Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Wednesday, July 25, 2012

Hujafa hujaumbika-74 hitimisho 32




Wakili mwanadada alionekana kuwa na mawazo mengi, na hata pale nilipomuuliza anasumbuliwa na nini hakutaka kuniambia ukweli, yeye alisema kuwa kuna jambo analifuatilia hajawa na uhakika nalo, na hawezi kusema lolote kwa sasa.

Mimi sikupenda kumsumbua kwasababu nilikuwa na mawazo yangu mengine, nikasubiri muda ufike twende huko hospitalini kuwaona wagonjwa wetu ili tujue wanaendeleaje. Nakumbuka hata nilipomuona mkuu mudamchache uliopita naye alionekana mwenye kukwera na jambo, maana kila alipoongea na vijana wake kwenye simu alionekana kutoa amri zahasira, nikajua kuna jambo halijaenda vyema.

‘Vipi kuna jambo ambalo mimi silijui maana mimi nijuavyo kesi imeshakwisha iliyobakia ni wagonjwa wapone wafikishwe mahakamani….au sio mkuu?’ Nikauliza.

‘Mambo ya sheria haya sio mchezo,…huwezi ukajua kesi imeisha mpaka ifike mahakamani na hukumu itolewe, …na kila siku tunaona mambo mapya yanajitokeza…ambayo yanatutia wasiwasi’akasema mkuu.
‘Kwanini unasema hivyo?’ nikamuuliza.

‘Wakili wa nesi anadai mteja wake hajamuua Kimwana, na yote aliyoyazungumza kipindi kile ilikuwa na katika hali ya kiugonjwa, na ilikuwa kama shinikizo, ….’akasema mkuu.

‘Lakini kwanini kauli hii  ije baadaye, kwanini hakusema wakati ule nesi anaongea mwenyewe?’ nikauliza.

‘Usifikiri wao ni wajinga, walikuwa wakiongea vile wa kivuta muda, na kama unakumbuka vyema, hakuna mahali nesi alitamka kuwa yeye ndiye aliyemuua Kimwana, kama ulifuatilia maelezo yake vyema,…inadaiwa kuwa yeye ndio kweli alifika pale lakini sio yeye aliyemuua Kimwana kama walivyofika mke wa wakili mkuu na rafiki yake,…’akasema mkuu.

‘Na hiyo bunduki aliipatapataje…?’ nikauliza.

‘Hapo ndio hatujapata ufafanuizi , na kauli yake mwenyewe…’akasema mkuu

‘Huoni kwamba anaficha ukweli,…..’nikasema.

‘Ndio maana nakuambia wao kila wanaloliongea walishalifanyia kazi, na nia na lengo lao ni kiifcha ukweli,lakini yote yatafikia mwisho, kwani jopo lamahakimi limekwenda huko hospitalini, ….’akasema mkuu.

‘Kwanini liende jopo la mahakimu?’nikauliza.

‘Kuna maamuzi nyeti ambayo yanahitaji vichwa zaidi ya kimoja, ….hayo tumewaachia wao wanaojua sheria zaidi…’akasema mkuu.

‘Nakumbuka wakili mwanadada alisema kuwa ana ushahidi wote wa kumweka ndani huyo muuaji wa Kimwana?’ nikauliza.

‘Ushahidi anao, lakini sehemu kubwa tulitegemea kauli ya Nesi mwenyewe ,kwani alionekana kukubali, na ukiviweka vielelezo unamkuta yeye ndiye mshukiwa, lakini kwa kauli ya wakili wao, inaonyesha dhahiri kuwa kuna jambo wao wameshalifanyia kazi, na huenda nesi akiwa katika hali nzuri atapinga kauli zake za mwanzo…kuna jambo baadaye tutalisikia kwa wakili mwanadada’akasema mkuu.

Baadaye nikiwa nawakili mwanadada nikamuuliza ;

‘Ina maana hali ya nesi inaendeleaje?’ nikauliza.

‘Bado haijawa njema, lakini kwa mtizamo wa dakitari, ile hali mbaya imeshatoweka…mengine ni masharti ambayo ni muhimu zaidi’akasema .

‘Masharti gani hayo, kuwa wasifanye kazi nzito, au ?’ nikauliza.

‘Hayo ni moja ya masharti, lakini wanatakiwa watulize vichwa vyao, na wasifikirie sana kuhusu kesi iliyopo mbele yao, ….na hili tumeliongea na hakimu na watu wa sheria, maana mambo mengine yanahitaji ubinadamu zaidi…nahisi ndio maana jopo la mahakimu limekwenda huko….’akasema.

‘Umezungumza kuhusu kesi, na nakumbuka mara ya mwisho hukuweza kumalizia yale maelezo,ulifikia pale ulipoigundua hiyo bunduki ilipokuwa imefichwa, je ni nani aliiweka hapo ulipoikuta hiyo bunduki, ni nesi au ni nani, ?’nikauliza.

‘Hilo tutaliongelea kwenye kikao cha leo, leo kuna kikao muhimu sana, na nashukuru kuwa nesi na wakili mkuu wamekibariki wakiwa na wakili wao, kwani wao ndio watu muhimu niliokuwa nikijaribu kuhakikisha kuwa wanalindwa…. ,hata kama ni wakosaji ,lakini kuna mambo mengine kisheria ni haki ya mtu…kwahiyo jiandae leo kuna kikao muhimu sana ambacho tutaongea mambo yote…’akaniambia huku akionyesha uso uliojaa huzuni

‘Sawa ,lakini leo nakuona huna raha, sio kawaida yako kuwa hivyo, nahiisi kuna jambo kubwa sana, nakama hutaki kuniambia siwezi kukulazimisha….’nikasema.

‘Usijali, …hakuna jambo kubwa sana, ila ni hali ya kawaida ya kibinadamu, tutaongea hayo baadaye kikaoni…’akaniambia na mimi nikaondoka kwenye mishe mishe zangu.

**********

Kikao kilikuwa na watu wale wale ambao tunahusika na hii kesi, alikuwepo mke wa wakili mkuu, rafiki yake, wakili mwanadada , mkuu kama mwenyekiti wa hicho kikao, na nilimuona docta ambaye nilikuja kumgundua kuwa ni bosi wa hospitali ya nesi, sikujua kwanini naye yumo humo.

Siku hiyo kwa vile najua nitakutana na Tausi nikavaie zile nguo zangu, kwani nilishaanza kujiweka kinamna ya kipekee, na kwa ushauri wa walili mwanadada, ukitaka kusomea sheria lazima uwe mtanashati, kwahiyo ni kavaa ile suti yangu maridadi na tai,…huwezi aminii kuwa ni yule mbeba maboksi kwa wahindi.

‘Ndugu zanguni, hiki ni kikao ambacho tunaweza kukiita kikao cha hitimisho ya kesi yetu ,licha ya kuwa hatupo mahakamani, lakini baada ya maongezi na hakimu na jopo lake, ilifikia hatua ya kukubalika kuwa kesi hiyo ihukumiwe ki namna ya kipekee kabisa, wao wenyewe wanajua jinsi gani ya kutoa hiyohukumu, na sisi hapa halituhusu sana….’akasema mkuu.

‘Kwanza tuna mengi tunahitaji kuyafahamu, na mojawapo ni je ni nani hasa alikuwa mmuaji wa Kimwana, hili atakuja kuliamlizia wakili mwanadada baadaye, lakini kabla ya hilo, labda nimtambulishe dakitari wetu,ambaye ni bosi wa nesi,…Nesi ambaye wengi tunajua hali yake ilivyo, na anahitaji utulivu, anahitaji matibabu na tunamumbea mungu apone, …..’akatulia mkuu.

`Docta natumai hatua zote za kisheria zimefuatwa, na tunakuomba useme lile tulilokuomba ukitumia utaalamu wako,najua unajau jinsi gani ya kuliweka hili swala sawa masikioni mwa watu ikizingatia kuwa wengi wao wanalijua,….’akasema mkuu.

Yule docta alisimama nakukohoa kidogo,akasema;

‘Mimi ni dakitari mkuu wa hospitali yetu hiyo hapo mbele,ninashukuru sana kuwa nami nimeweza kujumuika katika kesi hii, na nilikuwa tayari kutoa ushahid wangu kama ungelihitajika kisheria….kuna mengi yametokea na ukiangalia kitaaluma inatatiza sana, …lakini unajikuta kuwa huna jinsi inabidi ufuate sheria,…

Naona nisiwapotezee muda sana, labda niingie moja kwa moja kwenye jambo nililoitiwa hapa, ambalo hata nesi, na wakili mkuu, waliniomba niliongolee kwenu, …sio kwamba tu, tumeamua kufanya hivyo, hapana, wao wenyewe walisema siku wakiwa na nafuu watawaambia kila kitu, lakini kwa sasa wameomba tuwaambieni ukweli ulivyo,…’akatulia docta mkuu.

Mimi pale nilipo moyo ukaanza kwenda mbio,nikiwaza mengi,maana hali ya mabadiliko ya wakili mwanadada, na mkuu,i…sasa kaja dakitari, mambo haya yote, yalionyesha kuwa kuna jambo jingine, nikaona niwe nasubira ,maana kama walivyosema wao leo ni hitimisho…..labda kila kitu kitawekwa wazi, na kila jambo lina mwisho wake.

‘Nilimsifu sana nesi kwa ujasiri wake,….’akaendelea kuongea doacta.

‘Hasa siku ile alipokuja ofisni kwangu, kuniambai lile lilokuwa moyoni mwake,….. lakini sikujua kuwa angelichukua hatua hiyo aliyoichukua sasa ya kunywa sumu, na hata nilipokutana naye hivi karibuni,na kumuuliza vipi imekuwaje mpaka kufikia hatua hiyo, yeye alishindwa kuniambia lolote zaidi ya kusema kuwa `we acha tu, sio kuwa napenda kufanya hivyo,ila …hali imenilazimu…’akatulia docta.

‘Siku hiyo nesi alipokuja ofisini kwangu, hakuwa na raha, na ni kipindi ambacho wakili mkuu yupo katika hali mbaya ya shinikzo la damu,na aliniambai kuwa wakili mkuu, alikuwa mtu imara sana, afya yake ni thabiti tangu zamani,kwahiyo yeye anashangaa sana kumuona akiwa na mabadiliko hayo ya shinikizo la damu, na kuonyesha kwua kuna jambo jingine kubwa….’akasema.

‘Jambo gani ..?’ nikamuuliza.


‘Licha ya matatizo hayo ya kuchukuliwa mapicha mbaya ambayo nia na lengo ni kumuzalilisha, na kumkomoa, …kama alivyosema nesi,lakini alisema kuwa hayo ysingeliweza kumtingisha huyo wakili mkuu kama anavyomjua yeye, yeye anahisi kuwa kuna jamboo jingine limeathiriafya yake…’akasema huyo docta.

‘Nikamwambia kwani kuna nini cha zaidi …umeshachukua vipimo vyake vyote kama nilivyomuelekeza?’ nikamuuliza.

‘Ndio nimeshachuku vipimo vyote…lakini kuna kipimo kimoja ambacho hukukiweka,lakini kwangu mimi niliona ni muhumu sana kiwepo hicho kipimo, ….’akasema huyo nesi.

‘Kipimo gani,….maana hapo naona unaniingilia kazi yangu’nikamwambia kwa hasira.

‘Samahani sana docta,…sina nia mbaya ya kukuingilia katika kazi yako,…. lakini kuna umuhimu huo, maana mimi namjua vyemaa huyo mgonjwa, namjua sana hata kuliko anavyojijua yeye mwenyewe, haya mabadiliko yaliyoingia mwilini mwake sio ya kawaida lazima kuna jambo ingine tunahitaji kulichunguza…’akaniambia.

‘Haya kuwa muwazi , kwasababu hatuna muda hapa…’nikwambia.

‘Naomba tumempime na Ukimwi….’akasema.

Aliposema neno hilo huyo docta,mimi pale nilipokuwa mwili wote uliisha nguvu, akili yangu ikaanza kuchora ramani, …ikianzia kwa huyo wakili mkuu, ikaja kwa Kimwana na mistari ya ramani nikaiona ikiwa inaelekea kwangu,...wili mzima ukafa ganzi, lakini nikajipa moyo nakuwa na subira. Docta akawa anaendelea kuongea

`Mimi sikumjibu kitu, nikatulia kwa muda, na hilo lilikuwepo akilini mwangu maana tumekuwa na kawaida ya kuwashauri watu kupima, hata kama hali zao sio mbaya kiasi hicho, ni vyema tu kila mtu kwa wakati wake akapima afya yake, ili kujijua, na sio kwa kujipima tu kwa ajili ya ukimwi, lakini pia kwa ajili ya kujua afya yako…ni vyema tukaw an utamaduni huo….’akatulia docta.

‘Yule nesi ni rafiki yangu wa karibu sana, tangu afike pale amekuwa ni mtu muhimu sana kwangu, na namshukuru sana kuwa amekuwa akichapa kazi, na kujitolea kwa moyo wake wote,utafikiri yeye ndiye docta mkuu, …’akatulia.

‘Na mara nyingi naheshimu sana kauli yake, nikamwambia, ..wewe si unajua kanuni za mgonjwa, hatuwezi kumpima mgonjwa bila ya rizaa yake,na pili mimi sioni umuhimu wa kukimbilia hicho kipimo kwa sasa kwani ukimwambia mgonjwa kama huyo kwa sasa utamzidishia hayo mataizo aliyo nayo…’nikasema.

‘Ni vyema tukamuwahi sasa hivi kwani hali aliyo nayo, ni kuwa anajihisi kuwa keshapata huo ugonjwa, na nahisi ni kutokana na mawazo hayo,  ndiyo maana hali yake inakuwa ya mashaka,..ndio maana anajikuta akipatwa na shinikizo la damu . Kama nilivyokuambia mimi namjua vyema sana huyu mtu nimeishi naye kwa muda mrefu,…ni mtu mwenye ujasiri mkubwa,…afya yake ni njema …’akasema nesi.

‘Kwanini unahisi hivyo, kuwa huenda kaathirika?’ nikamuuliza.

‘Kwasababu namjua vyema….’akasema na baadaye akainama chini kwa uchungu , na aliponitizama mimi niliona machoni akiwa na machozi, nikaona hapo sasa mimi kama docta nahitajika kuwa makini. Na ikizingatiwa kuwa huyo ni mfanyakazi wangu, na mfanyakazi wangu,kwangu ni sehemu ya familia yangu.

‘Hebu niambie vyema, kumbuka kuwa wewe ni nesi, na ni kiyoo cha wagonjwa, wewe ni mtu muhimu sana, na nakutegemea sana kuwa mfano kwa wengine, ….naomba unieleze ukweli, hasa kuhusu wewe mwenyewe maana wewe ndiye mpenzi wake wa karibu…’nikamwambia.

‘Docta mimi na Kimwana ni marafiki sana, na mara nyingi hakuwa akinificha mambo yake,hadi pale tulipoanza kuonyeshana ubabe, na kugeuka kuwa maadui wakubwa…mwanzoni tuliivana sana, na licha ya kuwa marafiki kihivyo , hakuwahi kunitamkia lolote kuhusu yeye mwenyewe kuwa ana tatizo lolote la kiafaya,..kwanza hajawahi kuumwa, kabisa, ….’akatulia

Alipomtaja Kimwana mimi nikawa akili imekufa ganzi,….nikaanza kuhisi mwili ukiisha nguvu,na nilitaka kugeua kumwangalia rafiki wa mke wa mkuu yaani Tausi, lakini kichwa hakikuweza kugeuka, nikaanza kukumbuka maneno yake kuwa na kauli yake ile ya kusema`tupeane muda …’ kumbe kulikuwa na maana kubwa sana, nikajikuta kichwa kikiuma sana…..

‘Kwahiyo unataka kusema nini, kuhusu wakili mkuu, ….maana hapa unachanganya watu wawili, wakili mkuu na Kimwana,….’nikamwambia huku nikikumbuka kuwa aliwahi kuniambia kuwa wakili mkuu anatembea na 
Kimwana, na ndio maana hana raha.

`Docta siku moja nikiwa nyumbani kwa Kimwana niligundua vyeti vyake alivyopima, na hili nililigundua kipindi ambacho kakambia, na kwa vile mimi ni rafiki yake, nilikuwa nakujua kwake vyema, kwenye nyumba yake ya awali ambapo kulikuwa na vitu vyeka, nikafika kwake kuviweka vitu vyake sawa, na huku nikifanya akzi ya ngu ya ujasusi,…ndipo nikagundua kuwa alishawahi kupima na aligundulika kuwa kaathirika….’akaniambia na kunionyesha vyeti vyake.

‘Eti nini….?’ Mimii nikajikuta nikitamka kwa nguvu bila kujijua, na wote wakageuka kuniangalia.

‘Ndio ukweli ulivyoo kuwa Kimwana alikuwa kaathirika, na nimepewa kibali cha kumuongelea hapa, msije mkasema docta nakiuka miiko, hapana, sheria zote zimefuatwa, ….na kutokana na yeye ndio maana wakili mkuu alipogundua hilo, akawa hana raha,….hadi tulipompima baada ya kupata ushauru nasaha,nakweli na y eye kaathirika…..katuomba tuwaambie hili , na hata mke wake anajua…’akasema docta na kumwangalia mke wake ambaye alikuwa katulia kimiya.

‘Haiwezekani…’nikasema huku kichwa kikiniuma hasa, na yale maumivu ya kichwa yalinifanya nishindwe kuvumilia, nikainuka ple nilipokuwa nimekaa kwenye sofa na kwenda kukaa kwenye kiti cha chini huku nimeshikilia kichwa,….kilikuwa kinauma kupita maelezo, nikawa nahangaika na mara giza likatanda usoni, sikukumbuka jingine tena zaidi ya maumivu na mara giza giza nikapoteza fahamu,……

NB: Visa vyangu ni vya uhalisia, nI matukio yaliyotokea, najaribu kuviweka kitamthiliya ili viwe na mvuto, naomba kila unapoona nakosea usisite kunisahihisha ili niweze kuboresha zaidi.

*********************************************************************************

WAZO LA LEO: Ukweli unauma, lakini ni heri ya kuwa mkweli kuliko kuwa muwongo , hata kama uwongo huo,ni wa kumfanya mwenzako akupende, au bosi wako akuone ni wa maana,….Kuna watu wana tabia ya kuishi maisha ya kujipendekeza, ili waonekane wao ni zaidi,na hata inafikia hatua wanaongopa, wanasema uwongo au hata kuwazuliwa wenzao uwongo, ili waonekane wao ni wema. Hiyo sio tabia njema.Tuwe wakweli hata tukiona kuwa tumekosea,ni vyena tukakiri kuwa hapa tumekosea, ilitujifunze, …

**********************************************************************************



TOKA MAJUMBANI: Zoezi la kundikisha vitambulisho limekuwa ni kazi kubwa na kugeuka kuwa kero, kwa wananchi wa kawaida, imebidi watu kudamka saa kumi alifajiri, ili tu wakawahi namba, …kwani waandikishaji wanasema wao kwa siku wanahitaji kuandikisha hadi watu mia nne…..kwahiyo hugawiwa namba….sijui kuwa taratibu hizo zipo sehemu nyingine….lakini huki Kipunguni B ndivyo inavyofanyika.

Na wale wanaofanya kazi ya kuandikisha nao kama binadamu wengine mikono inachoka, na watu nao wanachoka kusubiri maana  inabidi waache kazi zao kwa siku nzima ili kufanikiwa kuandikisha,…na kuna wengine kama kawaida yetu wanachukulia nafasi hiyo kuwarubuni watu ili warizishe tamaa zao,…

Labda tungalie njia yingine rahisi kama ile ya wajumbe kupitia watu wake majumbani, au fomu hizo kugawiwa kwa kila mtu, au hawo watu kuongozana na wajumbe luwapitia watu, na wale wa maofisini kuzipata hizo fomu ofisini, na yule anayehitaji msaada wa kundikiwa ndiye amuone huyo muandikishaji, ….ili kupunguza kupoteza siku nzima au siku mbili nzima.

Ni mimi: emu-three

2 comments :

Anonymous said...

Hey! I know this is somewhat off-topic however I needed to ask.
Does operating a well-established blog such as yours take a
massive amount work? I'm brand new to writing a blog however I do write in my journal everyday. I'd like to start a
blog so I can easily share my own experience and views online.
Please let me know if you have any ideas or
tips for brand new aspiring bloggers. Appreciate it!
Also see my webpage :: acrylic displays

emuthree said...

Hey, `Anyon', above

To start a new blog is easy,

You have to create an account with Google, and then you visit the Blogger homepage https://www.blogger.com/....therein you will get everything you need for start a blog!