Binti Kis kama walivyokuwa wakimuita, akiwa keshafika ndani
ya jengo takatifu, ghafla woga ukaanza kuiteka nafsi yake, akihis sura nyingi
za watu zikimtizama, na moja wapo ilikuwa ya yule mzee anayetisha, na huku akikumbuka
maelezo mengi yanayosimulia kuhusu mahali hapo, mwanzoni alikuwa haogopi, lakini pale mguu
wake ulipokanyaga eneo jeupe la aradhi ya sehemu hiyo akili mwili ulilegea.
Akawa kaam sio yeye, akawa anatembea kwa uwoga, na ile hali
ilimfanya awe kama mgonjwa anayejikokota kufika kituo cha matibabu, na huku
akili yake ikianza kukumbuka yale aliyowahi kusimuliwa na bibi yake kuhusu eneo
hilo, na sauti ya bibi yake iliposikika kwenye ubongo wake,akahisi ageuka na kuanza
kukimbia kutoka eneo hilo.
Lakini cha ajabu hakuweza, miguu yake ikiwa imeisha nguvu,
akwa anajikongoka kuelekea sehemu kulipojengwa jengo, na humo ndani kuna
mahadaki mengi, ambayo humilikiwa na koo mbali mbali kama ofisi zao, na sauti
ya bibi yake ikaanza kumjia akilini ikimuelezea kwanini eneo hilo likaitwa
mahali patakatifu;
‘Mjukuu wangu enzi zetu tulipohamia hapa nilikuwa bado mbichi,
mwali ambaye alikuja kula fungate na mume wangu mpenzi, nilikuwa nampenda sana,
kama alivyonipenda mimi,, huyo ndiye babu yako ambaye aliponioa tu, ikaja
taarifa hiyo kuwa baadhi tunahamia makao mapya, yalibashiriwa, na mimi
niliipokea taarifa hiyo kwa furaha.
‘Ina maana ulifurahia kuwaacha wazazi wako na kwenda kuishi
sehemu ngeni?’ akauliza mjukuu.
‘Unapoolewa ujue utamuacha mama na baba yako, hata kama
unawapenda vipi, na hili tulishaambiwa na mashangazi, na walimuw ajadi, kuwa
mume wako sasa ndiye atakayekuwa mzazi wako wa pili, yeye na wewe mnakuwa kitu
kimoja.
‘Ndio kuna ilehali ya kuhisia hivyo, kwa vile wazazi ni
wazazi, hawawezi kuwa mtu mwingine,na uchungu wa mwana aujuaye ni mzazi,lakini
lazima ndoa iwepo, lazima mume na mke wawepo, ili kujenga kizazi kipya, na
vyema yake ni kukipaat hicho kizazi mkiwa wawili, mke na mume...
Mimi kwa usichana wangu na kazi nyingi zanyumbani, nilikuwa najiona nachoka sana,nikajua kuwa anenda kuolewa na nitapata muda wa kuwa na mume wangu ambaye
kila mara nilikuwa nikfokwa pindi ninapotaka kwenda kuongea na yeye, sasa
nitakuwa huru,kwanu keshanioa, na tunakwenda
kuanz maisha ya raha, maana kuolewa wengi tunajua hivyo, kuwa umeshampata
mwenzako unayempenda, basi mtaishi kwa raha…’
‘Siku babu yako aliponiambia kuwa tunekwenda eneo jipya, ili
tuweze kuwa huru zaidi, nilimwambia, kokote unapotaka kwenda mimi nipo na wewe
na nipo tayari kwenda, kwani mimi ni mkeo wako nipo tayari kwa ajili yako, na
nitatii kila utakachonielekeza nikifanye, najua yote uliyopanga ni kwa ajili
yetu sote’,
‘Lakini huko tunapokwenda koo nyingi zimepanga kwenda huko,
huenda tukaanza kugombana wenyewe kwa wenyewe, kwahiyo ujiandae kwenda kuishi
maisha ya vita’akaniambia, na mimi nikakubali sikujua lolote kuhusu vita, maana
nilichukuliwa kwenye mikono ya wazazi wangu nikiwa nalelewa kama mtoto, licha
ya kuwa vita vilikuwepo vya hapa na pale,lakini sisi watoto tulichungwa sana,
tulilindwa kuhakikisha kuwa akili zetu hazitekwi na mambo ya kivita.
‘Mimi na babu yako tukaanza maisha, lakini siku zote yeye
alikuwa msituni, wakipigana, na wakati mwingine anarudi akiwa kaumia , ana
majeraha kila sehemu ya mwili, mimi
ndiye nahangaika kumtibia, na ingawaje ujuzi wa matibabu niliupata toka huko
kwetu, lakini uzoefu zaidi wa kutibia watu walijeruhiwa kwenye vita niliupatia
kwenye eneo hilo takatifu.
Kila mume wangu aliporudi na kumtibia akapona haraka ndivyo
taarifa za ujuzi wangu zilivyozidi kuzagaa, na hata kutolewa kwenda mstari wa
mbele wa vita kuwatibia majeruhi. Nikawa sasa naishi vitani, natabia watu
walioumia, na wakati mwingine naitwa majumbani kama kuna wakina mama wanaotaka
kujifungua, au watoto wagonjwa nikawa tibabu wa eneo lote hili.
‘Eneo hilo takatifu ndipo babu yako alipofarikia, akiwa akimtetea
mfalme, kiongozi wa kwanza ambaye tulihama naye, alijitoa nafsi yake
kuhakikisha kuwa kiongozi huyo haumizwi, na alikufa kifo cha kishujaa..’akasema
bibi.
‘Kifo gani hicho, cha kishujaa,mbona sisi hatupo kwenye eneo
takatifu na kutambulikana kama wafamilia ya watu mashuhuru, hata kuolewa
nimekataliwa eti sisi sio familia mashuhuri?’ akaulizwa bibi.
‘Eneo hio kila mmoja likuwa akiligombea, kwani ndilo
walilotabiriwa kuwa ni eneo takatifu, na kila ukoo ulitaka ulimilki , kwahiyo
kila kiongozi wa ukoo, alifika hapo na jeshil lake, kukawa na mapigano ya huku
na kule, kila mmoja akipigana na mwenzake.. wakati mwingine ni vita vya kuviziana, huyu akimuone mwenzake ni ukoo wa mwingine anajitahidi amuue, ....
Babu yako yeye alikuwa mlinzi wa kiongozi wa ukoo wetu, na
katika vita hivyo, ikatokea tukazidiwa na kiongozi wetu akazingirwa, babu yako
akawa anapigana nao, na kuna muda wenzao maadui walitupa mishale, babu yako
akajiweka mbele ya kiongozi wake, na mishale ile ikazama mwilini mwake,
….’akasema bibi kwa uchungu.
‘Na huyo kiongozi ikawaje?’ akauliza.
Yule kiongozi alipiga magozi akawa anamlilia babu yako, huku
akiwa haamini, na hutaamini wengi wa viongozi wakafanya hivyo wakapiga magoti,
kila mmoja akimlilia mlinzi wake, maana maaskari wengi walishafariki,
waliobakia ni majeruhi tu.
Na kumbe huku tulipotoka walishafikia uamuzi watume jeshi
kubwa kuja kudhibiti hiyo hali, jeshi lilipofika ndio likakuta hiyo hali
imeshakuw ambaya, waliobakia ni viongozi wa ukoo, na mjeruhu wengi,wakavamia na
kuwaweka wote chini ya ulinzi, na amri ikatolewa kuwa hakuna kupigana tena,
kwani mizumu na mababu waliozikwa eneo hilo wamekasirika.
‘Mtamwaga damu zenu mpaka lini, hamjui nyie ni ndugu,
mkirudi kinyumenyume kimaisha babu zetu walikuwa ndugu baba na mama mmoja,
wakazaliwa hadi mkafikia kizazi chenu nyie, leo hii mnawakata matumbo wazee
wenu,maana kuuana ni sawa ni kuwakata wazee wenu matumbo yao…
‘Sasa basi,amri moja, sitisheni vita na toka leo eneo hili
litakuwa takatifu, sheri mtapewa kutoka huko mlipokuwa awali, kuwa eneo hili
halitakiwi madhambi tena, kila mmoja ni lazima afuate sheria hizo na yule
atakayekiuka adhabu kali itamuandama, na ikithibitishwa kuwa yeye ndiye
mkosaji, atatoswa kwenye mto,huo mto umejaa mamba waliokuwa wakifungwa na wazee
waliokuwa wakiishi hapa awali,..mamba hao ni wakurithi, wana baraka zake,kazi
yao ni kula miili iliyotenda dahambiili hizo dhambi zipotee kabisa, ….
‘Sasa toka leo yule mkosaji atatupwa kwenye huo mto,..’ ikatolewa
amri na kiongozi mpya akachaguliwa, na viongozi wengine wa kila koo, sisi
hatukupa nafasi hiyo, maana watoto wangu walikuwa bado wadogo, walikuwa kwenye
jeshi jipya. Na tangu siki hiyo ikawa sheria msimeno kile mkosaji hakuonewa
huruma, akawa anatoswa ziwani, mpaka watu wakaanza kuogopa. Ilifikia muda mtu
akifanya dhambi kwa siri, anajikuta kafichuliwa bila hata kujua ni nani
aliyefichua hiyo siri, watu wakaanza kuogopa, na sheri ikaanza kufuatwa…
‘Kwahiyo mjuu wangu ukifika kwenye eneo hilo takatifi usije
ukajidanganya kuwa hauonekani, wapo watu waliokufa hapo kwenye vita wanakuona,
roho zao kila mara zinapita kupalinda hapo mahali,na mwenyewe ukifika mhali
hapo, kama ni mkosaji utajihisi kweli wewe ni mkosaji, uatahisi watu wanakuangalia,
wanakupigia makelele, na unaweza ukadondoka na kupoteza fahamu….’maneno ya bibi
yake, yalimfanya ahisi kuwa yeye ni mkosaji,na alipohisi mwili ukisha nguvu,
akajua muda wowote anaweza akadondoka na kupoteza fahamu, na alichowaza ni
kugeuka nyuma na kurudi huko alipotoka.
‘Usiwe na wasiwasi, wewe ndiye mke halali wa yule mwanaume
unayempenda,pigania kwa nguvu zote, huoni kila anateyka kukuoa anashidwa,
usiogoe, sisi tupo nyuma yako…’akakumbuka yale maneno aliyoambiwa na mume wangu…na
mara akasikia mtu akiwa nyuma yake, aliogopa kugeuka, akijua sasa anambuliwa,
kumbe alikuwa mmoja wa walinzi ambaye alimwambia aendelee mbele,..
‘Hapa sasa hakuna kurudi nyuma..’akasema kimoyo moyo, na
kusonga mbele, licha ya kuwa mwili mzima
ulikuwa ukisisimukwa kuashiri awoga na kuhisi kuwa hizo roho zinamuona kwa
hicho anachotaka kukifanya,lakini baadaye akasema kimoyomoyo;
‘Mimi sifanyi haya kwa nia mbaya,nafanya haya kwa ajili ya
mtu ninayempenda, na nina nia safi ya kuwa mke mwema kumtumikia yeye vyovyote
iwavyo, tatizo ni kuwa wengi hawanijui kuwa mimi ni mke mwema….’ akasema kimoyomoyo
huku akijitahidi kutembea akiigiza vile vile anavyotembea bibi yake, na wale
maaskari vijana walionekana kutokumtilia mashaka, waliinama kwa adabu na yeye
akapita kwa mwendo ule ule wa kibibi-kibibi.
Alishukuru sana mzaha wake aliokuwa akimfanyia bibi yake,
kwani mara kwa mara alizoea kumuigiza bibi yake anavyotembea na akifanya hivyo
bibi yake humkimbiza kwa fimbo. Siku moja alivaa nguo za bibi yake, na
kujifunika kama anavyovaa bibi yake. Bibi yake huwa anavaa na kujifunika mwili
mzima na kuacha sehemu ya macho,kwani sehemu hiyo takatifu hawafiki wanawake
bila kazi maalumu na kuna sehemu ambayo anakaa malikia, ndipo hapo wanawake
wanaweza kufika,
Siku hiyo alivaa kama anavyovaa bibi yake akawa anatembea
kama anavyotembea bibi yake, na kupita mbele ya baba yake,. Baba yake alijua
kabisa ni mama yake anayepita, akainuka na kuinama kwa adabu, baadaye akaanza
kucheka.
‘Wewe binti, yaani umefikia kumchezea mama yangu, nitakupiga
kipigo ambacho hutakisahau, wewe hujui thamani ya bibi yako, bibi yako ni mama
mtakatifu, tibabu wa eneo hili, anaheshimik,a akipita kila mmoja huiana chini.
Yeye alistahili kuwa malikia wa eneo hili, ila watu wabaya walimfanyai fitina’akasema
baba yake.
‘Usimpige mjukuu wangu, huoni kuwa ananirithi, hata nikifa
najua nina mtu anayelandana na mimi, na hata hivyo sikuhitaji kuwa malikia,
kwani ningeliolewa tena, na mimi sikutaka kuolewa,tena, baba yako alikuwa ndiye
mume wangu pekee, alipofariki, na mimi nilitaka nimfuete, ….nilitaka kujiua, na
hilo tendo likaniondolea sifa ya kuwa malikia wa eneo letu’akasema.
Leo hii hakuwa anagiza, alitakiwa afanye kweli, kama
alivyokuwa akifanya bibii yake, kuvaa kutembea, na kila kitu, vinginevyo
akijulikana atakuwa chakula cha mamba na atamkosa yule aliyempenda,na
kuwaaingiza wengine kwenye matatizo makubwa akaona kumbe kabeba dhamana kubwa,
na ni lazima aitekeleze.
Akawa anawaza jinsi gani alivyofamyia bibi yake, na ilibidi
afanye hivyo,kwani bibi yake asingelikubaliana na hayo anayotaka kuyafanya, akawa
ana wasiwasi, akiogopa kuwa huenda dawa aliyompulizia bibi yake inaweza ikwa
nyingi, tofauti na walivyoagizwa na kama ni nyingi inaweza kumuua kabisa bibi
yake, kitu ambacho asingeliweza kukivumilia, kwani kama bibi yake atakufa na
yeye itabidi ajiue.
‘Umpulizie kidogo tu bibi yako kwa mbali asiokuone, na
akilala, chukua nguo zake, na mengine ni kama nilivyokuagiza’akakumbuka
alivyoelekezwa, na hayo hakutaka kuelekezwa zaidi kwani yeye ni mtaalamu wa
kuigiza, kama angelipewa nafasi hiyo angelikuwa muigizaji wa kimtaifa.
Akaingia ndani ya lile jengo na yule jemedari akainama na
kumruhusu apite, hakuamini kwani sifa za huyo jemedari ni kuwa anaweza kunusa
kuwa huyu ni adui, …lakini aliona ajabu ya huyo jemedari kuinama na kumuheshimu
akijua kuwa huyu ni mama tibabu, bibi yake. Yeye akapita na kuingia ndani ya
jengo hilo. Alipoingia huyo jemedari alikuwa nyuma yake, akachungulia mara moja
kuhakikisha kila kitu kipo tayari, halafu akasema;
‘Kama unahitaji msaada wowote niite nipo hapo nje’akasema huyo
jemedari , na yeye akatikisa kichwa huku akijifanya yupo kazini, kwa kuushika
shika ule mwili, hadi alipohakikisha kuwa yule jemedari katoka nje. Akashisha
pumzi kwa nguvu huku akimshukuru mungu wake!
Aliushika ule mwili na kuanza kuuvua nguo zote, akaupaka
dawa ya kulainisha ngozi kama alivyoagizwa, halafu akazivua nguo zake na
kuuvalisha ule mwili, na yeye wakati huo ameshavaa nguo za ule mwili, na
alipohakikisha kuwa kila kitu kipo tayari, akauchukua ule mwili na kuulaza
chini, huku akiwa kaufunika uso, na kuhakikisha kuwa hakuna atakaye gundua
haraka ni nani huyo binti. Kawaida mwanamke anajifunika mwili mzima, na nguo
zao maalumu za ngozi za wanyama laini.
Alipohakikisha kila kitu kipo tayari, akapanda kitandani, na
kuchukua dawa kiasi kwenye kidole chake ile nyingine akawa kaificha ndani ya
nguo zake akalala na kujifunika uso kama ulivyokuwa ule mwili, akaivuta ile
dawa puani, na huku akapiga ukelele….akazama kwenye giza.
*******
Huku nje mume wangu alikuwa keshafika na vijana wenzake
wakiwa wamejificha sehemu maalumu na kuvaa mavazi wanayotumia maadui zao, kwani
kila ukoo ulikuwa na uvaaji wake,wakawa wanasubiri sihara, ishara ambayo ni
kilio,..
Babu alikuwa na kikao maalumu na wazee wenzake kweye shemu
maalumu, sehemu ambayo haingiliki ovyo, na hata watu wakipiga kelele huko nje
huwa hawasikii, na kuna vijana wakuleta taarifa kama kuna lolote limetokea, wao
walikuwa kwenye mazungumzo maalumu na wazee wenzake;
‘Jamani mimi niewaita, maana siku moja niliwauliza kwanini
mwenzetu anatayarisha jeshi msituni, nyie mkasema ni jeshi la ukoo, sasa wakati
umefika wa kumuuliza kuwa je hilo jeshi kama ni la koo zote mbona hawachukui
vijana wa ukoo nyingine’akasema.
‘Kwani tuna wasiwasi gani, kama anataka kuleta fujo sisi
tuna vijana wetu, na swala la kuwaita na kuwaandaa, na hilo haliwezi kutokea
maana tuna kiapo kikuu, akikiuka wenzetu watakuja atashikwa na vijana wake
watatupiwa mamba’akasema mzee mmoja.
‘Muwe na akili yakufikiri, hivi akishavamia na vijana wake,
akahakikisha amechukua madaraka, na kutumaliza sisi wazee wote, akapata kura za
wazee wenzake, ni nani atapata muda wa kwenda kutoa taarifa, na hata hawo wakifika
huko hamuoni kuwa atakuwa keshajipanga na uwongo mwingine’akasema babu.
‘Tukuulize wewe mzee mwenzetu una lengo gani kusema hivyo,
una wasiwasi gani au umekuja na hoja gani?’ akaulizwa.
‘Mimi hoja yangu ni kuwa na kikosi chetu kama hicho, na
tukiulizwa majibu yetu yatakuwa kama wao, na vijana wetu wapo tayari muda
wowote, ni kiasi cha kuwapa maelekezo’
‘Hilo ni wazo jema sana, na hata mimi nilikuwa nikiwaza
hivyo hivyo..’akasema mzee mwingine.
‘Jingine ni kuhusu huo mwili waliouchukua kama ushahidi, ….nahitaji
msaada wenu, hapo muda ukifika,kuna jambo nalifuatilia kwanza, hilo sitawaambia
kwa sasa.Nafanya hivyo kwasababu tunahisi wenzetu wana lengo kubwa, na lengo
lao ni kuhakikihs kuwa ukoo wetu hauna nafasi ya madakara, kwahiyo tunachohitaji
ni kuhakiksiha kuwa huo mwili unarudi mikononi mwetu’akasema babu.
‘Kwa vipi naye kaushikilia na kuulinda kwa nguvu zote…na
kwanini tuhangaika na maiti,?’akaulizwa.
Hilo nitakuja kuwaambia baadaye ni kwa maslahi yetu sote, vijana
wetu wapo, wataifanya hiyo kazi, ila lolote litakalotokea naomba tuwe
pamoja’akasema babu.
‘Tupo pamoja mkuu wetu’wakaitikia na mara akaingia kijana
mmoja akihema
‘Vipi kuna nini huko?’ akaulizwa.
‘Kuna ukelele umetokea upande ule wa maadui, na huenda kuna
tatizo, ..’akasema huyo kijana mtoa taarifa.
Wale wazee wakainuka na kutoka mle ndani na kuelekea huko
ulipotokea huo ukelele.
WAZO LA LEO:Sio vyema ukitenda kosa kumsingizia mwenzako, kama umeona umetenda kosa ni vyema ukakiri kuwa umekosea ili kusahihiswa, unapolisukumia hilo kosa kwa mtu mwingine unakuwa umetenda kosa mara mbili, kosa la awali ulilolitenda na kosa la kumsingizia mwenzako, huo ubaya ni roho mbaya, kumbuka kutenda kosa sio kosa, bali kurudia kosa ndio kosa.
Ni mimi:
emu-three
5 comments :
Nimelipenda sana wazo la leo, KUTENDA KOSA SIO KOSA KOSA KURUDIA KOSA
HONGERA KAKA
I drop a сomment eаch time I liκе a article
on а blog or I have something to vаluable to contribute to the cοnversation.
Usuallу it's caused by the sincerness communicated in the article I browsed. And on this post "Uchungu wa mwana aujuaye ni mzazi-16". I was actually moved enough to drop a thought ;-) I do have 2 questions for you if it's okay.
Could it be only mе or does it loοk aѕ if liκе some of theѕе
responses арреar liκe left by bгain ԁead
people? :-P And, іf you are wrіting at aԁditional οnline sіtes,
I'd like to keep up with everything fresh you have to post. Could you make a list every one of your communal sites like your linkedin profile, Facebook page or twitter feed?
Check out my web page - Money
Can I use some of the content from your site on mine? I will make sure to link back to it :)
First of all to see the quality [url=http://www.blackuggs4boots.com]black ugg boots[/url] of a fabric is shoes, if appear, chemical fiber, blending materials made [url=http://www.blackuggs4boots.com]UGG boots black[/url], it must is false; UGG in foreign countries is down the price also is in one thousand yuan associated with above, with hundreds of yuan extremely affordable prices for sale to be careful is fake. Genuine Uggs workmanship, especially the villi distribution denseness and length of villi are constant, watching from the work also compares is [url=http://www.blackuggs4boots.com]black uggs[/url] fine, light foot wear will be very comfortable, will not have a stiff feather firm feet feeling, and shoes self-respect is very light, no weight sensation.
---------------------------------------------------------
[url=http://www.blackuggs4boots.com]black uggs[/url] [url=http://www.blackuggs4boots.com]black uggs[/url]
Post a Comment