‘Sawa kama hutaki kuniambai huo ukweli, mimi bado
nalifuatilia hilo, kama nitagundua kuwa unafahamu au unahusika kwa hilo, kwa
namna yoyote ile, basi, mimi na wewe hatutakuwa marafiki tena,tutakuwa kinyume
chake,...’ nakumbuka nilimwambia shemeji yangu hivyo, niliwaza sana kauli hii
niliyomwambia shemeji yangu, na moyoni nikifahamu kuwa sio yeye peke yake,
ambaye, alikuwa rafiki yangu
nikimwamini, nikajitoa kwa hali na mali juu yao, nikijua nafanya hivyo kwa
rafiki kumbe najidanganya mwenyewe, ...sio yeye peke yake, kumbe wapo wengi,
lakini mmoja baada ya mwingine, nitamuonyesha kuwa unafiki hauna mwisho mwema.
‘Huo unafiki wao, wa kujionyesha kuwa ni marafiki zangu,
sasa utawaumbua kwani utakuwa sio urafiki bali ni uadui...’nikasema kimoyo
moyo.
Niliichukua ile laptop yangu, na kuhakikisha nimeificha
mahali ambapo hakuna anayeweza kuiona, na ni baada ya kuiweka hiyo kumbukumbu
yangu muhimu, hewani kwenye mtandao wenye kifungo, kuwa ninaweza kuifungua
popote mwenyewe kwa ufunguo wangu, na
kwa hiyo hata kama hiyo laptop yangu ikatokea kuibiwa au kuharibika, bado nitaweza
kuwa na huo ushahidi, kwani upo kwenye mtandao wa kudumu.
‘Ahsante sana shemeji....japokuwa ulijitahidi kunificha, kwa
kuwajali wale uliowaona ni muhimu kwako, sasa tuone kama wataweza kukusaidia...’nikasema
kimoyo moyo.
Kwakweli baada ya kupata ushahidi huo, moyo wangu uliingiwa
na kiwingu kizito, nikajawa na ujasiri, nikijua kuwa hilo ninalokwenda
kulifanya nalifanya kwa nikiwa sahihi, kwani sio mimi niliyeanza, kwani mimi
nilitimiza wajibu wangu, nikajitolea kadri ya uwezo wangu, wao, ndio
walionisaliti, hata pale nilipowapenda na kuwasaidia kama ndugu zangu, ..yaani,hata
mume wangu...siamini.
Sikutarajia kuwa mambo mengi yaliyotendeka, yalikuwa
yamepangwa, na ilisubiriwa tu, kutokee tukio kama kichochezi, ...sikutarajia
kuwa wanadamu wanaweza kuwa na hali hiyo, wawe ni marafiki kwa upande mmoja na
huku upande wa pili wanatafuta njia ya kuhakikisha unaharibikiwa, unapoteza kil
kitu,...wanakuchuna, kwa nia tu ya kukufanya wewe uwe ni ngazi yao ya kufika
huko wanakotaka, na kukipata hicho wanachokitaka huku wakikubeza, na
kukudharau....
Kumbe ndivyo watu walivyo eeh, unaweza ukamwamini mtu, hata
kumweka kwenye nafasi ya ndugu, mpenzi, mume au mke, ukamsaidia, mkaishi
pamoja, kumbe moyoni mwa mwenzako haupo kabisa, kumbe mwenzako ana malengo mengine kabisa...anasubiria tu
kupatikane kisingizio....
Nilipowaza hivyo nikaona nihakikishe kwa mara ya
mwisho,...na kuhakikisha kuwa kile nilichokigundua ni kweli, hapo nikainua simu
na kumpigia rafiki yangu,....
Endelea na kisa chetu.........
***************
N...SOMA TOLEO JIPIA.
WAZO LA LEO: Mara
nyingi ni rahisi kuona mambo ya wenzetu, kuliko mambo yetu,ni mara nyingi
tunaweza kuona dhambi za wengine kuliko za kwetu, hata tukafikia kunyosha
kidole, na kulaumu, kusuta hata kukejeli, tukasahau kuwa makosa yetu , dhambi
zetu ni zaidi ya hizo za unayemnyoshea kidole.
Matatizo ya mke na mume
yanatatutuliwa na mke na mume, matatizo ya familia yanatatuliwa na wanafamilia
wenyewe, nk, ni vyema,tukajaribu kutumie hekima, katika kuingilia maswala hayo,
ni tufanye hivyo kama wenyewe wanataka tufenye hivyo,...
Ni mimi:
emu-three
2 comments :
Nimependa sehemu hii imenikumbusha na imenigusa kwa namna fulani ...pamoja daima.
Nashkuru sana kusikia hivyo ndugu wangu @Yasinta, kisa chetu kinagusa maisha yetu ya kila siku,TUPO PAMOJA
Post a Comment