Nesi akawa makini kusikiliza yale maelezo anayoongea wakili
mwanadada, na kila mara alitoa sauti ya kukubali kuwa ndivyo ilivyokuwa,…aliendelea
kufanya hivyo hadi pale hali lipombadilikia tena,na alianza kutikisika kwa
nguvu, na baadaye akawa anakoroma, na docta akatuambia tutoke nje haraka, kwani
mgonjwa anahitajika kupumzika, nasi ikatubidi tutoke nje kwa haraka kama
tulivyoagizwa.
Na tulipokuwa nje, ndipo tukaweza kupata muda wa kusikia
hali ya wakili mkuu ambaye alishapelekwa kwenye upasuaji. Na mkewe ambaye
alikuwa nasi, na alikuwa anajua hilo kuwa mumewe kapelekwa upasuaji, lakini
ilibidi awe nasi pia, kwani wote ni wagonjwa wake. Na mara tukiwa tunaulizana,
akatokea docta akiwa kwenye mavazi yake ya kikazi, akatuambia;
‘Upasuaji umekwenda vyema, …lakini bado
hajazindukana’akasema docta.
‘Kwahiyo mumeweza kuindoa hiyo sumu na athari zake?’
akauliza mke wa docta.
‘Tumeweza kufanya hivyo, na tunasubiri matokeo yake, tunataraji
mambo yatakwena vyema, msiwe na wasiwasi…’akasema docta ambaye alionekana kuwa
na haraka, akasema
‘Tunataka tukamhudumie huyo mgonjwa mwingine,maana bado
kulikuwa hakuna makubaliano, maana
mgonjwa mwenyewe alishakataaa ufanyiwa upasuaji,….’akasema docta.
‘Kwanini akatae …?’ mimi nikauliza kwa kushangaa.
‘Huoni kwamba yeye mwenyewe alitka kujiua kwasababu zake,..’akasema
mkuu.
‘Na je katika hali kama hiyo, mgonjwa anapokataa kufanyiwa
upasuaji na ndio njia pekee iliyobakisa kumsaidia mnafanyaje?’ akaulizwa docta
‘Wakati kama huo mara nyingi tunawasikiliza ndugu wa
mgonjwa, kwasababu kabla ya upasuaji lazima kuwa na ushahidi wa ndugu wa mgonjwa….
‘Sisi kama wawakilishi wa serikali tungelifurahi kama
upasuaji huo ungelifanyika, na tulikuwa tunahitaji maelezo mengi kutoka kwa
huyo mgonjwa, ….labda sisi twende tukaongee na ndugu wa huyo mgonjwa ili tujue
mawazo yao.
‘Ndugu wao walishakubali…’akasema docta na kuondoka kwa
haraka maana alikuwa akisubiriwa ….
Walipokutana na ndugu wa mgonjwa, wao walisema wazi kuwa
hawana kipingamizi chochote cha kufanyiwa upasuaji,kama ndio njia pekee ya
kuyaokoa maisha ya ndugu yao, wakasema wao wanaona ajabu kwanini yeye
anacheleweshwa.
Ndugu za nesi walishafika siku nyingi, na walikuwa
wakifuatilia kesi inavyoendelea ,walikuja siku kadhaa na baadaye wakaja ndugu
wa mke wa wakili mkuu, mama na pacha wa mke wa wakili, ….kulikuwa na
kutokuelewana kwa wanandugu hawa, kila mmoja akiwa upande wa mtoto wao, lakini
walipofika hapo hospitalini, wote wakawa na wazo moja, la kuhakikisha kuwa hawo
wagonjwa wanasaidiwa nakupona.
Wakati hayo yakiendelea mimi na wakili mwanadada, tukaungana
na mkuu, mke wa wakili mkuu, na familia ya mke wa wakili mkuu katika mezamoja
tukiwa na maongezi ya hapa na pale,na baadaye tukaitwa na hakimu na jopo lake.
‘Kutokana na hali ilivyo, hatuwezi kufanya lolote, na
nashauri kuwa tuahirishe hili zoezi hadi mgonjwa atakapokuwa na hali njema…’akasema
muheshimiwa hakimu.
‘Lakini hado hapo tumeshajua ni nani aliyemuua Kimwana’
akasema mmojawapo.
‘Hayo tuliyosikia kwa kauli yake, bado hayawezi
kujitosheleza kumuweka kwenye hatia, maana inawezekana akawa ni yeye, au akawa
mtu mwingine,…..yeye alikuwa kama mshiriki tu, tunahitaji ushahidi na vielelezo
thabiti, mahakamani,…na wakili mwanadada,baadaye tunakuhitaji ofisini, kwaajili
ya kukamilisha maelezo yako na vielelezo vyako, natumai kila kitu kipo tayari.
‘Muheshimiwa kila kitu kipo tayari,….’akasema wakili
mwanadada.
Baadaye tukakutana wenyewe nje tukiwa tunasubiri majaliwa ya
hawa watu wawili, na hapo tukapata muda wa kumsikiliza wakili mwanadada atupe
maelezo yake jinsi alivyoweza kumgundua muuaji wa Kimwana, maelezo ambayo
aliyakatisha pale nesi alipozidiwa.
********
Nilipopata maelezo ya yule nesi,…..’akasema wakili mwanadada
akiwa katulia kwenye kiti, na huku akiangalia mezani ambapo aliweka karatasi
yake, aliyokuwa akiandika mambo yake mwenyewe.
‘Nilipopata maelezo ya yule nesi,….nikajua kabisa kuwa kuna
jambo limejificha hapo, maana mengi aliyotuambia nesi huyu mgonjwa,mengi
yalionekana sio ya usahihi, licha ya kuwa kayapangilia vyema, kuonyesha kuwa
sio jambo la kubahatisha.
‘Kwa muda ule nilikuwa natafuta mwanya wa kufikanyumbani kwa
wakili mkuu, ili kuthibitisha mambo fulani, maana kwa ushahidi nilioupata
wakati ule ulikuwa ukithibitisha kabisa kuwa wakili mkuu ndiye muuaji wa
Kimwana. Na nilipopata haya maelezo ya nsei nikaunganisha moja kwa moja kuwa
huenda nesi alipofika kule, alikuta mauaji tayari, na alichofanya ni kumsaidia
mwenzake …
‘Kumsaidia mwenzake, kwa vipi?’ akaulizwa.
‘Tukumbuke kuwa wakili mkuu alikuwa ni mgonjwa, na hali yake
ingeliweza kubadilika wakati wowote, na hasa kama atakuwa kapambana na misuko
suko, na nesi alikuwa akijua hilo, na inawezekana kuondoka kwake ilikuwa an
dhamira hiyo, ndivyo nilivyokuwa nikiwazawakati ule….’akasema wakili mwanadada.
‘Ina maana hayo mawazo yako yalikuja kubadilika, na ni kitu
gani kilichofanya hayo nawazo yako yabadilike?’ akaulizwa.
‘Mauaji yalitokea,na kwa muda ule tulikuwa hatujapata hiyo
silaha iliyotumika, inagwaje kwa muda ule tulishagundua kuwa Kimwana hakuuwawa
na bastola kama ilivyozaniwa awali, aliuwawa kwa silaha kubwa, sasa je silaha
hiyo ipo wapi….’akatulia.
‘Ina maana hiyo silaha aliyokuja nayo nesi hapo hospitalini
haikuja kuonekana?’ akaulizwa.
‘Hiyo silaha ilipotea kiajabu, haikuja kuonekana na ujua mtu
pekee aliyekuwa akijua habari za hiyo silaha, zaidi ya huyo nesi mgonjwa, na
maidizi wake, nesi ambaye nilikuja kuongea naye baadaye..’akasema wakili
mwanadada,
‘Kwani yeye hakuwahi kwenda kuangalia pale alipoiona wakati
ule?’ akaulizwa.
‘Aliniambia kuwa kesho yake wakati huyo nesi hajafika,
aliingia humo, kwa ajili ya usafi na kuangalia hali ailivyo kwa mgonjwa,na
aingia chumba hicho cha kuabdilisha, nguo, aliangalai kila sehemu hakuweza
kuiona hiyp silaha tena.
‘Ina maana wakati wanaondoka, nesi- mgonjwa, hakuonekana
akiwa kabeba kitu chochote?’ akaulizwa.
‘Huyo nesi hakuonekana kubeba kitu chochote, na cha ajabu
hata muda alioondoka hakuna aliyejua, hata wale walinzi walisema hawakumuona
akipita hapo getini, kwani wakiondoka kila mmoja huwa anasaini hapo getini,
lakini yeye hakusaini kabisa hapo getini..
‘Ina maana kuna njia nyingine ya kupita?’ akaulizwa.
‘Hakuna njia nyingine labda uruke kuta, na kuruka ukuta sio
rahisi kwasababu ya zile nyanya za umeme….’akasema wakili mwanadada.
‘Kwahiyo lipitaje hapoi getini?’ akaulizwa wakili mwanadada.
‘Hilo labda tutakuja kulijua kutoka kwakauli yeke mwenyewe,
ila akipita hapo getini, akiwa sio yeye ,alikuwa mtu tofauti kabisa….’akasema
wakili mwanadada.
‘Hapo unatuchanganay kwa vipi, maana kama ulivyosema awali
nesi alikuwa akivaa nyele za bandia na walishazijua hizo nywele na kumtambua
kuwa ni yeye, ….’akauliza mkuu.
‘Huyu nesi ni komandoo,ni mjanja anayejua kila mbinu, …yeye
alijua kabisa kuwa keshagundulikana kuwa aliingia na mzigo, na hakutaka kabisa
kuja kugundulika akitoka na huo mzigo. Alichofanya kwanza yeye mwenyewe ni
kuhakikisha kuwa anatoka pale getini bila kujulikana, na pili huo mzigo unatoka
ki namna ambayo hakuna ambaye atakuja kuugundua.
‘Lifanyaje….?’ Akaulizwa.
‘Alifanyaje inakuwa kama kukisia tu,huenda alikuja kuutoa
usiku, lakini walinzi wangelimuona, au kuna magari huwa yanatoka, huenda
alikuja kuuweka kweney gari mojawapo, na huyo mwenye gari awe ni mtu ambaye
anajuana naye, au aliuweka kwenye gario, bila ya huyo mtu kujua..au vinginevyo,
aliirusha kwenye ukuta, na kukawa na mtu mwingine kwa nje, ambaye lishaambiwa
kuhusu hilo hiyo silaha.
‘Atakuwa ni nani huyo?’ akaulizwa.
‘Kwanza hilo mimi halikusnisumbua kwa muda,ule. Kwasababu nilishakua
kuwa silaha haipo humo ndani tena, cha muhimu ikawa kujua hiyo silaha ipo wapi?
Akasema wakili mwanadadana kutulia.
‘Hapo hata mimi siwezi kukisia ipo wapi maana tulihangaika
kila mahali hatukuweza kuipata, hata ulipoipata tulishangaa sana..’akasema
mkuu.
‘Kuna siri moja, …wanasema ukitaka kukificha kiatu,kiweke
sehemu yake….pale pale kwa wenzake,….hilo ndilo lililonijia akilini nikijua
kuwa napambana na mtu mwenye akili ya hali ya juu, Huyu nesi ni mjanja na
ukiangalai mambo mengi ya hilo kundi yalikuwa yakiendeshwa na yeye, na watu
walikuwa wakimzania kuwa ni Sokoti, Sokoti yeye alikuwa kam kiongozi wa kundi
na ujanaj wake,lakini kwa maswala kama haya ….nesi ndiye alikuwa kiongozi.
Mimi nilichofanya ni kwenda nyumbani kwa wakili mkuu, na
ukumbuke kuwa kwa muda ule akili yangu ilikuwa bado inamsadiki yeye kama ndiye
muuaji, …
‘Kwani hakuwa yeye ndiye muuaji?’nikauliza
‘Kwa vipi…?’ akauliza mkuu.
‘Zipo sababu nyingi ambazo unawezaukahisi kuwa wakili mkuu
ndiye muuaji,lakini hebu kumbuka siku ile,…mke wako alimuona akiwa kwenye lile
jengo la nyumba ya Kimwana, alikuwa kama anatafuta mwanya wa kumuua Kimwana,na
yeye alikuwa na bastola tu…..’
‘Unajuaje kuwa alikuwa na bastola?’ akaulizwa.
‘Hapo ndipo nataka kuwapeleka ili mjue jinsii iliyokuwa…’akasema
wakili mwanadada.
**********
‘Nilipogundua kuwa silaha haipo hapo ndani ya hospitalini,
nikawa natafuta wapi ili[opelekwa, na njia niliyokuwa nikiitafuta ni zile
kumbukumbu za walinzi, lakini kwenye kumbukumbu zao hakukuwa na maelezo yoyote
kuhusiana na mzigo alioingia nao nesi.
Kwenye kumbukumbu za awali zilisema kuwa aliingia na kitu ka
gitaa likiwa kwenye mfuko wake, haikusema silaha, na nilipoangalai kweney
kumbukumbu za watu kutoka naviti, hakuna sehemu iliyosema kuwa nesi huyo alitoka
na hilo gitaa, sasa hilo gutaa lilienda wapi?
‘Nesi alitoka saa ngapi?’nikawauliza walinzi.
‘Hatujui,maana hakusaini hapa getini,na kila mtu akitoka
hapa , hasa mafanyakazi wa humu, ni lazima asaini hapa kwenye hli daftari, yeye
siku hiyo hakuwsaini …..tukajua labda alikuwa an zamu za usiku, kaamua
kuunganisha …’akasema mlinzi, na hata niliokwenda kweney kitabu cha mlizni wa
juu, hakikuwa an maelezo yoyote.
‘Je hakuna muda uliowahi kuondoka hapa?’ nikamuuliza.
‘Muda nilioondoka hapa ni wakati mwenzangu alipokuja
kunipokea,…’akasema
‘Mwenzako yupi?nikamuuliza.
‘Mlinzi mwenzangu wa chini, nilmuita aje anipokee kidogo, name
nikashuka chini..’akasema.
‘Ilichukua muda gani huyo mlinzi wa chini kuja juu na wewe
kwenda chini?’ nikamuuliza.
‘Sio muda mrefu,ndio kulikuwa na kuchelewa kwa hapa na pale
maana tulijua muda kama huo hakuna watu wanaopita pita…’akasema.
‘Je mabadiliko hayo huwa yanajulikana ndani,….?’ Akauliza.
‘Ndio yanajulikana…wanajua wengi kuwa kila baaada ya masaa
manne tunabadilishana….’akasema.
‘Hapo akili ikanicheza, kama inajulikana ndani, na kwa mtu
kama huyo nesi,mbona ni muda muafaka wa kufanya lolote,….lakini kulikuwa na
mlinzi mwingine alibakia pale getini,hakuona mtu akitoka, ….nikawa na wasiwasi
na maeelzo yake, huenda naye katika huko kuchelewa chelewa, walikuwa wakifanya
jambo, ama kula, ama maongezi yaliyowafanya wasiona kila kitu, na ikizingatiwa
wenyewe walishajua kuwa kwa muda haukuna mtu anayewezakupita.
‘Kwahiyo yote hapo hapo ni hisia tu,hakuna ushahidi wa
vielelezo?’akauliza mkuu.
‘Hapakuwa naushahidi wa vielelezo,ilibidi nitumie hisia tu.
Kwahiyo hapo nikawa na kazi kubwa ya kuitafuta hiyo bunduki
imepelekwa wapi, maana mpaka siku ile hiyo bunduki haijajulikana wapi ilipo. Na
kwa maelezo ya huyo, nesi, anasema siku ya pili yake alifika pale alipofichwa
hiyo bunduki lakini hakuiona tena…..ndio ukaja huo usemi kuwa ukitaka kuficha ndala
weka sehemu zinzpowekkwa ndala…
Nilichofanya ni kwenda kule nyumbani kwa wakili mkuu, ambapo
silaha ilikuwepo awali,..na nilichofanya kwanza nilipofika pale ni kumuuliza
yule binti anayebakia pale nyumbani muda wote,…yaani yule mtoto wao kufikia ili
kujua siku hiyo alifika nani pale nyumbani;
‘Katika kumbukumbu zako siku ile ambayo ulisikia Kimwana
aliuliwa, unaweza kukumbuka ni nani na nani alifika hapa nyumbani?’
nikamuuliza.
‘Siku ile asubuhi sana mama alinituma sokoni mjini,na
akaniambia nikirudi kama nitakuta hayupo nisiwe na wasiwasi kwasababu yeye atachelewa
huko anapokwenda,…nilijua yupo mapumziko, lakini inavyoonekana alikuwa na
safari yake ambayo hakutaka kuniambia, …
Nilichelewa kurudi mjini, na nilipofika nyumbani cha ajabu
nilikuta mlango haujafungwa na ufunguo, na sio kawaida, mtu kama mama kuacha
mlango wazi, na hata aliporudi nilimuuliza akasema yeye alihakikisha kabis
akuwa alifunga mlango,… na ufunguo..
‘Nilishikwa na wasiwasi sana nikijua kuwa kuna mwizi kaingia
ndani na kuiba vitu, lakini nilipoingia ndani na kuchunguza vyema, nilikuta
kila kitu kipo sawa, hakuna kitu kilichochukuliwa….na nilipotafiti sana,
niligundua kuwa mlango ule uingiao,ofisini kwa baba ulifunguliwa,….’akasema,
‘Uligunduje ina maana ulikuwa wazi,haujafungwa na ufunguo?’ nikamuuliza.
‘Ulikuwa umefungwa na ufunguo, lakini kuna nguo nilikuwa
nimeziweka mlangoni, zilikuwa nimeziegesha tu pale pembeni ya mlango,,
..nilizikuta hazipo, zimedondoka chini na mojawapo ilikuwa imetumbukia kwa
ndani,…..
Nilimuuliza mama kamaaliwahi kuingia humo ndani akasema yeye
hajawahi kuingia humu, na wala hanampango wakuingia humo,….majibu ya mama ya
makto yaliniogopesha na sikupenda kumuuliza tena, lakini kwa akili yangu
nilijua kuwa kama sio mama kuna mtu aliingia humo.
Basi nikawa sina jinsi nikatafuta njia za kuingia humo,…nikamtafuta
mke wakili mkuu, na kumuomba ufunguo wa humo ndani, yeye
hakunikatalia,nikafungua,lakini baada ya kuhakikisha kuwa yeye kweli hakuingia
humo,na nilihakikisha kuwa nina shahidi mwingine toka idara ya usalama.
‘Tulipoingia mle tulihakikisha kuwa alama zote z vidole
zimechukuliwa, na tukawa na kzi ya kukagua mle ndani,nilimuuliza mke wa wakili
mkuu wapi silaha zinapowekwa?’
‘Pale kwenye lile kabati…?’ akanionyesha.
‘Nilifungua lilekabati, na hakukuwa na silaha yoyote’
‘Mbona hakuna silaha humo?’ nikauliza.
‘Bastola ipo humo angali vizuri, mimi niliiaha hapo hapo?’
akasema.
‘Bastola haikuwepo, na kwa muda ule sikujua nani aliichukua,
ila kwa hayo maelezo ya wakili mkuu ina maana yeye ndiye aliyekuja kuichukua,
na ndiye aliyeingia na kucha mlango wazi…na kwa maelezo yake ni kuwa alipofika
hapo hakuikuta bdunduki, lakini kwa muda ule hakuwa na mawazo nayo kwani lengo
lake ni kuichukua bastola.
‘Nilikuta bunduki haipo,….nikashituka kidogo, lakini
kutokana na muda na kuwa lengo langu ilikuwa ni bastola, nilichukua bastola na
kutoka kwa haraka, nakumbuka hata mlango nilishahu kuufunga’akasema.
‘Mlango upi?’ akaulizwa.
‘Mlango wa nyumba, mlango wa kule niliufunga, hilo nina
uhakika nalo…’alisema wakili mkuu.
Pale akili ikanicheza,kama silaha mle ndani haipo itakuwa
wapi…nikaanza kuichunguza ilenyumba, nikagundua kwua kuna kabati la nguo
zilizochakaa, na nilipomuuliza huyo binti wa hpo kuwa hapo kunawekwa nini,
akashangaa, alipoona kuwa lipo wazi.
‘Hilo kabati siku nyingi halijaguswa, mimi mwenyewe
naliogopa, maana kuna siku alionekana nyoka, hapo, tangu siku hiyo
sijaligusa,nahata mama anaogopa kabisa, nashangaa kuona limefunguliwa…’akasema
‘Umejuaje kuwa limefunguliwa,…?’ nikamuuliza.
‘Huoni huo mlango ni kama umeegeshwa, haukuwa hivyo, na nguo
hizo zimetokeza, au ndio huyo nyoka alikuwa anatoka,….’akasema huyo binti huku
akiogopa kabisa kulisogelea.
Mimi nikalisogelea na kuhakikisha kuwa alama za vidole
zimechukuliwa kwanza, halafu tukalifungua..mara silaha hiyo ikadondoka chini….’akasema
wakili mwanadada.
‘Silaha ipi hiyo?’ akauliza mkuu.
‘Silaha hiyo hiyo ilitumika kumuua Kimwana..’akasema wakili
mwanadada.
‘Nani aliiweka humo?’akaulzwa.
‘Tutakuja kumjua muda sio mfupi….’akasema wakili mwanadada.
********
NB: Kutokuwa na jembe la uhakika nyumbani,nashindwa kuafanya
mambo mengi, lakini hata hivyo hichi kidodgo kinatosha, nimekiandika asubuhi na
mapema, kabla wenyewe hawajafika.
********************************************************************************
WAZO LA LEO: Moja ya mafunzo ya kufunga, ni kuvumilia njaa,….na
kwanini iwe hivyo, kuna sababu nyingine, lakini mtizamo wangu upo kwenye sababu
ya `kuijua njaa’ …Unapofunga unaijua njaa
ilivyo, unajifunza jinsi gani mwenye njaa anavyosikia hiyo njaa, maana
mwenye shibe katu hamjui mwenye njaa.
Kuna watu wamejaliwa,
hawaijui njaa kabisa, kuna watu wanakula na kusaza, kuna watu wanamwanga
vyakula,kuna watu wanatumia pesa nyingi kuagiza vyakula mahotelini, kwa gharama
kubwa tu, na anakula kidogo tu chakula kingine akaniacha.
Tukumbuke kuwa kuna mtu anaamuka asubuhi hajui atakula nini,…kuna
watu wanakufa kwa njaa,watoto wadogo, wazee wasiojiweza, na wengine wanakufa
kwa njaa, kwasababu za kisiasa, kiuchumi, makazini wanalipwa pela isiyokidhi mahitaji muhimu, na sababu nyinginezo nyingi zilizopo juu ya uwezo wao.Kwa uhakika, hawa watu wanajikuta
katika hali hiyo ya njaa bila kupenda,....lakini cha ajbu, ...., leo hii wewe umejaliwa unamwanga chakula, matumizi yako ni hali ya juu isivyo kawaida …
Funga ya
swaumu,inakuonjesha jinsi njaa ilivyo, ili ukimuona mwenye njaa uwe na huruna
naye....
SWAUMU NJEMA,
************
MATUKIO YA MITAANI -Ubungo Kituoni: Kwa wengi wanapandia mabasi eneo la Ubungo, kuelekea sehemu nyingi za jiji,..hasa wa Gongolamboto na Mbagala, mumegundua kuwa siku hizi kuna mtindo wa vijana kukimbili mabasi na kushikilia viti, na kudai pesa, au kuwakimbilia abiria waliotoka mikoani kuwa wao wanaweza kukushikilia kiti, lakini unatakiwa kuwalipa pesa shilinngi elifu kwa kiti na elifu kwa mzigo.
Abiria wengi wamejikuta wakidaiwa pesa mara mbili, ili wapate kiti, na pia wengine ili tu waweze kuingia kwenye hilo basi baada ya mizigo ya kupandishwa juu ya basi, na wengine wameishiwa kuibiwa. Tulishuhudia akina mama wakiwa na watoto, wakidaiwa pesa mara mbili, nje kadaiwa pesa ya kupandishiwa mizigo na kuna pesa kalipa kwa ajili tu ya kushikiwa kiti, nagharama ya kiti ni elifu, gharama ya mzigo mmoja huanzia shilingi elifu moja,, na bado alipoingia ndani akadaiwa pesa na kondakta, kondakita akidai kuwa hayajui hayo makubaliano ya huko nje kwa hiyo alipie nauli yake na nauli ya mizigo kukaa ndani ya basi..,
Je wahusika mnalijau hili, je hawo vijana wamapewa na nani kibali cha kufnaya hiyo kazi?,...tuliangali hili swala kwa makini kabla halijaleta madhara zaidi, kwani msafairi unapotoka mikoni unakuwa hujui nini kinaendelea hapo, utaona labda ndio utaratibu.
Ni mimi:
emu-three
1 comment :
yaani mwisho wa hii stori utakuwa wa ajabu sana, hapa najiandaa kushangaa kwamba aliyeua itakuja kujulikana kuwa ni yule 'binti yatima!'. keep it up!
Post a Comment