‘Ulimjuaje huyo Kimwana?’ nikamuuliza huyo binti, akiwa
katulia , lakini hata hivyo alionekana kuwa na wasiwasi sana, kinyume na
kawaida yake tunapokutana.
‘Nani aisiyemjua Kimwana, kila mtu anamjue yeye, kwa uzuri
wake kila msichana anatamani kuwa mnzuri kama yeye, lakini uzuri wake kumbe ni
sumu kwa maisha ya watu, na badala ya watu kuupenda uzuri wake kwa wema, umegeuka
kuwa uzuri wa ubaya, na kila mmoja anataka kumharibu…’akasema huyo binti.
‘Lakini wewe alikufanyia kitu gani kibaya kwako?’
nikamuuliza.
‘Kama ana ukimwi, na mimi nimeshaupata huo ukimwi, lakini kwa
ajili yake, na….na, sijui nimewakosea nini…binadamu wenzangu,….mimi ni
masikini, sina baba, sina mama,…. Niliokuwa nikiwategemea kama wazazi wangu ….ooh,
angalia huyu baba akaja kunigeuka kuwa na kuwa sumu ya kunimaliza mimi. Sasa
mimi nina thamani gani tena katika hii dunia. Usichana wangu una maana gani
tena, …’akaanza kulia.
Nilitaka kumkatiza kwa kumbembeleza, lakini nikaona
nimpemuda wakumaliza machungu yake, nimuache alie kidogo, na akaendelea kusema;
‘Eti dada, mimi ni nani atanioa tena akisikia kuwa nina
ukimwi, …nilitamani sana mume wa kwanza kuugusa mwili wangu ndiye atakaye kuwa
mume wangu…ndio maana huyu baba aliponifanyia kitu kibaya, niliona ni heri …..ni
heri niwe tu mke wake, sasa ina maana
gani,..hebu niambie mimi nimewakosea nini wanadamu wenzangu, ina maana
umasikini na laana…..’akawa analia kwa kwikwi, kiasi kwamba hata mimi
niliyekuwa nikimsikiliza nikawa sina amani tena moyoni
Baadaye alitulia na kwa muda huo sikutamani kumuuliza tena maswali,
nikamwambia kwa upole;
‘Unajua mdogo wangu, sio kweli kuwa kila ukitembea na mwenye
ukimwi na wewe utakuwa nao, na pia sio kweli kuwa ukitembea na mwenye ukimwi
hutakuwa nao,…. cha muhimu ni kwenda kupima , ukipima utajua afya yako,….na
utajijua wewe mwenyewe kuwa usalama au la…ni kama ikiumwa na mbu, sio lazima
kuwa na malaria,lakini pia unaweza ukaambukizwa malaria,na ili ujue kuwa huna
au unao ni kupima kwanza……’nikamwambia.
‘Usinidanganye kwa hilo, mimi najua ninao, lakini kabla
sijatangulia, …..mmh,..we niache tu, ila dada nakuomba kitu, nakuomba nipo
chini ya miguu yako..’akasimama na kuja kunipigia magoti, na mimi sikupenda
kabisa hilo tendo, nikasimama na kumsimamisha.
‘Unafanya nini, mimi nilishakuambia kuwa kama una shida
yoyote niambie tu, nitakusaidia, sio mpaka kunipigia magoti, unashida gani
nyingine…hebu niambie mdogo wangu?’ nikamuuliza.
‘Nataka kwenda kijijini kwetu, nasikia kuna mtaalamu wa huu
ugonjwa, naomba nipo chini ya miguu yako…nipe nauli, mimi huwa naoteshwa na
kuelekezwa nini nifanye, …na kila inapotokea inakuwa kweli, nikipuuza najikuta
kwenye matatizo, kama hayo aliyonifanyia baba, kama ningelifuatilia
nilivyoelekezwa nisingelikutana na hayo matatizo…’akasema.
‘Ni nani huyo anakuelekeza?’ nikamuuliza.
‘Mimi sijui, huwa kuna hali inanijia nakuniashiria kuwa
uafanye hivi, au uende mahali fulani utapata hiki, na sasa imeniambia kuwa
nisipokwenda huko kijijini, nitaangamia kwa ugonjwa mbaya, na najua utakuwa huo
ukimwi….’akasema akionyesha wasiwasi .
‘Unataka kwenda kijijini kwa ajili ya kutibiwa ugonjwa ambao
hujajua kuwa unao, usiwe hivyo, sikia ,kesho mwambie mama kuwa unataka ukapime
kwanza, ukijijua nitakuambia nini cha kufanya,…’nikamwambia,
‘Je wewe siumesema kuwa upo tayari kunisaidia, sasa
nimekuomba huo msaada, wa nauli tu ….kama huwezi basi, ngoja nitatafuta kwa
wengine, lakini sio kwa huyu baba au kwa
mama wa watu…’akasema.
‘Kwani unataka kuondoka bila kuaga?’ nikamuuliza
‘Baba siwezi kumuomba lolote,…sitaki hata kumuona tena, mama
siwezi kumuomba kitu,kwasababu namsikitikia sana, mama wa watu mpole hana hatia
leo hii watu kwa tamaa zao wanamuangamiza, yeye sitaki kabisa kumuumiza tena,
na sitakuwa na raha tena nikimwangalia usoni, ..siwezi, na kama dada usiponipa hiyo
nauli, basi, …labda njia nyingine, ili nisimuona huyo mama akiwa an huzuni , ….nitakunywa
sumu, nife….’akasema na kuniacha nikiwa
nimeduwaa.
‘Eti nini..?’ nikasema kwa hamaki.
‘Dada hilo nimedhamiria,kama hutanipa nauli, basi …nitajua
la kufanya, ….siwezi, najua nimemkosea sana mama, ingawaje sio dhamira yangu, najua
…na nimejitahidi kumsaidia sana,lakini huenda isiiwe na tija, naona bado sijaweza
kumsaidia itakiwavyo, sitaona raha nikimuona akiteseka, ….hapana…’akasema na
hapo akaingia ndani na kuniacha nikiwa nimekaa pale sebuleni, nikiwaza.
Niliwaza sana, niliwaza hii familia, na kumuwaza mama mwenye
hii familia, sijui anajua nini zaidi , sijui alipojua kuwa mume wake katembea
na huyo Kimwana ambaye alikuja kugundua kuwa Kimwana kaathirika…sijui alijiskiaje.
Nikaona ni bora tu nimpe huyu msichana hiyo nauli, lakini lazima nihakikishe
kuwa anakwenda kupima kwanza.
Baadaye alitoka akiwa kabeba nguo zake ,akaniambia anataka
kufua nguo zake, kama nitampa hiyo nauli, basi ataondoka,..kwani alishaambiwa
kuwamimi ndiye ninaweza kumsadia , ..ila kama sitampa atajaribu kuomba kwa
yoyote mwingine, lakini hatakubali kukaa tena kwenye hiyo nyumba,….
‘Mimi nitakupa nauli lakini mpaka unihakikishie kuwa
utakwenda kupima kwanza…’nikamwambia.
‘Hilo la kupima usipoteze muda wako, ..siendi huko,…nilishaambiwa
kuwa nikipima tu,basi, sitaokoka tena, hawo watu nisiowajua wamesema
watainyonya hiyo damu yangu kama ina wadudu, na itaingia damu nyingine isiyo na
wadudu, wewe utaona tukikutana tena….’akasema akionyesha kuwa kweli anaamini
hivyo.
‘Lakini huoni kuwa hizo ni njozi tu, ni vyema ukawaona
madakitari wenye vipimo halisi..’nikjaribu kumshawishi.
‘Eti nini , madakitari, hawo madakitari wenyewe siwaamini tena, mimi
nikifika huko kijijini nitajua wapi pa kwenda,….huko najua nitaweza kuwalilia
wazazi wangu huko walipo, huko ndipo nilipozaliwa na kama ni kufa nifie huko
huko nilipotokea, ….najua nimeshamaliza kazi yangu hapa mjini…na hata hivyo
hawo watu wameshaniahidi kuwa huko nakwenda kuchukua Baraka zao, uniamini tu
dada yangu…’akasema.
‘Je uliwahi kwenda kumuona nesi?’ nikamuuliza ili kupoteza
lengo kwanza.
‘Hapana,…nampenda sana huyo dada, na huenda yupo kwenye
wakati mgumu, lakini sina la kufanya, yeye alikuwa kama mmoja wa ndugu zangu
wakaribu kama ulivyo wewe, lakini nimeshindwa hata kwenda kumpa pole….najua
hana hatia…, kama nitarudi tena nitampa pole,lakini kwa sasa, mimi nataka
nifike kijini kwetu….’akasema.
Nilitaka kumdadidi zaidi, lakini akatoka nje na nguo zake,
alionyesha kuwa hataki kuongea zaidi bila ya kumpa hiyo nauli, ….
Basi nilimpa nauli
nikiona ndilo jambo ninaloweza kumsaidia na kumuomba sana ajitahidi kwanza
akapime, na nilimwambia kwanza aongee na mama yake, kwani yeye alimchukulia kama
binti yake.Hakunijibu kitu, akawa anaendelea kufanya usafi wa guo zake, na mimi
nikaona sina la kufanya nikaondoka zangu.
Kesho yake nikapata taarifa toka kwa mke wa wakili mkuu kuwa
huyo binti keshaondoka, na mkononi alikuw akashika barua, sikujua ni barua ya
nini, nikamkaribisha na tukaanza kuongea …
‘Nilijua tu huyu binti atakuja kuondoka,lakini sikujua kuwa
ataondoka kwa njia hii, nilimchukulia kama binti yangu, nikamlea nakumpa kila
ambacho anastahili kupewa binti yangu,leo hii anaondoka kama tumekosana…’akalalamika
mke wa wakili mkuu.
‘Ni kuchanganyikiwa
tu, naomba umsamehe…’nikasema.
‘Mimi sina kinyongo naye, ila imeniuma sana, maana sasa huko
kijijini atakwenda kuishi na nani, hana wazazi kwa sasa, hana baba, wala mama, ….na
nilishangaa sana,..nilishamwambia kuwa pale mimi nitamlinda hatasumbuliwa tena na
mume wangu baada ay lile tukio, , lakini kumbe, mwenzangu alikuja kunigeuka, nilikuja
kusikia kuwa alikuwa bado anatoka na mume wangu….’akasema kwa uchungu.
‘Ulisikia kwa nani….?’ nikamuuliza.
‘Dunia hii ina siri….na huyu nesi, alikuwa shoga yake
mkubwa, nilishamkanay sana aiwe na mazoea na watu kama hawo, lakini hakunali,
sasa hebu angalia hawa watu wasio na huruma na binti wa watu kama huyo, …wamekuja
kumwangamiza binti wa watu akiwa bado mdogo…’akaniambia.
‘Kumwangamiza kwa vipi?’ nikamuuliza nikijifanya sijui
lolote.
‘Yaani kuna watu wanyama hapao duniani, na sijui kama
watakuja kusamehewa, hilo tuliache tu, maana kabla hujafa utakumbana na mengi, …’akasema
na hakutaka kuniambia lolote hata nilipomdadisi sana, na mwisho wake
nikamuuliza.
‘Wewe kama dakitari uliwahi kumshauri huyo binti yako
akapime, …..baada ya lile tukio ?’ nikamuuliza.
‘Nilitumia kila mbinu lakini hakukubali kabisa….nilitaka
kama inawezekana nimpe dawa za usingizi nimchukue damu lakini kila mbinu
nilizojaribu nilikuta anajua lengo langu ni nini, sikufanikiwa…ana kitu kama
mashetani, akama anvyodai yeye, kuwa yanamuelekeza, ….yaani huyo binti ana
maajabu, sasa sijui kwanini hayo mashetani hayakumsaida wakati anabakwa na huyo
mmwanaume….’akaniambia.
‘Na wewe je ulishapima, maana hili tunashauriana kila mtu..’?’nikamuuliza.
‘Siku nyingi, sana mimi ni dakitari, na huenda watu
watashangaa, na wengine wamekuwa wakitunyoshea vidole kwanini hatuna watoto, ….niliwaficha
mwanzoni, na ilitakiwa iwe siri yangu, ….lakini hata hivyo, hili nililiona
mapema,….ukiishi na mume utamjua tabia yake, mimi kama dakitari, nikawa namechukua
tahadhari mapema, namshukru mungu kuwa nilifanikiwa, sijui labda itokee jingine….’akaniambia.
‘Ina maana wewe umeshapima na kuwa huna tatizo la huo ugonjwa….maana siku hizi
maambukizi yapo ya iana nyingi ?’ nikamuuliza.
‘Amini usiamini mimi sina,mungu alininyowekea mkono wake wa ulinzi mapema,…..namshukuru
sana mungu,….ila niliona kuwa huyo muambukizaji ni bora aondoke hapa duniani
maana hana huruma na watu kama huyo binti yangu, lakini sikupata bahati ya
kumuondoa mimi dunia, ila aliyefanikiwa kumuondoa, naona kafanya kwa niaba
yangu…’akasema na alisituka pale alipogundua kuwa kaongea lile alilokuwa
akilikataa.
‘Una maana gani kusema hivyo, huyo muambukizaji ni nani, na
kamuambukiza nani, naomba uliweke hili wazi, mimi ni wakili wako…?’
nikamuuliza.
‘Tafadhali,sana na unisamehe sana, hilotuliache kwanza..ipo
siku nitakusimulia lakini sio leo…’akaniambia
‘Na unahisi ni nani muuaji wa Kimwana, maana kila mmoja
anakataa kuwa sio yeye…hata nesi keshakataa kuwa sio yeye?’nikamuuliza.
‘Akate asikatae ni huyo huyo nesi, na hawara yake….hilo sina
shaka nalo’akasema huku akionyesha kuwa kweli ana hasira fulani moyoni, na ana maana
hiyo.
‘Je kwa kauli yako hiyo kwa kumuita mume hawara yake,….inaonyesha
kuwa hujamsamehe mume wako, ..na hii nikuonyesha kuwa ndoa yenu ipo matatani,
au unataka kusemaje kuhusu ndoa yenu na majaliwa yake?’ nikamuuliza.
‘Najua wengi watasema namnyanyapaa mume wangu, lakini tungalia
ukweli na hali halisi, mimi nimeamua na sitaangalia
nyuma tena, ….nitakachofanya ni kuvuta subiri apone, na akitoka, naibariki ndoa
yao na nesi, kwani wao wanastahiliana, na kweli wanapendana ,maana haina haja
kuishi na mtu ambaye ana mtu wake wa siri, wanayependana,…mimi nimevumilia mengi
kwa upande wangu, na imetosha..’akaniambia.
‘Unasema kuwa watu watasema kuwa unamnyanyapaa mume wako
kwanini ufikirie hivyo..?’nikamuliza
‘Wewe ni wakili wangu, lakini siwezi kukuambia kila kitu,
kuna mambo mengine yakitaaluma yangu,
nahitajiwa kutoyasema, hilo najua hata wewe unalifahamu, kama ipo siku
utastahili kuambiwa utaambiwa lakini sio kwa sasa, nakuomba unielewe kwa hilo,
wewe chukua hii barua yako toka kwa huyu binti, sijui kakuandikia nini,labda
kuna jambo linanihusu, kama lipo naomba uniambie ili nijue kwanini kaamua
kunikimbia….’akaniambia.
‘Ina maana wewe ulipoiona hii barua hukutaka kabisa kuisoma
kwanza…ili ujue kwanini kaondoka, na ina maanahakuacha ujumbe wowote kwako….,?’nikamuuliza.
‘Mimi sina tabia hiyo,…hiyo barua unaona jinsi ilivyofungwa,
na imeandikwa jina lako…huyo muandikaji alitaka hii barua ikufikia wewe
mwenyewe, anakuamini sana kuliko hata mimi,na mimi sina tabia ya kupkenyua viti
vya watu kama kweli havinihusu, naheshimu sana maadili yangu…’akasema na mimi
nikaifungua ile barua na kuanza kuisoma.
Ilikuwa barua ndefu, na sijui alianza kuiandika lini, maana ilielezea
mambo mengi sana, maisha yake hapo kwenye hiyo nyumba, na mengine ambayo
alishawahi kunielezea, na kuna sehemu alianiagiza kuwa nikapate uhakika kwa
nesi, yeye ataniambia zaidi, na nilipofika sehemu ya mwisho wa hiyo barua ndipo
nikakutana na maelezo ambayo yalinifanya mwili mzima usisimukwe,….nilihisi
kizunguzungu,…sikuamni hadi nilipokutana na nesi,ambaye aliniithibitishia hilo.
‘Kweli nesi, alikuwa mtu wa pekee sana…..’
NB Natamani niendelee lakini muda hautoshi, tukutane tena
kwenye sehemu iliyobakia.
WAZO LA LEO: Siku
zite hazilingani,…usiwaze sana ukiona mambo yako hayaendi vyema, ujua kuwa
katika kuhangaika kote kuna kupata na kukosa. Ukipata mshukuru mungu, na
halikadhalika ukikosa mshukuru mungu wako.
**********************************************************************************
KUTOKA KWA WAZEE WETU:
Hili nimeipata kutoka kwa mzee wetu mstaafu, ambaye katika maisha yake yote
amekuwa kazini, kutoka ujanani hadi akaja kustaafu, na alipostaafu, kaingia
kwenye kazi ya ulinzi,…kwa umri huo alio nao, asingelistahili kufanya hiyo
kazi, ilitakiwa kukaa na kula pensheni yake…lakini hiyo pensheni ipo wapi?’
‘Sio kwamba napenda kuifanya hii kazi, bali ni hali halisi
ilivyo, miaka mingi nilikuwa kazini, mtiifu ,mchapakazi hodari, na hata
nilipotoka pale kazini niliacha jina langu likiwa ni maarufu, lakini nini
nilichokipata baada ya kupewa ile barua ya kuwa nimestaafu, ni mishahara yangu
miwili, na kuambiwa nikachukue pensheni
yangu.
Hela iliyokuwa ikikatwa kwenye mshahara miaka yote hiyo,
haikunisaidia kitu, kwasababu ilikuwa ni pesa ndogo kutokana na mshahara wangu,
kama ningeliitumia muda ule ilikuwa na thamani, angalau ingenunua kitu, lakini
kila muda unavyokwenda thamani yake hushuka….mia ya jana sio sawa nay a leo.
Haya nikahangaika mpaka nikaipata hiyo inayoitwa penshion, niifanyie nini..ikawa ni tatizo jingine,kwani
haiwezi kufanya lolote, ….na ukumbuke kuwa mimi wakati wote nilikuwa mtu wa
kutumikishwa kwenye maofisi, sijui biashara na wapi pa kuanzia,…lakini haina
jinsi nikaamua kufungua kigenge,…balaa likaniandama, wakaja hawa watu wa city na
kuvunjwa hilo genge na watu wa jiji, na vitu vyote, mtaji wote, ukaguduka, sina
mbele wala nyuma, watoto wengine bado wanahitaji ada, wanasoma, nifanyeje,…nikaona
ndio nitafute kazi hii ya ulinzi.
`Wazo langu kwa wenye makampuni,..matajiri …’akamalizia huyo
mzee kwa kusema, `Angalieni sana wazee waliotumikia makampuni yenu, wajalini
wanapoondoka,wao walijitolea sana…angalau wapeni kitu cha kuanzia maisha, hiyo
mishahara miwili na hiyo pensheni haitawasaidi lolote….wazee ndio Baraka ya
mafanikio yenu…au ndio tusubiri pension ya kuzikiwa, kwani ndio ilikuwa lengo
langu kuwa nifanye kazi kwa ajili ya kuja kuzikiwa?
Ni mimi:
emu-three
1 comment :
Hii imetumwa kwenye e-mail na mpendwa mmoja,anasema;
Hongera sana mkuu, haya mawazo yako kama yangelikuwa yanapitiwa na hawo jamaa mbona ingesaidia.
Akauliza hivi;
Hivi mkuu hivi visa unaviandika saa ngapi na je ni vya kweli, na hizo picha zao unazipata wapi, na je ni wahusika kwenye hivyo visa?
Mpenzi wa blog yako
Post a Comment