kushiriki kwenye
maamuzi ya kimahakama.
‘Basi mimi naomba tuitishe baraza la wazee tuhukumu hili,
maana tukiliachia likiendelea kuwepo heshima ya mahali hapa itaharibika’akasema
huyo mzee mwenzake na hata kabla hajajibiwa akatoka ikiwa na maana anakwenda
kuwaita wazee wa mahakama.
Shauri likapitishwa kuwa kikao hicho kifanyike,a usiku, sasa
ukumbuke mimi natambulikana kuwa ni maiti, je maiti ingeliweza kukaa siku tatu,
maana hiyo ilikuwa siku ya tatu , tangu nichukuliwe kule nilipokuwa
nimejitundika. Wao wana dawa za kuufanya mwili usioze, lakini mwili ukikaa
zaidi ya siku tatuu haifai tena kwa tambiko.
‘Babu akajaribu kuwaona wazee wenzake kulielezea hilo,
lakini ilishindikana kwana kauli ya huyo mzee wao inahehimika , kwa vile ana
wafuasi ambao wapo nyuma yake na ambao ni nusu ya wajumbe, kwani kwa muda ule
alishatafuta wazee wa namna hiyo waliomunga mkono, na wakizidi nusu basi ombi
lake linakuwa na nguvu.
‘Mjukuu wangu naona hilo limeshindikana, na iliyobakia hapa
ni jinsi gani ya kujilinda ili nisije nikashushwa daraja, na pia kuhakikisha
hawa watu watoi adhabu kubwa ambayo huenda ikaleta majonzi kwenye familia
yetu.’akasema Babu.
‘Babu nisamehe,sikujua kuwa ninaweza kukuingiza kwenye
matatizo kama haya ..’akasema mume wangu
‘Ndio maisha mjukuu wangu, katika maisha mambo kama haya
hutokea, cha muhimu ni kujipa moyo na kutafuta njia ya kukabiliana nayo’akasema
Babu.
‘Sasa tutafanyaje?’ akauliza mjuu wake.
‘Hapa kwanza niachie muda
nifikiri, na nitalifanyia kazi hili jambo, kwani ni lazima nifanye uchunguzi nijue ni
nini kilitokea, na kama kuna jambo tulijue tutafanyaje,maana mwenzangu
asingelifanya haya yote kama hana ushahidi na anajua kuwa hata nikifanay nini
sitaweza kumshinda, kwanza inabidi nitoke, kidogo’. Ikabidi Babu atoke humo
asafiri sehemu ya mbali kwa haraka.
‘Huko alipokwenda ni kijiji ambacho sheria nyingi za mila
zao ndipo zilipoasisiwa, wao walihamia hapo baadaye ili kutafuta maisha lakini
sheria zao nyingi zinatoka huko walipozaliwa mababu wa mababu zao. Huko
alitakiwa kukutana na wazee wa jadi , na pia kuna wataalamu ambao huangalia
matukio kwa mbali zaidi. Babu aliwaendea hawo akijua ndio kimbilio lake, ….
Babu alipofika huko kwa hawo wataalamu ndio wakamuelezea
ilivyokuwa, kuwa huyo binti hana hatia, ni binti aliyenusurika na uzalilishaji
, na hata kuzaliwa kwake ni mizimu yao iliyobariki, na ilijulikana kuwa ipo
siku atarudi hapo, halafu aolewe... Na wenzake walishajua kuwa huyu anaweza kuwa mmoja wa
warithi wa mama wa ukoo, na ndio maana na hastahili kutupwa kwa mamba, na
wenzake wanalijua hilo...’
‘Kwa vipi aolewe maana sisi tujuavyo ni maiti’akauliza babu.
‘Huyo binti hajafa, kapoteza fahamu tu, lakini kama ikifika
saa kumi na mbili anaweza asizindukane kabisa, kitakachomuokoa ni dawa
nitakazokupa wewe, hata wao hawajajua kuwa huyo binti anaweza kuzindukana
kutokana na dawa maalumu, wangelijua wangeshafikia mbali kufanya mamboo yao….’akasema huyo mtaalamu.
‘Sasa cha muhumi hapa ni muda, kwanza chukua hizi dawa nenda
kamnusishe puani, na akizindukana mfungisheni ndoa haraka, …’akaambiwa na babu
akaingiwa na hamasa, kwani aliwahi kuota ndoto inayomuelekeza kuwa amtafutie
huyo mjukuu wake mke, mke ambaye anaweza kusaidia familia yao kuwa watawala wa
hilo kabila lao.
‘Lakini hilo linatakiwa lifanyike kabla ya saa kumi na mbili
jioni , kwani ikifikia hapo huyo binti
hataweza kuzindukana tena, atakuwa keshakata roho, ..nyie cha kufanya ni
kuhakikisha ndoa inafanyika,na baada ya ndoa inatakiwa kweli tendo la mke na
mume liwe limeshafanyika, ili kuhalalisha na kuondoa kosa hilo ambalo mpinzani
wako anataka kukushika nalo’ akapewa hayo masharti.
‘Lakini kwanini ,ina maana hawajui kuwa yupo hai, na kama
wanajua hilo kwanini wanafanya hivyo makusidi ili huyo binti asizinduakne tena?’
akasema babu.
‘Hilo sio muhimu kwa sasa,….huenda bado hawajalifahamu hilo,
kwasababu huu utaalamu tunazidiana, nyie fanyeni kwa upande wenu, ili mjiokoe,
haraka, na mumuokoe huyo binti’, wa kusema lolote,..’akasema huyo mtaalamu.
‘Wenzenu hilo wamejpanga vyema,na mkifanya kosa, hamtakuwepo
humo tena na mbaya zaidi yatawaandama, fanyeni muwezavyo, na swala la muhimu
hapo ni muda.....’akasema huyo mtaalamu.
Babu aliondoka hapo akiwa na mawazo mengi, hakujua kuwa
mwenzake kumbe muda wote huo, alikuwa abdo anamtafuta, yeye alijua kuwa
wameshapatanishwa na uadui haupo tena, lakini kumbe wenzake wanahamu ya
kuwaondoa humo kwenye uongozi na ikibidi waangamizwe yeye na ukoo wake.
‘Kwa jinsi ilivyo, na
kwa vile ukoo wa huyu jamaa ni mkubwa na una wajumbe wengi, najua watampigia
kura yeye ili aonekane ni mkweli’. Babu akachanganyikiwa maana huyo ni mjuu
wake toka kwa binti yake kipenzi. Muda ulikuwa umekwenda kweli,na ilibidi arudi
huko mapema, ili kumuokoa huyo binti, kabla hajafanyiwa lolote…
Babu alipofika tu, akamchukua mjukuu wake na kumsomesha,
nini kinatakiwa kifanyike, kwa haraka, akawatafuta vijana wengine wawili
wanaomtii wa ukoo wao, na wakaanza kuutafuta
mwili wangu ulipo, maana hadi muda huo nilikuwa kama maiti tu.
Walikuja kugundua kuwa nipo sehemu anayokaa huyo mshindani
wake, ambapo ili uingie hapo nilipo
inabidi ukutane na huyo mshindani wake. Na yeye alijitahidi muda wote
kuwepo hapo, na kama hayupo wanakuwepo walinzi wake watiifu.
NB BLOG YENU INAWATAKIA IDD-EL HAJ NJEMA,
Ni mimi:
emu-three
4 comments :
A very impressive article. Well prepared. Very motivating!! Set off on to way
Kisa kinasisimua na kuogopesha....utamu unakolea. Nami nachukua nafasi na kuwatakieni wote IDD-EL HAJ NJEMA.
Vancouver led lighting store has over a hundred different kinds of products. Our LED lighting products mainly come from the factories in Taiwan, which could offer a cheaper price and good quality. Also, we can create any word or graphic in commercial LED lighting for our client and we will charge for a cheaper price than other companies. Please ask fo our employee for detail. http://www.vancouverledlighting.com/
bear grylls messer
Also see my page - bear grylls messer
Post a Comment