‘Hivi mumeo naye anaendeleaje?’ nikamuuliza mke wa wakili
mkuu. Mke wa wakili mkuu aliniangalia kwa macho yake yaliyolowana machozi
akasema;
‘Hajazindukana bado, na hali yake ni mbaya, ….ni mbaya sana,
….bado wanamhangaikia na wazo lililotolewa hadi sasa ni kufanyiwa upasuaji,…..nimewasiliana
na kaka yake, na yeye kakubali ufanyike tu,….maana hadi sasa sijielewi, naona
kama filamu ya kuigiza tu, sijui hawa watu wana nini,….’akasema mke wa wakili
mkuu, huku akijizuia kulia.
‘Ni moyo wa kupenda huo, mpaka kupitiliza,….maana mimi
nimejifunza kutoka kwa huyo rafiki yako, na nimegundua mengi, kuwa moyo
ukipenda, haumabiliki,…. akili inakuwa haina uweze wa kuchuja tena, na hili ni
tatizo….’akasema wakili mwanadada.
‘Lakini hata hivyo mimi sioni kuwa huo ni upendo wa dhati,
maana kama kweli ungelikuwa ni upendo wa dhati huyo mume wangu angeliniambia
mimi ukweli, na tukajadiliana na tungelijua hatima yake, ….lakini huku unapenda
na kule unapenda, kweli huo ni upendo au ni tamaa za kimwili tu?’ akauliza mke
wa wakili mkuu.
‘Lakini je ni kweli
mumeo alikubali kunywa hiyo sumu, ili wafe….kama alivyodai nesi, kuwa wanywe
wafe, wakaoane huko mbele kwa mbale, mimi hapa naona nesi kadanganya…na hebu
angalia hawa watu, huyo ni nesi anaongea hivyo, hilo lingeongelewa na watu
wasio na taaluma…’ nikasema.
‘Si ulimsikia livyosema mwenyewe kuwa pale hawezi kudanganya
tena, maana anajiona kama ni mtu wa kufa…nahisi mwenzake aliona kama ni uwongo,
alipoambiwa kuwa wanakunywa sumu ili wafe ….’akasema wakili mwanadada.
‘Unajua kwa hali ile waliyokuwa nayo, hasa wakili mkuu,
walikuwa kama wamechanganyikiwa, ikizingatia kuwa kuna kesi ya mauaji mbele
yao, na mambo ,mengi ya kuwazalilisha yameshapita, yale mapicha mbaya,
yamewaweka uchi mbele ya jamii, sasa aliona kabda ni heri ya kufa kuliko
kuaibika …’nikasema.
‘Siamini mtu kama wakili mkuu,ambaye anajua sheria, na yeye
ni kama askari angelichukua hatu kama hiyo. Hatua hiyo ni udhaifu kwa mpiganaji,
mara nyingi mtu kama askari, wengi hawapendelei sumu, wao hujiua kwa
risasi….’akasema mtu mmoja ambaye likuwa pembeni yetu akitusikiliza.
Mara akaja yule mlinzi na kusema tunaitwa tena huko ndani,
na tulipofia tulimkuta nesi akiwa kajiandaa kuongea na sisi…
********
‘Sijafa bado na siamini kuwa bado nipo hai,…., bado napumua,
na naomba safari hii niwasimulie kila kitu, msiniulize maswali tena, sikumbuki
vyema tuliishia wapi, …sikumbuki vyema niliwaambia kitu gani, ..mmh, …kumbukumbu
zinaanza kupotea….’akawa anajaribu kukumbuka.
‘Tulikuuliza je ndio wewe uliyemuua Kimwana…!’ akasema
wakili mwanadada.
‘Siku ile ambayo Kimwana aliuliwa, mimi nilibakia
hospitalini, na nilijua kabisa kuwa Kimwana siku hiyo hatapona, kwasababu
nilijua kuwa mke wa wakili mkuu, na rafiki yake wamekwenda huko kufanya mauaji,
na nilipoagana na wakili mkuu kuwa na y eye anakwenda huko nikajua sasa Kimwana
kapatikana….lakini…..’akatulia kama vile anatafuta hewa.
‘Niliingiwa na wasiwasi maana wote hawo nawajua, ….namjua
wakili mkuu udhaifu wake, nilijua akifika kwa Kimwana na akalegezewa yale
macho, hataweza kufanya hicho alichokusudia, na wale akina dada wawili,
hawawezi kumuua mtu, zile ni hasira tu, itafikia muda watashindwa kufanya hilo
walilolikusudia, hapo hapo nikampigia simu Sokoti, na kumwambia kuwa huko kwa
Kimwana kunatakiwa kufanyike jambo la haraka…
‘Jambo gani la haraka, mbona tulishakubaliana kuwa hawo
akina dada wawili watamaliza kila kitu…?’akaniambia Sokoti.
‘Sikiliza nina taarifa kuwa wakili mwanadada anamfuatilia
Kimwana, na ninavyojua huyo dada akipata mwanya wa kuongea na Kimwana, ataweza
kujua kila kitu, na ukumbuke kuwa Kimwana keshasema kuwa atabomoka, atasema
kila kitu kuhusu hili kundiletu, na mimi sikubali kwenda jela kwa uzembe huo…heri
ya kufa mapema, lakini kabla ya kufikia hatua hiyo, nataka nihakikishe
nimemlaiza adui yangu…..’nikamwambia Sokoti.
‘Sasa unataka tufanyeje?’akaniuliza.
‘Wewe nakuachia kazi moja, kuhakiisha kuwa unamziba mdomo
huyo wakili mwanadada,….maanahuyo ukimuachia mwanya umeumbuka, mpaka sasa
inanokena keshajua mambo mengi,anachotafuta ni ushahidi tu,….huyo hakikisha
hakatizi leo,… mimi niachie Kimwana huyo ni mtu wangu….’nikasema.
‘Hiyo haina shida, kuna mtu wetu yupo huko, anaweza kumaliza
kila kitu..nikimwambia tu, ….atatekeleza…’akasema.
‘Lakini nahitaji mawasiliano yako baadaye kidogo, uwe hewani…’nikamwambia
na wakati huo akili yangu ilishafanya kazi kwa haraka, na nilipoangalia saa
nikagundua kuwa kama wakili mkuu keshaondoka kwenda huko kwa Kimwana atakuwa
keshakaribia kufika, na mimi nilitaka nihakikishe kuwa najua nini anachokitaka
kukifanya…kama sio mbinu yao ya kukutana….’akatulia.
‘Sikujua kuwa kuna mtu mjanja angeligundua hilo, maana
nilifanya mambo yote kitaalamu, na siku wakili mwanadada alipokuja kunihadithia
haya, na akawa anaelezea jinsi nilivyokuwa nimepanga kama vile alikuwa kichwani
mwangu, sikuamini hilo….nikajua sasa sina ujanja,…mmh’ akaguna na kuhema kwa
nguvu, halafu akasema;
‘Naomba wakili mwanadada uwaelezee jinsi gani ulivyo gundua
maana naona pumzi kama inakwisha….
*******
Wote tulimgeukia wakili mwanadada ambaye alikuwa akimtizama
nesi kwa macho ya huruma, akasema kwa sauti ndogo;
‘Nilitaka yote yatoke kinywani mwako, maana huu sasa ni
ushahidi waliokuwa wakiuhitaji watu wa sheria, na nitaongea yale muhimu, kama
utaona nimesema uwongo naomba unisimamishe haraka…’akasema wakili mwanadada huku
akimwangalia hakimu na mkuu, na mwandishi maalumu wa mahakama ambaye alikuwa
akiandika taarifa zote.
‘Kama ulivyonielezea, ndivyo hivyo nilivyofanya, …wewe ongea
ninakusikiliza, maana hapa kichwa , tumbo vyote vinauma, kama roho ndivyo
inavyochomolewa hivi mbona kuna kazi…’akasema na kuhema kwa nguvu.
Docta alimsogelea na
kumuangalia….akahakikisha kuwa kila kitu kipo shwari,akasema wakili mwanadada
aendelee tu, mgonjwa yupo macho anawasikiliza…
‘Nawasikiliza, nipo shwari kwa sasa…’akasema nesi.
‘Nesi alipofika hapo hospitalini, alifanya mengi makubwa, na
hata ukienda kumuuliza mganga mkuu wa hiyo hospitali, atakuambia kuwa huyo nesi
ndiye aliyeifanya hiyo hospitalini iwe na uhai tena maana ilishafikia kubaya…na
kitu kimoja kikubwa alichokifanya ni kuhakikisha kuwa hospitali hiyo ina ulinzi
thabiti.
‘Yeye kwasababu alipitia uaskari, basi hata katika utendaji
wake wa kazi ulikuwa una alama ya uaskari. Kitu kimoja alichokifanya ni kuhusu
walinzi kuwa wawe na madafatri mawili. Moja ambalo wanasaini watu wanapoingia,
na la pili ni lakuandika kumbukumbu zote za wale watu wanaoingia au kutoka…nakwasababu fulani hawakuweza kuacha
kumbukumbu zao pale getini kwa mlinzi.
Daftari hili la pili anakuwa nalo mlinzi wa juu, maana pale
getini walijenga kitu kama kigorofa, na mlinzi wa juu kazi yake ni kuandika
kila kitu, anahitajika kuangalia kila mtu anayeingia na kutoka, na kuandika
kila tukio,…
Sasa utaratibu huo ndio uliokuja kummaliza nesi mwenyewe,
maana nilipopitia hilo daftari la huyo mlinzi wa juu, niligundua kuwa siku hiyo,
kwa maelezo ya mlinzi ndani ya lile
daftari, pale getini alitoka mtu na
pikipiki, akiwa kavalia koti refu na nywele za bandia, …..mlinzi huyo aliandika
kuwa mtu huyo sio mara ya kwanza kuonekana hivyo, akiwa kavalia hivyo na
alipoelezea wasifa wa huyo mtu, nikakumbuka yule mtu aliyewahi kukutana na
Msomali kipindi cha nyuma, akiwa na nywele nyingi, ambaye alikuja hata
kumkimbia Msomali…
‘Niligudnua kuwa kumbe ulikuwa ni ujanaj fulani wa kuigiza….’akatulia
na kumwangalia nesi, ambaye alionekana kuwa macho, akitabasamu kwa
kujilazimisha..
Kwahiyo kazi yangu kubwa ilikuwa kumtafuta mtu wa namna hiyo
ni nani, maana mtu huyo amekuwa kama jinamizi fulani linalokuja na kufanya
jambo halafu linatoweka,…hisia zangu zilinituma kabisa kuwa huyo anaweza akawa
mtu muhimu sana katika haya matukio.
Nilipopata hizo kumbukumbu, nikaingia ndani na kutafiti ,
nilikwenda hapo alipokuwa kalazwa wakili mkuu, nilitaka kujua ukweli kuwa je
alikuwa akiumwa kweli, maana kwa kipindi hicho nilishaingiwa na wasiwasi kuwa
huenda wakili mkuu ndiye aliyefanya haya yote, kwahiyo nilitaka kujua kuwa yupo
nesi mwingine aliyekuwa akishirikiana na nesi huyu na je anaweza akawa anajua
lolote.
Hapo ndipo nilipogundua mengi, ….nilipofika pale
hospitalini, niliongea na daktari aliyekuwa akimhudumia wakili mkuu,
nikamuuliza hali halisi ya mgonjwa, na yeye hakunificha aliniambia kila kitu,
kuwa kweli wakili mkuu alikuwa akikabiliwa an shinikiza la damu ..na tatizo
hilo, linatokana na msongo wa mawazo, kwahiyo kama atapata muda wa kutuliza
kichwa chake haitachukua mudaangelipona kabisa,lakini kama atashindwa kufanya
hivyo, anaweza akaishia kubaya…
‘Je docta ni nesi wa ngapi waliokuwa wakimuhudumia huyo
mgonjwa?’ nikamuuliza.
‘Wapo nesi wawili ambao nimewapa hiyo kazi, ..yupo nesi
ambaye ni rafiki mkubwa wa huyo mgonjwa na mwenzake mmoja ambaye sasa yupo
likizo…’akaniambia huyo docta.
‘Anatarajia kurudi lini?’nikamuuliza.
‘Ni baada ay siku kumi tano hivi, lakini nasiki kesharudi
kwani alikuwa akifuatilai malipo yake, kwahiyo haajsafiri bado. Kama unahitaji
kumuona nenda masijala watakupa taarifa zake….’akaniambia huyo docta, na
nilijua hana kubwa la kunisaida kwa muda huo, nikaona cha muhimu ni kumtafuta
huyonesi.
Kwanza nikaimbilia masijala, na kwa bahati nzuri, nikamkua
huyo nesi akiwa anasubiri taarifa zake humo. Kwani hapo ndipo wanapopatia
taarifa zao hasa wanapokuwa wakifuatiliwa mambo yao ya kikazi, na lionekana
hapo kama kajificha, hakutaka watu wamuone.
‘Wewe ndiye uliyekuwa ukimhudumia wakili mkuu, na
mwenzako,..?’nikamuuliza.
‘Nani kakumbia hivyo…?’ akaniuliza kwa wasiwasi, na ule
wasiwasi ukaniambai kuwa kuna jambo fulani analijua huyo nesi,na hakupenda kabisa
lijulikane, na hata hiyo likizo inaonekana kama alilazimishiwa, nahisi kwa
shinikizo fulani, ambalo nilikuja kugundua kuwa ni kutokana na yaliyotokea siku
hiyo.
‘Ni docta wako, kaniambia kila kitu,kuwa wewe ndiye
uliyepewa kazi pamoja na nesi wenu mkuu, kumhudumia waklii mkuu, na kuna siku
wakili mkuu alitoka nje bila ya taarifa ya docta ….’nikasema na yeye bila kujua
akaanza kuhaha na kutetemeka.
‘Mimi ni wakili na lengo langu nikukusaidia wewe na
mwenzako, iili misje mkaingia kwenye matatizo maana mwenzako keshaongea kila
kitu na kukutupia mzigo wewe,na usipoangalia vyema utajikuta kwenye matatizo,
makubwa ….’nikamwambia.
‘Nilijua tu,ndio maana kanilazimisha nichukue hii likizo ili
aje anichomee uwongo wake nikiwa huko likizo,sikubali…’ akasema.
‘Uwongo gani wakati ni kweli wewe ulikuwepo siku hiyo?’
nikamuuliza.
‘Ndio nilikuwepo, lakini mshiriki mkuu wa kumhudumia huyo
mgonjwa ni yeye, na alishatuambia kuwa sisi tutaelekezwa jinsi ya kufanya tu,
hatuna nafasi ya kuwa karibu na huyo mgonjwa,kwasababu ya wivu wake….’akasema
huku akiwa na wasi wasiwasi.
‘Sasa iku ile nilikuwa nipo ndani ya wodi nikiwahudumia
wagonjwa, nikawa nimepungukiwa na vifaa,…nikaenda kumfuata yeye. Bahati
sikumkukuta kwenye ofisi yake, nikakimbilia kule alipolazwa mgonjwa, wakati
nafika chumba cha kubadili nguo, nikamuona yeye akiingia humo kwenye hicho
chumba,na yeye muda huo hakuniona.…
Nikasubiri nikiwa na wasiwasi naye, maana siku hiyo nzima
alionekana kutokuwa na amani, alikuwa hasemi na akiongea huongea kwa hasira,
nikajua kuna jambo,….nikatulia kwa muda, na nilipoona kimiya nikasogelea pale
chumba cha kubadili, na nikashangaa mlango wa nyuma ambao mara nyingi
haufunguliwi, ukawa unafungwa kwa nje, ina maana yeye alitokea mlango huo wa
nyuma.
Nikakimbia haraka kwenye dirisha ambalo unaona kwa nje, na
nikamuona mtu akiwa kavalia nywele za bandia na koti refu akipanda kwenye
pikipiki,..nywele zile zilikuwa zikimfunika uso mzima, kwahiyo usingeliweza
kumuona sura yake, lakini viatu alivyokuwa kavalia siku hiyo vyekundu
vilimshitaki,nikajau kuwa ni yeye.
Nikajiuliz a huyu mtu anakwenda wapi saa hizi na nywele za
bandia, na jinsi alivyo ni kama hataki mtu amjue ….nikarudi haraka hadi kule
kwenye chumba cha kubadili, nikakuta nguo zake alizokuwa kavalia siku hiyo
zikiwa zimewekwa mle kwenye kabati lake, nikajua kuwa kuna jambo linaendelea.
Nikakimbilia kule kwenye chumba alicholazwa yule mgonjwa,
nikakuta kama kuna mgonjwa kalala pake kitandani, ..lakini ulalaji ule ukanitia
mashaka, kama ni mgonjwa, basi atakuwa maiti, nikatka kujiridhisha , nikaingia
ndani, na nilipofunua kitanda, nilikuta ni mito imewekwa mithili ya mtu
aliyelala…nikashituka ajabu….nikajua kuwa huenda hawa watu wamepanga kwenda
kufanya mambo yao…
‘Mambo gani….’nikamuuliza.
‘Mapenzi yao labda..sikuwa na uhakika zaidi ….’akasema huyo
nesi
‘Je uvaaji wa hizo nguo ulishawahi kumuona mara nyingine,
huyo nesi akiwa kavalia hivyo?’nikamuuliza.
‘Ndio sio mara ya kwanza,….na huvaa jioni wkati anatoka,
sijui huwa anakwenda wapi, na mra nyingi akivaa hivyo haagi mtu, anafanya kama
siri fulani. Na kwa jinsi ninavyomuogopa sijawahi kumuuliza, ila nilihisI huyu
nesi ana lake jambo ….’akasema.
‘Ikawaje?’ nikamuuliza.
‘Nilirudishia vile vile na kutoka nje,haraka nikiwa na
wasiwasi asije akanikuta humo ndani,…’akasema.
‘Ina maana ulikuta mlango upo wazi, au ulikuwa na ufunguo wa
hicho chumba?’ akaulizwa.
‘Mlango ulikuwa haujafungwa, ….lakini mara nyingi hicho
chumba hakuna anayeingia, na kuingia humo mpaka umuone yeye au dakitari,na
dakitari siku hiyo aliaga mapema kwani alikuwa na mkutano . Na huyo mgonjwa
alikuwa kwenye mamlaka ya nesi, …
‘Baadaye sana, akarudi ….na alirudia njia ile ile,…aliingia
na pikipiki lake,pikipiki hilo ni la huyo mgonjwa,lililetwa hapo kipindi huyo
mgonjwa alipoletwa kulazwa, na mara nyingi linakuwa hapo nje. Na pikipiki la
huyu nesi lilikuwa hakipo, sijui lilikuwa na nani kwa muda huo, lakini baadaye
lilionekana…
Aliporudi mimi nilikuwa pale dirishani,maana nilikuwa mara
kwa mara nafika hapo kuangalia je huyo nesi atarudi saa ngapi na akirudii atarudi
na huyo mgonjwa….na kama bahati nilipofika hapo dirishani nikamuona akifika na
pikipiki lake, akashuka kwa haraka na nyuma yake alikuwa kabeba kitu…’akasema
huyo nesi.
‘Kabeba kitu gani?’ nikamuuliza.
‘Kabeba kitu kirefu, inawezekana ni gitaa, ndivyo
nilivyowaza kwa muda ule, nikacheka kimoyomoyo, ina maana huyu nesi ni
mwanamziki pia, na sikuhanagaika tena nikarudi wodini, lakini baadaye moyo
ukawa haujatulia, nikatoka kwenda kumuona huyo nesi, sikumkuta ofisini kwake,
nikaondoka kwa haraka hadi kule wodini, sikumkukuta…nikaamua kuingia pale
alipolazwa mgonjwa.
‘Najuta kwanini nilifanya hivyo, maana nilipoingia pale
ndani, nilikuta mgonjwa kweli kalala, na katundukiwa ile mipira kama kawaida,
nikajua labda huyo nesi yupo kwenye sehemu ya kubadili nguo, nikaenda mle
ndani, na nikakuta hayupo pia, nikaingiwa na tamaa ya kuangalia kwenye kabati
lake, na hamadi nikaona yale manywele ya bandia aliyokuwa kavalia, na lile koti…
Nikawa na hamasa ya kuchunguza ule mzigo aliokuwa kabeba,
nikafungua vyema na kweli kwa ndani
nikakuta umeegemezwa, na kwa ujinga wangu,
nikautoa, na kuufungua maana ulifungwa kwa zipu, nilipofungua nafasi ya
kutosha, nikakuta ni chuma kimetokeza,….ooh,na akili yangu ikawaza, hiki sio
chuma kama cha bubduki kweli,…. nikafungua kwa mapana…oh,mungu wangu ilikuwa ni
bunduki,…nikaanza kutetemeka,…nikafunga ule mfuko kwa haraka na kulirudishia
pale nilipoikuta, na wakati nageuka kutoka mara nikasikia sauti ikisema kwa
hasira.
‘Wewe unafanya nini huku muda kama huu..?’ nilishituka,
karibu nidondoke chini, nikatoka hapo mbio,kwani alikuwa ni huyo nesi,na wakati
natoka aliniangalia kwa jicho la kiuaji kabisa.....
Nikasema ,`Kuna vifaa vimeniishia nakuhitaji boharini….’
‘Nakuona unachokonoa moto…chunga sana nyendo zako…’akaniambia
na mimi nikawa natetemeka,….
NB: Haya kwa leo tuishie hapa.
WAZO LA LEO:
Kufunga sio kufunga tu kula chakula, kufunga ni pamoja na kufunga matendo yote
mabaya, ni kujikurubisha kwa mungu zaidi kwa kufanya ibada zaidi,…kama vile
ndio siku ya mwisho wa uhai wako hapa duniani. Omba sana, tubu sana madhambi yako, na
uwe na huruma sana kwa wenzako, hasa masikini na wsiojiweza...
TWAWATAKIA WOTE RAMADHANI NJEMA NA WAAJIRI MUWASAIDIE WAFANYAKAZI WENU KUTOKA MAPEMA ILI WAWAHI KUFUTURU MAKWAO!
Ni mimi:
emu-three
1 comment :
dah, siamini kama natakiwa kusubiri hadi jumatatu kisa hiki kiendelee! kimefika patamu sana
Post a Comment