Tausi Binti Maringo, ni yupi....? nikajiuliza.
Je ni huyu mgeni niliyeambiwa
kaja toka kijijini akapitia hapo kwangu kuniulizia au ni huyu mwanadada rafiki
yake mke wa wakili mkuu? Nikajiuliza huku nikiwa nimeinama chini, wakati
namsubiri wakili mwanadada aniambie nini alichoniitia.
Wakili mwanadada akaja na kukaa kwenye sofa, baaada ya
kupnga mambo sawa humo ndani, akasema;
‘Usiwe na wasiwasi,mambo leo yatakuwa shwari, ni siku
maalumu sana leo, na na muomba mungu iwe hivyo,…,nahisi wapo njiani
wanakuja….’akasema.
‘Akina nani hawo wanakuja….na ni siku gani hiyo maalumu,
kuna nini ambacho mimi sikujui…?’ nikauliza.
‘Wahusika wa mkutano huu,…. kwani ujumbe wangu ulisemaje?’
akaniuliza.
‘Kuwa kuna kikao hapa kwako…’nikasema.
‘Sasa kikao ni cha watu wawili,kama ingelikuwa nakuita mimi
mwenyewe nisingetumia lugha ya `kikao’, au Kiswahili ni kigumu kueleweka,…kikao
maana kina wajumbe….’akasema.
‘Kwahiyo na hilo nalo ni siri, la kujua ni nani wanakuja,
maana sasa hivi kila jambo lako unalifanya la siri, nitakuita dada wa maswala
ya siri…’nikasema huku nikitabasamu, sikujua ni kikao cha namna gani na ninani
wanakuja, ila hisia zangu zilikuwa zinaniambia kuna jambo ambalo huenda
likawahusu wale dada wawili.
‘Yote hayo yanafanyika kwa ajili yako, na tunafanya hivyo ili mambo
yaende shwari,…wewe utaona jinsi itakavyokuwa, tukiharakisha mambo inaweza
ikaleta sintofahamu nyingi, kinachotakwa ni wahusika wakuu wenyewe wafunguke,
kila mmoja atoe kile kilichopo nafsini mwake….inapendeza na italeta tija, ’akaniambia.
‘Haya mimi naona sasa nisubiri tu, maana nitaumiza kichwa
changu kwa kuwaza,…naomba iwe ya heri tu….’nikasema na kutulia.
‘Ni kweli mvumilivu hula mbivu, na mwenye shida ndiye
anayefuata moto…uliwahi kuona moto ukifuata watu, wewe mwenye baridi ndiye
unatakiwa uufuate moto, na moto ukikufuata wewe ujue ni janga,..kwahiyo kazi ni
kwako.Mimi nimetimiza wajibu wangu, na leo nataka wote mfunguke, …muwe huru,
semeni ongeeni,….’akasema
‘Wote na nani…?’ nikauliza.
Na mara mlango ukagongwa, na wakili mwanadada akakimbilia
mlango kufungua, na akiwa na mcho ya furaha akasema;
‘Karibuni wageni…’akasema na wakaingia mke wa wakili mkuu,
na rafiki yake, na mwanaume mwingine nisiyemfahamu, na mawazo yangu yakawaza
mbali, nikijua huenda ni mchumba wa huyo rafiki wa mke wa wakili mwanadada.
‘Jamani kwa utambulisho,….ingawaje nafahamu mnafahamiana,
lakini ni vyema nikaweka haya mambo bayana,… huyu hapa ni rafiki yangu,ambaye
amekuwa ni kaka yangu wa kufikia, tofauti na watu wenye mawazo mafupi walioanza
kunivumishia. Mimi ni mtu mzima nina akili zangu sawa sawa, kama ingelikuwa
hivyo wanavyosema, kwanini tujifiche,….Kaka huyu, tumejuana katika mishe mishe
za hapa na pale, ….’akasema na kunishika kwenye bega.
‘Ni kweli kabisa wewe ni dada yangu mpendwa, bila wewe
maisha yangu yalikuwa taabuni , wewe ni zaidi ya ndugu….’nikajikuta nikisema.
‘Na huyu hapa ni mke wa bosi wangu, kwa maana hiyo ni bosi
wangu pia maana ndiye anayeniweka
mjini…kama mtu anakuajiri na kukupa mkate wako wasiku inabidi umuhuheshimu
sana, na nashukuru kesi inakwenda vyema usijali kabisa, ….’akamsogeleana
kumshika bega na mke wa wakili mkuu akasema kwa uchungu.
‘Nakushuru sana wakili mwanadada, na niseme wazi, kuwa wewe
ni mtu mwema sana, maana mtu ambaye anajitolea kuwajali wenzake, bila kujali
gharama, bila kujali matokea yake kuwa yatakuwa na faida kwake, unachojali ni
kuona wengine wanaondokana na matatizo waliyo nayo, ni wachache sana katika
dunia,…watu wengi husaidia pale wanapoona kuwa watapata chochote,….nakushukuru
sana na mungu akuzidishie…’akasema mke wa wakili mkuu.
‘Nashkuru kwa dua zako, na huyu hapa ni rafiki yake, mpendwa, natumai
wengi tunamjua kama docta, ….na mengi atakuja kuyasema mwenyewe, maana nhisi
kuwa yeye ni muhusika mkuu wa kikao hiki, nisingelipenda kumwaga mtama kwenye
kuku wengi, kabla muda haujafika….na huyu hapa ni…mmh,labda munisaidie
kumtambulisha.
‘Mimi ni kaka yake Tausi,..huyu hapa, mimi ni kaka
yake,ambay enilikuwa nje kimasomo, na nilirejea muda, nikawa kazini,na kama
unavyojua kazi zetu, ukiingia hupati muda wa kutoka. Ilibidi familia iliniagize
nije haraka ili niweke nguvu zangu, kwa vile na mimi ni mwanasheria nikaona ni
vyema nije kama inabidi niweze kumtetea ndugu yangu.….’akasema na aliposema
hivyo moyo wangu ukatulia.
‘Kesi sio mbaya, maana wale vinara wa hayo mauaji
wameshatambulikana, iliyobakia ni kuhitimisha tu, na kwa vyovyote vile kesho
inawezekana ikawa ni hitimisho la hii kesi. Unajua binadamu akishatenda kosa na
lile kosa likawa linahusu damu ya mtu, mata nyingi atakuwa haan raha, na ili
kuliondoa lile doa moyoni, hufikia hatua akasema ooh, ngoja nitubu mapema,
maana kuanleo na kesho, huna mamlakana roho yako…ukifa na deni la kuua, siju
utakwenda kusema nini…’akasema wakili mwanadada.
‘Ni kweli, labda mtu huyo awe ni mnyama…maana binadamua
kibadilika anaweza akawa ni zaidi ya mnyama, ..hata hivyo, kila jambo lina
mwanzo namwisho wake. Tutaona itakavyokuwa…..’akasema huyo mgeni.
‘Haya karibuni sana, na sitaki kupoteza muda wenu mwingi,
ninataka kuingia moja kwa moja kwenye msingi wa kikao hiki. Mimi ni wakili, na
pamoja na hayo, nimekuwa nikijihusiaha sana katika masuluhisho ya ndoa za watu.
Na hili limekuwa kama jambo muhimu katika maisha yangu. Nina kuwa na furaha
sana ninapoona watu wanapendana, watu wanaishi kwa amani, hasa kwa mke na mume,
na kinyume chake ni maumivu kwangu….
‘Katika tukio hili ambalo linaendelea mahakamani, limekuwa
kama kazi maalumu kwangu, kazi ambayo nahisi itakuwa ni sehemu muhimu ya
kukamisha mradi wangu wa kutunga kitabu cha maswala ya familia na maisha ya
ndoa. Kwa ujumla nimejifunza mengi sana kutoka kwa waliohusika katika sakata hili
zima. Na sasa nimepata kitu muhimu sana ambacho kinaweza kikasaidia watu
wengine baadaye.
‘Katika dunia hii ili kweli uonekane msomi, ni lazima ufanya
jambo linaloweza kuisadiai jamii. Mimi sioni usomi ambao unajisaidia wewe mwenyewe
tu, kuwa umesoma, na kinachofanyokani kushibisha tumbo lako na familia yako,
huo ni usomi wa kichoyo. Usomi ni pale jamii inapofaidika na kile ulichokisoma,
ukaisadia jamii, hata kwa gharama isiyo na tija, tija yake ni kile
ulichokifanya. Mfano ukisadia jamii, ikanufaika na ule usomi wako hiyo ni tija
yeney tahamani kubwa sana, kuliko pesa utakayopata.
‘Wapo wasomi, kutokana na usomi wao jamii imekuwa
ikiumia,..hutaamini hilo, mtu anasoma ili we mjanja kuiba mali ya uma, kuibia
wanajamii…hii ni dhulumakubwa sana. Huu sio usomi, huu ni ujambazi, na mtu kama
huyu ni sumu katika jamii. Tujue kabisa kusoma kwetu ni jasho la wazee wetu na
waliotangulia, walihangaika sana na sasa tupo huru,…kuna waliopteza roho zao na
hawakufanikiwa kabisa kukipata kile walichokihangaikia, ..hawa watalipwa na
nani, kama sio sisi wasomi kujitolea….hili kwangu nimeliona na ndio maana
najitoleakuwasiaida wenzangu.
‘Ndoa,….jamani ndoa ni tatizo …wengi wanakimbilia hadi
kusema ndoa ni ndoana, …sio kweli, ndoa haikutakiwa ieleweke hivyo. Kiujumla ndoa
sio ndoana,….ndoa ni sehemu ya kustarehe, kuunganisha nguvu, kusadiana, na
kuweka kitukiwe kamili,…. wanaofanya ndoa iwe ndoana ni wale wanahusika na hiyo
ndoa,….ambao wanaitwa wanandoa, lakini hawaijui hiyo nda ni misingi yake.
Wao kwa kutokuwa
makini, ….wakaingia kwenye chumba hicho kiitwacho wanandoa, bila kufumbua
macho, na kwahiyo wakaingia hapo bila kujua ni nini kipo humo, na wanahitajika
wafanye nini, ial walickwa kutokuhotaka ni siafa tu ya kuitwa waanndoa na
baadaye wanaharibu maana kamili ya ndoa, wanakichafua chumba…, hawa watu
wanajikuta wakihamanika, kushika huku na kule. Kwanini mfumbe macho, wakati
macho mnayo..ni ajabu kabisa….
‘Hili nimekuwa nikilirudia mara nyingi, kuwa mnapoingia
kwenye chumba cha ndoa ni muhimu mkayafungua
macho yenu vyema, ili mjue wapi mnapokanyaga, na nini kipi humo ndani,….maana
ukitemeba ukiwa umefumbamacho utajigonga
kwenye ukuta. ..
Ndugu zanguni, nyie wote hapa mumejaliwa kuwa kwenye ndoa,
na kwahiyo nikisema ndoa mnajua ndoa ni ni nini, na pia kwabahati mbaya wote
mumejikuta mkiwa katika matatizo ya ndoa, sijui kuhusu huyu mwenzetu mgeni,
kama yeye ndoa yake haijabahatika kuwa
na mataizo, lakini nijuavyo mimi, matatizo ya ndoa ni kitu cha kawaida….cha
muhimu ni kufungua macho, na kuwa makini,…ongeeni, matatizo yenu..kwanini
muogopane,..nashangaa kabisa!
‘Mimi sio mwalimu, najua wenzangu hapa ni walimu zaidi
katika maswala ya ndoa, na nilishangaa sana kuona kuwa mwalimu wa maswala y
andoa naye anajikuta katika matatizo ya kindoa, nikajua huenda ni kwasababu ya
ule usemi usemao, kwenye miti mingi mara nyingi hakuna wajenzi,sijui kama usemi
huo unafaa katika hayo yaliwasibu au la…’akatulia kwa muda huku akiwaangalia
washiriki humo ndani.
‘Naona nisiwapotezee muda, ngoja niingie kwenye lile nililowaitia
hapa, kama nilivyowaambia kuwa mimi katika moja ya kazi yangu ni kusuluhisha
matatizo katika ndoa. Na leo hii kuna tatizo moja katika ndoa ya aina yake.
Ndoa hiyo kisheria inaweza ikawa isikubalike, lakini kiroho, kiimani na
kiupendo ilikuwepo, na hata siku nilipohadithiwa mimi kuhusu hiyo ndoa
nilizania ni utani…’akatabasamu.
‘Hebu niwaulize, hivi kweli kuna upendo kati ya watoto chini
ya miaka kumi, yaani wapendane kiukweli hadi kuitwa wapenzi?’ akauliza na
kuniangalia mimi. Sikujibu lile swali kwanza nikacheka na baadaye nikasema;
‘Mara nyingi mapenzi hayo ni ya kama michezo ya kitoto, na
nahisi wengi wakishakua wakubwa wanayasahau, na kujikuta wamekutana na wapenzi
wengine na kuyasahau hayo ya utotoni, ila wapo waliobahatika na kujikuta
wakiendeleza mapenzi yao hayo,lakini ni wachache sana…’nikasema
‘Kwanini iwe hivyo, kama kweli mlipendana mkiwa watoto, na
mkawa na yakini ya mapenzi ya kweli, mpaka mfikie hata kuchumbiana kitoto,..hizo
fikira zinakujaje, maana kamamumefiukia hatu aya kujua kuwa mke na mume
wanatakiwa kuwa wachumba, kuwa mke na mume, huoni kuwa ila akili palesio ya
kitoto tena, kuna mwongozo mliupata toka kwamuumba, ….inakuwaje mkisha kuwa
wakubwa msiyakumbuke hayo ya utotoni?’akaniuliza.
‘Tatizo kubwa ni umri, mihangaiko ya maisha na kutwanyika
kila mmoja akaeleekea kwake, na huko kila mmoja alipo anajkikuata anakutana na
maisha mengine na wapenzi wengine, kwahiyo mnajikuta mumesahau yale ya
utotoni…’nikasema.
‘Kwahiyo yale ya utotoni hayakuwa mapenzi ya kweli, ni
michezo yakitoto tu?’ akauliza.
‘Inategemea mtu na mtu, inaweza ikawa mapenzi ya kikweli,
lakini kama nilivyosema watu mumetawanyika, huwezi jua mwenzako yupo wapi,
kweli utasubiri mpaka lini ,uzeeke ukimsubiri mwenzako, …, na je kama mwenzako
keshaolewa, …utakwenda kuvunja ndoa ya watu, .na vitu kamahivyo.’nikasema.
‘Na je kwanini afikie kuolewa kama kweli mliahidiana na
kuapizana kuwa mtakuwa wachumba, mtakuwa mke na mume?’ akauliza yule mwanadada
ambaye alikuwa katulia kimiya.
‘Tatizo hapo ni mawasaliano, kama yapo mawasiliano, sizani
kwamba itakuwa ni tatizo,…’nikasema.
‘Hata kama kuna mawasaliano, na mmoja akawa sio mwaminifu,
anatembea na wanawake wengine unaweza ukamwamwanije huyo mtu, kweli ana mapenzi
ya dhati, au ni mchezo huo wa kitoto kama ulivyouita, ?’ akaniuliza huyo
mwanadada.
‘Kila kitu kina muda wake, ujana una mambo yake, na inafika
sehemu mtu unatulia, ….haiwezekani ukawa na tabia hiyo hiyo hadi umri kama,
wangu….kama mtu alikuwa na tabia huyo, lazima inafika mahalii anasema sasa
basi…kama mimi hivi sasa siwezi nikawa na tabia ile ya ujananii tena…mtakiwa
niwe na mkenitulie….’nikasema.
‘Kwanini sasa huna mke?’ akaniuliza yule mgeni.
‘Nilikuwa naye,lakini matatizo yakatokea, maana imekuwa kama
unajaribu …na unajikuta kumbe sio yeye uliyemtaka….labda niseme wazi kuwa yupo
ambaye mungu alinipangia, na sijaweza kumpata tena, sijui yupo wapi?’nikajikuta
niksema kwa uchungu.
‘Hebu nikuulize swali, ambalo huenda nilishawahi kukuuliza , ila nakuuliza hapa kwa niaba ya wengine, wakusikie nini utaongea, Je wewe katika
ujana wako uliwahi kuwa na mpenzi wa ujanani,…?’ akaniuliza wakili mwanadada.
‘Ndio , nakumbuka nilishakaumbia hilo, niliwahi kuwa na
mpenzii wa utotoni,..hadi ujanani, na
ujanani nikawa na tabia ya kihuni, ….siunajau tena ujana ulivyo, lakini sasa
najuta maana niliyoyafanya ujanani,yaliniharibia yale niliyoyakusudia, na hata kumpoteze
mpenzi wangu niliyempenda sana….’nikasema.
‘Je huyo mpenzi hamjawahi kuwasilina naye….?’akaniuliza yule
mgeni.
‘Kama ningelijua yupo huru,hajaolewa,….nimejaribu kila njia
sijapata mawasiliano naye, …ningelijua kuwa yupo huru, hana mume, ningemfuata
huko alipo….’nikasema.
‘Una uhakika na hilo kweli?’ akauliza yule mwanadada.
‘Sasa ningelikuwa na uhakika, ningelisema hivyo jamani…hili
nalisema wazo mbele yenu,mungu angu ndiye shahidi, hamjui moyoni kwangu kuna
nini, ninateseka kweli nikimuwaza yeye….’nikasema kwa uchungu
‘Je kama akitokea,na tusema hana sura ile ya utotoni,maana
mtu akiwa mkubwa haubadilika, huwezi jua maisha yalivyo, unaweza kweli ukawa
naye licha ya mabadiliko hayo…?’ akaniuliza.
‘Kama kweli bado ananipenda, kwanini nisiwe naye tena, …kwakweli nitafurahi sana kuwa naye tena….maana
mapenzi yetu yalijengeka toka moyoni….’nikasema nikionyesha uso wa furaha.
‘Hebu nikuulize, ina maana mtu huyo ulikuwa ukimpenda ukiwa
mtoto, na pendo hilo lilikuwa la moyoni, ina
maana umri unaweza ukalibadili
hilo pendo, usimkumbuke huyo mtu kabisa,….?’ Akauliza yule mke wa wakili mkuu.
‘Sizani, ….sijui, kwakweli, maana umri upo na ni kweli umri
uanweza ukabadili sura za watu …lakini ina maana mtu abadilike kabisa uisweze
kumtambua ….!’ Nikakuta nikisema huku nikimwangalia yule mke wakili mkuuna tena
nikageuka kumwangali yule mwanadada mwingine na kushangaa akiwa anatoamachozi. Halafu
yule mwanadada akatikisa kichwa kwa kuonyesha kusikitika akasema;
‘Mimi nina amini kabisa kama mtu unampenda kweli huwezi ukamasahau
abadani, labda kama ulikuwa unampenda kubahatisha…. lakini kama yupo moyoni ,
hata awe mkubwa vipi sura itabakia moyoni, ….mimi nina imani kuwa wewe huyo
uliyekuwaukimpenda mkiwa watoto, alishafutika moyoni mwako kwasababu ya
kukutana na wasichana wengine hapo katikati..huna mapenzi yakweli wewe
usitudanganye….’akasema.
‘Kwanini unasema hivyo, ….wewe unanijulia wapi maisha yangu….’nikasema
kwa hamaki.Na kwaharaka nikatoa picha ya huyo msichana ninayemfahamu akiwa mdogo,
nikasema;
‘Hebu jamani nisaidieni, ..hebu niambieni, huyu hapa ndiye
aliyekuwa msichana wangu wa utotoni, niambieni mlishawahi kumuona wapi, ili uongo
wangu udhihiri, ni nani anayefanana naye ambaye mliwahi kumuona?’ nikawauliza.
Kila mmoja aliiangalia ile picha na kukuta kweli hakuna sura
ya msichana au mwanamke anayefanana naye wanayemjua…
‘Haya niambieni, ukweli ni msichana gani mliyewahi kumuona
hapa anayefanana naye?' Nikauliza na kuwaangalia, na mara yule mwanadada kwanza
aliniangalia kwa mshangao, na baadaye akageuka kama kunikwepa , na kuangalia pembeni, akitabasamu,na aliponigeukia mara ya pili kuniangalia nikashangaa kumuona macho yamejaa machozi, analia….
‘Unalia nini ….maana muda mwingi nakuona upo katika hiyo
hali…?’ Nikamuuliza yule mwanadada, nikimuonea huruma.
‘Kuhusu mabadiliko ya sura, ninaweza kusema sio kosa langu….sio
kosa langu kabisa ni madhila ya dunia….’akasema huku analia.
‘Ni kosa la nani hilo, na kwani unamjua huyu mwenye hii picha?’nikauliza.
‘Ni kosa la wale wasiojali wenzao, ambao kutamka kwao ahadi
ni rahisi kuliko kuitekeleza hiyo ahadi, hawana huruma na wenzao. Nakubali
kabisa huyo mwenye picha hiyo ni mimi,…’akasema yule mwanadada.
‘Ni wewe….hapana,….mbona hamfanani, …aah,mungu
wangu,nakajikuta nikiinuka na kwenda kusimama mbele yake huku nimeshika mdomo nikioana aibu, na kumchunguza kwa
makini....yeye aligeuka pembeni, ....
‘Ndio mimi, mwenye hiyo picha, lakini …kuna kipindi nilikuwa
nikitumia dawa ambazo zilifanya nibadilike sura, sikuwa na nia hiyo ya
kujibadili sura, dawa zile nilipewa kutokana na mataizo yangu, ya kiafya, ya
kuchanganyikiwa, na kila nikizitumia zikawa zinanibadili sura yangu nakuwa
mweupe kupita kiasi. …’akasema huku akibubujikwa na machozi.
‘Kwangu mimi sikujua wala kujali mabadilikohayo, kwani kwa
muda huo, nilikuwa nikjiona kawaida ,
kwani kwa kipindi kile sikutaka hata kujiangalia kwenye kiyoo, nilikuwa najiona
mfu anayetembe…mpaka kipindi nilipokwenda kijijini kwetu, na kujiikuta watu
wengi wakiniuliza mimi ni nani ndipo nikagundua kuwe kweli nimbeadilika,....’akatulia.
‘Hilo ni kweli, kwani hata mimi nilimsahau kabisa dada yangu, kwani nilikuwa nje kimasomo, na
niliporudi muda fulani, ili bidi nianze kuulizia dada yangu yupo wapi, nikaishia
kuchekwa, …hizo dawa nyingine za kienyeji mnatakiwa muwe makini nazo, lakini
kwa kipindi kile kwa dada yangu haikuwa na jinsi kilichotakiwa ni kumsaidia….mimi
mwenyewesiamini kuwa sasa dada yangu katulia,…’akasema huku akimwangalia dada
yake.
‘Lakini mimi naona ni nzuri, maana kama zilikubadili sura na
hakuna madhara mengine zaidi huoni kuwa zimekufanya ukawa mrembo
zaidi…..’akasema mke wa wakili mkuu ambaye muda mwingi alikuwa kimiya.
‘Kwani urembo ni weupe, mimi kwangu urembo ni ule wa asili,
hata kama uwe mweusi, mwekundu…lakini kama ni urembo urembo ni uasili wako, na
kama umejaliwa kuwa mrembo, wewe ni mrembo tu….ni mrembo ni mtu ni jinsi mtu
anavyomuiona yeye…’akasema kaka mtu.
‘Lakini huoni athari zake kwani yule niliyempenda
alishanisahau, na kama alinipenda kwasababu ya sura yangu ya asili,au linipenda
kwasababu ya sura tu, sasa hatanipenda tena….’akasema mwanadada.
Mimi nilibakia kuduwaa tu huku nikimwangalia huyu mwanadada,
nilikuwa bado nimesimama mbele yake, sikuwa bado naamini hayo maneno
nikikumbuka kuwa nimeambiwa kuwa kuna mgeni alikuja nyumbani ambaye alidai kuwa
ni rafiki yangu wa utotoni, sasa huyo mgeni ni nani….
‘Halafu nina mgeni toka kijijini alipitia nyumbani jana,
….’nikaanza kusema.
‘Mimi ndio nilipitia nyumbani kwako jana…kama una maana
mgeni aliyefika kwako akiwa ba begi,akakuulizia. Nilipita hapo kwako,
nilipotoka huko rumande, nia na lengo langu ni kufikia kwako, nijue ni kwanini
siku zote hukuweza kufika huko mahakamani,…na kukuuliza mengi,lakini sikukuta….’akasema
yule dada.
‘Kwahiyo wewe ndiye Tausi binti Maringo haswa…..eti, hebu
ringa kidogo..?’ akauliza wakili mwanadada na kusema kwa mzaha.
‘Kama yupo mwingine ni wa kuchongwa…najua kuna watu
walijaribu kuniigiza lakini mwisho wa siku walishindwa….’akasema huku
akionyesha uso wa huzuni
‘Mungu wangu ina maana wewe ndiye Tausi,..ooh, …’nikasema na
kujikuta nikipiga magoti mbele yake bila kuwajali wote waliohudhuria hapo , na
Tausi akaniangalai huku machozi yakimtoka, akaniwekea mkono wake kichwani
mwangu na kusema.
‘Ndio mimi mwanamke uliyemsaliti….’akasema huku akiwa
kaniangalia akatulia kidogo halafu akasema tena,
'Lakini mimi sikuweza kukusaliti hata chembe, mungu ndiye shahidi
yangu, nimeweza kuitunza ahadi yangu ya utotoni hadi hii leo, …uone jinsi sisi
wanawake tulivyo na upendo wa dhati….’akasema huyu mwanadada.
‘Naomba unisamehe maana yote yalikuwa ni majaribio ya kimaisha….sikujua
nini nitenalo kwa wakati ule… ,na nipo tayari kuipokea adhabu yoyote
utakayoitamka, ….’nikasema huku macho yakiwa na kiza za machozi, sikuamini …..
‘Adhabu yangu ni kuwa twende kijijini pale pale tulipowahi
kufunga ndoa na pale pale tukaifunge ndoa ya kiukweli ambayo unaiamini wewe
isiyo ya kitoto….’
‘Hilo tu, hata leo nipo tayari…’nikasema kwa furaha na watu
mle ndani wakashangilia.
Mara simu ya wakili mwanadada ikaita, haraka akaipokea na
kusikiliza kwa muda, alitulia na baadaye akawageukiwa washiriki humo ndani na
kusema;
‘Jamani mbona haraka hivyo, maana msisahau kuwa kesho ndio
siku ya kesi iliyopo mbele yetu, na kwa taarifa nilizozipata sasa hivi,
nesi na ….na wakili mkuu, wapo taabani
hospitalini, inasadakiwa wamekunywa sumu…na kwahiyo…’
‘Eti nini..’akasema mke wa wakili mkuu, na kuinuka pale
alipokuwa kakaa akijiandaa kuondoka.
NB:Tuwepo tena katika kumalizia kisa hiki.....nauliza tena kuna yoyote aliyebahatika kuwa na rafiki yake utotoni, na wakabatika kuja kuoana ..? Na je ni kweli kuwa sura inaweza kubadilika kabisa unakuwa mkubwa ukawa tofauti na ile sura ya utotoni? bado nawaza hili, natumai wewe unaweza kunisaidia, kama hutojali!
WAZO LA LEO: Ili
tuweze kuishi salama katika maisha yetu, ni vyema tukajifunza kusameheana. Na
ili kusameheana kuwepo, inabidi tuwe wepesi kukubali makosa pale tunapokosea.
Sisi ni wanadamu kukoseana kupo, hatuwezi tukawa wakamilifu wakati wote.
Ni mimi:
emu-three
2 comments :
kweli natamani ungeendelea mana umegusa mutima wangu what an happy ending kwa msomali baada ya madhila yote...
In my expertise, appraisals had been paid for at closing.
I personally believe chronic.cc they want you
to devote this guaranteed payday loans uk income up front in order that you're reluctant to walk away when lastly confronted with the bait and switch.
Post a Comment