Kila mtu kazaliwa na kipaji chake, mimi nilizaliwa na kipaji
cha kuongea, kipaji hiki kilianza kuonekana wakati nipo sekondari, kwani kwa
ajili ya kipaji hiki nilichaguliwa kuwa kiongozi wa shule, nilianza kama kaka
mkuu, na hata nilipofika chuoni nilijulikana kama waziri mkuu.
‘Huyu ndiye waziri mkuu mtarajiwa…’alikuwa mmoja wa walimu
wangu akipenda kuninadi katika moja ya shuguli zetu za kishule. Nami
nikawanavimba kichwa, …na nikawa nikijiweka kinamna ili nifanane na hicho cheo.
Siku moja wakati natoa moja ya mihadhara ya kisiasa, tukiwa
tumejumuika wanafunzi wengi, jicho langu lilitua pembeni mwa wasikizaji,ambao
walikuwa wakiongezeka kila siku. Macho yana maajabu yake, kwani jicho langu
lilipotua upende ule wa kushoto kwangu, moyo wote ulikuwa kama umeguswa na
umeme, nikajitahidi kujihimili, lakini nilihisi kuwa nimeguswa na jambo lisilo
la kawaida, nilihisi kama nimeona kitu ambacho ni muhimu sana katika maisha
yangu.
Baada ya ile shughuli tukawa tunagawiwa vinywaji na chakula,
na mimi nikawa naangaza huku na kule kama ninaweza kukiona kile klichoteka
akili na moyo wangu, na nilipohakikisha kuwa , hakuna hicho ninachokitafuta, nikamgeukia mmoja wa marafiki zangu,;
‘Hivi hapa wamealikuwa shule ngapi?’ nikauliza.
‘Shule nyingi tu, kama sikosei ni shule tano zilizokubali
mualiko kimaandishi, lakini baadaye walikuja wengine kwa rizaa zao, kusikiliza
hili kongamano, unajau siku hizi vijana tumeamuka, tunajaribu kuwa mbele,
na ile dhana ya taifa la kesho inaanza
kufifia……’akaniambia rafiki yangu huyo aijaribu kudonoa moja ya maneno yangu
niliyopenda kuyaongea.
‘Aaah, unajua kuna kitu ambacho kimenipata wakati nahutubu
pale juu, sijui ndio mitahani au ndio majaliwa ya mungu,….;nikasema huku
nikigeuka huku na kule.
‘Kitu gani kimekupata, usiseme umetupiwa majambo,maana dunia
hii haina heri..?’akaniuliza rafiki yangu akijaribu kufuatilia macho yangu,
huko ninapotizama.
‘Hapana sipo huko kabisa,.., hebu niambia shule gani za
wasichana walioalikwa hapa?’ nikamuuliza.
‘Shule mbili za wasichana,….na hizi zingine ni za wavulana,…na
kuna wengine wa shule z akaribu wamefika, wao wamevaa nguo za nyumbani,…kwani
kuna jambo gani, ?’ akaniuliza.
‘Kuna msichana mmoja nimemuona, na nahisi kama
namfahamu,alikuwa kaka pembeni, cha ajbu yeye alikuwa kama hanisikilizi, ila
mara kwa mara alikuwa akinitupia jicho, na kuniangalia kwa makini,sina uhakika
kuwa ni mwanafunzi au ni wasicha wa uraiani, maana nilimuoa akiwa kasimama
pembeni kabisa peke yake, halafu akakaa
na kushika shavu, na usimamaji wake, ulikuwa aina yake, kwani alionekana mwingi
wa huzuni…’nikasema.
‘Alisimamaje,?’ akaniuliza na kujaribu na yeye kuangalia
huku na kule, kama vile na yeye kavutika na hilo nililomuambia.
‘Alikuwa kasimama peke yake, huku kashika shavu, halafu alikuwa
ananiangalia bila kupepesa macho…’nikasema.
‘Unamfahamu kweli au ndio umeshazimia kwake, sema ,mimi
naweza kumtafiti na kumpata, yupoje kisura,….ukinielewesha vyema nitakwenda
kuzunguka kule walipo wasichana, na nitampata tu, kabla hawajaondoka,…’akasema
rafiki yangu ambaye nimjuavyo ni mwepesi wa kufautilai majambo.
‘Fanya hivyo…ukimuona nitonye, …alikuwa kasimama peke yake
mwishoni kabisa, ni mrembo kwakweli, na ni wale wasichana waliojaliwa urembo
usio mithilika…’akasema
‘Oooh,nahisi kama nilimuona, ..ngoja nikamwangalai kama ndio
huyo, nitamuona tu,..’akasema na kuondoka haraka, na mimi moyoni nikasema
nimefanya kosa kubwa,lakini sikuwa an jinsi maana mimi pale sikutakiwa
nionekane tofauti, kwani nilikuwa natayarishwa kama kiongozi mtarajiwa.
*****
Kiongozi unaitwa huku kwenye meza kubwa…’nikashikwa bega na mmoja
wa waandaji wa hilo kongomano. Nilishituka kidogo, maana sikuwepo kimawazo,
mawazo ambayo yalinipata siku ile yalikuwa mengine, mawazo ya kiutu uzima,
sikuwa na kawaida ya mawazo kamahayo kabla. Nilihis kuwa huenda ni wakati
umefika wa kuwa na rafiki wa kike.
Tulipokuwa meza kuu, nikapata mwanya wa kuongea tena, na
kutoa moja ya hutuba zangu ambazo wengi walizipenda, na kila hatua nilisikia mkofi
yakitanda hewani, na mimi nikisikia hivyo, akili inachanganya, mambo
yanajipanga kichwani utafikiri, nilikuwa nasoma kwenye karatasi, ,…
Wakati naongea nikatupa jicho upande ule wa kushoto kwangu,
na mara nikamuona rafiki yangu akiwa kasimama na msichana wakiongea kwa hamasa,
mwanzoni sikujali, nikawa natoa mambo yangu, lakini mara ya pili macho yangu
yalipotua pale aliposimama rafiki yangu, nikaweza kumuona yule msichana, ambaye
alikuwa akijaribu kuaniangalia, lakini rafiki yangu alikuwa kama anamzuia asiwe
makini na mimi, awe anamsikiliza yeye,nikajikuta ghafla nimeshikwa na
bumbuwazi,..kumbe alikuwa yule msichana.
Nilimalizia yale niliyotaka kuongea na kurudi pale nilipokuwa
nimekaa na hapo nikatupa macho yangu pale alipokuwa rafiki yangu, sikumuona
tena, na hapo moyo ukaanza kunipiga kwa wasiwasi, kuna kitu kikaniingia moyoni,
ilikuwa ni hisia ya ajabu. Nilijua huyo rafiki yangu alivyo, atakuwa keshaongea
na huyo msichana na huenda mengi yameshatendeka, ..ndivyo nilivyowaza kwa
wakati ule..wivu ukaniingia.
Ile shuguli ikawa imefikia tamati, na watu wengi wakawa
wanakuja kunipongeza, na hata hivyo sikuwa makini na pongezi zao, nikawa
namtafuta rafiki yangu kwa macho, hata hivyo sikuweza kumuona yeye wala yule
msichana, na wakati naagana na washiriki waliokuwa wakitaka kunipongeza,
nikageuka kuondoka, na mara nikajikuta nimesimama uso kwa uso na rafiki yangu,
akiwa anaonyesha kutahayari, akasema;
‘Bwana wee,nimemtafuta huyo binti lakini sikumuona…’akasema.
‘Usinitanie rafiki yangu, wewe mwenyewe umaniahidi kuwa
utampata, sasa hivi unabadili maneno…una uahkika na hayo unayoyasema kweli,….?’nikamwambia
kwa kumuuliza, huku nikijifanya sikumuona akiwa kasimama na yule msichana.
‘Ndivyo nilivyokuwa nimeahidi lakini unajau tena wapo
wasichana wengi, na sikuweza kumpata huyo msichana, labda siku
nyingine…’akasema huku akionyesha wasiwasi.
‘Sawa hamna shida nitamtafuta mwenyewe…maana unaweza ukampa
mshenga kazi, na mshena akageuka kuwa mtarajiwa….’nikasema huku nikiondoka na
kuelekea kule walipokuwa wamesimama wasichana, na rafiki yangu akawa
akinifuatilia kwa nyuma, baadaye yeye akasimama, na kuelekea upande mwingine.
‘Habari yao kaka,
kiongozi…’sauti nyororo yaikasikika masikioni mwangu, ilikuwa ile sauti adimu,
inayoweza ikaugusa hisia zilizoganda kwa baridi, ilikuwa ni sauti kike ambayo ingeliweza kumliwaza yoyote hususani mwanababa.
Na mimi nikageuka nikiwa nimeshajenga hisia kuwa huenda akawa yule binti, na
nilipogeuka nikiwa na tabasamu mdomoni, nikitarajia hivyo,lakini kumbe alikuwa
mmoja wa kiongozi wa shule hizo za
wasichana akitaka kuniaga.
‘Oh,kumbe ni wewe, nilikuwa na ….’nikasema huku nimeduwaa na
kukata tamaa.
‘Ulikuwa umearajia mtu mwingine nini, niambie ni nani,
nitakusaidia kumpata?’ akaniuliza huku akitabasamu.
‘Hapana, hakuna shida..’nikasema kwa kuona aibu.
‘Seme tu, najua ni nani, najua ni yule uliyekuwa ukimwangalia
wakati ukiotoa vitu vyako pale jukwaani,yule ni mmoja wa wasichana wanasoma
masomo ya kutwa, waliambiwa wafike kama wanataka, yeye yupo kidoto cha pili,……’akaniambia.
‘Ina maana uliniona nikimwangalia?’ nikamuuliza.
‘Hukuweza kujificha, na kwa vile na mimi nilikuwa
nikikuangalia mara kwa mara ,niliweza kukuona ukimwangalia yule msichana kwa
jicho la kujificha, na nikahisi umeguswa naye,… nilipoona hivyo, moyo wangu
uliingiwa na muwasho, fulani, maana ….’akakatisha.
‘Una maana gani kusema hivyo..?’ nikamuuliza.
‘Najua sisi wasichana kujielezea hisia zetu kwenu ni ngumu,
lakini kama ningelijaliwa hivyo, na kuwa na huo ujasiri nisingelisita kukuambia
ukweli wangu…’akaniambia yule mwanadada.
‘Wewe sema tu, mimi nimtu makini, na sijali kuwa wewe ni
msichana, nitakusikiliza, ....hiyo ni kawaida tu..’nikamwambia, lakini kiukweli
nilikuwa sipo makini na yeye , mawazo yangu yalikuwa mbali na kila mara
nilikuwa najaribu kuangalia huku na kule kama nitamuona yule aliyeugusa moyo
wangu.
‘Nimekuwa nikifuatilia sana makongamano ambayo na wewe
umeshiriki,kwani hata mimi ni mmoja wa wapenzi wa haya makongamano,na natarajia
kuwa mmoja wa wabunge watarajiwa, na kiujumla umekuwa ukinigusa, unvyoongea, na
mwenyewe ulivyo, nahisi kuwa karibu sana na wewe saana…’akaniambia na kabla
hajamaliza macho yangu yakatua upande wa pili nikamuona rafiki yangu akiwa
kasimama na msichana, nikajua ni yule yule msichana,…nikageuka kuwafuata.
Nilipofika pale waliposimama, nikatulia kwanza ili nisikie
ni nini wanachokiongea walikuwa hawajaniona, ndipo, nikamsikia rafiki yangu
akisema;
‘Unajua mimi nimekupenda sana, na nimeona uwe rafiki wangu
wa karibu, achana na yule muongeaji wa
jukwaani, hana kitu yule, …watu kama wale wanaopepeta mdomo hawajui kutafuta
pesa, sisi ambao hatuongei sana tunajua pesa zilipo, hatuhitaji kupiga domo…’nikamsikia
rafiki yangu akiongea na yule msichana. Hapo nikajifunza kitu, kumbe pesa nii
muhimu,….
‘Kwani ukipenda ni lazima umtafute mwenye pesa, mimi
nimevutiwa naye tu, ongea yake, na jinsi alivyo, sio kwamba nahitaji pesa zake,
…’akasema yule msichana.
‘Hilo sawa, lakini una uhakika kuwa kweli yupo makini na
wewe, maana mtu kama yule ana wengi, wengi wanamtizama yeye, wamatamani yeye, usije
ukaumia moyo wako bure,…..achana naye, wewe uwe na mimi, nina uhakika hutaumia
moyo wako….’na mara akageuka nyuma akaniona. Alishituka na kuanza kujibaragua,
akasema.
‘Oh, kumbe umekuja nilikuwa nabahatisha, kama ndio yeye, …lakini
nahisi sio huyu, ….’akasemam na mara nikasikia mtu akinishika bega, nilipogeuka
nikamuona yule msichana niliyekuwa nikiongea naye mwanzoni kafika, na yeye
akanikaribia na kuwa kama anapitisha mkono mgongoni mwangu, akasema;
‘Vipi mbona umenikimbia kabla hatujamalizana….’akasema na
yule msichana mwingine aliyekuwa akiongea na huyo rafiki yangu akaona lile
tendo la huyu msichana kupitisha mkono nyuma ya mgongo wangu, licha ya kuwa hakunishika
maana alishituka na kuuondoa haraka pale alipowaona rafiki yangu na yule msichana.
Na yule rafiki yangu aliliona hilo tendo, na hakutaka
kupoteza nafasi hiyo,akamgeukia yule msichana na kumwambia,….
‘Unaoan niliyokuambia….’Sikuamini kuwa rafiki yangu anaweza
kufanay hivyo, na ghafla yule msichana akageuka kwa haraka na akaondoka,
kuelekea kule walipokuwa wakisubiri gari lao, mimi nikashindwa kuvumilia
nikamkimbilia.
‘Hebu subiri nikuambie, sivyo kama unavyofikiria wewe…’nikasema.
‘Hapana wewe endelea na msichana wako….mimi sihitaji
marafiki wa kiume’akasema huku akiharakisha kuondoka na akaingia kwenye basi
lao,…..
NB: Hapo ndipo mwanzowa ushindani wa maisha ulipoanzia, pesa
, hadaa ikaanzia hapo.
WAZO LA LEO:
Rafiki utakayemuona ni wa kweli ni yule anayejitokeza wakati wa dhiki.
Ni mimi:
emu-three
4 comments :
story ya diary-yangu,nimeipenda sana wewe ni mtunzi bora..M,M
kisa kimeanza taratibu
well come m3 nakujuwa sana mtu wangu unatufanya wapenzi wa blog tusicheze mbali na hapa
hata hivo siku njema
Samira na wadau wengine nitajitahidi tuwe pamoja, nashindwa kupitisha siku bila kuandika chochote, maana kuandika ndiko kuwasilianana nyie, kwani...nawajali sana na nawapenda sana tuwe pamoja,
Nitajitahidi Insha-Allah!
Post a Comment