Hakimu akasema;
‘Mimi naona tumsikilize kwanza rafiki yako, maana
nimeyasiliza mazungumzo yako mengi umekuwa ukimuongelea huyo rafiki yako, na
nilitarajia kuwa wakili angekusimamisha kuwa uongelee mambo yako, lakini
nimeona labda ina sababu fulani, …..lakini kwa vile mwenyewe yupo hapa, mimi ninaona
ingelikuwa ni bora yeye akaongea kwanza kabla hatujafika huko unapotakiwa
uongee, …au unaonaje wakili …?’ akauliza muheshimiwa hakimu.
‘Muheshimiwa hakimu, ….lengo letu ni kila mmoja aongeee
kikomo cha yale anayohusika nayo,ndio maana hatukutaka kumkatisha, ni kweli
seehmu kubwa amekuwa akimuongelea rafiki yake, hii ni kwasababu seehmu kubwa
tunayoihitaji, ni ile ambayo yeye na rafiki yake walihusika,….mengne meng yanayomuhusu
huyu muongeaji tumeshayasikia toka kwa mzungmzaji wa kwanza na wa pili,
Hata
hivyo sio mbaya,tukimsimamisha rafiki yake akaongea kuhusu yale yanayomuhusu,
kabla hatujafikia sehamu hiyo muhimu…’akasema wakili mwanadada na kumgeukia
rafiki wa mke wa wakili mkuu, ambaye alionekana kuwa mbali kimawazo.
‘Ni zamu yako kukisikia …’’akasema na alipogundua kuwa huyo
mwanadada yupo mbali kimawazo aakmsogelea na kumshika bega.
‘Unaweza kuongea yale ambayo mwenzako kayaacha , naona sehmu
kubwa inayokuhusu wewe imeshaongelewa, hebu tuanze kwa wewe kutuambia mlijuana
vipi na Kimwanaau ulimjuaje Kimwana?’ akamuuliza.
Yule mwanadada akainuka pale alipokuwa kakaa na kuanza
kwenda mbele, na wakati anapita pela nilipokuwa nimekaa akaniangalia , halafu
akatabasamu,…Nilijiuliza sana akilini , mbona huyu mwanadada anakua kama vile
namfahamu.
Kabla hajaanza kuongea, simu yangu ikaashiria kuwa kuna ujumbe
wa maneno, nilipoaangalia nikagundua kuwa ni mmoja wa jamaa zangu ambaye
niliahidiana naye kuniletea mzigo,na ujumbe ulisema kuwa mzigo umeshafika
kwahiyo nahitajika bandarini haraka….ooh, nilishikwa na butwaa, maana sikupenda
kabisa kumkosa huyu mwanadada akiongea, …..lakini huo ujumbe ni moja ya maisha
yangu ya baadaye, nikainuka na kumuonyeseha ishara wakili mwanadada, akaja
karibu yangu;
‘Vipi kuna nini,…?’akaniuliza,nikamuonyeshea ule ujumbe,
maana nilishmafahamisha kuwa nina biashara nimeianzisha na yeye mwenyewe
akacnagia kiasi fulani cha mtaji.
‘Oooh, ina bidi uondoke, maana huo mzigo ni muhimu na
ukichelewa utakuta faini kubwa, mimi nitakuhadithia nini kimeendelea,
kamautafanikiwa kuutoa haraka ,rudi hapa huenda ukakuta bado tunaendelea,….’akasema
na kunishika mkono.
‘Usijali ….’nami nikamwangalia yule mwanadada akiwa
anaendelea kujieleza, huku natembea kutoka nje, kwahiyo yale mengi aliyoeleza mwanzaoni nilisimuliwa na wakili mwanadada. Na wakati natoka yule mwanadada alikuwa katizama
mbele , ya washiriki,hakuniona nikitoka…..
*****
‘Nilifika hapa Dar na wazazi wangu kutoka Kenya. Wazazi wangu waliamua kufanya
hivyo, baaada ya kuona kuwa biashara kule Kenya haiwaendei vyema,wakaona kuwa
ni bora kubadili mazingira, na kuja hapa Dar, na kwa vile wazazi wangu walikuwa
an ndugu zao hapa, haikuwa vigumu kwao, walichofanay ni kuwasilina na ndugu zao
mapema, kabla hawajafika hapa.
Mimi nilipata kazi moja kwa moja kwenye moja ya hospitali
hapa Dar, na muda mwingi nilikuwa nautumia kujisomea, …sikupendelea sana marafiki
au kujumuika na makundi, nikawa kama mpweke fulani na hata wanaume waliojaribu
kuniongelesha walinikuta sina maongezi nao.
‘Mawazo mengi yalikuwa yakiniandama mara kwa mara, na waakti
mwingine, ilibidi niwe nakunywa dawa za
usingizi.
‘Ulikuwa unawaza nini?’ akaulizwa.
‘Historia yangu ni ndefu, inaanzia utotoni, na huko haina
haja kuwaelezea hapa kwa sasa,naona ni mamb yangu binafsi, ila ninachoweza
kusema hapa ni kuwa, akili yangu ilikuwa ikimuwaza mtu niliyotokea kumpenda, ….’akasema
na kugeuka kunagalia pale alipokuwa kakaa mtoto wa Msomali, akashangaa kuona
ile sehemu ipo wazi.
‘Mtu huyo tuliahidiana naye toka utotoni,hadi …..naweza
kusema ni utoto, lakini akili yangu toka sasa inaona kuwa lile tendo
lililotokea pale ni la halali, na moyo, akili na mwili ukawa unaamini hivyo
kuwa tendo lile ni haki yangu, na sikutakiwa kuwa na mume mwingine zaidi yake…’akasema.
‘Tendo gani hilo?’ akauliza hakimu.
‘Tendo la ndoa…..’akasema na watu wengine wakaguna.
‘Kila mtu ninayemuhadithia kuhusu hilo anatokea kunicheka na
kuniona sina akili, lakini kama mtua ngeliingia kilini mwangu akanichambau
angeligundua kuwa mwili wangu wote ulikuwa umamshiba huyo jamaa…na niliona kuwa
kweli huy ndiye mwenzangu katika maisha.
‘Hata mimi mwenyewe kuna muda najilaumu nakusema kuwa huenda
kuna kasoro kichwani mwangu, maanamichezo ya kitoto ni utoto tu, ikishapita
umri huo huwezii kutazamia kuwa yale yanaweza kuwa kweli,lakini mimi tendo lile
nililina kama kweli na katika umri wangu wote toka siku ile niliojiona kam make
wa mtu.
‘Fikiria tokautoto, hadi usichana ,hadi umri kama huu, bado
namuwaza mtu huyo huyo, na abadaye uanjikuta yeye hana habari nay eye, yeye
yupo na watu wengine, halafu unasikia kabisa kuwa keshaoa,….kwakweli niliteseka
sana,…..na hali kam hiyo ilipokuwa ikijinia akilini nakuwa kama mtu
aliyechanganyikiwa…
Nilipofika hapa Dar na wazazi wangu , wao walinishauri kuwa
niachene kabisa na hayo mawazo , hata kama nitamuona huyo jamaa nihakikishe
kuwa siongei naye, maana ninaweza kuchanganyikiwa, kama keshaona, ni nini
natarajia, ….nivunjendoa ya watu, hapana, ni bora kuishi bila yeye, ingawaje moyo
unaumia. Hata hivyo sikuwezakuvumilia, kwani nilianza uchunguzi wa kumtafuta
yule aliyekuwa akiutesa moyo wangu.
‘Nilikuwa najua toka siku nyingi kuwa mtu huyo yupo hapa
Dar, lakini sikuwahi kuwasiliana naye …ningeliwasilina naye vipi wakati nilijua
hana habari ni mimi. Na mbaya zaidi ni aple niliposikia kuwa keshaoa binti wa huko kijijini, lakini
hata hivyo nilikuwa na nia ya kumuona tu, ili tu nijue yupoje, na nijue kwanini
kaamua kunifanya hivyo.
Nilijua kuwa akiniona hataweza kunikumbuka kwa haraka, maana
sura yangu ilibadilika sana, hata ndugu zangu wa huko kijijini ambao nilikuwa
nijakutana nao muda mrefu, walishanisahau,…labda ni kutokana na hali ya hewa,…sijui,
ilamimi nilijiona kama kawaida tu.
Nikawa kila mara
nikipita muda nazunguka sehemu mbali mbali hadi siku moja nikafika kwenye jengo
moja, ambalo nilisikia ni maarufu kama
sehemu ambayo wakina dada waliwekeza kwa ajili ya kujiuza kwa wanume, na hapo
hukutana na wanaume wenye pesa, na kuwahadaa, ndivyo nilivyosikia lakini sikuwa
na uhakika na hilo.
Nilipofika hapo moyo wangu ulikaribia kupasuka,…..nilimuona
mtu ambaye nilikuwa nazani ndio yeye,
mtu huyo alikuwa kasimama mlangoni mwa ile nyumba na baadaye akaingia ndani,
kwanza moyo wangu ulikuwa ukihakiki kuwa ndio yeye au la, na kw aupande
mwingine ukawa unamshuku kuwa huyu mtu kumbe ana tabia hiyo ya kutembea na hawa
akina dada,ambao jamii ilikuwa ikiwaona kuwa wanafanya mambo mabaya.
Nikasubiri kwa muda, na alipotoka nilihakikisha kuwa ndio
yeye, kwakweli niliumia sana , nikajiuliza ina maana huyu mtu ndio kaharibika
kiasi hicho, nikaahidi kumtafuta ili nijue ni kwanini kawa hivyo, na nilitamani
niwasiliane na wazazi wake, maana kama wangelijua hili sizani kama
wangemvumilia kwa jinsi ninavyojua familia yao ilivyo. Nikaona ni vyema kwanza
nihakikishe hilo kabla sijawasilina nao.
‘Lakini nakumbuka niliambiwa kuwa huyo jamaa keshaoa, binti
wa kijijini, sasa imekuwaje,….’nikajiuliza sana hilo swali bila jibu, na
nilijua njia njema ni kukutana na huyo jamaa, lakini haikuwa rahisi kiasi
hicho. Na nikakata tamaa kabisa.
Siki kadhaa nikapata habari toka kwa mtu anayemfahamu kuwa
keshaoa msichana mmojawapo wa hawa wanaoendesha hiyo biashara ambayo jamii
haikubaliani, nayo, sikuamini, na siku hiyo nilikuwa kaam mtu
aliyechanganyikiwa. Sijui kwanini nilikuwa hivyo maana baada ya yote hayo
nilitakiwa kuachana na huyu mtu, na kuamua moja,lakini ilishindikana.
Basi siku zikaenda na mara nikakutana na huyu mke wa wakili
mkuu,kipindi hicho nilishaamua kutokuhangaiak tena, na nishaamua kuwa mimi
sitaki wanaume, au kuolewa na mtu yoyote.Kila mwanaume aliyenijaribu kuniomba
niwe rafiki yake, nilikuwa kama mbogo, na kutokana na hali hii wengi walifikiri
nimechanganyikiwa.
Siku fulani nilikutana na huyu jamaa, kwakweli sikutaka hata
kumuona, na sijui ilikuwa ni kitu gani, maana nilimuona kama shetani fulani
hivi, nikamkimbia,….’hapo wakili akamsimamisha na kumuuliza swali.
‘Ulimuonaje huyo mtu kama shetani,…?’
‘Nilimuona hana sura ya kawaida, na kama ana mtu mwingine
nyuma yake…lakini nilikuja kujua kuwa ni ile chuki iliyokuwa imejijenga
akilini.
‘Je uliwahi kukutana na huyo jamaa mara nyingine, au ilikuwa
hiyo mara moja, na ukamkimbia?’ akaulizwa.
‘Kukutana naye uso kwa uso ni mara moja tu, sehemu nyingine
nilikuwa nikimuona kwa mbali, na nilijaribu kila uwezo wangu kuwa mbali kabisa na
yeye, …
‘Je uliwahi kufungwa , kushikiliwa na polisi kwasababu
zinazohusina na huyo mtu au jambo jingine?’akaulizwa.
‘Hapana, mimi sijawahi na kama nilivyokuambia baadaya hilo
tukioo la kukutana naye na kumkimbia sikuwahi kuwa naye karibu tena…’akasema.
‘Je uliwahi kuumizwa kwa risasi au kupata jeraha kama hilo,
kutokana na yeye?’akaulizwa.
‘Hapana ,sijawahi, ….ndio nilikuwa na upendo wa dhati na
huyo mtu, lakini nilishafikia sehemu nikaamua basi sio huyo mungu
eliyenipangia, na hata pale niliposikia kuwa kamuacha mke wake wakijijini na
kuoa mke mwingine,…nikaamua kuachana naye….’akasema.
‘Haya hebu tuambie ilikuwaje mpaka ukawa mmoja wa walimu wa
kufundisha hawo wasichana?’ akaulizwa.
‘Siku moja nilisikia kuwa yupo jamaa ambaye ni mtaalamu wa
kusaidia watu walioathirika kimawazo kama yangu, maana kwa ujumla nilikuwa kama
mtu aliyechanganyikiwa, nilijaribu sana kujizua bila mafanikio ,sijui ni kitu
gani kilikuwa kimewekwa akilini mwangu, ….niliwahi kusaidiwa na madakitari
bingwa lakini haikusaidia kitu,….basi nikaoan ngoja njaribu kumuona huyo jamaa
huenda akanisaidia.
Nilipokutana naye na kumhadathia matatizo yangu, akanichimba
undani wangu,…. kijumla niligundua kuwa ana kipaji hicho, maana alivyokuwa akinipa
zile nasaha na kutambua nini kilichokuwa kikinisibu, nikajua ni mtu ambaye
anayeweza kunisaidia,sikujua ana nini nyuma ya pazia…
Baadaye huyo jamaa akaniambia kuwa ili kuondokana na mawazo
ya mara kwa mara ni bora niwe nafundisha shule za kuwahudumia watu wanaohitaji
msaada wakindoa,… sikupenda tena kazi kama hiyo, nilikuwa nimeshatosheka na
kazi yangu ya udakitari.Nilikuwa nikijiuliza,kama mimi mwenyewe nimeshindwa
kujisaidia nitawezaje kuwasaidia wenzangu.
Huyu jamaa alinipa moyo akasema kuwa mimi nina kipaji hicho
na pia nina utaalamu wakuosmea,sio vyema kuupoteza hazina hiyo hivihivi tu, ni
bora niwasaidie wengine ili nipate ujasiri wa kupambana na matatizo ya
kimaisha. Na pia inaweza kunisaidia kugundua mengi katika maisha ya watu na
mhusiano yao. Nikaona ni jambo jema, kwahiyo nikaamua kufanya hivyo ,kama sehemu
ya kuniondolea mawazo,na kweli nilipojaribu tu,nikawa na hamasa kama ile
niliyokuwa nayo huko Kenya.
‘Je ulipokutana na Kimwana kama mmoja wa wanafunzi wako,na
kugundu ndiye alikuchukulia mpendwa wako ilikuwaje?’
‘Kitu cha kwanza ambacho niliona ni cha ajabu kwenye hiyo
shule ni pale nilipopewa masharti , nivae vipi, niwe vipi. Niliambuwa kuwa mwalimu
wa hiyo shule, alitakiwa asijulikane sura yake, nikaelekezwa jinsi gani ya
kuvaa, na kuwa nihakikishe kabisa wanafunzi hawanitambui hata mara moja,
kwasababu ninaweza kushindwa kuwasaidia , na mimi nilikubaliana na hilo maana
sikutaka hata kazini kwangu wajue kuwa nafanya hiyo kazi ya ziada,….
‘Kimwana nilimgundua hapo hapo,...sikuwa namjua sana kabla ya hapo, nilikuwa nasikia jina lake tu watu wakimuongelea. Na sikujua mwanzoni kuwa ni mpenzi wa
huyo jamaa ninyemtafuta, nilimuona kama mwanafunzi ambaye ni mwepesi kujua mambo, mcheshi muelekevu,…nikawakaribu
naye sana, na hata hivyo, ilionekana kuwa huyo mwalimu aliyekuwepo hapo
mwanzoni alikuwa naye karibu, maana maongezi yangu na yeye yalikuwa yakiashiria
kuwa ananijua sana.
Nilimdadisi sana kuhusu maisha yake, na nilikuja kugundua
kuwa anatokea huko kijijini kwetu,na nilipowauliza wazazi wangu kuhusu huyo
Kimwana, walisema hamjui, lakini watajaribu kutafuta wapi anatokea, baadaye
walikuja kuniambia kuwa nisiwe na urafiki naye, wanasema familia yao haina
muelekeo mwema , na hata huyo msichana mwenye inasemekana alitorokahuko kwao….
‘Nilipogundua hilo nikaona nilitafutie uhakika wake, na
kweli nillipomdadisi sana huyu mwanadada akanifunulia maisha yake ya toka
utotoni, …..nilichoka.
‘Sasa hivi nimempata bwege mmoja, ana nyumba,…..anatokea
huko huko kijijini kwetu,….huyo jamaa ana sura nzuri, anavutia, lakini hana
pesa sana, kamuoa binti mmoja toka huko kijijini, binti mwenyewe namfahamu,….mshamba
wa kutupwa, hajui mapenzi, ….mapenzi kwake ni kazi za nyumbani, kuwajibika kama
punda, lakini nini amfanyie mumewe hajui….sasa mtu kama huyo utamsaidiaje…’akaniambai
siku moja.
‘Kwani kakuomba umsaidia kama kakuomba,mshauri aje hapa,
ndio watejawe hawo, mlete hapa shuleni. Sisi tutajua jinsi gani ya kumfundisha…’nikamshauri.
‘Eti nini,nimlete hapa, ili afunguke , ….hapana aliyelala
usimwamshe, ukimwamsha, ooh, huyo mwache kama alivyo, nilisoma naye, ana
katabia ka uzamani,…hapendi mabadiliko, sasa nimeona ni bora nimuingize mjini ….ninachotaka
ni kumpata mumewe, …ile nyumba ni nzuri sana, ….ukiiona mwenyewe utaamini
maneno yangu, na ipo sehemu nzuri ya
biashara, ukiipata, na baaadaye unaweza ukaiuza kwa hela nyingi sana,…mimi
naona mbali , sio hapa….’akasema.
‘Mimi kama mwalimu wako nakushauri kabisa uachane na waume
za watu, hebu fikiria kama wewe ungelifanyiwa hivyo ungelifurahi….’nikamwambia.
‘Mimi nilishakuambia toka siku nyingi, hapa nimekuja kusoma,
maisha yangu ya mitaani sitaki mtu ayaingilie,…nimekumabia hili tu kwasababu
umeniuliza, vinginevyo nisingelikuamabi kwasababu hayakuhusu..’akasema kwa
ukali na kuondoka zake.
Baada ya siku kadhaa tukawa hatuongei sana kuhusu maisha
yake, lakini siku moja tukajikuta tukiongelea maswala hay o hayo, akaniambia
sasa hivi keshafanikiwa kumpata huyo anayemuita bwege wa kijijini, na ndoa ya
huyo jamaa imeshvunjika,….
‘Mungu wangu umefanya nini…’nikasema kwa huzuni.
‘Wewe unajali nini, kwani ni mume wako….wajinga ndio
waliwao, ..mjini hapa, kama mke kashindwa kuwajibika, nani wa kulaumiwa, huyo
mwaume kajileta mwenyewe, sikutumia nguvu, ni yale yale mahaba …mvuto, na ule
mkao wangu wa siku ile , aliponiona kwa mara ya kwanza ….siunajua tena….sasa nifanye
nini…mungu akupe nini,..kwahiyo mimi nimekuja kwako kukuambia tu, kuwa kuanzia
leo, nitapunguza siku za kuja hapa darasani, maana natarajia kuwa mke wa mtu…
‘Ina maana mumeshapanga kufunga ndoa tayari….?’nikamuuliza
‘Sasa,.. ndoa imeshapangwa ,na hilo ndilo lengo langu, hiyo
ni hatua ya kwanza, kitakachofuata ni urithi, nyumba lazima iandikwe kwa jina
langu, baadaye jamaa hana lake, namfukuzilia mbali….kwanza sasa hina
kazi,namlisha mimi….na atabakia hivyo hivyo, baba wa nyumbani….’akasema huku
akijiandaa kuondoka.
‘Mimi ni mwalimu wako, na itakuwa ni mtu wa ajabu
nikikiufundisha ubaya, hayo unayoyafanya sio mambo mazuri…hebu niambie ni nani
huyo mwanaume?’nikamuuliza.
‘Ni bwege mmoja wa huko kijijini,….eti wamekosa majina mpaka
wanajiita majina ya nchi nyingine…’akasema kwa dharau.
‘Jina gani hilo…?’ nikamuuliza.
‘Anaitwa Msomali……wengi wanamuita mtoto wa Msomali…’
‘Eti nani….?’nikasema na kujikuta nikipepesuka…….kiza
kikatanda usoni, na kupoteza fahamu.
NB: Usipende kumwamini kila rafiki, na ukawa unaongea
matatizo yako kwa kila mtu…hasa matatizo ya ndani ya ndoa. Huwezi jua ni nani
adui yako, maana siri ya kila mtu ipo moyoni mwake, inawezekana kabisa rafiki
yako wa karibu akawa ndiye adui yako…
Ni mimi:
emu-three
2 comments :
Kazi nzuri ujumbe mzuri, kaka keep it up, na tunga kitabu,mbona kazi zako nzuri sana
Tatizo weye unakatizia patamu!
Post a Comment