Utangulizi
wa kisa kipya-MKUKI NI KWA NGURUWE...kwa binadamu je?
Wakati tunamalizia kisa chetu cha
wema hauozi, nilitarajia
kupata maoni mbali mbali kwa wasomaji, lakini haijatokea hivyo, natumai wengi tunasoma
kimiya kimiya, na kutafakari ujumbe uliopo ndani yake,ujumbe ambao unaifaa
sana jamii yetu, ambayo sasa hivi
inaamini sana mambo ya kishirikina, sio vijijini tu, hata huku mjini. Ni jukumu
letu kuupeleka huu ujumbe kwa kila atakayejaliwa , na kwa vile siku hizi simu
zinaweza kuwepo mitandao, basi kazi hii itakuwa
rahisi zaidi.
Kwenye mtandao wa kijamii wa
facebook, kuna kisa
tunakiendeleza cha `mkuki kwa nguruwe...’ kisa hicho tutakifanyia marekebisho
na kukiweka hapa kwenye blog, kwani hapa ndipo kwenye maktaba yetu , hapa ndio
nyumbani, na kwa siku zijazo, tukijaliwa tunaweza kutumia maktaba hii kwa ajili
ya kutunga vitabu. ..hata e-books, kama tutapata wafadhili.
Kisa hicho cha mkuki kwa nguruwe kinaelezea udhaifu wetu wa
kibinadamu ambao huangalia zaidi nafsi zetu, bila kujali athari hiyo kwa
wengine. Unaweza ukatoa ushauri kwa wengine, ukiwa na nia njema, bila kufikiri
zaidi, ukijua kuwa akitenda uliyemshauri,atafanikiwa, na wewe utapata faida
fulani, au sifa fulani, lakini ukasahau kuwa huyo atakayetendewa na huyo
uliyemshauri, ataumia sawa sawa na wewe, kama ungelitendewa wewe...wewe hukujali hilo kwa muda huo, kwani
ulikuwa mkuki kwa nguruwe.
Yamungu ni mengi, mwenyezimungu anafahamu vyema kuliko sisi,
na kila jambo hutokea kwasababu fulani. Kwahiyo huenda ule ushauri ulioutoa kwa
mwenzako kuwa akatende jambo, kwa wengine, ili kufanikiwa jambo fulani, huyo
uliyemshauri akaja kulitenda hilo kwenye anga zako, na zile athari ambazo
ulitegemea hazitakugusa wewe zikaja kwako, zikakugusa wewe, mkuki ukageukia
kwako...
Inauma sana ...kusalitiwa, inauma sana mwenzako mumeo au
mkeo kuwa na mahusiano nje ya ndoa, sasa inakuwaje wewe umshauri rafiki yako
akatende hivyo kwa wenzako, eti ili apate mtoto, kwa vile hajaolewa, na umri
umekwenda sana,...na mbaya zaidi unamshauri akatende hata kwa mume wa mtu,
...je kama umemshauri akatembee na mume wa mtu, akija kutembea kwa mume wako
utajisikiaje..
Hayo utayapata kwenye kisa hicho cha `mkuki kwa nguruwe,...’
kwasasa kipo kwenye facebook, lakini huko tumekifinya sana, hapa ndipo mahali
pa kukiongelea kwa uwazai zaidi. Je ilikuwaje, na ikawaje na itakuwaje...tuwe
pamoja kwenye kisa hicho kipya.
Nawashukuru sana wafanyakazi wenzangu walionisaidia kukipata
hicho kisa, na nafahamu na wewe unacho kisa chako chenye mafundisho, kwanini
usikilete hapa kikasaidia jamii.Kuna baadhi wameanza kuniletea visa vyao, navifanyia kazi, wakati mwingine kisa kimoja kinaweza kumeza visa vingine, ...soma utaona kisa chako kikwa ndani ya kisa kingine, na ujumbe ukawa ni ule ule, ...tunashukuru sana, kwa moyo wenu huo,kwani ukiwa na jambo ukabaki nalo ni hasara, lakini ukilitoa kwa wenzako wakapata fadia ni akiba yako...ni fadia kwako...
Shukurani....na ahsanteni sana.
Ni mimi:
emu-three
2 comments :
NImesoma utanguliza na nasubiri kwa hamu nyingiiii sanaaaa..Kama hulivyosema ni kweli kama wengi wangekuwa wanasoma hivi visa vingewapa faidi wingi sana nina imani muda si mchache wengi watasoma na kufaidika.
HIKI KISA KINAELEKEA KITAKUWA KITAMU KAMA WEMA HAUOZI. NI KWELI TUPU HAYO ULOSEMA. HASA SISI WANAWAKE TUNADANGANYANA SANA UMRI UKIWA UMEENDA NA WENGI WAKIONA UMRI UMEENDA ANAMTAFUTA MUME WA MTU KWA UDI NA UVUMBA ILI AZAE NAE. JAMANI HII NI HATARI. RIDHIKA NA ULICHO NACHO.
Post a Comment