Wakili mwanadada alionekana kuwa na mawazo mengi, na hata
pale nilipomuuliza anasumbuliwa na nini hakutaka kuniambia ukweli, yeye alisema
kuwa kuna jambo analifuatilia hajawa na uhakika nalo, na hawezi kusema lolote
kwa sasa.
Mimi sikupenda kumsumbua kwasababu nilikuwa na mawazo yangu
mengine, nikasubiri muda ufike twende huko hospitalini kuwaona wagonjwa wetu ili
tujue wanaendeleaje. Nakumbuka hata nilipomuona mkuu mudamchache uliopita naye
alionekana mwenye kukwera na jambo, maana kila alipoongea na vijana wake kwenye
simu alionekana kutoa amri zahasira, nikajua kuna jambo halijaenda vyema.
‘Vipi kuna jambo ambalo mimi silijui maana mimi nijuavyo
kesi imeshakwisha iliyobakia ni wagonjwa wapone wafikishwe mahakamani….au sio
mkuu?’ Nikauliza.
‘Mambo ya sheria haya sio mchezo,…huwezi ukajua kesi imeisha
mpaka ifike mahakamani na hukumu itolewe, …na kila siku tunaona mambo mapya
yanajitokeza…ambayo yanatutia wasiwasi’akasema mkuu.
‘Kwanini unasema hivyo?’ nikamuuliza.
‘Wakili wa nesi anadai mteja wake hajamuua Kimwana, na yote
aliyoyazungumza kipindi kile ilikuwa na katika hali ya kiugonjwa, na ilikuwa
kama shinikizo, ….’akasema mkuu.
‘Lakini kwanini kauli hii
ije baadaye, kwanini hakusema wakati ule nesi anaongea mwenyewe?’
nikauliza.
‘Usifikiri wao ni wajinga, walikuwa wakiongea vile wa kivuta
muda, na kama unakumbuka vyema, hakuna mahali nesi alitamka kuwa yeye ndiye
aliyemuua Kimwana, kama ulifuatilia maelezo yake vyema,…inadaiwa kuwa yeye ndio
kweli alifika pale lakini sio yeye aliyemuua Kimwana kama walivyofika mke wa
wakili mkuu na rafiki yake,…’akasema mkuu.
‘Na hiyo bunduki aliipatapataje…?’ nikauliza.
‘Hapo ndio hatujapata ufafanuizi , na kauli yake mwenyewe…’akasema
mkuu
‘Huoni kwamba anaficha ukweli,…..’nikasema.
‘Ndio maana nakuambia wao kila wanaloliongea walishalifanyia
kazi, na nia na lengo lao ni kiifcha ukweli,lakini yote yatafikia mwisho, kwani
jopo lamahakimi limekwenda huko hospitalini, ….’akasema mkuu.
‘Kwanini liende jopo la mahakimu?’nikauliza.
‘Kuna maamuzi nyeti ambayo yanahitaji vichwa zaidi ya
kimoja, ….hayo tumewaachia wao wanaojua sheria zaidi…’akasema mkuu.
‘Nakumbuka wakili mwanadada alisema kuwa ana ushahidi wote
wa kumweka ndani huyo muuaji wa Kimwana?’ nikauliza.
‘Ushahidi anao, lakini sehemu kubwa tulitegemea kauli ya
Nesi mwenyewe ,kwani alionekana kukubali, na ukiviweka vielelezo unamkuta yeye
ndiye mshukiwa, lakini kwa kauli ya wakili wao, inaonyesha dhahiri kuwa kuna
jambo wao wameshalifanyia kazi, na huenda nesi akiwa katika hali nzuri atapinga
kauli zake za mwanzo…kuna jambo baadaye tutalisikia kwa wakili mwanadada’akasema
mkuu.
Baadaye nikiwa nawakili mwanadada nikamuuliza ;
‘Ina maana hali ya nesi inaendeleaje?’ nikauliza.
‘Bado haijawa njema, lakini kwa mtizamo wa dakitari, ile
hali mbaya imeshatoweka…mengine ni masharti ambayo ni muhimu zaidi’akasema .
‘Masharti gani hayo, kuwa wasifanye kazi nzito, au ?’
nikauliza.
‘Hayo ni moja ya masharti, lakini wanatakiwa watulize vichwa
vyao, na wasifikirie sana kuhusu kesi iliyopo mbele yao, ….na hili tumeliongea
na hakimu na watu wa sheria, maana mambo mengine yanahitaji ubinadamu zaidi…nahisi
ndio maana jopo la mahakimu limekwenda huko….’akasema.
‘Umezungumza kuhusu kesi, na nakumbuka mara ya mwisho
hukuweza kumalizia yale maelezo,ulifikia pale ulipoigundua hiyo bunduki
ilipokuwa imefichwa, je ni nani aliiweka hapo ulipoikuta hiyo bunduki, ni nesi
au ni nani, ?’nikauliza.
‘Hilo tutaliongelea kwenye kikao cha leo, leo kuna kikao
muhimu sana, na nashukuru kuwa nesi na wakili mkuu wamekibariki wakiwa na
wakili wao, kwani wao ndio watu muhimu niliokuwa nikijaribu kuhakikisha kuwa
wanalindwa…. ,hata kama ni wakosaji ,lakini kuna mambo mengine kisheria ni haki
ya mtu…kwahiyo jiandae leo kuna kikao muhimu sana ambacho tutaongea mambo yote…’akaniambia
huku akionyesha uso uliojaa huzuni
‘Sawa ,lakini leo nakuona huna raha, sio kawaida yako kuwa
hivyo, nahiisi kuna jambo kubwa sana, nakama hutaki kuniambia siwezi
kukulazimisha….’nikasema.
‘Usijali, …hakuna jambo kubwa sana, ila ni hali ya kawaida
ya kibinadamu, tutaongea hayo baadaye kikaoni…’akaniambia na mimi nikaondoka
kwenye mishe mishe zangu.
**********
Kikao kilikuwa na watu wale wale ambao tunahusika na hii
kesi, alikuwepo mke wa wakili mkuu, rafiki yake, wakili mwanadada , mkuu kama
mwenyekiti wa hicho kikao, na nilimuona docta ambaye nilikuja kumgundua kuwa ni
bosi wa hospitali ya nesi, sikujua kwanini naye yumo humo.
Siku hiyo kwa vile najua nitakutana na Tausi nikavaie zile
nguo zangu, kwani nilishaanza kujiweka kinamna ya kipekee, na kwa ushauri wa
walili mwanadada, ukitaka kusomea sheria lazima uwe mtanashati, kwahiyo ni kavaa
ile suti yangu maridadi na tai,…huwezi aminii kuwa ni yule mbeba maboksi kwa
wahindi.
‘Ndugu zanguni, hiki ni kikao ambacho tunaweza kukiita kikao
cha hitimisho ya kesi yetu ,licha ya kuwa hatupo mahakamani, lakini baada ya
maongezi na hakimu na jopo lake, ilifikia hatua ya kukubalika kuwa kesi hiyo ihukumiwe
ki namna ya kipekee kabisa, wao wenyewe wanajua jinsi gani ya kutoa hiyohukumu,
na sisi hapa halituhusu sana….’akasema mkuu.
‘Kwanza tuna mengi tunahitaji kuyafahamu, na mojawapo ni je
ni nani hasa alikuwa mmuaji wa Kimwana, hili atakuja kuliamlizia wakili
mwanadada baadaye, lakini kabla ya hilo, labda nimtambulishe dakitari
wetu,ambaye ni bosi wa nesi,…Nesi ambaye wengi tunajua hali yake ilivyo, na
anahitaji utulivu, anahitaji matibabu na tunamumbea mungu apone, …..’akatulia
mkuu.
`Docta natumai hatua zote za kisheria zimefuatwa, na
tunakuomba useme lile tulilokuomba ukitumia utaalamu wako,najua unajau jinsi
gani ya kuliweka hili swala sawa masikioni mwa watu ikizingatia kuwa wengi wao wanalijua,….’akasema
mkuu.
Yule docta alisimama nakukohoa kidogo,akasema;
‘Mimi ni dakitari mkuu wa hospitali yetu hiyo hapo mbele,ninashukuru
sana kuwa nami nimeweza kujumuika katika kesi hii, na nilikuwa tayari kutoa
ushahid wangu kama ungelihitajika kisheria….kuna mengi yametokea na ukiangalia
kitaaluma inatatiza sana, …lakini unajikuta kuwa huna jinsi inabidi ufuate
sheria,…
Naona nisiwapotezee muda sana, labda niingie moja kwa moja
kwenye jambo nililoitiwa hapa, ambalo hata nesi, na wakili mkuu, waliniomba
niliongolee kwenu, …sio kwamba tu, tumeamua kufanya hivyo, hapana, wao wenyewe
walisema siku wakiwa na nafuu watawaambia kila kitu, lakini kwa sasa wameomba
tuwaambieni ukweli ulivyo,…’akatulia docta mkuu.
Mimi pale nilipo moyo ukaanza kwenda mbio,nikiwaza
mengi,maana hali ya mabadiliko ya wakili mwanadada, na mkuu,i…sasa kaja
dakitari, mambo haya yote, yalionyesha kuwa kuna jambo jingine, nikaona niwe nasubira
,maana kama walivyosema wao leo ni hitimisho…..labda kila kitu kitawekwa wazi,
na kila jambo lina mwisho wake.
‘Nilimsifu sana nesi kwa ujasiri wake,….’akaendelea kuongea
doacta.
‘Hasa siku ile alipokuja ofisni kwangu, kuniambai lile
lilokuwa moyoni mwake,….. lakini sikujua kuwa angelichukua hatua hiyo
aliyoichukua sasa ya kunywa sumu, na hata nilipokutana naye hivi karibuni,na
kumuuliza vipi imekuwaje mpaka kufikia hatua hiyo, yeye alishindwa kuniambia
lolote zaidi ya kusema kuwa `we acha tu,
sio kuwa napenda kufanya hivyo,ila …hali imenilazimu…’akatulia docta.
‘Siku hiyo nesi alipokuja ofisini kwangu, hakuwa na raha, na
ni kipindi ambacho wakili mkuu yupo katika hali mbaya ya shinikzo la damu,na aliniambai
kuwa wakili mkuu, alikuwa mtu imara sana, afya yake ni thabiti tangu zamani,kwahiyo
yeye anashangaa sana kumuona akiwa na mabadiliko hayo ya shinikizo la damu, na
kuonyesha kwua kuna jambo jingine kubwa….’akasema.
‘Jambo gani ..?’ nikamuuliza.
‘Licha ya matatizo hayo ya kuchukuliwa mapicha mbaya ambayo
nia na lengo ni kumuzalilisha, na kumkomoa, …kama alivyosema nesi,lakini
alisema kuwa hayo ysingeliweza kumtingisha huyo wakili mkuu kama anavyomjua
yeye, yeye anahisi kuwa kuna jamboo jingine limeathiriafya yake…’akasema huyo
docta.
‘Nikamwambia kwani kuna nini cha zaidi …umeshachukua vipimo
vyake vyote kama nilivyomuelekeza?’ nikamuuliza.
‘Ndio nimeshachuku vipimo vyote…lakini kuna kipimo kimoja
ambacho hukukiweka,lakini kwangu mimi niliona ni muhumu sana kiwepo hicho
kipimo, ….’akasema huyo nesi.
‘Kipimo gani,….maana hapo naona unaniingilia kazi yangu’nikamwambia
kwa hasira.
‘Samahani sana docta,…sina nia mbaya ya kukuingilia katika
kazi yako,…. lakini kuna umuhimu huo, maana mimi namjua vyemaa huyo mgonjwa,
namjua sana hata kuliko anavyojijua yeye mwenyewe, haya mabadiliko yaliyoingia
mwilini mwake sio ya kawaida lazima kuna jambo ingine tunahitaji kulichunguza…’akaniambia.
‘Haya kuwa muwazi , kwasababu hatuna muda hapa…’nikwambia.
‘Naomba tumempime na Ukimwi….’akasema.
Aliposema neno hilo huyo docta,mimi pale nilipokuwa mwili
wote uliisha nguvu, akili yangu ikaanza kuchora ramani, …ikianzia kwa huyo
wakili mkuu, ikaja kwa Kimwana na mistari ya ramani nikaiona ikiwa inaelekea
kwangu,...wili mzima ukafa ganzi, lakini nikajipa moyo nakuwa na subira. Docta
akawa anaendelea kuongea
`Mimi sikumjibu kitu, nikatulia kwa muda, na hilo lilikuwepo
akilini mwangu maana tumekuwa na kawaida ya kuwashauri watu kupima, hata kama
hali zao sio mbaya kiasi hicho, ni vyema tu kila mtu kwa wakati wake akapima
afya yake, ili kujijua, na sio kwa kujipima tu kwa ajili ya ukimwi, lakini pia
kwa ajili ya kujua afya yako…ni vyema tukaw an utamaduni huo….’akatulia docta.
‘Yule nesi ni rafiki yangu wa karibu sana, tangu afike pale
amekuwa ni mtu muhimu sana kwangu, na namshukuru sana kuwa amekuwa akichapa
kazi, na kujitolea kwa moyo wake wote,utafikiri yeye ndiye docta mkuu, …’akatulia.
‘Na mara nyingi naheshimu sana kauli yake, nikamwambia,
..wewe si unajua kanuni za mgonjwa, hatuwezi kumpima mgonjwa bila ya rizaa
yake,na pili mimi sioni umuhimu wa kukimbilia hicho kipimo kwa sasa kwani
ukimwambia mgonjwa kama huyo kwa sasa utamzidishia hayo mataizo aliyo nayo…’nikasema.
‘Ni vyema tukamuwahi sasa hivi kwani hali aliyo nayo, ni
kuwa anajihisi kuwa keshapata huo ugonjwa, na nahisi ni kutokana na mawazo hayo,
ndiyo maana hali yake inakuwa ya
mashaka,..ndio maana anajikuta akipatwa na shinikizo la damu . Kama
nilivyokuambia mimi namjua vyema sana huyu mtu nimeishi naye kwa muda mrefu,…ni
mtu mwenye ujasiri mkubwa,…afya yake ni njema …’akasema nesi.
‘Kwanini unahisi hivyo, kuwa huenda kaathirika?’
nikamuuliza.
‘Kwasababu namjua vyema….’akasema na baadaye akainama chini
kwa uchungu , na aliponitizama mimi niliona machoni akiwa na machozi, nikaona
hapo sasa mimi kama docta nahitajika kuwa makini. Na ikizingatiwa kuwa huyo ni
mfanyakazi wangu, na mfanyakazi wangu,kwangu ni sehemu ya familia yangu.
‘Hebu niambie vyema, kumbuka kuwa wewe ni nesi, na ni kiyoo
cha wagonjwa, wewe ni mtu muhimu sana, na nakutegemea sana kuwa mfano kwa
wengine, ….naomba unieleze ukweli, hasa kuhusu wewe mwenyewe maana wewe ndiye
mpenzi wake wa karibu…’nikamwambia.
‘Docta mimi na Kimwana ni marafiki sana, na mara nyingi hakuwa
akinificha mambo yake,hadi pale tulipoanza kuonyeshana ubabe, na kugeuka kuwa
maadui wakubwa…mwanzoni tuliivana sana, na licha ya kuwa marafiki kihivyo ,
hakuwahi kunitamkia lolote kuhusu yeye mwenyewe kuwa ana tatizo lolote la
kiafaya,..kwanza hajawahi kuumwa, kabisa, ….’akatulia
Alipomtaja Kimwana mimi nikawa akili imekufa ganzi,….nikaanza
kuhisi mwili ukiisha nguvu,na nilitaka kugeua kumwangalia rafiki wa mke wa mkuu
yaani Tausi, lakini kichwa hakikuweza kugeuka, nikaanza kukumbuka maneno yake
kuwa na kauli yake ile ya kusema`tupeane
muda …’ kumbe kulikuwa na maana kubwa sana, nikajikuta kichwa kikiuma sana…..
‘Kwahiyo unataka kusema nini, kuhusu wakili mkuu, ….maana
hapa unachanganya watu wawili, wakili mkuu na Kimwana,….’nikamwambia huku
nikikumbuka kuwa aliwahi kuniambia kuwa wakili mkuu anatembea na
Kimwana, na
ndio maana hana raha.
`Docta siku moja nikiwa nyumbani kwa Kimwana niligundua
vyeti vyake alivyopima, na hili nililigundua kipindi ambacho kakambia, na kwa
vile mimi ni rafiki yake, nilikuwa nakujua kwake vyema, kwenye nyumba yake ya
awali ambapo kulikuwa na vitu vyeka, nikafika kwake kuviweka vitu vyake sawa, na
huku nikifanya akzi ya ngu ya ujasusi,…ndipo nikagundua kuwa alishawahi kupima
na aligundulika kuwa kaathirika….’akaniambia na kunionyesha vyeti vyake.
‘Eti nini….?’ Mimii nikajikuta nikitamka kwa nguvu bila
kujijua, na wote wakageuka kuniangalia.
‘Ndio ukweli ulivyoo kuwa Kimwana alikuwa kaathirika, na
nimepewa kibali cha kumuongelea hapa, msije mkasema docta nakiuka miiko,
hapana, sheria zote zimefuatwa, ….na kutokana na yeye ndio maana wakili mkuu
alipogundua hilo, akawa hana raha,….hadi tulipompima baada ya kupata ushauru
nasaha,nakweli na y eye kaathirika…..katuomba tuwaambie hili , na hata mke wake
anajua…’akasema docta na kumwangalia mke wake ambaye alikuwa katulia kimiya.
‘Haiwezekani…’nikasema huku kichwa kikiniuma hasa, na yale maumivu
ya kichwa yalinifanya nishindwe kuvumilia, nikainuka ple nilipokuwa nimekaa
kwenye sofa na kwenda kukaa kwenye kiti cha chini huku nimeshikilia kichwa,….kilikuwa
kinauma kupita maelezo, nikawa nahangaika na mara giza likatanda usoni,
sikukumbuka jingine tena zaidi ya maumivu na mara giza giza nikapoteza fahamu,……
NB: Visa vyangu
ni vya uhalisia, nI matukio yaliyotokea, najaribu kuviweka kitamthiliya ili viwe na mvuto, naomba kila unapoona nakosea usisite kunisahihisha ili niweze
kuboresha zaidi.
*********************************************************************************
WAZO LA LEO: Ukweli
unauma, lakini ni heri ya kuwa mkweli kuliko kuwa muwongo , hata kama uwongo
huo,ni wa kumfanya mwenzako akupende, au bosi wako akuone ni wa maana,….Kuna
watu wana tabia ya kuishi maisha ya kujipendekeza, ili waonekane wao ni
zaidi,na hata inafikia hatua wanaongopa, wanasema uwongo au hata kuwazuliwa
wenzao uwongo, ili waonekane wao ni wema. Hiyo sio tabia njema.Tuwe wakweli
hata tukiona kuwa tumekosea,ni vyena tukakiri kuwa hapa tumekosea, ilitujifunze,
…
**********************************************************************************
TOKA MAJUMBANI:
Zoezi la kundikisha vitambulisho limekuwa ni kazi kubwa na kugeuka kuwa kero,
kwa wananchi wa kawaida, imebidi watu kudamka saa kumi alifajiri, ili tu
wakawahi namba, …kwani waandikishaji wanasema wao kwa siku wanahitaji
kuandikisha hadi watu mia nne…..kwahiyo hugawiwa namba….sijui kuwa taratibu hizo
zipo sehemu nyingine….lakini huki Kipunguni B ndivyo inavyofanyika.
Na wale wanaofanya kazi ya kuandikisha nao kama binadamu wengine
mikono inachoka, na watu nao wanachoka kusubiri maana inabidi waache kazi zao kwa siku nzima ili
kufanikiwa kuandikisha,…na kuna wengine kama kawaida yetu wanachukulia nafasi
hiyo kuwarubuni watu ili warizishe tamaa zao,…
Labda tungalie njia yingine rahisi kama ile ya wajumbe
kupitia watu wake majumbani, au fomu hizo kugawiwa kwa kila mtu, au hawo watu
kuongozana na wajumbe luwapitia watu, na wale wa maofisini kuzipata hizo fomu
ofisini, na yule anayehitaji msaada wa kundikiwa ndiye amuone huyo
muandikishaji, ….ili kupunguza kupoteza siku nzima au siku mbili nzima.
Ni mimi:
emu-three
2 comments :
Hey! I know this is somewhat off-topic however I needed to ask.
Does operating a well-established blog such as yours take a
massive amount work? I'm brand new to writing a blog however I do write in my journal everyday. I'd like to start a
blog so I can easily share my own experience and views online.
Please let me know if you have any ideas or
tips for brand new aspiring bloggers. Appreciate it!
Also see my webpage :: acrylic displays
Hey, `Anyon', above
To start a new blog is easy,
You have to create an account with Google, and then you visit the Blogger homepage https://www.blogger.com/....therein you will get everything you need for start a blog!
Post a Comment