‘Achana naye yule,
kwanini ubabaika na watoto wa mitaani, wewe ni mtu muhimu sana…’aliniambia
rafiki yangu akiwa nyuma yangu,akinifuatilia….aliendelea kunihadithia rafiki
yangu,huku akionyesha kuwa ana haraka.
‘We niache kwanza, hayo hayakuhusu…’nikasema.
‘Hapo hupati kitu, …..nakuambia ukweli….’akasema kwa dharau.
‘Sawa, sio mbaya….’nikasema huku nikijitahidi kumkimbilia
huyo binti.
Inabidi nije nikuelezee
kuhusu huyu binti kwani ni mtu muhimu katika kisa cha maisha yangu….lakini kwa
leo tuushie hapa, nawahi mambo fuani,maana sijakata tamaa na kushindwa kwangu,….sikubali
kabisaa…’akaniambia rafiki yangu na tukaagana.
Sikuonana naye wiki mbili kwania alikwua akifuatilia kesi
yake, na mara nikasikia anaumwa, na hali yake ni mbaya sana. Mimi kama rafiki
yake nikafika hospitalini, sikumkuta, nikaambia kuwa keshatolewa, maana hayo
matatizo hayahitajii kulazwa sana, anahitajika akaugulie nyumbani.Basi ndio
nikamfuata huko nyumbani kwake.
‘Vipi rafiki yangu, imekuwaje, ….?’ Nikamdadisi.
‘Ni mitihani, siamini,…maana hili tatizo, limeanzia mbali,…nitakuja
kukuhaidithia kwenye kisa ,kile kisa nilichokuwa nakuahdithia, ….najau kabisa
limeanzia siku ile kule makaburini….’akasema huku akijaribu kukumbuka,
akachukau leso na kufata mate mdomoni, huku akiwa kaegemea mto,alikuwa akiongea
kwa shida, lakini ilionekana kuwa kuongea kwake huko kunamsaidia kupunguza
msongo wa mawazo.
******
Nilikuja kumtembelea kwake baada ya kusikia kuwa anaumwa, na
hali yake ilikuwa mbaya, …lakini isku nilipofika alikuwa hajamb kidogo, licha
ya kuongea kwa shida, kutokana na mdomo wake kuvutika upande kwa ajili ya
mshituko wa moyo.
‘Nashukuru sana umefika, maana siku ile nilipokutana nawe
pale mjini , tukaongea kidogo, sikuweza kukueelzea kisa change chote nilikatiza
kuwahi mambo fulani, najua wewe unapenda kuandika visa, kiandike hiki kisa changu,
ili waje wakisome watu, wajifunze kuwa maisha haya sio ya kukimbilia kwa pupa, …ni
kama mbio za sakafuni tu,mwisho wake ni ukutani tu….’akaniambia, na mimi
nikafurahi maana nilitarajia kuwa huenda angelinigomea.
‘Sasa sikiliza, mke wangu hayupo, naona tuanze huko
nilipokutana naye, ..maana yule binti niliyemjua sio huyu wa sasa, ni watu
wawili tofauti, wewe mwenyewe utaona, …kabadilika kabisa, na hapa nilipo
naogopa kabisa, kuwa huenda hata akaniwekea sumu..’akasema.
‘Kwanini iwe hivyo na huyo ni mkeo.?’ Nikamuuliza.
‘Kwasababu mmh, ….ukitaka
kujua kwasababu kwa sasa utakuwa umekivunja hiki kisa katikati,, ngoja
nikaunzie pale nilipokutana naye, ili uone binadamu tunavyobadilika, labda ni
kosalangu, nahis hivyo,lakini ndio maisha yalivyo…..
************
Yule binti akaanza kunisimulia msiha yake,;
‘Nilikuona kwa mara ya kwanza ukutoa hotuba zao nikavutika
sana na wewe, lakini sikuweza kuja mara kwa mara maana mimi naishi kama mtumwa,
…mama mdogo hanipi nafasi hiyo, nikitoka shule mimi ndiye mtumishi wa
nyumbani,….’ilikuwa sauti ya yule binti, baada ya kumkimbilia na kujaribu
kumshawishi
.Ingawaje mwanzoni hakukubali kabisa.
‘Wewe ulikuwa na dada mkuu, unatarajia nini kwangu,…unataka niishi shule kwa matatizo,…nyumbani nina matatizo kibao, na shuleni nako unataka niwe na
matatizo, we niache nenda kwa huyo dada, usije kunitia matatani bure..'akasema huku akiwa anakwenda kwa mwendo wa kusua sua, kama vile anajiuliza asimame au asisimame.
‘Yeye alikuwa akiniaga tu, lakini mimi nilikuwa na maongezi na
wewe hata yeye anajua hilo suiwe na shaka kuhusu yeye …’nikasema.
‘Maongezi gani na mimi,..wakati nyie ni watu wakubwa,
mnatakiwa muongee na wenzenu wakubwa…’akasema.
‘Mimi sio mtu mkubwa,mimi ini mwanafuzi tu, ….nakuomba
uteremke huko kwenye basi uje tuongee huku chini kidogo’ nikamwambia kwani wakati huo alishaingia ndani ya basi, lakini baadaye alikubali nakuteremka , tukasogea
pembeni na kuanza kuongea na hapo ndipo akanipa kisa chake cha kusikitisha na
mama yake wa kambo..
‘Mama yangu aliachika mapema, ….’akasema.
‘Kwanini aliachika..?’ nikamuuliza.
‘Mimi sijui maana aliachika nikiwa mdogo,nisiyejua nini
kinaendelea, na hata leo baba hajawahi kuniambia ni kwanini alimuacha mama
yangu na kumuoa huyu mke, asiye na huruma hata kidogo..’akasema.
‘Mama aliniacha nikiwa bado mdogo, ….mwanzoni kulitokea
ugomvi kati ya mama na baba, kila mmoja akinitaka mimi, na mwishowe ikafikia
muafaka kuwa niishi na bibi yangu, .... Kwani wakati huo baba alikuwa na mpngo
wa kumuoa mke mwingine..nahisi huenda matatizo na mama yanahusu huyo mke
mwingine, sina uhakika, kwani hata bibi hakuwahi kunisimulia.
Mimi na bibi tuliishi maisha ya shida, maana kijijini ni
shida tupu, umasikini ulituandama, lakini ndio maisha yetu, niliyazoea, nikawa
nasaidiana na bibi, ambaye watoto wake hawakumjali sana, …nyumba yake ilikuwa
ya majani, wakati watoto wake mjini wanaishi kwa raha, …nikijaliwa kupata kazi
nitahakikisha kuwa namjenga bibi yangu nyumba…’akasema huyo binti.
‘Kwanini sasa watoto wake hawamjengei mamayao nyumba ya
maana?’ nikamuuliza.
‘Watamjengea vipi waache kuwajengea wake zao, na kujenga
huko ukweni, ili waonekane wa maana, kwanii nyie wanaume mna maana, ….nasikia
baba kajenga huko kwa mke wake, nyumba ya maana tu, mama yake anaishii kwenye
nyumba ya nyasi, na hata pesa za matumzi hatumi, mpaka bibi alalamike wee,
sijui akichoka ataishije, natamani nirudi nikaishi naye, nimsaidie, …lakini
mimi hayo hayanihusu sana kwa sasa ipo siku nitamsaidia…’akasema.
‘Haya niambie kuhusu maisha yako, ilikuwaje baadaye….?’nikamuuliza,
nikiwa na hamu ya kumjua huyu binti vyema, maana akiongea utatamani umsikilize,
sikutaka sana kujua maisha ya kijijini maana kweli mengine yanasikitisha, hata
mimi kuna muda nilijisahau, lakini nashukuru niliwahii kuwajenga wazazi wangu
nyumba ya maana’akasema rafiki yangu huyu, huku akifuta mate kwa leso yake.
Yule binti akaendelea kunihadithia maisha yake, akasema;
‘Baada ya kumaliza
darasa la saba, baba akanichukua ili nisomee huku mjini. Kwa mara ya kwanza
nilfurahi maana nakwenda kusomea mjini. Kila mtu kwenye umri wetu huo alitamani
sana kuja kuishi huku mjini. Lakini nilipoika na kukaa wiki moja tu,
nilimkumbuka bibi yangu ambaye alikuwa akinipenda sana….nilitamani nirudi huko
kijijini, lakini sikuwa na jinsi, maana nilijua nina malengo ya misha yangu ya
baadaye.’akasema kwa huzuni.
‘Mama alinifanya mimi ndiye mfanyakazi wake wa nyumbani,
kila kazi ni mimi,nilitakiwa niamuke saa kumi na moja kasoro, ili nihakikishe
nimefanya usafi wa ndani, nimefua nguo za mtoto, maana yeye alikuwa na mtoto
mdogo, nifue na nguo zao, halafu nipike chai, nitenge mezani, wao wakiamuka
wanajiandaa wanakunywa chai, hao wanaondoka zao kazini….sasa na mimi hapo Napata
muda wa kujiandaa kwenda shule…’akasema.
‘Kwani hapo unapoishi sio mbali na shule, na mtoto anabakia
na nani?’ nikamuuliza.
‘Ni mbali, lakini hawanichukui kwenye gari lao, wanamchukua
mtoto wao hadi shule ya chekechea anayosoma. Mimi napewanauli ya daladala,
wanasemawakinichukua mimi watachelewa, kwasababu ya kuogopa foleni, …mimi hilo sijali’akasema
na kukunja uso kwa huzuni.
‘Nimezoea maisha ya shida, kama wasingenisimanga, sioni
taabu,huwa napannda daladala, hadi shuleni, nikifika shuleni nimechoka kutokana
na kazi za asubuhi, wakati mwingine najikuta nimelala darasani. Na ikifikia
jioni nakimbilia nyumbani nakutana na kazi zile zile, …kitanda kwangu ni
kuanzia saa sita za usiku, na hapo nipo hoi, sijui kama kuna home work ,….yaani
we acha tu..’akasema.
‘Sasa kwanini humwambii baba yako, akatafuta mfanyakazi wa
ndani….?’ nikamuuliza.
‘Baba …ooh, ukitaka ugomvi na baba uongee ubaya kuhusu mke
wake, yeye anasema mke wake ni mzungu, hana tabia mbaya,..basi tena, mimi
nimeshajionea kawaida, ndio maana nikikaa peke yangu namkumbuka mama yangu….nasoma
kwashida sana, huenda ipo siku nitajitoa kwenye haya maisha,,’akasema.
‘Kwani mama yako yeye yupo wapi?’ nikamuuliza.
‘Kaolewa na mume mwingine na wanaishi Mwanza, huwa sina
mawasiliano naye sana , na nikionekana nawasilina naye cha moto nitakiona…basi
huwa sitaki hata kumpigia, kwanzamume wake aliyemuoa naye ni wale wale….sitaki
hata kwenda kwao,naona ni heri nibakia hapa hapa hadi kitakapoeeweka….yote
maisha.’akasema.
‘Pole sana, sikutarajia mrembo kama wewe uwe na maisha ya
taabu kiasi hicho, Sasa nikuulize mwenzangu alikuambia nini kuhusu mimi?’
nikamuuliza.
‘Mwenzako yupo, ooh, yule mvulana, ..aaah, mimi sikuwa
namsikiliza sana, anasema yeye ana pesa sana, …nikiwa naye sitakuwa na maisha
ya shida, …hata sikuwa namtilia maanani, ila tu kwa vile alikuwa akinitoa
upweke ikabidi nimsikilize’akasema na kunyamaza kimiya.
‘Mimii sitaki nikuharibie maisha yako, au kukudanganya sana,
ila nakuahidi kuwa ukiwa rafiki yangu nitahakikisha kuwa hupati shida…’nikasema
huku moyoni nikijua kuwa namdanganya, mimi mwenyewe kula kulala, wapi
nitampatia hayo mahitaji yake , lakini niliona niweke karata kubwa zaidi ya
mwenzangu.
‘Nyie wanaume bwana, kwani hayo yote ya nini, mimi bado
nasoma na wala sitaki urafiki na mwanaume yoyote, nisije nikalikoroga, niliyo
nayo yanatosha,…hata sijui kwanini nimekusimulia maisha yangu, labda…’akasema
akitaka kuondoka.
‘Sikiliza, mimi nakuahidi kuwa hata kama ni ada nitajitahidi
nikulipie..’nikamdanganya.
‘Kwani wewe unafanya kazi…wewe si bado mwanafunzi,
usinidanganye kama mtoto, …?’ akasema huku akiniangalia kwa kujiiba, huku
anatafuna ukucha.
‘Mimi sifanyi kazi ndio, lakini wazazi wangu hawana
shida,….nikitaka pesa wananipa tu, hata hivyo, pesa za matumzi wanazonipa ni
nyingi sana, kwanza chukua hizi hapa ukapande taksi…’nikataoa pesa nilizopewa
kama zawadi wakati wa kutoa mada kwenye huo mkutano., nia na lngo langu ni
kujifaharisha, ili tu nisije nikashindwa na yule rafiki yangu.
‘Aah,…mimi sitaki pesa yako, usije ukanitia kwenye majaribu
bure…’akakataa kata kata, lakini nikamshinikiza kwenye mkono na kuondoka
haraka. Huo ulikuwa mwanzo wa urafiki wetu, sikujua kuwa ndio chanzo cha
uadui na rafiki yangu hadi hii leo,….uadui ulikuja kuingia hadi kwenye mamo ya
siasa.
NB. Nitakuwa naandika kidogkidogo, ili na mimi nipate muda wa
kukipitia kisa kilichopita na kikiweka sawa, muda ndio huo huo, na jembe la kazini,..msijali tutafika tu, kidogokidogo
WAZO LA LEO: Kila mtu ana mbinu zake za kutafuta
maisha,lakini tuwe makini na mbinu ambazo mwisho wake ni majuto,…tukumbuke kuwa majuto ni
mjukuu, huja baada ya kitendo.
Ni mimi:
emu-three
9 comments :
Wengi wa wanablog hupenda kuweka picha zao, na inakuwa rahisi kuwajua , lakini wewe mbona haupo wazi, tungelifurahi kukujua zaidi, kisura, jina ...ni wazo tu mkuu, maana wewe ni mkali.
Duuh, nimekubali!
Kisa hiki kimenigusa ila mbaya nimejikuta nikisoma hiuku nikilia. Maisha kwa kweli ni mafundisho sana na kweli polepole ndio mwendo na mvumilivu hula mbivu...Nakubalina na mwandishi kuwa utakuwa ukiandika kidogokididogo itakuwa safi ukifanya hivyo. Kazi nzuri ndugu wangu.
Visa vyako vinavuta hisia kama vile unaangalia movie, wewe ungelifaa uwe mtunzi wa movie,ingekufaa sana!
Kazi nzuri m3
well done m3 kisa kimeanza kusikitisha sana
tupo pamoja milele
Kazi njema m3!
Kazi njema m3!
Kazi njema m3!
Duuh jirani wewe ni nomaaa,endelea kutupa uhondo.
Post a Comment