Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Monday, December 2, 2013

Mkuki ni kwa Nguruwe-38



‘Sawa kama hutaki kuniambai huo ukweli, mimi bado nalifuatilia hilo, kama nitagundua kuwa unafahamu au unahusika kwa hilo, kwa namna yoyote ile, basi, mimi na wewe hatutakuwa marafiki tena,tutakuwa kinyume chake,...’ nakumbuka nilimwambia shemeji yangu hivyo, niliwaza sana kauli hii niliyomwambia shemeji yangu, na moyoni nikifahamu kuwa sio yeye peke yake, ambaye, alikuwa rafiki  yangu nikimwamini, nikajitoa kwa hali na mali juu yao, nikijua nafanya hivyo kwa rafiki kumbe najidanganya mwenyewe, ...sio yeye peke yake, kumbe wapo wengi, lakini mmoja baada ya mwingine, nitamuonyesha kuwa unafiki hauna mwisho mwema.

‘Huo unafiki wao, wa kujionyesha kuwa ni marafiki zangu, sasa utawaumbua kwani utakuwa sio urafiki bali ni uadui...’nikasema kimoyo moyo.

Niliichukua ile laptop yangu, na kuhakikisha nimeificha mahali ambapo hakuna anayeweza kuiona, na ni baada ya kuiweka hiyo kumbukumbu yangu muhimu, hewani kwenye mtandao wenye kifungo, kuwa ninaweza kuifungua popote mwenyewe kwa ufunguo wangu,  na kwa hiyo hata kama hiyo laptop yangu ikatokea kuibiwa au kuharibika, bado nitaweza kuwa na huo ushahidi, kwani upo kwenye mtandao wa kudumu.

‘Ahsante sana shemeji....japokuwa ulijitahidi kunificha, kwa kuwajali wale uliowaona ni muhimu kwako, sasa tuone kama wataweza kukusaidia...’nikasema kimoyo moyo.

Kwakweli baada ya kupata ushahidi huo, moyo wangu uliingiwa na kiwingu kizito, nikajawa na ujasiri, nikijua kuwa hilo ninalokwenda kulifanya nalifanya kwa nikiwa sahihi, kwani sio mimi niliyeanza, kwani mimi nilitimiza wajibu wangu, nikajitolea kadri ya uwezo wangu, wao, ndio walionisaliti, hata pale nilipowapenda na kuwasaidia kama ndugu zangu, ..yaani,hata mume wangu...siamini.

Sikutarajia kuwa mambo mengi yaliyotendeka, yalikuwa yamepangwa, na ilisubiriwa tu, kutokee tukio kama kichochezi, ...sikutarajia kuwa wanadamu wanaweza kuwa na hali hiyo, wawe ni marafiki kwa upande mmoja na huku upande wa pili wanatafuta njia ya kuhakikisha unaharibikiwa, unapoteza kil kitu,...wanakuchuna, kwa nia tu ya kukufanya wewe uwe ni ngazi yao ya kufika huko wanakotaka, na kukipata hicho wanachokitaka huku wakikubeza, na kukudharau....

Kumbe ndivyo watu walivyo eeh, unaweza ukamwamini mtu, hata kumweka kwenye nafasi ya ndugu, mpenzi, mume au mke, ukamsaidia, mkaishi pamoja, kumbe moyoni mwa mwenzako haupo kabisa, kumbe mwenzako  ana malengo mengine kabisa...anasubiria tu kupatikane kisingizio....
Nilipowaza hivyo nikaona nihakikishe kwa mara ya mwisho,...na kuhakikisha kuwa kile nilichokigundua ni kweli, hapo nikainua simu na kumpigia rafiki yangu,....

Endelea na kisa chetu.........

***************
N...SOMA TOLEO JIPIA.


WAZO LA LEO: Mara nyingi ni rahisi kuona mambo ya wenzetu, kuliko mambo yetu,ni mara nyingi tunaweza kuona dhambi za wengine kuliko za kwetu, hata tukafikia kunyosha kidole, na kulaumu, kusuta hata kukejeli, tukasahau kuwa makosa yetu , dhambi zetu ni zaidi ya hizo za unayemnyoshea kidole. 

Matatizo ya mke na mume yanatatutuliwa na mke na mume, matatizo ya familia yanatatuliwa na wanafamilia wenyewe, nk, ni vyema,tukajaribu kutumie hekima, katika kuingilia maswala hayo, ni tufanye hivyo kama wenyewe wanataka tufenye hivyo,...

Ni mimi: emu-three

2 comments :

Yasinta Ngonyani said...

Nimependa sehemu hii imenikumbusha na imenigusa kwa namna fulani ...pamoja daima.

emuthree said...

Nashkuru sana kusikia hivyo ndugu wangu @Yasinta, kisa chetu kinagusa maisha yetu ya kila siku,TUPO PAMOJA