Sherehe fupi ikaandaliwa, na wote waliohusika katika familia
hiyo, majirani na baadhi ya wanakijiji mbali mbali walihudhuria,.na wageni
rasmi wakawa watetezi muhimu wa kesi hiyo, mwanadada na mwanasheria na familia
zao. Watu wawili hawo mwanadada na mwanasheria walikuwa kivutio kikubwa kwa
wengi na kila mmoja alitaka kuwaona.
Ilipofika muda wao wa kuongea, alisimama mshehereshaji wa
sherehe, na kutoa utaratibu wa shughuli nzima, na baadaye akamuomba baba wa
mwanadada kukaribisha wageni na kueelzea dhumuni la shughuli hiyo, na
alipomaliza, kukawa na burudani kidogo, halafu mshehereshaji akamkaribisha tena
baba wa familia , kutoa hizo shukurani
zake kwa niaba ya ya familia, kwani ndio dhumuni hasa la shughuli hiyo, na
alipomaliza akakaribishwa mama naye akatoa shukurani zake,
Mwanamama hakuwa muongeaji, japokuwa alikuwa kwenye kundi la
kushukuru, lakini yeye aliomba asiongee kabisa, akawa msikilizaji, nay eye
alikuwa kakaa pembeni ya wazazi wake na pemebeni yake alikaa mtoto wake, akiwa
makini kuona ni kitu gani kinaendelea kama ujuavyo watoto, wanakuwa amkini sana
katika shughuli kama hizo na kuhifadhi tukio hilo kwenye ubongo wake.
Baadaye ikaja nafasi ya wageni muhumi kuongea, na aliyepwa anfasi hiyo kwa niaba alikuwa mwanasheria,
na kama wanavyomuita mbunge mtarajiwa, akaona atumie muda huo kujinadi, na watu
wakawa wakimshangilia, akasimama kwa
tambo,kwanza aliwaangalia watu, halafu akageuka kule walipokuwa wamekaa
mwanamama, halafu akamwangalia mwanadada aliyekuwa kakaa karibu yake, halafu
halafu akaanza kuongea;
‘Wandugu zanguni, nafahamu nyote mumeona yaliyotokea, hakuna
haja ya kuelezea zaidi, kwani kila mmoja alikuwa ni shuhuda wa hayo yote, na
hayo yaliyotokea hayakutokea tu, kwasababu watu walipanga iwe hivyo,...ndio
kuna waliopanga, wakijua wao wana uwezo huo, wakafanya waliyofanya na kuumiza
wengine.
Nichukue muda huu kuwaombea wale waliotangulia mbele za haki kutokana
na hili, hawa tutawatambua kama wapiganaji, ...mashujaa wa kijiji, mungu walaze
mahali pema peponi...’watu wakaitikia `amiiiiini’.
Lakini kila kunapotokea tukio, kwa wenye akili na hekima,
wanaliweka tukio hilo kwenye kumbukumbu zao,na kulitafakari kwa mapana yake,
..ukiangalia matukio hayatokei tu, yana
sababu, na sababu hizo ni vyema tukajifunza kwayo, na ...na hili lilitokea hapa
kijijini kwetu,sote tupate fundisho, na
kwa ujumla ninaweza kusema tatizo kubwa lililofanya haya kufika hapa ni adui
ujinga,na huyu tusipojitahidi kumshinda, tutakuwa tukitwanga maji kwenye kinu.
‘Naomba tujipange kama jamii, tukianzia kwenye familia,
..kila mmoja afahamu kuwa adui huyu ni mbaya, na yupo ndani kwake,..., na ili
tufanikiwe hili tuweke viongozi wenye upeo mpana,sio lazima wawe wasomi sana,
lakini ningelishauri tuwatafute wasomi wataalamu kwa ajili ya kuwasaidia
viongozi wetu katika kijiji chetu.
‘Mimi nilikuwa nashauri sana, watu hawo wawe ni wazawa wenye
uchungu na eneo hili, ....tusipotafuta wazalendo, ambao watakuwa na uchungu wa
eneo letu hili, tutaishia kuona mali asili yetu ikihamishwa usiku na mcahana na
kudanganywa kuwa ni mchanga unaokwenda kufanyiwa utafiti, na mwisho wa wote
tutabakiwa na ardhi isiyo na thamani , tutabakiwa na mahandaki..yaliyojaa chatu
na wadudu wabaya...
‘Pamoja na kuwa tumemfunga mtaalamu lakini kwa namna moja au
nyingina nampa nafasi yake kama mtetezi mzuri wa kijiji chetu, japokuwa yeye
alitumia njia ya ubinafsi, akaweka, umimi mbele, na hilo ni tatizo jingine
ambalo tunatakiwa tupambane nalo, kama kijiji, kama jamii, tunatakiwa
tushirikiane kwa maendeleo ya kijiji chetu.
‘Kama unaona kuna jambo la kufanyika kwa masilahi ya kijiji,
liwekeni wazi, na viongozi walifanyie kazi...
‘Na jingina ambalo linatokana na adui ujinga ni imani za
kishirikina,...jamani hivi katika karne hii bado tunatawalia na imani hizo,
....wenzetu wanahangaika kwenda kwenye mwezi kwa mashine, sisi tunahangaika
kwenda huko kwa kuota, kwa kishirikina, kwenye giza, tukiwa uchi....’watu
wakacheka.
‘Kama basi inafaa hivyo, kuwa mtu anaweza kusafiri na ungo,
kwanini ifanyike usiku na mkiwa uchi, boresheni basi ili uwe usafiri ulio
tambulikana,..lakini kwa sababu ya adui ujinga tunaendeleza hayo, tunajenga
chuki, tunauwana...wivu, usio na tija, hatutafika kwa mtindo huo.
‘Jamani tuamuke, wenzetu walishaamuka zamani, wakatoka, na
kuanza kuchapakazi, sisi bado tumelala, tunakoroma, huku tunalalama , njaa,
shida, umasikini..je hayo yatakuja tukiwa tumelala...kwahiyo tuachane na imani
potofu za kishirikina, hizo ndio zimekichafua kijiji chetu na kuwa kijiji
chenye sifa mbaya...
‘Kijiji chetu kimejulikana sana, kila mahali wanakiongelea,
lakini kimejulikana kama kijiji cha wachawi, kinachoua wazee , kinachoa watu
wenye matatizo ya ngozi..kinachowanyanyasa wanawake, na mengine mengi mabaya,
hebu tujiulize haya yote yametusaidia nini, kama sio kutengwa na jamii, kama
sio chuki, visasi na mauaji ya kila siku. Tuyaache hayo, kwani haya ni tabia za
kishetani, na sisi ni wanadamu , sisi sio mashetani, sisi sio
Ibilisi...’akasema na watu wakacheka kidogo.
‘Napenda kuchukua nafasi kutangaza jambo kubwa muhimu, na
nimechukua muda sana kulitafakari japokuwa ni swala la kifamilia zaidi, lakini
hapa tupo familia, japokuwa kuna waalikwa, ...lakini wote lengo letu ni
moja....sina budu kulifanya hili hapa kwa nia njema kabisa.
‘Moyoni, kiujumla nasema mbele yenu kila mtu alisikie, kuwa
mimi natarajia kuoa, nafahamu jamii, wanandugu wamekuwa wakinisakama kwa hilo,
na wakati nakabidhiwa majukumu ya kuwa kiongozi wa familia nilipingwa sana na
ndugu zangu, na wanajamii wengine, wakiumia hilo kuwa mimi sijao, kwahiyo
sistahili kuwa kiongozi wa familia yetu. Na ndio maana mpaka leo
sijatambulishwa rasimi kama kiongozi wa familia yetu, mpaka niwe nimeoa,..na
sasa nataka hili likamilike wiki hii....’akasema na watu wakapiga makofi na
kumshangilia
‘Hata ikiwezekana leo...’akasema pale aliponong’onezwa kitu
na mwanadada, na watu wakashanglia kwa vifijo na vigelegele
‘Mila zetu zinatupendelea sana wanume...’hapo akina mama
wakacheka na kusema;
‘Sema baba..’
‘Nasema hivi sio kwa vile nataka kura zenu nikigombea
ubunge.....’akasema na akina mama wakadakia na kusema;
‘Kura zetu zote utachukua wewe baba..sema ...’
‘Wanaume tunapendelewa sana, maana unaweza kuoa mke zaidi ya
mmoja, eti pia unaweza ukarithi mke hata bila kutoa mhari,..mmh, jamani kwani
mhari ni ya nani,....si ya mke, na umempata mke, kwanini usitoe mahari, eti kwa
vile alishatoa ndugu yako ambaye ni marehemu...sijui, labda wazee wetu wanajua
zaidi.
‘Lkini nia yangu si kupingana na haya,...kwani wazee wetu
walikuwa na hekima yao, ila karne zinatofautiana, tukubali maabdiliko, yale
yenye kulete tija,..maana unapomrithi mwanamke, unakuwa kama umemlazimisha, au
sio jamani....?’ akauliza na watu wkacheka, na wengine wakaguna.
‘Inawezekana, kuwa ni sehemu ya kumliwaza mjane, inawezekana
ikawa ni sehemu ya kumsaidia mjane na familia yake, lakini sasa , awe na uhuru
wa kuamua hilo, kuwa yupo tayari kuolewa tena, na apewe haki zake kwanza....sio
tutumie njia hiyo kwa ajili ya kuchukua haki zake, eti ili zisitoke nje, ya
familia....hilo ni tatizo...’akatulia na hapo watu walikaa kimiya.
‘Nasema tena, mimi sio mpingaji wa mila na desturi zenu,
...msije mkanielewa vibaya, ila pale tunapoweza kupaboresha, tupaboreshe, kwa
nia njema..., kila mtu anayo haki na uhuru wa kuamua, na kupanga ilimradi
sivunje sheria, na basi kwanini huyu mwanamama hatumpi uhuru huo, huyu
mjane,...sio mtu jamani...?’ akauliza
‘Ni mtu..’wakasema akina mama.
‘Sasa utakuta huyu mjane ana watoto, na watoto hawa
wanahitajia matunzo, kutoka kwa mali aliyoacha baba yao, mali hii inachukuliwa
na ndugu za mume wake, wanaanza kugawana, hakumbuki kuwa huyo ndugu yao
alihangaika kwa ajili ya hiyo familia, kama wao wanavyohangaika kwa ajili ya
familia zao, na utakuta ndugu huyu alikuwa akihangaika bega kwa bega na mkewe,
hakuna aliyekuwa akiwasaidia...
‘Sasa mume kaondoka, wanandugu wanamezea mate mali
zilizojasho lao, wanakuja kuchuma mali ya mayatima na wajane, wanashindwa kujua
kuwa leo ni kwa yule, kesho itakuwa zame yake...tuamuke na tuwe amkini, tupange
kwa busara na kwa hekima, haya mambo yanahitajika kuboreshwa...’akatulia
kidogo.
‘Mimi kama itatokea nikagombea ubunge, mimi kama kiongozi wa
familia, nikipewa huo wadhifa, hili tatizo nitajitahidi tulitatue na kuliweka
katima mstari utakaoleta tija.., lakini
pamoja na kusema hayo, nakubali kuwa kama kiongozi natakiwa nioe, kwahiyo mimi
kama kiongozi wenu mtarajiwa natakiwa kuonyesha mfano...wa kuoa, maana sina mke
ndio maana mumekuwa mkinisakama kwa hilo, na wengine hata kunishuku
vibaya,....mm, mimi ni mwanaume bwana...’watu wakacheka na kushangilia.
‘Sikatai kuoa, ....eti kwa vile ...wanasema sijiamini, kwanini
nisijiamini , mmh, mimi ni mwanaume, na
ni mwanaume kweli....’watu wakacheka na kumshangilia.
‘Lakini mimi kidogo nimefuta ujinga, naelewa njia na mipaka
yangu na ya wenzagu, siwezi kualmisha, kwani kuna maswala ya nafsi kupenda,
kupenda kwa mtu kunatofautiana, kwahiyo huwezi kulazimishana kuoa mtu ambaye hakupendi, ....nakiri kusema hata
hili swala la kurithi limepitwa na wakai,...
‘Mnielewe silipingi, lakini kuwe na makubaliano...kama
mumekubaliana, hakuna shida, inatakiwa kuwe na makubaliano kati ya wanandoa
hao,...tusilazimishane kwa hilo, kwangu mimi kama kiongozi wa damu mpya,
napendekeza hilo tuliangalie upya..’akasema na watu wakamshangilia kwa nguvu
sana.
‘Na kutokana na hilo ninaanza kwa vitendo, ...’akainua pete
mbili hewani.
**********
Mimi pale nilipokuwa nimekaa nilipoona zile pete mbili
nikajua moja ni yake na moja ni kwa ajili ya kumvalisha mwanadada, nikamgeukia
mwanadada, na kumbe na yeye alikuwa akinigeukia mimi tukajikuta tukitizamana,
akatabasamu, na mimi nikajilazimisha kutabasamu...
Mwanasheria huku akiendelea kumwaga sera, na watu
wakimshangilia, akaendelea kusema;
‘Mimi nawapenda sana wanawakei, nasema hili wote msikie, kama
ningelikwua na uwezo ningelioa wake wengi sana,....huenda ndio maana
nimechelewa kuoa, maana nitamuoa yupi, wakti kila nimuone nampenda,...sitanii,
..nawapenda wanawake wote...’akasema na akina mama wakashangilia kwa vifijo.
‘Lakini kuna utaratibu, huwezi kujifanya wewe ni mitume,
ambao waliweza kuoa wake wengi, na mababu zetu ambao walikuwa na uweo huo,
vizazi vyetu, havina nguvu kama walizokuwa mababu zetu,...siwezi kusema watu
kama hawo kwasasa hawapo , wapo wenye nguvu hizo, na ....hata mimi kidogo naona
nina nguvu hizo...’akasema na kumwangalia mwanadada.watu wakacheka.
‘Ndio maana leo hii nina pete mbili,...pete hizi ni wanawake
wawili, na wote nawapenda, nawapenda sana, kiasi kwamba nimefika mahali
nashindwa niamue yupi ni yupi, na kwasababu hiyo, nikaona hapana kwa vile mimi
ni miongoni mwa wanaume waliojaliwa,...sitanii hili....’watu wakacheka.
‘Basi nataka niwaoe wote wawili....’hapo ikawa ni kelele za
kushanglia na vigelegele.
‘Sitanii..nasema hili kutoka ndani ya nafsi yangu,..kwani
wote nawapenda, nikianzia hapa kwa mwenzangu aliyepo karibu karibu
yangu,...huyu anaitwa mwanadada, ni mchumba wangu wa siku nyingi, nampenda sana
mwanadada, kwani tulitoka naye mbali na pendo letu ni la ujana, na la asili, na
nisingeliweza kuishi kwa raha bila kuwa na yeye...’aliposema hivyo watu wakashangilia,
na kupiga vigelegele...
‘Tumekubaliana na yeye na kehskubali kuolewa na mimi hana
shida..ananifahamu, ..’akasema na watu wakcheka.
‘Kwa vile ananifahamu, akasema nahitajia mwenza....maana
anaona kazi itamwia nzito kidogo,...’hapo watu wakacheka.
‘Hili lipo jamani, wote hatupo sawa..kama vilivyo vidole,
ndivyo hata hisia na nguvu zetu za kimwili zinatofautioana...wengine nguvu zetu
ni zaidi ya wengine, je tufanyaje, ...tukatange tange mitaani, hapana mimi kama
kiongozi ni lazima niwe na busara, lakini busara yangu sio kama ya wengine,
sitaki kulazimisha....ndio maana nilipomuona shemji yupo huru, japokuwa
kisheria nilitakiwa kumchukua, lakini ....’watu wakacheka na kusema
‘Huyo huyo....’wakasema
‘Lakini kuna shemeji yangu....na yeye namtaka pia, nampenda
saaana, hata mwanadada analifahamu hilo....’hapo watu wakacheka na kushangilia.
‘Siku kaka yangu anamuoa shemeji, niliumwa, nilikosa
raha,....wakati huo bado mimi nasoma, namalizia masomo yangu, na wakati huo
nilikuwa sijajuana sana na mwanadada, alikuwa mwanafunzi mwenzangu tu, ...nilikuwa
sina habari na yeye maana moyoni kulikuwa na nafasi ya mtu ambaye, niliwahi
kumuona huko kijijini, na nilitarajia siku nikifika tena, nikamtafute,
nikamtambulishe kwa wazazi wangu. Mimi na mwanadada kipindi hicho hatujaingia
kwenye makubaliano ya kuwa marafiki,..tulikuwa tunaelewana tu, ...na ndio nikaja
likizo, na lengo la kumtafuta huyo binti
‘Siku hiyo kaka akasema ana mazungumzo na mimi, anataka
kunitambulisha kwa mchumba wake, nikafurahi na mimi nikasema kimoyo moyo, kuwa
ukimaliza na mimi nakwenda kumtafuta huyo wa kwangu, tutaoa pamoja...nilikuwa
nimedhamiria kweli, ujana tena...
‘Mara akaingia binti, mimi nilikuwa nasoma, sikuwa
nimengalia wakati binti huyo anaingia, kaka, akaja na kunipiga piga mgongoni na
kusema;
‘Msalimie shemeji yako huyu...’akasema na mimi nikainua suo
kumwangalia,oh,...nilitamani nipayuke niseme, ...
‘Huyu ni wa kwangu, nikbakia nimeduwaa...nikimwangalia huyo
binti, hadi huyo binti akageuka, na kuaga kuwa aanondoka,.. kaka akanitambulisha
kuwa huyo binti ndiye mchumba wake, ni mke wake mtarajiwa, ambaye ndiyo huyo mwanamama...
‘Nilishituka, nilipomuona kuwa ni yule yule msichana ambaye
nilikuwa namuona akipita, na sikuwa nafahamu wapi nitampata, nilifanya juhudi
sana kipindi cha nyuma kumtafuta lakini kipindi hicho walikuwa wakiishi kijiji
cha jirano na alikuwa akifika hapa kusalimia tu, baadaye ndio familia yao ikaja
kuhamia kwenye kijiji hiki.
Binti aliyekuwa kauteka moyo, binti niliyemuona mara moja,
na safari ya pili, ikawa ndio hii kaka ananitambulisha kuwa huyo ndiye mchumba
wake, ndio huyo mwanamama.Jamani hebu fikirieni jinsi gani
nilivyoumia,...niliumwa, hata wakati narejea chuoni nilikuwa kama mtu
aliyefiwa.
Na mwanadada alikuja kunigundua kuwa sina raha, akawa ananidasi
kuwa nina tatizo gani, mwanzoni nilimficha, lakini baadaye nikamwmbia, na akawa
mtu wangu wa karibu,wakunipa ushauri nasaha,...kwakweli alinisadiai sana hadi
kuja kutulia....nilifikia kubaya, kweli kupenda ujanani ni hatari....
Kutokana na kuwa karibu na mwanadada nikaanza kujenga
urafiki naye wa karibu,nikaja kugundua kuwa ni mtu ambaye tunaivana, na macho
yangu yakafunguka, kumbe ni dada mrembo, moyo ukafunguka, lile penzi lililokuwa
likimataka mtu mwingine likageukia kwake...nikampenda kwa dhati...sasa hapa
najiuliza nimuoe yupi...’ watu wakashangilia, na kusema
‘Oa wote wawili....’
‘Mnasemaje..?’ akauliza tena, na watu kwa fujo wakasema;
‘Oa wote wote waili
‘Sasa, tatizo sio kwa mwanadada...mwanadada keshakubali,
hakuna shida, tatizo lipo kwa mwanamama,naombeni mnisaidie, nisije nika.....au
niamulieni nimuoe nani...?’akakatisha na watu wakicheka, watu wakacheka, na kucheka, na kila mmoja
akawa anasema lake, wengine mwanamama , wengine mwanadada.....ikaw kama vurugu.
‘Hapa nina pet e mbili mkononi,...nilizinunua, nikiwa na
haja ya kuzitumia zote, ili niweke rekodi hapa kijiji ni ya kidume aliyeoa wake
wawili kwa siku moja, ...sasa ili nieleweke vyema, nifanya hivi, maana wa
kwanza kumpenda kwanza,...au sio ..mmh, ‘akageuka kumwangalia mwanadada na
mwanadada akawa anatabasamu na kutikisa kichwa kukubali, na kitendo hicho
kiliwafanya watu wazidi kushangilia.
Mwanasheria akatoka pale alipokuwa amekaa kwa wageni rasmi
na kutembea hadi meza ya akina mwanamama na wazazi akapiga magoti mbele ya
mwanamama, akainua mkono, akionyesha ile pete hewani, na kusema;
‘Mwanamama ninakuomba
sana, usione nalifanya hili kwa kukunyanyapaa,hapana,nafanya hili
nikiudhihirishia kwa uma, kuwa kweli nakupenda, na nisingelitaka niumie,
...wakati jamii ipo, na haijui kwanini naumie ndani kwa ndani,..nakuomba ukabali
uwe mke wangu...’na watu wakaitikia kwa vigelegele wengine wakisema
‘Keshakubali huyooo, ni wako huyooo..’
Mwanamama alikuwa kama kapigwa na butwaa, na akageuka
kuwaangalia wazazi wake, na akawaona wazazi wake ni miongoni mwa watu
wanashangilia hiyo kauli ya mwanasheria. Na mwanasheria alikuwa akiendelea
kuongea;
‘Mimi nimetamka mbele ya kadamnasi, kuwa kweli ninakupenda,
na nipo tayari kuku-oa,, sio kwa ajili ya penzi tu, bali pia kwa ajli ya mtoto
wetu, kwa ajili ya marehemu kaka yangu, kwa ajili ya jamii na kwa ajili yangu
mwenyewe, nimeshasema nilikupenda hata kabla ya kaka yangu, kwahiyo sioni
kwanini nisikuoe ukawa mke wangu...’watu wakashangilia na kumkatisha, na yeye
akawa anatabasamu, na mara akainama kusmikiliza mwanadada, ambaye alikuwa
akimnong’oneza jambo, halafu akatabsamu na kusema;
‘Mke wangu wa kwanza...kwahiyo sioni kwanini nisikuoe ukawa
mke wangu wa kwanza....’mwenzangu kanisahihisha hapa, akasema akimuonyeshea
mwandada, na mwanadada akawa anatabasamu huku akiangalia mbele, akiwaangalia
watu ambao walikuwa wakishangilia na kupiga vigelegele....
‘Ninashukuru kuwa tumeliongelea hili na mwanadada akanielewa,
na hili nalifanya nikiwa nimekubaliana naye, hakuna tatizo kwa hili, yeye yupo
radhi kwa lolote lile, kwasababu tunapendana kiukweli , na mungu ndiye shahidi
yetu, na licha hilo kaniahidi na kuniambia kutoka ndani ya moyo wake kuwa
anampenda sana mwanamama, ..haoni ubaya akiwa ni mwenza wake wa maisha.’akatulia
akigeuka upande ule waliokaa mwanamama na familia yake huku watu wakiendelea
kushangilia na wengi wakiongea hili na lile.
‘Nasema kiukweli kutoka ndani ya moyo wangu, kuwa mwanamama
alikuwa moyoni mwangu, na naweza kusema yeye alikuwa ni tonge nililonyang’anywa
mdomoni, japokuwa niliumia, lakini niliona sio mbaya, kwa vile lilichukuliwa na
ndugu yangu ambaye hakujua kuwa na mimi nilikuwa nampenda huyo binti, lakini
kumbe mwenzangu aliwahi na kuchukua,....’akasema na watu wakacheka.
‘Lakini sasa tena ndugu yangu kwa bahati mbaya keshatangulia
mbele ya haki , yote ni mapenzi ya mungu, ....sikuomba iwe hivyo, na hakuna
anayeweza kuomba hivyo, eti kwa vile alininyang’anya tonge mdomoni, hapana yote
hayo ni mapenzi ya mungu na yeye ndiye mwenye mamlaka na uhai wa mtu..namuomba
mungu amuweke mahali pema peponi.....’hapo akaongea kwa huzuni na watu
wakaitikia `amiin..’
‘ Na kwa minajili hiyo, natakiwa nifanyenini,....ili hali
mtu niliyempenda yupo huru hana mtu, na
kila nikiota namuota kaka yangu akinisihi nifanye hivyo, ...nimchukue mwanamama
awe mke wangu,.... hata nilipokuwa nimepoteza fahamu, ndugu yangu huyu ananitaka
nimchukue shemeji, ili awe mke wangu, ...kwahiyo nifanye nini....wakati mtu
nampenda, sio tu kwa ajili ya hili shinikizo lakini ndani ya nfasi yangu nakiri
kuwa nampenda....sasa, nifanyeje?’ akawa kama anauliza na watu wakadakia na
kusema.
‘Mchukue, ni wako....’ aliposikia hivyo, akamgeukiwa
mwanadada, na mwanadada, akawa anatabasamu huku akionyesha kwa kutikisa kichwa, kukubali na wanayosema
watu.
‘Kwakweli ndivyo ninavyotaka iwe hivyo, lakini je wmenzangu
huyo anakubaliana na hilo,...sipendi kufanya hayo kwa shinikizo, kwa kulazimishana...hapana,
hilo ni swala la hiari ya mtu,...nataka kwa hiari yake mwenyewe akubali...lakini mimi
moyoni siwezi kuliachia tena hilo tonge, ..likaja kuchukuliwa na watu wengine,
baki....nitaumia sana’akasema na watu wakacheka na kushangiliza.
‘Sitaki niongee mengi..nafanya haya kwa vitendo...’akasema,
na hapo mwanasheria akatoka sehemu ile
aliyokuwa amesimama na kwenda pale walipokuwa wamekaa mwanamama na familia yao, na kwanza akasimama
mbele yao, na kuinama kidogo, halafu akasogea karibu na muelekeo wa pale
alipokuwa kakaa mwanamama, akatoa pete
moja na kuiweka hewani na kusema;
‘Mwanamama, nakuomba ukubali uwe mke wangu wa kwanza, ili
tuje tufunge ndoa tuishi kwa raha, na shida, hadi hapo mungu atakapoamua...pokea
pete hii kama ishara ya kukubali ombi langu hilo...’akasema na watu wakawa
wametulia kimiya...
Alitulia vile kwa muda, na baadaye akapiga magoti, na
kuyarudia yale maneno, huku akiwa kainua kichwa kumwangalia
mwanamama....kimiya...
Mwanamama alikuwa kama kashikwa na mshangao na kutahayari,
akageuka kuwaangalia wazazi wake, ambao nao walikuwa katika hali kama hiyo, wameshikwa
na butwaa, na huku wakimwaglia binti, alivyotulia, haonyeshi kukubali, au
kukataa,, kukapita kitambo kidogo, na watu wakaanza chokochoko, na kusema;
‘Chukua, kubali, chukua.....’
Mwanamama akainama chini kama mtu anayemuomba mungu wake, na
alipoinua kichwa,kulikuwa na mchozi machoni,... akageuka, kwanza kuwaangalia
wazazi wake tena, wazazi wake wkaonyesha ishara ya ukubali, akageuka
kumwangalia mwanadada, na mwanadada akawa anamuonyesha ishara ya kukubali, na
alipogeuka kuangalia pale alipokuwepo mtoto wake, akamuona mtoto wake anainuka
kuondoka kweye kiti alichokaa,...
Akanyosha mkono kumzuia asitoke kwenye kile kiti lakini alikuwa keshachelewa, yule
mtoto aliinuka kwenye kile kiti na akapita kwenye ile meza iliyokuwa mbele
yake, akasogea hadi pale alipokuwa kakaa mwanasheria, na yeye akapiga magoti ...
kama alivyopiga baba yake huyo mdogo
Watu kuona vile wakaangua kicheko, na kushangilia, yule
mtoto kama vile kafundishwa kufanya hivyo, kwanza akamwangalia baba yake huyo
mdogo, na baadaye akainua mikono, kuigiza kama alivyokuwa kafanya baba yake
huyo mdogo....
Yule mtoto akanyosha mkono, kama alivyofanya mwanasheria
akaigiza kama vile kashika pete, kama alivyokuwa kashika pete mwanasheria
japokuwa yeye hakuwa na pete kidoleni mwake, akawa anamuashiria mama yake kama
anamuomba, akubali maombi ya baba yake huyo mdogo...
NB: Kidole kinauma, tutamalizia sehemu ndogo iliyobakia, je
ilikuwaje?
WAZO LA LEO: Ndoa
ni makubaliano kati ya mume na mke, na hukamilika kwa hiari ya watu hawo wawilibila
shinikizo,na kwa vile inajengwa na watu wawili kuja kuwa kitu kimoja, ni vyema
kukawa na upendo ndani yake. Je kuna mtu anachukia sehemu ya mwili wake? Kila
mtu anapenda mwili wake, kwani ni muhimu kwake, na kwa vile mke na mume
wanakuja kuwa kitu kimoja mwili mmoja, ni lazima kuwe na upendo ndani yake...
Ni mimi:
emu-three
1 comment :
Kisa kitamu hiki jamani!
Post a Comment