Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary', na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..pia tunakaribisha mijadala na yale yote unayopenda yawemo humu. Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu. SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthreeTuesday, July 3, 2012

Hujafa hujaumbika-62 hitimisho -20Niliwahi kurudi pale mahakamani, baada ya kupokea huo mzigo tulioagiza toka nje, zilikuwa bidhaa za kibiashara. Ingawaje kila biashara niliyowahi kufanya nilikuwa sifanikiwi. Na nilipoupokea huo mziga na kuhakikisha umefika seehmu yake, niliharakisha kurudu mhakamani.

Nilipofika mlango wa chumba kunapoafanyika hayo mahojiano,nilisikia jina langu likitajwa, nikawa na wasiwasi, maana sikujua kwanini jina langu litajwe, nikaharakisha kuingia ndani, ili nimuone huyo aliyenitaja, nilipofungua mlango na kuingia ndani, nilikuta yule mwanadada, rafiki yake  mke wa wakili mkuu akiwa bado anaendeela na maelezo yake.

Niliingia na kukaa sehemu yangu, na nikawa na hamu sana ya kutaka kujua kwanini jina langu lilitajwa, lakini kwa muda ule sikuweza kumuuliza yoyote, kwani kila mmoja alikuwa katega masikio akimskiliza huyo mwanadada , nikamtupia jicho yule mwanadada, ambaye bado alikuwa akiongea na wakati huo alikuwa akiulizwa maswali na wakili mwanadada.

‘Umesema ulipoteza fahamu, na ulipozindukana Kimwana alikuwa hayupo, ukasema alikuwa kakimbia, na aliyekuwa akikuhudumia na Sokoti, yeye alijuaje kuwa umepoteza fahamu?’ akaulizwa.

‘Huyo Sokoti alisema kuwa alipgiwa simu, na mmoja wa walinzi wa hapo na haraka alikuja na kuhakikisha napata matibabu ya haraka, na baada ya tukio hilo nikawa mbali kabisa na Kimwana, na hata mahudhirio yake darsani yalikuwa yanapungua, na baadaye nilisikia keshaolewa na pia anafanya kazi, kwenye kampuni moja.  ….

‘Uliambiwa kaolewa na huyo huyo mtu wako?’ akaulizwa.

‘Wengi niliowauliza walikuwa a shaka, lakini baadaye niligundua kuwa kweli kaolewa na huyo mtu niliyekuwa nikitamfuta…’akasema huyo mwanadada, na kuonyesha uso wa huzuni.

Nikawa nateseka moyoni, na sikujua nini nifanye, …kwani licha ya kuwa sikuwa na mwasilino na huyo mtu na…sikuwa na uhakika kuwa kweli bado ananipenda, lakini sikupenda mtu amadhuru, niliona kama vile mimi ndiye ninayefanyiwa hivyo. Nikiwa nahangaika huku na kule, ili angalau nikutae na huyo jamaa, ndio nikaja kukutana na mke wa wakili mkuu.

Na kama alivyoelezea jinsi gani tulivyokutana, na bahati nzuri, kumbe na yeye alikuwa na mataizo yake, na yote yanamlenga Kimwana, na katika kujuana kwetu, ndipo akaja na wazo hilo, la kuhakikisha kuwa tunamuondoa huyu mtu maana ni sumu kwa ndoa za watu.

Kwa kweli wazo hilo nililipokea kwa haraka sana bila kujali madhara yake ya baadaye,ingwaje mara kwa mara nilikuwa nikijiuliza ni kitatokea na jinsi gani ya kujihami na hilo tulilodhamiria kulifanya. Hata hivyo, moyo wangu ulishaingia sumu, sumu ya unyama…nilijiukua na mimi nikiwa na hasira, na chuki , na wivu uliopindukia dhidi ya huyo mwanadada, …

Kama hata wewe ungelikutana naye ukasikia kauli yake, ungelipandwa na hasira maana kauli anayotoa mdomoni, inakera, inawafanya wale waliopo kwenye ndoa zao kuwa hawajui majukumu yao, na yeye ndiye mjuzi, na aheri angelikuwa na nia njema, lakini yeye alikuwa kadhamiria mabaya katika ndoa za watu, kuharibu na kufisidi kabisa. Na sikupenda hilo, ….nikamkubalia mke wa wakili mkuu wazo lake, nikiwa na dhamira ya kweli,na hasa pale aliponisimulia masahibu yake,…

`Basi yeye akaahidi kuwa atapata hiyo silaha…..’Alipofika hapo hakimu akaangalia saa yake na kusema kuwa muda umekwisha anaona ni bora maelezo mengine yasubiri kesho yake, na akasisitiza kuwa sote tuwepo kwani tupo kwenye kiapo cha uaminifu kuwa hakuna hata mmoja atayekosa kwenye hayo mahojiano.

                                                          *******

‘Hebu niambie maana nilipofika hapo mahakamani nikiwa nimetokea bandarini nikasikia jina langu likitajwa, na nahisi aliyelitaja jina langu ni huyo mwanadada aliyekuwa akiongea, kwanini kanitaja, ana nijua wapi mimi…..?’ nikamuuliza.

‘Ina maana tangu aanze kuongea, hadi sasa hujamjua ni nani?’ akaniuliza.

‘Ningelijua nisingelikuuliza,…na kama ujuavyo, sikuwepo wakati anaongea,….ndio kusemaukweli mara nyingine nahisi kuwa ni mtu fulani, lakini huyo ninayemuhisi kuwa ni yeye hafanani nahuyo mwanadada rafiki wa mke wa wakili mkuu, na huyo ninayemjua mimi najua yupo huko Kenya na huenda keshaolewa ,….’nikasema.

‘Huyo unayemuhisi ni nani, au ndiye yule mchumba wako wa utotoni..?’ akaniuliza

‘Huwa mara nyingine kutokana na maelezo yake, namlinganisha na huyo mchumba wangu wa utotoni, lakini sizani kama ni yeye, maana ni muda mrefu atakuwa keshaolewa na huenda ana watoto ….’nikamwambia.

‘Kwanini unahisi hivyo, kuwa huenda ni yeye, au huenda sio yeye? Akaniuliza.

‘Kwasababu yule msichana, nilikuwa namfahamu sana, haiwezekani abadilike kiasi hicho, na kama ingelikuwa ni yeye angeshaniambia, maana tulikuwa tunapendana sana, ….’nikasema.

‘Kwa mara ya mwisho mliachana naye akiwa na umri gani?’ akaniuliza.

‘Alikuwa mdogo,msichana mdogo tu…’nikasema nikijaribu kukumbuka sura yake ya usichana.

‘Na mlikuwa hamuwasilini naye tena?’ akaniuliza.

‘Hatukuweza kuwasiliana naye tena, maana kwa mara ya mwisho kuachana naye, ilikuwa baada ya kunifumania na msichana mmoja wa kule kijijini, alikuwa kakasirika sana,…..na licha ya kujitahidi kutafuta mawasiliano naye, lakini sikuweza kupata anuani yake, na hata wazazi wangu hawakujua wapi ninaweza kupata hayo mawasiliano na yeye, kwani wao hawakuwa na upendeleo na huyo msichana na familia yao.

Na kwa kupindi hicho nilijifanya kama sijali, na siku nilipokwenda kijijini kutafuta mke wa kuoa, niliomba kama inawezekana nikutane naye, na kila msichana niliyekutana naye nilimlinganisha na  huyo msichana na ndio maana sikuweza kupata msichana kwa anayenifaa zaidi ya yule msichana wa kijijini, ambaye nilimuoa kwasababu ya huruma ….

‘Ina maana hakuna jambo ambalo linaweza kukumbusha kuhusu yeye, hakuna kitu kwenye mwili wake ambacho kinaweza kukukumbusha kuwa ni yeye, ….?akaniuliza.

‘Siwezi kukumbuka, zaidi ya sura yake ya utotoni,… maana ndio tulikuwa karibu sana naye, lakini kwa muda ule sikuwa na wazo la kumchunguza maumbile yake ya mwilini, kwani ukumbuke licha ya utundu wangu kwa wasichana, lakini huyo , yeye nilimuheshimu sana, na nilikuwa nikisema moyonu, huyo ni mke wangu, na siku ya kuujua mwili wake ni hapo tutakapofunga ndoa,….lakini mmmh, labda macho yake…..na ..na….’nikasita.

‘Na na..nini?’ akaniuliza.

‘Huyu mwanadada nikimwangalia naona nahisi macho yake,yanafanana sana na yeye, lakini hata hivyo sijapata mwanya wa kumwangalia vyema, na kila mara tukiangaliana inakuwa kama vile namjua na inakuwa kama vile kuna hisia za namna ya ajabu…..’nikasema.

‘Hisia kama zipi?’akaniuliza.

‘Siwezi kuzielezea vyema, lakini nahisi moyo wangu ukienda mbio..na nashikwa na kitu kama ganzi, unajikuta unamwangalia bila kupepesa macho,……’nikasita kuendelea.

‘Ni hisia za kupenda,…usijifanye hujui wewe ni mtu mzima bwana, na unasema hujapata muda wa kumwangali, na sasa unasema ukimwangalia, unataka kumwangalia kwa vipi ili umjue vyema…..’akaniambia.

‘Unaweza kuziita hivyo..hisia za kupenda, lakini mbona ninakuwa mwoga….nahisi kama vile mimi ni mkosaji, au nikisema lolote kwake anaweza aka…..nahisi kama nitapata maneno ya mbaya..yaani sielewi, …nahitaji muda wa kumwangalia kwa makini, maana muda ninaoangaliana na yeye, unakuwa kama mtu aliyepigwa na ganzi, na akili inakuwa haifanyi kazi vyema….’nikasema.

‘Labda kwa vile unahisi ni huyo msichana wa kijijini na unaogopa kuwa ulimkosea ndio maaa unamuogopa?’akaniuliza kama vile anaongea.

‘Hapana sio hivyo….ila kila nikimuona nahisi moyo ukinienda mbio,nakuwa na wasiwasi sana,nakuwa sijielewi, kwahiyo, aah, sijui nikuambie nini…..’nikamwambia.

‘Usijali yote hayo yataisha,…na kama kweli mnapendana basi mambo yataenda shwari…’akaniambia huyu mwanadada wakili.

‘Lakini wewe inaonekana unamjua vyema huyo mwanadada, hakuwahi kukugusia kuwa yeye ni nani na anaotoka wapi?’ nikamuuliza.

‘Wewe ndiye mwenye shida naye, na wewe ndiye uliyewahi kuishi naye, kwahiyo kama ni yeye ingelikuwa ni rahisi kwako kumjua , mimi siwezi nikahakikisha moja kwa moja kuwa ni yeye, kwani wapo wengi walishajifanya kuwa wao ni watu fulani, na kumbe sio, lengo lao ni kupata kile wakitakacho. Cha muhumu ni tususbiri kwanza, tutamsimamisha tena tutamuhoji, na mwisho wa siku ukweli utajulikana…’akasema huyo mwanadada wakili.

‘Kwa maelezo yao yeye na mke wa wakili inaonyesha ndio waliomuua Kimwana, ….huoni kuwa bado kuna safari ndefu ya kujuana na huyo mwanadada, maana kama wameua mwisho wao ni jela, au sio?’ nikamuuliza , na yeye akanianglai na kutabasamu, akasema;

‘Ukweli wa yote utagundulika ndani ya mahakama, kama wao ndio wameua, sheria ipo wazi, na mwenye mamlaka hayo na msimamizi wa sheria ni hakimu, ndio maana tumemuita yeye, na yeye atatushauri nini kifanyike, hatukutaka kesi hii tuikimbizie ndani ya mahakama kwanza, tuliona tuiweke kinamna hiyo kwanza, ili kama kuna uwezekano fulani, hawo wenye makosa waangaliwe kwa jicho la huruma….’akasema.

‘Hilo kweli sizani kama linawezekana, ukiua upo hatiani, hata kama ni kwa bahati mbaya,….utasikia unahukumia miaka thelathini, au kumi, kwa kosa la kuua bila ukusudia, …na kwa maelezo yao, hawakuua kwa bahati mbaya walidhamiria kabisa….sababu ya wivu, na kutaka kulipiza kisasi….’nikasema na yeye akaniangalia kwa makini na kusema.

‘Usiwe na shaka, na usikimbilie huko, hatuna uhakika bado kuwa ni wao walioua, bado hatujafikia hatua hiyo,…..kama ni wao tutaona, na kama kuna mtu mwingine tutamsikia, wewe vuta subira….’akaniambia.
‘Na nilikuwa na ombi moja….’nikasema

‘Ombi gani,…?’ akaniuliza.

‘Naomba nionane na huyo mwanadada rafiki wa mke wa wakiliki mkuu,….nataka niongee naye, nimuhoji mwenyewe nimjue kuwa yeye ni nani….’nikasema.

Wakili mwanadada akaniangalia kwa makini, kwa yale macho yake ya kawaida na baadaye akageuka kuangalia dirishani, halafu baadaye akanigeukia na kusema;

‘Kwanini uniombe mimi, ..yeye sio mfungwa, na wala hana mume, kusema kuwa atamzuia, ni wewe mwenyewe kwa juhudi zako kwenda kumuomba yeye na muongee, kwani unamuogopa, …wewe unajulikana na kiwembe, mtaalamu wa wanawake,..au sasa unajifanay kwangu, kuwa huna tabia hiyo….au unataka niwe mshenga wako, …?.’akasema.

‘Mhh, mengine wananipakazia tu, hiyo tabia ilikuwa ya ujanani, sio sasa. Na hata hivyo wewe ni wakili wangu ingawaje sina pesa za kukulipa, ningelifurahi, ukawa mtu wa kati, kati yangu mimi na yeye, lakini ni yeye, na kama sio huyo ninaye mzania, basi , sina haja ya kuhangaika naye, safari hii sitaki kufanya makosa tena , ……’nikatulia huku nikiwaza.

‘Je kama ni yeye unataka ufanye nini na yeye..?’ akaniuliza.

‘Nitamuomba tufunge naye ndoa,..,’nikasema huku nikiwa naangali juu.

‘Sawa,…yule kule anakuja na rafiki yake, unataka muongee naye sasa hivi?’ akaniuliza, na nikageuka na kujikuta tukiwa tunaangaliana, …..

********

NB Kwa leo tuishie hapo, tukitafakari hayo yaliyoongelewa na wahusika wa kisa hiki, je ni nini kitafuta , tuombe mungu tukijaliwa tena!

WAZO LA LEO: Kila mtu anapenda kupata maisha bora,… lakini kupenda huko kusiwe zaidi ya kipato chetu, ni bora tukajenga tabia ya kurizika, na kile tulicho nacho na kama tunapenda kupata zaidi basi tujitahidi zaidi katika kazi zetu biashara zetu,…bila kuvuka mipaka.tukumbuke kuwa tamaa ni mbaya, na asiyetosehaka na kidogo alicho nacho hata akipata kingi hatatosheka.

Ni mimi: emu-three

4 comments :

EDNA said...

Jirani umesalimika wewe? Siku njema pamoja na familia yako.

emu-three said...

Jirani yangu Edna, nimesalimika namshukuru mungu , wasi juu yako mpendwa wangu!

Rachel siwa Isaac said...

Ndugu wa mimi kazi inazidi kusonga zaidi na zaidi, kwangu ni furaha sana.

Mungu azidi kukubariki sana.
Pamoja Daima ndugu wa mimi!!!!!!1

emu-three said...

Ndugu wa mimi tupo pamoja sana, ubarikiwe na mambo yako yabarikiwe pia!