Usemi huu hujafa
hujaumbika nimetokea kuupenda sana, nikiimanisha jinsi gani mtu unavyoweza
kukutana na mambo mengi ya ajabu ambayo hukutegemea kukutana nayo. Kila hatua
unakutana na jambo la kushangaza, ulitarajia iwe hivi lakini unakuta inakuja
kuwa tofauti kabisa, na kubakia kushangaa.. .
Hii inaonyesha kuwa sisi ni
binadamu tu,yapo mengi ya ajabu, na huwezi kuyamaliza, kuyamaliza kwako labda
ile siku unawekwa kaburini…’alisema rafiki yangu huyu, siku anaendelea
kunimalizia kisa hiki, nikatulia kumsikiliza.
Huyu wakili mwanadada, ninawea kumuita kuwa ni jembe, ni
wale wanawake wenye akili ya ziada, dada huyu hana papara katika kazi yake,
anakuwa makini na kinachomsaidia sana ni kuwa yupo karibu sana na watu wa aina
zote, hajali kuwa huyo mtu yupoje,….
Hebu turejee kidogo kule hospitalini tuone nini kinaendelea
maana kule tuliacha wagonjwa, na mimi ilibidi niache shughuli zangu niwe
nawatembelea wagonjwa, maana sasa hawo wagonjwa wameshakuwa jamaa zangu.
Ukumbuke tulishaelewana na yule mchumba wangu wa utotoni, lakini
kukutana kwetu ilikuwa ni nadra sana kwani yeye ni mtu wa kazini, na akitoka kazini
anakuwa kwake na mara nyingi anahitaji mudawakupumzika.
Na mimi sikupenda
kwenda kwake kumsumbua, kwani kila nilipofika kwake,nilimkuta akiwa kachoka
kweli…huwa namuonea huruma naondoka zangu nakumuacha apumzike!
Hata hivyo alishaniambia kuwa mimi na yeye tutakuwa pamoja
pale tu tutakapofunga ndoa na ndoa yetu ilitakiwa ikafanyike huko kijijini,nami
sikumkatalia, kama alivyoesema yeye mwenyewe inabidi tupeane muda wakutafakari
na kujipima je tupo tayari kuishi pamoja kama mke na mume, maana ndoa sio kitu
cha kukurupuka tu, ….
‘Ndio Msomali, naona kiukweli mambo yetu yameisha na mimi
nipo tayari kuwa na wewe,lakini mengi yamepita kati yetu, siwezi nikajua undani
wako kwa sasa, halikadhalika wewe huwezi ukajua undani wangu kwa sasa, cha
muhimu ni kupeana muda, kila mtu atafakari kwa makini, na mwisho wa siku tuje
kuambiana ukweli, kwamba je tupo tayari kuishi kama mke na mume…’aliniambia.
‘Lakini mimi nimeshakuambia kuwa nipo tayari kuishi na wewe
kama mke wangu. Mimi kwasasa nahitaji kuwa na mke,na mke ambaye nilikuwa
nikimuwaza muda wote ni wewe…’nikamwambia.
‘Kauli ni rahisi sana kuitoa mdomoni, lakini ukweli wa mtu
ni nafsi yake, na muda ndio unaweka mambo hadharani, ni vyema tukayafanya haya
mambo kama watu wenye hekima, sio kwamba sikupendi, mimi nakupenda sana, lakini
tuwe makini sana na kitu kinachoitwa ndoa,….’akaniambia na kuanza kunitia
wasiwasi maana sikutegemea tena kama itakuwa hivyo.
‘Kwani kuna tatizo gani?’ nikauliza
‘Hakuna tatizo,… wewe chukua muda wako jitahidi sana kila
upatapo nafasi, jaribu kutafiti, na kujisomea nini kuhusu ndoa, nini kuhusu
mwenzako katika ndoa, nini kuhusu maisha na mahusiano katika ndoa,…ukimaliza
kujifunza, jiulize mwenyewe nafsini
mwako kuwa je upo tayari kuishi na mwenzako…..’akaniambia.
‘Mimi nipo tayari….sina wasiwasi na hilo….’nikasema kwa haraka.
‘Bado hujawa tayari, kama ungelikuwa tayari, usingelimuacha
yule binti watu wa kijijini, yule ni mke kweli kweli, alihitaji msaada kidogo
tu, alihitaji kuelimishwa mambo mengine ambayo kwake yalikuwa ni mapya, lakini
wewe ulimchukua na kuja kumtelekeza, unajua nini kilimsibu moyoni mwake,…?’
akaniuliza.
‘Kwani hayo yanakuaje tena hayo….’nikasema kwa kushangaa.
‘Ni muhimu sana kuelewa hilo,….unajua jinsi gani mtu anapata
maumivu pale anapoambiwa kuwa mimi na wewe basi….wakati mtu huyo bado unakupenda,
na wakati mwingine hujui kabisa kosa lako ni nini….’akaniambia na kunitonesha
kidonda.
‘Lakini yote haya yalitokea kwasababu ya Kimwana, natumai
kama isingelikwua Kimwana yasingelitokea hayo yaliyotokea….’nikasema.
‘Unaona, nikuambie ukweli, dunia hii Kimwana wapo wengi, …kauli yako hapo, inaonyesha ukweli fulani,…mwenyewe
umejifunga, lakini sio mbaya, kweli kama isingelikuwa Kimwana kukuonyesha yale
usiyoyajua yasingelitokea hayo,..je huoni kwamba tukioana sasa hivi,na ukakuta
sina hicho ambacho Kimwana alikuwa nacho utajikuta ukijilaumu …na maisha
yatakuwa yakubahatisha,…huoni kuwa wewe unachotaka ni mke tu,ilimradi unahitaji
mke,….?’ Akaniuliza.
‘Hapanaaa, sio hivyo,….sio
kwamba kwasababu nahitaji mke tu,….nakuhitaji wewe,maana hata nilipokuwa na
Kimwana nilikuwa nakuwaza wewe, wewe
ndiye mke ambaye yupo akilini mwangu..nakuomba sana Tausi usiniweke rehani
tena, sihitaji kuwa katika majaribio mengine, nimeshawiva na nipo tayari kuwa
mume mwema…’nikamwambia.
‘Sawa, kauli yako nimeisikia,lakini msimamo wangu upo
palepale, kuwa tupeane muda, …muda wakutafakari,muda wa kujifunza maisha ya
ndoa, muda wa kujipima je nina uwezo wa kuishi namwenzangu, na je ni nani huyo
mwenzangu…huenda siku kadha unaweza ukakutana na mtu ambaye hukuwahi kukutana
naye ukabadili mawazo,….’akaniangalia kwa makini.
‘Hiyo haiwezekani….wewe ndiye kila kitu kwangu
nakuhakikishia hilo…’nikamwambia.
‘Rahisi sana kuatamka.., mimi nakushauri kuwa tupeane muda
na ifanyie kazi akili yako, ili ijue nini kinachokuja mbele yako, baadaya
kuitwa mwanandoa…sio kitu cha mchezo , sio sehemu ya kufanyiana majaribio..ndoa
ni jambo takatifu, ….kwahiyo kihitaji kuwa makini …..’akaniambia na hata nilipojaribu
kumshawishi hakubadili msimamo wake.
Baadaya mazungumzo hayo nilioanana na wakili mwanadada nakumuomba
anisaidie kumshawishi Tausi, maana nahisi kuwa huenda ana mtu mwingine, na
anashindwa kuniambia ukweli, na kama kweli yupo mtu mwingine, nitaumia sana.
‘Una uhakika na hilo, kuwa ana mtu mwingine?’akaniuliza
‘Nahisi hivyo tu, maana hili la kuniambia, kila mmoja apate muda wa kutafakari,….nahisi
kuna mtu ambaye alishakubaliana naye, na sasa anajaribu kutafuta njia …’nikasema
na kukatiza.
‘Sio kweli, mwenzako anajua nini anachokifanya, ujue yule ni
dakitari , na ni mwalimu wa wanandoa, anajua jinsi gani watu wanapata taabu
katika ndoa zao, kwasababu tu ya kukurupuka kuingia kwenye ndoa, bila kuijua
ndoa yenyewe,….ndio maana anajaribu kukuelimishawewe ili uijue ndoa ni
nini,kabla hamjaingi akwenye ndoa.Itakuwa ni aibu kwake, muoane na baada ya
siku kadhaa muanze kusigishana…fikiria sana na jitahidi kufanya hayo
aliyokuelekeza…’akaniambia.
‘Sasa nitajifunza nini kipya katika maswala ya ndoa, ndoa
niijuavyo mimi ni kuwa muoane, na mengi mnajifunza mkiwa wawili, nitajuaje wewe
unanipenda nini, kama hatupo pamoja, nitajuaje kuhusu wewe kama hatupo pamoja….’nikasema.
‘Hiyo ni hatua baada ya ndoa, kuna mambo mengi unatakwia
uyajue kabla yahayo, kwanza ujue kwanini mnatakiwa muoane,kwani ni lazima
kuoana, wakati wewe ukihitaji mwanamke unaweza kumpata mitaani, ….hebu jiulize
hilo, je mwaname au mwanamke yupoje,ukumbuke watu hutofautiana, je ukimkuta
yule ambaye yupo tofauti na wewe utafanyaje…’ akaniambia na kuniangalia kwa
makini.
‘Hayo mbona nayaelewa tu…na hata hivyo mbona yeye namjua
toka utotoni…’nikasema, na yeye bila kujali maelezo yangu hayo akasema;
‘Je wewe mwenyewe umeshajiweka sawa kuishi na mwenzako,
maana usione ni jambo tu lakumchukua mwenzako na kuishi naye kama mke na mume ….eti
kwa vile unamjua toka utotoni,….utotoni sio sawa na ukubwani, sio sawa na hali
halisi ya mke na mume,…’akaniambia.
‘Mimi nipo tayari,…’nikasema.
‘Nakushauri,jaribu kutulia ,tuliza kichwa chako, ondoa tamaa,
tafakari kwanza, ili baadaye msije mkaanza kuhangaika kuwa mtaishije…kuna mambo
mengi…ya kujifunza, cha muhimu, kama ingelikuwa mimi ni wewe kwanza ningelimuuliza
mwenzangu, maana yeye ni mwalimu….na ni vyema hapa ukaondoa `udume’, weka akili
ya kujifunza mbele,mimi kama wewe ningelijishusha na kumuuliza, nifanyeje, au
nianze vipi, mchukulie kama mwalimu wako,…’akanishauri.
*************
Basi tulipofika hospitalini, nikawa na wazo moja, la
kumuomba tukutane tukitoka hapo, lakini haikuwa rahisi maana mambo mengi
yalitokea hapo hospitalini, na baadaye tukatawanyika bila hata ya kupata muda
wa kuongea naye.
‘Hali ya nesi sio nzuri…..tumejitahidi sana, lakini sumu
yake ilishaharibu sehemu kubwa ya ndani ya mwili, …lakini tumejitahidi tuwezavyo….’akasema
docta.
‘Ina maana hatapona?’ nikauliza kwa huzuni.
‘Siwezi kusema hivyo….kupona anaweza akapona,tumejaribu lile
liwezakanavyo,iliyobakia ni kumuachia mwenyewe mungu tu..’akasema docta na
kuondoka na jinsi alivyoongea na muoenekano wake ulionyesha wazi kabisa kuwa
hali ya huyo nesi sio nzuri, hapo kila mmoja aliinama chini akiomba kivyake.
‘Hapa sasa hakuna lakufanya iliyobakia ni kwenda kumuona
wakili mkuu, tujue naye anaendeleaje, maana sumu ni hiyo hiyo waliyokunywa
wote, ….’akasema wakili mwanadada, na sote tukaondoka kwenda kumuona wakili
mkuu, na tulimkuta akiwa kachoka kweli,hata kuongea kwake ilikuwa ni kwa taabu
kweli.
‘Nawashukuru sana kwa kunijali, …licha ya mengi yaliyotokea,
…’akasema.
‘Yote ni kawaida, binadamu hukutana na mengi, na mwisho wa
siku ni kujifunza, na usipojifunza kwa haya, basi wewe ubinadamu wako una
kasoro….’akasema mkuu.
‘Aaah,ndio hivyo tena, maana mimi hapa nilipo najiona mwenye
mikosi , ….’akasema
‘Kwa vipi?’ akaulizwa.
‘Mwenzangu hataki …’akasema na kuonesha wingu la machozi
machoni.
‘Cha muhimu wewe kwasasa ni kutulia, na kuangalia hali
yako,kuhusu mwenzako, ni kawaida ni hasira za kawaida, usitarajie kuwa yeye
atakukubalia kwa sasa kuwa mambo ni yote ni safi, ….cha muhimu wewe ni kutulia
upone, baadaye hayo yatazungumza, mtazungumza na mkihitaji msaada, tupo
tutasaidiana na najua mambo yakakwenda vyema…’akasema wakili mwanadada.
‘Unasema tu,kwa vile humjui mke wangu, mimi namjua vyema,
huwa akisema neno lake, ninaweza kulipima kuwa hili kalisema kwa kujaribu,
lakini kuna jingine akilisema najua kabisa kazamiria, …..nahisi moyo wake haupo
tena kwangu…’akasema..
‘Labda wewe mwenyewe unavyoongea umeshaweka hitimisho,
inaonyesha kuwa unataka iwe hivyo, maana ni mapema sana kuhukumu hivyo, ….jiulize
kama ingelikuwa wewe umetendewa hivyo ungefanyaje,…yeye kama binadamu anahitaji
muda wa kutafakari…’akaambiwa.
‘Nawaombeni sana, mujaribu kumshawishi,maana yeye ni mke
wangu, na nilisha mtendea mabaya ambayo kiukweli yanaumiza, lakini yote hayo
tuyaache yapite tugange yajayo, mimi nampenda sana na nimeona kuwa yeye ndiye
anayenifaa….’akasema.
Mimi pale nikawa nawazo hivi kwanini inakuwa hivyo, nahisi
kama nesi atakuja na kukaa naye pale
karibu huenda akabadili hayo maneno yake, maana ilivyojionyesha toka
awali, anampenda sana nesi,….
‘Niwaulize kwanza, nesi anaendeleaje….?’akauliza swali
tusilolitegemea toka kwake.
‘Wewe jiangalie kwanza hali yako, yeye anaendelea vyema na
matibabu yake…usiwe na wasiwasi nay eye…’akasema wakili mwanadada.
Mara simu ya mmoja
wawanafamilia ikaita tukiw amle ndani , na yule mwanafamilia kasogea pembeni, akawa
anaongea na huyo aliyempigia, na katika kuongea kwake akasema;
‘Docta kasema nesi hali yake sio ya kupona….’ile sauti
akasikiwa na wakili mkuu.
Wakili mkuu, alituangalia na mara akageuza macho, na hali
ikabadilika ghafla, hata alipoitwa docta, hali haikuwa vyema,…tukataoka pale
tukiwa tumechanganyikiwa na watu wakaanza kumlaumu yule jamaa aliyekuwa kiongea
na simu, …lakini ndio hivyo tena, hali za watu hawa waili zikawa ni mbaya, na
hadi tunaondoka hapo hospitalini hali zao zilikuwa ni za kusikilizia tu….
‘Hali zao sio nzuri, tunajitahidi kufanya kila
liwezekanavyo.lakini hali zao zimebadilika na hatukutarajia hili…nawaomba
muondoke,mtuachie tufanye kazi, ….’akasema docta, nasi tukaondoka kilammoja
akiwa kachanganyikiwa, na kila mmoja akaelekea kwake, huku akiwaza kivyake.
NB Hiki kidogo kilibakia tukaona tukimalizie, kabla hatujahitimisha, ….
WAZO LA LEO:
Tujaribu kuchunga sana kauli zetu, maana kutamka ni rahisi
sana,lakini matokeo yake yanaweza yakawa mabaya kwa mwenzako. Ni vyema kabla
hajutamka jambo kwa mwenzako hasa mkiwa katika hali ya kufarakana,ukatafakari
kwanza.
Katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhani, tunatakiwa tuchunge
sana ndimi zetu, tujaribu kukwepa kusema mambo yatakayobatilisha swaumu zetu, kama
vile matusi, kusengenya,…kusema uwongo…..utani
usio na maana yoyote. Kufunga ni pamoja na matendo yetu.
KUTOKA MAJUMBANI:
Siku hizi wezi wanaiba mchana kweupe,…wanakuchunguza nyendo zako,…iwe ni mama
wa nyumbani au mfanyakazi, na hata mlinzi, kuwa unatoka saangapi nyumbani au
lindoni, na wanachofanya mmoja mwenye simu anakuwa nawe karibu unapotoka hapo nyumbani….,
na wenzao wanakwenda nyumbani kwako,….kwahiyo kazi ya yule ambaye yupo nawe ni
kuwasiliana na wenzao waliokwenda kwako kuiba….
Wale walikwenda kwako wanavunja mlango kwa pisipisi, na
kuchukua vitu huku wakiwa wanawasilina na mwenzo ambaye yupo na wewe…..Tuwe
makini majumbani
Ni mimi:
emu-three
2 comments :
Hiki kitu ulichotuwekea leo hakieleweki mikono imeanzia wapi wa miguu imeishia wapi! yaani hamna connection kabisa na pale ilipoishia, wala haina mwendelezo uliotulia. kweli leo umeamua kutuchosha ndugu! dah
Oh, Anony,...ina maaa sehemu hii haijaeleweka,hebu wengine ambao hawajaelewa, waniambie ili nijue nini cha kufanya,lakini sehemu hii ina maana yake!
Ukikisoma vyema hiki kipande kwa makini, utajua wapi naelekea,.....
Mwisho wa kisa utakuja kuelewa tu ndugu yangu, vuta subira!
Post a Comment