Niliwahi kurudi pale mahakamani, baada ya kupokea huo mzigo
tulioagiza toka nje, zilikuwa bidhaa za kibiashara. Ingawaje kila biashara
niliyowahi kufanya nilikuwa sifanikiwi. Na nilipoupokea huo mziga na kuhakikisha
umefika seehmu yake, niliharakisha kurudu mhakamani.
Nilipofika mlango wa chumba kunapoafanyika hayo mahojiano,nilisikia
jina langu likitajwa, nikawa na wasiwasi, maana sikujua kwanini jina langu
litajwe, nikaharakisha kuingia ndani, ili nimuone huyo aliyenitaja,
nilipofungua mlango na kuingia ndani, nilikuta yule mwanadada, rafiki yake mke wa wakili mkuu akiwa bado anaendeela na
maelezo yake.
Niliingia na kukaa sehemu yangu, na nikawa na hamu sana ya
kutaka kujua kwanini jina langu lilitajwa, lakini kwa muda ule sikuweza
kumuuliza yoyote, kwani kila mmoja alikuwa katega masikio akimskiliza huyo
mwanadada , nikamtupia jicho yule mwanadada, ambaye bado alikuwa akiongea na
wakati huo alikuwa akiulizwa maswali na wakili mwanadada.
‘Umesema ulipoteza fahamu, na ulipozindukana Kimwana alikuwa
hayupo, ukasema alikuwa kakimbia, na aliyekuwa akikuhudumia na Sokoti, yeye
alijuaje kuwa umepoteza fahamu?’ akaulizwa.
‘Huyo Sokoti alisema kuwa alipgiwa simu, na mmoja wa walinzi
wa hapo na haraka alikuja na kuhakikisha napata matibabu ya haraka, na baada ya
tukio hilo nikawa mbali kabisa na Kimwana, na hata mahudhirio yake darsani
yalikuwa yanapungua, na baadaye nilisikia keshaolewa na pia anafanya kazi,
kwenye kampuni moja. ….
‘Uliambiwa kaolewa na huyo huyo mtu wako?’ akaulizwa.
‘Wengi niliowauliza walikuwa a shaka, lakini baadaye
niligundua kuwa kweli kaolewa na huyo mtu niliyekuwa nikitamfuta…’akasema huyo
mwanadada, na kuonyesha uso wa huzuni.
Nikawa nateseka moyoni, na sikujua nini nifanye, …kwani
licha ya kuwa sikuwa na mwasilino na huyo mtu na…sikuwa na uhakika kuwa kweli
bado ananipenda, lakini sikupenda mtu amadhuru, niliona kama vile mimi ndiye
ninayefanyiwa hivyo. Nikiwa nahangaika huku na kule, ili angalau nikutae na
huyo jamaa, ndio nikaja kukutana na mke wa wakili mkuu.
Na kama alivyoelezea jinsi gani tulivyokutana, na bahati
nzuri, kumbe na yeye alikuwa na mataizo yake, na yote yanamlenga Kimwana, na
katika kujuana kwetu, ndipo akaja na wazo hilo, la kuhakikisha kuwa tunamuondoa
huyu mtu maana ni sumu kwa ndoa za watu.
Kwa kweli wazo hilo nililipokea kwa haraka sana bila kujali
madhara yake ya baadaye,ingwaje mara kwa mara nilikuwa nikijiuliza ni kitatokea
na jinsi gani ya kujihami na hilo tulilodhamiria kulifanya. Hata hivyo, moyo
wangu ulishaingia sumu, sumu ya unyama…nilijiukua na mimi nikiwa na hasira, na
chuki , na wivu uliopindukia dhidi ya huyo mwanadada, …
Kama hata wewe ungelikutana naye ukasikia kauli yake,
ungelipandwa na hasira maana kauli anayotoa mdomoni, inakera, inawafanya wale
waliopo kwenye ndoa zao kuwa hawajui majukumu yao, na yeye ndiye mjuzi, na
aheri angelikuwa na nia njema, lakini yeye alikuwa kadhamiria mabaya katika
ndoa za watu, kuharibu na kufisidi kabisa. Na sikupenda hilo, ….nikamkubalia
mke wa wakili mkuu wazo lake, nikiwa na dhamira ya kweli,na hasa pale
aliponisimulia masahibu yake,…
`Basi yeye akaahidi kuwa atapata hiyo silaha…..’Alipofika
hapo hakimu akaangalia saa yake na kusema kuwa muda umekwisha anaona ni bora
maelezo mengine yasubiri kesho yake, na akasisitiza kuwa sote tuwepo kwani tupo
kwenye kiapo cha uaminifu kuwa hakuna hata mmoja atayekosa kwenye hayo
mahojiano.
*******
‘Hebu niambie maana nilipofika hapo mahakamani nikiwa
nimetokea bandarini nikasikia jina langu likitajwa, na nahisi aliyelitaja jina
langu ni huyo mwanadada aliyekuwa akiongea, kwanini kanitaja, ana nijua wapi
mimi…..?’ nikamuuliza.
‘Ina maana tangu aanze kuongea, hadi sasa hujamjua ni nani?’
akaniuliza.
‘Ningelijua nisingelikuuliza,…na kama ujuavyo, sikuwepo
wakati anaongea,….ndio kusemaukweli mara nyingine nahisi kuwa ni mtu fulani,
lakini huyo ninayemuhisi kuwa ni yeye hafanani nahuyo mwanadada rafiki wa mke
wa wakili mkuu, na huyo ninayemjua mimi najua yupo huko Kenya na huenda keshaolewa
,….’nikasema.
‘Huyo unayemuhisi ni nani, au ndiye yule mchumba wako wa
utotoni..?’ akaniuliza
‘Huwa mara nyingine kutokana na maelezo yake, namlinganisha
na huyo mchumba wangu wa utotoni, lakini sizani kama ni yeye, maana ni muda
mrefu atakuwa keshaolewa na huenda ana watoto ….’nikamwambia.
‘Kwanini unahisi hivyo, kuwa huenda ni yeye, au huenda sio
yeye? Akaniuliza.
‘Kwasababu yule msichana, nilikuwa namfahamu sana,
haiwezekani abadilike kiasi hicho, na kama ingelikuwa ni yeye angeshaniambia,
maana tulikuwa tunapendana sana, ….’nikasema.
‘Kwa mara ya mwisho mliachana naye akiwa na umri gani?’
akaniuliza.
‘Alikuwa mdogo,msichana mdogo tu…’nikasema nikijaribu
kukumbuka sura yake ya usichana.
‘Na mlikuwa hamuwasilini naye tena?’ akaniuliza.
‘Hatukuweza kuwasiliana naye tena, maana kwa mara ya mwisho
kuachana naye, ilikuwa baada ya kunifumania na msichana mmoja wa kule kijijini,
alikuwa kakasirika sana,…..na licha ya kujitahidi kutafuta mawasiliano naye,
lakini sikuweza kupata anuani yake, na hata wazazi wangu hawakujua wapi
ninaweza kupata hayo mawasiliano na yeye, kwani wao hawakuwa na upendeleo na
huyo msichana na familia yao.
Na kwa kupindi hicho nilijifanya kama sijali, na siku
nilipokwenda kijijini kutafuta mke wa kuoa, niliomba kama inawezekana nikutane
naye, na kila msichana niliyekutana naye nilimlinganisha na huyo msichana na ndio maana sikuweza kupata
msichana kwa anayenifaa zaidi ya yule msichana wa kijijini, ambaye nilimuoa
kwasababu ya huruma ….
‘Ina maana hakuna jambo ambalo linaweza kukumbusha kuhusu
yeye, hakuna kitu kwenye mwili wake ambacho kinaweza kukukumbusha kuwa ni yeye,
….?akaniuliza.
‘Siwezi kukumbuka, zaidi ya sura yake ya utotoni,… maana
ndio tulikuwa karibu sana naye, lakini kwa muda ule sikuwa na wazo la
kumchunguza maumbile yake ya mwilini, kwani ukumbuke licha ya utundu wangu kwa
wasichana, lakini huyo , yeye nilimuheshimu sana, na nilikuwa nikisema moyonu,
huyo ni mke wangu, na siku ya kuujua mwili wake ni hapo tutakapofunga ndoa,….lakini
mmmh, labda macho yake…..na ..na….’nikasita.
‘Na na..nini?’ akaniuliza.
‘Huyu mwanadada nikimwangalia naona nahisi macho yake,yanafanana
sana na yeye, lakini hata hivyo sijapata mwanya wa kumwangalia vyema, na kila
mara tukiangaliana inakuwa kama vile namjua na inakuwa kama vile kuna hisia za
namna ya ajabu…..’nikasema.
‘Hisia kama zipi?’akaniuliza.
‘Siwezi kuzielezea vyema, lakini nahisi moyo wangu ukienda
mbio..na nashikwa na kitu kama ganzi, unajikuta unamwangalia bila kupepesa
macho,……’nikasita kuendelea.
‘Ni hisia za kupenda,…usijifanye hujui wewe ni mtu mzima
bwana, na unasema hujapata muda wa kumwangali, na sasa unasema ukimwangalia,
unataka kumwangalia kwa vipi ili umjue vyema…..’akaniambia.
‘Unaweza kuziita hivyo..hisia za kupenda, lakini mbona
ninakuwa mwoga….nahisi kama vile mimi ni mkosaji, au nikisema lolote kwake
anaweza aka…..nahisi kama nitapata maneno ya mbaya..yaani sielewi, …nahitaji
muda wa kumwangalia kwa makini, maana muda ninaoangaliana na yeye, unakuwa kama
mtu aliyepigwa na ganzi, na akili inakuwa haifanyi kazi vyema….’nikasema.
‘Labda kwa vile unahisi ni huyo msichana wa kijijini na
unaogopa kuwa ulimkosea ndio maaa unamuogopa?’akaniuliza kama vile anaongea.
‘Hapana sio hivyo….ila kila nikimuona nahisi moyo ukinienda
mbio,nakuwa na wasiwasi sana,nakuwa sijielewi, kwahiyo, aah, sijui nikuambie
nini…..’nikamwambia.
‘Usijali yote hayo yataisha,…na kama kweli mnapendana basi
mambo yataenda shwari…’akaniambia huyu mwanadada wakili.
‘Lakini wewe inaonekana unamjua vyema huyo mwanadada,
hakuwahi kukugusia kuwa yeye ni nani na anaotoka wapi?’ nikamuuliza.
‘Wewe ndiye mwenye shida naye, na wewe ndiye uliyewahi
kuishi naye, kwahiyo kama ni yeye ingelikuwa ni rahisi kwako kumjua , mimi
siwezi nikahakikisha moja kwa moja kuwa ni yeye, kwani wapo wengi
walishajifanya kuwa wao ni watu fulani, na kumbe sio, lengo lao ni kupata kile
wakitakacho. Cha muhumu ni tususbiri kwanza, tutamsimamisha tena tutamuhoji, na
mwisho wa siku ukweli utajulikana…’akasema huyo mwanadada wakili.
‘Kwa maelezo yao yeye na mke wa wakili inaonyesha ndio
waliomuua Kimwana, ….huoni kuwa bado kuna safari ndefu ya kujuana na huyo
mwanadada, maana kama wameua mwisho wao ni jela, au sio?’ nikamuuliza , na yeye
akanianglai na kutabasamu, akasema;
‘Ukweli wa yote utagundulika ndani ya mahakama, kama wao
ndio wameua, sheria ipo wazi, na mwenye mamlaka hayo na msimamizi wa sheria ni
hakimu, ndio maana tumemuita yeye, na yeye atatushauri nini kifanyike,
hatukutaka kesi hii tuikimbizie ndani ya mahakama kwanza, tuliona tuiweke
kinamna hiyo kwanza, ili kama kuna uwezekano fulani, hawo wenye makosa waangaliwe
kwa jicho la huruma….’akasema.
‘Hilo kweli sizani kama linawezekana, ukiua upo hatiani,
hata kama ni kwa bahati mbaya,….utasikia unahukumia miaka thelathini, au kumi,
kwa kosa la kuua bila ukusudia, …na kwa maelezo yao, hawakuua kwa bahati mbaya
walidhamiria kabisa….sababu ya wivu, na kutaka kulipiza kisasi….’nikasema na
yeye akaniangalia kwa makini na kusema.
‘Usiwe na shaka, na usikimbilie huko, hatuna uhakika bado
kuwa ni wao walioua, bado hatujafikia hatua hiyo,…..kama ni wao tutaona, na
kama kuna mtu mwingine tutamsikia, wewe vuta subira….’akaniambia.
‘Na nilikuwa na ombi moja….’nikasema
‘Ombi gani,…?’ akaniuliza.
‘Naomba nionane na huyo mwanadada rafiki wa mke wa wakiliki
mkuu,….nataka niongee naye, nimuhoji mwenyewe nimjue kuwa yeye ni nani….’nikasema.
Wakili mwanadada akaniangalia kwa makini, kwa yale macho
yake ya kawaida na baadaye akageuka kuangalia dirishani, halafu baadaye
akanigeukia na kusema;
‘Kwanini uniombe mimi, ..yeye sio mfungwa, na wala hana
mume, kusema kuwa atamzuia, ni wewe mwenyewe kwa juhudi zako kwenda kumuomba yeye
na muongee, kwani unamuogopa, …wewe unajulikana na kiwembe, mtaalamu wa
wanawake,..au sasa unajifanay kwangu, kuwa huna tabia hiyo….au unataka niwe mshenga
wako, …?.’akasema.
‘Mhh, mengine wananipakazia tu, hiyo tabia ilikuwa ya
ujanani, sio sasa. Na hata hivyo wewe ni wakili wangu ingawaje sina pesa za
kukulipa, ningelifurahi, ukawa mtu wa kati, kati yangu mimi na yeye, lakini ni
yeye, na kama sio huyo ninaye mzania, basi , sina haja ya kuhangaika naye,
safari hii sitaki kufanya makosa tena , ……’nikatulia huku nikiwaza.
‘Je kama ni yeye unataka ufanye nini na yeye..?’ akaniuliza.
‘Nitamuomba tufunge naye ndoa,..,’nikasema huku nikiwa
naangali juu.
‘Sawa,…yule kule anakuja na rafiki yake, unataka muongee
naye sasa hivi?’ akaniuliza, na nikageuka na kujikuta tukiwa tunaangaliana, …..
********
NB Kwa leo tuishie hapo, tukitafakari hayo yaliyoongelewa na
wahusika wa kisa hiki, je ni nini kitafuta , tuombe mungu tukijaliwa tena!
WAZO LA LEO: Kila
mtu anapenda kupata maisha bora,… lakini kupenda huko kusiwe zaidi ya kipato
chetu, ni bora tukajenga tabia ya kurizika, na kile tulicho nacho na kama tunapenda
kupata zaidi basi tujitahidi zaidi katika kazi zetu biashara zetu,…bila kuvuka
mipaka.tukumbuke kuwa tamaa ni mbaya, na asiyetosehaka na kidogo alicho nacho hata
akipata kingi hatatosheka.
Ni mimi:
emu-three
4 comments :
Jirani umesalimika wewe? Siku njema pamoja na familia yako.
Jirani yangu Edna, nimesalimika namshukuru mungu , wasi juu yako mpendwa wangu!
Ndugu wa mimi kazi inazidi kusonga zaidi na zaidi, kwangu ni furaha sana.
Mungu azidi kukubariki sana.
Pamoja Daima ndugu wa mimi!!!!!!1
Ndugu wa mimi tupo pamoja sana, ubarikiwe na mambo yako yabarikiwe pia!
Post a Comment