Kila mfanyakazi tunayemchukua hakai hapa nyumbani, sasa
nimechoka kabisa kutafuta mfanyakazi wa nyumbani, naona ni heri njifanyie kazi
zangu mwenyewe, kwanza nililelewa kama mfanyakzia wa nyumbani…’akasema mke
wangu.
Kipindi hicho maisha yetu yapo juu, tuna kila kitu, …lakini
maisha ya ndani yalikuwa na mitihani yake, na ilionyesha wazi kuwa tulihitaji
msaidizi, ili na yeye apate muda wa kufuatilia miradi yetu.Niliinuakichwa na
kumtizama kwa macho ya huruma, …maanaalikuwa mtu wa pilikapilika, shughuli
zandani, shughuli zamiradi, shughuli za kijamii, zote alikuwa akijitahidi
kujumuika nazo.
Nilimwangalia na kutabasamu, na hapo nikakumbuka siku za
nyuma, wakati akiwa binti, wakati nampigania kumpata, ilikuwa kama kampeni za
siasa ambazo nilikuwa nikipambana nazo, na hata siku anaingia kwangu kama mke
wangu sikuamini.
‘Unanikumbusha mbali sana mke wangu, sijui kama ningekukosa
ingelikwuaje…’nikasema.
‘Siungeoa mke mwingine, wanawake
tupo wengi,….’akaniambia huku akipanga panga vitu pale ndani, na mimi
nikajikuta nikiwaza maisha yaliypita…
*******
Nilipomaliza chuo kikuu tu, nilianza maisha kwa kuajiriwa
serikalini, na nilikuwa mmoja wa mameneja, na kwa ujumla nilijitahidi sana
kwenye kazi yangu hiyo, kwani nilikuwa nakipaji cha kuwavuta wateja, kwahiyo
maswala ya biashara yakawa yapo juu kweney hilo shirika langu,lakini mshahara
wangu hakuwa mkubwa kiasi hicho.
Nikiwa nahangaika huku na kule kuweza kumudu maisha, maana
pamoja ya kuwa sijaoa lakini nilikuwa na majukumu ya kuwasomesha wadogo zangu,
nilikuwa na mjukumu ya nyumbani kwa wazazi wangu, achhilia mbali akina mjomba,
ambao walikuwa bega kwa bega, kunisaidia kufanikisha elimu yangu.
Siku moja nikakutana na rafiki yangu. Yeye aliajiriwa kwenye
mshirika ya watu binafsi, na mshahara wake ulikuwa mkubwa, kwahiyo hata maisha
yake yalikuwa mazuri ukilinganisha na mimi, na kila tulipokutana alikuwa
akinikoga kuwa mimi kazi yangu ni kuongea tu, na nimefanya makosa kukimbilia
serikalini….
‘Wewe nimegundua kuwa,unafaa uwe mtu wa majukwaa, ofis
haikufai, …’akaniambia siku moja.
‘Hilo ni moja ya malengo langu, lakini maswala ya majukwaa, maswala
ya kisiasa, yanahitaji uwe umejiimarisha kwanza,….ipo siku nitatimiza lengo
langu hilo la kuwa kiongozi…’nikasema.
‘Sawa,..tyaache hayo, maana wewe na ndoto zako za kuwa
kiongozi, siziwezi, hebu niambie utaoa
lini?’ akaniuliza.
‘Swaali kama hilo, ninaweza kukuuliza hata wewe…hivi wewe
utaoa lini?’nikamuuliza huku nikiwaza hilo swali, kwani nilishaulizwa na wazazi
wangu, lakini sikuwa na jibu la haraka kiasi hicho.
‘Mimi sizani kama itapita mwezi, utasikia sasa hivii
nikitagaza harusi yangu, mambo yameshajipa, …’akaniambia huku akishika kidevu
chake.
‘Ina maana unaye mchumba tayari?’ nikamuuliza nikiwa na wazo
jingine kichwani, namjau sana rafiki yangu huyu anao marafiki wengi wa kike,
lakini wote walihsniambai kuwa hawafi kuolewa, na marafiki wakupitisha muda.
‘Hilo sio swali, nitaoa bila ya kuwa na mchumba…yupo
msichana bomba, …mrembo,…!’akasema huku akionyesha tabasamu pana mdomoni, na
kutikisa kiwati hake cha bei mbaya sakafuni, alionyesha kabisa kuwa ana furaha
ya aina yake.
‘Mbona hujanitambulisha,…wewe ni rafiki yangu wa siku
nyingi, na tumekuwa tukiambizana kuhusu maswala yetu,…’nikamwambia.
‘Hilo ni swala binafsi,…kwanza wewe sikuamini….maana
tumetoka mbali,nakujau sana.’akasema na kucheka.
‘Sawa, hata mimi nipo mbioni , sizani kama nitamaliza mwezi….’nikasema
nikiwa sina uahkika na huo usemi wangu,kwani nilikuwa bado sijaamua kuoa, mambo
bad yalikuwa yakinichanganya.
‘Unamuoa nani…?’ akaniuliza kwa hamasa, na uso wake ukabadilika
na kuonyesha wasiwasi.
‘Hayo ni maswala binafsi hayakuhusu wewe..’nikamwambia huku
nikigonga na kidole kwenye meza.
‘Aaa-haaa, nimegundua ina maana wewe ndiye unayemfanya
mchumba wangu, asikubaliane na mimi , kila siku ananiambia bado atanipa jibu,….sikiliza,
wewe ni rafiki yangu, sioni kwanini, uwe
king’ang’anizi, wewe bado hujakamilika
kimaisha, wapo wanawake wengi, subiri ukikamilika kimaisha, utapata msichana mwingine…kwanini
tuingie kwenye ushidani usio na maana’akaniambai rafiki yangu huyo.
‘Sijakuelewa, una maana gani kusema hivyo, kwani huyo
unayetaka kumuoa ni nani,…?’ nikamuuliza huku nikiwa nimekunja uso kwa hasira.
‘Kwani wewe huyo unayetaka kumuoa ni nani, maana usije
ukaleta yale maisha ya kishulehapa, …sasahivi tupo uraiani, tunahitajika
kufanya kweli, mimi ninakushauri, kwanza jipange kimaisha,…, jenga nyumba,
halafu nunua gari ….’akasema huku akiangalia gari lake, lilikuwa mbeel yetu.
‘Halafu .., ndio uwaze maswala ya kuoa, mimi vyote hivyo
ninavyo, sina shida, hata wakisema mahara ni shilingi milioni ngapi, nitalipa tu,..fikiria bibi yake, nimeshamjengea
nyumba safi pale kijijini hakuna tena, sasa ….wewe tuliza kichwa,jenga nyumba
kwanza, maswala ya kuoa yapo tu…’akaniambia.
‘Ina maana imefikia hapo rafiki yangu….!’ Nikasema huku
siamini hayo ninayoysaikia toka kwa huyu rafiki yangu, maana kama ni huyo
binti,nilisha jitambulisha hadi kwao, hadi kwa huyo bibi yake, na
walishanitambua kamamchumba wa binti yao, sasa……
‘Rafiki yangu huko unapokwenda nikubaya,…sioni kwanini uwe
unajenga ushidani na mimi, kwanini na wewe usitafute msichana mwingine, ….mpaka
awe huyo, ilihali unajau kabisa mimi nay eye tunapendana….?’ Nikamuuliza .
‘Mnapendana…ni nani anayejua kwua mnapendana…’akasema huku
kicheka, na kuniangalai kwa dharau.
‘Mimi nilishakuambai hilo, na ndio maana nikaliweka wazi
kwako..’nikasema.
‘Lakini hukusema kuwa unataka kumuoa,…mnapendana, mbona
mimii nlishakuonyesha wasichana wengi, nikakuambia kuwa tunapendana, lakini
sikuwa na malengo ya kuwaoa,….sasa nimeamua kuoa, ndio nikamchagua huyo, kwanza
hebu muangalie, yule binti,….anakufaa wewe kweli..’akaniambai huku akinitizama
juu chini.
‘Siamini, kama na huyo, siamini….’nikasema.
‘Utaamini siku hiyo, ukiona tunakwenda Zanzibar kwenye asali
ya mwezi….fungate al nguvu….’akasema huku akishika kidevu.
‘Unajidanganya rafiki yangu, hapo tunazungumza kuhusu pesa
na maisha bado hujaangalia mapenzi, je huyo unayetaka kumuoa anakupenda,maana
umeshaanza kuweka walakini, kuwa huy o unayetaka kumuoa anakuwekewa kiwingu, hajakupa
jibu la uhakika,..au sio, ina maana hakupendi..’nikamwambia.
‘Ninajidanganya, unajidanganya,…mapenzi gani, bila pesa, hayo
mapenzi yapo kweli,labda….huko kijijini, lakini yule keshaishi haa mjini,
anajua nini maana ya pesa….nikuambie ukweli tafiki yangu,mapenzi ili
yakamilike, unahitajikana wewe mwenyewe uwe umekamilika, habu niambie, kwa
mfano mumeshaoana, ndani hakuna
kitu,kweli kutakuwa na raha, kweli kutakuwa na mpenzi hapo….acha ,mambo yako ya
jukwaani bwana…’akaniambia.
Mara simu yangu yangu ikaita, nikaipokea kwaharaka bila kuangalia
ni nani aliyepiga hiyo simu, na nilipoweka sikioni nikasikia ile sauti
inayonikosesha usingizi. Nikamgeukia rafiki yangu, ambaye alionyesha wazi kuwa
anajua ni nani huyo aliyepiga simu.
‘Nina mazungumzo na wewe ya haraka sana..’akaniambia.
‘Kuna nini kimetokea,?’nikauliza kwa wasiwasi, nikainuka pale
kwenye meza nakusogea pembeni, rafiki yangu aakwa akinifuatilia kwa macho.
‘Wazazi wangu wameshapokea posa, ….’akasema.
‘Posa ya nani?’ nikauliza kwa hasira.
‘Posa ya kwangu, …na….sikuhusishwa kabisa,…, sijui nifanye
nini…’sauti ya huzuni ikatanda masikioni mwangu.
`Unasema nini?’ nikauliza kwa hamaki, na simu ikakatika, na
hata nilipojaribu kupiga tena ikawa haipatikani, nilipogeuka kumwangalia rafiki
yangu, nikamkuta akiniangali kwa dharau, huku akiwa na tabasamu tele mdomoni.
Aliangalia saa yake, na kuinuka,…. akanisogelea na kunishika bega, akasema;
‘Rafiki yangu pesa …ni kila kitu, ukiwa na pesa, na maisha
mazuri, huwezi kushindwa maisha, utapata kila ukitakacho,nyumba nzuri, gari
zuri…mke mzuri, huna shida,….’akaniambia huku akiniminya miniya kwenye bega,
nilitamani niinuke nimtie ngumi,lakini nikatulia moyoni nikisema;
‘Sikubali….’ Yule rafiki yangu akawa anatembea pole pole
akielekea kwenye gari lake, na huku akigeuza kichwa kuniangalia kwa nyuma, mimi
nikasema;
‘Ina maana wewe rafiki yangu, umenigeuka tena…tulishakubaliana kuhusu
huyu msichana, ukasema huna haja naye tena,…?’ nikamuuliza. Yeye akacheka huku
akifungua mlango wagari lake, na baadaye akageuka na kuniangalia kwa dharau
akasema;
‘Mimi huyo-huyo….kuwa nilikubaliana na wewe,..hahaha hayo ni
maisha binafsi bwana..na kwanini nikubaliane na wewe, wakati yeye mwenyewe,
huyo binti, alishasema mwenye kisu
kikali ndiye atakaye kula nyama, ….au umesahau,.. sasa ujue kuwa kweli mimi
ndiye mwenye kisu kikali…’akasema huku akichezesha vidole kuonyesha kuwa yeye
ana pesa.
Nikaduwaa,mwili wote ukaisha nguvu, ….niliumia moyoni,
sijawahi kumia kiasi hicho, nikaingiwa na hasira, chuki, na …sijui kama
ningelikwua na slaha pale ningelifanay nini,….lakini moyoni nikasema;
‘Kama yeye ana pesa,
mimi nina mdomo, mimi ninacha zaidi yake yeye, ….nina penzi la kweli ,huyo
binti ananipenda mimi kiukweli..hilo nina uhakika nalo…sijakata tamaa..’
NB: Hayo ni maisha ya mwenzangu huyu, je wewe uliwahi
kukutana na mambo hayo, huo ni mwanzo tu, wamaisha ya huyu jamaa kipindi kileeee,je….,ilikuwaje.
5 comments :
Hivi tukiweka waandishi wa stories kama hizi, tunaweza kukulinganisha na nani? Nawaza tu,hongera sana M3, SIONI MFANO WAKO HAPA bONGO, UNA KIPAJI!
Kuna blogs nyingi sana zimeibuka hapa bongo, na wengi wanaishiwa na kuanza umbeya, ww nakusifu upo na msimamo wako, endelea hivyo hivyo, usijali, ipo siku watakuona,ipo siku hawa watoa matangazo watakuona.
-Adili
Pesa pesa pesa pesa inavunja urafiki, undugu n.k utu umeisha kwenye jamii kwa ajili ya PESA. PESA lini utaiacha dunia hii iwe ya upendo, amani, mshikamano n.k.
M3 unatishaaaaaaaaa kwa kweli ni zaidi ya kipaji ulichonacho.
M3 MBONA LEO KIMIYA?
Mmmmhh ndugu wa mimi kazi imeanza vyema, yaani Mungu yu pamoja sana tuu.Kipaji MUNGU Amekujalia.
Pamoja Daima.
Post a Comment