Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary', na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..pia tunakaribisha mijadala na yale yote unayopenda yawemo humu. Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu. SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthreeWednesday, July 18, 2012

Hujafa hujaumbika-69 Hitimisho 27

Tausi Binti Maringo, ni yupi....? nikajiuliza.

Je ni huyu mgeni niliyeambiwa kaja toka kijijini akapitia hapo kwangu kuniulizia au ni huyu mwanadada rafiki yake mke wa wakili mkuu? Nikajiuliza huku nikiwa nimeinama chini, wakati namsubiri wakili mwanadada aniambie nini alichoniitia.


Wakili mwanadada akaja na kukaa kwenye sofa, baaada ya kupnga mambo sawa humo ndani, akasema;

‘Usiwe na wasiwasi,mambo leo yatakuwa shwari, ni siku maalumu sana leo, na na muomba mungu iwe hivyo,…,nahisi wapo njiani wanakuja….’akasema.


‘Akina nani hawo wanakuja….na ni siku gani hiyo maalumu, kuna nini ambacho mimi sikujui…?’ nikauliza.

‘Wahusika wa mkutano huu,…. kwani ujumbe wangu ulisemaje?’ akaniuliza.

‘Kuwa kuna kikao hapa kwako…’nikasema.

‘Sasa kikao ni cha watu wawili,kama ingelikuwa nakuita mimi mwenyewe nisingetumia lugha ya `kikao’, au Kiswahili ni kigumu kueleweka,…kikao maana kina wajumbe….’akasema.

‘Kwahiyo na hilo nalo ni siri, la kujua ni nani wanakuja, maana sasa hivi kila jambo lako unalifanya la siri, nitakuita dada wa maswala ya siri…’nikasema huku nikitabasamu, sikujua ni kikao cha namna gani na ninani wanakuja, ila hisia zangu zilikuwa zinaniambia kuna jambo ambalo huenda likawahusu wale dada wawili.

‘Yote hayo yanafanyika  kwa ajili yako, na tunafanya hivyo ili mambo yaende shwari,…wewe utaona jinsi itakavyokuwa, tukiharakisha mambo inaweza ikaleta sintofahamu nyingi, kinachotakwa ni wahusika wakuu wenyewe wafunguke, kila mmoja atoe kile kilichopo nafsini mwake….inapendeza na italeta tija, ’akaniambia.

‘Haya mimi naona sasa nisubiri tu, maana nitaumiza kichwa changu kwa kuwaza,…naomba iwe ya heri tu….’nikasema na kutulia.

‘Ni kweli mvumilivu hula mbivu, na mwenye shida ndiye anayefuata moto…uliwahi kuona moto ukifuata watu, wewe mwenye baridi ndiye unatakiwa uufuate moto, na moto ukikufuata wewe ujue ni janga,..kwahiyo kazi ni kwako.Mimi nimetimiza wajibu wangu, na leo nataka wote mfunguke, …muwe huru, semeni ongeeni,….’akasema

‘Wote na nani…?’ nikauliza.
Na mara mlango ukagongwa, na wakili mwanadada akakimbilia mlango kufungua, na akiwa na mcho ya furaha akasema;

‘Karibuni wageni…’akasema na wakaingia mke wa wakili mkuu, na rafiki yake, na mwanaume mwingine nisiyemfahamu, na mawazo yangu yakawaza mbali, nikijua huenda ni mchumba wa huyo rafiki wa mke wa wakili mwanadada.

‘Jamani kwa utambulisho,….ingawaje nafahamu mnafahamiana, lakini ni vyema nikaweka haya mambo bayana,… huyu hapa ni rafiki yangu,ambaye amekuwa ni kaka yangu wa kufikia, tofauti na watu wenye mawazo mafupi walioanza kunivumishia. Mimi ni mtu mzima nina akili zangu sawa sawa, kama ingelikuwa hivyo wanavyosema, kwanini tujifiche,….Kaka huyu, tumejuana katika mishe mishe za hapa na pale, ….’akasema na kunishika kwenye bega.

‘Ni kweli kabisa wewe ni dada yangu mpendwa, bila wewe maisha yangu yalikuwa taabuni , wewe ni zaidi ya ndugu….’nikajikuta nikisema.

‘Na huyu hapa ni mke wa bosi wangu, kwa maana hiyo ni bosi wangu  pia maana ndiye anayeniweka mjini…kama mtu anakuajiri na kukupa mkate wako wasiku inabidi umuhuheshimu sana, na nashukuru kesi inakwenda vyema usijali kabisa, ….’akamsogeleana kumshika bega na mke wa wakili mkuu akasema kwa uchungu.

‘Nakushuru sana wakili mwanadada, na niseme wazi, kuwa wewe ni mtu mwema sana, maana mtu ambaye anajitolea kuwajali wenzake, bila kujali gharama, bila kujali matokea yake kuwa yatakuwa na faida kwake, unachojali ni kuona wengine wanaondokana na matatizo waliyo nayo, ni wachache sana katika dunia,…watu wengi husaidia pale wanapoona kuwa watapata chochote,….nakushukuru sana na mungu akuzidishie…’akasema mke wa wakili mkuu.

‘Nashkuru kwa dua zako,  na huyu hapa ni rafiki yake, mpendwa, natumai wengi tunamjua kama docta, ….na mengi atakuja kuyasema mwenyewe, maana nhisi kuwa yeye ni muhusika mkuu wa kikao hiki, nisingelipenda kumwaga mtama kwenye kuku wengi, kabla muda haujafika….na huyu hapa ni…mmh,labda munisaidie kumtambulisha.

‘Mimi ni kaka yake Tausi,..huyu hapa, mimi ni kaka yake,ambay enilikuwa nje kimasomo, na nilirejea muda, nikawa kazini,na kama unavyojua kazi zetu, ukiingia hupati muda wa kutoka. Ilibidi familia iliniagize nije haraka ili niweke nguvu zangu, kwa vile na mimi ni mwanasheria nikaona ni vyema nije kama inabidi niweze kumtetea ndugu yangu.….’akasema na aliposema hivyo moyo wangu ukatulia.

‘Kesi sio mbaya, maana wale vinara wa hayo mauaji wameshatambulikana, iliyobakia ni kuhitimisha tu, na kwa vyovyote vile kesho inawezekana ikawa ni hitimisho la hii kesi. Unajua binadamu akishatenda kosa na lile kosa likawa linahusu damu ya mtu, mata nyingi atakuwa haan raha, na ili kuliondoa lile doa moyoni, hufikia hatua akasema ooh, ngoja nitubu mapema, maana kuanleo na kesho, huna mamlakana roho yako…ukifa na deni la kuua, siju utakwenda kusema nini…’akasema wakili mwanadada.

‘Ni kweli, labda mtu huyo awe ni mnyama…maana binadamua kibadilika anaweza akawa ni zaidi ya mnyama, ..hata hivyo, kila jambo lina mwanzo namwisho wake. Tutaona itakavyokuwa…..’akasema huyo mgeni.

‘Haya karibuni sana, na sitaki kupoteza muda wenu mwingi, ninataka kuingia moja kwa moja kwenye msingi wa kikao hiki. Mimi ni wakili, na pamoja na hayo, nimekuwa nikijihusiaha sana katika masuluhisho ya ndoa za watu. Na hili limekuwa kama jambo muhimu katika maisha yangu. Nina kuwa na furaha sana ninapoona watu wanapendana, watu wanaishi kwa amani, hasa kwa mke na mume, na kinyume chake ni maumivu kwangu….

‘Katika tukio hili ambalo linaendelea mahakamani, limekuwa kama kazi maalumu kwangu, kazi ambayo nahisi itakuwa ni sehemu muhimu ya kukamisha mradi wangu wa kutunga kitabu cha maswala ya familia na maisha ya ndoa. Kwa ujumla nimejifunza mengi sana kutoka kwa waliohusika katika sakata hili zima. Na sasa nimepata kitu muhimu sana ambacho kinaweza kikasaidia watu wengine baadaye.

‘Katika dunia hii ili kweli uonekane msomi, ni lazima ufanya jambo linaloweza kuisadiai jamii. Mimi sioni usomi ambao unajisaidia wewe mwenyewe tu, kuwa umesoma, na kinachofanyokani kushibisha tumbo lako na familia yako, huo ni usomi wa kichoyo. Usomi ni pale jamii inapofaidika na kile ulichokisoma, ukaisadia jamii, hata kwa gharama isiyo na tija, tija yake ni kile ulichokifanya. Mfano ukisadia jamii, ikanufaika na ule usomi wako hiyo ni tija yeney tahamani kubwa sana, kuliko pesa utakayopata.

‘Wapo wasomi, kutokana na usomi wao jamii imekuwa ikiumia,..hutaamini hilo, mtu anasoma ili we mjanja kuiba mali ya uma, kuibia wanajamii…hii ni dhulumakubwa sana. Huu sio usomi, huu ni ujambazi, na mtu kama huyu ni sumu katika jamii. Tujue kabisa kusoma kwetu ni jasho la wazee wetu na waliotangulia, walihangaika sana na sasa tupo huru,…kuna waliopteza roho zao na hawakufanikiwa kabisa kukipata kile walichokihangaikia, ..hawa watalipwa na nani, kama sio sisi wasomi kujitolea….hili kwangu nimeliona na ndio maana najitoleakuwasiaida wenzangu.

‘Ndoa,….jamani ndoa ni tatizo …wengi wanakimbilia hadi kusema ndoa ni ndoana, …sio kweli, ndoa haikutakiwa ieleweke hivyo. Kiujumla ndoa sio ndoana,….ndoa ni sehemu ya kustarehe, kuunganisha nguvu, kusadiana, na kuweka kitukiwe kamili,…. wanaofanya ndoa iwe ndoana ni wale wanahusika na hiyo ndoa,….ambao wanaitwa wanandoa, lakini hawaijui hiyo nda ni misingi yake.

 Wao kwa kutokuwa makini, ….wakaingia kwenye chumba hicho kiitwacho wanandoa, bila kufumbua macho, na kwahiyo wakaingia hapo bila kujua ni nini kipo humo, na wanahitajika wafanye nini, ial walickwa kutokuhotaka ni siafa tu ya kuitwa waanndoa na baadaye wanaharibu maana kamili ya ndoa, wanakichafua chumba…, hawa watu wanajikuta wakihamanika, kushika huku na kule. Kwanini mfumbe macho, wakati macho mnayo..ni ajabu kabisa….

‘Hili nimekuwa nikilirudia mara nyingi, kuwa mnapoingia kwenye chumba  cha ndoa ni muhimu mkayafungua macho yenu vyema, ili mjue wapi mnapokanyaga, na nini kipi humo ndani,….maana ukitemeba ukiwa umefumbamacho  utajigonga kwenye ukuta. ..

Ndugu zanguni, nyie wote hapa mumejaliwa kuwa kwenye ndoa, na kwahiyo nikisema ndoa mnajua ndoa ni ni nini, na pia kwabahati mbaya wote mumejikuta mkiwa katika matatizo ya ndoa, sijui kuhusu huyu mwenzetu mgeni, kama yeye  ndoa yake haijabahatika kuwa na mataizo, lakini nijuavyo mimi, matatizo ya ndoa ni kitu cha kawaida….cha muhimu ni kufungua macho, na kuwa makini,…ongeeni, matatizo yenu..kwanini muogopane,..nashangaa kabisa!

‘Mimi sio mwalimu, najua wenzangu hapa ni walimu zaidi katika maswala ya ndoa, na nilishangaa sana kuona kuwa mwalimu wa maswala y andoa naye anajikuta katika matatizo ya kindoa, nikajua huenda ni kwasababu ya ule usemi usemao, kwenye miti mingi mara nyingi hakuna wajenzi,sijui kama usemi huo unafaa katika hayo yaliwasibu au la…’akatulia kwa muda huku akiwaangalia washiriki humo ndani.

‘Naona nisiwapotezee muda, ngoja niingie kwenye lile nililowaitia hapa, kama nilivyowaambia kuwa mimi katika moja ya kazi yangu ni kusuluhisha matatizo katika ndoa. Na leo hii kuna tatizo moja katika ndoa ya aina yake. Ndoa hiyo kisheria inaweza ikawa isikubalike, lakini kiroho, kiimani na kiupendo ilikuwepo, na hata siku nilipohadithiwa mimi kuhusu hiyo ndoa nilizania ni utani…’akatabasamu.

‘Hebu niwaulize, hivi kweli kuna upendo kati ya watoto chini ya miaka kumi, yaani wapendane kiukweli hadi kuitwa wapenzi?’ akauliza na kuniangalia mimi. Sikujibu lile swali kwanza nikacheka na baadaye nikasema;

‘Mara nyingi mapenzi hayo ni ya kama michezo ya kitoto, na nahisi wengi wakishakua wakubwa wanayasahau, na kujikuta wamekutana na wapenzi wengine na kuyasahau hayo ya utotoni, ila wapo waliobahatika na kujikuta wakiendeleza mapenzi yao hayo,lakini ni wachache sana…’nikasema

‘Kwanini iwe hivyo, kama kweli mlipendana mkiwa watoto, na mkawa na yakini ya mapenzi ya kweli, mpaka mfikie hata kuchumbiana kitoto,..hizo fikira zinakujaje, maana kamamumefiukia hatu aya kujua kuwa mke na mume wanatakiwa kuwa wachumba, kuwa mke na mume, huoni kuwa ila akili palesio ya kitoto tena, kuna mwongozo mliupata toka kwamuumba, ….inakuwaje mkisha kuwa wakubwa msiyakumbuke hayo ya utotoni?’akaniuliza.

‘Tatizo kubwa ni umri, mihangaiko ya maisha na kutwanyika kila mmoja akaeleekea kwake, na huko kila mmoja alipo anajkikuata anakutana na maisha mengine na wapenzi wengine, kwahiyo mnajikuta mumesahau yale ya utotoni…’nikasema.

‘Kwahiyo yale ya utotoni hayakuwa mapenzi ya kweli, ni michezo yakitoto tu?’ akauliza.

‘Inategemea mtu na mtu, inaweza ikawa mapenzi ya kikweli, lakini kama nilivyosema watu mumetawanyika, huwezi jua mwenzako yupo wapi, kweli utasubiri mpaka lini ,uzeeke ukimsubiri mwenzako, …, na je kama mwenzako keshaolewa, …utakwenda kuvunja ndoa ya watu, .na vitu kamahivyo.’nikasema.

‘Na je kwanini afikie kuolewa kama kweli mliahidiana na kuapizana kuwa mtakuwa wachumba, mtakuwa mke na mume?’ akauliza yule mwanadada ambaye alikuwa katulia kimiya.

‘Tatizo hapo ni mawasaliano, kama yapo mawasiliano, sizani kwamba itakuwa ni tatizo,…’nikasema.

‘Hata kama kuna mawasaliano, na mmoja akawa sio mwaminifu, anatembea na wanawake wengine unaweza ukamwamwanije huyo mtu, kweli ana mapenzi ya dhati, au ni mchezo huo wa kitoto kama ulivyouita, ?’ akaniuliza huyo mwanadada.

‘Kila kitu kina muda wake, ujana una mambo yake, na inafika sehemu mtu unatulia, ….haiwezekani ukawa na tabia hiyo hiyo hadi umri kama, wangu….kama mtu alikuwa na tabia huyo, lazima inafika mahalii anasema sasa basi…kama mimi hivi sasa siwezi nikawa na tabia ile ya ujananii tena…mtakiwa niwe na mkenitulie….’nikasema.

‘Kwanini sasa huna mke?’ akaniuliza yule mgeni.

‘Nilikuwa naye,lakini matatizo yakatokea, maana imekuwa kama unajaribu …na unajikuta kumbe sio yeye uliyemtaka….labda niseme wazi kuwa yupo ambaye mungu alinipangia, na sijaweza kumpata tena, sijui yupo wapi?’nikajikuta niksema kwa uchungu.

‘Hebu nikuulize swali, ambalo huenda nilishawahi kukuuliza , ila nakuuliza hapa kwa niaba ya wengine, wakusikie nini utaongea, Je wewe katika ujana wako uliwahi kuwa na mpenzi wa ujanani,…?’ akaniuliza wakili mwanadada.

‘Ndio , nakumbuka nilishakaumbia hilo, niliwahi kuwa na mpenzii wa utotoni,..hadi ujanani,  na ujanani nikawa na tabia ya kihuni, ….siunajau tena ujana ulivyo, lakini sasa najuta maana niliyoyafanya ujanani,yaliniharibia yale niliyoyakusudia, na hata kumpoteze mpenzi wangu niliyempenda sana….’nikasema.

‘Je huyo mpenzi hamjawahi kuwasilina naye….?’akaniuliza yule mgeni.

‘Kama ningelijua yupo huru,hajaolewa,….nimejaribu kila njia sijapata mawasiliano naye, …ningelijua kuwa yupo huru, hana mume, ningemfuata huko alipo….’nikasema.

‘Una uhakika na hilo kweli?’ akauliza yule mwanadada.

‘Sasa ningelikuwa na uhakika, ningelisema hivyo jamani…hili nalisema wazo mbele yenu,mungu angu ndiye shahidi, hamjui moyoni kwangu kuna nini, ninateseka kweli nikimuwaza yeye….’nikasema kwa uchungu

‘Je kama akitokea,na tusema hana sura ile ya utotoni,maana mtu akiwa mkubwa haubadilika, huwezi jua maisha yalivyo, unaweza kweli ukawa naye licha ya mabadiliko hayo…?’ akaniuliza.

‘Kama kweli bado ananipenda, kwanini nisiwe naye tena,  …kwakweli nitafurahi sana kuwa naye tena….maana mapenzi yetu yalijengeka toka moyoni….’nikasema nikionyesha uso wa furaha.

‘Hebu nikuulize, ina maana mtu huyo ulikuwa ukimpenda ukiwa mtoto, na pendo hilo lilikuwa la moyoni, ina 
maana umri unaweza ukalibadili hilo pendo, usimkumbuke huyo mtu kabisa,….?’ Akauliza yule mke wa wakili mkuu.

‘Sizani, ….sijui, kwakweli, maana umri upo na ni kweli umri uanweza ukabadili sura za watu …lakini ina maana mtu abadilike kabisa uisweze kumtambua ….!’ Nikakuta nikisema huku nikimwangalia yule mke wakili mkuuna tena nikageuka kumwangali yule mwanadada mwingine na kushangaa akiwa anatoamachozi. Halafu yule mwanadada akatikisa kichwa kwa kuonyesha kusikitika akasema;

‘Mimi nina amini kabisa kama mtu unampenda kweli huwezi ukamasahau abadani, labda kama ulikuwa unampenda kubahatisha…. lakini kama yupo moyoni , hata awe mkubwa vipi sura itabakia moyoni, ….mimi nina imani kuwa wewe huyo uliyekuwaukimpenda mkiwa watoto, alishafutika moyoni mwako kwasababu ya kukutana na wasichana wengine hapo katikati..huna mapenzi yakweli wewe usitudanganye….’akasema.

‘Kwanini unasema hivyo, ….wewe unanijulia wapi maisha yangu….’nikasema kwa hamaki.Na kwaharaka nikatoa picha ya huyo msichana ninayemfahamu akiwa mdogo, nikasema;

‘Hebu jamani nisaidieni, ..hebu niambieni, huyu hapa ndiye aliyekuwa msichana wangu wa utotoni, niambieni mlishawahi kumuona wapi, ili uongo wangu udhihiri, ni nani anayefanana naye ambaye mliwahi kumuona?’ nikawauliza.

Kila mmoja aliiangalia ile picha na kukuta kweli hakuna sura ya msichana au mwanamke anayefanana naye wanayemjua…

‘Haya niambieni, ukweli ni msichana gani mliyewahi kumuona hapa anayefanana naye?' Nikauliza na kuwaangalia, na mara yule mwanadada kwanza aliniangalia kwa mshangao, na baadaye akageuka kama kunikwepa , na kuangalia pembeni, akitabasamu,na aliponigeukia mara ya pili kuniangalia nikashangaa kumuona macho yamejaa machozi, analia….

‘Unalia nini ….maana muda mwingi nakuona upo katika hiyo hali…?’ Nikamuuliza yule mwanadada, nikimuonea huruma.

‘Kuhusu mabadiliko ya sura, ninaweza kusema sio kosa langu….sio kosa langu kabisa ni madhila ya dunia….’akasema huku analia.

‘Ni kosa la nani hilo, na kwani unamjua huyu mwenye hii picha?’nikauliza.

‘Ni kosa la wale wasiojali wenzao, ambao kutamka kwao ahadi ni rahisi kuliko kuitekeleza hiyo ahadi, hawana huruma na wenzao. Nakubali kabisa huyo mwenye picha hiyo ni mimi,…’akasema yule mwanadada.

‘Ni wewe….hapana,….mbona hamfanani, …aah,mungu wangu,nakajikuta nikiinuka na kwenda kusimama mbele yake huku nimeshika mdomo nikioana aibu, na kumchunguza kwa makini....yeye aligeuka pembeni, ....

‘Ndio mimi, mwenye hiyo picha, lakini …kuna kipindi nilikuwa nikitumia dawa ambazo zilifanya nibadilike sura, sikuwa na nia hiyo ya kujibadili sura, dawa zile nilipewa kutokana na mataizo yangu, ya kiafya, ya kuchanganyikiwa, na kila nikizitumia zikawa zinanibadili sura yangu nakuwa mweupe kupita kiasi. …’akasema huku akibubujikwa na machozi.

‘Kwangu mimi sikujua wala kujali mabadilikohayo, kwani kwa muda huo,  nilikuwa nikjiona kawaida , kwani kwa kipindi kile sikutaka hata kujiangalia kwenye kiyoo, nilikuwa najiona mfu anayetembe…mpaka kipindi nilipokwenda kijijini kwetu, na kujiikuta watu wengi wakiniuliza mimi ni nani ndipo nikagundua kuwe kweli nimbeadilika,....’akatulia.

‘Hilo ni kweli, kwani hata mimi nilimsahau kabisa  dada yangu, kwani nilikuwa nje kimasomo, na niliporudi muda fulani, ili bidi nianze kuulizia dada yangu yupo wapi, nikaishia kuchekwa, …hizo dawa nyingine za kienyeji mnatakiwa muwe makini nazo, lakini kwa kipindi kile kwa dada yangu haikuwa na jinsi kilichotakiwa ni kumsaidia….mimi mwenyewesiamini kuwa sasa dada yangu katulia,…’akasema huku akimwangalia dada yake.

‘Lakini mimi naona ni nzuri, maana kama zilikubadili sura na hakuna madhara mengine zaidi huoni kuwa zimekufanya ukawa mrembo zaidi…..’akasema mke wa wakili mkuu ambaye muda mwingi alikuwa kimiya.

‘Kwani urembo ni weupe, mimi kwangu urembo ni ule wa asili, hata kama uwe mweusi, mwekundu…lakini kama ni urembo urembo ni uasili wako, na kama umejaliwa kuwa mrembo, wewe ni mrembo tu….ni mrembo ni mtu ni jinsi mtu anavyomuiona yeye…’akasema kaka mtu.

‘Lakini huoni athari zake kwani yule niliyempenda alishanisahau, na kama alinipenda kwasababu ya sura yangu ya asili,au linipenda kwasababu ya sura tu, sasa hatanipenda tena….’akasema mwanadada.
Mimi nilibakia kuduwaa tu huku nikimwangalia huyu mwanadada, nilikuwa bado nimesimama mbele yake, sikuwa bado naamini hayo maneno nikikumbuka kuwa nimeambiwa kuwa kuna mgeni alikuja nyumbani ambaye alidai kuwa ni rafiki yangu wa utotoni, sasa huyo mgeni ni nani….

‘Halafu nina mgeni toka kijijini alipitia nyumbani jana, ….’nikaanza kusema.

‘Mimi ndio nilipitia nyumbani kwako jana…kama una maana mgeni aliyefika kwako akiwa ba begi,akakuulizia. Nilipita hapo kwako, nilipotoka huko rumande, nia na lengo langu ni kufikia kwako, nijue ni kwanini siku zote hukuweza kufika huko mahakamani,…na kukuuliza mengi,lakini sikukuta….’akasema yule dada.

‘Kwahiyo wewe ndiye Tausi binti Maringo haswa…..eti, hebu ringa kidogo..?’ akauliza wakili mwanadada na kusema kwa mzaha.

‘Kama yupo mwingine ni wa kuchongwa…najua kuna watu walijaribu kuniigiza lakini mwisho wa siku walishindwa….’akasema huku akionyesha uso wa huzuni

‘Mungu wangu ina maana wewe ndiye Tausi,..ooh, …’nikasema na kujikuta nikipiga magoti mbele yake bila kuwajali wote waliohudhuria hapo , na Tausi akaniangalai huku machozi yakimtoka, akaniwekea mkono wake kichwani mwangu na kusema.

‘Ndio mimi mwanamke uliyemsaliti….’akasema huku akiwa kaniangalia akatulia kidogo halafu akasema tena,     

'Lakini mimi sikuweza kukusaliti hata chembe, mungu ndiye shahidi yangu, nimeweza kuitunza ahadi yangu ya utotoni hadi hii leo, …uone jinsi sisi wanawake tulivyo na upendo wa dhati….’akasema huyu mwanadada.

‘Naomba unisamehe maana yote yalikuwa ni majaribio ya kimaisha….sikujua nini nitenalo kwa wakati ule… ,na nipo tayari kuipokea adhabu yoyote utakayoitamka, ….’nikasema huku macho yakiwa na kiza za machozi, sikuamini …..

‘Adhabu yangu ni kuwa twende kijijini pale pale tulipowahi kufunga ndoa na pale pale tukaifunge ndoa ya kiukweli ambayo unaiamini wewe isiyo ya kitoto….’

‘Hilo tu, hata leo nipo tayari…’nikasema kwa furaha na watu mle ndani wakashangilia.
Mara simu ya wakili mwanadada ikaita, haraka akaipokea na kusikiliza kwa muda, alitulia na baadaye akawageukiwa washiriki humo ndani na kusema;

‘Jamani mbona haraka hivyo, maana msisahau kuwa kesho ndio siku ya kesi iliyopo mbele yetu, na kwa taarifa nilizozipata sasa hivi, nesi  na ….na wakili mkuu, wapo taabani hospitalini, inasadakiwa wamekunywa sumu…na kwahiyo…’

‘Eti nini..’akasema mke wa wakili mkuu, na kuinuka pale alipokuwa kakaa akijiandaa kuondoka.

NB:Tuwepo tena katika kumalizia kisa hiki.....nauliza tena kuna yoyote aliyebahatika kuwa na rafiki yake  utotoni, na wakabatika kuja kuoana ..? Na je ni kweli kuwa sura inaweza kubadilika kabisa unakuwa mkubwa ukawa tofauti na ile sura ya utotoni? bado nawaza hili, natumai wewe unaweza kunisaidia, kama hutojali!

WAZO LA LEO: Ili tuweze kuishi salama katika maisha yetu, ni vyema tukajifunza kusameheana. Na ili kusameheana kuwepo, inabidi tuwe wepesi kukubali makosa pale tunapokosea. Sisi ni wanadamu kukoseana kupo, hatuwezi tukawa wakamilifu wakati wote. 

Ni mimi: emu-three

2 comments :

Pam said...

kweli natamani ungeendelea mana umegusa mutima wangu what an happy ending kwa msomali baada ya madhila yote...

Anonymous said...

In my expertise, appraisals had been paid for at closing.
I personally believe chronic.cc they want you
to devote this guaranteed payday loans uk income up front in order that you're reluctant to walk away when lastly confronted with the bait and switch.