Nilimkuta nesi akiwa kakaa kitandani huku kashikilia
karatasi mkononi mwake , ilikuwa ni barua, na nilipomtizama usoni mwake niliona sura
iliyojaa huzuni na hata machozi ambayo yalikuwa hayajakauka ambayo yaliacha michirizi
usoni yalionekana wazi wazi. Mimi nikamsogelea, lakini ilionyesha wazi kuwa hakuwepo
hapo ki-akili. Nikamsogelea pale kitandani na kumgusa begani, akashituka na
haraka akafuta yale machozi usoni, akasema.
‘Leo hii sijisikii vyema…, na ningelifurahi kama
nisingelisumbuliwa na mtu yoyote, lakini kwa vile ni wewe nitavumilia tu kwasababu
nahitaji kuongea na wewe…’akasema.
‘Kuongea na mimi kuhusu kitu gani, na kwanini upo katika
hiyo hali na nimesikia kuwa leo hutaki kuongea na mtu, Ila mimi nikija
niruhusiwe kukuona, kuna kitu gani kinakusumbua…au ni katika ile mipango yako
….?’ nikamuuliza.
‘Ama kama kuna kitu gani kinanisumbua, wewe unajua jibu
lake, sizani kama ni swali la kuniuliza hilo kama kweli unajali hisia za watu,
lakini sio mbaya, nikakuambia ni jambo gani lililonifanya hadi nifikie hatua
hii na hali kama hii unayoniona nayo, mimi sio mtu wa kulia lia, lakini
nashangaa leo machozii yananitoka….’akasema na kuifunua ile karatasi aliyokuwa
nayo mkononi mwake.
‘Najua kuna barua umeipata,…kutoka kwa yule binti wakufikia
wa wakili mkuu. Hapa kwenye hii barua niliyopewa na mama yake kaandika kuwa
kakuandikia barau iliyoelezea kila kitu, nay eye keshaondoka,….. na hatarajii
kurudi tena, labda kama akija ni kwa ajili ya kuniokoa mimi nisiingie matatani…kama
itaingia matatani, lakini kwa maelezo yake kasema anajua kabisa mimi sitaingia
matatani…..’akasema.
‘Matata gani hayo…..?’ nikamuuliza na yule nesi akainua uso
na kuniangalia , na safari hii ulikuwa ule uso wa ujasiri, akasema;
‘Sizani kama mpaka sasa hivi hujajua lolote kuhusu huyu
binti, najua unamjau vyema, na hata kabla hajakuandikia hiyo barua,najua
ulishajua nini alichokifanya, nikuulize, hiyo bunduki ulipoipata uliangalia
alama zote za vidole, sizani kama iliwahi kutolewa pale nilipoificha..kabla
hujaigundua wewe…’akasema.
‘Ina maana ni wewe uliyeificha pale, mbona hukutuambia
hilo?’ nikamuuliza.
‘Sikuwaambia hilo na mengine mengi, lakini niliyafanya hayo
kwa ajili ya huyu binti Yatima na nilisubiri wakati muafaka,…kwasasa nipo tayari kubeba yote yanayomuhusu huyo
binti, namjali na kumuonea huruma,na sijui kama nyie mna huruma na yeye, kwani
aliyoyatendewa hayakumstahili….’akasema.
‘Lakini mtendaji wa hayo yote ni mpenzi wako’nikamwambia.
‘Najua hilo,….na siku nilipopata hiyo habari kwa mara ya
kwanza nilimlaani sana huyu jamaa yangu, nilitaka nimfanye kitu mbaya,lakini
nikiwaza nakujiuliza kwanini alifikia hatua hiyo….huenda yeye mwenyewe
angelikuwa na jibu zuri, lakini mimi moja kwa moja namtupia lawama
mkewe…’akasema
‘Kwanini umtupie lawama mkewe?’ nikamuuliza.
‘Huenda mimi ni tofauti na wanawake wengine,huenda
nikaonekana mbaya, lakini huwa nasema kuwa mke anaweza akabeba lawama pale
mumewe anapokwenda nje ya ndoa.Hebu nikuulize wewe unayejifanya
kuwatetea,….hivi kama mke anamtosheleza mumewe,
na kutimiza yote yale yanayostahili, huyo mume angeliweza kutoka nje ya ndoa,
ukiona hivyo,kuna walakini, ….na ukiangalia hii ndoa ya mtu wangu, walioana kwasababu tu ya
mslahi fulani , lakini sio kwa ajili ya upendo..’akasema.
‘Maslahi gani hayo?’ nikamuuliza.
‘Wanayajua wenyewe, …huyu jamaa yangu, asingeliweza kumaliza
masomo yake huko Ulaya kama asiingeliweza kupata msaada wa huyo mkewe, wakati
huo alikuwa binti mwenye nazo,….yapo mengi yaliyotokea huko, …sina muda wa
kukusimulia,…Ila jamaa ilibidi ajifanye kuwa anampenda,ili afanikiwemalengo
yake, ingawaje ni kweli kuwa binti wa watu yeye alishampenda, ….ikabidi waingie
kwenye pendo la kuigiza,mmoja akijua ni kweli anapendwa lakini mwingine
akifanya ili apate anachokitaka….’akasema.
‘Una uhakika na hilo kuwa alifanya hilo kwa kuigiza tu,
….kwani kwa hali halisi inaonyesha kuwa jamaa yako huyo hajatulia ni tabia
yake, huoni, mara kwa huyu na hata akajikuta yupo kwa Kimwana,ina maana kwa
Kimwana nako alikuwa naye kwa ajili gani,?’ nikamuuliza.
‘Kimwana,Kimwana….mmh,sikiliza nikuambie ukweli, Kimwana
alivyo, kila mwanaume angejikwaa kwake, alikuwa kajipanga iwe hivyo,..ndio ni
mzuri, ana sura ya mvuto, umbo lililojijenga vyema, lakini yeye hakuwa na
upendo na mwanaume yoyote,zaidi ya kutaka kile akitakacho kwa huyo
mwanaume….bahati mbaya, akawa hajali kuwa anaiangamiza jamii….’akasema na
kutulia.
‘Kwa vipi aiangamize jamii?’ nikamuuliza,na hilo swali
likamfanya aningalie kwa macho ya ukali, akasema;
‘Maswali mengine bwana, yanakera, wewe siulishasikia kuwa
Kimwana alikuwa na ngoma, na yeye ndiye aliyemuambukiza wakili mkuu, na wakili
mkuu akaniambukiza mimi, na sijui wangapi wameshaambukizwa kutokana na yeye na
kwa udadisi wako unajifanya hujui, haya nimeshakuambi kuwa na mimi nina ngoma,
nenda katangaze mahakamani….’akatulia na kuonyesha kuwa alikuwa akivumilia
maumivu fulani moyoni.
‘Una uhakika gani kuwa yeye ndiye aliyemuambukiza wakili
mkuu,huenda wakili mkuu aliambukizwa na mtu mwingine, na wakili mkuu
akamuambukiza Kimwana….?’ Nikamuuliza.
‘Mimi namjua sana Kimwana, namjua kuliko wengine wote,pamoja
na kuwa rafiki yake,lakini mimi nilimfanyia uchunguzi wa maisha yake toka
alipotoka huko kijijini kwao,….na mtu aliyemuambukiza huo ukimwi ni tajiri
mmoja, aliyekuja na mapesa yake, akawa anayamwanga kama njugu, …Kimwana kwa
tamaa zake akajiingiza kichwa kichwa, nilimkanya…..’akasema.
‘Jamaa huyo licha ya pesa,….kweli alikuwa mrembo na kila
akipita mitaani na gari lake la kifahari, wanawake wenye pupa wakawa wakijipitisha
kwake,na yeye hakuwa na hiana, akawa anawamwagia pesa na kuwaachia
virusi….’akasema.
‘Wewe ulijuaje yote hayo kuhusu huyo jamaa?’ nikamuuliza.
‘Mimi ni jasusi
…licha ya kuwa niliacha hiyo kazi, lakini huwa naifanya kama sehemu ya starehe
zangu, na huwa kila jambo nalifanyia uchunguzi kwanza kabla sijaliingia. Siwezi
kukudanganya kuwa mimi sikuvutika kwake,….kama wengine nilitamani awe mpenzi wangu,lakini
mimi nilichowaza zaidi ya wengine ni kuhus hizo pesa, na wapi kazipatia, na
katokea wapi?’ akasema.
‘Uligunduje hayo?’ nikamuuliza.
‘Mtandao,…..na nina washikaji wengi idara ya mambo ya nje,na
….naona huko tusiende, ila kama nilivyokuambia mimi ni jasusi, yule jamaa
niliweza kuingia hadi chumba alichofikia, na nikaweza kupitia mizigo yake, na
hatimaye nikapata kile nilichokitaa…..nilikuta kitabu chake cha kumbukumbu, na
katika maelezo yake, kuna sehemu kajielezea kabia, kuwa siku alipojua kuwa ana
ukimwi, ndipo alipojua kuwa utajiri wake hauna maana tena, na aliapa kuwa
atawaambukiza watu zaidi ya elifu, kabla hajatulia na utajiri wake….’akasema.
‘Uliwafahamisha watu wa usalama?’ akaulizwa.
‘Wewe unanionaje mimi, unaniona kama mtoto mdogo, unafikiri
mimi sina huruma na wanadamu wenzagu,…aliyefanya huyo jamaa akamatwe ni nani
kama sio mimi….lakini niliwaambia kuwa wasinitaje kabisa, maana mimi sio
askari..nashukuru kuwa nilitimiza wajibu wangu, na nikawa nawapitia wale wote
niliowajua kuwa waliwahi kutembea na huyo jamaa kuwaonya, na ikibidi
wakapime….’akasema.
‘Ulifanikiwa kwa hilo?’
‘Nikuambie ukweli, hawa akina dada ambao wameamua kujiingiza
nah ii tabia,….hawajli kabisa, wenyewe wameshajichukulia kuwa wapo kazini, na
kwenye kazi yoyote kuna ajali yake,…kuna hatari yake, na moja ya hatari ni huo
ugonjwa,kwao wao ni tumia upatapo maana
maisha ni mafupi…’akasema.
‘Kimwana naye alisemaje?’ nikamuuliza.
‘Kimwana nilipomuambia, alichukulia kuwa ni ule upinzani
wetu,na hata nilipomshurutisha, hakunijali,akasema hajali, kwani kama anao,
hata mimi nitakuwa nao,na wengine wengi,kwahiyo kifo cha wengi ni
harusi…nilimchukia kweli kwahiyo kauli yake,….’akasema.
‘Kama wewe ulijua hilo kwanini bado ukawa una mahusiani na
wakili mkuu….?’ Nikamuuliza.
‘Kwa kipindi kile sikujua kuwa ana mahusiano na wakili
mkuu,na nilipogundua nilikuwa nimeshachelewa….na hakuna siku nilipoumia sana
kama ile siku niliposikia kuwa alimbaka binti wao wa nyumbani,…oooh, niliumia
sana…’alisema.
‘Ni nani alikuambia hilo…?’ nikamuuliza.
‘Aliniambia yeye mwenyewe, siku hiyo nilimkuta alikila, na
hakuteka kusema kuna nini kimtokea, nilimdaddii sana na hatimaye akaniambia,….,lakini
sijui …maana niliwahi kumkanya yule binti kuwa asimuamini sana huyo jamaa,
maana nilimuona anavyomtizama nilipokuwa mle ndani,….huyu jamaa namjua mimi
vyema, na bahati mbaya hakuwahi kuwa mume wangu, mimi ningehakikisha kuwa
namuweka sawa..’akasema kwa kujiamini.
‘Huyo binti nikamkanya kuwa kama ilitokea hivyo, basi
atafute sehemu nyingine, na kama inawezekana aje tushi na mimi, hakukubali, na
alisema atajitahidi kujilinda kuanzia sasa, na kila mara namuuliza kuwa je kuna
lolote linaloendelea kati yake na huyo jamaa, yeye alikataa kata kata kuwa hana
mahusiano tena na yeye, alipobawa mara moja na safari nyingine, alipobembelezwa
aliacha kabisa kuwa naye tena….’akasema.
‘Ni kweli kuwa alikuwa kesha acha kabisa kutembea na huyo
baba yake?’ nikamuuliza.
‘Hapo nilifanya uchunguzi , na sina uhakika zaidi maana watu
wanaishi nyumba moja, na lolote linaweza kutokea…..ila yeye nilipokutana naye
baada ya kusikia mama yake akiongea na huyo mumewe,na kuambiwa ukweli kuwa
Kimwana ana ngoma, huyo binti alichanganyikiwa kabisa….’akasema.
‘Huyo binti ilikujaje mpaka akakuambia kuwa alisikia hayo mazungumzo?’ nikamuuliza.
‘Nikuambie ukweli kama isingelikuwa mimi ,huyo binti angelishaondoka hapo nyumbani, na
huenda angelishajiua, mimi ndiye niliyemfundisha ujasiri, na nikamfundisha
mazoezi ya viungo kwa jili ya kujilinda, na hata kutumi silaha…’akaniambia,
‘Kwanini umfundishe hadi kutumia silaha,ulikuwa na mipango
gani na y eye?’ nikamuuliza.
‘Najua utasema hivyo kuwa labda nilimfundisha kutumia
silaha,nikiwa na mipango fulani na yeye au bila yeye kujua, lakini sikuwa na
mipango yoyote na yeye….hili ulielewe kiukweli. Wakati namfundisha kutumia
silaha, nilimfundisha kwasababu tu nilimuona akiwa muoga wakati risasi inapolia
kipindi kile tulipokuwa pamoja kama familia ya wakili mkuu, tukienda kuwinda,….’akasema
na kutulia kidogo baadaye akasema;
‘Mimi nilitaka tu kumuondoa huo uwoga, kwa kumfundisha
kuitumia hiyo silaha kwa nia njema kabisa, na baadaye ndipo nikagundua kuwa
kumbe ana kipaji cha kutumia silaha…kipaji cha kulenga shabaha….’akasema.
‘Ulisema kuwa ulipokutana naye siku ambayo, alikuambia kuwa alimsikia
mama yake akimkanya mumewe kuwa asitembee na Kimwana, kwa vile imegundulika
kuwa Kimwana ameambukizwa ukimwi, ulimkuta kachanganyikiwa, ulimasaidieje
katika hali hiyo….maana natumai wewe kama nesi unayajua mambo hayo vyema,
ulitakiwa umchukue akapime….au sio?’ Nilimuuliza.
‘Pamoja ya kuwa mimi ni rafiki yake wa karibu, lakini huyo
binti ana tatizo,…nahisi hivyo…nafikiri ni kutokana na maisha yake huko alipotokea,
….yeye mwenyewe anadai kuwa ana mashetani…..ambayo humsaidia na kumkinga na
matatizo, na hata siku aliyobakwa na huyo baba yake wa kufikia aliambiwa akapuuza,….na
kuna mengine anadai akikanywa hivyo hivyo akapuuzia, …..matokea yake alikiona
cha mtema kuni, na akaniambai kuwa kuanzia sasa hatapuuza tena maagizo
yao…’akasema.
‘Alisema kuwa aliambiwa kuwa kama atapima, kwasasa, ataonekana kweli kaambukizwa huo
ugonjwa, na ili aokoke na hilo tatizo anahitajika kufuata masharti, ambayo ni
pamoja na kufika huko kwao kijijini,huko atakutana na mzee mmoja ambaye
atamfanyia dawa, itakayosafisha damu yake, kwa kupitia hayo marue rue anayoyaita
mashetani, mimi siyajui hayo mambo….’akasema.
‘Sasa kwanini alichelewa kuondoka,..?’ akauliza.
‘Aliniambia kuwa kuna kazi kaagizwa aimalize kwanza kabla ya
kuondoka, na hiyo kazi ni mojawapo ya
msharti
ya matibabu yake,….’akasema.
‘Kazi gani hiyo?’ nikamuuliza.
‘Unaweza mwenyewe kukisia,…na najua kuwa atakuwa kakuandikia
kwenye hiyo barua uliyopewa, …kwani kwenye hii barua yangu kasema kuwa amekupa barua
iliyoelezea kila kitu,sijui kwa vipi kakuelezea, …je kuna barua yoyote umepewa?’akaniuliza
huku akiniangalia kwa makini.
‘Mimi nashindwa kuelewa, maana kutokana na maelezo yako na
tabia yako toka awali, nashindwa kukuamini,inaonekana kabisa kama mlipanga …au
ulipanga iwe hivyo, na hata kumuelekeza huyu binti afanye mambo gani ili mwisho
wa siku, iwe kwa ajili ya maslahi yako,…kwani hayupo hapa kuthibitisha hayo, na
huenda ni wewe uliyemshauri aandike hiyo barua kama ilivyo,…..’nikasema.
‘Mimi sijali kwa vyovyote utakavyowaza wewe…sasa hivi sijali
tena lolote, ndio maana nikakuita wewe kwanza,nakufahamu sana, kuwa unafuatilia
mambo kiundani, ….sio tu nimekuambia wewe, baadaye haya yote nitayaongea kwa
wahusika, mahakamni,kwani sasa nina amani kama huyo binti keshaondoka… cha
muhimu wewe ukitaka kuthibitisha hili, jitahidi umalizie uchunguzi wako kwa
vidhibiti mbali mbali, na ikiwezekana ulizia watu, wapo watu waliona…’akatulia
na baadaye akasema.
‘Watu gani hao walioona,….au…?’ nikataka kumuuliza swali, na
yeye akadakia.
‘Wewe ni wakili, na unajua jinsi gani ya kuwapata, siwezi
kukufundisha hilo, maana utasema nimewapandikiza mimi, …fanya kazi yako
utawagundua…’akasema na wakili mwanadada akatabasamu, kwani hili alishalifanyia
kazi, alichotaka kwa huyo nesi ni maelezo yake binafsi.
‘Nlishamwambia huyo binti kuwa asijali, kama kuna lolote
limetokea mimi nitajitolea kwa ajili yake, na nilimshauri kabla ya yote,
atafute sehemu salama,..kwani hapo anapoishi sio salama tena,… licha ya kuwa
yeye alishaniambia kuhusu mpango wake wa kwenda huko kwao,…’akasema na kutulia
kwa muda.
‘Kwahiyo unafikiri kwa kufanya hivyo ndio umemsadia, huoni
kuwa umemuweka kwenye hatari, ya kushukiwa jambo ambalo halina uhakika ……’nikamwambia.
‘Kwangu mimi nimemsaidia vya kutosha, nab ado nipo tayari
kumsaidia,….nachojutia mapaka sasa ni kuwa sikuweza kuisafisha ile bunduki,
kuondoa alama za vidole, kama ningelifanikiwa hilo, nisingelikuwa na wasiwasi
juu yake, mimi nilikuwa tayari kujitolea kwa ajili yake….’akasema.
‘Hapo sijakuelewa unataka kusema nini…?’ nikamuuliza,
nikikumbuka kuwa kwenye ile bunduki kuna alama za vidole, alaam zile zilikuwa
hazijagundulikana kuwa ni za nani, na wakili mwanadada, alishaingiwa na
wasiwasi na mmojawapo kwenye ile familia huenda aliigusa ile bunduki, lakini ni
nani zaidi ya huyo binti Yatima na kwanini hakutaka kusema ukweli, maana
alimuuliza, huyo binti akakataa kata kata kuwa hajaigusa hiyo bunduki,…
‘Hilo kabati naliogopa, mimi naogopa sana nyoka…..’alisema
huyo binti. Kwahiyo akilini mwake hakuwa na wazo kabisa na huyo binti, kwahiyo
hakuahangaika kabisa kama walivyokuwa polisi, na kwa vile wote walishaamini
kuwa nesi ndiye muuaji, jambo hilo likawa limeachwa kihivyo. Sasa kwa maelezo
ya huyu nesi wakili mwanadada akawa na uhakika wa kile alichokuwa akikiogopa kukifanya.
Alikumbuka siku alipoona ile bunduki, alijaribu kufuatilia
kujua imefikaje hapo, na ndipo akagundua kuwa huyo binti Yatima ana mchumba
wake, …akamfuatilia mpaka akamjua, na kuongea naye kwa kifupi,hakutaka kujua
undani wa mahusiano yao, lakini kwa hali ilivyo, aliona ni muhimu akamshauri
huyo kijana akapime.
******************
‘Samhani sana, kwa kuja kwako bila taarifa, lakini mimi ni
wakili na naisaidia familia ya wakili mkuu katika matatizo, ni pamoja na familia yao, akiwemo yule Binti ,….msichana anayeishi hapo kwenye hiyo familia, ambaye nimeambiwa wewe ni
mchumba wake, au sio…?’nikamuuliza huyo kijana.
‘Sijui nani kakuambia maana mimi na yeye tulipanga haya
mambo yawe siri hadi hapo nitakapojitambusliha kwao, siunajau tena ile familia
ilivyo, unaweza ukafungwa, na ukaoze jela…., lakini haina shaka, ..mimi ndiye
mchumba wake, na natarajia kujitambulisha hivi karibuni…kuna lolote limetokea…’akasema.
‘Nashukuru kwa kuwa muwazi kwangu, na mimi sina nia mbaya, na
hakuna baya lililotokea, ninachotaka kujua ni jambo moja tu, nimeona hiyo
pikipiki hapo nje,na najua wewe ulishamfundisha mchumba wako kuendesha hiyo
pikipiki, alishaniambia kuwa anajua kuendesha pikipiki, je huwa mara kwa mara
anakuazima pikipiki yako?’ nikamuuliza.
‘Ndio….mimi ndiye niliyemfundisha, na katika kumfundisha
huko ndio tukazoeana, na niligundua kwua ni msichana mwema, nawezakuishi naye
kama mke,…nampenda sana,…kwa vile nampenda na kumjali mara nyingi anaiomba
pikipiki yangu, sipendi kumuuzi,ila naogopa sana anapoondoka nayo, hadi akirudi
ndipo moyo wangu unakuwa na amani,….’akasema.
'Urafiki wenu ni muda mrefu?' nikamuuliza.
'Ni wa muda, maana kwa vile nipo karibu na wao, wakihitaji kwenda mahali wananipigia simu mimi, na mara nyingi huyu binti akienda, sokoni ananiita mimi, tukazoeana....'akasema huku akionyesha wasiwasi
‘Siku gani alikuazima na kwenda nayo mbali,akachelewa kurudi….?’nikamuuliza.
‘Kwa mara ya mwisho kuniazima ndipo aliponiambia kuwa
anakwenda mbali kidogo, na akichelewa nisiwe na wasiwasi, ….kawa hali
sikukubali nikasema kama ni mbali nitampeleka mimi mwenyewe, akasema hapana
hiyo safari anahitaji kuwa peke yake, akanisisitizia hadi nikakubali kumpa…..’akasema.
‘Alisema anakwenda wapi?’ nikamuuliza.
‘Hakuniambia kabisa,yeye alisema nisiwe na wasiwasi, ana
ulinzi nyuma yake,…alisema kuna jambo analifuatilia…’akasema.
‘Ana ulinzi nyuma yake,ulinzi gani huo,…?’nikamuuliza.
‘Yeye huwa anadai kuwa hua ana ulinzi wake wa asili, sijui
ni ulinzi gani,….huwa namshangaa sana, anaweza akakuamba jambo ulilolifanya hata
kama hayupo, sijui anajuaje, wakti mwingine namshauri awe mnajimu, ….huwa
namtania hivyo,ila sipendi hiyo tabia na yeye alisema hana tabia hiyo , na wala
hataki kuwa mnajimu…’akasema.
‘Unasema alisema kuwa atachelewa sana , je alichelewa kihivyo,
na wewe ulipoona hivyo, ulifanya nini…?’ nikamuuliza.
‘Nilikwenda kwao, kuulizia na nikakuta hapo nyumbani hakuna
mtu, niliingiwa na wasiwasi sana, lakini baaadaye alirudi, na kuniambia
alichelewa kwasababau ya foleni, na yeye anaogopa sana kupita katikati ya
magari….’akasema.
‘Hukumuuliza alitokea wapi kwenye hiyo foleni..?’
nikamuuliza.
‘Nilimuuliza , akasema alitokea Mwenge,…..alipitia Mwenge,
akiwa katokea sehemu nyingine ambayo hakutaka kuitaja, na mimi sikutaka
kumdaidisi sana…’akasema.
‘Nikuulize kitu kimoja ni muhimu sana….katika maisha ya
sasa, ni muhimu sana kupima kabla ya kuingi kwenye mahusiano, je wewe na mpenzi
wako mlishawahi kufanya hilo..?’ nikamuuliza na yeye akaonyesha uso wa
kustaajabu, akasema.
‘Kwanini nipime, wakati sina mahusiano na mtu mwingine yoyote,
na hata huyo binti hatujawahi kuwa na mahusiano naye, ni ucchumba tu, mtu
mwenyewe mgumu kama nini kasema hadi tuoane kwanza….’akasema huku akionyesha
uso wa aibu,
‘Kupima ni muhimu hata kama huna mahusiano na yeye au na
mwingine yoyote nakushauri ufanye hivyo, na umshauri mwenzako, hilo ni muhimu
sana,kwa ajili ya misha yenu ya baadaye, nakuomba sana, ufanye hivyo,kwani mimi
ni wakili na nawajibika kuilinda ile familia kwa kila hali…’nikamwambia.
‘Mimi nitapima na nakuhakikishia kuwa mimi sina ugonjwa
wowote mbaya, na kama inawezekana nataka siku hiyo tuongezane mimi na wewe na
nitamshauri huyo binti, tuongozane, maana najua hata yeye hana matatizo…mengine
niliyosikia kwa watu siyaamini, kabisaaa..mimi namwamini sana yule binti…’akasema.
‘Wanasema nini hawo watu?’nikamuuliza.
‘Eti baba yake mwenyewe kambaka..haiwezekani, siku
niliposikia hivyo, nilitamani kwenda kupambana na huyo mzee, lakini baadaye
nilipomuuliza huyo binti akasema ni uwongo, nikamwamini.
**************.
‘Ina maana kwenye huyo barua hajakuelezea vyema,….?’
Akaniuliza nesi.
‘Kunielezea kuhusu nini, …maana kaelezea mengi, na hata hili
la mwisho, hakufafanua vyema, na hata hivyo, sikuweza kukubaliana na hisia
hizo, nahisi kuna kitu kimefanyika ili kuficha ukweli,….ndizo hisia
zangu,….ndio maana nataka kusikia maelezo kutoka kwako wewe uelezee jinsi
ilivyokuwa, na naomba uwe ukweli mtupu, ili tumalizane na haya mambo….’nikamwambia.
‘Sawa mimi nitakuelezea jinsi ilivyotokea siku ile Kimwana
alipouliwa,na hivyo ndivyo ilivyokuwa, mengine yaliyotokea, yalitokea ndio,…lakini
haya ninayokuelezea sasa ni siri niliyotaka ibakie na nife nayo ili mwisho wa
siku, ….niweze kumsaidia mtu asiye na hatia,nasema asiye na hatia, kwa vile
aliyotendewa jamii haikuona, ila alichotenda yeye inaonekana ni kosa…ni kosa
kuua,lakini huyo anayeua wengine polepole, haonekani, na anaua wtu wangi.
Nasema hivi mimi nimejitolea kwa ajili yake, hata kama atatokea leo, naomba ….’akatulia
na kujiweka vyema.
`Narudia tena, mimi nimeamua kubeba mzigo wake, naomba tena sana
kuwa mimi nihukumiwe kwa yale yote yaliyotokea, kwa jili yake, …’akatulia.
‘Mimi nilishaamua nife na siri hiyo ,ili kiumbe huyu asiye na hatia asizidi kudhulumiwa katika maisha yake,lakini naona bado uhai wangu
upo, labda ni ili niwe shahidi, labda ni ili nione machungu ya jela, labda
….labda’akatulia na kufumba macho,
‘Ninacho kuomaba kwa sasa ni wewe ukae chini na unisikilize
kwa makini usikie nini kilitoea, lakini kilitokea kwasababu ya hayo yaliyotokea
nyuma, jamii ikaziba masikio, ikafumba macho, haikuona machozi na kilio cha
aliyedhulumiwa, yule aliyeuliwa na huenda kifo chake kikawa cha taratibu,
hakionekani,……na kwa vile yeye ni masikini, ni yatima, hana thamani mbele yao.
Leo hii mtu
mashuhuri, katendewa, kwasababu yeye matokea ya kifo chake ni ya moja kwa moja,
macho na masikio yamefunguka wameona na wanataka kuhukumu, wanamtafauta muuaji,,….’akasema
na huku akiwa kakunja uso kwa hasira, na baadaye akayafumba macho yake tena na
kutulia kwa muda…nikajua eehe,….ni yale yale yaliyotokea siku zilizopita….nikageuka
kuangalia kama docta yupo tayari, Lakini
nikasikai sauti, ikiongea.
Nilipogeuka nikamuona akiwa kaniangalia kwa yale macho yake
ya ujasiri, akasema hivi;
‘Hivi ndivyo Kimwana alivyouliwa…’
NB: Naona nitaandika mambo mengi kwenye sehemu hii, kwani
nakimbilia kukimaliza hiki kisa, lakini kila ninapoandika najikuta kuna mengi
yalitokea na sijayaweka hewani…..msichoke, tunafikia ukingoni….
WAZO ZA LEO:
‘Hivi wewe mbona wenzako wameinuka, wamejenga,na mlikuwa
ofisi moja, ….una tatizo gani?....nilimuuliza rafiki yangu ambaye yupo kwenye
ofisi za kodi.
Swali hilo lilionekana kumumiza sana, akasema ;
‘Sasa hivi sipo huko tena, kwasababu zanu binafsi, ila
kiukweli ninakumbuka maisha ya ofisini, jinsi wenzangu walivyokuwa wakiishi,
wao wakifika ofisini, kazi yao ni kutafuta jinsi ya kupata pesa, mimi nikawa
nahangaika na kazi, uaminifu wangu, kufanya kazi kwangu kwa bidii sikuambulia
chochote zaidi ya mshahara wangu, na wenzangu wakawa wanajijenga,…je uaminifu
wangu na kufanya kazi kwangu kwa bidii hii ndio adhabu yaka….’akasema jamaa
yangu huyo kwa uchungu.
Usijali,…maisha ndiyo yalivyo, huenda ni wengi ambao sasa ni
wazee, na wanajutia hayo maisha kuwa kama wangelijua na wao wangelifanya hivyo…..lakini
ni vyema ufe masikini kwa uaminifu wako, kuliko kuwa tajiri kwa dhuluma, maana
dhuluma haidumu, dhuluma huumiza wengi kuliko unavyozania wewe..je hivyo vilio
vya hawo uliowadhulumu, unafikiri vitaishia hapa hapa tu….tuogope kuishi kwa
kudhulumu,kwani dhuluma ni dhambi kubwa sana.
Ni mimi:
emu-three
2 comments :
Kama naangalia movie,hongera M3, Ubarikiwa sana.
Simply want to say your article is as surprising. The clarity
for your publish is just nice and that i can suppose you're an expert on this subject. Fine along with your permission allow me to take hold of your RSS feed to stay updated with forthcoming post. Thank you 1,000,000 and please carry on the enjoyable work.
Also visit my site ... Phone Counseling
Post a Comment