Mke wangu aliniangalia nikitandika vile vitambaa ,
akatabasamu na kuchukua baadhi ya vitambaa na kuanza kutandika, na mara mlango
ukagongwa, akaingia mtu mmoja, akanisogelea na kuninong’oneza sikioni, haraka
niliviweka vile vitambaa kwenye kocho na kuanza kuondoka, nilipofika mlangoi
nikakumbuka, nikageuka na kumwambia mke
wangu.
‘Kuna kikao cha dharura
mke wangu, kuhusu hayo maswala yetu…’nikamwambia.
Mke wangu aliniangalia bila kusema kitu, akakaa kweney kocho
na kushika shavu, na aliposhika lile shavu nikakumbuka ile siku ya kwanza
nilipomuona waakti nahutubia , na isingelikuwa huyo mwenzangu ningelirudi
niongee na mke wangu, lakini jamaa alishika mkono na kunivutia nje,akasema;
‘Achana na maswala ya mke, mambo huko sio mzuri, ukiendelea
kukaa ndani na mkeo, utabakia hivhi hivyo, siasa sio mchezo, siasa inatakiwa
mbinu, kuongea na kuwa mjanja,….’akaniambia.
‘Sawa lakini nijuavyo mimi siasa na uongozi huanzia
nyumbani,…kama nizpoiweka familia yangu vyema, nina uhakika hata huo uongozi
hautakuwa na maana kwangu…’nikasema.
‘Sikiliza,mimi mambo haya nimeyaanza siku nyingi, ukiwa
katika kampeni, unakuwa kama upo vitani, unatakwia usahau kabisa familia,
….familia itakuja kukuona wa maana hapo ukiitwa muheshimiwa, sasa hivi haioni
nini unachokifanya,….sikiliza, sasa hivi kuna mambo muhimu yakufuatilia, kwanza
tunahitaji wadhamini, kwasababu tunahitaji pesa,…’akasema.
‘Tunahitaji pesa, na ili tupate pesa tunahitajika kupata
wadhamini, lakini hata hawo wadhamini, wanategemea nguvu yako kwanza, je
umajiuandaaje, maana tusije tukaadhirika…’akasema jamaa yangu huyo akizidi
kunitonesha, maana haijapita mwezi tangu nilipouza shamba langu kubwa na
nyumba, kwa ajili ya kuweza kufanikisha kupitihwa jina langu, sasa jina
limepita, lakini…..
‘Hela yako hiyo itarudi, ukiingia kwenye bungeni, mambo
yatanyooka…wewe ni kiongozi, uwaziri kwako upon je nje…’akanipa moyo, na tukawa
kimiya kwa muda huku gari likiwa kwenye foleni tukielekea sehemu ya kikao maalumu
kwa ajili ya kujiandaa kwa uchaguzi….
Wakati tumetulia mawazo yangu yalikwenda mbali, yakikumbuka
siku ile ya ushindi, siku ambayo kwangu niliiona kuwa ni yaushindi wa maisha
yangu, …lakini sikujua kuwa kuna mengine yanakuja mbele, ambayo yana hitaji
juhudi za ziada,…..mara sauti za siku ile zikatanda amsikioni mwangu…
******
‘Nataka nikutoroshe, ….siwezi kukubali uolewe na huyo jamaa,
nimekuja leo na kundi langu, hiyo harusi kesho haifungiki….’nikasema kwa sauti
ya kuwewesa, maana humo niliingia kwa ufichohakuna anayejua ujio wangu na kundi
langu, ….watu nje walikuwa kwenye pilika pilika za maandalizi ya hiyo harusi.
‘Mimi sielewi, …’akaanza kusema yule binti.
Nilimuangalia kwa makini na kwajinsi alivyokonda kwa siku
chache ungelimuonea huruma, ilionyesha wazi kabida kuwa hayupo tayari na hiyo ndoa, lakini angelifanyaje, ….wazazi
wake, walikuwa wakali kupita kiasi na wameshachukua pesa nyingi toka kwa rafiki yangu, na wameanzishiwamiradi ya
biashara,…..
‘Mwaanngu unaona sasa mimi ni mzee, nguvu za kupambana na
maisha zimepungua na hali yangu ya kuumwa, inanafanya nisihangaike tena, hapa
sana sana namtegemea mama yako,…lakini kama umjuavyo mama yako, ubinfasi
umemzidi, nakuwa kama sio mume ndani ya nyuma….’hiyo ilikuwa kauli ya baba wa
binti wakati ananismulia kwanini kaamua kukubali kuolewa.
‘Baba nakuelewa, lakini huyo mume sio chaguo langu,
nilishampaat mtu ambaye ndiye chaguo langu…’akajitetea binti.
‘Binti yangu skiliza kwanza haya ninayotaka kukuambia, najua
hilo, ulishaniambia, lakini uangalai na mimi misha yangu, huyu mchumba wako
keshaniwekea mradi ambao utaniingizia pesa, sitakuwa nahangaika tena, ….na juzi
tu nimepata tenda ambayo itaniwezesha kusimama kwa miguu yangu, na mimi
nitaitwa baba tena, nitaitwa mume tena, na pia itaniwezesha kuendelea na
matibabu yangu bila kuwa omba omba….sasa nakuomba, mwanangu,…ni kwa ajili ya
afya yangu, ….’akasema baba yake.
Binti alimwangalai baba yake akiwa kitandani, …alikuwa
kakonda, ….na kwa kipindi kile mama hakuwa karibu naye sana, kwa sababu ya pilika pilika za kibiashara, mama alikuwa ndiye akihangaika kwa ajili ya
familia, baba ni mgonjwa hajiwezi.
‘Sikiliza mwanagu, nakupenda sana, ….na napenda furaha yako,
napenda na wewe uishi maisha mazuri, na nina uhakika ukimpata huyo mume
hutapata shida, pesa anazo, ….ana ajira yenye uhakika, na sasa kafungua kampuni
yake, sasa unataka nini, unataka ukaishie kwenye maisha ya dhiki, na huyo ….’akasema
huku akikunja uso kwa maumivu.
‘Baba sijui nifanyeje miye …maana nilishaahidiana na mhumba
wangu ninayempenda, yeye kanisaidia sana toka zamani, kumteleekza sasa hivi ni
dhambi kubwa sana ambayo sitaweza kuivumilia,…baba yeye atakusaidia tu….’akasema
binti.
‘Atanisaidia tu, lini…na hali unavyoiona,…au unataka nife,
ndio uone kuwa naumwa, hali unaiona, na mtu kajitolea kuniasaidia, ..mwanagu hii
ni kwa ajili ya afya yangu, na pia ni kwa ajili ya bibi yako kule kijijini, kwa
ajili ya kuniokoa na huu umasikini ulionikumba,kwaajili ya kunifanya na mimi
nionekane mume tena…’akasema kwa uchungu huku machozi yakimtoka.
‘Baba …..’binti akataka kusema neno na mara baba yake
akagugumia kwa maumivu, na hali ikawa mbaya,….docta alipoitwa, akasema kuwa hali
kama hiyo itakuwa ikitokea mara kwa mara, mapaka hapo matibabu ya maana
yatakapopatikana, akasema baba anahitajika upasuaji wa haraka,…lakini ni
vyemamatibabu hayo, yakafanyika India ambapo kuna uhakika zaidi,….na hivyo basi
inahitajika pesanyingi tu…..
‘Hizo pesa tutaizpatia wapi…!’akalalamika mama akionyesha
kukata tamaa.
‘Mama msiwe na shaka,mimi nimeshawaambia,kuwa…..kwa vile mimi
ni mkwe wenu mtarajiwa, nitajitolea kila kitu, hilo swala la matibabu ya baba,
niachieni mimi, nitahakikisha waiki hii anasafiri kwenda India kwa matibabu…baada
ya ndoa yetu’akasema rafiki yangu, mimi hayo nilikuwa siyajui,alikuja kunisimulia
huyu binti, dakika hizo za mwisho, akiwa tayari keshaandaliwa kama bibi harusi
mtarajiwa.
‘Kwahiyo baba anatakiwa akatibiwe kwa pesa za huyu jamaa, na
ni moja ya makubaliano kuwa uolewe na yeye….kwanza….halafu ndio akatibiwe au sio?’ nikamuuliza.
‘Ndivyo ilivyo, yeye hajasema moja kwa moja hivyo …, ila kasema
kuna mipango ya kusafiri, vibali na mambo mengine, ambayo inabidi ayafuatilie,
na huku yakifuatiliwa ni vyema ndoa hiyo ifungwe mapema, ili baba ashuhudie.,
na hata hivyo akasema kuwa weweni mtu mjanja sana, ili mamo waweze kukudhibiti,
ni vyema kuwe na mkataba wa matidhiano, kati ya familia yangu, na mimi nay
eye na familia yake kwa upande mwingine, ili kukuzuia usifanye lolote, amesema
ni kwa ajili ya kujilinda kisheria,…’akasema huyo binti.
‘Mkataba!?… ‘Mimi hapo naona kuna jambo limejificha, sina
uhakika bado, …’nikasema kwa kushangaa sikujua hayo, nikageuka na kuinama
chini, binti akasema;
‘Baba anaumwa kweli,anatakiwa
akatibiwe, unataka uhakika gani tena, ukumbuke kuwa baba bado hajaondoka,
ataondoka kesho kutwa , na inatakiwa ashuhudie kufungishwa kwa ndoa hii, ni
moja ya makubaliano katika huo mkataba, na ilibidi nikubali mbele yake kuwa
nipo tayari kuolewa na huyo jamaa ili baba akapatiwe hayo matibabu, na kwa
ajili ya…ya uhakika kuwa wewe hutaweza kuleta matatizo tena, …’akasemahuyo
binti.
‘Kwanini mpaka
mkataba,…,mimi nilijua alikuwa akimsaidia baba yako kwa nia njema , ina maana
pendo lako kwake ni kwa shinikizo, huoni kuwa ndoa yenu itakuwa haina upendo,
huoni kuwa hapo kuna kitu katikati kimejificha,,….hamuoni kuwa huyo sio mtu
mwenye huruma,….’nikasema kwa hamaki.
‘Mimi najua yote hayo, lakini yeye alidai kuwa wewe ni mtu
mjanja sana, unaweza ukanihadaa mimi nikabadili kauli yangu,kwahiyo ili
kukubana wewe , inabidi kuwe na mkataka wa kisheria, ndio ukayarishwa huo mkataba
na mwanasheria wake, ambao nilitakiwa mimi ,na wazazi wangu kukubaliana nao,
ili wewe ukija kwangu usiwe na nguvu tena…’akasema huyo binti.
‘Hiyo sasa kali….lakini nikuulize neno moja,…..je kweli
unanipenda mimi?’ nikamuuliza.
‘Hilo sio swali lakuniuliza,nimeshakuambia kuwa mimi
nakupenda, nakupenda sana,…lakini angalia hali ya wazazi wangu, ….baba ni mtu
muhimu sana katika misha yangu, licha ya mapungufu yake ya kukosana na
mama,lakini mara nyingi alikuwa uapnde wangu, pale inapobidi, baba ni mzazi
wangu, anahitajika kutibiwa, …kwahiyo inabidi nikubali, kwa ajili yake na kwa
ajili ya bibi….nasikitika sana kwa hilo,….’akasema.
‘Mimi sijakubali,…kama kweli unanipenda nataka tufanye jambo…’nikamwambia.
‘Jambi gani hilo?’ akaniuliza akiwa nawasiwasi.
‘Unajua kutoroshwa,mimi nataka nikutoroshe….leo hii,
nimejiandaa kwa hilo…’nikamwambia
‘Hapana,.kumbuka kuwa kuna mkataba wa kisheria, kumbuka kuwa
baba yangu anatakiwa akatibiwe, kumbuka nyumba ya bibi, kumbuka miradi ya baba
ambayo akirudi ndiyo anaitegemea kuendeleza misha yake..kumbuka, hapana, naomba
tukubali matokeo….’akasema binti.
‘Nakuuliza tena, je kweli unanipenda mimi?’ nikamuuliza.
‘Ndio nakupenda,ndio maana, pia sitaki wewe uzurike, ….’akasema
na kuziba mdomo.
‘Nitazurika na lipi tenai?’ nikamuuliza.
‘Huyo rafiki yako alisema kama nitafanya kinyume na hayo
makubaliano, atakufanyia jambo baya sana, mwenyewe sitaamini,…’akasema huyo
binti.
‘Hawezi kunifanya kitu mimi, hivyo ni vitisho tu…’nikasema
nikikumbuka jinsi nilivyonusurika kumwagiwa tindika, kumbe ni kipindi ambacho
huyo binti alikuwa akionyeshwa moja kwa moja jinsi gani nitafanyiwa kama
asipokubaliana na mimi.
‘Hawezi…unasema hawezi, .. , wakati siku hiyo alimtuma mtu
wake aje kukumwagia tindikali, na akawa ananionyesha waziwazi kwenye kanda
waliyoitegeshea….siwezi kukuona ukifa kwa shida kwa ajili yangu, nakupenda sana
na nipo tayari kufanya lolote ili nione wewe huzuriki….’akasema huyo binti
akionyesha wasiwasi mkubwa…
‘Hivyo ni vitisho tu…..hawezi kunifanyai hivyo, ndio
walikuja watu kunitishia na hiyo tindikali, mimi nilijua ni viabaka tu,na
sikujua kuwa ni yeye na watu wake, lakini hilo lipo mikononi mwa polisi,
nitahakikisha kuwa anakamatwa…kilichotakiwa ni ushahidi, na wewe ukiwa upande
wangu ukatoao huo ushahidi najua atakamatwa…sasa sikiliza muda unakwenda, tuangalie
hili nililokuja nalo…
Mara mlango ukagongwa…na
mimi nikajificha nyuma ya mlango, alikuwa shangazi mtu alikuwa kuweka ammbo
sawa,alipotoka nikajitokeza kwa yule binti, nikamwambia ajiandae, maana
nimeshawasiliana na watu wangu, ….
‘Mbona hunielewi…jamani, …mimi naogoap sana….’akalalamika.
‘Nimekuelewa, lakini tusipofanya huo mpango sasa hivi,
haitawezekana tena, kama kweli unanipenda wakati ndio huu, jiandae,…’nikasema na kujificha
pale pembeni ya mlango ulipogongwa tena, na walioingia safari hii,ni watu nisiowajua….nikasikia
wakisema;
‘Fanyeni haraka, nimesikia msafara wa bwana harusi upo
njiani, kama hataki mbebeni kwa nguvui…’sauti ikasema ikitoke kwa nje, nikashikwa
na butwa, na kujiuiza hawa ni akina nani tena ….
NB : Ninajaribu kufupisha , maana hapo kulikuwa na matukio mengi, lakini muda,...
WAZO LA LEO: Pigania penzi lako kwa umpendaye kwa dhati, ukijua kuwa mpende akupendaye!
Ni mimi:
emu-three
3 comments :
Subira upo, tuwasiliane kwenye e-mail!
Nipo, mie huwa sikosi humu hata nitingwe kiasi gani.
Nitakuandikia InshaAllah
Eid Mubarra
Kisa kinasisimua,na pia kimenikumbusha familia fulani ambayo haikutaka binti yao aolewe na aliyempenda bali na waliompenda familia ..sijui hapa ni familia ndio wataisha na huyo mume au?...nasubiri muendelezo
Post a Comment