Kila mmoja alikuwa na hamu sana ya kutaka kujua majaliwa ya
hawo ndugu ambao inasadakiwa kuwa wamekunywa sumu, na haikujulikana kabisa vipi
hiyo sumu iliwafikia hawo watu wawili, cha ajabu Sokoti yeye alikuwa salama
kabisa, na wale waliokuwa na mtizamo wa haraka wakamshuku yeye kuwa huenda
kahusika na hilo.
‘Kwani ilikuwaje?’ mmoja wa wanafamilia akauliza.
‘Kwani inajulikana….! Bado polisi hawajasema lolote, lakini
kwa taarifa za awali ni kuwa, wakili mkuu na Nesi na Sokoti walipata muda wa
kukaa pamoja kwenye chakula cha mchana,na inavyosadikiwa , sumu hiyo ilinywea
muda huo….
‘Ilinywea na wao wenyewe wa kikusudia au waliwekewa bila ya
wao kujua?’
‘Hapo ndipo haijajulikani, ikizingatiwa kuwa wote wawili
wampoteza fahamu hadi sasa hivi …
‘Sokoti yeye vipi?’ akauliza jamaa mwingine.
‘Sokoti yeye hajambo , na yeye anashangaa kwa tukio hilo,
yeye anadai kuwa walipokutana ule mchana, walikaa pamoja na kuongea mambo yao,
lakini hakujua lolote kuhusu hiyo sumu, na anasema waliongea kwa muda, halafu
yeye akaitwa…’akasema huyo jamaa.
‘Akaitwa na nani?’ akaulizwa.
‘Yeye aliitwa na wakili wake, kwani yeye alikuwa na wakili
wake tofauti na wengine, na muda huo wakili wake alishafika na aliitwa ili wakaongee
naye, na hakupata muda wa kukutana na hawo wenzake tena, maana muda
ulishakwisha na waliamriwa kuingia kwenye vyumba vyao, na wakati wakiwa humo
,ndipo yeye akasikia kuwa wakili mkuu ana hali mbali …
`Ilikuwaje nesi akaja kukutana na wakili mkuu?’akaulizwa.
‘Nesi ndiye aliyeomba kuwa ana maongezi na wakili mkuu, na
alikubaliwa kwa utaratibu mzuri tu,kwasababu yote walishayasema na haikuwa na
haja ya kumzuia, waliruhusiwa wakutane…
‘Na humo rumande, wanakaaje, yaano Sokoti na wakili mkuu,
najua wanawake wana rumande yao, lakini hawa wawili hawakuwa karibu?’
‘Hawakai pamoja….walikuwa wametenganishwa tangia awali,
kwani walitakiwa wasikutane kipindi kile cha uchunguzi,….,hadi hiyo jana
walipokutansihhwa kwa maombi yao kuwa walikuwa na maongezi yao, ….’
‘Mimi bado nina wasiwasi na huyo Sokoti, huyu mtu anaweza
akawa anahusika kwa namna moja au nyingine, ..’akasema mwanafamilia.
*******
‘Mnaitwa huku, Msomali na wakili mwanadada….’tukasikia
tukitwa pale tulipofikahospitalini kuwaona waginjwa, …kulikuwa na ulinzi mkali,
na hata tulipoomba kuwa tunahitaji kuwaona hawo wagonjwa hatukuruhusiwa moja
kwa moja, ilibidi ombiletu lipelekwe kwa wakuba, na tukaambia tusubiri, na
baadaye ndio tukasikia tukiitwa….na kuelekea huko kwenye chumba cha wagonjwa
maalumu, nikahisi mwili mzima ukisismuka pale tulipoitwa.
Tukaingia kwenye
hicho chumba, baada ya kukaguliwa na
mlinzi, …na tulipoingia pale ndani tukamkuta mke wa wakili mkuu akiwa kasimama
mbali na kile kitanda na pembeni yake yupo Hakimu , yule hakimu aliyekuwa
akisikiliza maelezo yetu ya awali,…bado docta alikuwa akimuandaa yule mgonjwa,
na tuliambia tusubiri kwanza kidogo, baadaye akasema mgonjwa yupo tayari
kuongea na sisi, na tukamsogelea, yule nesi ambaye alikuwa kawekewa mipira
mwilini akafunua macho na kusema;
‘Mimi naona safari yangu imewadia, lakini nimeona kabla hiyo
saa haijafika, niongee na nyie, kwani najua kabisa nyie nimewatendea isivyohalali,nilihitaji
watu wengi zaidi ambao kwa ujumla nina uhakika nimewatendea mabaya, lakini nyie
ni muhimu zaidi kwa haya nitakayoyasema…’akahema kwa nguvu.
‘Muheshimiwa hakimu, wewe nimekuita uwe kama shahidi,….sina
makosa na wewe…lakini ni muhimu ukayasikia haya nitakayoyaongea pamoja na mkuu,
nyie ni kama mashahidi tu…na naomba nitakayoyaiongea hapa myawakilishe huko
kunakohusika,…na nashukuru kuwa mumekuja na vitu vya kurekodia,….leo nitaambia
kila kitu mungu akinipa pumzii ya kuongea….
‘Usijilazimishe,….’akasema docta
‘Usijali Docta,….unajua kila mtu atakufa, lakini kama
utaweza kupata mwanya wa kutubu dhambi zako, kwa wale uliowakosea ni bora sana,
kwani utakuwa umepunguza yale madhambi uliyoyafanya, yaliyobakia tena utakutana
nayo huko mbele ya muumba…na kila mtu ni mkosaji, na mbora wao ni yule anayejua
kosa na akatubu, na kutubu kwema ni kumuomba msamaha yule uliyemkosea…au sio…?.’akafunua
macho ktuangalia na sisi tulibakia kumwangali tu kwa macho ya huruma.
‘Msiwe na wasiwasi, na wala msionionee huruma, maana mimi
mwenyewe sijionee huruma, nyie kwanini mjione mna huruma sana kwa ajili yangu, …hapa
nilipo huenda nahesabu masaa,maana sikujua kama itafika muda kama huu, kutokana
na hiyo sumu, nilijua kabisa muda kama huu ingelikuwa dunia nyingine, …kama
nitanusurika basi ni majaliwa ya mungu…lakini sizani….
‘Ina maana unajua kuhusu hiyo sumu,…maana sisi tunahisi kuwa
kuna mtu kawawekea hiyo sumu?’ akauliza mkuu, na hakimu naye akaonyesha
kushangaa na kusogea karibu.
‘Sumu hiyo nilikuwa nayo mimi mwenyewe kwa muda wote….mimi
ni askari na kuna kitu sikuwahi kuwaaambia kuwa pamoja na uaskari wangu,
nilisomea ukomandoo, ingawaje hawakutaka nielekee huko kwasababu ya kuniona
nina hasira sana…anyway…hayo tuyaache. Sumu hiyo nilikuwa nayo, kwa namna ambyo
hakuna angeliigunuda, kwani nilijua itafika muda ambao nahitajika kuitumia,
tatizo ni kuwa dozi yake ilikuwa ya mtu mmoja, sasa nimeichanganya kwa watu
wawili, kwahiyo nguvu yake imepungua….sijui,…lakini yote ni majaliwa ya mungu..’akasema
‘Sasa kwanini ufikie hatua hiyo, ya kutaka kujiua?’
akaulizwa.
‘Ndio maana nimewaita hapa,..naomba mnisikilize kwa makini….maaan
sijui muda na saa za kuondoka, huenda nikashindwa kuwaambia kila kitu nilichokusuida
kuwaambia….kwahiyo naomba mnipe muda wa kuongea….’akasema na kunyosha mkono
mmoja ulikuwa huru kumuelekezea mke wawakili mkuu.
Mke wakili mkuu kwa muda huo alikuwa akimwangalia huku kashika shavu, na uso wake ulikuwa umejaa huruma...hakujali kuwa ni adui wake, hapo huruma ya kibidamua ilimtanda, na hata wakati mwingine kujilaumu kuwa kama angelijua asingelioana na wakili mkuu.....
‘Pole sana ndugu yangu,…..Wewe ni ndugu yangu katika
familia, kwanza kabisa naomba nikuombe msamaha kwa yote niliyokukosea, najua ni
vigumu sana kuelewa hili, lakini hadi hivi sasa nahisi kama wewe ndiye
uliyeninyang’anya pendo langu….najua moyoni utabisha hili, lakini kiukweli,
mimi na mume wako tulikuwa wapenzi wa muda mrefu…..’akatulia na mke wa wakili
mkuu akawa anazua machozi yasitoke.
‘Tulifikia hadi kuvishana pete, na hadi siku ya mwisho
nasikia kuwa anakuchumbia wewe ,mume wako mwenyewe alinipigia simu akasema hayo ni ya uwongo,…na taarifa zilipozagaa na
kuipata kuwa ni kweli anataka kukuoa wewe, aliniambai kuwa yeye anachofanay ni
kwa ajili ya kukamilisha mambo fulani huko Ulaya,eti kuna mambo ambayo mkiwa
mume na mke mnayapata…sijui, ni yapi…’akatulia.
‘Mimi kwasababu nilimpenda sana mume wako, nikamkubalia, …nikijua
ni taratibu tu za muda, ….hata wakati mnafunga ndoa nilijua kuwa ni geresha tu,
lakini siku hiyo nikahisi kuwa nimepigwa changa la macho, …nikajaribu
kuwasiliana na mume wako kwa simu, akawa hapatikani tena kinyume na makubalian
yetu, kila mara nikimpigia simu akubali kuongea name, ili nijue nini
kinaendelea…’akatulia.
‘Haya ninayo kuambia sasa hivi ndiyo ya ukweli, maana sina
muda wa kumdanganya mtu, nidangaye ili iweje, wakati ndio nakwenda huko kwa
hakimu wa mahakimu, asiyedanganyika. Basi kwa siku ile sikuweza kulala, hasira
chuki na wivu vikanijaa, hebu fikiria mtu wako unajua hivi sasa yupo na mke
mwingine, na hebu ichukulie katika hali halisi, ingelikuwa ni mke mwenza sawa,
lakini hiyo haikuwa ya mke mwenza, …lakini
hata hivyo namshukuru mungu kuwa nimejaliwa moyo wa chuma,moyo wauvumilivu, nilijua
ipo siku nitakuja kulipiza kisasi, kama kweli huyo mume wako aliamua kunitendea
hayo kwa kunidanganya……
‘Wiki na miezi ikapita, na nilipopata bahati ya kuongea na
mume wako, akanithibitishia kuwa msimamo wake upo pale pale, ..kuwa kakuoa ili
kufanikisha mambo fulani fulani, akiyaweka sawa, atakuacha wewe na tutafunga
ndoa mimi nay eye…lakini hilo likachukua muda sana, sikuona dali li hiyo. Na hayo
mambo anayoyafanya ni yapi, hakuwahi kuniambia…..
‘Basi siku moja akanipigia simu kuwa ananiomba nifanye kila
njia nije huku Dar…yeye atafanikisha mambo ya ajira, …..kwahiyo kuja kwangu
huku Dar na mengineyo, ilikuwa ni dhamira ya kuja kukamilisha kile
alichoniahidi mume wako, kuwa anataka kuimaliza ndoa yenu, ili aje anioe mimi,
na ndio maana kafanya kila mbinu msipate mtoto…’akasema
‘Eti nini….?’ Akashangaa mke wa wakili mkuu.
‘Umesahau kuwa mimi ni nesi,…ndio weweni docta ,….ndio najua
kama docta unajua mengi zaidi yangu,….lakini mimi ni nesi na mzoefu wa mambo
mengina….ambayo wewe na udakitariw ako huyajui, sio kwamba huyajui kiutalaamu,
unayajua kihivyo, lakini kwa utendaji,..kwa uzoefu, mimi najua mengi, …ambayo
wewe kama docta usingeliweza kuyahalalisha….mume wako kuna dawa alizokuwa akizitumia,
ili msipate uja uzito…’akasema.
‘I can’t believe this….this is too much….’akasema mke wa wakili
mkuu, akiwa kakunja ngumi kwa hasira.
‘Sisemi hili kwa nia ya kukuumiza wewe, nasema hili ili
kutoa kile chote kilichokuwa kimejificha, nafsini mwangu, ili mwisho wa siku
usije ukajilaumu na kunilaumu mimi. Na pia usije ukajilaumu kuwa huenda
hukujaliwa kuwa na mtoto na mume wako,…yote hayo ni mipango yangu na mume wako,
kama angelikuwepo hapa angelithibitisha hili…lakini najua hali yake huko alipo
naye anahesabu masaa, na nijuavyo mimi wanaume hawana kinga kubwa ya uvumilivu
kama sisi …sijui nisikukatishe tamaa…’akasema huku akionyesha maumivu fulani
tumboni.
‘Nilipofika hapa Dar, nikagundua kuwa pamoja na kuwa mume
wako ananipenda, lakini ….ana tamaa sana, hakuwa na subira, hakutaka kuvumilia,
hasa pale alipokuwa kija kwangu,kwa nia ya kustarehesha mwili wake, na mimi
namtolea nje, kwa kuwa yeye ni mume wa mtu, na anastahili kuwa makini kwa hilo.
Hili lilimtesa sana, na ndio maana akawa anaruka nje,…na hili sikulipenda
kabisa, ndio maana nikaingia kwenye uadui na akina Kimwana.
‘Wivu nilioupata kwa akina Kimwana, ulizidi wivu nilioupata
kwako wewe, kwa vile kuolewa kwako wewe kulikuwa na sababu maalumu na
nilifahamishwa hilo kuwa ni kwa mipango ya muda…na nilijua ipo siku utaachika,
na hilo ndivyo ilivyokuwa ndio maana kwenye ndoa yenu kulikuwa hakuna upendo….’akasema
na kutulia.
Lakini kusikia kuwa mume wako anatembea na Kimwana..hiyo
sikukubali, nikajua kuwa ni tamaa za mume wako…, na hata hivyo kauli ya Kimwana
ambaye nilikuja kumweka kama rafiki yangu, kwa ajili ya kujua nini kinaendela
ilikuwa ianumiza zaiidi ya kuchomwakisu cha moto. Kimwaan ana majigambo ya
kuuzi, ….
Kauli ya Kimwana ilinifanya nimuwekwe kwenye kundi la maadui
wangu wakubwa…kwako wewe sikujali sana, kwa viel nilijua kuwa huenda huna hatia
na hili, ingawaje sijui kulitokea ushawishi gani hadi akaamua kukuoa wewe, na
wakati wewe mwenyewe nahisi ulijua kuwa huyo ni mchumba wangu….’akasema na mke
wa wakili mkuu akasema kwa hasira.
‘Mimi sikujua hilo….ningelijua nisihangaika kiasi hicho….’akasema
.
‘Huu ni muda wangu wa kuongea,kama hukujua hilo, sina
makosa, lakini nakumbuka kuna siku nilikuambia kuwa nina mchumba wangu, mnasoma
naye huko Ulaya, huenda kosa langu ni kutokumtambulisha kwenu nyie….sijui
nilijisahau vipi,lakini ndivyo ilivyokuwa, kuwa huyo alikuwa mchumba wangu na
ahadi ya kuoana ilishapitishwa,....'aatulia kudogo, na sauti sasa ilikuwa inatoka kwa shida.
'Sasa hebu fikiria wewe menyewe kama ungelikuwa kwenye
nafasi yangu ulingelichukua hatua gani….najua utasema ningaliachia mbali,
wanaume wapo wengi, lakini hebu fikiria huyo mume anakuja kwangu na kuniambia
kuwa bado yupo na mimi, na mimi kweli nampenda….’akatulia kidogo
‘Kwahiyo nilipofika hapa Dar na kukutana na huyu Kimwana
nikajua sasamambo yameharibika, maana mimi ilivyomchunguza Kimwana nikamjua
kiundani na jinsi ninavyomjua mume wako, nikajua kuwa kama nitamlegezea Kimwana
tutakosa wote, na kukosa huko kutakuwa kubaya zaidi,maana Kimwana hajatulia,…nikajiona
kama mtu aliyeruka mkojo na kuja kukanyanga mavi….
‘Kimwana aliamua kushindana na mimi na kusema kuwa
atahakikisha kuwa huyoo mume wako anakuacha na kumuoa yeye,na pili atahakikisha
kuwa kila mlichochuma naye anakichukua yeye, na mwisho wa siku atahakikisha
kuwa unaukimbia huu mji,…..kwa muda ule hakujua kuwa mimi na wewe tuna udugu
fulani….kwangu mimi ilikuwa kama mtu mzima kutishiwa nyau, lakini mwisho wa
siku nikagundua kuwa kweli Kimwana kazamiria…
Ndipo kundi hilo likaanzishwa, na pamoja na mengine,
nikagundua kuwa kundi hilo litanisaidia sana kummaliza Kimwana kiujanja, na
yeye hakulijau hilo,….hadi siku ile alipokutana na mauti yake, najua siku ile
alishagundua mengi..na lishagundua kuwa mengi yanayomsibuu ni kutokana na mimi,
na alishajiandaa kuja kukabiliana na mimi, lakini alichelewa…
‘Kwahiyo wewe ndiye uliyemuua Kimwana…?’akaulizwa.
‘Subirini,bado naona roho ipo, nitawaambia kila kitu,….’akatulia,…na
mara tukamuona akibadilika, akajitahidi kufunua mdomolakini hakuweza,… na mara
macho yakafunga…na hata ile mashine ya kusaidia kupumualia ikaanza kupiga ukulele…docta
akaja kwa haraka na kuanza kumhudumia.
‘Tafadhali tokeni nje….’akasema docta na kuzungusha lile
pazia la kumzuia mgonjwa asionekane….
NB: Kila nikijaribu kumalizia najikuta kuna sehemu
nimeiacha, na kwahiyo inabidi niiongezee, lakini kama mnavyoona kisa kinafikia
ukingoni.
*********************************************************************************
WAZO LA LEO:
Mwezi wa Ramadhani huo unakuja, na mwezi huu ni sehemu ya kusafisha amdhambi yetu.
Ni kama vile shati chafu, na unataka kulifua, …ni kama vile gari ulilolitumia
kwa muda mrefu linahijika kulifanyiwa service…miili yetu imekuwa ikila vyakula
vingi kwa mwaka mzima, na mwezi huu mmoja ni sehemu ya kuufanyia mwili wetu`service’.
Sio mwili tu, kiroho pia, kutubu dhambi, kunyenyekea na kuwa na huruma kwa
kusaidiana,na hasa kuwasaidia masikini.
Karibu mgeni wetu, karibu Ramadhani, mungu atujalie sote
tuweze kutimiza ibada hii muhimu.
DIARY YANGU INAWATAKIA KILA LA HERI WASILAMU WOTE DUNIA KATIKA MFUNGO HUU MTUKUFU WA RAMADHANI.
*********************************************************************************
picha hii toka kwa :
http://abdallahmrisho.blogspot.com/
Blog yenu hii inaungana na Watanzania wengine kwa majonzi haya yaliyotupata kwa ajali nyingine ya Meli, na hili linaanza kuwa donda sugu, tunaishia kuongea kipi kifanyike, lakini sijui kama kuna utekeelzaji. Poleni sana kwa wale waliopoteza ndugu zao, mungu awape subira, na waliotangulia mungu awalaze mhala pema peponi, kwani, Kwake yeye ndipo tumetoka na Kwake yeye tutareja.
Ni mimi:
emu-three
4 comments :
mimi nawasifu kwa kuandika jamani....tena mpangilio mzuriii...mafundisho....keep it up
Kaka, naikubali sana kazi yako, yaani
natamani uwe unaweka mpaka cku za wikiend, hongera sana!!! Mimi S.
Poleni sn kwa janga,lililotokea huko Znz,Mungu mwenye rehema,awape unafuu wale wt waliokumbwa na janga hilo na kuzipokea roho za wale wt waliotangulia kwake,kupitia kwa janga hilo.
Nakutakieni mfungo mwema wa Ramadhani,inshalaa,tupo pamoja,mnaanza kesho au?
Mimi C
Ndugu wa mimi kazi inazidi kukuwa nafurahi mno!Mungu azidi kukubariki na nakutakia Mfungo mwema!!!!!
Pamoja Daima ndugu wa mimi.
Post a Comment