Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Thursday, July 19, 2012

Hujafa hujaumbika-70 Hitimisho 28



Kila mmoja alikuwa na hamu sana ya kutaka kujua majaliwa ya hawo ndugu ambao inasadakiwa kuwa wamekunywa sumu, na haikujulikana kabisa vipi hiyo sumu iliwafikia hawo watu wawili, cha ajabu Sokoti yeye alikuwa salama kabisa, na wale waliokuwa na mtizamo wa haraka wakamshuku yeye kuwa huenda kahusika na hilo.

‘Kwani ilikuwaje?’ mmoja wa wanafamilia akauliza.

‘Kwani inajulikana….! Bado polisi hawajasema lolote, lakini kwa taarifa za awali ni kuwa, wakili mkuu na Nesi na Sokoti walipata muda wa kukaa pamoja kwenye chakula cha mchana,na inavyosadikiwa , sumu hiyo ilinywea muda huo….

‘Ilinywea na wao wenyewe wa kikusudia au waliwekewa bila ya wao kujua?’

‘Hapo ndipo haijajulikani, ikizingatiwa kuwa wote wawili wampoteza fahamu hadi sasa hivi …

‘Sokoti yeye vipi?’ akauliza jamaa mwingine.

‘Sokoti yeye hajambo , na yeye anashangaa kwa tukio hilo, yeye anadai kuwa walipokutana ule mchana, walikaa pamoja na kuongea mambo yao, lakini hakujua lolote kuhusu hiyo sumu, na anasema waliongea kwa muda, halafu yeye akaitwa…’akasema huyo jamaa.

‘Akaitwa na nani?’ akaulizwa.

‘Yeye aliitwa na wakili wake, kwani yeye alikuwa na wakili wake tofauti na wengine, na muda huo wakili wake alishafika na aliitwa ili wakaongee naye, na hakupata muda wa kukutana na hawo wenzake tena, maana muda ulishakwisha na waliamriwa kuingia kwenye vyumba vyao, na wakati wakiwa humo ,ndipo yeye akasikia kuwa wakili mkuu ana hali mbali …

`Ilikuwaje nesi akaja kukutana na wakili mkuu?’akaulizwa.

‘Nesi ndiye aliyeomba kuwa ana maongezi na wakili mkuu, na alikubaliwa kwa utaratibu mzuri tu,kwasababu yote walishayasema na haikuwa na haja ya kumzuia, waliruhusiwa wakutane…

‘Na humo rumande, wanakaaje, yaano Sokoti na wakili mkuu, najua wanawake wana rumande yao, lakini hawa wawili hawakuwa karibu?’

‘Hawakai pamoja….walikuwa wametenganishwa tangia awali, kwani walitakiwa wasikutane kipindi kile cha uchunguzi,….,hadi hiyo jana walipokutansihhwa kwa maombi yao kuwa walikuwa na maongezi yao, ….’

‘Mimi bado nina wasiwasi na huyo Sokoti, huyu mtu anaweza akawa anahusika kwa namna moja au nyingine, ..’akasema mwanafamilia.

*******

‘Mnaitwa huku, Msomali na wakili mwanadada….’tukasikia tukitwa pale tulipofikahospitalini kuwaona waginjwa, …kulikuwa na ulinzi mkali, na hata tulipoomba kuwa tunahitaji kuwaona hawo wagonjwa hatukuruhusiwa moja kwa moja, ilibidi ombiletu lipelekwe kwa wakuba, na tukaambia tusubiri, na baadaye ndio tukasikia tukiitwa….na kuelekea huko kwenye chumba cha wagonjwa maalumu, nikahisi mwili mzima ukisismuka pale tulipoitwa.

 Tukaingia kwenye hicho chumba,  baada ya kukaguliwa na mlinzi, …na tulipoingia pale ndani  tukamkuta mke wa wakili mkuu akiwa kasimama mbali na kile kitanda na pembeni yake yupo Hakimu , yule hakimu aliyekuwa akisikiliza maelezo yetu ya awali,…bado docta alikuwa akimuandaa yule mgonjwa, na tuliambia tusubiri kwanza kidogo, baadaye akasema mgonjwa yupo tayari kuongea na sisi, na tukamsogelea, yule nesi ambaye alikuwa kawekewa mipira mwilini akafunua macho na kusema;

‘Mimi naona safari yangu imewadia, lakini nimeona kabla hiyo saa haijafika, niongee na nyie, kwani najua kabisa nyie nimewatendea isivyohalali,nilihitaji watu wengi zaidi ambao kwa ujumla nina uhakika nimewatendea mabaya, lakini nyie ni muhimu zaidi kwa haya nitakayoyasema…’akahema kwa nguvu.

‘Muheshimiwa hakimu, wewe nimekuita uwe kama shahidi,….sina makosa na wewe…lakini ni muhimu ukayasikia haya nitakayoyaongea pamoja na mkuu, nyie ni kama mashahidi tu…na naomba nitakayoyaiongea hapa myawakilishe huko kunakohusika,…na nashukuru kuwa mumekuja na vitu vya kurekodia,….leo nitaambia kila kitu mungu akinipa pumzii ya kuongea….

‘Usijilazimishe,….’akasema docta

‘Usijali Docta,….unajua kila mtu atakufa, lakini kama utaweza kupata mwanya wa kutubu dhambi zako, kwa wale uliowakosea ni bora sana, kwani utakuwa umepunguza yale madhambi uliyoyafanya, yaliyobakia tena utakutana nayo huko mbele ya muumba…na kila mtu ni mkosaji, na mbora wao ni yule anayejua kosa na akatubu, na kutubu kwema ni kumuomba msamaha yule uliyemkosea…au sio…?.’akafunua macho ktuangalia na sisi tulibakia kumwangali tu kwa macho ya huruma.

‘Msiwe na wasiwasi, na wala msionionee huruma, maana mimi mwenyewe sijionee huruma, nyie kwanini mjione mna huruma sana kwa ajili yangu, …hapa nilipo huenda nahesabu masaa,maana sikujua kama itafika muda kama huu, kutokana na hiyo sumu, nilijua kabisa muda kama huu ingelikuwa dunia nyingine, …kama nitanusurika basi ni majaliwa ya mungu…lakini sizani….

‘Ina maana unajua kuhusu hiyo sumu,…maana sisi tunahisi kuwa kuna mtu kawawekea hiyo sumu?’ akauliza mkuu, na hakimu naye akaonyesha kushangaa na kusogea karibu.

‘Sumu hiyo nilikuwa nayo mimi mwenyewe kwa muda wote….mimi ni askari na kuna kitu sikuwahi kuwaaambia kuwa pamoja na uaskari wangu, nilisomea ukomandoo, ingawaje hawakutaka nielekee huko kwasababu ya kuniona nina hasira sana…anyway…hayo tuyaache. Sumu hiyo nilikuwa nayo, kwa namna ambyo hakuna angeliigunuda, kwani nilijua itafika muda ambao nahitajika kuitumia, tatizo ni kuwa dozi yake ilikuwa ya mtu mmoja, sasa nimeichanganya kwa watu wawili, kwahiyo nguvu yake imepungua….sijui,…lakini yote ni majaliwa ya mungu..’akasema

‘Sasa kwanini ufikie hatua hiyo, ya kutaka kujiua?’ akaulizwa.

‘Ndio maana nimewaita hapa,..naomba mnisikilize kwa makini….maaan sijui muda na saa za kuondoka, huenda nikashindwa kuwaambia kila kitu nilichokusuida kuwaambia….kwahiyo naomba mnipe muda wa kuongea….’akasema na kunyosha mkono mmoja ulikuwa huru kumuelekezea mke wawakili mkuu.

Mke wakili mkuu kwa muda huo alikuwa akimwangalia huku kashika shavu, na uso wake ulikuwa umejaa huruma...hakujali kuwa ni adui wake, hapo huruma ya kibidamua ilimtanda, na hata wakati mwingine kujilaumu kuwa kama angelijua asingelioana na wakili mkuu.....

‘Pole sana ndugu yangu,…..Wewe ni ndugu yangu katika familia, kwanza kabisa naomba nikuombe msamaha kwa yote niliyokukosea, najua ni vigumu sana kuelewa hili, lakini hadi hivi sasa nahisi kama wewe ndiye uliyeninyang’anya pendo langu….najua moyoni utabisha hili, lakini kiukweli, mimi na mume wako tulikuwa wapenzi wa muda mrefu…..’akatulia na mke wa wakili mkuu akawa anazua machozi yasitoke.

‘Tulifikia hadi kuvishana pete, na hadi siku ya mwisho nasikia kuwa anakuchumbia wewe ,mume wako mwenyewe alinipigia simu akasema  hayo ni ya uwongo,…na taarifa zilipozagaa na kuipata kuwa ni kweli anataka kukuoa wewe, aliniambai kuwa yeye anachofanay ni kwa ajili ya kukamilisha mambo fulani huko Ulaya,eti kuna mambo ambayo mkiwa mume na mke mnayapata…sijui, ni yapi…’akatulia.

‘Mimi kwasababu nilimpenda sana mume wako, nikamkubalia, …nikijua ni taratibu tu za muda, ….hata wakati mnafunga ndoa nilijua kuwa ni geresha tu, lakini siku hiyo nikahisi kuwa nimepigwa changa la macho, …nikajaribu kuwasiliana na mume wako kwa simu, akawa hapatikani tena kinyume na makubalian yetu, kila mara nikimpigia simu akubali kuongea name, ili nijue nini kinaendelea…’akatulia.

‘Haya ninayo kuambia sasa hivi ndiyo ya ukweli, maana sina muda wa kumdanganya mtu, nidangaye ili iweje, wakati ndio nakwenda huko kwa hakimu wa mahakimu, asiyedanganyika. Basi kwa siku ile sikuweza kulala, hasira chuki na wivu vikanijaa, hebu fikiria mtu wako unajua hivi sasa yupo na mke mwingine, na hebu ichukulie katika hali halisi, ingelikuwa ni mke mwenza sawa, lakini hiyo haikuwa ya mke mwenza,  …lakini hata hivyo namshukuru mungu kuwa nimejaliwa moyo wa chuma,moyo wauvumilivu, nilijua ipo siku nitakuja kulipiza kisasi, kama kweli huyo mume wako aliamua kunitendea hayo kwa  kunidanganya……

‘Wiki na miezi ikapita, na nilipopata bahati ya kuongea na mume wako, akanithibitishia kuwa msimamo wake upo pale pale, ..kuwa kakuoa ili kufanikisha mambo fulani fulani, akiyaweka sawa, atakuacha wewe na tutafunga ndoa mimi nay eye…lakini hilo likachukua muda sana, sikuona dali li hiyo. Na hayo mambo anayoyafanya ni yapi, hakuwahi kuniambia…..

‘Basi siku moja akanipigia simu kuwa ananiomba nifanye kila njia nije huku Dar…yeye atafanikisha mambo ya ajira, …..kwahiyo kuja kwangu huku Dar na mengineyo, ilikuwa ni dhamira ya kuja kukamilisha kile alichoniahidi mume wako, kuwa anataka kuimaliza ndoa yenu, ili aje anioe mimi, na ndio maana kafanya kila mbinu msipate mtoto…’akasema

‘Eti nini….?’ Akashangaa mke wa wakili mkuu.

‘Umesahau kuwa mimi ni nesi,…ndio weweni docta ,….ndio najua kama docta unajua mengi zaidi yangu,….lakini mimi ni nesi na mzoefu wa mambo mengina….ambayo wewe na udakitariw ako huyajui, sio kwamba huyajui kiutalaamu, unayajua kihivyo, lakini kwa utendaji,..kwa uzoefu, mimi najua mengi, …ambayo wewe kama docta usingeliweza kuyahalalisha….mume wako kuna dawa alizokuwa akizitumia, ili msipate uja uzito…’akasema.

I can’t believe this….this is too much….’akasema mke wa wakili mkuu, akiwa kakunja ngumi kwa hasira.

‘Sisemi hili kwa nia ya kukuumiza wewe, nasema hili ili kutoa kile chote kilichokuwa kimejificha, nafsini mwangu, ili mwisho wa siku usije ukajilaumu na kunilaumu mimi. Na pia usije ukajilaumu kuwa huenda hukujaliwa kuwa na mtoto na mume wako,…yote hayo ni mipango yangu na mume wako, kama angelikuwepo hapa angelithibitisha hili…lakini najua hali yake huko alipo naye anahesabu masaa, na nijuavyo mimi wanaume hawana kinga kubwa ya uvumilivu kama sisi …sijui nisikukatishe tamaa…’akasema huku akionyesha maumivu fulani tumboni.

‘Nilipofika hapa Dar, nikagundua kuwa pamoja na kuwa mume wako ananipenda, lakini ….ana tamaa sana, hakuwa na subira, hakutaka kuvumilia, hasa pale alipokuwa kija kwangu,kwa nia ya kustarehesha mwili wake, na mimi namtolea nje, kwa kuwa yeye ni mume wa mtu, na anastahili kuwa makini kwa hilo. Hili lilimtesa sana, na ndio maana akawa anaruka nje,…na hili sikulipenda kabisa, ndio maana nikaingia kwenye uadui na akina Kimwana.

‘Wivu nilioupata kwa akina Kimwana, ulizidi wivu nilioupata kwako wewe, kwa vile kuolewa kwako wewe kulikuwa na sababu maalumu na nilifahamishwa hilo kuwa ni kwa mipango ya muda…na nilijua ipo siku utaachika, na hilo ndivyo ilivyokuwa ndio maana kwenye ndoa yenu kulikuwa hakuna upendo….’akasema na kutulia.

Lakini kusikia kuwa mume wako anatembea na Kimwana..hiyo sikukubali, nikajua kuwa ni tamaa za mume wako…, na hata hivyo kauli ya Kimwana ambaye nilikuja kumweka kama rafiki yangu, kwa ajili ya kujua nini kinaendela ilikuwa ianumiza zaiidi ya kuchomwakisu cha moto. Kimwaan ana majigambo ya kuuzi, ….

Kauli ya Kimwana ilinifanya nimuwekwe kwenye kundi la maadui wangu wakubwa…kwako wewe sikujali sana, kwa viel nilijua kuwa huenda huna hatia na hili, ingawaje sijui kulitokea ushawishi gani hadi akaamua kukuoa wewe, na wakati wewe mwenyewe nahisi ulijua kuwa huyo ni mchumba wangu….’akasema na mke wa wakili mkuu akasema kwa hasira.

‘Mimi sikujua hilo….ningelijua nisihangaika kiasi hicho….’akasema .

‘Huu ni muda wangu wa kuongea,kama hukujua hilo, sina makosa, lakini nakumbuka kuna siku nilikuambia kuwa nina mchumba wangu, mnasoma naye huko Ulaya, huenda kosa langu ni kutokumtambulisha kwenu nyie….sijui nilijisahau vipi,lakini ndivyo ilivyokuwa, kuwa huyo alikuwa mchumba wangu na ahadi ya kuoana ilishapitishwa,....'aatulia kudogo, na sauti sasa ilikuwa inatoka kwa shida.

'Sasa hebu fikiria wewe menyewe kama ungelikuwa kwenye nafasi yangu ulingelichukua hatua gani….najua utasema ningaliachia mbali, wanaume wapo wengi, lakini hebu fikiria huyo mume anakuja kwangu na kuniambia kuwa bado yupo na mimi, na mimi kweli nampenda….’akatulia kidogo

‘Kwahiyo nilipofika hapa Dar na kukutana na huyu Kimwana nikajua sasamambo yameharibika, maana mimi ilivyomchunguza Kimwana nikamjua kiundani na jinsi ninavyomjua mume wako, nikajua kuwa kama nitamlegezea Kimwana tutakosa wote, na kukosa huko kutakuwa kubaya zaidi,maana Kimwana hajatulia,…nikajiona kama mtu aliyeruka mkojo na kuja kukanyanga mavi….

‘Kimwana aliamua kushindana na mimi na kusema kuwa atahakikisha kuwa huyoo mume wako anakuacha na kumuoa yeye,na pili atahakikisha kuwa kila mlichochuma naye anakichukua yeye, na mwisho wa siku atahakikisha kuwa unaukimbia huu mji,…..kwa muda ule hakujua kuwa mimi na wewe tuna udugu fulani….kwangu mimi ilikuwa kama mtu mzima kutishiwa nyau, lakini mwisho wa siku nikagundua kuwa kweli Kimwana kazamiria…

Ndipo kundi hilo likaanzishwa, na pamoja na mengine, nikagundua kuwa kundi hilo litanisaidia sana kummaliza Kimwana kiujanja, na yeye hakulijau hilo,….hadi siku ile alipokutana na mauti yake, najua siku ile alishagundua mengi..na lishagundua kuwa mengi yanayomsibuu ni kutokana na mimi, na alishajiandaa kuja kukabiliana na mimi, lakini alichelewa…

‘Kwahiyo wewe ndiye uliyemuua Kimwana…?’akaulizwa.

‘Subirini,bado naona roho ipo, nitawaambia kila kitu,….’akatulia,…na mara tukamuona akibadilika, akajitahidi kufunua mdomolakini hakuweza,… na mara macho yakafunga…na hata ile mashine ya kusaidia kupumualia ikaanza kupiga ukulele…docta akaja kwa haraka na kuanza kumhudumia.

‘Tafadhali tokeni nje….’akasema docta na kuzungusha lile pazia la kumzuia mgonjwa asionekane….

NB: Kila nikijaribu kumalizia najikuta kuna sehemu nimeiacha, na kwahiyo inabidi niiongezee, lakini kama mnavyoona kisa kinafikia ukingoni.

*********************************************************************************

WAZO LA LEO: Mwezi wa Ramadhani huo unakuja, na mwezi huu ni sehemu ya kusafisha amdhambi yetu. Ni kama vile shati chafu, na unataka kulifua, …ni kama vile gari ulilolitumia kwa muda mrefu linahijika kulifanyiwa service…miili yetu imekuwa ikila vyakula vingi kwa mwaka mzima, na mwezi huu mmoja ni sehemu ya kuufanyia mwili wetu`service’. Sio mwili tu, kiroho pia, kutubu dhambi, kunyenyekea na kuwa na huruma kwa kusaidiana,na hasa kuwasaidia masikini.


Karibu mgeni wetu, karibu Ramadhani, mungu atujalie sote tuweze kutimiza ibada hii muhimu. 

DIARY YANGU INAWATAKIA KILA LA HERI WASILAMU WOTE DUNIA KATIKA MFUNGO HUU MTUKUFU WA RAMADHANI.

*********************************************************************************


                                     picha hii toka kwa :http://abdallahmrisho.blogspot.com/
Blog yenu hii inaungana na Watanzania wengine kwa majonzi haya yaliyotupata kwa ajali nyingine ya Meli, na hili linaanza kuwa donda sugu, tunaishia kuongea kipi kifanyike, lakini sijui kama kuna utekeelzaji. Poleni sana kwa wale waliopoteza ndugu zao, mungu awape subira, na waliotangulia mungu awalaze mhala pema peponi, kwani, Kwake yeye ndipo tumetoka na Kwake yeye tutareja.


Ni mimi: emu-three

4 comments :

Interestedtips said...

mimi nawasifu kwa kuandika jamani....tena mpangilio mzuriii...mafundisho....keep it up

Anonymous said...

Kaka, naikubali sana kazi yako, yaani
natamani uwe unaweka mpaka cku za wikiend, hongera sana!!! Mimi S.

Anonymous said...

Poleni sn kwa janga,lililotokea huko Znz,Mungu mwenye rehema,awape unafuu wale wt waliokumbwa na janga hilo na kuzipokea roho za wale wt waliotangulia kwake,kupitia kwa janga hilo.

Nakutakieni mfungo mwema wa Ramadhani,inshalaa,tupo pamoja,mnaanza kesho au?

Mimi C

Rachel Siwa said...

Ndugu wa mimi kazi inazidi kukuwa nafurahi mno!Mungu azidi kukubariki na nakutakia Mfungo mwema!!!!!

Pamoja Daima ndugu wa mimi.