‘Kwani kumetokea nini?’ nikauliza nilipofumbua macho.
‘Ulidondoka ghafla jana, na inaonekana ulikuwa ukiumwa
kichwa,...kwani ulikuwa umeshikilia kichwa na docta kasema, ulikuwa na maumivu ya kichwa kutokana na msongo wa
mawazo, vipi unajisikiaje kwa sasa…’akaniuliza Tausi.
‘Sijambo,…najisikia ahueani, sijui kwanini kichwa kiliniuma
kiasi kile.sijawahi kuumwa kichwa kiasi kile....’nikasema.
‘Wakati mwingine unaweza ukawa unakabiliwa na mambo mengi
kwa wakati mmoja, na ukawa ukiwaza hili au lile bila kupata jibu la moja kwa moja.
Nikuulize ni nini kikusumbuacho?’ akaniuliza Tausi.
‘Hata mimi nashindwa kuelezea,maana pale nilikuwa najiuliza maswali mengi kichwani, hasa alipokuwa akielezea Docta kuhusu Wakili mkuu na Kimwana, ukumbuke
kuwa Kimwana alikuwa mke wangu …kabla hajaniasi, kwahiyo ukiongelea kuwa
ameathirika, huoni kuwa ninakuwa kwenye njia panda..’nikasema nikiwa na huzuni.
‘Ndio maana tunashauriwa kupima, ukipima hutakuwa na mawazo
tena,…unakuwa umejihakikishia kuwa unaumwa au huumwi, na kama unaumwa, utajua
jinsi gani ya kukabiliana na huwo ugonjwa, wazo la kuwa naumwa nini halipo
tena,..na kama huumwi, basi unajiweka sawa kujilinda….’akaniambia Tausi.
‘Ni ngumu sana kuchukua uamuazi wa kupima, hasa ukijua kuwa
kuna mtu ulikuwa naye kaathirika, lakini sina jinsi inabidi nikapime tu, nijue
moja…’nikasema.
‘Ni vyema kujipima,…na hili linatakiwa kwa kila mtu ili
kujijua,maana siku hizi kuna mgonjwa mengi, ambayo ukiyawahi unakuwa salama, na
ukichelewa unajiweka katika maisha hatarishi….’akasema Tausi.
‘Nashukuru kwa mawazo yak ohayo,na sasa nimejua kwanini
ulikuwa hunipi jibu la moja kwa moja kuwa umekubali tukafunge ndoa,..’nikasema.
‘Hayo ndio mawazo mabaya,ambayo huenda ndiyo yaliyokufikisha katika hali hiyo ya kuumwa kichwa, usiwe na mawazo ya dhana, na ubora wa kuondoa dhana, na
kuchunguza kitaalamu, hukuwa na haja ya kunizania kuwa nina mawazo hayo, ambayo
siyo kweli, lengo langu lilikuwa jema kabisa….’akasema an kutulia.
‘Una maana hukuwa na mawazo hayo, …..?’ nikaulizahuku
nikimwangalia kwa makini,halafu kablahajajibi nikamuuliza swali jingine;
‘Ina maana hukuwa unajua lolote kuhusu kuathirika kwa
Kimwana au mume wa rafiki yako?’ nikauliza.
‘Hata kama nilikuwa najua lolote kuhus hayo, sikuwa na maana
hiyo, lengolangu kwako lilikuwa kujiandaa na kuwa tayari na kitu kinachoitwa
ndoa,…hayo mengine ni mkusanyiko wa maandalizi hayo, na ni kweli inahitajika
kwa wale wanaotaka kuoana kujijua afya zao, ili kukwepa matatizo mengine ambayo
yangeliweza kuathiri afya zenu na vizazi vyenu vijavyo…lakini sikuwa nimelenga huko …’akasema
na kuangalia saa yake.
‘Hata hivyo nashukuru sana, maana kamakweli nimeathirika,
..ningejisikia vibaya sana kama ningelikuwa tumeshaingia kwenye mahusiano,…ningejiona
kama muuaji…’nikasema.
‘Haya ni mawazo duni, maana kila mmoja hajijui, kujijua
kwake ni mpaka kupimwa,na kupimwa sio mara moja tu, inatakwia upime mara mbili
hivi ili kujihakikishia,….kwani wewe una uhakika gani na mimi, maana hatujawahi
kuongea kuhusu mimi kuwa labda nimeshajipimaau la,…kuwa dakitari sio lazima uwe
umejipima, wapo wengi ni madakitar lakini hawajajipima…’akasema.
‘Haiwezekani, yaani mtu upo jikoni, usionje chakula….’nikasema
na kujiinua , nikapima maumivu ya kichwa, sikusiki maumivu tena,…ina maana kuna
kitu kimenisaidia sana, hasa kuongea na huyu mrembo, kuwa kwake karibu ilinipa
faraja sana, nikawa nawaza mbali kuwa kama nitamkosa basi sijui
nitaishije,lakini kama nimeathirika, sina jinsi, siweze kumwingiza binti wa
watu kwenye matatizo…
‘Kwahiyo wewe hujawahi kujipima?’ nikamuuliza.
‘Kwangu mimi, ingawaje ni siri ya kila mtu, lakini
nimeshajipima maar nyingi,….’akasema.
‘Kwanini sasa uliamua kujipima?’ nikamuuliza.
‘Mimi ninakawaid aya kupimaafya yangu mara kwa mara, kuna
kujipima kwa kila mwezi, kuna vipimo vvya kila baadaya miezi mitatu,mitatu…ni
kawaida yangu, na nashukuru kuwa imenisaidia sana,….hii tabia niilijenga pale
nilipooanza kusumbuliwa na maumivi ya kichwa na kuwa kama mtu
aliyechanganyikiwa,….’akasema.
‘Pole sana,na samahani sana kwa kukutia kwenye hayo mateso, …na
kama nitajaliwa nitahakikisha kuwa nalipa hayo mateso niliyokusababishia…’nikasema.
‘Kwa vipi utalipa hayo mateso, maana mateso ya ndani ya
moyo, si rahisi kuyalipa, kwani huwezi jua ukali na ukubwa wa mateso hayo,
kiujumla niliteseka sana, lakini mwisho wa siku nilijilaumu mwenyewe, na
kujiona tena mjinga, kwani unateseka wakati mwenzako hana habari na hayo mateso…’akasema
huyo binti.
‘Nina kuhakikishia kuwa nikipata nafsi ya kukuoa, nitalipa
hayomateso yote,nitakupenda kuliko nilivyowahi kupenda kabla…’
‘Tuombe mungu, atupe huo uzima, na jitahidi kutokuwaza sana,
ili afya yako iiswe matatani, na cha muhimu kama nilivyokuambia,ni kujiandaa,
kwanza kwa kusoma na kujua nini maana ya ndoa na unatakiwa ujiandae vipi, …’akasema.
‘Na pia natakiwa nikapime nijue kuwa nipoje,au sio?’
nikauliza.
‘Hilo unatakiw ahata kama hujafikiria maswalaya ndoa, hilo
ni kwa rika lolote,…ni muhimu kupimaafya zetu. Basi mimi nakuacha, maana
natakiwa kwenda kuwajibika, afya yako ikiwa tayari, tunatakiwa kukutana tena
ili kuliongelea lile swala tulilokatisha, ni muhimu sana tukasikia mwisho wake
tukiwa pamoja…’akasema huyu mwanadada.
‘Swala lipi hilo?’ nikauliza nikiwa sina uhakika
anazungumzia swala gani.
‘Ni nani alimuua Kimwana, na kwasababu gani,…ujue wengi
tumejikuta tukihusishwa…. ,na ni vyema hilo swala likaongelewa na ili
kujitakasa wenyewe…kuna mengi yamejificha hapo, na wengi wanamtizama nesi kwa
jicho la ubaya..sasa ni vyema wote ambao tunaona tunahitaji kusikia mwisho wake
tukamsikiliza wakili mwanadada….’akasema.
‘Sawa, nitafurahi kusikia hilo na kwa muda huo nitakuwa nimeshajijua kuwa nipo
wapi, labda nipo kwenye ramani ya barabara iliyounganiswa toka kwa Kimwana…’nikasema.
Yule mwadada, akatabasamu, akaniangalia na kusema,
‘Ondoa wasi wasi kwa hilo, jenga ujasiri moyoni, ukijua kuwa
kila kitu kinatokea kwa sababu, …kuumwa au kutoumwa,yote hutokea kwa mwanadamu, hakuna anayependa itokee hivyo , kuwa aumwe, hata wale wanaokunywa madawa ya kulevya, au
vitu hatarishi, hawana nia kuwa afya zao ziharibike,kuwa waumwe….ila cha muhimu kwa kila mtu, ni
kutafakari kwa kila jambo, kuwa je nikifanya hili ni nini matokea yake….’akasema
na kujiandaa kuondoka.
‘Ni kweli ,…unanikumbusha mbali sana, nasiku ya leo
sitaisahau kabisa katikamisha yangu,…’nikasema.
‘Hata mimi, inanikumbusha mbali sana,na huenda mungiu
akijalia tutakuwa tukijikumbusha maisha yetu ya raha ya utotoni, natamanai kama
ile siku ingelirejea tena…’akasema na akabusu shavuni na kuondoka.
************
Wakili mwanadada alitulia kuhakikisha kuwa kila mtu kakaa sehemu
yake, akiwa mkoba wake, akatoa makaratasi fulani, akawa anayakagua halafu
akatuangalia sote, …alipitia kila mtu mmoja mmoja kumwangalia usoni,nala ilipofika
kwangu akatabasamu. Na mimi nikatabsamu, kwani alitabasamu lile tabasamu la nje
ya mahakama.
‘Nawashukuru sana kukubali mualiko huu, na nashukuru pia
kuwawote mpo salama, na mengi yamepita, na mengi mumeyasikia,ila kuna mengo
bado yanafanyiwa kazi , na sis hatuna mamlaka nayo, cha muhimu ni kuangalia
yale yanayotuhusu kwanza…’akasema wakili mwanadada.
Mimi hapa ninachotaka kuelezea ni yale niliyogundua
katikauchunguzi wangu, ….nikishirikiana na wenzetu wa usalama, kwani bia wao
nisingeliweza kugundua haya, na sikutaiwa kuyaelezea awali kwasababu yalikuwa
yapo mbele ya mahakama, na sasa nimeshapewa kibali kuyaelezea bila wasi wasi,
na mengine mtayasikia pindi, maana baadaye msemaji wa mahakama atakuja hapa kuwalezea
mwenyewe,..’akasema na kutabasamu.
‘Wiki mbili zilizopita nilikuwa na huzuni sana, maana mengi
yaliyoajiri na niliyokuja kugundua yalikuwa ya kunitia simanzi, maana kuna watu
ambao wanajikuta matatizoni, lakini sio kosa lao, ….na sheria haitatambua
hilo,kama umetenda kosa,basi hukumu ipo wazi,…’akatuliakidogo.
Mimi nitaanzia moja kwamoja siku ile nilipogundua ile silaha
iliyofanyia mauaji,….siku ile nilipofika pale kwenye lile kabati ambalo
lilihifadhia nguo na matakataka mengine ambayo yalikuwa hayatumiki, na kwa
taarifa za yule binti wa pale nyumbani, alisema humo pia paliingia nyoka, na
kwasaabbu ya huyo nyoka hakuna aliyeweza kuligusa hilo kabati.
Mimi sikujali, nililifungua, nikiwa na tahadhari zote,…na
nashukuru nyuma yangu alikuwepo mtu wa usalama, na mara nikaiona hiyo bunduki,
ikiwa imetumbukizwa hum ndani,na jinsi ilivyowekwa, kama vile kuigeshwa na
mlango,ikadondoka kwa nje, nikaiwahi mikononi,…
Ina maana kuwa muwekaji aliiweka kwa haraka, na kuufunga
mlango wa hilo kabato kwa haraka,kwahiyo ile bunduki ikawa imejiegemeza kwa
ndani kwenye huo mlango, na kama mlango huo usingelikuwa imara , …basi mlengo
huo ungelifunguka na bunduki ingelidondoka....
‘Kwa matizamo ule, ilimaanisha kuwa muwekaji aliiweka kwa
haraka,…akiwa anakimbia, au wakati anaiweka alisikia jambo, kwahiyo akaiweka
kwa haraka na kufunga mlango wa hilo kabati….kwa kujihami kuonekana, au kwa
kuogopa jambo fulani.
Niliwaomba watu wa usalama kuhakikisha kuwa humo hakuna
nyoka,na alama zote za vidole zimechukuliwa,…na walipotoa kila kitu, walikuta kuwa hakuna nyoka...ili kulikuwa na kitu kama kiota cha nyoka, kuwa likuwa akiishi hapo awali,... na alama
zote za vidole zilichukuliwa, na ile silaha ikawekwa chini ya usalama.
‘Mungu wangu imefikaje hapohiyo silaha..ooh, mungu wangu…’nilisikia
kilio cha yule binti baada ya kuichukua ile silaha, niligeuka kumwangalia
nikakuta kashika kichwa, huku akiingalai ile silaha kwa macho ya uwoga.
‘Unajua lolote kuhusu hii silaha?’nikamuuliza.
‘Mmmh,ndio najua ni silaha ya baba, huwa inakaa kule ofisini
kwake,sijuiimefikaje hapo..’akasema.
‘Kwa mara ya mwisho uliiona wapi hii silaha?’ nikamuuliza.
‘Kwa mara ya mwisho…sikumbuki, maana huwa inawekwa huko
ofisini kwake…’akasema huku akiwa anaingalai ile silaha kwa wasiwasi.
‘Ulishawahi kuitumia hii silaha kabla…?’ nikamuuliza.
‘Na wewe maswali yako bwana, nitaitumiaje na wakati silaha
hiyo inakaa huko kwa baba, na inafungiwa, niliwahi kuingia zamani sana wakati
nasafisha hicho chumba, na baadaye tukapigwa marufuku kuingia huko ndani,
sijawahi tena kuingia huko…’akasema kwa kujiamini.
‘Nimekuuliza hivi, ..au nikuulize hivi,katika misha yako
ulishawahi kuutumia silaha kama hii?’ nikamuuliza.
‘Ndio, wakati tunakwenda kuwinda na akina baba ,baba alikuwa
akitupa na sisi tutumie,maana mwanzoni nilikuwa naogoapa snakuutumia, ..nikisia
mlipuko wake, nashituka na kuhsika masikio,…akaona ni vyema na mimi nikaondoa
uwoga …akanifundisha na mimi…’akasema.
‘Wakati anakiufundisha, …mlikuwa na mama na nani wengine?’nikamuuliza.
‘Wakati mwingine nilikuwa na mama, na mama mdogo,na watu
wengine.
‘Mama mdogo ni nani?’ nikamuuliza.
‘Ni yule nesi…..ndugu wa mama’akasema.
‘Kuna kipindi mlishawahi kwenda wewe na baba peke yenu…?’
nikamuuliza.
‘Mmmh,hayo maswali siyapendi, …maana naogopa, …’akasema
‘Usiogope, mimi nipo pamoja na wewe, na hili nakuuliza kwa
ajili ya kukulinda wewe, ukinificha unaweza kuwa hatarini, sema kila kitu, ili
nijue jinsi gani ya kukusaidia…’nikamwambia.
‘Unisaidie kwa nini……kwani nimesema kuwa nahitaji kusaidiwa,
kwani kuna tatizo gani na mimi….naona kama unanisakama sana…’akasema.
‘Hili ni swala la kawaida tu,na ni muhimu mimi kama wakili
nikajua, maana nyie wote mpo kwenye orodha ya watu ninaotkaiwa kuwasaidia,
hajakuambia mama, kuwa mimi nawasaidia nyie, kuhusiana na kesi, iliyopo
mahakamani, kwahiyo sema ukweli, ili asije akajikuta kwenye matatizo, na ujue
kuwa kama yeye yupo kwenye matatizo na wewe pia utachukuliwa kuisadiai polisi….’nikasema.
‘Ohh, hayo tena makubwa, …lakini kuhussu kwenda na baba
kuwinda, mama alikuwa hajui, …na baba likuwa kinishawishi tu…na ilitokea wakati
ule….na kunilazimisha,….mimi sikupenda…’akaanza kulia.
‘Ulishaniambia hayo, na nilishakuambia kuwa ili uweze
kuyashinda hayo, ni lazima uwe jasiri, uwe tayari kukubali matokea, maana
yalishafanyika, na wewe hukuondaiwe hivyo, au ulipenda iwe hivyo, ulikuwa
ukimpenda baba yako?’ nikamuuliza.
‘Skupenda,…ila yeye alinishawishi, …akanibembeleza, na ndio
akawa annipeleka huko kwenye kuwinda, na…siku baadaye ndio akanilizamisha
kufnay naye mabaya,…akansihika kwa nguvu…baadaye akawa ananibembeleza kuwa
ananipenda…’akasema.
‘Ina maana tendo hilo halikutokea mara moja…?’nikamuuliza.
‘Mara mbili…mmh, hapana mara sijui ngapi zile…nikawa
nimezoea, ila sikupoenda maana nilimuona kama baba yangu,….baadaye ndio
nikamwambia mama, maana niliona imezidi na mama akijua itakuwa ni matatizo.
‘Je wewe hizo siku zote ulikuwa ukisikiaje,…ilikuwa ina
kuuma sana, au ulikuja kuzoea nakuona jamboo la kawaida?’ nikamuuliza.
‘Mwanzoni niliumia sana, nililia sana…na baba alipoona hivyo
akawa anaibembeleza, na ndio akawa ananipelak huko kuwinda ananionyesha jinsi
ya kutumia silaha, nikawa naijua na nikawa nimejifunza kuitumia,…..na kuna siku
tukiwa na mama mdogo, mama mdogo ananifundihs jinsi y akulenga shabaha, nikawa
najua kulenga vizuri sana….kama yeye…’akasema.
‘Je hukuwa ukiumia sana, kuwa umetenda machafu na baba
,wakati kuna mama yako,….?’nikamuuliza.
‘Iliniuma sana…nimekuambia sikupenda iwe hivyo….alinishika
kwa nguvu….’akaanza kulia.
‘Unajua kuwa baba yako alikuwa na mwanamke mwingine zaidi ya
mama yako…?’ nikamuuliza.
‘Yaani we acha tu,…sijui kwanini siku nilipomuona baba na
yule mwanamke, nilumia sana,maana niliwaona wakiwa kitandani…nilumia sana,…nilitamani
nimuambia mama, nikashindwa…sijui kwanini nilumia kiasi kile,…unajau baba
alishaniambia kuwa ananipenda mimi,sasakumbe anawapenda wengine, nilimuona kuwa
ni muongo…’akasema na kuona aibu.
‘Ina maana uliingiwa na wivu?’ nikamuuliza.
‘Sijui ..sielewi, ila nilimchukia sana huyo mwanamke….nilimuona
kama mwizi…nilimchukia kupita kiasi,..’akasema.
‘Hukumwambi mama yako?’ nikamuuliza.
‘Sikuweza kumwambi siku hiyo..ila siku ile niliposikia mama
akiongea na baba kuhusu huyo mwanamke, ndipo nikaamua kumwambia mama ukweli
kuwa nilishawaona wakifanya machafu yao’akasema.
‘Ulisikia nini wakiongea mama na baba yako?’ akaulizwa.
Hapo akaanza kulia…..alilia kwa muda mrefu na baadaye
akasema;
‘Mama alimwambia baba kuwa huyo mwanamke anayetembea naye
imegundulikana kuwa kaathirika, na moja ya kazi zake ni kuambukiza watu…sasa
fikiria, kama huyo mwanamke katembea na baba, na baba katembea na mimi, si na
mimi nimeathirika….’akaanza kulia kwa kwikwi….
‘Huyo mwanamke anaitwa na nani?’ nikamuuliza.
‘Anaitwa….Kimwana.
NB: Sehemu hii nimeiandika kwaharaka kidogo juu kwa juu, na sijapata muda wa kuipitia, kama kuna makosa naomba tusameheane, na kama yanahitaji kurekebishwa uwe na mimi niambie ili nijue.
WAZO LA LEO: Dhana nyingi kichwana ni hatari, na zikizidi sana huletwa msongo wa mawazo, ...kiafya sio vyema, na kama unaumwa, nenda kapime, usiweke dhana,kuwa labda naumwa ugonjwa huu au ule, vipo vipimo, wapo wataalmu, tuwaone, na pia tujenge tabia ya kukagua afya zetu mara kwa mara.
Ni mimi:
emu-three
1 comment :
Huyo dada hapo nilisoma naye, sijui siku hizi yupo wapi?
Post a Comment