Maua alijaribu kuficha uchungu, uchungu wa uzazi, aliona ni
heri kama inawezekana ajifungulie humo humo ndani,alijitahidi sana, lakini
ikafikia muda hakuweza tena kuficha yale maumivu, maumivu makali yalimjia
,akakunja uso, na kushika tumbo, ….na wakati huo mwenzake alikuwa akitizama
nje, hakuwa amemtizama Maua, ikawa ndio heri kwake, na mwenzake akawa anasema;
‘Hicho ndio kisa changu cha kuwa mwenyeji , na kuolewa na
hawa watu wa msituni, na nimeishi nao hadi sasa najua mila na desturi zao, na
tunasubiri muda ufike niingie sehemu hiyo inayotambulikana kama sehemu
takatifu, ingawaje wenzetu bado wameweka pingamizi kuwa hatanitambua hadi
miujiza yote ikamilike, kwani walitaka niolewe na mjukuu wao….’akasema.
‘Lakini muda utasema, siku ikifika hakuna pingamizi tena, hata
wao wanajua hilo. ..’akasema huyu binti huku akizidi kuangalai nje.
Yale maumivu yakapita, na Maua akaweza kutoa sauti huku
kijasho kikimtoka, akasema;
‘I-ina maana wao hawajakukubali kuwa wewe ndiye malikia
mtarajiwa ?’ akauliza
‘Kukubali moja kwa moja hawajakubali, kwani wanaona
wakikubali wataumbuka, ila heshima zote ambazo nastahili nazipata,kwa mfano
pale inapotokea tafrija ambayo wakina mama wanahitajika, wanahakikisha
nimefika,na kupewa kiti maalumu…kama malikia mtarajiwa’akasema.
Maua akatulia, kwani alihisi maumivi mengine yakija kwa
kasi, akainama ili mwenzake asione, na mwenzake alikuwa akiangalia nje, alikuwa
na wasiwasi wa mume wake, kwani ilitakiwa kwa muda huo awe amesharudi. Moyoni
akahisi kuna tatizo, akageuka kumwangalia Maua, ambaye alishajikausha kwani yale
maumivi yameshapita.
‘Hawa watu pamoja na kupigana kote, lakini inapofika sehemu
ya imani yao, wanaogopa sana, wote wanahisi kuwa mimi ndiye malikia mtarajiwa,
na wakinifanyia lolote baya , maafa yatawaandama, na kinachofanyika kwa sasa ni
kunishawishi mimi niolewe na mjukuu wao, au waniteke kimawazo na kuwaona wao ni
watu wema, …
'Wanajua kabisa kwa kuolewa na mjukuu wao ni kitu ambacho ni kigumu sana, kwani
mume wangu ameshawashinda, na ukishinda basi wewe ndiye unastahili kuwa mfalme
mtarajiwa’akasema.
‘Sasa kikwazo ni nini?’ akauliza.
‘Kwanza muda haujafika kwa mimi kutawazwa, lakini pia mume
wangu anahitajika kuonyesha kuwa kweli anastahili kuwa mfalme, na pamoja kuwa
aliwahi kuua simba, lakini anahitajika kufanya mambo mengine makubwa, ….wana
imani kuwa mfalme wa nchi ni lazima awe mtu jasiri, mtu ambaye uwezo wake sio
wa kawaida’akasema.
‘Kwahiyo hata hilo bado linasubiriwa…yaani mpaka atende
mambo ya ajabu, kama asipotenda na wewe umeshaolewa naye itakuwaje?’ akauliza,
huku akijinyisha kidogo, kwani maumivu yalishapoa, na alihisi huenda hali
ikatulia,…..hakujua nini kitafuata baadaye.
‘ Yule mtabiri, alisema malikia mtarajiwa ataolewa na mume
jasiri, mume ambaye atakuwa naye anatenda mambo yasiyotendeka, ya ujasiri,
kusaidia watu, …’akasema na kumwangalia Maua.
‘Kwani hayo ya kusaidia watu, …na na….’akasema Maua huku
akijikunja, maumivu yalikuwa yanakuja kwa kasi.
‘Ndio hilo nalo ni moja ya miujiza iliyotabiriwa kuwa kama
kweli mume wangi ni mfalme mtarajiwa, atakuja kufanya jambo la ajabu , mimi mwenyewe nimeshuhudia mengi aliyoyafanya
, na nimefikia hatua ya kuamini hivyo , kwani mume wangu ni mtu ambaye amekuwa
kila siku akionyesha uhodari, akisaidia watu, akifanya mambo ambayo wengine
wanashindwa kuyafanya.
‘Aaah, Maua akajikunja na hakuweza tena kuhimili,
akalalachini, ….’ Mwenzake akainuka, akashika
kichwa, akawa anashindwa afanye
nini, kwani muda kama huo mume wake alitakwia awepo, na walijadiliana na mume
wake kuwa atakuja na kutafuta njia za kumuokoa huyo binti, lakini hajafika, …
‘Ooh, sasa nitafanya nini mpendwa…nakuonea huruma maana huyo
mama akija, sitakuwa na la kufanya, na haitakiwi ujifungulie humu, na
ukijifungulia hapa mimi na mume wangu tutakuwa chakula cha mamba…’akasema huku
akiangalia huku na kule, na alipomwangalia Maua ambaye alikuwa chini katulia,
hatingishiki
Akamsogelea na kumgusa, akamkuta yupo kimiya,….na mara Maua
akainua kichwa na kupiga ukelele, ukelele uliosikia nje, ukelele ulioharibu
kila kitu,maana hakukuwa an siri, mama mkunga ambaye alikuwa nje na kikosi
chake watakuwa wameshasikia, na muda wowote wataingia…lakini kukawa kimiya,na
mara vurugu zikasikika mlangoni kuonyesha kuna watu wengi wanakuja kwa kasi…na
hapo Maua hakuweza kuhisi jingine zaidi ya maumivu.
***********
Mzee wa upande wa Maudui alikuwa akongea na wazee wenzake,
na moja ya ajenda yao kubwa ni jinsi gani ya kuweza kumwangamiza kijana ambaye
kila siku inaonekana ndiye atakayeshika kiti cha ufalme,na kwa vile keshamuoa
binti, malikia mtarajiwa, na wameshaishi naye kipindi kirefu, hakukuwa na
jinginela kufanya.
‘Mimi naona tukubali ukweli, kwani yote tuliyowahi kujaribu
kuyafanya yameshindikana, na hili ni kuonyesha kuwa kweli huyo kijana ndiye
chaguao la wazee wetu, ….’akasema mzee mmoja.
‘Kwanini ukubali kirahisi hivyo,hatujaambiwa kuwa huyo
kijana ndiye chaguo la wazee, tumeambiwa juhudu za kijana yoyote ndizo
zinamfanay awe mfalme, kumuoa huyo malikia sio tatizo, kwani anaweza akamuacha,
anaweza akafariki….yoye hayo yanawezekana’akasema mzee kwa hasira.
‘Kwahiyo una maana tufanye jambo….hapana,hilo litaleta
mkosi, ….’akasema mzee mwingine.
‘Mambo yatajileta yenyewe, ukumbuke kuwa hawa watu
wamemchukua mtu ambaye hatakiwi kweney jamiii yetu, na akajifyungulia kwenye
ardhi yetu, ni kashifa kwao, na niwajuavyo,wanaweza wakapuuzia hilo, na sisi
tunahitajika tuwe makini, …hapo wakiteleza tu, tumewanasa, kijana yule
tunamtupia Mamba na abu yake ambaye kamshupalia anafuatia na sisi tunamchukua
malikia wetu…’akasema.
‘Unafikiri wanaweza kuafanay kosa hilo, akati kabisa wanajua
kuwa huyo mwanamke hatakiwi kujifungulia kweney ardhi yetu,…?’ akauliza
mmojawapo.
‘Kama wangelikuwa wana nia hiyo, huyo mwanamke
asingelikuwepo huko nyumbani kwa kijana hadi muda huu, alitakiwa awekwe karibu
na mto wa mamba, ile tone la damu lisimwagike kwenye ardhi yetu, lakini hadi
sasa hivi nasikia bado yupo huko’akasema.
‘Na yule kijana wao yupo wapi, mbona haonekani?’ akauliza
mmojawapo.
‘Labda yupo kambini, nasikia anasimamia kikosi chao, ..’akasema
mmojawapo.
‘Mtafuteni, mjue wapi alipo, huyu kijana ana mambo ya ajabu
anaweza akafanay mambo mengine ambayo yatamfanya aonekane mtu mashuhuri,
fuatilieni, na ikibidi mumunyamaizishe hadi hilo tukio litokee, apoteze fahamu
kwa muda…’akaamurisha mzee.
‘Sawa mzee, hilo litafanyika…’wakasema vijana makomandoo
wakiondoka kufautilia nyendo za huyo kijana.
Mzee aliinamana akiwaza jinsi gani alivyoweza kughilibiwa na
yule binti, hadi kuingia mle ndani na kufungishwa ndoa na kijana wake,
hakuamini kuwa yule binti angelikwua mjanja hivyo, …
‘Huyu atakuwa alisaidiwa na hawa wenzangu,….’akasema
akikumbuka tukio lilivyokuwa
********
‘Tayarisheni sherehe kubwa, na waalikeni wakuu wote, hasa
majirani zetu, maana leo ni siku muhimu sana, ni siku ambayo kila mtu alikuwa
akiisubiria…’mzee akawa anatoa amri huku na kule, na kujaribu kufuatilia
kilajambo,ili kuhakikisha mambo yanakwenda vyema.
Aliingia kwenye ofisi yake na kuanza kuandaa baraza la
mawaziri, akiwaangalia watu wake mashuhuri,ambao wataweza kuwa karibu na kijana
wake,huku moyoni akisema;
‘Lazima mwanzoni nimuelekeze jinsi gani ya utawala, ni nanii
anastahili kuwa nani kweney utawala wake, ili asije akaharibu’akasema huku
akihakikisha watu wake muhimu wapo kwenye ordha yake, halafu akatoka nje.
‘Hawajamaliza tu,….hawa vijana bwana, ingelikuwa enzi zangu,
…aah, mambo ningeshayamaliza mapema, sisi tulikuwa imara,..., lakini bado muda upo…’akasema huku akitembea kwa
tambo, huku akiangalia upende ule wa maadui zake, na moyoni akisema;
‘Nyie sasa hapo hamtaonekena tena,hapo watakuja kukaa watu
wangu muhimu,…’akatikisa kichwa na kutabasamu, akageuka na kuelekea huko
walipokuwepo watu walioalikwa, na kila hatua aliona watu mashuhuri wakiingia,
wakiwa wamevalia mavazi rasmi ya sherehe , akawa anawakaribisha kwa furaha, na
kusema;
‘Mambo yameiva,mambo yamekuja kama yalivyotabiriwa…kijana
wetu ameshinda, yupo anamalizia kazi’akasema na kuingie eneo ambalo kijana wao
atafikia baada ya kumaliza kazi aliyokuwa akiifanya ili ile ahadi itimie….
**********
Kijana akiwa na furaha kuwa hatimaye keshampata malikia matarajiwa
akasogea pale alipowekwa huyo binti,kwani alishazinduliwa na alikuwa kaka kwenye
kiti maalumu, hajafanulia bado,kwani yeye ndiye aliyestahili kumfunua,
hakutakiwa mtu mwingine kumuona sura yake kwa wakati huo.
Hata yule aliyempulizi hiyo dawa, alitakwa afanye hiyo kazi
bila kumuona sura, akimuona sura yake atapata mkosi, kwani anayestahili kumuona
sura yake, baada ya kutangazwa kuwa ni mchumba wa mtu, yupo tayari kufungishwa
ndoa ni yule muoaji peke yake.
Yule mupuliziaji dawa alipofanya kazi yake, na kuhakikisha
kuwa huyo binti keshazindukana, akatoka na kumuachia kazi hiyo shangazi mtu na
watu wawili ambao walimvalisha nguo za harusi , na kuhakikisha kuwa hamtizami
machoni , huyo muolewaji,.
Kinachofanyika ni kufunikiwa kitambaa kikubwa, na huyo muolewaji
anaelekezwa afanye nini, na kukihitajika msaada, huyo binti anahakikisha kajifunika
uso wake, na wenzake humsaidia bila ya kumuangalia usoni, na baadaye alipokamilika
akapelekwa kwenye kiti maalumu, kikubwa kama kitanda, ili bwana harusi aje
afungishwe ndoa,…
‘Ndoa ikafungwa, ikawa ni zamu ya bwana harusi kumfunua
mkewe, na muda huo wazee muhimu wapo kwa pembeni na wanawake wakushangilia wapo
karibu, na hayo yalitakiwa yafanyike haraka kutokana na muda uliopangwa,…na
muda huo giza giza lilifanya wengi wasimuone vyema huyo binti, cha muhimu na
bwana harusi kumuona.
Alikuwa keshavalishwa ki malikia mtarajiwa, mavazi ya
kipekee yenye mapambo ya kila aina,..
Bwana harusi akasogea, na kumfunua mkewe akiwa na ndoto za
ajabu kichwani, …ndoto za kumuona binti mrembo wa aina ya pekee, na kwa wakati
huo wazo la kumkosa mtu aliyempenda sana lilishafutika kichwani, yeye alikuwa
kwenye ndoto ya kumuoa binti malikia mtarajiwa, binti ambaye sifa zake zilisha
elezewa na mtabiri,kuwa atakuwa mrembo, mwili wake laini, …macho yake malegevu…na
sifa nyingi zilizokuwa zikiongelewa kila siku!
Kwahiyo kijana alishampenda kinadharia huyo malikia
mtarajiwa, kama walivyo vijana wengine, ambao walikuwa wakiombea nafasi hiyo
waipate, ….lakini nafasi hiyo ilitakiwa ipatikane kwa mtu mashuhuri, kutoka
kwenye ukoo uliotambulikana, sio kila ukoo ungelipata nafasi hiyo, na ingawaje
kulikuwa na koo nyingine bora, na kila ukoo ulikuwa akivutia kwake, lakini nafasi
kubwa ilieelkezwa kwa ukoo wa huyu mzee.
Kijana akaishika ile nguo,na kuiinua, hatua kwa hatua,na
macho yake yalipofikia kumwangalia huyo binti usoni,bila kujua akataka kuiachia
ile nguo, lakini mkono ukashindwa kufanya hivyo, akabakia mdomo wazi,
akashindwa kuamini, ina maana huyo binti malikia mtarajiwa anafanana na mtu
aliyempenda, haiwezekani.
‘Haraka haraka jamani muda unakwenda…’sauti iaktoka nje na
hawa wanandoa ikabidi wafanya haraka, kama walivyoamrishwa hakukuwa na muda
tena wa kuchunguzana, akanyosha mkono juu kuashiria kuwa mambo
tayari,viegelegele vikatanda, na watu wakaondoka kuwaachia uwanja , ili kazi
nyingine ifanyike.
‘Hivi wewe sio Kais,..?’ akauliza pale walipobakia peke yao.
‘Mimi ndiye malikia mtarajiwa, ambaye maisha yako yote
yalikuwa yakimtarajia, naahidi kuwa nitakuwa mke mwema na malikia mwema,karibu
mpenzi wangu , maana muda unakwenda mbio, tunasubiriwa nje..’binti yule akatoa sauti,sauti
ambayo ilikuwa kiburudisho cha huyu kijana kabla, huwa akiisikia mwili wake
wote hujawa na raha, leo hii ….
‘Hata sauti kama yake….’akasema kimoyo moyo….na kuingia
kwenye zoezi jingine.
Walipotoka hapo baada ya kumaliza hilo zoezi muhimu, wakiwa
wameshikana mkono, wakaingia ukumbi wa sherehe, na wakati huo binti kajitanda
inavyotakiwa, lakini aliwekewa kitambaa mbele usoni, hakutaka kuonekana mpaka
amuone mzee, ..
Kiutaratibu ilitakiwa kijana amtambulishe huyo binti kwanza
kwa mzee , mkuu wa ukoo, halafu ndio huyo mzee atawatambulisha kwa waalikwa
wote, na ni kipindi hicho, wakati huyo kijana akielekea pale alipokaa mzee,
huku akiwa na wasiwasi, akishindwa kujua ni nini kimetokea hadi iwe vile, kwani
alikuwa hajajua kwanini huyo binti ndiye aletwe hapo badala ya huyo malikia
mtarajia, moyoni, alisema huenda ni mbinu nyingine imetayarushwa na huyo mzee
ili kuwazidi ujanja wenzake.
Akawa anamsogelea yule mzee, ambaye alikuwa kajawa na furana kicheko hadi jino la mwisho, na
wenzake wakijipendekeza kwake kwa furaha, huku mioyo yao ikiima, kwani kila
mmoja alitaka kijana waoawe ndiye huyo anayemuoa malikia mtarajiwa, …
Kabla kija hajamfikia huyo mzee, mara akaingia kijana mmoja
askari, na kumsogelea yule mzee, akamnong’oneza mzee sikioni. Yule mzee akainua
uso kwa mshangao, akatikisa kichwa mara nyingi, akawakodolea macho wanandoa
hawo, uso uliokuwa umejaa tabasamu na furaha ukageuka na kuwa uso mwingine
tofauti.
Mzee, akakunja uso,…sura ikabadilika, unyama ukatanda usoni,
na taratibu mkono ukashuka hadi sehemu anapochomeka kisu chake, …akaanza
kukuvuta taratibu, …..
******
NB, Hii ni sehemu nyingine ya kisa chetu….najua itakuwa na
makosa mengi, umeme umekuwa tatizo, lakini tuwepo pamoja, na ukiona makosa
yasahihishe hata kwa ukimiya- kimya.
WAZO LA LEO: Kila
lililopangwa na mungu kuwa litatokea, litatokea tu, sisi wanadamu hatuna mamlaka nalo, kwani kauli ya mwenyezimungi ni thabiti, akisema kuwa, hapo hapo huwa.
Ni mimi:
emu-three
No comments :
Post a Comment