Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary', na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..pia tunakaribisha mijadala na yale yote unayopenda yawemo humu. Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu. SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthreeThursday, July 26, 2012

Hujafa hujaumbika-75 hitimisho 33‘Kwani kumetokea nini?’ nikauliza nilipofumbua macho.

‘Ulidondoka ghafla jana, na inaonekana ulikuwa ukiumwa kichwa,...kwani ulikuwa umeshikilia kichwa na docta kasema, ulikuwa na maumivu ya kichwa kutokana na msongo wa mawazo, vipi unajisikiaje kwa sasa…’akaniuliza Tausi.

‘Sijambo,…najisikia ahueani, sijui kwanini kichwa kiliniuma kiasi kile.sijawahi kuumwa kichwa kiasi kile....’nikasema.

‘Wakati mwingine unaweza ukawa unakabiliwa na mambo mengi kwa wakati mmoja, na ukawa ukiwaza hili au lile bila kupata jibu la moja kwa moja. Nikuulize ni nini kikusumbuacho?’ akaniuliza Tausi.

‘Hata mimi nashindwa kuelezea,maana pale nilikuwa najiuliza maswali mengi kichwani, hasa alipokuwa akielezea Docta kuhusu Wakili mkuu na Kimwana, ukumbuke kuwa Kimwana alikuwa mke wangu …kabla hajaniasi, kwahiyo ukiongelea kuwa ameathirika, huoni kuwa ninakuwa kwenye njia panda..’nikasema nikiwa na huzuni.

‘Ndio maana tunashauriwa kupima, ukipima hutakuwa na mawazo tena,…unakuwa umejihakikishia kuwa unaumwa au huumwi, na kama unaumwa, utajua jinsi gani ya kukabiliana na huwo ugonjwa, wazo la kuwa naumwa nini halipo tena,..na kama huumwi, basi unajiweka sawa kujilinda….’akaniambia Tausi.

‘Ni ngumu sana kuchukua uamuazi wa kupima, hasa ukijua kuwa kuna mtu ulikuwa naye kaathirika, lakini sina jinsi inabidi nikapime tu, nijue moja…’nikasema.

‘Ni vyema kujipima,…na hili linatakiwa kwa kila mtu ili kujijua,maana siku hizi kuna mgonjwa mengi, ambayo ukiyawahi unakuwa salama, na ukichelewa unajiweka katika maisha hatarishi….’akasema Tausi.

‘Nashukuru kwa mawazo yak ohayo,na sasa nimejua kwanini ulikuwa hunipi jibu la moja kwa moja kuwa umekubali tukafunge ndoa,..’nikasema.

‘Hayo ndio mawazo mabaya,ambayo huenda ndiyo yaliyokufikisha katika hali hiyo ya kuumwa kichwa, usiwe na mawazo ya dhana, na ubora wa kuondoa dhana, na kuchunguza kitaalamu, hukuwa na haja ya kunizania kuwa nina mawazo hayo, ambayo siyo kweli, lengo langu lilikuwa jema kabisa….’akasema an kutulia.

‘Una maana hukuwa na mawazo hayo, …..?’ nikaulizahuku nikimwangalia kwa makini,halafu kablahajajibi nikamuuliza swali jingine;

‘Ina maana hukuwa unajua lolote kuhusu kuathirika kwa Kimwana au mume wa rafiki yako?’ nikauliza.

‘Hata kama nilikuwa najua lolote kuhus hayo, sikuwa na maana hiyo, lengolangu kwako lilikuwa kujiandaa na kuwa tayari na kitu kinachoitwa ndoa,…hayo mengine ni mkusanyiko wa maandalizi hayo, na ni kweli inahitajika kwa wale wanaotaka kuoana kujijua afya zao, ili kukwepa matatizo mengine ambayo yangeliweza kuathiri afya zenu na vizazi vyenu vijavyo…lakini sikuwa nimelenga huko …’akasema na kuangalia saa yake.

‘Hata hivyo nashukuru sana, maana kamakweli nimeathirika, ..ningejisikia vibaya sana kama ningelikuwa tumeshaingia kwenye mahusiano,…ningejiona kama muuaji…’nikasema.

‘Haya ni mawazo duni, maana kila mmoja hajijui, kujijua kwake ni mpaka kupimwa,na kupimwa sio mara moja tu, inatakwia upime mara mbili hivi ili kujihakikishia,….kwani wewe una uhakika gani na mimi, maana hatujawahi kuongea kuhusu mimi kuwa labda nimeshajipimaau la,…kuwa dakitari sio lazima uwe umejipima, wapo wengi ni madakitar lakini hawajajipima…’akasema.

‘Haiwezekani, yaani mtu upo jikoni, usionje chakula….’nikasema na kujiinua , nikapima maumivu ya kichwa, sikusiki maumivu tena,…ina maana kuna kitu kimenisaidia sana, hasa kuongea na huyu mrembo, kuwa kwake karibu ilinipa faraja sana, nikawa nawaza mbali kuwa kama nitamkosa basi sijui nitaishije,lakini kama nimeathirika, sina jinsi, siweze kumwingiza binti wa watu kwenye matatizo…

‘Kwahiyo wewe hujawahi kujipima?’ nikamuuliza.

‘Kwangu mimi, ingawaje ni siri ya kila mtu, lakini nimeshajipima maar nyingi,….’akasema.

‘Kwanini sasa uliamua kujipima?’ nikamuuliza.

‘Mimi ninakawaid aya kupimaafya yangu mara kwa mara, kuna kujipima kwa kila mwezi, kuna vipimo vvya kila baadaya miezi mitatu,mitatu…ni kawaida yangu, na nashukuru kuwa imenisaidia sana,….hii tabia niilijenga pale nilipooanza kusumbuliwa na maumivi ya kichwa na kuwa kama mtu aliyechanganyikiwa,….’akasema.

‘Pole sana,na samahani sana kwa kukutia kwenye hayo mateso, …na kama nitajaliwa nitahakikisha kuwa nalipa hayo mateso niliyokusababishia…’nikasema.

‘Kwa vipi utalipa hayo mateso, maana mateso ya ndani ya moyo, si rahisi kuyalipa, kwani huwezi jua ukali na ukubwa wa mateso hayo, kiujumla niliteseka sana, lakini mwisho wa siku nilijilaumu mwenyewe, na kujiona tena mjinga, kwani unateseka wakati mwenzako hana habari na hayo mateso…’akasema huyo binti.

‘Nina kuhakikishia kuwa nikipata nafsi ya kukuoa, nitalipa hayomateso yote,nitakupenda kuliko nilivyowahi kupenda kabla…’

‘Tuombe mungu, atupe huo uzima, na jitahidi kutokuwaza sana, ili afya yako iiswe matatani, na cha muhimu kama nilivyokuambia,ni kujiandaa, kwanza kwa kusoma na kujua nini maana ya ndoa na unatakiwa ujiandae vipi, …’akasema.

‘Na pia natakiwa nikapime nijue kuwa nipoje,au sio?’ nikauliza.

‘Hilo unatakiw ahata kama hujafikiria maswalaya ndoa, hilo ni kwa rika lolote,…ni muhimu kupimaafya zetu. Basi mimi nakuacha, maana natakiwa kwenda kuwajibika, afya yako ikiwa tayari, tunatakiwa kukutana tena ili kuliongelea lile swala tulilokatisha, ni muhimu sana tukasikia mwisho wake tukiwa pamoja…’akasema huyu mwanadada.

‘Swala lipi hilo?’ nikauliza nikiwa sina uhakika anazungumzia swala gani.

‘Ni nani alimuua Kimwana, na kwasababu gani,…ujue wengi tumejikuta tukihusishwa…. ,na ni vyema hilo swala likaongelewa na ili kujitakasa wenyewe…kuna mengi yamejificha hapo, na wengi wanamtizama nesi kwa jicho la ubaya..sasa ni vyema wote ambao tunaona tunahitaji kusikia mwisho wake tukamsikiliza wakili mwanadada….’akasema.

‘Sawa, nitafurahi kusikia hilo na kwa  muda huo nitakuwa nimeshajijua kuwa nipo wapi, labda nipo kwenye ramani ya barabara iliyounganiswa toka kwa Kimwana…’nikasema.

Yule mwadada, akatabasamu, akaniangalia na kusema,

‘Ondoa wasi wasi kwa hilo, jenga ujasiri moyoni, ukijua kuwa kila kitu kinatokea kwa sababu, …kuumwa au kutoumwa,yote hutokea kwa mwanadamu, hakuna anayependa itokee hivyo , kuwa aumwe, hata wale wanaokunywa madawa ya kulevya, au vitu hatarishi, hawana nia kuwa afya zao ziharibike,kuwa waumwe….ila cha muhimu kwa kila mtu, ni kutafakari kwa kila jambo, kuwa je nikifanya hili ni nini matokea yake….’akasema na kujiandaa kuondoka.

‘Ni kweli ,…unanikumbusha mbali sana, nasiku ya leo sitaisahau kabisa katikamisha yangu,…’nikasema.

‘Hata mimi, inanikumbusha mbali sana,na huenda mungiu akijalia tutakuwa tukijikumbusha maisha yetu ya raha ya utotoni, natamanai kama ile siku ingelirejea tena…’akasema na akabusu shavuni na kuondoka.

************

Wakili mwanadada alitulia kuhakikisha kuwa kila mtu kakaa sehemu yake, akiwa mkoba wake, akatoa makaratasi fulani, akawa anayakagua halafu akatuangalia sote, …alipitia kila mtu mmoja mmoja kumwangalia usoni,nala ilipofika kwangu akatabasamu. Na mimi nikatabsamu, kwani alitabasamu lile tabasamu la nje ya mahakama.

‘Nawashukuru sana kukubali mualiko huu, na nashukuru pia kuwawote mpo salama, na mengi yamepita, na mengi mumeyasikia,ila kuna mengo bado yanafanyiwa kazi , na sis hatuna mamlaka nayo, cha muhimu ni kuangalia yale yanayotuhusu kwanza…’akasema wakili mwanadada.

Mimi hapa ninachotaka kuelezea ni yale niliyogundua katikauchunguzi wangu, ….nikishirikiana na wenzetu wa usalama, kwani bia wao nisingeliweza kugundua haya, na sikutaiwa kuyaelezea awali kwasababu yalikuwa yapo mbele ya mahakama, na sasa nimeshapewa kibali kuyaelezea bila wasi wasi, na mengine mtayasikia pindi, maana baadaye msemaji wa mahakama atakuja hapa kuwalezea mwenyewe,..’akasema na kutabasamu.

‘Wiki mbili zilizopita nilikuwa na huzuni sana, maana mengi yaliyoajiri na niliyokuja kugundua yalikuwa ya kunitia simanzi, maana kuna watu ambao wanajikuta matatizoni, lakini sio kosa lao, ….na sheria haitatambua hilo,kama umetenda kosa,basi hukumu ipo wazi,…’akatuliakidogo.

Mimi nitaanzia moja kwamoja siku ile nilipogundua ile silaha iliyofanyia mauaji,….siku ile nilipofika pale kwenye lile kabati ambalo lilihifadhia nguo na matakataka mengine ambayo yalikuwa hayatumiki, na kwa taarifa za yule binti wa pale nyumbani, alisema humo pia paliingia nyoka, na kwasaabbu ya huyo nyoka hakuna aliyeweza kuligusa hilo kabati.

Mimi sikujali, nililifungua, nikiwa na tahadhari zote,…na nashukuru nyuma yangu alikuwepo mtu wa usalama, na mara nikaiona hiyo bunduki, ikiwa imetumbukizwa hum ndani,na jinsi ilivyowekwa, kama vile kuigeshwa na mlango,ikadondoka kwa nje, nikaiwahi mikononi,…

Ina maana kuwa muwekaji aliiweka kwa haraka, na kuufunga mlango wa hilo kabato kwa haraka,kwahiyo ile bunduki ikawa imejiegemeza kwa ndani kwenye huo mlango, na kama mlango huo usingelikuwa imara , …basi mlengo huo ungelifunguka na bunduki ingelidondoka....

‘Kwa matizamo ule, ilimaanisha kuwa muwekaji aliiweka kwa haraka,…akiwa anakimbia, au wakati anaiweka alisikia jambo, kwahiyo akaiweka kwa haraka na kufunga mlango wa hilo kabati….kwa kujihami kuonekana, au kwa kuogopa jambo fulani.

Niliwaomba watu wa usalama kuhakikisha kuwa humo hakuna nyoka,na alama zote za vidole zimechukuliwa,…na walipotoa kila kitu, walikuta kuwa hakuna nyoka...ili kulikuwa na kitu kama kiota cha nyoka, kuwa likuwa akiishi hapo awali,... na alama zote za vidole zilichukuliwa, na ile silaha ikawekwa chini ya usalama.

‘Mungu wangu imefikaje hapohiyo silaha..ooh, mungu wangu…’nilisikia kilio cha yule binti baada ya kuichukua ile silaha, niligeuka kumwangalia nikakuta kashika kichwa, huku akiingalai ile silaha kwa macho ya uwoga.

‘Unajua lolote kuhusu hii silaha?’nikamuuliza.

‘Mmmh,ndio najua ni silaha ya baba, huwa inakaa kule ofisini kwake,sijuiimefikaje hapo..’akasema.

‘Kwa mara ya mwisho uliiona wapi hii silaha?’ nikamuuliza.

‘Kwa mara ya mwisho…sikumbuki, maana huwa inawekwa huko ofisini kwake…’akasema huku akiwa anaingalai ile silaha kwa wasiwasi.

‘Ulishawahi kuitumia hii silaha kabla…?’ nikamuuliza.

‘Na wewe maswali yako bwana, nitaitumiaje na wakati silaha hiyo inakaa huko kwa baba, na inafungiwa, niliwahi kuingia zamani sana wakati nasafisha hicho chumba, na baadaye tukapigwa marufuku kuingia huko ndani, sijawahi tena kuingia huko…’akasema kwa kujiamini.
‘Nimekuuliza hivi, ..au nikuulize hivi,katika misha yako ulishawahi kuutumia silaha kama hii?’ nikamuuliza.
‘Ndio, wakati tunakwenda kuwinda na akina baba ,baba alikuwa akitupa na sisi tutumie,maana mwanzoni nilikuwa naogoapa snakuutumia, ..nikisia mlipuko wake, nashituka na kuhsika masikio,…akaona ni vyema na mimi nikaondoa uwoga …akanifundisha na mimi…’akasema.
‘Wakati anakiufundisha, …mlikuwa na mama na nani wengine?’nikamuuliza.
‘Wakati mwingine nilikuwa na mama, na mama mdogo,na watu wengine.
‘Mama mdogo ni nani?’ nikamuuliza.
‘Ni yule nesi…..ndugu wa mama’akasema.
‘Kuna kipindi mlishawahi kwenda wewe na baba peke yenu…?’ nikamuuliza.
‘Mmmh,hayo maswali siyapendi, …maana naogopa, …’akasema

‘Usiogope, mimi nipo pamoja na wewe, na hili nakuuliza kwa ajili ya kukulinda wewe, ukinificha unaweza kuwa hatarini, sema kila kitu, ili nijue jinsi gani ya kukusaidia…’nikamwambia.

‘Unisaidie kwa nini……kwani nimesema kuwa nahitaji kusaidiwa, kwani kuna tatizo gani na mimi….naona kama unanisakama sana…’akasema.

‘Hili ni swala la kawaida tu,na ni muhimu mimi kama wakili nikajua, maana nyie wote mpo kwenye orodha ya watu ninaotkaiwa kuwasaidia, hajakuambia mama, kuwa mimi nawasaidia nyie, kuhusiana na kesi, iliyopo mahakamani, kwahiyo sema ukweli, ili asije akajikuta kwenye matatizo, na ujue kuwa kama yeye yupo kwenye matatizo na wewe pia utachukuliwa kuisadiai polisi….’nikasema.

‘Ohh, hayo tena makubwa, …lakini kuhussu kwenda na baba kuwinda, mama alikuwa hajui, …na baba likuwa kinishawishi tu…na ilitokea wakati ule….na kunilazimisha,….mimi sikupenda…’akaanza kulia.

‘Ulishaniambia hayo, na nilishakuambia kuwa ili uweze kuyashinda hayo, ni lazima uwe jasiri, uwe tayari kukubali matokea, maana yalishafanyika, na wewe hukuondaiwe hivyo, au ulipenda iwe hivyo, ulikuwa ukimpenda baba yako?’ nikamuuliza.

‘Skupenda,…ila yeye alinishawishi, …akanibembeleza, na ndio akawa annipeleka huko kwenye kuwinda, na…siku baadaye ndio akanilizamisha kufnay naye mabaya,…akansihika kwa nguvu…baadaye akawa ananibembeleza kuwa ananipenda…’akasema.

‘Ina maana tendo hilo halikutokea mara moja…?’nikamuuliza.

‘Mara mbili…mmh, hapana mara sijui ngapi zile…nikawa nimezoea, ila sikupoenda maana nilimuona kama baba yangu,….baadaye ndio nikamwambia mama, maana niliona imezidi na mama akijua itakuwa ni matatizo.

‘Je wewe hizo siku zote ulikuwa ukisikiaje,…ilikuwa ina kuuma sana, au ulikuja kuzoea nakuona jamboo la kawaida?’ nikamuuliza.

‘Mwanzoni niliumia sana, nililia sana…na baba alipoona hivyo akawa anaibembeleza, na ndio akawa ananipelak huko kuwinda ananionyesha jinsi ya kutumia silaha, nikawa naijua na nikawa nimejifunza kuitumia,…..na kuna siku tukiwa na mama mdogo, mama mdogo ananifundihs jinsi y akulenga shabaha, nikawa najua kulenga vizuri sana….kama yeye…’akasema.

‘Je hukuwa ukiumia sana, kuwa umetenda machafu na baba ,wakati kuna mama yako,….?’nikamuuliza.

‘Iliniuma sana…nimekuambia sikupenda iwe hivyo….alinishika kwa nguvu….’akaanza kulia.

‘Unajua kuwa baba yako alikuwa na mwanamke mwingine zaidi ya mama yako…?’ nikamuuliza.

‘Yaani we acha tu,…sijui kwanini siku nilipomuona baba na yule mwanamke, nilumia sana,maana niliwaona wakiwa kitandani…nilumia sana,…nilitamani nimuambia mama, nikashindwa…sijui kwanini nilumia kiasi kile,…unajau baba alishaniambia kuwa ananipenda mimi,sasakumbe anawapenda wengine, nilimuona kuwa ni muongo…’akasema na kuona aibu.

‘Ina maana uliingiwa na wivu?’ nikamuuliza.

‘Sijui ..sielewi, ila nilimchukia sana huyo mwanamke….nilimuona kama mwizi…nilimchukia kupita kiasi,..’akasema.

‘Hukumwambi mama yako?’ nikamuuliza.

‘Sikuweza kumwambi siku hiyo..ila siku ile niliposikia mama akiongea na baba kuhusu huyo mwanamke, ndipo nikaamua kumwambia mama ukweli kuwa nilishawaona wakifanya machafu yao’akasema.

‘Ulisikia nini wakiongea mama na baba yako?’ akaulizwa.

Hapo akaanza kulia…..alilia kwa muda mrefu na baadaye akasema;

‘Mama alimwambia baba kuwa huyo mwanamke anayetembea naye imegundulikana kuwa kaathirika, na moja ya kazi zake ni kuambukiza watu…sasa fikiria, kama huyo mwanamke katembea na baba, na baba katembea na mimi, si na mimi nimeathirika….’akaanza kulia kwa kwikwi….
‘Huyo mwanamke anaitwa na nani?’ nikamuuliza.

‘Anaitwa….Kimwana.

NB: Sehemu hii nimeiandika kwaharaka kidogo juu kwa juu, na sijapata muda wa kuipitia, kama kuna makosa naomba tusameheane, na kama yanahitaji kurekebishwa uwe na mimi niambie ili nijue.

WAZO LA LEO: Dhana nyingi kichwana ni hatari, na zikizidi sana huletwa msongo wa mawazo, ...kiafya sio vyema, na kama unaumwa, nenda kapime, usiweke dhana,kuwa labda naumwa ugonjwa huu au ule, vipo vipimo, wapo wataalmu, tuwaone, na pia tujenge tabia ya kukagua afya zetu mara kwa mara.Ni mimi: emu-three

1 comment :

Anonymous said...

Huyo dada hapo nilisoma naye, sijui siku hizi yupo wapi?