Kesi ilianza kama kawaida nikasimamishwa na sasa nikihojiwa
na wakili wangu, ilichukua muda mrefu kunihoji, nikiwa niulizwa maswali najibu,na
hapa na pale kunatokea ubishani wa kisheria, na inafikia hatua wakili Yule mwanamama
anaomba kuniuuliza maswali tena na baadaye anaikuja wakili wangu mtetezi, na
ikawa kama mimi ndio mpira unaochezwa na sehemu zote mbili, na ikaonekana
dhahiri kuwa mimi ndiye nitakuwa ufunguo wa kushinda au kushindwa na baadaye
ikafika muda wa mapumziko.
‘Vipi mbona unajibu tofauti na nilivyokuambia, kuna tatizo
gani,huoni ulivyoniweka katika wakati mgumu, ilikuwa kazi rahisi tu, sasa wewe
umaifanya imekuwa ngumu, kuliko maelezo, kuna tatizo gani…?’ akasema wakili
wangu kwa hasira.
‘Mbona mimi nimjibu itakiwavyo….wewe ni wakili, na wakili
unahitaji nini toka kwa mshitakiwa,…unahitaji ukweli au uwongo, ….ndani ya
mhakama unatakiwa useme ukweli kwasababu ya kiapo, ….na ndivyo nilivyojaribu
kusema ukweli….naomba unielewe hivyo,mimi sio mtaalamu wa uwongo….na hasa
sehemu kama hii ambayo ina kiapo….’nikasema.
‘Kiapo….,ndio nakubaliana na wewe, lakini tangia mwanzo
tulikuwa yuankwenda vizuri, kwa maslahi yako, na ndio jukumu langu kukutetea,
au sio…?’ akasema na kuniangalia, na mimi nikawa kimiya nikiwa nimetingwa na
mawazo tele kichwani, nilikuwa nimechoka kutokana na akzi hiyo ngumu.
‘Sikiliza mimi nipo hapa kwa ajili yako,kukutetea, na ndio
kazi yangu, ….kama ulivyoona, nimekuwa nikijaribu humo ndani kukuweka sawa,
lakini tunakuwa watu wawili tofauti, ….nikumabie ukweli ilishafikia sehemu
nzuri,…leo tungemaliza mambo, kesi hii haina
miguu,haina ushaidi, wanakutegemea wewe tu, wengine wote hawana la kusema …sasa
wewe umeshajitia doa mwenyewe,sijui nikimwambia bosi wako atasemaje….’akasema
huku akikuna kichwa.
‘Nikuulize kitu muheshimiwa,…hivi wewe umesomea nini…?’
nikamuuliza na swali hilo lilimshitua na akageuka kuniangalia kwa muda.
‘Swali gani hilo, huoni nini ninachokifanya hapa….’akasema
huku akikuna kichwa kuonyesha kuwa ana mawazo mengi kichwani.
‘Wewe ni wakili , na unajua kuwa ukiuliza swali unatakiwa
ujibu, ….kama ulivyokuwa ukifanya ndani ya ulingo, ..au ukitoka nje uwakili
unakuwa hauna maana, …mbona unakwepa swali langu….?’nikamwambia.
‘Haya ….unataka nikujibu, sawa, mimi nimesomea
sheria…’akajibu
‘Sheria ambayo inakutaka useme ukweli au uwongo, utetee
haki, au uwongo…?’nikamuuliza
‘Nimesomea sheria, ….unanielewa, mimi ni wakili, na hapa
niwakili mtetezi, … kutetea haki yako, …uelewe hilo…sasa haki ipi , inategemea wewe mwenyewe, …unaweza ukatenda kosa,
lakini kwa kutokujua sheria, ni haki yako kutetewa,hapo sijatenda uwongo
unaodai….kwanza nikuulize kwanini umeniuliza hilo swali?’ akaniuliza.
‘Kwasababu wewe unajua kabisa kuwa unachotetea ni
uwongo,…mambo wanayodai hawo akina mama na serikali ni kweli tupu,…tuseme
ukweli tuwe wapenzi wa mungu, wewe
unayapinga, unasaidia huo uovu…huoni kuwa unakiuka miiko ya sheria..?’
nikamwambia kama nauliza.
‘Miiko ipi, niliyoikiuka….tatizo lako huelewi sheria,….hilo
niachie mimi….nia na lengo langu ni kukutetea wewe, na kwa vipi, ni mambo ya
kisheri ambayo huyajui,…nikuambie ukweli,watu wengi hufungwa, kwasababu hawajui
sheria, na hawataki kututumiwa sisi, tukawatetea,…unanielewa lakini…’akasema
wakili huku akionyesha kuwa nampotezea muda wake.
‘Zipo sheria zipo wazi hata kama hujasomea sheria….zinaonekana
katika upeo wakibinadamu….utu wa mtu ni muhimu sana,na unatakiwa ulindwe, mambo
ya kiutu,kibanadamu mambo yapo dhahiri….yaliyotendendeka haya utu,hayana
ubinadamu, ndio maana mtu anashindwakuvumilia, hakutarajia,…..inafikia hatua
mapigo ya moyo wake yanashindwa kuvumilia….’nikasema huku nikiwa ndani ya
hisia.
‘Nataka uelewe nafasi yangu kama wakili mtetezi, ….imefikia
hatua uanze kuamua moja, unataka kutoka jela au uanataka kufungwa,maana kama utajibu
kinyume na nilivyokueleza,hakuna jinsi ni lazima utafungwa….’akasema na
kuniangalai kwa makini.
‘Na je na wewe hutachukuliwa hatua kwa kutetea uwongo,
katika kazi zenu hazina miiko hiyo…maana ikifikia hatua hiyo nitasema ukweli
kuwa hata wewe ulijua hilo, lakini ukawa upande wa mteja wako,ukitafuta pesa
badala ya ukweli…niambie ukweli, unafanya hyo kwaajili ya maslahi au unafanya
kuangalia ukweli na haki..?’nikasema na huyo wakili akaniangalia kwa makini na
kusema;
‘Tatizo lako hujui sheria…nakuuliza tena, unataka nikutetee
utoke jela, au niache, maana natapoteza muda wangu kwa mtu ambaye hana
ushirikiano na mimi….,mimi kazi yangu ni kukutetea, na si vinginevyo, kama haki
na ukweli, sheria itaamua,…hiyo ni kazi ya hakimu, ila mimi kama wakili mtetezi
natimiza wajibu wangu, …maswal ya maslahi ni mengine, ….nakuuliza tena,upo
tayari nikutetee au hutaki..?’ akaniuliza.
‘Kwani mimi nimekataa usinitete…..sijakataa, kabisa, …kunasehemu
nimesemakuwa sikutaki unitetee? ’nikauliza huku nikionyesha uso wa kuchoka.
‘Hujasema kwa kauli ya moja kwamoja, lakini umekuwa ukijibu
maswali kinyume na makubaliano, wakati nakuelekeza jinsi ya kujibu maswali
unajibu tofauti….tunakuwa hatuna makubaliano…kwamatindo huo unampa mwanya
mwenzangu kunishinda….sijui unanielwa hapo?’ akauliza na kuniangalia machoni.
‘Nakuelewa,na mimi nataka unielewe pia…’nikasema.
‘Hebu nikuulize kuna ninii kimekupata,hadi ukabadilika
kipindi hiki muhimu, niambie ili nijue nini cha kufanya, kwaninii umebadilika
wakati tulikuwa tunakwenda vyema…?’ akaniuliza.
‘Ndugu muheshimiwa…mimi ni binadamu na nina hisia sawa na
binadamu wengine, sitaweza kujibu uwongo, ambao matokeo yake ni kuangamiza
vizazi vyetu..hebu fikiri wewe mtoto wako afanyiwe hayo
tunayoyatetea,..utajisikiaje….tuwe binadamu wenye hisia na kuwajali watu
wengine hata kama lengo letu nikutafuta maslahi…’nikasema
‘Una maana gani kusema hivyo….kwani hayo niliyokuelekeza
ujibu, tena nakuelekeza mbleya mhakama, ni uwongo, je ina maana ulihusika
katika kifo cha huyo muheshimiwa…nimabie kamakuna amblo mimi silijui, ili nijue
jinsi gani ya kukutetea?’ akaniuliza
‘Sijahusika…sijasema nimehusika, ila najibu yale ambayo ni
sahihi ninapoulizwa, lakini ukiniuliz a kuwa nimehusika, jibu la mkato nii kuwa
sijahusika, kwasababu kweli sikuhusika,…ila kama sababu ya mtendo yangu, yalifikia
hatua hiyo , hapo ukiniuliza nitasema yale matendo sahihi niliyoyafanya….je
hilo ni kosa ndugu muheshimiwa…?’nikauliza
‘Matendo yapi,… na hujui ukisema hivyo unajihusisha moja
kwamoja na kifo chake, pili unajidhihirisha kuwa kweli unatumiwa….na…tatu…wewe
mtu, hivi nikuambieje, ndio maana nataka uniachie mimi, ufanye vile
ninavyokuelekeza, tatizo lako hujui sheria, ndio maana watu kama sisi tupo, ili
kukulinda uisije ukaumia…utaozea jela wewe…..’akasema huku akingalia saa yake.
‘Hilo nakubaliana nalo, nisilokubaliana nalo ni kusema
uwongo , uwongo ambao upo dhahiri, moyo wangu unanisuta, na nitashindwa kuishi
kwa amani, nitashindwa hata kuwaangali watoto wangu, nikijua kuna watoto wa
wengine, nilishindwa kuwatetea mahakamani , ….huoni hawo wanaoathirika ni
watoto wa wengine, sawa na watoto wako….?’nikasema kama nauliza huku namwangalia
machoni. Na yeye akawa naniangalia kwa mashaka.
‘Kwahiyo utajibu kinyume na makubaliano yetu…au sio,… na kwa
msingi huo hatupo pamoja, basi haina haja ya mimi kukutetea, ngoja niongee na
bosi wako,kama inawezekana amtafute mtu mwingine unayemkubali…maana nitakuwa
napoteza muda wangu na mwisho wa siku nitaonekana sijui kazi….’akasema.
Akaitoa simu yake huku akisita sita, na kabla hajampigia huyo
anayetaka kumpigia, mara akaja askari na kusema huyo wakili anaitwa na hakimu.
Cha ajabu aliiweka ile simu palemezani, na kuondoka haraka bila ya hiyo simu,….
*****
Nilibakia peke yangu kwenye chumba maalumu cha kuongelea na
mara simu ya Yule wakili ikaita, nikaiangalia inavyoita,mpaka ikanyamaza,
ikaita tena….na safari hii nikaingiwa na
hamu ya kujua ni nani anayepiga nikaisogelea na pale nikaona jina la Docta
Mama, nikacheka,…
Iliita mpaka ikanyamaza tena, ukapita muda , halafu ikaanza
kuita tena, hapo nikatizama kule mlangoni,mlango ulikuwa umefungwa, nakaichukua
ile simu na kuibonyeza kupokea na kuiweka sikioni.
‘Nakuambia hivi, chelewesha chelewesha hiyo kesi, maana huyo mtu hatutaki aonekane tena
…tutajua nini la kufanya…maana nimepata taarifa kuwa hana ushirikiano,na
tukimuachia anaweza kutukaanga, umenielewa…fuata ninayokuagiza, …umenielewa
lakini…?’akauliza huyo mwanamama,nikatulia kimiya…
‘Umenielewa…au …’nikakata ile simu na haraka nikatafuta
sehemu ya kufuta simu hiyo iliyoingia na kuhakikisha haipo kabisa hata kwenye
sehemu ya kumbukumbu ya simu zilizofutwa,halafu nikairudisha pale mezani ….na
wakati naiweka wakili akaingia…
‘Huyu hakimu anataka kuleta mambo mengine…anataka kesi hii
imalizwe haraka iwezekanavyo,nahisi keshaona jinsi ulivyo jibu hayo maswali leo.
Ilikuwa ifanyike haivyo, lakini sasa nimeshindwa nifanyeje,kwani nikisema sawa,
basi hakuna jinsi, utakwenda jela…
‘Hata hivyo bado una nafasi hawajui mtego wangu,ila yote
yanategemea wewe…upo tayari nikutetee, au una nini cha zaidi,hebu niambie…?’akauliza
na kuniangali, halafu akaichukau simu yake na kuangalia kama kuna simu
iliita,hakuona kitu ,akanigeukia na kusema;
‘Hapa kuna simu iliita,….mmmh,ok, haian shida…’akasema na
kunigeukia
‘Umefikia wapi, maana nataka kumpigia bosi wako ili
nimfahamishe nini kinachoendelea, na ili anipe jibu, ili nikionana na hakimu
nijue nini la kusema....yaani umaniweka katika wakati mgumu sana,..hii kesi ilikua
yetu, haikuwa na kipingamizi, sasa sijuu hata nifanyeje, lakinii bado una
nafasi,mimi nipo kwa ajili yako…je upo pamoja na mimi au nini uamuzi wako…?’
akaniuliza.
‘Mpigie bosi wako…...najua nini atakuambia,…hilo
lilishapangwa, hata kama kesi hii itakwishamtakavyo, lakini uamuzi
ulishapitishwa kuhusu mimi na huyo bosi, bosi wako…., nawajua sana hawa
watu, lakini mjue nyie sio
mungu,..’nikasema
‘Unajua usipokuwa muwazi kwangu mimi sitaweza kufanya kazi
yangu vyema, niambie tatizo lipo wapi ili nione jinsi ya kusaidia, na huyo sio
bosi wangu, ni bosi wako….’akasema huku kakunja sura, halafu aaktabasamu.
‘Usiwe na wasiwasi bwana …unaona jinsi ninavyopambana kwenye
ulingo wa kisheria, …ina maana ukinielewa vyema hutashindwa hii kesi, lakini
kwanza nijue undani wa tatizo lenyewe, ili nijue vipi tutalitatua, kwani kuna
nini kimetokea mpaka usiniamini mimi….?’akasema
‘Sio kwamba sikuamini wewe, lakini je hawo waliokutuma wana
lengo gani kwangu, …huenda hujui au unajua lakini kwasababu ya maslahi au
kwasababu ya wito wa kazi yako utajifanya hujui…kwasababu ya mslahi au misingi
ya kazi yako….sawa utajifanya hujui, lakini yote ni kwasababu ya mslahi,
tusidanganyene, nia hapo mnataka mimi niseme uwongo,kwa manufaa yenu, au
sio….?’ nikauliza
‘Useme uwongo upo, mbona sikuelewi, …hakuna uwongo hapa, sisi tunafuata sheria, wapi tumekwenda
kinyume cha sheria ili uitwe uwongo, mimi ninaangali sheria inasema nini
kuhusiana na hilo tatizo, kwa jili ya kukutetea….je kuna sehenu umekiuka
sheria, kama umekiuka, tutaangalai kwa vipi,na utetewe vipi….lakini kwa kesi
yako hujavunja sheria, ila watu wanataka ukubali kuwa umevunje sheria ili
kufanikisha malengo yao, ndivyo ilivyo sasa, sasa sisi tunaujua sheria lazima
tuwatetee nyie msioijua...natumai umenielewa…’akasema huku akiangalia saa yake.
‘Sasa huko mumeongea nini na hakimu….?’ Nikamuuliza na yeye
akacheka na kuniangalia kwa muda akasema;
‘Hayo ni mambo ya kisheria hayakuhusu….ila la muhimu ni kuwa
hakimu anataka kesi hii iishe haraka maana inavuta hadhira , kila siku watu
wanaongezeka, na mtokeao yake inaweza ikageuzwa na kuwa mambo ya kisiasa,na
inaweza ialeta vurugu ….kwahiyo anataka haki itendeke,kesi hii imalizike haraka
iwezekanavyo….’akasema wakili.
‘Haki itatendeka kweli….je itatendeka kweli, wakati nyie mnataka kuufuta ushahidi na ukweli
upotoshwe…’nikasema
‘Ufutwe kwa vipi….kwa vipi tuupotoshe….mmh,..?’akauliza na
mara simu yake ikalia, akaniangalia kwa muda kabla hajaipokea, halafu akasogea
pembeni, akageuka tena kuniangalia na safari hii uso wake ulibadilika,sio ule
wa tabasamu tena, alionyesha makunyazi usoni,sikuelewa kwanini na akasogea
mbali na kuipokea hiyo simu.
Kwa muda ule sikujali kwasababu nilishajua ni nani kampigia
na ataambiwa nini,tatizo ni hapo akaiulizwa je simu yake yakwanza aliipokea
nani….sikujali…
‘Hapa nikuwaza jinsi gani ya kujiokoa na janga hilo…sasa
inabidi nianza mapigano ya nafsi yangu,…’nikasema kwa sauti, huku nikakumbuka
yale maneno ya mwanadada, ambaye ni wakili, licha ya kuwa walikuwa
wakibadilishana na wenzake mara kwa mara ndani ya mahaka ,lakini yeye alisimamia
katika kutetea haki za akina mama, yeye alipenda sana huo usemi kuwa `nipambane
kiume’
‘Inabidi sasa nipambane kiume.’ Nikasema
huku nikinyosha
‘Kwa uzoefu wangu, wewe ndiwe umeweza kuvumilia muda mrefu
hadi hatua hii, kesi nyingi zilizopita zilikuwa hazichukui muda mrefu hivi,
…’nikakumbuka meneno ya wakili wangu huyu anayenitetea
‘Kwanini zilikuwa hazichukui muda mrefu hivi, kwani zilihusu
mauaji….?’ Nikadadisi.
‘Zilikuwepo za mauaji,na nyingine lakini chanzo ni mambo haya haya, na cha
jabu kesi za mauaji ndizo zilikuwa hazikuchukui muda mrefu, maana mshitakiwa
anaamua kuchukua sheria mikononi mwake, anajihukumu mwenyewe kabla
hajahukumiwa,…sijui kwanini hawa watu hawajiamini,nashukuru wewe unajiamini
kidogo…’akaniambia kwani ilikuwa kipindi cha mwanzoni wakati najibu anavyotaka
yeye.
‘Wanachukua sheria mikononi mwao kwa vipi, wakati wapo
mahabusu ,ina maana wanajiua….?’ Nikauliza.
‘Nawashangaa sana, unakwedna nao vizuri, mwanzoni wanafuata
unavyowaelekeza, lakini mwishoni
wanajikanyaga, halafu wanaona kujiua ndio njia ya mkato, hawajui kuwa huo ni
uoga. Huweze ukajiua ukiwa vitani, pambana…., hata kama ni kufa ufe ukiwa
unapambana, …huenda ungelishinda, na hii kesi ni yakushinda tu….’ Akasema akijiamini,
hakujua nini kilichokuwepo kichwani mwangu.
Wakati nawaza haya Yule wakili akarudi, na alionyesha ule
uso wake wa tabasamu, lakini sio kama ilivyokuwa mwanzoni,…kwa muda mfupi niliokuwa
naye nimejifunza mengi kuhusu huyu mtu, sura yake inaweza kubadilika, lakini
anajitahidi sana akikuangalia machoni,awe anatabasamu,…nahapo huwezi kujua ana
lengo gani, …. akaniangalia kwanza kwa muda bila kusema kitu, akasogea na kunishika begani akasema;
‘Watu wa zamani wanasema; mtoto akililia wembe mpe…..sijui
nini kilichokusibu, na lengo langu lilikuwa jema kabisa, nia yangu ilikuwa
kukusaidia, maana najua wewe ni mhanga wa mambo ambayo huna makosa nayo, inaonyesha
kabisa wewe ni mtu mwema sana, lakini labda kwasababu ya hii shida ya kimaisha,umejikuta
ukiingia katika msukosuko huu, kama wengine…. pole sana…’akawa kama ananiminya
begani.
‘Pole ya nini…muheshimiwa…?’ nikauliza.
‘Kwasababu mimi sina la kufanya tena, tusubiri maana
waanshauriana huko ndani,haijajulikana kama kesi itaendelea leo, …..kama
msimamo wako ndio huo, mimi nitajitoa, labda iwe vinginevyo,kwasababu mimi
nakwenda kwa mujibu ya matakwa yenu, kama bosi wako kasema kama hukubali kuwa
pamoja nami , basi….sasa mimi nifanyaje…’akaniangalia machoni.
‘Lakini mimi sijakataa uwe wakili wangu…nimekuambia kuwa
nimekataa?’ nikamuuliza.
‘Unaweza ukakataa kwa kauli au kwa vitendo, wewe umekataa
kwa vitendo, na vitendo ndivyo nguzo ya hii kesi, nakuambia pita huku wewe
unapita unapotaka wewe, nitafanyaje hapo, hebu chukulia wewe upo nafasi yangu
ungelifanyaje?’ akaniuliza.
‘Ningelifuata misingi na masharti ya kazi yangu, …kusimamia
sheria katika misingi ya haki….’nikasema.
‘Tutarejea mjadala ule ule na hautaleta tija…ila
ninachokuambia ni kuwa tupo pamoja…..hata kama bosi wako anasema nikuache,
lakini mimi nitakuwa na wewe….nafikiri muda umefika,muda ambao hata mimi
nilikuwa nausubiri….’akasema na kunishika bega.
‘Mnaanza kugeukana nini…?’ nikasema kimoyomoyo.
‘Kazi hii ya uwakili, unaweza ukaifanya kwa malengo mema kabisa, na kama kazi nyingine lengo ni
kupata pesa kwasababu ni ajira….na nia na makusudio yetu ni kimlinda mteja
wako, ili ashinde kesi yake,….ndio lengo letu kubwa ndio maana unaitwa wakili
mtetezi…huwezi ukachukuliwa kama wakili mtetezi halafu uwe kinyume chake…nafikiri
unanipata hapo…?’akasema huyo wakili.
‘Ina maana hata ukiona kuwa mteja wako ni mkosaji, yupo
hatiani, utamteta tu, hata bila ya kumpa ushauri, utakubali tu hiyo kesi
kwasababu ya maslahi…?’ nikamuuliza.
‘Kazi yetu kubwa unapopewa kazi ni kuhakikisha unaijua ile
kesi,na kweli kesi nyingi za huyu mama zinautata, na mimi kama wakili
wake,namshauri inavyowezekana,lakini lengo letu lipo pale pale, kumtetea na
kumlinda mteja wako ….lakini..!’akatulia kwanza na kuangalia pembeni.
‘Lakini vipi muheshimiwa….ujue wewe bado ni wakili wangu,
unatakiwa unitete kama inavyotakiwa, kama unaona nipo kwenye hatia
nishauri,kama nipo kwenye kudhulumiwa naomba unisimamie na mungu atakulipa…’nikajikuta
nikisema.
Yule wakili aligeuka na kuniangalia, akasogea karibu yangu
na kunishika tena begani, hakusema kitu, akageuka na kuanza kuondoka, nikabaki
nimeduwaa, nikijua ni yale yale….Lakini alipofika hatua mbili mbele akageuka na
kusema;
‘Nikumabie kitu, usikate tamaa, upi sahihi, na tupo pamoja,ila
kama nilivyokuambia mimi ni wakili mtetezi,…siwezi kugeuka kuwa kinyume chake,….pigana
kiume, tukijaliwa tutaonana…na mungu atakulinda…’akasema na kuondoka.
Nilibakia peke yangu nikiwaza hili na lile na mara askari akaja
na kusema mawakili wameshakubaliana kuwa kesi hiyo iahirishwe mpaka kesho
kutwa, na wakili wangu kasema kuwa kapata dharura, hakuweza kuja kuniaga,ila
yupo pamoja na mimi…
‘Sasa tafadhali naomba nionane na muheshimiwa
hakimu..tafadhali nipo chini ya miguu yako…nakuomba sana…kwani ikipita
leo,..sijui itakuwaje…nakuomba tafadahali….’nikapiga hata magoti.
‘Wewe huruhusiwi kuonana na hakimu….haitawezekana, ni wakili
wako tu…na kwasababu maalumu…’akasema.
‘Hili halihitaji kusubiri, na kama litasubiri,kitakachotokea
kitakuwa juu yako, nakuomba tafadhali, wewe timiza wajibu wako kafikishe huo ujumbe….ni
muhimu sana…’nikasema huku nimepiga magoti, na wakati huohuo nikaona wakili yule
mwanadada akitoka,na wasaidizi wake, akaniona nikiwa nimepiga magoti…
Je nini kitatokea, tuzidi kuwa pamoja, na hapa nifupisha sana kutokana na muda na hali halisi....
WAZO LA LEO: Kusema uwongo
imekuwa ni jambo la kawaida kwetu na hata kama mtu anajua kuwa anachose ni
uwongo, ataahidi tu, ili watu wamuone, na haja yake itimie…na hata kutatafuta njia za kuhalalisha uwongo
wake, tujue kabisa hizo ni dalili za unafiki,….
Jamani,jamani tukumbuke kuwa ahadi ni deni.
Ni mimi:
emu-three
1 comment :
Kwanza nikupe pele kwa kazi kubwa unayoifanya ambayo sijui kama kuna malipo yoyote kipesa unayopata zaidi ya kukupongeza.
Sisi hatuna cha kukulipa ila nikukuombea kwa mungu akuzidishie kipato chako.
Post a Comment