Nikiwa bado nipo kwenye kochi nikiwaza ,nilimuangalia mke
wangu, na kutabasamu, yeye aliponiona nikimwangalia nakutabsamu, akasimama na
kukunja uso kwa hasira, alijua labda namsanifu, akasema;
‘Ina maana unaniona mimi mjinga nikihangaika na mikazi ya
hapa nyumbani,…unanisanifu au sio..?’ akaniuliza huku akiniangalia kwa hasira.
Mimi nikamwangalia kwa makini bila kusema neno, alipoona
siongei , akasema;
‘Sasa kuanzia leo tunapangia zamu, mimi nikipika wewe upige
deki nyumba, au ufagie, sio kukaa hapo kwenye kochi na kukunja nNe, huku,
unanicheka, unafikirii mimi hapa nafaidi, unafikiri mimi hapa nacheza,…’akasema
kwa hasira na yeye akakaa kwenye kochi na kutupa vitambaa alivyokuwa kavishika
mkononi.
Niliinuka na kuvichukua vile vitambaa, nikaanza kuvitandika
kwenye kochi,huku kumbukumbu za nyuma zikiwa zimetanda tena kwenye ubongo
wangu, nikikmbuka jinsi nilivyoweza kufanikiwa kumchukua, huyu binti,katiak
dakika za mwisho, wakati kila kitu kilashakamilika na rafiki yangu ndiye
alikuwa anasubiriwa afike, wafunge ndoa. Hali hii nilitarajia itakuwa pia kwenye
mambo yangu ya kisiasa, lakini haikuwa hivyo, …..
********
Kila nikipiga simu ya yule binti ilikuwa haipatikani,
nikaona ni bora nifunge safari niende huko huko , kwani yeye alikwenda huko kijijini
kumsaida bibi yake kazi na akiwa kwenye likizo fupi, likizo ambayo mwenzangu
aliichukulia kinamna yake .
Mimi nilipofika ofisini, niliomba likizo ya zarura, na
nikakubaliwa bila pingamizi, na kesho
yake nikaingia kwenye basi kuelekea huko kijijini. Nikiwa ndani ya basi
nilimuwaza sana huyu rafiki yangu. Sikuamini kuwa angeinifanyia hivi, na
niliumia sana pale nilipokumbuka kauli zake za zarau kuwa mimi sina chochote,
na siwezi kushindana na yeye.
Nilijaribu kukumbuka maisha yetu ya shuleni, jinsi
tulivyokuwa karibu, na jinsi gani nilivyokuwa nikimsaidia kimasomo, maana yeye
alikuwa sio chochote, katika masomo, nilikuwa nikimsaidia sana, mpaka akafikia
hatua hiyo,lakini sasa kimaisha yeye yupo juu, na mbaya zaidi hakumbuki fadhia
zangu, anasihai kunisimanga. Nikaamini ule usemi wa kuwa kuwahi sikupata, ….
Nilikumbuka siku zile za mwisho zamitihani, ambapo alijua
kabisa yeye anaweza akafeli, aliniambia;
‘Ndugu yangu nisaidie tu, ili nifaulu huu muhula wa mwisho (semester),
maana nikifeli hapa,nimefeli mambo mengi. Wazazi wangu wamenihakikishia kwua
nikfaulu na kupata cheti, basi, mambo safi kabisa huko duniani,tatizo ni haya
mavitabu na mahesabu, …nikipata hilo ganda lao tu,utaona vumbi
langu…’akaniambia.
‘Kwani huko duniani kwenye ajira hawaangalii kufaulu kwa
mtu?’ nikamuuliza.
‘Aaa wapi, huko hawana habari na makaratasi yako , eti
ulipata `A’ kubwa, hakuna kitu kama hicho, huko akili kichwani kwako, huko ni
nini bosi anataka, ukimjulia bosi wako, basi umeula, kwanza tukitoka hapa
unachotakiwa ni kuhakikisha unapata ajira sehemu yenye maslahi, na ili uipate
nafasi kama hiyo, unatakiwa uwe na refa…huko hawaangalii maksi zako
bwana..’akasema huku akikiuna kichwa.
‘Sawa mimi sina shida, nitakusaidia tu rafiki yangu, na wewe
natumai huko duniani hutanitupa, lakini , tatizo lako hutulii darasani, vipindi
vingi unakosa, na hata ukiwa darasani unaonekana huwi makini na anachofundisha
mkufunzi,….’nikamwambia.
‘Hapa, mimi ninawaza kupata pesa tu, kupata pesa haihitaji
mahesabu, magumu, …sasa nakuomba kitu wewe nionyeshe jinsi ya kulifanya hili
swali,…wewe lifanye , halafu mimi nitanakili, mengine baadaye, na kwenye
mtihani nitajitahidi tukae karibu, nikikuminya wewe usogeze karatasi yako
karibu na mimi,nikitupa jicho moja, tu,nimeshalipata jibu,…siunanifahamu zangu,
na huko duniani ndio hivyo hivyo, ukipata dili, ni mara moja pesa ipo
kibindoni, huhitaji mahesabu makali….’akaniambia.
Ni kweli huyu jamaa alikuwa mwepesi sanawa kuibia,na
hutaamini alifaulu kiajabu ajabu sana, na kama alivyosema kuwa tatizo lake ni
kupata hicho cheti, akishakipata hicho cheti maisha kwake yamenyooka, na ndivyo
ilivyokuwa, sisi tuliokuwa tukiumia vichwa kwa kukesha na kukokotoa mahesabu
magumu, na kufaulu mtihani kwa maksi nyingi, ilikuwa ni kazi bure, mtihani wa
maisha ukatuginga,….
******
Nilifika kijijini, na haraka nikapata baiskeli, na kuelekea
huko ndani ndani , ambapo mgonjwa
akiumwa hubebwa kwa mkokoteni, au baskeli, na mara nyingi wajawaziti huishia
kujifungulia njiani,…niliangalai ile hali ya maisha pale kijijini, nikaumia
moyoni, na nikasema mimi nikiwa mbunge nitahakikisha najitahidi nipambane ana
hii hali. Hapo ndipo wazo la kuingia kwenye siasa, likaanza kujijenga.
Nilipofika kule kijijini, nilimkuta bibi wa yule binti akiwa
anafagia, aliponiona akasimama kuniangalia kwa makini, akauliza;
‘Wewe ndiye mchumba wangu?’ akauliza kwa mzaha.
‘Ndio mimi mumeo,…siku hizi unaniita mchumba wako tena, mimi
ni mumeo…uchumba ulikuwa miaka ile….au umeshasahau…’ nikasema kitani huku nikimsogelea
huyu bibi.
‘Siku hizi macho hayaoni vyema, nashukuru sana, maana hapa
kijijini sasa natamba, hakuna mwenye nyumba nzuri kama hii…wewe ndiye peke yake
unayefaa kumuoa binti,mjukuu wangu…’akasema.
‘Ina maana nyumba ndiyo mahari ya kumuoa binti yako…?’
nikamuuliza huku nikishangaa, kwani huyu bibi anajua kuwa mimi ndiye
niliyejenga hii nyumba, kumbe ni mwenzangu, na sikuwa nalijua hili hadi
aliponiambia jamaa yangu mmoja, na nilipomuuliza huyu binti, alisema yeye hajui
ni kwanini anamjenga bibi yake nyumba.
Yule bibi akaniambia,
‘Pamoja na hayo,…sasa nitajuaje kuwa kweli unanipenda, kama hukuonyesha kwa mifano
kama hii,…karibu ndani..’akanipokea lile begi langu lilokuwa nimeweka
zawadi,lakini hizo zawadi niliziona niliziona kama sio mali kitu ukilinganisha
na hiyo nyumba, maana kijumla nyumba hiyo ilikuwa ninzuri, nasijui jamaa alitumia
shilingi ngapi kuikamilisha, maana aliijenga kwa muda mfupi tu ….
*******
Baadaye alikuja binti mwenyewe, alikuwa kabeba mfuko,
kuonyesha kuwa alitokea sokoni, na aliponioa alishituka na haraka akakimbia
ndani kuweka ule mfuko, akarudi akiwa na huzni tele usoni, na kwa heshima akanisalimia, na
kuniangalia kwa muda, na hapo hapo
machozi yakaanza kumtoka akasema, ….
‘Mbona umekuja ghafla, bila hata taarifa….?’ Akaniuliza,
akionyesha kuwa na wasiwasi mwingi.
‘Imebidi iwe hivyo, ili nije nihakikishe mwenyewe,maana
mengi yametokea na mengi nimeyasikia na jinsi nilivyoona nahisi kuna jambo
….’nikasema, na wakati huo yule bibi alishatoa.
‘Najua unavyojisikia, lakini sina uwezo zaidi,…nashindwa
kuhimili hii hali tena,….ungelikuwa kwenye sehmu yangu ungelinielewa, …. nasikitikika
sana, na naomba ukubali matokeo,ili ..hata sijui niseme nini..’akainama
akionyesha uchungu.
‘Nikubalije matokeo,…mbona sikuelewi ina maana mumeshaongea
na huyo jamaa mkamkubaliana?’ nikamuuliza.
‘Wameongea na wazazi wangu, mimi nimekuja kujulishwa tu,….kuwa
kuna mtu anataka kunioa na mahari imeshapokolewa, na zaidi ya hayo,
wameshamjengea bibi yangu nyumba, wakasema sasa kama kweli nampenda bibi ,
nikubali kuolewa....maana nitajisikiaje bibi ambaye kijiji kizima wamekuwa wakimsifia, leo hii anafukuzwa kwenye hiyo nyumba....’ akasema kwa uchungu.
‘Mimi siamini hayo unayoniambia, ina maana wewe hujawahi
kukutana na huyo mtu mkaongea , ukamwambia msimamo wako, au ndio mslishakubaliana naye, unanivunga tu hapa?’ nikamuuliza.
‘Huyu mtu , alikuwa akija mara kwa mara wakati nipo huko
mjini, na nilishawahi kumwamia kuwa mimi sipo tayari kuolewa na yeye, akasema kuwa yeye ni chaguo la wazazi wangu, kwahiyo nijiandae kuwa yeya atakuwa mume wangu, mimi nilijua kwua ni utani tu, kumbe mwenzangu kazamiria,...kuna hata siku alitaka kuninunulia gari, mimi
nikakataa’akasema.
‘Oh, sasa mbona hukuwa unaniambia yote hayo,....lakini sio kitu, cha muhimu ni misamamo wako, namjau yule mwenzangu, kazamiria shari,... kwahiyo wewe sasa unasemaje..?’
nikamuuliza.
‘Mimi nisemeje, kwa hali kama hiyo,…hebu niambie, …sio
kwamba sikupendi, nakupenda sana, lakini ….angalia, hali ilivyo, nampenda sana
bibi yangu, na kitu nilichokuwa nikikiombea ni yeye kuwa katika nyumba nzuri,
na ukumbuke kuwa wazazi wangu wameshachukua pesa za mahari, na wamenitishia kuwa nikikataa
kuolewa na huyo jamaa, wao hawana radhi nami…..’akaniangalia kwa macho yaliyojaa huruma.
‘Kwani mimi nisingeliweza kuyafanya hayo, ni swala la muda
tu, na mapenzi yetu yanaingilianaje na hili la nyumba ya bibi yako,…?’ nikamuuliza
kwa masikitiko.
‘Hebu niambie mimi nifanyeje kwa hali kama hii….?’
akaniuliza. Niliinama na kuwaza mpango wangu niliokuwa nimeupanga, kichwani mwangu,nikahisi hautafaa tena,.... nikamwamgalia yule binti,na wivu ukanitinga, ina maana nitamkosa huyu binti hivi hivi, hapana, lazima kufanyike kitu, lazima...
Na kabla sijasema neno, mara tukasikia sauti ya pikipki zikija kwa kasi, na kusimama nje ya nyumba, na ghafla mlango ukafunguliwa bila hodi.....sote tukageuka kumwangalia ni nanii huyo anayeingia kwa fujo, .......
NB. Mambo ndivyo yalivyo, lakini tutajitahidi kidogo kidogo.
WAZO LA LEO: Mapenzi ni kati ya wapendanao, wengine ni wasindikizaji tu.
Ni mimi:
emu-three
3 comments :
m3 mkasa umenoga tunasubiri next.
Eid mubarak
Samira mpendwa, minalifaidhina, tupo pamoja, Mungu akipenda!
This text is invaluable. How can I find out more?
My website > It Works Body Wraps
Post a Comment