Mume wangu alipopata taarifa hiyo toka kwa babu kuwa huyo
msichana aliye mchukua bado yupo hai, wakati yeye alijua kabisa kuwa kabeba maiti,
na huenda kumbe huenda huyo msichana ndiye yule aliyewahi kutabiriwa kuwa
atakuwa maliki wa koo zao, na kwahiyo atakayemuoa , anayakiwa kumwa kiondozi wa
koo zote.
Kawaida kablahili lenye koo ndogo ndogo nyingi,huwa
zinamchagua mama , au malikia ambaye anapewa heshima kama mama wa kabila, mama
ambaye anaheshimiwa kama mkuu wa kabila, ni sawa na kuitwa mfalme. Mume wake ndiye mtawala wa kabila na ndiye
amiri jeshi , kiongozi wa mapambano, ..pamoja na sifa nyingine anatakiwa awe
keshawahi kupambana na simba peke yakem na kumuua,
Mume wangu alishapitia mitihani hiyo, alishawahi kumuua
simba peke yake, lakini pamoja na hayo asingeliweza kuingia kwenye eneo
takatifu mpaka mambo mengine ya kiutawala yapitishwe, kama vile kukubaliwa na
nusu ya wajumbe wote, na asiwe na sifa zozote mbaya, ikiwemo kuchafua eneo
takatafu kwa matendo yasiyokubalika.
Kutokana na utabiri wa mtabiri mkuu, ambaye alipokuja
kuwatembelea wakati wanazindua eneo hilo jipya,aliwaambia ukoo huo ili uwe na nguvu,
utahitajika kumpata malikia, lakini malikia huyo hatatokana na wao,..licha ya
kuwa damu ya asili ni wao, lakini atakuwa kazaliwa sehemu nyingine, huyo atakuja
hapo kwa njia ya kipekee kabisa….’huyo mtabiri akasema na walipomuuliza njia
gani hiyo ya kipekee, alisema;
‘Hayo mambo ya ndani sana, hata mimi siwezi kuyajua, ila
ujio wake, sio wa kawaida, na juhudi zenu ndizo zitamfanya aweze kuolewa na
miongoni wa vijana wenu, na huyo kijana muda wake ukifikia, kuwa mtawala, atamiliki
eneo hili, ila itachukua muda mpaka kukubalika…’akasema.
Waliambiwa akifika hapo kutatokea mambo mengi, ambayo
yatakuja kijileta yenyewe hadi ifikie hatua ya kutawaza kuwa malikia, lakini
yote hayo yanategemeana na juhudi za kila ukoo ili mmoja wa kijana wao aweze
kuwa mume wa huyo binti. Mume wake atakabiliwa na mitihani mingi, lakini mwisho
wa siku ndiye atakayekuwa mtawala wa eneo hilo, hapo umri ukifikia.
‘Babu isije ikawa mimi ndiye niliyetabiriwa na huyo binti
ndiye malikia mtarajiwa?’ akasema mume wangu.
‘Usiitoe hiyo kauli tena, kama ni wewe hayo yatajileta
yenyewe, maana wenzako wakisikia hilo, watafanya kila mbinu kuhakikisha kuwa
huyo binti, wanampata wao, au ikishindikana wakiona hawatampata wao wanaweza
hata kumuua,.. hilo hakuna mwenye uhakika nalo kuwa ni nani aliyetabiriwa ni
siri kubwa sana, hata huyo mtabiri hajui ni nani mstahili…’akasema babu.
‘Cha muhimu kwa sasa ni kuhakikisha tunamuokoa, na hapa la
muhimu zaidi ni muda, ..kwani ikifika saa kumbi mbili, hatutaweza kumpata tena,
na huenda ikawa ndio mwisho wake wa kuishi, sasa tutaingiaje mle ndani,..?’
akajiuliza babu.
‘Babu kama ni hivyo,basi tutumie nguvu,mimi nitawatayarisha
vijana wenzagu tutavamia na kumteka huyo binti’akasema mjukuu.
‘Hilo likitokea hiyo sifa ya huyo mtu wa kumuoa huyo malikia
itakuwa imefutika, na ukumbuke kuwa mwenzetu alishajiandaa kwa lolote lile,
kama unakumbuka vyema,siku za nyuma hapa mwenzetu huyu amakuwa akiandaa jeshi ,
mapaka tukawa tunajiuliza lengo lake hasa ni nini, wakati tumeshasuluhishwa, na
wote kwa hivi sasa bado wapo maporini wakijifunza mbinu za kivita, wameandaliwa
tayari kwa lolote,akitoa amri wataibuka toka huko mafichoni,…’akasema babu.
‘Sasa tufanyeje?’ akauliza.
‘Wewe ndiye unatakwia kufikiria, ujue mtawala bora ni yule
anayefikiria zaidi ya wengine, na mawazo yake yanakuwa na tija, ..hasa kipindi
kama hiki, amacho kila mmoja anakuwa na mawazo yake, ubinafsi mwingi, na kila
ukoo unavutia kwake, lakini mtawala bora mwenye hekima ataweza kuwaunganisha na
kuwa kitu kimoja, bila kujali tofauti zao…’akasema babu.
‘Sawa nimekuelewa babu, naomba nikayafanyie kazi mawazo yako,
ngoja niwahi, maana naona muda unakwisha, na tusipofanikiwa hili, moyo wangu
utauma sana,kwani mimi ndiye niliyemchukua binti wa watu nikijua kuwa ni maiti,
kwahiyo lolote baya likitokea nitakuja kujilaumu kwenye nafsi yangu, licha ya
hayo mengine, ..’akasema na babu yake akamshika kichwa, ishara yao ambayo
inajulikana kama ishara ya baraka.
Alipoondoka, babu akabakia
akiwaza jinsi gani ya kuingia mle ndani, lakini akilini mwake akajua kuwa
mjukuu wake atafanikiwa, cha muhimu yeye ni kuhakikisha kuwa anaweza
kuwashawishi wazee wengine ili wamuunge mkono.Akainuka na kuelekea eneo lao
walijualo kama eneo takatifu.
*********
Katika upande wa pili, nyumbani kwa mpinzani, kulikuwa na
punda wa kimila, punda huyo alikaribia kujifungua, na anatakiwa
akijifungua,maziwa ya kwanza yanyewe na mzee wa kimila na ya pili yanyewe na kijana
ambaye wanamtambua kama mtarajiwa wa kuingia kwenye uongozi , na muda wa
kumtafuta kijana kama huyo ulishakaribia.
Wao kama wazee kazi yao ni kutoa maelekezo, na vijana ndio
watenda kazi, na ili hilo lifanikiwe ni lazima awepo jemedari, jemedari huyo ni
yule atakayemuoa malikia, malikia ndiye mama mtawala, anayeheshimika, mlezi wa
koo zote.
Babu ambaye ni mpinzani wa mume wangu alikuwa haondoki kule
makao makuu kwa ajili ya kulinda mwili ambao alishauona ni ushahidi wa kummaiza
adui yake kisiasa. Yeye kutokana na taarifa na ushahidi alio nao, alishaliona
kuwa mpinzani wake ana makosa, na akiweza kuuwakilisha mbele ya wazee wenzake,
mwenzake huko atafukuzwa, na kijana wake anayemtegemea anaweza kuhukumiwa kuwa
chakula cha mamba.
Lakini kuna mambo ya kimila ambayo katika ukoo wake, inabidi
ashiriki, kwao waoo punda ni mnyama muhimu sana, akijifungua, wanaona ni sehemu
ya baraka, na maziwa yake, yanachukuliwa kama dawa, pia kama maziwa ya baraka.
Na yeye kama mkuu wa ukoo, anatakuwa awe wa kwanza kuyanywa , na kuhakikisha kuwa
mjukuu wake ambaye ndiye waliyemuandaa kwenye kugombea ujemedari wan a uongozi
wa kabila anakuwa wa pili kuyanywa hayo..
Alishawaambia nyumbani kwake, kuwa huyo punda akikaribia
kujifungua aitwe haraka, lakini akajikuta ana akzi hiyo muhimu ambayo
aliihitaji yeye mwenyewe aisimamie, kwani wengine wanaweza kushawsihika
wakaachia nafasi muhimu kama hiyo. Akawa anawaza je ikitokea huyo punda akajifungua
siku hiyo atafanyeje, kwani yote hayo yanamuhitaji yeye, alipowaza hilo
akamuita mmoja wa makamanda wake, akamwambia;
‘Huenda nikaitwa nyumbani, nikiondoka hapa nataka wewe
ubakie hapa mlangoni, hakikisha haingii mtu yoyote humo ndani, hasa hawa
wapinzani wetu, mtu utakayemruhusu kuingia hapa ni yule mama tibabu ambaye
anatakiwa kuhakikihsa humo mwili hauozi kabla ya wakati wake…..’akatoa amri.
‘Sawa mzee,mimi nipo kwa ajili yako’akasema huyo jemedari ni
kutoka nje akisubir amri nyingine.
********
Wakati huo huo, mume wangu alifika eneo ambalo ni la ukoo wa
maadui zao, kipindi cha nyuma walikuwa wakitembeleana, lakini ni kwa nadra sana
na kwa kificho, na akiingia mtu wa upande wa pili anaangaliwa kwa makini ili
watu wajue nini anachofuata. Mume wangu alitumia mbinu za kificho asionekane,
akijua kuwa akionekana anaweza hata kuuwawa.
‘Bibi Kis, najua unampenda mtoto wa mzee, adui wa ukoo wetu,
lakini yeye hakupendi kwa vile unatoka katika familia ya kimasikini, leo
nimekuja na jambo litakalokuwezesha kuolewa na huyo unayempenda, ikifuata
masharti yangu’akasema mume wangu baada ya kuweza kupenda hadi kwenye familia hiyo
kwa uficho, na akatafuta mbinu za kumuita huyo binti, kwenuye kichaka, ambapo
walianza kuongea kwa sauti ya chini kwa chini.
Binti huyo alikuwa miongoni wa warembo wa hapo kijijini,na
alikuwa miongoni wa ukoo wa babu adui wa ukoo wa mume wangu.Binti huyo, aliwahi
kukutana naye kipindi cha nyuma na mume wangu alitokea kumpenda sana, lakini
kutokna na hisitoa ya uadui wao, hakukubaliwa kumuoa, kutoka kwao, na kutoka
kwa koo hiyo ambayo ni adu mkubwa wa ukoo wao. Kutokana na uadui wao, hakuna
aliyejenga nyumba, ambazo ni ni mahandaki mlango, ukaelekea upande wa maadui
zao.
Huyu binti hakuwa akimpenda sana mume wangu, kwasababu hizo
zakihistoria, alijua hawezi kuolewa naye tena, akawa akimpenda sana mtoto wa babu
huyo adui wa ukoo wa mume wangu. Na mapenzi yao yalifikia hadi kutaka kuoana,
lakini walipolifikisha hilo mbele ya wazee wa ukoo, wakalipinga, wakidai kuwa
huyo binti hastahili kuolewa na huyo kijana, kwani hana sifa zinazotakiwa,kwani
malkia mtarajiwa anasubiriwa.
‘Na ukumbuke familia zote hapa, koo zote hapa, zinamsubiri malikia
mtarajiwa ambaye tumeambiwa atakuja kwa njia ya ajabu, wewe sio huyo malikia,
maana wewe ni mzaliwa wa hapapapa,na huyo malikia atakuja kutoka nje,ndiye
atakayeolewa na kijana wetu,…’akaambiwa,
Wazee hawo wakisema neno, linakubalika mara moja, hakuna
anayepinga, kwani ukipinga lazima utakutwa na mambo mabaya, ambayo yanaweza
hata kuimaliza familia nzima kwa vifo vya ajabu ajabu au magonjwa yasiyotibika.
Huyu binti alijua hilo, kwahiyo akatulia na kusubiri mume mwingine, lakini alipokuja
huyo mume mwingine ambaye ndiye mume wangu, akakataliwa nay eye, hapo akakata
tamaa.
Aliwauliza wazazi wake, je ina maana yeye hataolewa tena,
maana watu wawili aliowapenda wanakataliwa. Wazazi wake wakampa matumaini kuwa
ipo siku atakuja ambaye anamfaa, anachotakiuwa ni kuvuta subira.
*******
‘Wewe umefuata nini tena hapa, hukumbuki tulivyoambiwa kuwa
nyie ni maadui wa ukoo wetu, hustahli kunioa, kama isingelikuwa hivyo,
ningekubali unioe kuliko kubakia hapa nyumbani, wenzangu wote wa umri wangu wameshaolewa,
mimi kila mume anayekuja kunitaka kunioa nakataliwa…’akasema huyo binti.
‘Usijali binti, kila jambo lina muda wake, na natumai sasa
utaolewa, lakini yote inategemea ujasiri wako,…’akaambiwa. Yule binti,
akashikwa na mshangao, akatizama huku na kule akiogopa asije akaonekana, kwani
alishabigwa marufuku kukutana na huyu mwanaume aliyesimama mbele yake,akauliza
kwa mshangao
‘Ujasiri gani huo!?’
akauliza.
Walikaa kwa muda huku
mume wangu akimuelekeza nini cha kufanya , na yule binti alipoelewa, akakubali,
na kusema yupo tayari kujitolea kwa hilo ilimradi, ahakikishe kuwa mwisho a
yote hatapata madhara.
‘Kiutaratibu, wewe hutadhurika,kwasababu kwaza huyo atakaye
kuoa anakupenda, na mambo yakikamiliak na kufanyika ndani ya jengo takatifu,
hayastahili kutenguliwa tena,…na hilo lutachukuliwa kama majaliwa ya wazee, na
mzimu ya hapo, …cha muhimu ni kuhakikisha mbinu hizi unazifuatilia hatu kwa
hatua, bila kutetereka.
‘Sawa, ngoja nikajiandae, na najua bibi yangu anazo hizo
dawa, ….’akasema akijua kuwa bibi yake ndiye tibabu wa ukoo kwa wanawake, na
ndiye peke yake aliyeruhusiwa kuingia kuuona huo mwili, na bibi yake ni mtiifi
mkubwa wa wazee, na anatambulikana na kuheshimika. Alijua atamdanganya
hatamwambia ukweli nini anachotaka kufanya.
‘Dawa sio shida dawa hizi hapa ninazo..’akasema huku
akimkabidhi vifurushi vidogo viwili vya dawa huku akisema;
‘Hii dawa ya jani hili lililokaula ni ya kumzindua huyo
binti ni ya unga unga, imo humo ndani, na akishazindukana, wewe utapiga
ukelele, …’akasema kwa haraka haraka, na yule binti akatabasamu, na kusema;
‘Nimekuelewa, …najua kwanini nipige ukelele, ili waingie,
wakiingia, mimi nitakuwa nimechukua nafasi ya hiyo wanayoiita maiti, lakini je
wakinichunguza, si wanaweza kunigundua kuwa ni mimi , ndoa itafungwaje na pia,
huyo ….hiyo maiti itakayofufuka, isipofuata hayo ,mnayotaka nyie, yafanyike itakuwaje?’
akauliza.
‘Hayo hayatakuhusu tena, kuna watu watakuwa wanafutailia
kila hatua, …wewe usiwe na shaka’akaambiwa.
‘Basi kama ni hivyo tu, mbona rahisi sana …, mimi nipo tayari
kufanya lolote ilimradi nihakikishe nimeolewa na yule mume, lakini kikwazo ni babu
yake, …namuogopa yule mzee,mpaka wakati mwingine namuota kama shetani, ananijia
huku akinitisha, ..lakini licha ya hayo yote, nina uhakika nikishaolewa pale
watanifurahia baadaye kuwa kweli wamepata mke…’akasema huku akitabasamu kwa
furaha.
‘Lakini kumbuka maelekezo yangu,kwenye hiyo dawa ya pili, hiyo
ina nguvu sana, ukishainusa tu puani kwako, unakuwa kama umekufa….kwahiyo
hakikisha kuwa kabla hujainusa,uwe umeshajiandaa, uwe umeshavaa nguo za huyo
binti, na uwe umeshalala sehemu yake, kwani ukiivuta tu, utashikwa na usingizi
mnzito sawa na mtu aliyekufa…’akaambiwa.
Yule binti kwanza akasita akiwazia hilo neno kuwa atakuwa
kama mtu aliyekufa,akajiuliza je wasiponiwahi ndio maana nimeshakuwa marehemu.
Lakini wasiwasi huo ukaondolewa kwani aliambiwa;
‘Usiwe na wasiwasi, utawahiwa kama sio wao, mimi mwenyewe
nitakuja kukunusisha hiyo dawa ili uzindukane, kwani kuinuka kwako ni mpaka kukunusisha dawa nyingine, na hilo litafanyika
tu usiwe na shaka’ Binti aliposikia hivyo akaichukua zile dawa, huku akiwa na
mawazo mengi kichwani.
Baadaye wakaagana na huyo jamaa,ambaye ndiye mume wangu, na
akarudi nyumbani haraka, alipofika nyumbani kwao,kabla hajapumzika tu ili ajiandae
kwa kazi hiyo aliyopewa, akasikia hodi, na alipofungua mlango akakutana uso kwa
uso na babu , babu ambaye amekuwa kikwazo katika mapenzi yake na mjuuku wa huyo
babu, akahisi mwili ukiisha nguvu, akatoa macho kwa woga na kabla hajasema
neno,yule babu akasema;
‘Nimekuja kukupa onyo…nimesikia kuwa wewe ni msaliti,wewe
unatoa taarifa zetu kwa maadui zangu , kwa yule kijana, wao, ….kwanza nimeshakuambia,
kuwa hatutaki kabisa ukoo wetu kuolewa huko, …pili wewe hustahiki kuolewa na
mjuu wangu, kwasababu ambazo huhitajiki kuzijua..‘akasema huku akiwa katoa
macho , macho ambayo binti huyu alikuwa akiyaogopa kama nini.
‘Sasa siku nikikufuma na huyo kijana, siku nikipata
ushahidi, nitahakikisha unakuwa nyama ya mamba, nitakubeba mwenyewe na
kuhakikisha umetafunwa hadi mfupa wa mwisho…’akasema huku akimnyoshea fimbo
yake iliyovikwa ngozi ya nyoka.
‘Kama nikuolewa utaolewa na kijana yoyote wa ukoo wetu,
..lakini sio mjukuu wangu, hilo ulisikie na uliweke akilini, unasikia?’ yule
babu akasema huku akitoa macho yake ya kutisha,na hakusubiri yule binti atamke kitu,
akageuka na kuondoka, na kumuacha yule binti akiwa anatetemeka mwili mnzima.
NB: Umeme umekuwa kikwazo, lakini hiki kipnde kwa leo
kinatosha.
WAZO LA LEO:
Mitihani ni sehemu ya maisha, tunahitajika kukabiliana nayo, tukijua kuwa mungu
yupo pamoja nasi wakati wote, tuzidi kumuomba kila mara, ipo siku tutafanikiwa,
tusikate tamaa.
Ni mimi:
emu-three
1 comment :
Kwanini usiingie ubia wa watu wa BONGO MOVIE, mimi naona hiki ni kipaji muhimu sana, usikipoteze bure.
Post a Comment