Ukelele ule uliwazindua walinzi wa eneo hilo, na kujiweka
tayari kusikia amri ya mkubwa wao, lakini walishangaa kuona kimiya, na wakati
huo msaidizi wa mkuu wa ulinzi alikuwa akihangaika kumtafuta mkuu wake, alipoona
kuwa mkuu wake hajarudi, akaona achukua hilo jukumu, kwani huenda ni tatizo
kubwa sana, japo kuwa alionywa kuwa asiingie humo ndani;
‘Mimi natoka kidogo, nemitwa nyumbani mara moja, mke wangu anatarajia kujifungua,
naona kuna dharura, sasa wewe angalia hapa mlangoni, hakikisha haingii mtu humo
ndani, hata wewe sioni haja ya kuingia humo, maana kilichopo humo na mwili wa
wa mtu, ambaye inatambulikana kuwa ni maiti…’akasema mkuu.
‘Sasa kwanini tunalinda maiti mkuu, ..?’ akauliza msaidizi
wake, licha ya kuwa alijua kuwa wanafanya hivyo kutokana na amri ya mzee
kiongozi wao.
‘Hilo sio swala la kuuliza, najua unajua jukumu lako nini, mimi
sitachukua muda mrefu, na usimwambia mtu yoyote kuwa nimetoka’akasema na
kuondoka kwa njia za kujificha, hakutaka ajulikane kuwa kaondoka humo, maana
hakuruhusiwa kuondoka hapo, hadi Mzee arudi, lakini mke wake ambaye yupo karibu
kujifungua kamuita huenda anahitaji msaada.
Alipotoka hapo, alikimbia moja kwa moja hadi nyumbani kwake,
na alipofika, alimkuta mkewe anahudumiwa na wakunga, na ilikuwa kama vile
alikuwa akisubiriwa yeye kwani alipokanyaga seheu ya kuingilia ndani, mara, akasikia kilio cha mtoto mchanga kuashiria
kuwa mkewe kajifungua, ….na vigelegele vikasikia.
Alitulia kidogo, akisbiri amri ya wakunga, na baadaye
yulemkunga mkuu akatoka na kumuashiria kuwa anaweza kwenda kumuona mkewe.
‘Umejuaje kuwa mambo tayari?’ akamuuliza, na yeye
akatabasamu, huku akijiuliza kichwani
mbona amesikia kuwa anaitwa na huyu mkunga anaongea kama vile hajui kuwa
anaitwa, hakujali akaingia ndani kumuona mkewe, na kwa furaha ile hakukumbuka
hata kumuulizia mkewe sababu ya yeye kuitwa kwa haraka hivyo.
‘Nawashukuruni sana , na sina muda wa kukaa ,kwani
nimeachiwa kazi kubwa huko, naombeni mumuhudumia mke wangu na nikipata muda
nitakuja’akasema baada ya kumwangalia mkewe na mtoto. Moyoni alikuwa na furaha
sana, lakini kwa upande mwingine alikuwa akisikitika maana kipindi kama hicho
alihitajika kuwa karibu na mkewe , lakini majukumu ya kikazi hayakumruhusu.
Alitoka pale akagundua kuwa katumia muda mrefu tofauti na
alivyotazamia, kwa haraka akaingia njia za vichochoroni, na alipofika sehemu ya
njia panda,ambapo angeliweza kuonekana, akaingia vichakani na kukatisha mmoja
wa msitu, akijichukua tahadahri zote za kutokuonekana na mtu yoyote.
Msitu huo anaujua vyema, kama jemdari, alijua kila eneo, na
wapi apite ili afike sehemu anayotaka kufika, na kwa muda huo alitaka atokee
eneo la sehemu yao takatifu. Alikuwa akitembea mwendo wa kasi, na mara akajikwaa,….
Kumbe ulikuwa ni mtego wa wanyama, hakuuona, akajikuta
akirushwa hewani na kuning’inia juu kwa juu, na haraka akatoa kisu kukata ile
kamba, kabla mishale ya ule mtego haijafyatuka, kama ni mtego wa kuua mnyama,
lakinikama ni mtego wa kumnasa tu mnyama, haitakuwa na shaka, lakini hakuwa an
muda wa kuthibitisha hilo, na hata hivyo kumbe kisu kilikuwa kimedondoka chini
wakati aanrishwa hewani.
Ni wakati anahangaika kujinasua ndio akasikia sauti ya
mtu,au watu, akafanya haraka kujinasua kwa kutumia mbinu za kivita, akadondoka
chini, alihisi alidondoka karibu na miguu ya mtu, lakini hakupata muda wa
kumwangalia, kwani alishikwa usingizi mnzito…na alipoamuka ndio akasikia.
‘Mkuu vipi, unaumwa nini…
*******
Huku makaoni,
msaidizi wake alipoona mwenzake hayupo, ikabidi achukua hatua, kwani huo mlio
uliashiria kuwa huyo bibi Tabibu huenda anahitaji msaaada wake, akaangalia huku
na kule na kuwaashiria vijana wake wawe tayari kwa lolote, kwani yeye anakwenda
huko ndani kuangalia kuna nini kimetokea,…
Mlio huo ulikuwa ni ishara kwa upande wa pili, kwani wao
walishajiandaa, na walijua huo muda hautakuja tena , na ukipotea bila mafanikio
watakuwa wamekosa kila kitu. Mlio huo uliashiria kuwa muda umefika, muda wa
kumuokoa binti ambaye anasadikiwa kuwa huenda akawa malikia mtarajiwa.
Kama ilivyopangwa Vijana maaskari wenye sare
inayotambulikana walifika hapo, wakisema wamesikia sauti na wametumwa na mkuu ,
kuangalia kuwa kuna nini kimetokea. Wale maasakri wakasema wakasita kusema
lolote, na wale vijana, wakachukua nafasi hiyo kupita kwa haraka, na hata wale
walinzi walipotaka kuwazuia wakawa wameshachelewa, wale vijana walisema wao
wanafuata amri ya mkuu , jemedari wao.
Walipofika ndani, walimkuta yule msaidizi akijaribu kumuinua
yule anayetambulikana kama bibi tabibu, na kabla hajafanikiwa kumuinua ndio
akasikia hawo watu wakiingia, akasimama haraka akiwa keshatoa silaha yake,
tayari kwa mapambano;
‘Bosi tumetumwa na mkuu, ngoja tukusaidie, maana bibi Tabibu
tangu jana hali yake sio nzuri, tulimshauri apumzike, lakini akaona aje
aangalie mara moja,… tunamuomba tumchukue akapatiwe matibabu huko
nyumbani,…’akasema mmoja wa wale maaskari waliokuja, ambaye haraka alimfikia
yule bibi Tabibu, na kumuinua,……
‘Sawa, lakini ni nani aliyewaruhusu kuingia humu ndani?’
akauliza yule msaidizi wa mkuu.
‘Ni mkuu,….kapatwa na dharura kidogo, lakini atafika hapa
muda sio mfupi, na hivi , cha muhimu ni afya ya huyu mzee wetu..au unasemaje
mkuu’akasema yule askari wakati keshamweka huyo bibi tibabu begani kutoka naye
nje.
‘Mkuu, kapatwa na dharura gani….?’ Akauliza, lakini wale
vijana ambao ni wepesi, wakawa wameshatoka nje, na mmoja akasema;
‘Atakuambia mwenyewe akija….’wakawa wameshaondoka. Huyu
msaidizi, akawa anajaribu kuwakumbuka hawa vijana, wanatokea kikosi gani,
lakini hakuweza kuzikumbuka zile sura, kwani yeye anawajua karibu askari wote
kwenye kikosi chake, akauangalai ule mwili, na alipohakikisha hakuna tatizo,
akatoka mle ndani, akiwa na hasira kwanini hawo walinzi wamewaruhusu hawo
vijana kuingia, na vijana wenyewe hajawatambua vyema ni akina nani.
********
Kwa haraka wakatoka eneo hilo na kuingia msituni, halafu
huko wakakutana na wazee, ambao, walimchukua yule anayetambulikana kama bibi
Tabibu na kumuhudumia na alipopata fahamu, wakamvalisha nguo maalumu za harusi
na kubadilishwa nywele, akavalishwa na kufanana na watu wa humo msituni,usingeliwezsa kujua kuwa ni mimi yule niliyetoka uraiani.
Baada ya kukamilika, nikarudishwa sehemu takatifu na mambo ya harusi yakaanza kufanyika kwa haraharaka, sikuwa najua nini kinaendelea kwa muda huo, woga ulishaniondoka, na kujihisi nipo dunia nyingine. Mara akanijia mzee, mmoja mwenye mvi nyingi, kichwani akasema;.
‘Binti hapa tunakwenda na muda, hili ni kwa manufaa yako na
manufaa ya eneo letu, tunatarajia kuwa wewe ndiye malikia mtarajiwa wa eneo
hili, ….’akasema mzee, na kunielezea kwa kirafu ni kwanini hayo yametokea, na ni nini wanachoamini.
Nilijitahidi kujitetea, lakini busara za huyo mzee, zilinizidi, , hata hivyo sikuwa na la kufanya, vinginevyoo ningelikuwa chakula cha mamba, au kuingia mikononi mw ahawo waasi, nikakubali shingo upande
Yule binti, ambaye ndiye mimi, nikakubali, sikuwa na jinsi,
ikabidi niolewe na tendo la ndoa litimilizwe ili mambo yaende sawa. Kazi ikawa
jinsi gani ya kuwashawishi wenzetu, kuwa mimi ndiye binti mtarajiwa yule
waliyekuwa wakimsubiri, hilo halikuhitajia haraka, kwani kama ingelichukuliwa
haraka, wenzetu wangelifanya fujo, hata kaunzisha vita.
Na hata hivyo kwa jinsi wanavyomjua yule mzee, vita haitaepukika kwani baada ya muda walisikia baragumu la hatari....Baragumu lililoashiria kuwa vita inakuja, wote wakasimama juu, na malikia mtarajia akabakia ameduwaa pale mume wake alipotoka nje na kurudi akiwa kashika upinde na mshale,, ....
'Mke wangu nahisi kuna vita, na nakuahidi nitakulinda hadi tone la mwisho kwani wewe ndiye ubavu wangu, na wewe ndiye malkia mtarajiwa, ...kila mtu anakuhitaji wewe,...'akasema na kuja kumbusu shavuni.
*******
Huku kwa maadui alipoona wale wameondoka, na mwili upo ,
akatoka na kuwauliza wenzake kwanini wamaruhusu watu kuinga humo ndani. Wao
wakasema, hawo watu wamedai wametumwa na mkuu wao,.
‘Kamaunavyowaona wana sare za kikosi chetu, na hawakusubiri,
walipitiliza, tulitaka kuwazuia lakini hatuhisi kuwa wanaweza kuleta tatizo,
kwanini kuna tatizo mkuu?’ akauliza askari.
‘Wewe huoni kuwa hilo ni tatizo, hili lisirudiwe tena, huku
haparuhusiwi kuingia mtu yoyote, hata mimi sikuruhusiwa, nimeingia tu kwa hii
dharura, na hili lisijulikane kuwa limefanyika, vinginevyo, mnajua adhabu yake,
mtakuwa chakula cha mamba.’akasema kwa hasira.
‘Ndio mkuu tumesikia,…’wakasema wale maaskari.
Yule msaidizi wa mkuu wao, jemdari wa kikosi cha mzee, adui
wa mzee wa mume wangu, akawa na wasiwasi kuhusu mkuu wake, kwani alisema
hatachelewa, na muda mrefu umepita, mzee anaweza akafika muda wowote, na
akimkuta hayupo, wataulizwa na hawatakuwa na jibu la maana, akaona inabidi
afuatilie , huenda mwenzake yup hatarini.
‘Huyu mtu kapatwa na
matatizo gani’ akasema na kumuita kijana wake mmoja na kumuelekeza afuatilie
huko nyumbani kwa bosi wake kuhakikisha usalama wake. Na kweli huyo kijana
akamfuatilia huyo bosi hadi nyumbani kwake, alipofika huko wakashangaa, kwani
huyo mtu wanayemuulizia aliondoka hapo muda mrefu.
‘Msiwe na shaka nitafuatilia nijue wapi alipo’akasema yule
askari na kuanza kufuatilia nyayo, wao wanajua njia zao, akazifuatilia hadi
alipofika msituni, na kumkukuta bosi wake akiwa kalala kwenye majani, huku
kamba ya mtego ikiwa pembeni mwake.
‘Bosi vipi leo kwa mara ya kwanza umeingia mtegoni, maana
wewe hunaswi namitego kama hii, ulichanganyikiwa kidogo nini, na unaonekana
haupo sawa, kuna tatizo bosi?’ akaulizwa.
‘Oh,kwani kumetokea nini, maana inaonekana nimepatwa na
usingizi wa ajabu na hii sio kawaida yangu, lazima kuna kitu kimefanyika,
..’akasema na kuinuka huku akipepesuka, na yule kijana mlinzi akashangaa kwani
hajawahi kumuona bosi wake katika hiyo hali.
‘Mkuu naona unaumwa, ..’akasema yule mlinzi, lakini mkuu
wake hakujali haraka akakimbia kwa shida hadi kwenye eneo ambalo alikuwa
habanduki, kuhakikisha hicho alichokuwa akikilinda kipo sawa, na alipoona ule
mwili upo kama ulivyokuwa awali, akatulia na kutafuta sehemu kujiegemeza, na
usingizi ukamshika tena.
‘Nafikiri mkuu anaumwa’yule mlinzi akamwambia msaidizi wa
mlinzi.
‘Inaonekana …lakini mwache apumzike, kama anaumwa nitamuita
bibi Tibabu atampa dawa, subiri kidogo, atulie’akasema huyo msaidizi wa mkuu.
Na mara Mzee kafika, akionekena kuwa na wasiwasi, aliulizia
jemedari yupo wapi, masaidizi wake akamwambia mzee, yeye anahisi Mkuu anaumwa,
lakini hatakii kupumzika.
Yule mzee, akaelekea ndani, na kwa muda huo
jemedari,alishaamuka lakini bado alikuwa akipepesuka, na alipomuona mzee,
akajikakamua , kuonyesha kwua hakuna lolote.
‘Wewe naona unaumwa, na nimesikai mke kajifungua, nenda
kajitibie, kama utahidi msaada wowote niambie, hapa leo kuna wageni na shughuli
muhimu sana, ….’akasema na kwenda kuchungulia ndani baadaye akarudi pale alipomuacha huyo
jemedari akasema.
‘Hutaamini, huyu huenda akawa ndiye yule malikia matarajiwa,
nimeletewa hizi taarifa nyumbani, kwahiyo sasa hivi anakuja mjukuu wangu,
tutamfungisha ndoa haraka, na mengine yatafuta baadaye, wewe nenda
kajisikilizie hali yako na kumwangalia mkeo, nitakuhitaji baadaye kama utakuwa
umepona….hii ni bahati kubwa sana’akasema mzee.
‘Hongera mzee,maana kijana akimuoa huyo binti, utawala wote
utakuwa mikononi mwetu, na hawa maadui zetu, watatafuta sehemu ay
kukimbilia’akasema jemedari.
‘Na nitahakikisha wanaondoka eneo hili, na tutabakia ukoo
wetu tu, na wale ambao wapo karibu na sisi, …ngoja hili la harusi
likamilike’akasema huyo mzee.
‘Umuejuaje kuwa huyo ndiye malikia mtarajiwa?’ akaulizwa, na
yule mzee akiwa na furaha akaanza kuelezea;
‘Nikiwa nyumbani, yule punde wangu akawa anaanza kujifungua,
na ujuavyo, ukianza kuyanywa yale maziwa ya mwanzo, baraka inakujia, na ndivyo
ilivyokuwa, kwani wakati nameza fundo la kwanza, mlango ukagongwa…
Walikuja wazee wawili toka ukoo wetu, wakiltea taarifa kuwa
imegundulikana kuwa hapo kwenye eneo letu takatifu malkia aliyetabiriwa keshafika,
na kama ilivyotabiriwa, kafika kwa aina ya kipekee kabisa.
‘Mbona hatujamuona?’ nikawauliza wale watu
‘Hakuna binti aliyefika eneo hilo kwa namna ya kiajabu?’
akauliza mzee mmoja.
‘Hakuna maana mimi muda wote nilikuwepo humo, sasa huyo
binti angekujaje nisimuone?’ nikasema.
‘Hebu tuambia wanawake waliofika hapo karibuni?’
wakaniuliza.
Sikumbuki mwanamke aliyefika zaidi ya bibi
Tabibu…’nikawaambia.
‘Huyo bibi Tabibu anakuja kufanya nini?’ wakauliza.
‘Kuna mwili uliofikishwa hapo, ambao tunajua kuna makosa
yamefanyika, na tunataka kumshitaki mwenzetu, na tuna uhakika kuwa wamefanya
kosa, na ikigundulikana ni kosa, huyo mzee na kundi lake itabidi wafukuzwe
hapo, na huyo aliyeuleta huo mwili, anaweza kuwa chakula cha mamba, na hilo
nimeshalifanyia kazi’akasema.
‘Huo mwili ni wa msichana, na hujuilizi tangu aletwe hapo,
kuna dalili yoyote ya kuharibika, maana mwili hata ukiuweka dawa, unakuwa na
hali fulani tifauti, je uliwahi kuuchunguza vyema, ?’ akaulizwa.
‘Hapana, sijafanya hivyo, sikupenda kuondoa ushahidi nia na
lengo letu ni kumnasa huyu jamaa yetu,…’nikawaambia.
‘Huyo ndiye malikia aliyetabiriwa?’ akasema mzee mmoja.
‘Eti nini…?’ nikawauliza huku nikiwa siamni maneno yao.
‘Hilo ndilo lililotuleta hapa na sasa muda unakaribia
kuisha, kwani huyo malkia natakiwa aozeshwe kabla ya saa kumi na mbili na tendo
la ndoa lifanyike…na huyo atakayemuoa ili awe kahalalishwa kuwa mfalme, ,mume
wa amlikia mtarajiwa…’akaambiwa.
‘Ooooh, kumbe,ndio maana, ..kweli, ..’nikasema na wao
wakanipia maagizo na jinsi gani ya kufanya, wakanipa dawa za kumpulizia huyo
binti, ili apate kuzindukana na akizindukana watafaunga ndoa na mjukuu
wetu,…’akasema kwa furaha.
‘Kwahiyo ina maana sasa hivi wanafungishwa ndoa?’ akauliza
jemedari
‘Ndio hivyo, mimi nimeshatoa kibali, na hilo zoezi linaendelea,
na ……sasa hivi mjukuu wangu atakuwa mfalume mtarajiwa….wewe nenda kapate
matibabu, upate nguvu,…..’akasema huku akiondoka kuingia ndani.
Yule jemedari alitaka kujitetea kuwa haumwi, lakini akaoana
haina haja, kwa vile amepata nafasi ya kwenda kuwa karibu na mkewe, na kichanga
chao, akaondoka haraka kuelekea nyumbani kwao, na wakati anapita eneo la maadui
zao, akaona sherehe za harusu zikiendelea, …
‘Hawa na wao wana harusi,ni nani anaoa na kuolewa,mbona
sijasikia …?’ akawa anajiuliza mwenyewe, na alipomkaribia mmoja wa watu waliokuwa
wakitoka huko akamuuliza, lakini yule mtu alisita kumwambia chochote kwani
anamjua kuwa yeye ni nani, lakini kwa vile ilionyesha dhahiri kuwa ni harusi
mmoja asiye na subira akasema;
‘Tumesikia kuwa ni mjuukuu wa Mzee anaoa,….’akaambiwa
‘Mjukuu wa mzee,…?!’ akauliza kwa mshangao, halafu akasema;
‘Anamuoa nani…mbona mimii sijui?’ akajuliza mwenyewe
kichwani, huku akikumbuka kuwa hata kwao kuna harusi ya kisiri amayo wanajua
kuwa wenzao hawajui. Akawa akiwaza je huenda harusi hiyo nayo inamuhusu huyo
malikia mtarajiwa, na huyo malikia mtarakiwa wapo wangapi.
Alipoona anajiwa na maswalimengi bila majibu, akaona
ajiondokee, kwani hamasa yake ilikuwa ni kufika nyumbani, kumuona mke wake na
mtoto wao. Hata hivyo, kimoyomoyo akaahisi kulifuatilia hili jambo, ili ajue ni
nini kinachoendelea, au atamtuma mmoja wa vijana wake afanye uchunguzi, maana
yeye kama jemedari ni lazima mambo yote ya hapo hasa kwa maadui zake ayajue.
Alipofika kwake, akakuta vijana wawili maaskari wa msituni,
wameshafika nyumbani, wakimsubiri akashangaa , na kuwauliza ni nini
kilichowaleta, mmoja wao akasema;
‘Mkuu, malikia mtarajiwa keshapatikana, lakini
inavyoonekeana wenzenu wametuzidi ujanja, keshaolewa na mjuu wa mzee wa kwao…
‘Eti nini?’ akashangaa.
‘Kwahiyo mzee, katutuma, kuwa tufike haraka,kwani anataka
kuanzisha vita…kuhakikisha tunamteka huyo binti kabla haijafika saa kumi na
mbili, hajaolewa, kabla….’
‘Hiyo ni ndoto…tayari keshaolewa, vinginevyo, labda kama
tutnataka kuafanya maasi’akasema jemedari, huku akiingia ndani kusalimiana na
mke wake na kichanga chake, lakini kabla hajatulia akasikia mlio wa baragumu,
mlio ulioashiria hatari, akamgeukai mkewe na kichanga, na kusema.
‘Mke wangu, naona hali sio shwari tena, vyovyote iwavyo,
nitawalinda kwa nguvu zangu zote, kwani nyie ndio familia yangu, nyie ndio changu,
tuombe mungu iwe salama,na kama ni vita kuna kufa na kupona, yote yakitokea
uyakubalia kwa moyo wako…’akambusu kwenye paji la uso, na kumwangalai mtoto
wake, akakimbilia nje…
NB: Haya ndiyo maisha yetu yalivyo, kila mtu kajawa na
ubinafsi, …hatako mwenzake apate, hata kama anajua kuwa huyo anatakiwa kupata
kama yeye na ni haki yake, moyoni mwake hariziki, angalau mwenzake apate ili
awe sawa na yeye, na atatafuta kila njia ya kuhalalisha ubinafsi wake, je kwa mtaji huo tutafika. Tukutane sehemu
ijayo.
WAZO LA LEO: Haki
inapobezwa, na ubinafsi ukatawala dunia, chuki , husuda ndiyo itakuwa tabia yetu,
na amani itakuwa msamiati wa kufikirika. Lakini tukumbuke, sote ni wanadamu tumezaliwa,
na muda wa kuishi ni mchache tu, ni nini tunachokitafuta. Tukumbuke kuwa tupo
safarini, na yote tutakayoyafanya hapo ndio akiba yetu ya huko kwenye maisha ya
kudumu.
Ni mimi:
emu-three
2 comments :
Mmmmhhh Utamu kolea ndugu wa mimi...Pamoja Daima!!!!!!
wenyewe mpoo? nilipita kutimiza wajibu wangu kama jirani mwema.
Post a Comment