Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary', na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..pia tunakaribisha mijadala na yale yote unayopenda yawemo humu. Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu. SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthreeMonday, July 2, 2012

TUPO PAMOJA-TUNASHUKURU SANA KUPIGIA KURA BLOG YAKO Wahenga walisema chema chajiuza na kibaya chajitembeza. Itakuwa sio busara kutowashukuru wale wote waliopiga kura zao kwa ajili ya kuiwezesha blog hii kushika nafasi ya kwanza katika kipengele hiki cha best poetry and writing.

Pia nawashukuru waandaji wote wa shindano hili kwa kazi yao kubwa, kwani kitokana na wao tumegundua kuwa wapo Watanzania wengi wenye blogs, zenye mambo mengi, ni swala la muda tu, ingeliwezekana kila mmoja angeziweka hizo blogs kwenye blog yake, ili kuonyesha ushirikiano.

Sijajua kwanini kusiwe na umoja maalumu, ingawaje niliskia kuwa umoja huo upo, lakini je, kuna mchakatoo gani wa kuziorodhesha hizi blog zote na kuwa na msimamo wa pamoja? Hili pengine linakuwa kuwa gumu kwasababu wengi wameanzisha hizi hizi blog kama kitu cha kujifurahisha tu, ...lakini huenda kwa namna moja au nyingine blog hizi zinaweza kuwa na faida, licha ya kutoa ujumbe.

Blog zote ni nzuri, na kiujumla kushika nafasi ya kwanza sio kwamba blog hii inafanya vizuri kuliko nyingine zilizoshiriki, la khasha kila moja ina nafasi yake katika hilo lililoandikwa kwa siku hiyo, au kila siku, ni mtizamo wa wapenzi , kwani kila mmoja ana nafasi yake katika kupenda jambo.

Na ukiangalia hpa katika uandishii kuna kuandika stories na mashahiri, huyu mashahiri kama atashindanishwa na wanamashahiri anaweza kuwa wa kwanza, lakini hapa kawekwa kwenye kundi la utunzi wa hadithi, visa,...
Lakini kwavyovyote iwavyo, hili ni jambo la kujivunia kuwa kuna wenzetu, ambao wametanguliwa kwenye fani hii, na bado wanawajali wenzao.
Hebu jiulize ni wagapi wakongwe wa fani hii, ambaye alidiriki kufanya jambo kama hili, je waliwahi kuwafikiria wenzao kwa namna yoyote ile, kama hivi,...huu ni moyo wa kipekee, moyo wa upendo, na kujali wengine.

Na hii ni nia njema kuwa blogs kwani ni sehemu ya kutoa habari, ujumbe na ili ijulikane vyema, ni vyema kukawa na vitu kama hivi vya kutangazwa. Na ni vyema kama Watanzania tukatumia blog hizi kutangaza utamaduni wetu hasa wa lugha ya KISWAHILI....Tuipende lugha yetu kwani ni moja ya kitu kinachotuweka pamoja,...

  Huenda kama kungelikuwa na zawadi  changamoto ingekuwa kubwa na hata hamasa za watu kujishughulisha ingekuwa kubwa zaidi. Tuombe mungu kuwa safari ijayo inaweza kuwa hivyo. Na wahisani wajitokeze ili kuwezesha fani hii nayoo iwe sehemu ya watu kujuana kuejieleza na kueleza yale yanayofaa kuelezana.

Nawashukuru tena sana wote, na karibuni hapa kwa ajili ya kupata visa vya maisha kwa uhalisia wake, Tupo pamoja-
Ni mimi: emu-three

5 comments :

Dina Ismail said...

hongera sana mdau mwenzetu ni jitihada zako za kuwapa mambo mazuri zaidi wasomamji ndiyo zimekuwezesha kupata ushindi.Kila la heri mtu wangu.

emu-three said...

Nashukuru sana mtu wangu Dina Ismail kuingia kjiwe hiki na kusema lolote, najua unaingia mara kwa mara,lakin hupat muda wa kusema lolote. Tupo pamoja, mtu wangu

Anonymous said...

Hongera sana, kazi yako nzuri, imeenda shule, sio ya copy and paste

Anonymous said...

Wewe ni mshindi tu sote tunajua hilo, sisi twahitaji story bwana, muendelezo wa kisa chetu, kwani ukishinda unapewa zawadi gani, hakuna kitu hapo, wakupe kilaptop basi...muendelezo wa kisa ndio muhimu kwetu...lete vitu, achana na mashindano haya ya kukupotezea muda

Anonymous said...

iko fresh ile mbaya, kazi nzuri sana.. nakutakia kila la kheri.

http://www.staryte.ucoz.com